Dah!
Smile mdogo wangu wa moyoni, kwanza hongera kwa kuamua kujua ukweli manake huo ni ujasiri sana. ILa pia nasikitishwa sana na haya maisha kwani yanapomfunza mtu basi mifano inayotumika ni migumu na hata kanuni pia hazi apply kabisa mwishowe unakuja gundua kuwa mwanafunzi hajaelewa na mfano bado ni complicated kwa muhusika.
Sababu kubwa zinazomfanya mtu aolewe ni kwamba ili kupata mwenza wa kushirikiana naye katika maisha. nisemapo mwenza wa kushirikiana naye simaanish kitu kingine bali mwenza wa kukidhi haja yako ya kimwili(tendo la ndoa), na zaid yako upate mtu wa kushare naye yaani msiri wako. Mambo mengine kuzaa, kufanya kazi za ndani siyo ishu sana katika hili.
Matatizo meng yanayojitokeza katika ndoa za siku hizi ni kwasababu tu ya mambo yafuatayo, mmomonyoko wa maadili kwa ujumla ila nikitaka kuyaweka mepesi sana nitasema tamaa zisizo na mpango. Binadamu tumekuwa hatuna tena hofu ya Mungu, hakuna menye kuheshimu utu wake na mwili wake. Kwangu mimi hili ni jambo baya sana.
Mfano ukimuona baba bdani ya nyumba antembea na beki 3 jua basi anawez kutembea na mwanae wa kumzaa. Kwanini nasema hivi? Binti wa kazi za ndani ni kama mtoto wako manake unabeba full responsibility juu yake kama mzazi. sasa inapotokea ukamtamani skutofautish kama na kumtamani mwanao wa kumzaa au mtoto wa mkeo. Ni taba mbaya na ya kishenzi.
Nirudi kwako mwenyewe
Smile, wewe ni kwamba umefundishwa haya maisha kwa kutumia mifano migumu sana au la niseme maisha yalikufunza kabla hujafikia umri wa kupata shule. hapa naona hujanielewa.
namaanisha mfano mtoto wa miaka 5, labda mzazi analazimisha asome darasa la 1 wakati mtoto huyu ni bado yuko mdogo kiakili na hata kiuwezo wa kupambanua mambo kiasi kwamba akiwa darasani alishazoea kuandka sentensi 2 tu huko nursery hapa lakwanza anatakiwa aandike 10 ni wazi kuwa atashindwa na atakomea kwenye hizi 2 tu. na ukimlazimisha mwisho wa siku utakuja kuua kabisa nia yake ya kupenda kusoma na matokeo nikama haya mtoto kuacha shule au kukata tamaa na shule kabisa.
kwa mfano huo basi mimi nikwambie tu njia iliyotumika kwako ndio haikuwa nzuri katika kukufundisha juu ya maisha. Kuna wenye bahati mbaya ambao mwanzo mwisho wanakutana na mitihani baut hawa ni wachache na hivyo lazima wasikike sana manake wanakuwa wanahangaika katika kutafuta suluhisho la maisha yao. wale wanaopata raha ni wengi pia na hawa hawawez kusema hadharan kwan mgema akisifiwa tembo hutia maji.
Ndoa inauzuri wake sana tu, atleast unapata mtu wa kukufichia siri, kushare na wewe misha na ambaye unabeba full responsibility juu yake. Tatizo ni kwamba inapotokea kitu kibaya basi sisi binadamu hukimbilia kulaumu ndoa kuliko kuangalia nini tatizo.
Pia smile maisha haya ni Mungu tu ndiye anayeongoza na si utash wa mtu pekee. So kwakila kitu mwombe yeye na tamka unataka akufanyie nini basi na si vinginevyo. usipende sana kusikiliza ushuhuda wa kushindwa kama huwez kuutoa akilini kwani utakuharibia maisha yote ma dia.
Unalo tatizo tu la kisaikolojia.
Follow Us Here