Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla...! SEHEMU YA MWISHO

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 36
    1. #1
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8249
      Likes Given
      17379

      Default Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla...! SEHEMU YA MWISHO



      Picha hii haihusiani na habari hii.........


      Nilipelekwa hospitlini na wale wanakijiji. Dada na wanae hawakujali kabisa. Kale kabinti kake ka mwisho yaani Msekwa, kalilia sana kalipoona nimeunguzwa. Nakumbuka nilipolazwa hospitalini ndiko pekee kutoka nyumba ile kalikokuja kunitazama.

      Nililazwa hospitalini kwa wiki mbili na wale wanakijiji walionipeleka hospitalini ndio waliochangishana na kunilipia gharama za kukaa hapo hospitalini. Nilitoka nikiwa na nafuu kubwa, ingawa shavu langu lilikuwa na alama kubwa ya kuunguzwa kule. Hata hivyo nilijua kwamba, hata baada ya kupona ningebaki na kovu hilo mileleNilipotoka hospitalini sikuweza kurejea kule kwa dada yangu na wale wanakijiji walionisaidia pia waliogopa kunipokea. Waliogopa kwa sababu dada yangu alikuwa akiwatisha kwamba nikifa watanila nyama. Ilibidi nifikirie namna mpya ya kuishi. Kumbuka wakati ule, tena vijijini, watu hawakuwa wanjua kitu kinachoitwa haki za binadamu, achilia mbali haki za mtoto. Watu walikuwa waoga kuingilia mambo ya familia za watu, hata kama mtu anakufa.

      Unajua ni kwa nini nimekuuliza kuhusu maono? Ni hivi. Saiku ile nilipotoka hospitalini nililazimika kwenda kwenye mashamba yampunga ambapo niliomba kibarua cha kufukuza ndege kwa wenye mashamba hayo. Nakumbuka watoto wengi na watu wazima walikuwa wakifanya kibarua hicho.
      Kwa bahati nzuri mama mmoja aliniambia angenisaidia lakini malipo yangu ningepata baada ya mavuno. Aliniambia ningekula na kulala kwake hapo hapo shambani. Niliona kama vile nimepata dhahabu. Nilikubaliana naye.

      Ilikuwa ni usiku wakati nikiwa bado sijapata usingizi vizuri, nilipokiona kitu hicho. Hapo kwenye kibanda cha shambani nilimokuwa, niliona kitu kama kivuli kidogo. Kivuli hicho kililkuwa mbele yangu. Kwa sababu ya giza sikujua kama ni kivuli cha mtu au hapana.

      Niliogopa kupindukia na nilikuwa natetemeka pale kwenye godoro la sufi nilipokuwa nimelala. Halafu nilisikia kama sauti, ambayo sikujua kama inatoka kichwani mwangu au kwenye kile kivuli. Ilikuwa ikisema 'Muone tu mama mkubwa, ni lazima usome, ile sauti ilirudia tena na tena. Ilikuwa ni sauti niliyokuwa ninaifahamu.

      Ilizidi kunisisitiza tena na tena. Nilishindwa kuvumilia ambapo nilipiga yowe kubwa na kuamka. Nilipapasa hapo chini na kuchukua kiberiti. Niliwasha kibatari huku mikono yangu ikitetemeka. Nilitazama mle kibandani na sikuona kitu. Nilikumbuka sauti ile kwa mbali sana. Ilikuw ni sauti ya mama yangu au mdogo wangu, sikuwa na uhakika sana.

      Nilianza kufikiria kuhusu huyo mama mkubwa. Mimi sikuwa na mama mkubwa, sasa ni mama mkubwa yupi ambaye huenda sauti zile zilikuwa zikinielekeza kwake. Nilijiuliza karibu usiku mzima. Hatimaye kwa njia fulani ya ajabu nilikumbuka kwamba, wakati nikiwa nimelazwa pale hospitalini Bwagala, kulikuwa na watu waliokuwa wakimtaja mtu aliyeitwa mama mkubwa, ambaye wengine walisema ndiye mwenye hospitali ile.

      Nilichukuliwa na usingizi kwenye saa kumi na nilishtushwa na mama mwenye shamba. Alikuwa akiniita huku akitukana kwani mpunga ulikuwa unashambuliwa na ndege. Nilitoka kibandani kwa kasi na kukutana naye mlangoni. ‘Samahani mama nimechelewa kuamka…’Hakusubiri nimalize kwani alinitaka niondoke pale shambani kwake saa ile ile. Niliondoka bila kuhitaji kujitetea, labda nilishazoeshwa kuishi kwa amri.
      Nilitembea asubuhi hiyo hadi hospitalini. Nilikwenda upande wa utawala na kuomba nimwone mama mkubwa. Ilikuwa ni vigumu sana kwa sababu ya watu ambao siku hizi wanitwa ‘wapambe’ Walikuwa wananizuia kwa maelezo kwamba mama mkubwa haonwi hovyo tu. Wakati tunabishana, kwani nami nilikuwa mkali nikiwa sijui nilitoa wapi nguvu hiyo ya kubishana, alitokea mamammoja mzungu aliuliz kulikoni, ambap walimweleza. Alinisogelea na kuniambia nimweleze shida yangu. Sikumwambia kuwa niliota kuhusu mama mkubwa bali nilimsimulia kwa kifupi madhila yangu na kumwambia nilikuwa nataka msaada w kusoma.Alinisikiliza sana na baadae alisemaangepanga nionane na huyo mama mkubwa. Saambili baadae nilikuwa ofisini kwa mama mkubwa. Alikuwa ni mama wa kizungu mtu mzima sana, lakini mjanja na msikivu sana. Nilizungumza naye kwa kirefu nikimweleza kia kitu. Alishindwa kuvumilia kwani alimwaga chozi.Hapo nikafanikiwa kupata mfadhili wa kunisaidia kusoma. Nilikwenda shuleni na kuendelea na masomo.

      Nilikuwa ninaishi chini ya uangalizi wa mzee mmoja aliyekuwa anaitwa Alois, ambaye nimeambiw ameshafariki. Nilikuwa nikiishi kwenye chumba kimoja karibu na wodi ya wagonjwa hapo hospitalini. Wale ambao bado wapo hospitalini pale kama watumishi wanakumbuka, bila shaka. Nilimaliza darasa la saba na kuanguka kwa njia ambayo bado ni mshangao kwangu, hadi leo. Mama mkubwa alisikitika sana. Alimwomba Mzee Alois anitafutie shule nirudie. Nilirudia shule nyingine ya jirani. Mwaka mwaka uliofuatia nilifaulu peke yangu shuleni hapo.

      Niliendelea na masomo. Bila shaka huhitaji kujua habari za shule ya sekondari. Lakini nilimaliza kidato cha sita mwaka 1987 na kumaliza masomo ya chuo kikuu nchini Uholanzi mwaka 1992. Nilirudi nchini na kuanza kazim kwenye kampuni9 moja ya madini kule shinyanga.

      Mwaka 1994 nilikwenda Turiani, lengo likiw ni kwasalimu wote ambao nilikuw nafahamiana nao pamoja na dada yangu. Kwa kweli nilikuw nimemsamehe dada yangu yule kutoka ndani kabisa ya moyo wangu. Niliamua kwa makusudi niende nikashukie kwake. Nilipofika pale nyumbani kwake kulikuwa na mabadiliko sana. Ile nyumba ilikuwa imechakaa karibu kuanguka na palionyesha ukiwa wa wazi. Nilibisha hodi na mama mmoja mtu mzima sana alifumgua mlango kutokea ndania na kusimama mlangoni.

      Kwa muda sikuweza kumjua. Lakini htimaye nilijua kuwa ni dada yangu.
      ‘Dada shikamoo, habari za siku’ nilimsalimia, lakini yule mama pale mlangoni alishindwa kujibu na kwa muda fulani ilionekana kama vile hakuwa anajua kinachoendelea. ‘Marahaba’ Alijibu, lakini ilikuwa ni kwa mazoea tu. ‘Nani mwenzangu, maana na huu uzee nao,’ Alisema akijichekesha.

      ‘Ni mimi Joseph, mdogo wako Joseph, mtoto wa mzee Richard Mbega wa Sindeni.’
      Nilisema kwa kumfafanulia. Nilimwona dada akijishika vizuri pale mlangoni, lakini hakuweza. Alienda chini pole pole na kukaa kati kati ya mlango. Kw muda fulani nilijua alikuwa hajui alipo na kinachoendelea.

      Wakati nikiwa najiuliza nifanye nini mama mwingine aliingia kutokea huko nyuma ya nyumba. Nilimtazama lakini sikumfahamu. Yeye alipiga kelele. ‘Kaka Jose jamani, kaka Jose,wala siamini…….’ Ilikuwa zamu yangu kushngaana laijua hilo kwani aliniambia, ‘Ni mimi mpwa wako Msekwa.’ Nilihisi kitu kikilipuka huko moyoni na matumbo yangu yalishikw na kubana ghafla.

      Msekwa, alikuwa ni mama mzima, amechakaa na kuchoka kabisa. Kati yetu, yeye angeonekana kuwa mkubwa sana kuliko mimi. ‘Mungu wangu nashukuru nimekukuta…’
      Halafu tulimsikia dada yangu akipiga yowe la kilio akidai kwamba hakuwa anajua alichokuwa anakifanya. Akiwa anaongea Kizigua alisema, ‘Mungu wangu mie nifanyeje sasa, naumbuka ….’ Nilimbembeleza, ingawa Msekw alisema nimwache augulie kwa sababu anastahili.

      Baada ya kupumzika, nilijua kwamba wale wapwa zangu watatu wengine, aliyekuwa hai ni mmoja tu wa kike. Mmoja alifariki kwa kuajribu kutoa ujauzito na yule wa kiume alikuwa amefariki kwa kunywa sana pombe. Huyu mwingine alikuwa ameolewa na kuachwa na alikuwa eneo linaloitwa Dakawa. Nilikaa Turiani siku tatu na nilimwomba Msekwa tuondoke wote aje Dar ajifunze kozi yoyote. Hapa ninaposimulia makala haya, ni muuguzi siku nyingi. Dada yangu alikataa katakata kuja kwangu kwa aibu.

      Inasikitisha hata hivyo kwamba, miezi mitatu tu tangu nilipofika kwake alifariki.Wanasema kila wakati alikuwa akijilaumu kwa yale aliyokuw amenitendeana alianza kujiambia kwamba, hana sababu ya kuishi kwa sababu hana maana. Naamini tunapanda nguvu hasi na huja kuturudia wenyewe.

      Tulienda kuzika na kurejea Dar. Juhudi yangu yote ilikuwa ni kumpata yule shemeji yangu, iwe yuko hai au kaburi lake lilipo ili angalau nilijengee kama zawadi yangu kwake. Lakini juhudi zangu ziligonga ukuta kwa kadiri nilivyojitahidi. Nilikwenda hadi TPC, Moshi lakini sikumpata.

      Hata hivyo hatimaye nilimpata katika mazingira ambayo sitaweza kuyasimulia hapa.
      Naamini kwa simulizi hii, kuna jambo ambalo umejifunza. Katika maisha haya tunayoishi ni vyema tukawa tunapanda mbegu chanya na sio hasi, kwani kwa kupanda kwetu mbegu hasi, ndio hatimaye huturudia mara tatu zaidi ya kile tulichopanda na maumivu yake kihisia huwa ni makubwa sana. Lakini kama tukipanda mbegu chanya, hakika mavuno yake huwa makubwa kuliko kawaida, hebu jaribu uone.
      Jambo lingine ni kusamehe, kusamehe ni muhimu kwetu, hata kama utakuwa umefanyiwa jambo baya kiasi gani. Kwa kusamehe kwetu tunakuwa tumejipa nafuu dhidi ya maumivu ya kihisia pale tukumbukapo juu ya yale tuliyotendewa na wenzetu. Zipo faida nyingi sana tunazopata pale tunaposamehe, lakini kubwa zaidi ni kule kumudu kusahau yale tuliyotendewa na hivyo kuwaza mambo mazuri ya yenye tija katika maisha yetu, badala ya kufikiria mabaya au kulipiza kisasi dhidi wale waliotutendea kinyume na matarajio yetu.

      *******MWISHO********

      Sehemu ya kwanza ya habari hii, bofya hapa:
      http://www.jamiiforums.com/mahusiano...wa-ghafla.html


      Ndugu wana JF, habari hii hainihusu mimi MTAMBUZI, bali iliwahi kuandikwa katika gazeti la Jitambue. Hii ni habari ya kweli kabisa ambayo ilimpata msomaji wa gazeti la Jitambue, ambapo kwa hiyari yake aliamua kuiweka habari ya maisha yake katika gazeti hilo ili wasomaji wapate kujifunza kupitia uzoefu wake.
      RR, Rutashubanyuma, AZIMIO and 1 others like this.

    2. Miaka 50

    3. #2
      Lizzy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Location : UngaLTD!
      Posts : 21,403
      Rep Power : 14597
      Likes Received
      7869
      Likes Given
      1969

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Sasa kwanini hujaziunganisha?

      Nwy hayo ni mambo yanayowakuta watu kila siku. . .na wakuumbuka wanaumbuka si kidogo.
      Mtambuzi likes this.

    4. #3
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,647
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Mhh siyo mchezo. Kufa kufaana.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    5. #4
      HorsePower's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd August 2008
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 2,658
      Rep Power : 3798
      Likes Received
      1673
      Likes Given
      1495

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Asante Mtambuzi kwa uzi mzuri. Ni kweli tunatakiwa kupanda mbegu chanya na kuwa na roho za kiungwana na kuwajali wenzetu. Tuko duniani, na yule tunayemuona leo yuko hivi au uwezo wako uko chini, kesho anaweza kubadilika akawa mtu tofauti kabisa na wa msaada katika maisha yako. Ni vyema tupendane na kutendeana mema.

      Thanks Mtambuzi.
      Don’t judge each day by the harvest you reap but by the seeds that you plant.

    6. #5
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8249
      Likes Given
      17379

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Quote By Lizzy
      Sasa kwanini hujaziunganisha?

      Nwy hayo ni mambo yanayowakuta watu kila siku. . .na wakuumbuka wanaumbuka si kidogo.
      Lizzy nilitaka kufanya hivyo, lakini nikaona ingekuwa ndefu sana.......................... .
      Nadhani kwa kufanya hivi, nitawapa wavivu kama kina fazaa wasome kwa utulivu huku wakinywa chai na mkate wa Boflo.............................. ...........
      fazaa and Boflo like this.


    7. #6
      Smile's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th July 2011
      Location : paradise
      Posts : 11,323
      Rep Power : 23406
      Likes Received
      8237
      Likes Given
      5854

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      daaah huo ndio ukristo wa kweli
      Adharusi likes this.
      It’s good to test a guy first before you believe him. But don’t let him wait that long

    8. #7
      TaiJike's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2011
      Posts : 1,156
      Rep Power : 607
      Likes Received
      387
      Likes Given
      347

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Mhh..malipo ni hapahapa duniani, kile usichopenda wewe kutendewa usimtende mwenzio.
      Jewel and mkomatembo like this.
      * Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi? * - Julius Kambarage Nyerere


    9. #8
      fazaa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th May 2009
      Posts : 2,985
      Rep Power : 1107
      Likes Received
      971
      Likes Given
      770

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Quote By Mtambuzi
      Lizzy nilitaka kufanya hivyo, lakini nikaona ingekuwa ndefu sana.......................... .
      Nadhani kwa kufanya hivi, nitawapa wavivu kama kina fazaa wasome kwa utulivu huku wakinywa chai na mkate wa Boflo.............................. ...........
      Hahaha utani pembeni mimi ni mvivu sana wa kusoma line zikisha zidi 10 au kuandika line 10, nilipokuwa collage kuna instructor mmoja alikuwa hapendezewi kabisa nikiwa nandika assignments zangu in short akawa ananipa B tu, badala A au A+ mpaa kuna siku nikamueleza are you looking for quantity or quality, akasema quality, nikamuambia mimi naona wewe unatazama quantity zaidi kuliko quality, nda akanza kunipa A+

    10. #9
      Boflo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2010
      Posts : 3,770
      Rep Power : 5461
      Likes Received
      3679
      Likes Given
      3727

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Quote By Mtambuzi
      Lizzy nilitaka kufanya hivyo, lakini nikaona ingekuwa ndefu sana.......................... .
      Nadhani kwa kufanya hivi, nitawapa wavivu kama kina fazaa wasome kwa utulivu huku wakinywa chai na mkate wa Boflo.............................. ...........
      Mtambuzi kuna siku na ww utatambuliwa
      Mtambuzi and mkomatembo like this.
      There are some people who could hear you speak a thousand words and still not understand you. And there are others who will understand—without you even speaking a word.

    11. #10
      Cantalisia's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th September 2011
      Location : Dar es salaam
      Posts : 4,953
      Rep Power : 3054
      Likes Received
      2630
      Likes Given
      2829

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Duh!mpaka nimeshindwa kula lol!inasikitisha na kufundisha,
      Km vp wape wataalam wa kuandika script maana ni story nzuri inayoweza tengenezwa bonge la movie!!!
      Mtambuzi likes this.
      "Be good to the people on your way up,coz you might meet them on your way down"

    12. #11
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8249
      Likes Given
      17379

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Quote By Cantalisia
      Duh!mpaka nimeshindwa kula lol!inasikitisha na kufundisha,
      Km vp wape wataalam wa kuandika script maana ni story nzuri inayoweza tengenezwa bonge la movie!!!
      Cantalisia Nimesha-andaa script tayari, bado natafuta Casting kwa ajili ya shooting..................

    13. #12
      NATA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th May 2007
      Posts : 4,255
      Rep Power : 8417
      Likes Received
      1134
      Likes Given
      390

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Mbona hujanitonya kama unavibwagizo katikati ya wiki?
      Mtambuzi likes this.

    14. #13
      Cantalisia's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th September 2011
      Location : Dar es salaam
      Posts : 4,953
      Rep Power : 3054
      Likes Received
      2630
      Likes Given
      2829

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Quote By Mtambuzi
      Cantalisia Nimesha-andaa script tayari, bado natafuta Casting kwa ajili ya shooting..................
      Nikikosekana humo hiyo movie haitafanyika walahhh baba!
      Mtambuzi likes this.
      "Be good to the people on your way up,coz you might meet them on your way down"

    15. #14
      mkomatembo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th December 2011
      Location : Bweleo
      Posts : 1,019
      Rep Power : 638
      Likes Received
      228
      Likes Given
      1269

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Quote By Boflo
      Mtambuzi kuna siku na ww utatambuliwa
      Teh teh teh jamani nimecheka !
      Mtambuzi likes this.

    16. #15
      mkomatembo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th December 2011
      Location : Bweleo
      Posts : 1,019
      Rep Power : 638
      Likes Received
      228
      Likes Given
      1269

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Quote By NATA
      Mbona hujanitonya kama unavibwagizo katikati ya wiki?
      Mwenzangu ! Mtambuzi AMECHAKACHUWA ! .... well done mtambuzi , story nzuri sana sana ! inasikitisha ila mwisho wake ni mzuri sana ispokuwa sijapata picha BABA YAKE ! aliishia wapi? na huyu shemeji ?
      Mtambuzi likes this.

    17. #16
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8249
      Likes Given
      17379

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Quote By mkomatembo
      Mwenzangu ! Mtambuzi AMECHAKACHUWA ! .... well done mtambuzi , story nzuri sana sana ! inasikitisha ila mwisho wake ni mzuri sana ispokuwa sijapata picha BABA YAKE ! aliishia wapi? na huyu shemeji ?
      mkomatembo........ Baba hajulikani alipo mpaka leo, lakini katika hitimisho, Joseph alimuona shemeji yake katika mazingira ambayo hakuyasimulia.

    18. #17
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8249
      Likes Given
      17379

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Quote By Cantalisia
      Nikikosekana humo hiyo movie haitafanyika walahhh baba!
      Cantalisia .....Wewe utacheza kama MSEKWA

    19. #18
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,098
      Rep Power : 27015
      Likes Received
      8249
      Likes Given
      17379

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Quote By NATA
      Mbona hujanitonya kama unavibwagizo katikati ya wiki?
      NATA sikutaka usome hii habari kwani nilihisi ungelia kwa huzuni...............!

    20. #19
      bulldoza's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th September 2011
      Posts : 133
      Rep Power : 413
      Likes Received
      42
      Likes Given
      76

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      Kweli hili ni darasa.

    21. #20
      zimwimtu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2012
      Posts : 406
      Rep Power : 445
      Likes Received
      119
      Likes Given
      139

      Default Re: Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............! SEHEMU YA MW

      I salute you mtambuzi, asante sana

    Page 1 of 2 12 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...