ULIMTAMBUA VIPI KUWA HUYU NDIYE MWENYEWE….. (Getting to know her/him)
Hivi mwandani wako ulimtambuaje kuwa ndiye yeye?
Hivi ni maujanja yepi wewe uliyatumia kumpima yeye?
Ni vigezo vipi vilikutongoza hadi kujua umelamba dume?
Hivi ni vichocheo vipi vilikufanya uone ya kuwa umewasili? Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu
Kauli yake mwenyewe huitia kitanzini na kuishibisha azma zake!
Aongeacho mara nyingi sicho kilichopo moyoni kwake wala!
Tabasamu lake lalenga kuijenga kauli ambayo si lazima iwe na kweli!
Kamwe kauli au hata tabasamu lake kuwa kioo cha moyo wake! Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu
Kauli na taswira yake huoana na moyo wake masijala ya kukataa…
Pindi moyo wake umekuasi kata katu basi shabaha wewe hulengwa…
Bila haya au huruma jipu kukupasulia kuwa hakuhitaji nawe kulia..
Na kwa kufanya hivyo huwa kajitendea mwenyewe ubinadamu.. Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu
Ni mitihani ipi uliitumia kuupima moyo wake?
Hata kuridhia yeye ndiye na hakuna mwingineo?
Kama ulienda mkichamkichwa basi ilikula kwako!
Kama uliserereka na kauli au taswira basi wewe teja! Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu
Last edited by Rutashubanyuma; 27th June 2012 at 09:17.
Reason: paragraphing
Remmy mbona mada tayari iko mezani.....................kub wa chunguza moyo wake na usikubali hadaa za kauli au hata hisia za usoni kwake kwai hizo zimo ndani ya uwezo wake wa kukupeleka kusiko..................
Nitautambuaje huo moyo Ruta? Umejificha na watu tunaweza sana kupretend.
Mila na desturi haziniruhusu kuongelea haya mambo ya ni jinsi gani au ni nini kilinivutia kwa mtani wa jadi. Ila kwa taarifa tu ningepata fursa ya kuchagua upya ningechagua yuleyule na hii ni zaidi ya miaka kumi na mbili baada ya kufanya uchaguzi wa awali.
mie alikuwa kama sio kunipigia basi atanitext asubuhi,na kuniuliza nimeamkaja...siku njema etc,na jioni hivyo hivyo ataniuliza nimeshindaje nilale salama,kimbembe ilikuwa nikose simu yake/text mbona naumwa kabisaaaa..hivyo nikajua huyu ndie niliyetoka katika ubavu wake,ukimpata anayekupenda utajua tu ni raaaaaaaaaaaaaaaaaaahhhhhhhhhh hhhhhhhhhaaaaaaaaaaaaaa
mie alikuwa kama sio kunipigia basi atanitext asubuhi,na kuniuliza nimeamkaja...siku njema etc,na jioni hivyo hivyo ataniuliza nimeshindaje nilale salama,kimbembe ilikuwa nikose simu yake/text mbona naumwa kabisaaaa..hivyo nikajua huyu ndie niliyetoka katika ubavu wake,ukimpata anayekupenda utajua tu ni raaaaaaaaaaaaaaaaaaahhhhhhhhhh hhhhhhhhhaaaaaaaaaaaaaa
cacico kama mwenye hivyo vidole ni huyohuyo mwenye macho ya hiyo avatar yako sishangai kumwona Rogi akihitaji aone zaidi juu ya hivyo vidole vyako........................l ol
ndiye mwenyewe haswaaaaa! Rogi sasa hivi tunawasiliana PM kwa sana, atakupa results but shshshsh polepole Young_Master asisikie!
cacico hongera sana mie am still looking..................and searching these hearts for heartstrings...........to no avail, so far.................but still busier than ever before............
basi ungeniambia hata yule tu aliyedai umuongezee matumizi ya mtoto ulimpataje, just lidogo tu kha! au hata wa ujanani ulimuadmire kwa lipi?? tel us kidogo!
Follow Us Here