Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

    Report Post
    Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast
    Results 21 to 40 of 42
    1. #1
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,089
      Rep Power : 27012
      Likes Received
      8208
      Likes Given
      17307

      Default Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Nyumba ndogo mwanzoni tamu kweli.........Ikiolewa utamu wote unakwisha
      (Picha haihusiana na habari hii)

      Bila shaka mmeshawahi kusikia wanawake walioachwa au kutelekezwa na waume zao wakidai kwamba waume hao watawakumbuka. Bila shaka pia mmeshawahi kusikia kuhusu wanawake ambao walisababisha ndoa za wanawake wenzao kuvunjika, ambao nao baada ya kuolewa ndoa zao zimekuja kuvunjwa na wanawake wengine. Kusikia kwa matukio kama hayo hakutokani na unasibu (coincidence) wa mambo, bali ukweli wa kimaumbile ambao hakuna mtu anayeweza kupingana nao. Katika maisha kuna kanuni za kiamaumbile ambazo ni kazi bure binadamu kujaribu kubishana nazo. Ni upotezaji wa muda kwa mfano mtu kujaribu kupinga tendo la jiwe kuzama majini linapotupwa ndani ya maji.

      Hali ya kimaumbile pia inatawala uhusiano wetu. Hebu fikiria juu ya mtu ambaye anamdharau mkewe na kumtelekeza au kumuacha kwa sababu amepata mwanamke mwingine bora zaidi. Ninavyofahamu mimi ni kwamba kunapokuwa na tatizo katika ndoa wanandoa hukaa na kujadili njia za kulitatua. Inaposhindikana kabisa ndipo kutengena au kuachana hutokea. Mwanaume ambaye hutafuta ‘nyumba ndogo’ wakati akiwa bado na ndoa yake na baadae kuamua kufunga ndoa ya wazi au ya siri na ‘nyumba ndogo’ hiyo ni mwanaume ambaye hata mtu asiye na elimu ya nafsi atajua kwamba ana matatizo ya kisaikolojia.

      Sababu ya kutafuta nyumba ndogo……..

      Kuna sababu nyingi ni kwa nini wanaume huwa na ‘nyumba ndogo’ , lakini sababu zote hakuna hata moja inayoweza kuhalalisha jambo hilo. Kwa muktadha huo tuache kwanza kuhusu sababu hizo, bali tujadili msingi au mahali zinapochipukia tabia hizo. Mtu anayetafuta ‘nyumba ndogo’ ni mtu ambaye haridhishwi na mkewe katika mambo fulani, bila kujali kama ni mambo ya kinyumba au nje ya hayo.

      Mtu huyu anaamini, hata kama sio waziwazi bali nyuma ya ubongo, kwamba hiyo ‘nyumba ndogo’ ndiyo yenye ukamilifu, ndiyo inayoweza kuchukuwa nafasi ya mke ambaye ana kasoro. Bila shaka mmeshawahi kusikia wanaume na hata baadhi ya wanawake wakisema kwamba mke mjeuri inabidi atafutiwe mke mwenzie, yaani mke mdogo.

      Hawa wana maana kwamba, mwanaume akiona udhaifu kwa mkewe inabidi atafute mwingine ili kuziba pengo hilo na pia kumtia adabu huyu mke wa kwanza. Lakini udhaifu huu unakuwa ni wa kupewa nguvu tu. Kama kuna uchovu wa hisia, yaani mwanaume ameanza kuchujukiwa na penzi la mkewe katika hali mbalimbali dawa au suluhu ya uchovu huu si kutafuta ‘nyumba ndogo’

      Kutafuta Suluhu…………

      Kama mwanaume ambaye suluhu ya kuchoka kwa hisia zake au kuchuja mapenzi kama kunavyoitwa, ni kutafuta mwanamke mwingine ni wazi hawezi kuishi na mwanamke mmoja. Atatafuta mwanamke wa pili ambaye naye hisia zake zitamchoka na hivyo kuhitaji mpya atakayeziamsha hisia hizo, ambaye naye baada ya muda fulani atakuwa hivyo. Inakuwa ni mtindo wa maisha yake kuwabadilisha wanawake kama nguo……………..

      Tafiti za hapa nchini zinaonyesha kwamba kila wanaume saba kati ya kumi ambao huwaacha wake zao na kuoa ‘nyumba ndogo’ . baadae ndoa zao na nyumba ndogo hizo huvunjika. Hebu fikiria ni wanaume watatu tu kati ya kila kumi ambao wataweza kuendelea kuishi na ‘nyumba ndogo’ zao,wengine saba wataangukia kwenye kutafuta au kuona ‘nyumba ndogo’ nyingine………

      Nawaomba wale wanawake ambao huwa wanafanywa ‘nyumba ndogo’ na baadae kuja kuolewa, wasidhani wamefika mwishowa safari zao. Nao wataachwa kama wenzao baada ya nyumba ndogo nyingine kupatikana……………..
      Last edited by Mtambuzi; 13th June 2012 at 11:57.

    2. FemaTV & Radio

    3. #21
      nyumba kubwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 4,047
      Rep Power : 2305
      Likes Received
      2874
      Likes Given
      3969

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Unabenda kubembelezwaeeeh. Haya tuone kama utaendelea kubembelezwa mpaka ukiwa unafungwa pampus. Lol.

      Kuna mmoja aliacha nyumba yake kubwa upanga kaenda kusihi vichochoroni na nyumba ndogo for more than 10 years. Alirudi mwneyewe alipoanza kuvaa pampus. Kakuta watoto wameshakuwa tena wa kwanza ni MD. Mkewe kamsamehe lakini kamuonyesha chumba cha wageni, kamtunza mpaka alipo dead. Mimi ningemtimulia mlangoni aisee. Ukiwa mzima unatanua na vimada, unaumwa unakumbuka kuwa una nyumba kubwa. Msonyoooo.

      Quote By Power
      Tunachofuata huko ni kubembelezwa na kudekezwa baada ya kupata shuruba za kazini na za nyumba kubwa.
      Yummy likes this.

    4. #22
      Jestina's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2011
      Posts : 3,622
      Rep Power : 1446
      Likes Received
      842
      Likes Given
      337

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      mie mbona baba yangu kadumu mwaka wa kumi huu sasa tangia aopoe kabinti,,,,,kuna theory ukishaacha mke wa kwanza,ukampata wa pili ukagundua na yeye ana mapungufu,UNAJIFUNZA kuwa labda wanawake wote wana mapungufu hivyo swala la kutafuta mkamilifu linakutoka,hivyo unasettle.

    5. #23
      nyumba kubwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 4,047
      Rep Power : 2305
      Likes Received
      2874
      Likes Given
      3969

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Ni ngumu kukubali au kukataa theory yako; kwani si wanaume wengi wanaama nyumba zao sababu ya vimada hivyo ni ngumu kupata evidence. Katika jamii ni aibu kubwa kwa baba mwenye familia kukimbia nyumba yake no matter what.

      Na ina effect kubwa sana kwa watoto; kuna dada rafiki yangu toka Uganda alikuwa analia daily kwa kuwa baba yao ameama mji. Na anasema hatakaa aolewe. Sasa nambie huyo mwanaume ambaye si mkewe tu bali hata watoto wanamlilia unadhani atakuwa na bright future huko aendako kama si laana!

      Quote By Jestina

      Last edited by nyumba kubwa; 13th June 2012 at 17:00.

    6. #24
      mbalu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 18th May 2012
      Location : Ntuzu
      Posts : 214
      Rep Power : 395
      Likes Received
      98
      Likes Given
      68

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Point taken ya mkoloni naiachia nasafi. wabhe'ja nkoi.
      Ong'wizukuru Shimba nawe Shimba.

    7. #25
      WALIMWEUSI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2011
      Location : DSM
      Posts : 947
      Rep Power : 569
      Likes Received
      276
      Likes Given
      354

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Quote By Caroline Danzi
      Madame x wanawake ni hopeless always including me. Hatuna akili yakuchanganua kwamba huyo mwanaume anatuchezea akili ama la. Hivi wewe kwa akili isiyohitaji kusoma, kuna chochote nyumba ndogo inamzidi mke original? Excuse me! Nyumba ndogo always ni za kutolea uchovu end of the day unaachwa kwenye mataa, ikibahatika kuolewa ihesabie anakuja mwingine ku-overtake!

      Kama siyo ukilaza na upumbavu uliopitililza, mwanamke na akili zilizochanganyika na matope unaolewa mke wa 3, hao wa wawili mbele yako ni ni majuha? Wanawake amkeni acheni ujinga na upumbavu, tuache kunyonga, tujifunze kuchinja
      Well said CD, mimi hili huwa nikiongea watu wananitokea cheche!! Simlaumu mwanamke anayetembea na mwanaume pasipokujua kuwa huyo ni mume wa mtu! LAKINI kwa wewe unayefahamu kuwa MR. X kamuoa dada Y, wana watoto kadhaa, na bado ukatembea nae na hata kufikia hatua ya kuzaa naye, nakuhakikishia kuwa hiYo ni LAANA MAISHANI MWAKO NA KWA VIZAZI VYAKO, hii naisema special kwa non islamic ambao ndoa zetu ni za mke mmoja. Laana hiyo inaweza isikupate wewe directly lakini vizazi vyako vinaweza kuathirika vibaya.

      Nina mfano halisi in my family, kuna mwanamke aliingilia ndoa ya my mother, na akazaa 4 children na mzee! Mwisho wa siku huyo mama akafumaniwa na friend wa mzee, alitimuliwa kama mbwa mwizi! Katika hao 4 children, mmoja ni msichana, sasa dogo anabeba ile laana ya mama yake! Sitaki kusimulia whats happening to her.
      The best mind-ultering drug is truth.

    8. Study Abroad

    9. #26
      nyumba kubwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 4,047
      Rep Power : 2305
      Likes Received
      2874
      Likes Given
      3969

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Mfano nilikuwa naangalia CNN juzi kati; huyu mke wa Kennedy alojiua; si amekaa kwenye ndoa miaka kumi na sita sijuhi; leo hii anaambiwa its over anaamua kujimaliza wakati amesahau mmewe alikuwa mume wa watu; aka divorce amuoe yeye. Zamu yake imefika anakataa ukweli, kuwa what goes around comes around.

    10. #27
      Caroline Danzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th December 2008
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 2,708
      Rep Power : 1072
      Likes Received
      647
      Likes Given
      214

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Vitabu vimeandika, hatuoni wala kusikia, end of the day yale uliyofanya kwa mwenzako yanakuja vile vile. Tuombe mungu wanawake wote, tuwe na akili ya kupambanua!

    11. #28
      Ennie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th January 2011
      Location : DAR ES SALAAAM
      Posts : 1,593
      Rep Power : 817
      Likes Received
      498
      Likes Given
      539

      Default

      Quote By nyumba kubwa
      Mfano nilikuwa
      naangalia CNN juzi kati; huyu mke wa Kennedy alojiua; si amekaa kwenye
      ndoa miaka kumi na sita sijuhi; leo hii anaambiwa its over anaamua
      kujimaliza wakati amesahau mmewe alikuwa mume wa watu; aka divorce amuoe
      yeye. Zamu yake imefika anakataa ukweli, kuwa what goes around comes
      around.
      Amesahau kuwa kwa mwali huliwa na kwa kungwi pia huliwa!
      nyumba kubwa likes this.

    12. #29
      MwalimuZawadi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st September 2007
      Posts : 623
      Rep Power : 723
      Likes Received
      50
      Likes Given
      3

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Quote By nyumba kubwa
      Ni ngumu kukubali au kukataa theory yako; kwani si wanaume wengi wanaama nyumba zao sababu ya vimada hivyo ni ngumu kupata evidence. Katika jamii ni aibu kubwa kwa baba mwenye familia kukimbia nyumba yake no matter what.

      Na ina effect kubwa sana kwa watoto; kuna dada rafiki yangu toka Uganda alikuwa analia daily kwa kuwa baba yao ameama mji. Na anasema hatakaa aolewe. Sasa nambie huyo mwanaume ambaye si mkewe tu bali hata watoto wanamlilia unadhani atakuwa na bright future huko aendako kama si laana!
      Nyumba Kubwa fikiria
      1. Chukulia mwanaume unagundua mke na mwanaume mwingine. Mnasuluhisha, mara ya kwanza, ya pili.... unagundua bado wanaendeleza libeneke. Unamwomba basi kila mtu 50 zake anakataa. Ndoa ni zile zisizovunjika, na una watoto. Unafanyaje hapo?

      2. Chukulia mwanaume unagundua mke ni mshirikina. Mnasuluhisha, mara ya kwanza, ya pili.... unagundua bado anaendeleza za kwa mutimuti. Unamwomba basi kila mtu 50 zake anakataa. Ndoa ni zile zisizovunjika,na una watoto. Unafanyaje hapo?

      3. Chukulia mwanaume unagundua mke ni mwizi. Mnasuluhisha, mara ya kwanza, ya pili.... unagundua bado anaendeleza udokozi. Unamwomba basi kila mtu 50 zake anakataa. Ndoa ni zile zisizovunjika, na una watoto. Unafanyaje hapo?
      Sent from my Nokia rinGo using JamiiForums

    13. #30
      King'asti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th November 2009
      Location : The Jungle
      Posts : 17,115
      Rep Power : 28888
      Likes Received
      11619
      Likes Given
      4783

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Wanasema mbio za sakafuni huishia ukingoni, na hakuna marefu yasiyo na ncha. Kuna kaka alishawahi kujitapa kwangu kuwa ana anniversary ya 10 yrs na small house ambayo ni mke wa mtu na mtoto wamezaa bila kustukiwa na yeyote. 3 yrs later namuuliza sijaskia small house, hajambo? Alinijibu 'myayusho, tushamwagana'.

      Na mie nasaka nyumba ndogo jamani, ngoja nianzishe uzi.
      nyumba kubwa likes this.

    14. #31
      nyumba kubwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 4,047
      Rep Power : 2305
      Likes Received
      2874
      Likes Given
      3969

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Nikisema laana sina maana inampata mtu aso na kosa. Hata wanawake japo si wengi kama wanaume, wapo wanaokimbia nyumba zao. Nawajua wawili; mmoja huyo ni mtu wangu wa karibu mwingine ni jirani.

      Huyu mama jirani (kwa wazazi wangu) alipata kazi ofisi mojawapo za UN nje ya nchi; mmewe alikuwa yupo yupo hana kazi, nadhani alikuwa na kazi before akatimuliwa au alikuwa na biashara, amefulia, walikuwa ni wageni kitaani hivyo sina details. Mwanamke alienda nje sijuhi contract ya miaka miwili (kama sikosei) hakuwahi hata kupiga simu, miaka imekatika mpaka wa leo hajarudi kwa mumewe; ni more than 10 years now na watu wanasema kamkimbia mumewe arosto. Na watoto aliwaacha, imagine! Sidhani kama mambo yake yanamnyookea popote alipo.

      Mwingine huyu ni mdogo wa wifi yangu; baba yao ni tajiri sana. Binti kaolewa na pedegee mmoja lakini kijana akashindwa ku mantain life style anayopenda binti baada ya ku shake kiuchumi. Binti karudi kwao na mtoto wake na kakomba vitu vyote vya ndani. Baba yake na ndugu zake wakamwambia hawana uwezo wa kumlazimisha ndoa, ila arudishe vitu vya watu. Kwa ufupi kilichofuata akawa anaama nyumba moja baada ya nyingine; mwisho aliamia kwa jamaa mmoja maarufu mujini, akamfanya mke bila ndoa; jamaa keshakufa na HIV, binti hata soko kwa sasa hana. Wanaume wanamuogopa kama ukoma.

      Quote By MwalimuZawadi
      Nyumba Kubwa fikiria
      1. Chukulia mwanaume unagundua mke na mwanaume mwingine. Mnasuluhisha, mara ya kwanza, ya pili.... unagundua bado wanaendeleza libeneke. Unamwomba basi kila mtu 50 zake anakataa. Ndoa ni zile zisizovunjika, na una watoto. Unafanyaje hapo?

      2. Chukulia mwanaume unagundua mke ni mshirikina. Mnasuluhisha, mara ya kwanza, ya pili.... unagundua bado anaendeleza za kwa mutimuti. Unamwomba basi kila mtu 50 zake anakataa. Ndoa ni zile zisizovunjika,na una watoto. Unafanyaje hapo?

      3. Chukulia mwanaume unagundua mke ni mwizi. Mnasuluhisha, mara ya kwanza, ya pili.... unagundua bado anaendeleza udokozi. Unamwomba basi kila mtu 50 zake anakataa. Ndoa ni zile zisizovunjika, na una watoto. Unafanyaje hapo?

    15. #32
      BADILI TABIA's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Location : DUNIANI
      Posts : 14,553
      Rep Power : 5612
      Likes Received
      6210
      Likes Given
      2281

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      mtambuzi umenikuna kweli leo.....najitolea kuwa nyumba ndogo yako....
      Mtambuzi likes this.

    16. #33
      Yummy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th September 2011
      Posts : 1,751
      Rep Power : 1894
      Likes Received
      1274
      Likes Given
      983

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Natamani naniliu aje asome hapa..... Mtambuzi nikupe namba yake ya simu umtumie sms umwambie kuna habari inamhusu hapa?
      Mtambuzi likes this.

    17. #34
      Kaizer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th September 2008
      Posts : 13,983
      Rep Power : 21891
      Likes Received
      6934
      Likes Given
      7782

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Wajameni, kuna mtu aliyebaki wa kunipa taarifa kuwa hapa tunadiskasheni nini? kama ni mjadala wa nyumba ndogo, naomba nisishiriki. Kama ni kitu kingine , hebu naombeni mmojawenu aniambie?
      Mtambuzi and Yummy like this.
      "Bunduki bila risasi yaua namna gani"
      Email: [email protected]

    18. #35
      Yummy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th September 2011
      Posts : 1,751
      Rep Power : 1894
      Likes Received
      1274
      Likes Given
      983

      Default

      Quote By nyumba kubwa
      Unabenda kubembelezwaeeeh. Haya tuone kama utaendelea kubembelezwa mpaka ukiwa unafungwa pampus. Lol.

      Kuna mmoja aliacha nyumba yake kubwa upanga kaenda kusihi vichochoroni na nyumba ndogo for more than 10 years. Alirudi mwneyewe alipoanza kuvaa pampus. Kakuta watoto wameshakuwa tena wa kwanza ni MD. Mkewe kamsamehe lakini kamuonyesha chumba cha wageni, kamtunza mpaka alipo dead. Mimi ningemtimulia mlangoni aisee. Ukiwa mzima unatanua na vimada, unaumwa unakumbuka kuwa una nyumba kubwa. Msonyoooo.
      nyumba kubwa hii habari imenishtua kama ya marehemu ninae mfahamu,ila yy watoto ndio waliomuomba mama yao ampokee baba yao amuuguze maana ND ilishamkimbia na kuchukua mali zooote! Ila wanawake nawapeni pongezi mna huruma sana jamani mi pia nilisema ningemtoa baruuu,wamama watu wazima wakaniambia nasema tu kwakua halijanifika bado.
      Mtambuzi likes this.

    19. #36
      Yummy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th September 2011
      Posts : 1,751
      Rep Power : 1894
      Likes Received
      1274
      Likes Given
      983

      Default

      Quote By Kaizer
      Wajameni, kuna mtu aliyebaki wa kunipa taarifa kuwa hapa tunadiskasheni nini? kama ni mjadala wa nyumba ndogo, naomba nisishiriki. Kama ni kitu kingine , hebu naombeni mmojawenu aniambie?
      Lol Kaizer hapa inshu ni NK na ND hivyo basi naomba tu ukalale ili kesho usichelewe kuamka,kumbuka unatakiwa kuwahi pale mahala petu.
      Njozi njema
      Kaizer and Mtambuzi like this.

    20. #37
      Sashel's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th March 2012
      Posts : 177
      Rep Power : 398
      Likes Received
      71
      Likes Given
      102

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Quote By MwalimuZawadi
      Nyumba Kubwa fikiria
      1. Chukulia mwanaume unagundua mke na mwanaume mwingine. Mnasuluhisha, mara ya kwanza, ya pili.... unagundua bado wanaendeleza libeneke. Unamwomba basi kila mtu 50 zake anakataa. Ndoa ni zile zisizovunjika, na una watoto. Unafanyaje hapo?
      2. Chukulia mwanaume unagundua mke ni mshirikina. Mnasuluhisha, mara ya kwanza, ya pili.... unagundua bado anaendeleza za kwa mutimuti. Unamwomba basi kila mtu 50 zake anakataa. Ndoa ni zile zisizovunjika,na una watoto. Unafanyaje hapo?
      3. Chukulia mwanaume unagundua mke ni mwizi. Mnasuluhisha, mara ya kwanza, ya pili.... unagundua bado anaendeleza udokozi. Unamwomba basi kila mtu 50 zake anakataa. Ndoa ni zile zisizovunjika, na una watoto. Unafanyaje hapo?
      Ok napenda kushea uelewa wangu juu ya "ndoa zisizovunjika", kwanza kabisa ndoa ni kiapo cha makubaliano ya kuishi mme na mke hapa duniani, hivyo si agano la milele ndio maana mmoja akifariki mwenza huwa huru kuoa/olewa , pili si kweli kwamba ndoa haivunjiki- kuna mambo hupelekea kuvunjika kwa ndoa nayo ni hiyo namba moja UASHERATI, iwapo mme/mke atafanya uasherati mwenzi wake anaweza na anaruhusiwa kutoka kwenye hiyo ndoa maana agano la ndoa limevunjika. namba mbili ni UCHAWI / USHIRIKINA-japo huwa ni ngumu kuthibitisha kuwa mme/mke ni mchawi, lakini ikithibitika ndoa inaweza kuvunjwa kabisa. Wandugu ndoa si adhabu kwamba ukubaliana na uovu wowote mme/mke atakao kufanyia no no its not true! ila kama mtu mwenyewe kwa sababu zake ataendelea kuishi kwenye "ndoa jina" good for him/her. Mimi huwa natafakari wakati mwingine kwamba ikiwa ndoa kwa maana ya agano huvunjika mtu anapofanya uasherati hivi mbele za Mungu kuna ndoa ngapi.. maana ndoa sio cheti cha ndoa bali ni lile agano/yamini. God help us
      Mtambuzi likes this.
      10% of conflicts is due to difference in opinion and 90% is due to WRONG TONE OF VOICE

    21. #38
      Kaizer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th September 2008
      Posts : 13,983
      Rep Power : 21891
      Likes Received
      6934
      Likes Given
      7782

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Quote By Yummy
      Lol Kaizer hapa inshu ni NK na ND hivyo basi naomba tu ukalale ili kesho usichelewe kuamka,kumbuka unatakiwa kuwahi pale mahala petu.
      Njozi njema
      Baas Yummy...am out.....LOL
      Yummy and charminglady like this.
      "Bunduki bila risasi yaua namna gani"
      Email: [email protected]

    22. #39
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,089
      Rep Power : 27012
      Likes Received
      8208
      Likes Given
      17307

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Quote By yummy
      lol kaizer hapa inshu ni nk na nd hivyo basi naomba tu ukalale ili kesho usichelewe kuamka,kumbuka unatakiwa kuwahi pale mahala petu.
      Njozi njema
      NK = nyumba kubwa
      ND = nyumba ndogo
      Yummy and charminglady like this.

    23. BAK
      #40
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,538
      Rep Power : 44951
      Likes Received
      8281
      Likes Given
      8280

      Default Re: Wanaume wanaooa ‘nyumba ndogo’ huwa hawadumu nazo……………….!

      Quote By nyumba kubwa
      Unabenda kubembelezwaeeeh. Haya tuone kama utaendelea kubembelezwa mpaka ukiwa unafungwa pampus. Lol.

      Kuna mmoja aliacha nyumba yake kubwa upanga kaenda kusihi vichochoroni na nyumba ndogo for more than 10 years. Alirudi mwneyewe alipoanza kuvaa pampus. Kakuta watoto wameshakuwa tena wa kwanza ni MD. Mkewe kamsamehe lakini kamuonyesha chumba cha wageni, kamtunza mpaka alipo dead. Mimi ningemtimulia mlangoni aisee. Ukiwa mzima unatanua na vimada, unaumwa unakumbuka kuwa una nyumba kubwa. Msonyoooo.

      Hahahahah lol! mbona hukumalizia bana nyumba kubwa!!!? Msonyooooo mrefuuuu...
      Mxchyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu uuu hahahahah lol!
      Mtambuzi and charminglady like this.
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    24. Miaka 50
    Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...