Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 39 of 39
    1. #1
      juma sal's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 18th December 2011
      Posts : 147
      Rep Power : 408
      Likes Received
      36
      Likes Given
      128

      Default Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      Inahuzunisha lakini kuna fundisho kuu kwetu sote.
      “Nilipofika nyumbani usiku ule, mke wangu aliponitayarishia chakula, nilimshika mkono na kumwambia, Kuna kitu nataka nikwambie. Mke wangu alikaa chini na kula chakula kimya akiwa tayari kunisikiliza. Tena nikagundua macho yake yalionyesha anaumizwa. Nilishindwa hata namna ya kuanza kufumbua kinywa changu. Lakini ilibidi nimwambie ili ajue nilikuwa nikifikiri nini juu yake.

      Nataka kukupa talaka. Nilianza kusema kwa utulivu. Alionekana kutokereka na maneno yangu badala yake aliniuliza kwa sauti ya upole ‘kwa nini?’ Sikumjibu swali lake. Kutojibu kulimfanya akasirike. Akatupa kijiko na akanikaripia, ‘wewe si mwanamume!’ Usiku ule, hakukuwa na maongezi kati yetu. Alikuwa akilia kwa kwikwi. Nilifahamu kwamba alitaka kujua ni nini kimetokea kwenye ndoa yetu. Lakini kwa hakika nisingeweza kumpa jibu wala sababu ya kuridhisha; alionekana si mali kitu kwangu penzi langu lilihamia kwa Jane. Sikumpenda tena mke wangu mawazo yote yalikuwa kwa Jane. Kwa kweli nilimdharau mke wangu!

      Huku moyo wangu ukijua wazi kwamba nafanya kosa, niliandika talaka ambayo ilionyesha kwamba yeye (mke wangu) angepata nyumba yetu, gari na atakuwa na hisa 30% ya kampuni yetu. Aliangalia talaka ile na kuichana vipande vipande.

      Mke ambaye tumeishi nami kwa miaka 10 alionekana mgeni machoni mwangu. Nilimuonea huruma kwa muda, rasilimali na nguvu alizopoteza lakini sikuweza kurudi nyuma kwa sababu Jane aliuteka moyo wangu kisawasawa. Hatimaye mke wangu alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo kwa hakika nilitarajia. Kwangu mimi kilio chake kilinipa nafuu.


      Wazo la kuachana na mke wangu limenisumbua kwa majuma kadhaa na sasa limeendelea kuimarika na kuwa jambo la hakika zaidi.

      Siku iliyofuata nilikuja nyumbani kwa kuchelewa sana nikakuta mke wangu akiandika jambo mezani. Sikutamani hata kula chakula alichonipikia nilikwenda moja kwa moja chumbani na usingizi ulinichukua mara moja kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kula raha za kufa mtu na Jane.

      Usiku nilishtuka usingizini mke wangu alikuwa bado akiandika. Sikujali kabisa nikajifunika vyema shuka na kulala tena. Asubuhi yake alinikabidhi masharti ya talaka yake: hakutaka kitu chochote kutoka kwangu lakini alihitaji apate angalau mwezi mmoja wa kujiandaa kabla hajaachika. Akaomba kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja sote mimi na yeye tujitahidi kuishi maisha ya upendo au kawaida kwa kadiri itakavyowezekana. Sababu yake ilikuwa ndogo lakini muhimu: mwanetu wa kiume alikuwa akikaribia kufanya mtihani katika mwezi uliofuata kwa hiyo hakupenda mtoto aathirike kisaikolojia kwa sababu ya kuachana kwetu. Hili halikuwa tatizo kwangu, nilikubali mpango wake. Lakini alikuwa na sharti la ziada, aliniomba nikumbuke jinsi nilivyombeba siku za fungate yetu hasa siku ya harusi yetu. Akaniomba na kunisihi kwamba katika kipindi hicho cha mwezi mmoja niwe nambeba kutoka kitandani kwetu mpaka mlango wa kutokea kila asubuhi. Nilidhani anakaribia kuwa kichaa. Ili kufanya siku zetu za mwisho zisiwe na migogoro nilikubaliana na masharti yake ya ajabu.


      Nilimsimulia Jane kuhusu masharti ya kuachana na mke wangu. Jane alicheka sana, aliona ni ujinga. ‘Hata akitumia ujanja wa namna gani talaka ni lazima’, alisema Jane tena kwa dharau. Mimi na mke wangu hatukuwahi kugusana tangu nilipomweleza dhamira ya kumtaliki. Kwa hiyo nilipombeba kwa mara ya kwanza sote tulinuniana. Mwanetu alifurahi sana na kupiga makofi nyuma yetu, ‘aah baba kambeba mama mikononi mwake’. Maneno yake yalinichoma moyoni moja kwa moja. Kutoka chumbani kwetu hadi sebuleni, halafu tena mpaka mlangoni, ni zaidi ya mita kumi nimembeba mke wangu. Alifumba macho na kusema kwa sauti laini na ya upole; usimwambie mwanetu juu ya talaka. Nilikubali kwa kichwa, ingawa nilijisikia vibaya. Nilimuweka chini nje ya nyumba.

      Alienda kituoni kusubiri basi la kazini kwake nami nikaendesha gari kwenda ofisini kwangu. Siku ya pili, zoezi lilikuwa rahisi kwetu sote. Aliegemea kifuani pangu. Nilisikia harufu nzuri ya uturi aliofukiza kwenye blauzi yake. Nikagundua kwamba sijamuangalia kwa makini mke wangu kwa kipindi kirefu sana. Nikagundua hakuwa binti tena. Kulikuwa na mikunjo usoni na nywele zake zilianza kuwa nyeupe! Ndoa yetu imekula urembo wake. Kwa dakika moja nikafikiri kwa nini namfanyia hivi.

      Siku ya nne nilipombeba hisia za mapenzi kati yetu zilirejea. Huyu ni mwanamke aliyejitoa kuishi nami na tumeishi kwa miaka kumi sasa. Siku ya tano na ya sita ilikuwa wazi kwamba mapenzi yetu yalikuwa yakimea upya. Sikumwambia Jane kuhusu jambo hili. Kadiri mwezi ulivyokaribia kwisha niliona raha kumbeba mke wangu na zoezi likawa rahisi zaidi. Pengine kufanya kazi hii kila siku kuliniimarisha zaidi.

      Alikuwa akichagua nini cha kuvaa asubuhi. Alichagua mavazi kadhaa hakupata linalomfaa. Kisha akaguna, ‘nguo zangu zote zimekuwa kubwa’. Nikagundua kwamba mke wangu amepungua sana, nadhani ndiyo maana niliweza kumbeba kirahisi. Ghafla jambo likanichoma... mke wangu ana uchungu na maumivu makuu moyoni mwake. Bila kujitambua nikamgusa kichwa chake. Mara mtoto wetu akatokeza na kusema ‘baba ni wakati wa kumbeba mama muende kazini’. Kwake kumuona baba akimbeba mama likawa ni jambo la furaha sana. Mke wangu alimuonyesha ishara mwanetu asogee karibu na akamkumbatia kwa upendo mkuu. Niligeuza uso wangu nisije nikabadili mawazo katika dakika ya mwisho. Kisha nikambeba mikononi mwangu kutoka chumbani, sebuleni halafu mpaka mlangoni. Mkono wake laini ulikuwa umeizunguka shingo yangu kwa upendo. Nilimkumbatia mwili wake; ilikuwa ni mithili ya siku ya ndoa yetu. Lakini wepesi wake ulinitia mashaka.

      Siku ya mwisho nilipombeba nilipata shida hata kupiga hatua moja. Mtoto wetu alishakwenda shuleni. Nilimshika kwa karibu na kumwambia sikubaini kwamba maisha yetu yalikosa upendo. Nikaenda zangu ofisini…. Nikashuka garini hata bila kufunga mlango. Maana nilihisi nikichelewa tu ninaweza kubadili nilichoamua.... nikapand ngazi. Jane alifungua mlango nikamwambia, ‘Samahani, Jane, sihitaji tena kumtaliki mke wangu’. Akaniangalia kwa kustaajabu, halafu akagusa kichwa changu. Akaniuliza ‘Unaumwa?’ Nikaondoa mkono wake kichwani kwangu. ‘Samahani, Jane, nimesema sitaki kumtaliki mke wangu. Nadhani ndoa yangu haikuwa na furaha kwa sababu sikuthamini undani wa maisha yetu, mimi na mke wangu, si kwamba hatupendani. Nimetambua hilo tangu nilipombeba siku ya ndoa yetu nilitakiwa kumbeba siku zote za maisha yetu, nampenda mke wangu sitamuacha mpaka kifo kitakapotutenganisha.’

      Ikawa kama Jane alizinduka usingizini. Akanizaba kibao cha nguvu, akajiegemeza mlangoni na kuanza kulia. Nikashuka ngazi na kuondoka zangu. Nikaingia kwenye duka la maua nikaagiza maua mengi mazuri kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji akaniuliza aandike nini kwenye kadi. Nikatabasamu na kuandika “Nitakubeba kila asubuhi mke wangu mpaka kifo kitakapotutenganisha”. Jioni ile nilifika nyumbani na maua mikononi mwangu, tabasamu kubwa usoni nikakimbia mpaka chumbani, nikapokelewa na maiti ya mke wangu kitandani.
      Kumbe mke wangu alikuwa akisumbuliwa na saratani kwa miezi kadhaa nami nilishindwa kubaini kwa sababu nilihamishia akili yangu kwa Jane. Alijua kwamba angekufa karibuni na alitaka asiniingize katika chuki na mwanetu kama ningelazimisha talaka mapema.
      Angalau machoni mwa mwanangu naonekana ni mume mwema…

      Jamani vitu vidogo vidogo vizuri ni vya msingi sana katika mahusiano yetu... Siyo majumba au magari au fedha zilizoko kwenye benki. Hivi vitakupa tu mazingira ya kufurahi lakini vyenyewe siyo furaha. Kwa hiyo jitahidi kuwa na muda mzuri na mazingira rafiki ya kuwa na mwenzi wako, kuwa rafiki wa mwenzi wako. Fanya vitu mlivyofanya wakati wa uchumba na wa ndoa yenue ambavyo vitawaweka karibu siku zote. Muwe na ndoa yenye furaha. Mara nyingi watu hushindwa katika ndoa kwa kutotambua ni kwa kiasi gani walikuwa karibu wakati wa kujenga uhusiano wao
      Mungu awabariki nyote mliosoma na kujifunza hapa



      Last edited by juma sal; 15th July 2012 at 15:48.
      Wanachama wa Chadema Wengi wao humu kweli ni maboga nazi na akili zao ni wepesi kuchotwa akili.........By Shardcole wa jamii forum.01/01/2013



    2. #21
      BIG Banned's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2012
      Location : Banned
      Posts : 263
      Rep Power : 411
      Likes Received
      63
      Likes Given
      77

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      Somo zuri
      juma sal likes this.
      Vua GAMBA Vaa GWANDA

    3. #22
      watu8's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th February 2010
      Location : Juu ya Tukutuku
      Posts : 16,651
      Rep Power : 31607
      Likes Received
      8438
      Likes Given
      8791

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      wasanii wa bongo got to come out with these kind of stories ktk muvz zao...muvz sio kuigiza tu kwenye mijengo mikali au kumualika Omotola kuja kushuhudia uzinduzi
      juma sal likes this.

    4. #23
      roby2006's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th September 2011
      Posts : 315
      Rep Power : 453
      Likes Received
      45
      Likes Given
      12

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      Nimejikuta chozi likinidondoka,somo zuri kwa wana ndoa na wanaotarajia kuingia kweanye ndoa
      juma sal likes this.

    5. #24
      webondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Location : Chini ya mwembe
      Posts : 1,169
      Rep Power : 593
      Likes Received
      178
      Likes Given
      381

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      Very touching story, imetugusa sana.
      juma sal likes this.

    6. #25
      Godlisten shoo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st May 2012
      Posts : 37
      Rep Power : 364
      Likes Received
      7
      Likes Given
      5

      Default

      Kumbe mambo ya ndoa ni magumu sana kama huzingatii lakin ni kinyume kama unazingatia.

      Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
      juma sal likes this.


    7. #26
      Mwanawalwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2012
      Posts : 346
      Rep Power : 425
      Likes Received
      97
      Likes Given
      54

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      dah japo si mwanandoa imenigusa sana , but many marriage problems exist because of lack of friendship btn the two .dah
      juma sal likes this.

    8. #27
      Mbimbinho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st August 2009
      Posts : 1,850
      Rep Power : 873
      Likes Received
      476
      Likes Given
      213

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      I can't believe na uanamume wangu nafight na machozi hapa., what a sad story.
      I promise I'll be carrying my wife all days of our marriage life, but under one condition, she shouldn't get fat
      juma sal likes this.
      Mbwa ukimjua jina wala hakupi shida....

    9. #28
      cacico's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th March 2012
      Location : DSM
      Posts : 7,121
      Rep Power : 14538
      Likes Received
      6475
      Likes Given
      5043

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      nitampenda hubby wangu milele na milele! i have learned something here! GOD bless u, iliyeleta hii story!
      juma sal likes this.
      "the problem is not me! the problem is you understading me!"

    10. #29
      Ikunda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2010
      Posts : 717
      Rep Power : 597
      Likes Received
      142
      Likes Given
      49

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      Dha! inasikitisha.
      na ni fundisho tosha.
      juma sal likes this.
      Wapandao kwa machozi, watavuna kwa kelele za furaha. Zab 126:5

    11. #30
      TrueLove's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th January 2012
      Posts : 73
      Rep Power : 389
      Likes Received
      11
      Likes Given
      102

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      Jamani mm bado sijaolewa, ila hii Thread imenifanya nilie sana, ki ukweli imeniumiza sana, Asante kwa somo.

      Quote By WALIMWEUSI View Post
      Asante kwa ujumbe mzuri

    12. #31
      Barnabas Shadrack's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd July 2011
      Posts : 2,061
      Rep Power : 815
      Likes Received
      186
      Likes Given
      12

      Default

      Quote By GTesha View Post
      umetransilate ile ya kingereza eeh? hakuna jipya
      Kwako sio mpya lakini kwangu hata kama imetafsiriwa bado ni mpya na yenye mafunzo hasa.
      The unseen is illustrated by the seen.
      juma sal likes this.

    13. #32
      farkhina's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2012
      Location : Toronto,CANADA
      Posts : 940
      Rep Power : 555
      Likes Received
      252
      Likes Given
      199

      Default

      Quote By ruttashobolwa View Post
      Sijawai kulizwa na story lakini hii imenitoa machozi.

      So sad
      tumelia wengi wallah
      juma sal likes this.

    14. Uda is offline
      Uda
      #33
      Uda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2010
      Posts : 438
      Rep Power : 1822
      Likes Received
      215
      Likes Given
      14

      Default

      Quote By farkhina View Post
      tumelia wengi wallah
      oooh kweli inauma,lakini wanaume wengne mjifunze kupitia hii story,mmmh nazidi kuogopa maisha ya ndoa,wat can i do?mungu nipe nguvu!
      juma sal likes this.

    15. #34
      farkhina's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2012
      Location : Toronto,CANADA
      Posts : 940
      Rep Power : 555
      Likes Received
      252
      Likes Given
      199

      Default

      Quote By Uda View Post
      oooh kweli inauma,lakini wanaume wengne mjifunze kupitia hii story,mmmh nazidi kuogopa maisha ya ndoa,wat can i do?mungu nipe nguvu!
      hahaha umenipa sifa isikuwa yangu.sikulaumu najua haukutambua.mimi shost wako

    16. #35
      PetCash's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th March 2012
      Location : searching....
      Posts : 642
      Rep Power : 562
      Likes Received
      351
      Likes Given
      104

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      Well, Its still a copy n paste...halafu ujaribu kukopia mbali basi si page ya kwanza ya google we unabeba (at least page ya 100)
      juma sal likes this.
      You are what you eat

    17. #36
      CUTE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th March 2012
      Posts : 1,237
      Rep Power : 1504
      Likes Received
      582
      Likes Given
      331

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      uu ujumbe mkali sana asante sana mkuu

    18. #37
      Raph2nyi's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 21st November 2011
      Posts : 1
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      Asante kwa true love story yenye kutufunza wana jamiiforum

    19. #38
      maumbo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st June 2012
      Posts : 21
      Rep Power : 356
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Inakuhusu sana uwe kwenye ndoa au unaelekea, soma

      Kiukweli ni somo tosha kwetu nashukuru uliyeleta hii story hapa maana unatufundisha na ss tunaoelekea huko kwenye ndoa mungu akubariki na amkumbushe kila mwanandoa kiapo chake cha kanisani au msikitini ..........................nc

    20. #39
      roby2006's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th September 2011
      Posts : 315
      Rep Power : 453
      Likes Received
      45
      Likes Given
      12

      Default

      Ni somo tosho ili utakapoingia kwenye ndoa yakitokea ujue jinsi ya kukabiliana nayo
      Quote By TrueLove View Post
      Jamani mm bado sijaolewa, ila hii Thread imenifanya nilie sana, ki ukweli imeniumiza sana, Asante kwa somo.

    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...