Kuna makosa mengi ya jinai ambayo yanatokea katika mazingira ya makusudi na watu wanafanya hivyo kwa kujua kwamba watafikishwa mahakamani na baada ya hapo kutakuwa na mwenendo wa kesi ambayo inaweza kukaa mahakamani na kuchukua zaidi miaka 10 bila ya kufika mwisho wa kesi hiyo, kwa mfano makosa ya kukamatwa na bangi, mazao ya malia asili kinyume na sheria, pesa za bandia, wezi wa aina yoyote waliokamatwa na vitu walivyoiba "read handed" kama ng'ombe, magari na kadhalika iundwe sheria ya kuwapeleka moja kwa moja jela pasiwepo na muda wa kufanya upelelezi, Inashangaza kuona unaambiwa majambazi yekamatwa na silaha za kivita na risasi zake lakini majambazi hao watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika!! Je hapo upelelezi gani? Tuige baadhi ya nchi ulimwenguni kama China ambazo ukikamatwa na vitu vya hatari kama madawa ya kulevya unauawa au unafungwa jela miaka 70 pasipo na kusubiri upelelezi kwani hapa kwetu hata hizo dawa za kulevya wakati zinasubiri upelelezi zinageuka na kuwa unga wa nganu au sembe