Miaka ya hivi karibuni imegundulika kwamba hata wanaume hupata hedhi-ingawa wanaume hawana alama za nje za kuwaonesha kwamba wako kwenye hedhi, kama walivyo wanawake ambao hutoka damu siku zao za hedhi zinapofika na kukamilika.
Kwa karne na karne hakuna mtu aliyekuwa akifikiria kwamba wanaume wangeweza kuwa wanapata nao hedhi kama wanawake. Kama mwanaume akiamua kuweka kumbukumbu zake kwenye dayari na kujiangalia kila siku hali yake inavyobadilikana kuwa ya kusikitika, ya kawaida, furaha na hasira……akiifuatilia hali yake namna hiyo kwa siku zote 28 za mwezi, halafu na mwezi unaofuata, akafanya hivyo hivyo, halafu mwezi wa tatu nao akatenda hivyo, na halafu ailinganishe miezi hiyo mitatu atashangaa.
Kuna siku tatu, nne au tano ambazo zitafanana katika dayari zote tatu, lini ana hasira ana masikitiko, ni mharibifu, na tabia nyingine kama hizo. Hivyo ndivyo vipindi vya hedhi kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake. Zoezi hili anaweza kufanya mwanaume yeyote, akishindwa kupata matokeo anaweza kuwasiliana na mimi na kuuliza ni kwa nini nimeandika uongo.
Dalili za mwanaume aliye kwenye hedhi ziko akilini zaidi na sababu ziko wazi: mwanamke asili yake ni kimwili zaidi, kihisia zaidi, na mwanaume ana asili ya ubongo zaidi. Lakini mwanaume anapata usumbufu ule ule anaopata mwanamke anapokuwa kwenye hedhi. Tofauti ni moja tu, kwamba mwanaume hatoki damu. Lakini kila mwezi, baada ya siku 28, hali fulani ya kiakili na kihisia itakuwa inajirudia.
Na kama umejaribu kujichunguza kwa mwaka mzima, utashangaa kwamba, ulikuwa na hasira mgomvi, mwenye huzuni na vingine vya aina hiyo, si hivihivi tu bali ni kwa sababu ulikuwa kwenye hedhi. Kama ukishafanya zoezi nililokwambia la dayari, jiulize, kama ulipokuwa kwenye hali hizo ulikuwa umekerwa na yeyote au chochote. Utagundua kwamba hukuwa umekerwa bali ulikuwa unasumbuliwa na hedhi yako.
Ina maana basi kwamba mwanaume naye ni lazima kila mwezi awe na mabadiliko ambayo yatamfanya aingie mahali ambapo atavutana na mwanamke kimapenzi. Hili ni suala la maumbile ili kufanya kuzaliana kuwepo. Utajuaje kuwa mwanaume ameingia kwenye hali hiyo? Ndiyo pale ambapo wataalamu wamegundua hizo siku nne au tano za mabadiliko ya kiakili kwa mwanaume!
Follow Us Here