Iwe mlienda mahakamani,
au japo mashahidi jirani.
Ikiwa karatasi alisaini
kuwa utampa kiasi gani,
sasa iweje leo azue tafrani?
Mshauri afungue kesi nyengine,
ikiwa ni lazima kile mlichochuma mgawane
lakini sio leo hivi kesho vile. Lazima mkubaliane.
Vyenginevyo, atakuchuna huyo mpaka ukome.
Lakini kabla ya hapo, mburuze mkapime DNA,
isijekuwa anakuchuna kumbe mtoto ni wa mwengine.
Anecdote:
Kuna jamaa alilazimishwa kumlipia mtoto hadi atakapotimia miaka 18.
Siku ya malipo ya mwisho, alimkabidhi "bintiye" kimemo akampe mama yake.
"Hatimaye, haya ni malipo ya mwisho," kimemo kilisema.
Mama akamrejeshea kimemo pia, "Nakushukuru, kwani huyu mtoto hata si wako".
Ruta, chunga sana.
Follow Us Here