JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

  Report Post
  Page 1 of 5 123 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 90
  1. Young Master's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 22nd December 2008
   Location : Arusha, Tanzania.
   Posts : 7,947
   Rep Power : 105386014
   Likes Received
   2694
   Likes Given
   2247

   Default Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Ikiwa wale wanaokusudia kuoana hawataki kuwa na mashaka mengi wala kuwa na mambo kadha wa kadha ya kuwanyima furaha baada ya kufunga ndoa, imewalazimu kufikiria vyema na kwa moyo wote juu ya jambo hili na kwa wakati huu kabla ya kuoana. Ikiwa hatua hii itafanywa kipumbavu, itakuwa mojawapo ya mambo makuu mno yawezayo kuharibu mafao ya mvulana ama msichana wawapo wamekwisha kuoana. Kwao maisha yataonekana kuwa kama mzigo wa laana. Kaitka ulimwengu huu hakuna awezaye kumnyima mwanamke furaha, ama kumharibia maisha na kufanya yamuelemee na kumchoma moyo zaidi ya mumewe; na hali kadhalika hakuna mwenye uwezo wa kupooza matumaini na jitihada za mwanaume na kuposha nguvu zake, kuharibu mvuto wake na maendeleo yake zaidi ya mkewe. Mara nyingi ni tangu dakika ile baada ya harusi ambapo maisha huanza kuwaelemea wanawake na wanaume wengi. Ndoa ni jambo ambalo lina mvuto katika ulimwengu huu, na litakuwa na mvuto katika ulimwengu ujao pia.

   Wengi hawaelewi vyema muungano huu wa ndoa. Wengi wao hudhani ya kwamba, muungano huu ni mojawapo ya njia ya kufikia upeo wa furaha; lakini laiti wangefahamu kiasi kidogo tu cha uchungu walionao wale waliounganishwa kwa kiapo cha ndoa ambacho kimewafunga kwa minyororo wasiyothubutu kuikata, hawangeshangaa kwa maelezo haya. Ndoa nyingi zinazofungwa huwa ni mkatale wa huzuni. Kuna maelfu ya watu waliounganishwa katika ndoa lakini hawapatani.

   Wale wanaofikiria kuoa ama kuolewa ni lazima wajishauri vyema kuhusu hali na mwenendo wa ndoa wanayokusudia kuwa nayo. Ni lazima vijana wafanye uchunguzi wa kutosha katika mambo yanayohusu kuchagua mpenzi na kufanya uchumba. Ewe kijana mwenzangu, jihadhari ili kile unachodhania kuwa ni dhahabu ama lulu safi kisije kikawa takataka tu. Jambo hili halipaswi kufanywa haraka. Wakati ungali bado unaweza kupenda, jihadhari usije ukapenda kama kipofu.

   Fikiria sana uone kama maisha yako na yule unayemchagua kuwa mwenzi wako wa maisha yatakuwa ya furaha ama ya kutopatana na kuhuzunisha baada ya harusi. Wanawake na wanaume wengi wameoana kana kwamba jambo la pekee lililowapasa kulijali ni kuwa wanapendana au la. Kuchagua mwenzi wa maisha kwafaa kufanywa kwa busara ili kuwawezesha wazazi na watoto pia, kuwa na hali nzuri kiroho, kiakili na kimwili.

   Mambo ya kuzingatia katika kuchagua msichana wa maisha
   Kijana wa kiume unapaswa uchague msichana ambaye atasiamama kando yake na ambaye ataweza kuchukua sehemu ya mzigo wa maisha yake, mke ambaye mvuto wake utamfanya mumewe na heshima na kumwezesha kuwa na mwenendo mwema, na ambaye kwa jili ya upendo wake, atamfanya kuwa na raha maishani mwake.

   Ewe kijana wa kiume na mwanaume mwenzangu naomba ujishauri kwa uangalifu mkubwa kuhusu mambo haya yafuatayo na bila shaka kama yakizingatiwa kwa umakini yatakuwa msaada mkubwa kwako wewe mvulana mwenye nia ya dhati ya kuoa;

   • Je huyo unayekusudia kumuoa atafanya nyumba yenu iwe ya furaha?
   • Je yeye ni mwangalifu awezaye kutunza mali, ama akishaolewa hatapoteza mapato yenu tu bali pia atazitawanya mali zenu huku akionyesha upendo wa juu juu tu?
   • Je huyo unayemtaka awe mwenzi wako ana hofu na kumcha Mungu?
   • Je ana afya njema?
   • Je ana bidii katika kazi?
   • Je msafi wa kimwili na kiroho?
   • Je ni mlevi?
   • Je ni mtii, mnyenyekevu na mwenye adabu?
   • Je anajiheshimu na kuvaa mavazi yenye heshima?
   • Je ni mwaminifu?
   • Je ni mtu anayetunza siri katika uhusiano wenu?
   • Je ni mkristo, mpagani au mwislamu mwenzangu?
   • Je mwenendo na tabia yake ikoje kwa wakati huu?


   Nafahamu kwamba mvulana ambaye ametumbukia katika kisima cha mapenzi atayadharau maswali haya kana kwamba hayana maana wala manufaa yoyote, lakini hayana budi kufikiriwa kwa umakini na kwa ungalifu mkubwa zaidi.

   Wakati wa kuchagua mke, tafakari na uelewe tabia na mwenendo wale, uone kama atakuwa mstahimilivu na mwenye bidii. Uone kama atachoka kuwatunza wazazi wako walo wazee wakati ule ambao watahitaji msaada wako. Uone kama atakushawishi utengane nao na kukushawishi umpende yeye peke yake na kusahau baba na mama ambao badala ya kupata binti watakuwa wamempoteza mwana.

   Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mvulana wa maisha
   Kabla msichana hajatoa mkono wake kwa mvulana na kuvishwa pete ya uchumba, kwanza na ajiulize kama yule mvulana wanayekaribia kuoana anafaa ama vipi. Mwenedo wake na tabia yake ya siku zilizopita ulikuwa wa namna gani? Je maisha yake ni masafi? Je upendo akuonyeshao unatoka moyoni na unaonyesha heshima na tabia njema ama ni upendo wa hivi hivi tu? Je anao mwendendo ambao utanifanya kuwa na furaha? Mimi kama mke nitaweza kuwa na furaha niwapo kwake? Je ataniruhusu kudumisha tabia yangu na kunipa uhuru ama itanilazimu kutupilia mbali yote na kufuata matakwa yake? Maswali kama haya yakizingatiwa kwa busara yatakuwa na manufaa sana katika maisha yajayo ya msichana ambaye anatarajia kuolewa.

   Kila msichana anayetamani kuwa na familia yenye furaha na amani, ambayo haitakuwa na udhaifu wala huzuni katika siku za baadae na ajiulize maswali haya kabla ya kutoa ukubali wake wa upendo.

   • Je huyo unayemtaka awe mwenzi wako ana hofu na kumcha Mungu?
   • Je ana afya njema?
   • Je ana bidii katika kazi?
   • Je msafi wa kimwili na kiroho?
   • Je ni mlevi?
   • Je ni mtii, mnyenyekevu na mwenye adabu?
   • Je anajiheshimu na kuvaa mavazi yenye heshima?
   • Je ni mwaminifu?
   • Je ni mtu anayetunza siri katika uhusiano wenu?
   • Je ni mkristo, mpagani au mwislamu mwenzangu?
   • Je mpenzi wangu anaye mama?
   • Je tabia ya mama yake ikoje?
   • Je anatambua wajibu wake kwa mamaye?
   • Je anajali upendo na furaha ya mama yake?
   • Ikiwa hajali wala hamheshimu mama yake, kweli ataweza kuonyesha heshima na upendo, wema na usikivu kwa mkewe?
   • Je harusi itakapokwisha atakuwa na huruma kwa makosa yangu ama atakuwa ananikosoa mara kwa mara huku akiwa mgomvi na mkali?


   Katika kuyajibu maswali haya shauklu nyingi yaweza kupishia mbali makosa na kasoro za mchumba wako, lakini upendo wa kweli hautaficha neno. Katika kuchagua mwenzi wa maisha, msichana na achague mvulana mwenye tabia na mwenendo safi wa kibinadamu, aliye na bidii, mwangalifu, mwenye heshima na aliye mwaminifu na mnyofu.

   Ikiwa umefanya uchumba na mtu ambaye huelewi vyema tabia yake, usidhani kushika uchumba kutakulazimisha kuchukua kiapo cha ndoa na kuungana na mtu ambaye humpendi na ambaye wala hutamheshimu maishani mwako. Jihadhari sana unapofanya uchumba wenye masharti; lakini hata ukiwa ni uchumba wenye masharti, ni bora mara kumi kuuvunjilia mbali huo uchumba kabla ya kufunga ndoa kuliko kuja kuvunja ndoa baadae kama wengi wafanyavyo.

   Written & Prepared by:
   Young Master
   Last edited by Young Master; 12th March 2015 at 19:35.
   If you love me let me know, If you don't then let me go.


  2. King Kong III's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th October 2010
   Location : Enaboishu-Umenyeni
   Posts : 23,599
   Rep Power : 168829830
   Likes Received
   9030
   Likes Given
   3536

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Weka source ya hio kitu,bado haujapata upeo wa kuandika makitu kama hayo!!

  3. Young Master's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 22nd December 2008
   Location : Arusha, Tanzania.
   Posts : 7,947
   Rep Power : 105386014
   Likes Received
   2694
   Likes Given
   2247

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Quote By King Kong III View Post
   Weka source ya hio kitu,bado haujapata upeo wa kuandika makitu kama hayo!!
   Umdhaniae siye kumbe ndiye. Kama huamini ni mimi ndiye niliyeandika, search on the google uone kama utapata kitu kama hiki. Dont judge a book by its cover.
   If you love me let me know, If you don't then let me go.

  4. Reserved's Avatar
   Moderator Array
   Join Date : 16th September 2008
   Location : Maswa
   Posts : 740
   Rep Power : 5402
   Likes Received
   64
   Likes Given
   87

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Appreciate
   Umejitahidi kuandika

   Asante sana

  5. Young Master's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 22nd December 2008
   Location : Arusha, Tanzania.
   Posts : 7,947
   Rep Power : 105386014
   Likes Received
   2694
   Likes Given
   2247

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Quote By JF Moderator 1 View Post
   Appreciate
   Umejitahidi kuandika

   Asante sana
   You are welcome
   If you love me let me know, If you don't then let me go.


  6. Aisha Adam's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th April 2011
   Posts : 463
   Rep Power : 633
   Likes Received
   95
   Likes Given
   20

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Thanks kwa somo nafikiri litafaa kwa yule atakae lielewa na kulifanyia kazi

  7. rifwima's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st April 2010
   Posts : 438
   Rep Power : 680
   Likes Received
   136
   Likes Given
   442

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Good and contented! Nimejifunza kitu mpwa! Hongera sana.

  8. Pokola's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th July 2010
   Location : Tanzania
   Posts : 709
   Rep Power : 722
   Likes Received
   145
   Likes Given
   125

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   You are trying to be a theorist. With many emotional gaps in your boyish composition above, I perceive you as an erratic and immature author.

   However, keep trying.
   Watanzania ikimbieni Rushwa!!

  9. Young Master's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 22nd December 2008
   Location : Arusha, Tanzania.
   Posts : 7,947
   Rep Power : 105386014
   Likes Received
   2694
   Likes Given
   2247

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Quote By Aisha Adam View Post
   Thanks kwa somo nafikiri litafaa kwa yule atakae lielewa na kulifanyia kazi
   U are welcome. Nadhani itapendeza zaidi kama wewe ndio ukiwa wa kwanza kulifanyia kazi
   If you love me let me know, If you don't then let me go.

  10. Young Master's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 22nd December 2008
   Location : Arusha, Tanzania.
   Posts : 7,947
   Rep Power : 105386014
   Likes Received
   2694
   Likes Given
   2247

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Quote By Pokola View Post
   You are trying to be a theorist. With many emotional gaps in your boyish composition above, I perceive you as an erratic and immature author.

   However, keep trying.
   Nobody can become mature without being an immature
   If you love me let me know, If you don't then let me go.

  11. Young Master's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 22nd December 2008
   Location : Arusha, Tanzania.
   Posts : 7,947
   Rep Power : 105386014
   Likes Received
   2694
   Likes Given
   2247

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Quote By rifwima View Post
   Good and contented! Nimejifunza kitu mpwa! Hongera sana.
   Asante sana mkuu.
   If you love me let me know, If you don't then let me go.

  12. mkonowapaka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th February 2010
   Location : Udinde
   Posts : 1,466
   Rep Power : 895
   Likes Received
   645
   Likes Given
   345

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   una miaka mingapi.umeoa?? na je umejifunza kutokana na 'makosa' au ndivyo ulivyoelimishwa kabla................maana uzoefu wangu unaonyesha 'yaliowashinda' huwa wazuri saaana kushauri....hehehe source kaka yangu

  13. Young Master's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 22nd December 2008
   Location : Arusha, Tanzania.
   Posts : 7,947
   Rep Power : 105386014
   Likes Received
   2694
   Likes Given
   2247

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Quote By mkonowapaka View Post
   una miaka mingapi.umeoa?? na je umejifunza kutokana na 'makosa' au ndivyo ulivyoelimishwa kabla................maana uzoefu wangu unaonyesha 'yaliowashinda' huwa wazuri saaana kushauri....hehehe source kaka yangu
   Mpaka sasa sijaoa mkuu. Na elimu hii ya mapenzi nilikuwa nayo tokea zamani ambapo niliipata elimu hii kutokana na kujivunza, kufanya uchunguzi na kusoma vitabu vingi vya mapenzi. Mwanzoni nilikuwa daktari na mwalimu wa mapenzi ambapo nilikuwa nikitoa elimu na ushauri wa mapenzi kwa watu wa rika zote ila niliamua kuacha kazi hiyo miaka miwili iliyopita baada ya kuzidiwa na majukumu.
   If you love me let me know, If you don't then let me go.

  14. mgeni10's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th November 2010
   Location : Morogoro
   Posts : 1,100
   Rep Power : 440209
   Likes Received
   362
   Likes Given
   1281

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Young _ Master Mbona unapigana vita ambayo haipo???

   Usirushe ngumi Hewani Hakuna adui huko

   Sema tu Hakuna chanzo ila Nimeshushiwa na Mungu niwape wengine, Inatosha

  15. Kuchayaa's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 28th December 2011
   Posts : 106
   Rep Power : 526
   Likes Received
   10
   Likes Given
   0

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Good Job mwanawane, keep it up!

  16. cheseo's Avatar
   Member Array
   Join Date : 21st September 2011
   Location : morogoro
   Posts : 79
   Rep Power : 534
   Likes Received
   18
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By Young_Master View Post
   Nobody can become mature without being an immature
   We noma,mpe huyo mshamba hajielewi

  17. DOMA's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th March 2011
   Posts : 926
   Rep Power : 0
   Likes Received
   308
   Likes Given
   5

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   We umeoa?

  18. NGENDA NGOLOMA's Avatar
   Member Array
   Join Date : 18th February 2012
   Posts : 23
   Rep Power : 501
   Likes Received
   10
   Likes Given
   0

   Post Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   It's good analysis dogo. Make sure that u make what u trust

  19. Young Master's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 22nd December 2008
   Location : Arusha, Tanzania.
   Posts : 7,947
   Rep Power : 105386014
   Likes Received
   2694
   Likes Given
   2247

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Quote By mgeni10 View Post
   Young _ Master Mbona unapigana vita ambayo haipo???

   Usirushe ngumi Hewani Hakuna adui huko

   Sema tu Hakuna chanzo ila Nimeshushiwa na Mungu niwape wengine, Inatosha
   Ha ha haaaa!! Sawa sawa mkuu. Nimekupata.
   If you love me let me know, If you don't then let me go.

  20. Young Master's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 22nd December 2008
   Location : Arusha, Tanzania.
   Posts : 7,947
   Rep Power : 105386014
   Likes Received
   2694
   Likes Given
   2247

   Default Re: Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mwenzi wa maisha

   Quote By Kuchayaa View Post
   Good Job mwanawane, keep it up!
   Thnx mwanawane. I will keep up the good job i have started
   If you love me let me know, If you don't then let me go.


  Page 1 of 5 123 ... LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...