Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Sikuamini kama ni yeye………!

    Report Post
    Page 1 of 3 123 LastLast
    Results 1 to 20 of 41
    1. #1
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,182
      Rep Power : 27035
      Likes Received
      8457
      Likes Given
      17777

      Default Sikuamini kama ni yeye………!

      Alikuwa ni zaidi ya mama..........

      Sikumbuki umri wangu kamili wakati ule, lakini bila shaka nilikuwa na umri wa miaka kama sita hivi.
      Nakumbuka sisi nyumbani tulikuwa miongoni mwa familia za awali kupata simu nyumbani pale Tabora. Hata hivyo, nilikuwa tu nasikiliza baba au mama akizungumza na simu, kwani ilikuwa ikikaa juu kwenye meza fulani ndefu. Hata hivyo siku moja wakati nikicheza na nyundo, nilijigonga kidole na kuumia. Kwa sababu nilikuwa peke yangu, nilianza kulia kwa maumivu. Lakini, wazo lilinijia ambapo nilikumbuka kuhusu simu.

      Baba au mama, mara zote walipokuwa wakitaka kupiga simu, nilikuwa nikiwasikia wakisema, ‘opereta tafadhali.’ Halafu baada ya hapo, wangeuliza au kuomba jambo, ikiwemo kusaidiwa wazungumze na watu fulani.
      Nilitafuta stuli na kupanda juu yake. Halafu niliinua simu na kusema, ‘opereta tafadhali.’ Upande wa pili wa simu ulijibu, ilikuwa ni sauti ndogo ya kike. ‘Ehe nikusaidie nini mwanangu?’ Nilianza kulia, labda kwa sababu, sasa nilisikia sauti ya mtu, yaani niliamua kudeka.

      ‘Nimeumia kwa nyundo, nataka mama aje.’ Ile sauti ya upande wa pili iliniuliza, ‘unatoka damu?’ nilijibu, ‘sitoki damu ila nimeumia,’ Ile sauti ambayo wakati huo sikuwa najua kwamba ni ya operetta ilijibu. ‘kama kuna friji nyumbani, chukua barafu halafu weka kwenye kidole chako, kitapoa tu wala usilie.’ Nilirudisha mkono wa simu na kufanya hivyo.
      Nilikuwa naijua vizuri friji kuliko simu, hivyo sikupata shida. Nilipata nafuu na kujiambia, ‘kumbe hawa maopereta wanajua vitu vingi.’ Kwa hiyo mara kwa mara sasa wazazi wanapokuwa hawapo nyumbani, nikawa nainua mkono wa simu na kumwita opereta, ambapo nilikuwa naongea naye mambo mengi sana. Nilikuwa namuuliza maswali mbalimbali naye akawa anajibu.

      Basi tukazoeana angalau kwa sauti tu, bila kujuana.
      Nakumbuka kuna wakati kasuku wa jirani yetu mmoja mwarabu alikufa. Alikuwa ni kasuku ambaye tulimpenda sana. Alikuwa akijua kuiga sauti hata kuimba. Nilipojua kwamba, kasuku amekufa, niliinua simu na kumwambia opereta juu ya kifo cha kasuku yule. Opereta alisema, ‘kuna dunia nyingine ambapo watu huenda na kuendelea kuimba.’ Nililipenda jibu lake, kwani lilinipa moyo kwamba, kasuku ataendela kuimba huko alikoenda.Nakumbuka nikiwa darasa la pili, siku moja nilimuuliza opereta maana ya ‘kabwela’ Aliniambia kabwela ni mtu anayeamka akiwa hajui atakavyolala. Lakini usiku ukifika hulala. Sikulielewa vizuri jibu lake lakini nililipenda. Wakati huu nilishajua jina la operetta kuwa ni Marry na mimi alishajua jina langu, ingawa tulikuwa hatujawahi kuonana..Wakati huohuo nikiwa la pili, baba alipata uhamisho kwenda mkoani Tanga.

      Nilijua zikiwa zimebaki siku tatu tu kuondoka. Kwa kule kubabaika labda, nilisahau kumwita operetana kumwambia kuhusu kuhama.
      Usikuwa kuamkia siku ya safari ndipo nikakumbuka kuhusu opereta wangu. Kwa kuwa wazazi walikuwepo nyumbani nisingeweza kupiga simu. Niliamua kuchukua picha yangu ambayo nilipigwa shuleni na kuiweka kwenye bahasha. Juu ya bahasha niliandika opereta Marry. Kabla hatujaondoka nilikwenda nyumbani kwa rafiki yangu mmoja tuliyekuwa tukisoma naye darasa moja .Nilipofika nilimkabidhi ile bahasha na kumwomba ampe mama yake aipeleke kwa opereta. Tuliondoka Tabora nikiwa sijui kama operetta yule alipewa bahasha ile au hapana.Siku zikapita na nilisoma na kumaliza kidato cha nne ambapo nilipata kazi au ajira ya moja kwa moja {direct employment} kwenye shirika la reli {TRC} nilipangiwa Tabora kama kituo changu cha awali cha kazi.

      Kwa kweli hali haikuwa nzuri kwa sababu ajira ya moja kwa moja haikuwa nzuri kimaslahi hata kiheshima. Kwa vile pia ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kuwa nje ya nyumbani, nilihuzunika sana.
      Wiki ya pili tu tangu kufika Tabora, nikawa ninataka kupiga simu kwa baba {mama alishafariki}, baada ya kuinua simu nilimuomba opereta. Ajabu ni kwamba, sauti ile niliyoisikia masikioni nilihisi kama sauti niliyowahi kuisikia miaka mingi iliyopita haikuwa ni ngeni kwangu. Kwanza sikuelewa hasa ni kitu gani, lakini baada ya muda nikakumbuka.‘Nini maana ya Kabwela’ nilijikuta nauliza.

      ‘Kama hujaumiza kidole chako kwa nyundo na kasuku wa jirani hajafa , usiniambie uko Tabora,’ ..........nilijihisi nikitetemeka. ‘Mama Marry’ niliita nikiwa kama naota. ‘Ni wewe mwanangu Hussein……’ yule opereta alisema. Ilinichukua muda kujibu.
      Sina haja ya kusema mengi sana, kwani yule mama alinielekeza kwake baada ya kumjulisha kwamba nilikuwa nimepangiwa kazi pale Tabora. Jioni ya siku ile nilikwenda kwake. Kwa mara ya kwanza nilimwona Marry. Hakuwa mtu mzima sana ingawa alionekana kuwa umri umeenda. Lakini kilichonishangaza ni kuona picha yangu ile niliyomtumia ikiwa kwenye fremu nzuri pale ukutani.

      Yeye ndiye aliyeniambia kwamba ilikuwa ni picha yangu, vingenevyo nisingeikumbuka. Lakini kwa nini aliiweka pale. Katika mazungumzo aliniambia kwamba hakuwahi kuwa na mtoto maishani mwake na hivyo kule kumsumbua kwangu kwa maswali kulikuwa kukimpa furaha na faraja sana. Alikuwa akijihisi kama vile nilikuwa mwanaye na alikuwa akifurahia sana hali ile. Kuondoka na kumwachia ile picha, anasema kwamba kulimfanya ahisi kwamba kapoteza mtoto, yaani kafa, hivyo akaamua kuiweka picha yangu kama kumbukumbu.

      Lakini ukweli ni kwamba, mama yule alikuwa amenivutia sana kwa namna alivyokuwa akijibu maswali yangu na kuvumilia usumbufu wangu. Mama yangu mzazi hakuwa na uwezo ule na wala hakuwa nyumbani muda mwingi. Kwa hiyo akawa zaidi ya mama yangu kwa sauti tu. Nilimpa picha yangu kama zawadi pekee ambayo ningeweza kumpa. Nilihamia pale nyumbani kwake nikawa nimepata mama mpya, naye akawa amepata mtoto. Niliamini na bado naamini kwamba, usije ukadhani lolote unalomtendea mtu ni dogo. Liwe ni zuri au baya, lolote unalomtendea mtu, jua linamgusa kwa njia ambayo wewe hujui.

      Kumgusa kwake huja kujirudia moja kwa moja au kupitia njia nyingine na ni lazima litakuumiza au kukusaidia, inategemea tu ulitenda nini. Leo hii hanidanganyi mtu kuhusu wema au ubaya tunaotenda unavyokuja kuturudia katika mazingira ambapo tunakuwa hatujui kabisa. Lakini, nimejifunza maana ya kuwavumilia wengine.

    2. #2
      Purple's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th February 2012
      Location : mjini
      Posts : 1,795
      Rep Power : 730
      Likes Received
      607
      Likes Given
      415

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Hata mie nimejifunza kitu kwenye hadithi hii, asante!
      Mtambuzi likes this.

    3. #3
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,182
      Rep Power : 27035
      Likes Received
      8457
      Likes Given
      17777

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Quote By Purple View Post
      Hata mie nimejifunza kitu kwenye hadithi hii, asante!
      Purple hii siyo hadithi bana, ni mkasa wa kweli........................
      Bujibuji likes this.

    4. #4
      Bazazi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th August 2008
      Location : Mzururaji
      Posts : 1,318
      Rep Power : 816
      Likes Received
      351
      Likes Given
      111

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Quote By Mtambuzi View Post

      Alikuwa ni zaidi ya mama..........

      Lakini ukweli ni kwamba, mama yule alikuwa amenivutia sana kwa namna alivyokuwa akijibu maswali yangu na kuvumilia usumbufu wangu. Mama yangu mzazi hakuwa na uwezo ule na wala hakuwa nyumbani muda mwingi.
      Mtambuzi hivi visa umevihifadhi wapi jamani? Ni zao tena la Jitambue? Kweli Munga Tehenan alikuwa kiboko. Namkumbuka sana katika gazeti la majira "Mzee wa nepi" Gazeti la Dunia na mwisho JItambue & Mshauri. Kama ulikuwa mdau hebu yarudisheni magezeti hayo.

      Kongosho
      Zinduna, gfsonwin FirstLady, MwanajamiiOne na wakinamama wengine wa JF mmeona umuhimu wa kukaa na watoto wenu na kuongea nao kwa upendo? Ni muhimu sana katika makuzi ya watoto.

      Bazazi!
      Bibie! Usijisifu Kuwa Una Mimba: Msifie Aliyekupa Mimba.

    5. #5
      Mr Rocky's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th October 2007
      Location : Hungumalwa
      Posts : 9,706
      Rep Power : 68642
      Likes Received
      7079
      Likes Given
      5587

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Mtambuzi asante sana kwa kisa hiki
      Kweli inapaswa kukaa na watoto karibu na kujua hisia zao na nini wanachohitaji
      Ni fundisho zuri sana mkuu
      Asante sana
      When you are in Love you can't fall asleep because reality is better than your dreams

    6. #6
      Mukalunyoisa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 16th March 2012
      Posts : 139
      Rep Power : 393
      Likes Received
      19
      Likes Given
      2

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      leo nimejifunza kitu hapa, sie ndo akina mama kila tunaporudi majumbani watoto wamelala
      Mtambuzi likes this.

    7. #7
      FirstLady1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th July 2009
      Location : Mama Mwenye Nyumba
      Posts : 15,046
      Rep Power : 3721
      Likes Received
      3618
      Likes Given
      5870

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Asante sana Mzee Mtambuzi barikiwa zawadi yako inakija by DHL
      Mtambuzi likes this.
      No one is in charge of your happiness except you...
      God time is the best..
      Hadi tufike 2015 tutakuwa tumekoma

    8. #8
      platozoom's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th January 2012
      Posts : 4,081
      Rep Power : 8294
      Likes Received
      2767
      Likes Given
      3788

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Quote By Bazazi View Post
      Mtambuzi hivi visa umevihifadhi wapi jamani? Ni zao tena la Jitambue? Kweli Munga Tehenan alikuwa kiboko. Namkumbuka sana katika gazeti la majira "Mzee wa nepi" Gazeti la Dunia na mwisho JItambue & Mshauri. Kama ulikuwa mdau hebu yarudisheni magezeti hayo.

      Kongosho
      Zinduna, gfsonwin FirstLady, MwanajamiiOne na wakinamama wengine wa JF mmeona umuhimu wa kukaa na watoto wenu na kuongea nao kwa upendo? Ni muhimu sana katika makuzi ya watoto.

      Bazazi!
      Kongosho muda wote yupo na konyagi watoto anaongea nao saa ngapi, Zinduna yuko bize na Talk show, FirstLady anaponya majeraha ya rafiki yake muda anautoa wapi kukaa na watoto, MwanajamiiOne yeye mawazo ya kuumizwa bado yanamsumbua muda haha, gfsonwin mmmh naogopa kusema.
      Bazazi, Mtambuzi, Kongosho and 1 others like this.
      "Education is something that remain in your head after forgeting what you learn at school"

    9. #9
      platozoom's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th January 2012
      Posts : 4,081
      Rep Power : 8294
      Likes Received
      2767
      Likes Given
      3788

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Kisa kizuri sana, nimemkumbuka mama yangu (R.I.P) Alitupenda sana.....Nakumbuka katika zile nyakati baba hana kazi alivyokuwa anapanga bajeti sijapata kuona hata katika wizara zetu. Mpole japo mboko zake nilikula, baadaye anakubembeleza kula. Kwake watoto wake lilikuwa ni chaguo la kwanza.

      Nakukumbuka sana mama.
      "Education is something that remain in your head after forgeting what you learn at school"

    10. #10
      gfsonwin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 12th April 2012
      Posts : 11,274
      Rep Power : 34404
      Likes Received
      10492
      Likes Given
      14558

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Quote By Bazazi View Post
      Mtambuzi hivi visa umevihifadhi wapi jamani? Ni zao tena la Jitambue? Kweli Munga Tehenan alikuwa kiboko. Namkumbuka sana katika gazeti la majira "Mzee wa nepi" Gazeti la Dunia na mwisho JItambue & Mshauri. Kama ulikuwa mdau hebu yarudisheni magezeti hayo.

      Kongosho
      Zinduna, gfsonwin FirstLady, MwanajamiiOne na wakinamama wengine wa JF mmeona umuhimu wa kukaa na watoto wenu na kuongea nao kwa upendo? Ni muhimu sana katika makuzi ya watoto.

      Bazazi!
      Bazazi kaka yangu wa moyoni unalolisema ni kweli kabisa aisee. na hata Mtambuzi anatukumbusha mambo muhimu sana katika maisha yetu ya kila sku. Unajua wazazi wengi huwa tuna underestimate umuhimu wa kuongea na wanetu na kuwasikiliza kirafki ila ukitaka kujua gharama ya kutokumsikiliza mtoto wako uwe mzazi ama mlezi basi muulize mtu ambaye analea mtoto ambaye hakuwahi kusikilizwa hivyo walimwengu wakamsikilizisha.
      "thought takes man out of servitude into freedom"
      'daima tudumu katika upendo'

    11. #11
      gfsonwin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 12th April 2012
      Posts : 11,274
      Rep Power : 34404
      Likes Received
      10492
      Likes Given
      14558

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      [QUOTE=platozoom;4136568]Kongosho muda wote yupo na konyagi watoto anaongea nao saa ngapi, Zinduna yuko bize na Talk show, FirstLady anaponya majeraha ya rafiki yake muda anautoa wapi kukaa na watoto, MwanajamiiOne yeye mawazo ya kuumizwa bado yanamsumbua muda haha, gfsonwin mmmh naogopa kusema.[/QUOamTE]

      platozoom am a responsible mother, wife and a lady for my family aisee. Hata kama nitakuwa natoa mfyonzo but nahakikisha it is doens't cost my kids or anyone else at my family.

      my brother your family is the only priceless asset you have under the sky, and to me that is the only thing which gives me pleasure and joy.
      Mtambuzi and platozoom like this.
      "thought takes man out of servitude into freedom"
      'daima tudumu katika upendo'

    12. #12
      Candy kisses's Avatar
      Member Array
      Join Date : 4th June 2011
      Posts : 46
      Rep Power : 416
      Likes Received
      9
      Likes Given
      1

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Dah kisa kizuri sana,
      Mtambuzi likes this.

    13. #13
      Kongosho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2011
      Location : Location loading...
      Posts : 26,156
      Rep Power : 25447
      Likes Received
      14873
      Likes Given
      15811

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Quote By platozoom View Post
      Kongosho muda wote yupo na konyagi watoto anaongea nao saa ngapi, Zinduna yuko bize na Talk show, FirstLady anaponya majeraha ya rafiki yake muda anautoa wapi kukaa na watoto, MwanajamiiOne yeye mawazo ya kuumizwa bado yanamsumbua muda haha, gfsonwin mmmh naogopa kusema.

      Wee acha tu, wakiona komputa wanaanza kulalamika, yaani mama anacheka na komputa tu lol
      Anyway, tutafika tu
      Quote By Bazazi View Post
      Mtambuzi hivi visa umevihifadhi wapi jamani? Ni zao tena la Jitambue? Kweli Munga Tehenan alikuwa kiboko. Namkumbuka sana katika gazeti la majira "Mzee wa nepi" Gazeti la Dunia na mwisho JItambue & Mshauri. Kama ulikuwa mdau hebu yarudisheni magezeti hayo.

      Kongosho
      Zinduna, gfsonwin FirstLady, MwanajamiiOne na wakinamama wengine wa JF mmeona umuhimu wa kukaa na watoto wenu na kuongea nao kwa upendo? Ni muhimu sana katika makuzi ya watoto.

      Bazazi!
      Yaani Bazazi, mama mwenyewe ni bazazi, hata ya kuwaambia watoto yapo?
      Anyway, wanakua kwa nguvu za Mwenyezi tu
      Mtambuzi and platozoom like this.
      No matter how hot your anger is, it can not cook yams-Nigeria

    14. #14

    15. #15
      PetCash's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th March 2012
      Location : searching....
      Posts : 642
      Rep Power : 562
      Likes Received
      351
      Likes Given
      104

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Sina mengi ya kuongea; 'U made my day in learning-wise'
      Mtambuzi likes this.
      You are what you eat

    16. #16
      Tangawizi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th June 2009
      Posts : 943
      Rep Power : 696
      Likes Received
      188
      Likes Given
      184

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Thanks Mtambuzi kwa hadithi hii nzuri
      "Carpe Diem...Seize the Day"

    17. #17
      platozoom's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th January 2012
      Posts : 4,081
      Rep Power : 8294
      Likes Received
      2767
      Likes Given
      3788

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      platozoom am a responsible mother, wife and a lady for my family aisee. Hata kama nitakuwa natoa mfyonzo but nahakikisha it is doens't cost my kids or anyone else at my family.

      my brother your family is the only priceless asset you have under the sky, and to me that is the only thing which gives me pleasure and joy.[/QUOTE]

      Mtu akisema hivi huwa namuona kama mzee!......vijana wa siku hizi mmh
      Mtambuzi likes this.
      "Education is something that remain in your head after forgeting what you learn at school"

    18. #18
      HorsePower's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd August 2008
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 2,783
      Rep Power : 3826
      Likes Received
      1760
      Likes Given
      1626

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Quote By Mtambuzi View Post

      Alikuwa ni zaidi ya mama..........

      Lakini ukweli ni kwamba, mama yule alikuwa amenivutia sana kwa namna alivyokuwa akijibu maswali yangu na kuvumilia usumbufu wangu. Mama yangu mzazi hakuwa na uwezo ule na wala hakuwa nyumbani muda mwingi. Kwa hiyo akawa zaidi ya mama yangu kwa sauti tu. Nilimpa picha yangu kama zawadi pekee ambayo ningeweza kumpa. Nilihamia pale nyumbani kwake nikawa nimepata mama mpya, naye akawa amepata mtoto. Niliamini na bado naamini kwamba, usije ukadhani lolote unalomtendea mtu ni dogo. Liwe ni zuri au baya, lolote unalomtendea mtu, jua linamgusa kwa njia ambayo wewe hujui.

      Kumgusa kwake huja kujirudia moja kwa moja au kupitia njia nyingine na ni lazima litakuumiza au kukusaidia, inategemea tu ulitenda nini. Leo hii hanidanganyi mtu kuhusu wema au ubaya tunaotenda unavyokuja kuturudia katika mazingira ambapo tunakuwa hatujui kabisa. Lakini, nimejifunza maana ya kuwavumilia wengine.
      Mtambuzi hapo penye bold pamenigusa sana. Laiti tungelikuwa na uwezo wa kuyasoma haya yote na kuyafanyia kazi naamini jamii yetu ingeishi kwa amani sana.
      Thanks kwa makala nzuri.
      Mtambuzi likes this.
      Don’t judge each day by the harvest you reap but by the seeds that you plant.

    19. #19
      cacico's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th March 2012
      Location : DSM
      Posts : 7,117
      Rep Power : 14537
      Likes Received
      6473
      Likes Given
      5043

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      NICE STUFF BABU Mtambuzi! nitakuwa nawasikiliza na kuwavumilia kwa utundu wao kha!
      Mtambuzi and Bujibuji like this.
      "the problem is not me! the problem is you understading me!"

    20. #20
      Eiyer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th April 2011
      Posts : 8,961
      Rep Power : 6904
      Likes Received
      2747
      Likes Given
      36

      Default Re: Sikuamini kama ni yeye………!

      Nimehisi uchungu sana hasa kwa mimi ambae sijalelewa na mama yangu mzazi!
      Mtambuzi likes this.

    Page 1 of 3 123 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...