As Shabab watishia kukabiliana vilivyo na vikosi vya Kenya huko Somalia Wanamgambo wa as Shabab wa Somalia leo wameonya kuwa watakabiliana vilivyo na vikosi vya Kenya vilivyoingia Somalia ili kuwatafuta raia wanne wa kigeni waliotekwa nyara na wanamgambo hao. Sheikh Hassan Turki kiongozi wa ngazi za juu wa as Shabab sambamba na kuahidi kuwa watavirejesha nyuma vikosi vya Kenya, amewataka wapiganaji wote wa kundi hilo na wananchi wa Somalia kuilinda nchi yao dhidi ya askari wa Kenya aliowaita kuwa ni vikosi vya adui. Askari wa jeshi la Kenya jana waliingia kilometa 100 kaskazini mwa nchi jirani ya Somalia kwa lengo la kupambana na wapiganaji wa as Shabab ambao hivi karibuni walishambulia maeneo ya mpakani mwa Kenya na kuwateka nyara raia wa kigeni.
Maafisa wa Kenya wanasema kwamba hatua hiyo imechukuliwa kwa lengo la kulinda ardhi na mipaka yake pamoja na kuimarisha usalama.
JF the best place to be. and the POWER of God be with us all the time.
kibaru hicho, mfupa ulioishinda serikali ya mpito ya Somalia na vikosi vya kusimamia amani vya Umoja wa Afrika utaweza kuliwa na majeshi ya Kenya
Turn back?
JF the best place to be. and the POWER of God be with us all the time.
kama wana ubavu si wangeenda kupigania kisiwa cha MIGINGO
ewe shujaa uliyemngoa nduli tia mguu pale kama unaweza
Alshababu kwa sasa, is becoming a virtual militia! wanapigana vita vya lelemama kwenye twitter account yao.
Mkuu haya mambo ni kumuomba Mungu awape Al Shabaab akili za kufikili kwamba kuwahua/kujeruhi watu/raia wasio na hatia ni dhambi. Ogopa sana kupigana na militia/guerrilla wasio vaa uniform - HIT and RUN tactics ni ngumu sana kuzi-contain, cha muhimu na raia wa Kenya kushikamana kwa kusahau tofauti zenu; mkifanikisha hilo Al Shabaab watapata wakati mgumu kutimiza malengo yao, mkijisahau na kuanza kuwaita kwamba ni Virtual Militia hilo linaweza kuwa-cost an arm and leg msidhalau chochote - any lead however crude may save your lives. Mimi ndio ushauri wangu.
Najua haya lakini tukitizama nia ya wanaoleta makala kama hii, hakuna uchangunuzi wanakusudia kufanya, na hata ukiangalia mtiririko wa posts vile zinavowekwa ndio utakuta hayana maana kumbe. Ni ligi tu inayobuniwa na wasioelewa kiini cha ugaidi na madhara yake AM. Nasikitika kuwa jukwaa la kenya limekuwa dumpsite. Ashante kwa ushauri wako mzuri, lakini naonelea tuchukue a pragmatic approach na hekima zote tulizopewa na mwenyezi Mungu kumaliza ugaidi. Hakuna kushindwa mpaka dhamira yako itakapolegea na kukubali kushindwa.
Swala la Somalia/Ugaidi isiwe tu ni kitu ambacho kitawekewa hema kwa muda mrefu bila suluhu ya kuleta amani ya kudumu. Tazama matatizo yote iliyokuwa sehemu za Namibia na na sasa kuna ustawi na maendeleo. Ilichukua shughuli ya mataifa mengine Africa na wakati huu wana amani, siyo kusema mataifa husika yalimsahau Mungu wakati huo.
Kumbe bado wapo? Kutishia hakusaidii waamue kwenda kulima tu wajue moja. Vita haina msaada
We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
Ralph Waldo Emerson
Follow Us Here