Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

    Report Post
    Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 116
    1. #1
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8245
      Likes Given
      17377

      Default Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!


      Nikakabidhiwa mwali niondoke naye.................
      (Picha haihusiani na habari hii)

      Hili ni tukio ambalo lilikimbiza jijini Dar mwaka 1987, ikiwa ni mwaka mmoja tangu nitie timu hapa mjini ili kujiunga na shule ya sekondari baada ya kumaliza elimu ya msingi huko kijijini.

      Nilikuja mjini na kufikia kwa kaka yangu maeneo ya Magomeni Makanya. Pale mtaani kulikuwa na mzee mmoja alikuwa na mziki wa kukodisha na jenereta, ilikuwa kila inapotokea kuna shughuli ya kumtoa mwali au harusi watu wakija kukodi ule mziki, mimi nilikuwa ni mmoja wa vijana ambao tulikuwa tunaenda na huo mziki kama mafundi mitambo.

      Kutokana na kiherehere changu, nilikuwa nimejichomeka na kuwa mmoja wa wadau wa kupigisha mziki mpaka nikajijengea jina kwa yule mzee. Ikitokea yule kijana aliyekabidhiwa hupo mziki na huyo mzee hayupo, nilikuwa napewa mie mikoba ya kwenda kupigisha mziki huko ulipokodishwa.

      Kama mnakumbuka kipindi hicho kulikuwa hakuna CDs, ilikuwa ni kanda za kaseti ambazo tunazirekodi miziki kulingana na uhitaji wa shughuli mbalimbali, hata haya mambo ya jingo na vijembe kulikuwa hakuna zaidi ya kutumia taarabu, au mchiriku kulinga na shughuli yenyewe.

      Ilitokea siku moja mziki ulikodishwa kwenye shughuli ya kumtoa mwali huko Ununio, na hivyo kama kawaida siku ya Ijumaa tukaondoka na pick up yetu hadi Ununio na kufunga mziki wetu, tukiwa na jenereta letu, kwani kipindi hicho Ununio kulikuwa hakuna umeme. Ununio ipo njia ya kwenda Bagamoyo.


      Tulikuwa na mazoea ya kujitwalia vibinti na kuvibanjua tutakavyo kila shughuli ya kumtoa mwali tunayokwenda na hiyo ndiyo iliyonifanya niipende sana kazi hiyo na kusahau shule ambayo ndiyo iliyonileta mjini. Nakumbuka kaka yangu alikuwa ananigombeza sana na kunionya niachane na mambo ya Kiswahili lakini haikuniingia akilini. Kijana rijali damu ilikuwa inachemka na umri wa ubaruaru ndio ulikuwa umeshika kasi, utaniambia nini.

      Ilikuwa kama naenda ngomani mpaka zile siku tatu za shughuli zikiisha naweza kujikuta nimebanjua vibinti visivyopungua vitatu mpaka vitano tena kavu kavu, bila kondom, kitu ambacho ninahisi huenda nimeacha utitiri wa watoto huko Uzaramoni. Nashukuru ukimwi ulikuwa haujashika kasi maana ningeshakufa zamaani na JF msingenijua. Tulikuwa tunagombewa kweli, maana tumetoka mjini na ile kuwa mpigisha mziki ilikuwa ni bonge la CV kujipatia vimwana na kujivinjari utakavyo bila hata kuhonga.

      Tulipofika Ununio tulipokewa vizuri na mwenyeji wetu mwenye shughuli ya kumtoa mwali alikuwa ana uwezo si haba kwani alikuwa na nyumba tatu, pale kijijini na wake zake watatu. Tukapangiwa kila mtu mahali pake pa kulala ambapo, mimi nililala kwenye nyumba ya mke mdogo ambapo ni mbali kidogo na nyumba ambayo ilikuwa inafanyika shughuli hiyo na wenzangu walilala kwenye nyumba ya mke mwingine mdogo wa mzee huyo kwa kuwa ilikuwa na vyumba vingi. Shughuli yenyewe ilifanyikwa kwa mke mkubwa.

      Siku ya kwanza ya shughuli sikwenda kulala kule nilikopangiwa kwani nilipata kabinti fulani na nilipata mwenyeji pale pale akanipa ghetto nikajipigia mpaka asubuhi huku wenzangu wakikesha ngomani. Asubuhi nilikwenda kujipumzisha kule nilipopangiwa kulala, na nilipofika nikakuta binti mmoja mzuri kweli. Baada ya kumdadisi aliniambia kwamba ni mdogo wake na mke wa yule mzee. Nilimpenda kweli na nikajisemea moyoni, lazima nimlambe. Alionekana amelelewa kwenye maadili kweli maana alikuwa na ile heshima ya kijijini na pia alikuwa na staha.

      Nilishinda pale nyumbani kutwa nikipiga naye stori na nilitumia muda huo kujifagilia kwamba ule mziki ni wa kwangu nililetewa na kaka yangu aliyekwenda masomoni Japan. Nilimdanganya kwamba ninamiliki nyumba mbili jijini Dra zikiwemo daladala 3 aina ya Isuzu Journey nilizotumiwa na kaka yangu kutoka Japan. Yule binti alionekana kuniamini kweli, na hiyo ikawa na nafasi kwangu kumtongoza na hakuonekana kuwa mgumu nikawa nimemnasa njiwa tunduni.

      Tulikubaliana tukienda ngomani aseme anajisikia vibaya ili arudi nyumbani, iwe ni nafasi nzuri kwangu kwenda kujivinjari naye pale pale kwao. Alionekana kufurahia wazo langu kwani awali alisema ingekuwa ngumu mtoto wa dada yake anachezwa ngoma halafu yeye asiwepo kukesha na dada yake.
      Usiku kama kawaida nilifika ngomani na kuanza kupigisha mziki na niliwadokeza wenzangu kuwa nitaondoka mapema na kwa sababu ilikuwa ni Jumapili siku ya mwisho ya shughuli ilikuwa ina shamra shamra nyingi na kulikuwa na dalili ya kukesha mpaka asubuhi.

      Nilimuona yule binti akipita na dada yake mke wa yule mzee mwenyeji wetu. Yule dada yake aliniangalia sana kisha akawa anatabasamu, sikuelewe ni kitu gani kinaendelea. Niliendelea kupigisha mziki na ilipofika mida ya saa sita usiku kakaja kabinti kamoja na kuniambia kwamba naitwa nimfuate. Nilikafuata hadi upenuni mwa ile nyumba ya shughuli, nilipofika pale nilimkuta yule binti na aliniambie tuondoke.

      Nilikwenda kuwaaga wenzangu na kuondoka na yule binti, tulipofika akanipeleka chumbani kwake ambapo aliniandalia chakula nikala kisha tukalala. Asubuhi nilishtuliwa na mlango ukigongwa kwa nguvu. Nilishtuka sana na nilimuona yule binti akiwa hana wasiwasi. Alijizoazoa pale kitandani na kwenda kufungua mlango na kutoka nje na kufunga mlango kwa nje. Nilisikia watu wakiongea huko nje na mmoja wa watu hao alikuwa ni yule mzee mwenyeji wetu.

      Baada ya muda yule binti alirudi akiwa amejitanda kanga kisha akaniambai nivae kuna wageni wanataka kuingia kunisalimia. Nilishtuka sana na nilivaa haraka haraka. Baaada ya kuvaa yule binti alifungua mlango na mara nikamuona mwenyeji wetu akiingia na wazee wanne na kina mama watatu na mkeka na chetezo cha ubani. Kwa akili yangu ya wanzuki mie sikajua labda wanataka tu kusoma dua kwa ajili ya ile shughuli hivyo nikanyanyuka ili nitoke. Nilizuiwa pale mlangoni na kuambiwa kuna kikao kidogo. Nilikaa na sikuwa na wasiwasi.

      Yule mzee alianza kuwambia wale wenzake aliofuatana nao……

      “Wazee wenzangu samahanini sana kwa kuwakurupusha kuja kukamilisha jambo hili la muunganiko wa watu wawili kati ya mtu mume na mtu mke, kama Kurani tukufu ilivyotuusia kwamba tusiikurubie zinaa, na hivyo basi huyu bwana hapa nimemfuma akizini na shemeji yangu na kwa mujibu wa dini yetu ya kiislamu mimi kama mlezi siwezi kuingia katika dhambi hivyo nimeona nihalalishe kabisa niwafungishe ndoa……”

      Muda wote wakati yule mzee anazungumza mimi nilikuwa kama ninaota na nilikuwa siamini kile kinachotaka kunitokea. Nilianza kuwaza, nitampeleka wapi mimi huyu binti wakati mie kula kulala na bado ninasoma.

      “Samani wazee mimi sijazini wala nini, nililetwa hapa na huyu mzee kwenye shughli ya kuwatoa mabinti zake na baada ya uchovu nilikuja kujipumzisha hapa kama nilivyoelekezwa na mke wa huyu mzee……….” Nilijikakamua na kujitetea…

      Yule mzee alinikata kalma na kuwaambia wale mashehe kwamba ni kweli alinipangia nilale pale lakini chumba alichoniandalia ni cha nje na si cha ndani. Hicho chumba nilicholala ni cha shemeji yake ambaye ndiye niliyefumaniwa naye. Wale mashehe wakasema wasipotezewe muda na niliamriwa nikae kwenye mkeka nifungishwe ndoa niondoke na mke wangu.

      “Wazee wangu naomba mnisamehe kwani mie bado mwanafunzi na nikakaa kwa kaka yangu na sina hata uwezo wa kujitegemea…..”
      Nilijitetea ili kujinusuru na ndoa ile ya fedheha.

      Yule dada yake na binti niliyefumaniwa naye akadakia……
      Si wewe ulomwaambia mdogo wangu kwamba una nyumba mbili Dar na daladala tatu, sasa habari ya kusoma na kwamba huna uwezo wa kuishi na mke inatoka wapi? Tena ulimuahidi utamuoa, sasa tatizo liko wapi, wewe ondoka naye utatuletea mahari yetu hata mwakani.” Kusikia hivyo, nikajua nkondo igwa. Jasho lilinitoka.

      Wakati wote wa kadhia hiyo nje kulijaa umati wa watu waliokesha kwenye ngoma na wale wenzangu niliokuja nao walikuwa hapo nje wananisubiri ili tuondoke.

      Nikiwa bado nimeduwaa, ubani ulichomwa na ndoa ikafungwa, lakini muda wote mwili wangu ulikuwa umekufa ganzi na sikuelewa kinachoendelea kabisa kwani chaneli zikikata.

      Baada ya dua nilisikia huko nje mdundiko ukipigwa na watu wakicheza kwa kwa furaha na nyimbo za vijembe zikitawala. Mwanaume lilinishuka shuu………

      Nilitolewa nje nikiwa nimefunikwa kwa kanga na mke wangu huku nikisindikizwa na vigelegele. Yule mwenyeji wetu aliagiza pick up yetu isogezwe ili maharusi tupande na safari ya kurudi Dar ianze.

      Niliposikia hivyo nilipata fahamu, nilichomoka hapo mbio hata wale waliojaribu kunikimbiza waliambulia vumbi. Hata sikumbuki nilifikaje barabarani maana kijiji chenyewe kipo mbali kidogo na barabara. Nilipanda basi na kurudi Dar. Nilipofika nilikushanya nguo zangu na kukimbilia Keko Magurumbasi kwa mjomba wangu. Pale nilikaa siku tatu baada ya kupata nauli nilirudi kijijini kujipanga upya…………..

    2. Miaka 50

    3. #21
      mashambaJr's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th May 2012
      Location : Loading....
      Posts : 368
      Rep Power : 426
      Likes Received
      58
      Likes Given
      27

      Default

      Quote By Mtambuzi
      Nilimpotezea mkuu, si unajua maisha ya ujana kizungumkuti...............!
      kweli Ujana ulikusumbua,lakini ulifanya kitu kibaya ulimuachia Mkosi Binti wa Watu.
      Mtambuzi likes this.

    4. #22
      Bishanga's Avatar
      JF Tanzanite Member Array
      Join Date : 29th June 2008
      Location : SIRIUS
      Posts : 13,399
      Rep Power : 33554
      Likes Received
      8073
      Likes Given
      7565

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Quote By Mtambuzi
      Kwa hiyo nikikuta kaolewa naweza kum sue mtu kwa kumuoa mke wangu halali wa ndoa ya mkeka eh, yaweza kuwa dili hiyo au?
      ndoa ni ndoa tu mkuu,mradi ilikuwa solemnized,guy you are legally married to her!
      Mtambuzi likes this.
      THE WEAK NEVER FORGIVES,THE STRONG ALWAYS DO.....Mahatma Ghandi.

    5. #23
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8245
      Likes Given
      17377

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Quote By elly_black
      kweli Ujana ulikusumbua,lakini ulifanya kitu kibaya ulimuachia Mkosi Binti wa Watu.
      Nimetubu zile zambi zangu zote na sasa nimezaliwa upya kabisa..................
      cacico likes this.

    6. #24
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8245
      Likes Given
      17377

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Quote By Bishanga
      ndoa ni ndoa tu mkuu,mradi ilikuwa solemnized,guy you are legally married to her!
      No siwezi kumrudia yule mwanamke, nadhani atakuw amzee hivi sasa, hata hivyo I am Happly Married mama Ngina wange......

    7. #25
      Mbimbinho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st August 2009
      Posts : 1,834
      Rep Power : 865
      Likes Received
      470
      Likes Given
      210

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Quote By Mtambuzi
      Kwa hiyo nikikuta kaolewa naweza kum sue mtu kwa kumuoa mke wangu halali wa ndoa ya mkeka eh, yaweza kuwa dili hiyo au?
      Kisheria una haki aisee, ila kiuhalisia haijakaa njema (Hivi kum-abandon family ni kosa kisheria? if Yes, then wataku-sue wewe sasa)
      Mtambuzi likes this.
      Mbwa ukimjua jina wala hakupi shida....

    8. RukaaJuu Final

    9. #26
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8245
      Likes Given
      17377

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Quote By Mnama
      Ha haaaa hii kali ,ulikuwa mkali sana mkuu ugenini lakini unakomaa nayo mwanzo mwisho mpaka kucheee...
      Mnama unajua vibinti vya vijijini vitamu kweli maana ni halisi kabisa, wenyewe tunaita kuku wa kienyeji, havina kalikiti, mikorogo wala pafyum, unapata ile harufu halisi ya mwili wa binadamu, ukikutana navyo unaweza kusahau kwenyu.................

    10. #27
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8245
      Likes Given
      17377

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Quote By Mbimbinho
      Kisheria una haki aisee, ila kiuhalisia haijakaa njema (Hivi kum-abandon family ni kosa kisheria? if Yes, then wataku-sue wewe sasa)
      Mbimbinho mh, bora niuchune maana sijatafutwa na nadhani wameshanisahau.............
      Isije ikawa kuna ndugu yake humu JF..................LOL
      Mbimbinho and gfsonwin like this.

    11. #28
      HorsePower's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd August 2008
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 2,658
      Rep Power : 3798
      Likes Received
      1673
      Likes Given
      1495

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Mtambuzi, nafikiri unatakiwa kuwa mwalimu wa malezi, maana ujanani kwako umezunguka mno na umekumbwa na mikasa mingi ya kimaisha na kimapenzi, hivyo una experience ya kutosha kushauri vijana. Nahisi lolote unalolisikia sasa la kimaisha ni kama marudio kwako, loh!
      Mtambuzi likes this.
      Don’t judge each day by the harvest you reap but by the seeds that you plant.

    12. #29
      King'asti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th November 2009
      Location : The Jungle
      Posts : 17,234
      Rep Power : 28912
      Likes Received
      11714
      Likes Given
      4819

      Default

      Mie naomba kuuliza na sio kuchangia kiduchu dingi, I promise sitamuambia mama.

      Where was I conceived?
      Quote By Mtambuzi
      Cantalisia, King'asti, Asnam, mbalu, TaiJike, cacico, Erotica na FirstLady1 marufuku kuchangia huu uzi,
      Mkithubutuuu, mtanitambua................... ...LOL

    13. #30
      Mbimbinho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st August 2009
      Posts : 1,834
      Rep Power : 865
      Likes Received
      470
      Likes Given
      210

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Quote By Mtambuzi
      Mbimbinho mh, bora niuchune maana sijatafutwa na nadhani wameshanisahau.............
      Isije ikawa kuna ndugu yake humu JF..................LOL
      Hahahahaa, mara unaona pm za kukualika pub flani zimekuwa nyingi, ile unafika tu unashangaa unakumbatiwa., kazi kweli kweri..!
      Mtambuzi likes this.
      Mbwa ukimjua jina wala hakupi shida....

    14. #31
      toghocho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th March 2011
      Location : here here
      Posts : 1,000
      Rep Power : 615
      Likes Received
      138
      Likes Given
      29

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      hahahahaha, mtambuzi unatisha mkuu...kwahiyo dar lini tena?
      Mtambuzi likes this.

    15. #32
      Asabaya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th February 2012
      Posts : 619
      Rep Power : 490
      Likes Received
      127
      Likes Given
      21

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Mtume mbavu zangu! unko umenichekesha leo,hicho kisa kilimtokea mdogo wangu alikwenda tanga kusalimu bibi akajifanya kidume yakamkuta hayo hayo lakini yeye hakueza kukimbia ilibidi mke akaekwa kwa bibi baada ya miezi miwili akampa talaka yake.
      Mtambuzi likes this.

    16. #33
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8245
      Likes Given
      17377

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Quote By King'asti
      Mie naomba kuuliza na sio kuchangia kiduchu dingi, I promise sitamuambia mama.

      Where was I conceived?
      King'asti wewe unatafuta laana ya mchana sasa,......... maswali gani hayo sasa unaniuliza hadharani....................
      Nikisikia mama yangu ananipiga vijembe kwa kuimba Kizaramo, nitajua umeshasema umbea, nitakuchapa ujinga ukutoke..... LOL
      Rutashubanyuma likes this.

    17. #34
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8245
      Likes Given
      17377

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Quote By toghocho
      hahahahaha, mtambuzi unatisha mkuu...kwahiyo dar lini tena?
      Weweee nilirudi Town mwaka 1990 nikiwa nimebadilika kabisa kitabia.................... toghocho

    18. #35
      figganigga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th October 2010
      Location : dar es salaam
      Posts : 8,210
      Rep Power : 12015
      Likes Received
      2663
      Likes Given
      1584

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Hii imenikumbusha enzi namaliza o-level pale Ihungo Bukoba. Siku ya sherehe tukiliita bogy alikuja kupiga Bonge na vyomba vyake vya pamba musics sound.
      Baada ya mziki kuna kademu nilikua nacheza nako kutoka rugie(rugambwa sec) ikabidi nikatoroshe.
      tukala chochoro hadi kyaruyonga, tukashuka omumwani tukaibukia rwamishenye. deal ilikua ni kwenda guest ambayo ipo karibu na shule yao ili saa tisa usiku aingie room. tukapata chumba pale maeneo ya tanesco kibeta. tulilala kushituka saa nne asubuhi..P.T.O. mia
      Mtambuzi likes this.

    19. #36
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8245
      Likes Given
      17377

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Quote By Asabaya
      Mtume mbavu zangu! unko umenichekesha leo,hicho kisa kilimtokea mdogo wangu alikwenda tanga kusalimu bibi akajifanya kidume yakamkuta hayo hayo lakini yeye hakueza kukimbia ilibidi mke akaekwa kwa bibi baada ya miezi miwili akampa talaka yake.
      Asabaya ngoja na mie nipeleke talaka , maana naweza kuibukiwa na vitoto vya wababa wengine niambiwe ni vya kwangu.............
      Unajua sie wanaume tunafanya ukware halafu hatuangalii nyuma, ndio maana nina nidhamu hata humu JF, maana miaka hiyo ya 80, kama niliacha mimba huko uzaramoni, maana nilivuruga Mzenga yote, Kazimzumbwi, Mkuranga, Visiga, Kisarawe, Bonyokwa Pugu enzi hizo ni porini kweli, isije ikawa napigana vikumbo na wanangu mitaani na humu JF...........LOL

    20. #37
      King'asti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th November 2009
      Location : The Jungle
      Posts : 17,234
      Rep Power : 28912
      Likes Received
      11714
      Likes Given
      4819

      Default

      Sasa ukileta kutishiana utaharibu dingi. Niambie tu nilikuwa conceived kwenye ngoma gani. Haiwezekani nikawa sina akili shule kiasi hichi!
      I demand to know kabla sijaita kikao cha ukoo
      Quote By Mtambuzi
      King'asti wewe unatafuta laana ya mchana sasa,......... maswali gani hayo sasa unaniuliza hadharani....................
      Nikisikia mama yangu ananipiga vijembe kwa kuimba Kizaramo, nitajua umeshasema umbea, nitakuchapa ujinga ukutoke..... LOL
      Mtambuzi likes this.

    21. #38
      mashambaJr's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th May 2012
      Location : Loading....
      Posts : 368
      Rep Power : 426
      Likes Received
      58
      Likes Given
      27

      Default

      Quote By Mtambuzi
      Nimetubu zile zambi zangu zote na sasa nimezaliwa upya kabisa..................
      Hapa kwenye nyekundu,inamaanisha ukiendelea kugrow utarudi hali yako ya zamani.
      Au niko nje na mtazamo wako kuhusu kuzaliwa upya?
      Mtambuzi likes this.

    22. #39
      FirstLady1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th July 2009
      Location : Mama Mwenye Nyumba
      Posts : 14,976
      Rep Power : 3704
      Likes Received
      3582
      Likes Given
      5771

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      Mtambuzi naomba kujua kama hili tukio ni la kweli hahahah maana nimebakia mdomo wazi
      Baba miaka ile ulikuwa hukamatiki ..naona vijana wa sasa wanafanya marudio tu..
      Mtambuzi and Rutashubanyuma like this.
      No one is in charge of your happiness except you...
      God time is the best..

    23. #40
      mtotowamjini's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2012
      Location : None of Your Business
      Posts : 4,533
      Rep Power : 1263
      Likes Received
      1109
      Likes Given
      28

      Default re: Nikapigwa ndoa ya mkeka Ununio…!

      wewe lazima utakua mwandishi wa habari au unaandikaga vitabu maana topic zako ndefu mno alafu kama huja copy n paste mahali inaonyesha ni jinsi gani una muda mwingi wa kukaa chini na kuandika gazeti lote hilo...lakini unajitahidi siwezagi kusoma posts zako coz ni ndefu sana bt am sure zina ujumbe mzuri
      Every saint has a past, every sinner has a future' ...Oscar Wilde

      One man's good fortune is another man's misfortune


    Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...