<font color="#0000cd">
Hivi denda ni nini kama siyo kunyonyana ndimi kwa wapendanao?
Kwa nini watu wazima wako tayari kunyonyana ndimi na hata kuhatarisha maisha yao....
Jibu ni kuwa wanapendana na hawana namna nyingine ya kuonyeshana ya kuwa wanapendana
Wengineo hupeana denda ili kuwashawishi wenzio wawape watakacho kwa kufanya hivyo ni hila..
Ni kweli denda lina ujumbe mzito..
Yupo nguli wa muziki wa zamani kule majuu ya UK
Yeye (Right Said Fred) alitunga wimbo mwaka 1991 na kuuita "Don't talk just kiss........."
Ujumbe wake ukiwa wewe m'mwagie madenda motomoto na mengineyo yatajipa tu.....
Usiongee na acha domo kaya kwenye mahaba kwa sababu utakaribisha ubishi usio wa lazima..
Ni kweli denda lina ujumbe mzito........
Kama denda limechukua nafasi ya kujibizana sasa ujumbe wa ukweli uko wapi?
Kama denda linatumika kuficha dhamira ya wahusika sasa mawasiliano ya kweli yako wapi?
Kama denda pia laweza kuwa ni hadaa sasa penzi la kweli utalijuaje?
Kama denda ni kiini macho mbona hutiliwa mkazo kuwa kutoa ishara ya mapenzi?
Ni kweli denda lina ujumbe mzito.........
Denda ni kizungumkuti hata korosi nenepa kusukumiwa nawe kulimeza bila mawengwe............
Karaha za kifua kikuu usizione kwa kisingizio nimependa.......
Tishio la magonjwa ya kinywa kutoweka kisa nimependwa........
Hamaki za kutapeliwa kufifilishwa na tamaa ya kupendeka na kukubalika..........]
Ni kweli denda lina ujumbe mzito........
Machaguo siyaoni kwani jamii imekwisha toa maamuzi..
Ya kuwa denda ni jeuri ya wapendanao na athari zake lazima kuvumiliwa na kubebeka.......
Mie sina kauli ila kuwatakia kila la kheri..........
Kwani tembo wapambanapo ziumiazo ni nyika......
Ama kwa hakika denda lina ujumbe mzito nami nauogopa.............sijui kwako denda limekaaje?

Reply With Quote
A baby is something you carry inside you for nine months, in your arms for three years and in your heart till the day you die





" 
Follow Us Here