Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

    Report Post
    Page 1 of 5 123 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 84
    1. #1
      Biznocrats's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 241
      Rep Power : 439
      Likes Received
      26
      Likes Given
      23

      Default Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Naona Watanzania wanaonyesha ushabiki wao kuhusu nani wanamtaka awe Rais Kenya kati ya Raila na Uhuru. Si vibaya kufanya hivyo kwani Kenya ni ndugu zetu. Tumetenganishwa tu na mipaka iliyowekwa na wakoloni kwa ajili ya kutupora utajri wetu. Huu mimi ni mtazamo wangu kuhusu kinyang'anyiro hicho cha Urais:

      Mimi ni kati ya watu wale ambao walipenda sana Odinga achukuwe madaraka kipindi kilichopita ili kuondoa hali ya kabila moja kutawala Kenya lenyewe tu na kuyaacha makabila mengine kwani ni jambo linalotudhalilisha Waafrika wote!!!!!

      Bahati mbaya sana Odinga hakuweza kuchukua madaraka juu ya kwamba yeye alikuwa na kila support ya Wakenya wenyewe na dunia nzima kwa ujumla kwamba ni mshindi halali wa uchaguzi ule. Lakini the so called “mbabe wa dunia” wakati ule chini ya urais wa Bush Junior akatumia ubabe wa Taifa lake kulazimisha Wakenya na Dunia nzima wakubali Raila ni Rais wa Kenya against the will of Kenyans kwa kutumia maneno ya kibabe kama LAZIMA maamuzi feki ya kupikwa yaheshimiwe ili Kibaki apite!

      Kibaki akapita kwa mgongo wa Marekani (Bush Junior) na tena kwa gharama kubwa ya damu ya raia wa Kenya wasio na hatia! Kiasi gani Kibaki alimlipa Bush kupitia mali za Kenya ili amkingie kifua kuendelea kun’gan’gania madaraka Mungu ndio anayejua.

      Bush ukaisha mda wake wa utawala. Akaingia Rais mwingine, Barrack Obama. Kwa mtazamo wangu akaona kwamba Odinga ameonewa na Wakenya wameuliwa kwa makosa kwa ajili ya Bush Junior kuangalia maslahi yake binafsi zaidi ya maslahi ya Wakenya. Nadhani ikamuuma sana kwa sababu hakuna mtu angeweza kuishawishi Mahakama ya Kimataifa iwafuatilie wauaji wa kimbari wa Kenya kwenye uchaguzi ule wa Kenya ambapo Raila alikuwa mshindi rasmi zaidi ya Marekani kwa sababu aliyeufunika ule ukatili alikuwa ni Rais wa Marekani wa wakati ule (Bush Junior) kwa kunyamanzisha mataifa yote ya ulimwenguni ambayo hayakuwa tayari kuona Wakenya wananyimwa haki yao halali ya kumchagua Rais wao (Waingereza ambao walikuwa wakoloni nchini Kenya walijitokeza wazi wazi kwenye sakata lile na wakaamua kua upande wa Mungu kwa kutetea haki za Wakenya wampate Rais wao waliyomchagua lakini walifyata mkia baada ya Bush Junior kutumia ubabe kutishia dunia nzima kuhusu mpango wake wa kuhakikisha kwamba Kibaki anakua Rais wa Kenya kwa gharama yeyote ile! )

      Sasa baada ya kuingia Obama, vumbi la kuwavurumisha madagaa wa uuwaji wa kimbari Kenya (Kina Uhuru etal) na kuwaacha waasisi wakuu wa mauaji hayo ya kimbari (Kibaki na Bush) likapamba moto!!

      Ni wazi kwamba Mwafrika yeyote mwenye akili timamu hata support move hii ya kumhukumu Uhuru kwani aliyeruhusu mauaji ya kimbari ya Wakenya in the first place ni Rais wa Markenai (Bush Junior chini ya utawala wake) na anayetaka kugeuza kibao kwa kuwaacha wahalifu halisi na kuwavamia vidagaa ni Rais huyo huyo wa Marekani (Obama).

      Am sorry to say that itakuwa ni ujinga mkubwa sana kwa Wakenya kutompigia kura Uhuru kwa sababu wanahofia ataburutwa the Hague kutokana na hayo niliyoyaeleza hapo juu. Lakini nafahamu vile vile kwamba Wakenya si wajinga. Ni kati ya Waafrika ambao ni waerevu.

      Kama kweli tunataka kutoa hukumu kwa mauaji ya kimbari yaliyofanyika Kenya basi ni lazima Bush Junior na Kibaki wawe washtakiwa wakuu huko the Hague. Vinginevyo tuache kuwadharau Waafrika. Hata kama sisi ni masikini wa kutupwa kwani umasikini wetu ni mfumo tu wa dunia wa uloloni mambo leo unaokumbatiwa na watawala wetu wasioona mbali ambao wanapewa support na mataifa yaliyoendelea ambayo hayana nia yeyote ya kutunyanyua sisi Waafrika zaidi ya kutuibia na kutudharau!!!!!

      Kizazi kipya cha Afrika chenye kujiamini na ambacho kiko tayari kupambana kwa nguvu zote na udhalilishaji wa Waafrika duniani kimeanza kujiweka sawa. Tumegundua kwamba hatuwezi kutegemea viongozi wetu wa kisiasa wanaowekwa kwa maslahi ya mataifa machache kutukomboa sisi Waafrika.

      A Bottom up movement is around the corner and it will spread throughout Africa for the betterment of not only Africans but the rest of the world since a productive African will add value to the rest of the world and increase economic space for all global citizens and hence a better world for all.

      MUNGU IBARIKI AFRICA. MUNGU IBARIKI DUNIA.

    2. FemaTV & Radio

    3. #2
      lane's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th January 2013
      Posts : 226
      Rep Power : 363
      Likes Received
      72
      Likes Given
      21

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      asasnte kwa darasa
      Biznocrats likes this.

    4. #3
      master peace's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th December 2012
      Posts : 1,295
      Rep Power : 582
      Likes Received
      393
      Likes Given
      388

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Good evening Sir / Madam !!
      I have gone through your post, however it comes to my attention that you have forgotten one thing, Please take a note that "there is no fairness under the sun"
      muonamambo and Biznocrats like this.
      "Uzuri ni kipimo cha Ubaya"

    5. #4
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,669
      Rep Power : 975
      Likes Received
      580
      Likes Given
      10

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Biznocrats nakuomba huwe makini,achana na siasa za majitaka,mshindi wa kura ya urais uchaguzi huo alikua Mwai Kibaki.

    6. #5
      Askari Kanzu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th January 2011
      Posts : 3,747
      Rep Power : 4735
      Likes Received
      766
      Likes Given
      1086

      Quote By Biznocrats
      ...(Waingereza ambao walikuwa wakoloni nchini Kenya walijitokeza wazi wazi kwenye sakata lile na wakaamua kua upande wa Mungu kwa kutetea haki za Wakenya...)...
      Duhu, aisee yaani ni kweli unaamini kwamba waingereza huwaga wanasimama upande wa Mungu "kutetea" haki za Wakenya?

    7. Miaka 50

    8. #6
      Edzeame's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th August 2012
      Posts : 161
      Rep Power : 373
      Likes Received
      23
      Likes Given
      17

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By Biznocrats

      Kama kweli tunataka kutoa hukumu kwa mauaji ya kimbari yaliyofanyika Kenya basi ni lazima Bush Junior na Kibaki wawe washtakiwa wakuu huko the Hague. Vinginevyo tuache kuwadharau Waafrika. Hata kama sisi ni masikini wa kutupwa kwani umasikini wetu ni mfumo tu wa dunia wa uloloni mambo leo unaokumbatiwa na watawala wetu wasioona mbali ambao wanapewa support na mataifa yaliyoendelea ambayo hayana nia yeyote ya kutunyanyua sisi Waafrika zaidi ya kutuibia na kutudharau!!!!!

      MUNGU IBARIKI AFRICA. MUNGU IBARIKI DUNIA.
      Ilikuwa ni Kibaki na Raila kuenda kujibu mashtaka. Lakini Annan aliwahimiza kibaki na Raila kutia saini MOU ya amani, na hii ikawaondolea lawama wawili hao ya umwagikaji wa damu. Makosa kubwa ambayo raila aliongozwa kufanya na kofi-annan.
      If you tell the truth you don't have to remember anything - Emmanuel FB

    9. #7
      Biznocrats's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 241
      Rep Power : 439
      Likes Received
      26
      Likes Given
      23

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By master peace
      Good evening Sir / Madam !!
      I have gone through your post, however it comes to my attention that you have forgotten one thing, Please take a note that "there is no fairness under the sun"
      Surely there isn't. But remaining numb isn't fair either. Better raise up the voice so as to raise awareness of the disadvantaged ones with a view to harnessing their energy towards finding a solution to this. Africa Unity will go too far in addressing many of these problems and empower the Africans to take posit in this unfair world. Hence the bottom up non-partisan movement we are engineering that will tell the fellow Africans of the need to unite as a single country in the long run and campaigning for Africans to elect leaders who are pro African Union.

    10. #8
      Biznocrats's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 241
      Rep Power : 439
      Likes Received
      26
      Likes Given
      23

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By timbilimu
      Biznocrats nakuomba huwe makini,achana na siasa za majitaka,mshindi wa kura ya urais uchaguzi huo alikua Mwai Kibaki.
      Mimi niko makini sana na SITAHARUKI. Kama mshindi alikuwa Kibaki kwa nini aliamua kugawana madaraka na Odinga ambaye hakushinda?
      FirstLady1 likes this.

    11. #9
      Biznocrats's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 241
      Rep Power : 439
      Likes Received
      26
      Likes Given
      23

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By Askari Kanzu
      Duhu, aisee yaani ni kweli unaamini kwamba waingereza huwaga wanasimama upande wa Mungu "kutetea" haki za Wakenya?
      Kusimamia haki ya mshindi halali wa kura za wananchi ni kuwa upande wa Mungu. Hicho ndicho walichokifanya Uingereza wakati ule.

    12. #10
      Askari Kanzu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th January 2011
      Posts : 3,747
      Rep Power : 4735
      Likes Received
      766
      Likes Given
      1086

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By Biznocrats
      Kusimamia haki ya mshindi halali wa kura za wananchi ni kuwa upande wa Mungu. Hicho ndicho walichokifanya Uingereza wakati ule.
      Endelea kuamini hivyo!

    13. #11
      Biznocrats's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 241
      Rep Power : 439
      Likes Received
      26
      Likes Given
      23

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By Edzeame
      Ilikuwa ni Kibaki na Raila kuenda kujibu mashtaka. Lakini Annan aliwahimiza kibaki na Raila kutia saini MOU ya amani, na hii ikawaondolea lawama wawili hao ya umwagikaji wa damu. Makosa kubwa ambayo raila aliongozwa kufanya na kofi-annan.
      Sasa kama wahusika wakuu wa mauaji yale wamesamehewa kwa sababu yoyote ile kwa nini waburutwe vidagaa (accomplices)? Does it make sense?

    14. #12
      Biznocrats's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 241
      Rep Power : 439
      Likes Received
      26
      Likes Given
      23

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By Askari Kanzu
      Endelea kuamini hivyo!
      Sina rafiki wala adui wa kudumu. Nina maslahi ya kudumu.

    15. #13
      Askari Kanzu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th January 2011
      Posts : 3,747
      Rep Power : 4735
      Likes Received
      766
      Likes Given
      1086

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By Biznocrats
      Sina rafiki wala adui wa kudumu. Nina maslahi ya kudumu.
      Hauna haja ya kujitetea. Hakuna anayekushutumu!

    16. #14
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,131
      Rep Power : 41571
      Likes Received
      6038
      Likes Given
      1054

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Ukishataka mtu ashinde urais kwa sababu " ili kuondoa hali ya kabila moja kutawala Kenya lenyewe tu na kuyaacha makabila mengine" ushakubali kwamba unaendeleza ukabila.

      Wala huumalizi ukabila kama unavyojidanganya.

      Maana unafanya kabila liwe kigezo cha urais.
      FirstLady1 likes this.
      Banda lishavunjika, jogoo kaondoka. Vifaranga hangaika, kumtoa nyoka.

    17. #15
      Biznocrats's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 241
      Rep Power : 439
      Likes Received
      26
      Likes Given
      23

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By Kiranga
      Ukishataka mtu ashinde urais kwa sababu " ili kuondoa hali ya kabila moja kutawala Kenya lenyewe tu na kuyaacha makabila mengine" ushakubali kwamba unaendeleza ukabila.

      Wala huumalizi ukabila kama unavyojidanganya.

      Maana unafanya kabila liwe kigezo cha urais.
      Hili nimelizungumzia kwa context ya Kenya. Unless kura zinapigwa kwa ukabila in the first place, haiwezekani kabila moja tu likatawala Kenya kwa sababu Kenya kuna watu makini wengi kutoka kwenye makabila mengine ambao wanao uwezo wa kuwa marais wa Kenya.

    18. #16
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,131
      Rep Power : 41571
      Likes Received
      6038
      Likes Given
      1054

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By Biznocrats
      Hili nimelizungumzia kwa context ya Kenya. Unless kura zinapigwa kwa ukabila in the first place, haiwezekani kabila moja tu likatawala Kenya kwa sababu Kenya kuna watu makini wengi kutoka kwenye makabila mengine ambao wanao uwezo wa kuwa marais wa Kenya.
      Ukishasema fulani awe rais kwa sababu kabila fulani limetawala sana urais, unampa mtu urais kwa misingi ya ukabila.

      Humalizi ukabila, unaendeleza ukabila.

      Context notwithstanding, dunia nzima.

      Mwisho utataka urais wa kupokezana kama Nigeria huko, akitoka Muislamu wa kaskazini aje Mkristo wa Kusini, and vice versa kama clockwork.

      Afrika tuna safari ndefu sio tu kwa sababu tuna ukabila.

      Afrika tuna safari ndefu kwa sababu hata wanaousema ukabila, wanatupa suluhisho la ukabila.
      Last edited by Kiranga; 7th March 2013 at 01:08.
      Banda lishavunjika, jogoo kaondoka. Vifaranga hangaika, kumtoa nyoka.

    19. #17
      Biznocrats's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 241
      Rep Power : 439
      Likes Received
      26
      Likes Given
      23

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By Kiranga
      Ukishasema fulani awe rais kwa sababu kabila fulani limetawala sana urais, unampa mtu urais kwa misingi ya ukabila.

      Humalizi ukabila, unaendeleza ukabila.

      Context notwithstanding, dunia nzima.
      Sijasema kwamba fulani awe rais kwa sababu kabila fulani limetawala sana. Ukweli ni kwamba Wakenya waliamua kumchagua Raila wakati ule lakini wanaodhani wao wana haki ya kutawala dhidi ya makabila mengine nchini Kenya ndio walioamua kuanzisha vurugu na kuua watu ili wao waendelee kutawala. Hii ni aibu kubwa Africa na ni lazima ipigwe vita kwa nguvu zote.

    20. #18
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,131
      Rep Power : 41571
      Likes Received
      6038
      Likes Given
      1054

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By Biznocrats
      Naona Watanzania wanaonyesha ushabiki wao kuhusu nani wanamtaka awe Rais Kenya kati ya Raila na Uhuru. Si vibaya kufanya hivyo kwani Kenya ni ndugu zetu. Tumetenganishwa tu na mipaka iliyowekwa na wakoloni kwa ajili ya kutupora utajri wetu. Huu mimi ni mtazamo wangu kuhusu kinyang'anyiro hicho cha Urais:

      Mimi ni kati ya watu wale ambao walipenda sana Odinga achukuwe madaraka kipindi kilichopita ili kuondoa hali ya kabila moja kutawala Kenya lenyewe tu na kuyaacha makabila mengine kwani ni jambo linalotudhalilisha Waafrika wote!!!!!

      Bahati mbaya sana Odinga hakuweza kuchukua madaraka juu ya kwamba yeye alikuwa na kila support ya Wakenya wenyewe na dunia nzima kwa ujumla kwamba ni mshindi halali wa uchaguzi ule. Lakini the so called “mbabe wa dunia” wakati ule chini ya urais wa Bush Junior akatumia ubabe wa Taifa lake kulazimisha Wakenya na Dunia nzima wakubali Raila ni Rais wa Kenya against the will of Kenyans kwa kutumia maneno ya kibabe kama LAZIMA maamuzi feki ya kupikwa yaheshimiwe ili Kibaki apite!

      Kibaki akapita kwa mgongo wa Marekani (Bush Junior) na tena kwa gharama kubwa ya damu ya raia wa Kenya wasio na hatia! Kiasi gani Kibaki alimlipa Bush kupitia mali za Kenya ili amkingie kifua kuendelea kun’gan’gania madaraka Mungu ndio anayejua.

      Bush ukaisha mda wake wa utawala. Akaingia Rais mwingine, Barrack Obama. Kwa mtazamo wangu akaona kwamba Odinga ameonewa na Wakenya wameuliwa kwa makosa kwa ajili ya Bush Junior kuangalia maslahi yake binafsi zaidi ya maslahi ya Wakenya. Nadhani ikamuuma sana kwa sababu hakuna mtu angeweza kuishawishi Mahakama ya Kimataifa iwafuatilie wauaji wa kimbari wa Kenya kwenye uchaguzi ule wa Kenya ambapo Raila alikuwa mshindi rasmi zaidi ya Marekani kwa sababu aliyeufunika ule ukatili alikuwa ni Rais wa Marekani wa wakati ule (Bush Junior) kwa kunyamanzisha mataifa yote ya ulimwenguni ambayo hayakuwa tayari kuona Wakenya wananyimwa haki yao halali ya kumchagua Rais wao (Waingereza ambao walikuwa wakoloni nchini Kenya walijitokeza wazi wazi kwenye sakata lile na wakaamua kua upande wa Mungu kwa kutetea haki za Wakenya wampate Rais wao waliyomchagua lakini walifyata mkia baada ya Bush Junior kutumia ubabe kutishia dunia nzima kuhusu mpango wake wa kuhakikisha kwamba Kibaki anakua Rais wa Kenya kwa gharama yeyote ile! )

      Sasa baada ya kuingia Obama, vumbi la kuwavurumisha madagaa wa uuwaji wa kimbari Kenya (Kina Uhuru etal) na kuwaacha waasisi wakuu wa mauaji hayo ya kimbari (Kibaki na Bush) likapamba moto!!

      Ni wazi kwamba Mwafrika yeyote mwenye akili timamu hata support move hii ya kumhukumu Uhuru kwani aliyeruhusu mauaji ya kimbari ya Wakenya in the first place ni Rais wa Markenai (Bush Junior chini ya utawala wake) na anayetaka kugeuza kibao kwa kuwaacha wahalifu halisi na kuwavamia vidagaa ni Rais huyo huyo wa Marekani (Obama).

      Am sorry to say that itakuwa ni ujinga mkubwa sana kwa Wakenya kutompigia kura Uhuru kwa sababu wanahofia ataburutwa the Hague kutokana na hayo niliyoyaeleza hapo juu. Lakini nafahamu vile vile kwamba Wakenya si wajinga. Ni kati ya Waafrika ambao ni waerevu.

      Kama kweli tunataka kutoa hukumu kwa mauaji ya kimbari yaliyofanyika Kenya basi ni lazima Bush Junior na Kibaki wawe washtakiwa wakuu huko the Hague. Vinginevyo tuache kuwadharau Waafrika. Hata kama sisi ni masikini wa kutupwa kwani umasikini wetu ni mfumo tu wa dunia wa uloloni mambo leo unaokumbatiwa na watawala wetu wasioona mbali ambao wanapewa support na mataifa yaliyoendelea ambayo hayana nia yeyote ya kutunyanyua sisi Waafrika zaidi ya kutuibia na kutudharau!!!!!

      Kizazi kipya cha Afrika chenye kujiamini na ambacho kiko tayari kupambana kwa nguvu zote na udhalilishaji wa Waafrika duniani kimeanza kujiweka sawa. Tumegundua kwamba hatuwezi kutegemea viongozi wetu wa kisiasa wanaowekwa kwa maslahi ya mataifa machache kutukomboa sisi Waafrika.

      A Bottom up movement is around the corner and it will spread throughout Africa for the betterment of not only Africans but the rest of the world since a productive African will add value to the rest of the world and increase economic space for all global citizens and hence a better world for all.

      MUNGU IBARIKI AFRICA. MUNGU IBARIKI DUNIA.
      Post yako yote hii hapa
      Banda lishavunjika, jogoo kaondoka. Vifaranga hangaika, kumtoa nyoka.

    21. #19
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,131
      Rep Power : 41571
      Likes Received
      6038
      Likes Given
      1054

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By Biznocrats
      Sijasema kwamba fulani awe rais kwa sababu kabila fulani limetawala sana. Ukweli ni kwamba Wakenya waliamua kumchagua Raila wakati ule lakini wanaodhani wao wana haki ya kutawala dhidi ya makabila mengine nchini Kenya ndio walioamua kuanzisha vurugu na kuua watu ili wao waendelee kutawala. Hii ni aibu kubwa Africa na ni lazima ipigwe vita kwa nguvu zote.
      You are righ, hujasema. Umeandika. Na maandishi yapo hapa.

      Unakataa maneno yako mwenyewe wakati yapo hapa JF?

      Umeandika

      Mimi ni kati ya watu wale ambao walipenda sana Odinga achukuwe madaraka kipindi kilichopita ili kuondoa hali ya kabila moja kutawala Kenya lenyewe tu
      Ulitaka Odinga ashinde kwa sababu za ukabila, kwamba kabila moja limetawala sana, sasa zamu ya kabila lingine, si ndivyo ulivyosema hivyo? Kuna mtu kaandika kitabu kizima kuhusu hili "It's Our Turn To Eat :The Story of a Kenyan Whistleblower".

      Sasa mimi nikikwambia unaendekeza ukabila badala ya kuumaliza, kwamba unafanya kabila la mtu kuwa kigezo cha kwamba anafaa kuwa rais au hafai, utakataaje?
      Last edited by Kiranga; 7th March 2013 at 01:31.
      Banda lishavunjika, jogoo kaondoka. Vifaranga hangaika, kumtoa nyoka.

    22. #20
      Biznocrats's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 241
      Rep Power : 439
      Likes Received
      26
      Likes Given
      23

      Default Re: Awe Uhuru au Raila, Africa bado tuna safari ndefu. Tutafakari!!

      Quote By Kiranga
      You are righ, hujasema. Umeandika. Na maandishi yapo hapa.

      Unakataa maneno yako mwenyewe wakati yapo hapa JF?

      Umeandika

      Ulitaka Odinga ashinde kwa sababu za ukabila, kwamba kabila moja limetawala sana, sasa zamu ya kabila lingine, si ndivyo ulivyosema hivyo? Kuna mtu kaandika kitabu kizima kuhusu hili "It's Our Turn To Eat :The Story of a Kenyan Whistleblower".

      Sasa mimi nikikwambia unaendekeza ukabila badala ya kuumaliza, kwamba unafanya kabila la mtu kuwa kigezo cha kwamba anafaa kuwa rais au hafai, utakataaje?
      Kama umeona hoja yangu ni kuendeleza ukabila basi mimi nitaona fahari sana kuitwa mkabila kwenye mazingira ya Kenya. Lakini vilevile soma article yangu yote halafu uipime na sio kuchukua kisehemu tu ukakishupalia kama mtu ambaye ni mvivu wa kufikiri anayetafuta jambo analodhani ni rahisi kuling'an'gania ili aonekane na yeye yupo.

    Page 1 of 5 123 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...