Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Jaji Warioba: Kazi ya kukusanya maoni yaiva

    Report Post
    Results 1 to 5 of 5
    1. #1
      Kakke's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th December 2010
      Posts : 712
      Rep Power : 571
      Likes Received
      137
      Likes Given
      0

      Default Jaji Warioba: Kazi ya kukusanya maoni yaiva


      Jaji Joseph Warioba

      Tume ya kuratibu maoni kwa ajili ya kuandika Katiba mpya inatarajia kuzindua zoezi la ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wananchi muda wowote kuanzia sasa.

      Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na NIPASHE ofisini kwake.

      “Maandalizi yote tumeishayakamilisha na muda wowote tutazindua zoezi rasmi la ukusanyaji wa maoni kama tulivyopanga na wananchi wasiwe na wasiwasi,” alisema.

      Alitaja baadhi ya vitu vilivyokamilika kuwa ni masula ya kisheria na pamoja na namna watakavyoanza kuendesha zoezi hilo.

      “Wananchi wasiwe na wasiwasi, watulie muda wowote zoezi la kukusanya maoni litaanza na kila mmoja atapata fursa ya kushiriki,” alisema Jaji Warioba.

      Mwezi uliopita tume hiyo ilizinduliwa rasmi na kukabidhiwa ofisi huku Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akieleza kuwa itapewa zana za kisasa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ikiwemo magari na nyumba za kuishi jijini Dar es Salaam.

      Akizungumza na tume hiyo baada ya kuikabidhi ofisi, Balozi Sefue alisema kuna mambo 10 ambayo serikali itayafanya kwa ikiwemo utekelezaji wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati alipoiapisha Tume hiyo Aprili 13, mwaka huu.

      Akziungumza baada ya kukabidhiwa ofisi, Jaji Warioba aliahidi kwamba watatumia uwezo wao wote kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata fursa ya kutoa maoni yao.

      “Tutatumia uwezo wetu wote kutekeleza yote ambayo Watanzania wanayataka, tunakwenda kwa Watanzania watuambie wanataka Tanzania ya aina gani,” alisema Jaji Warioba.

      Rais Kikwete aliipa Tume miezi 18 kukamilisha kazi ya kukusanya maoni.


      CHANZO: NIPASHE
      (<a href="http://www.widgeo.net">widget</a>)

    2. FemaTV & Radio

    3. #2
      Sungurampole's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 17th November 2007
      Posts : 705
      Rep Power : 729
      Likes Received
      121
      Likes Given
      556

      Default Re: Jaji Warioba: Kazi ya kukusanya maoni yaiva

      Nakushauri uanze na hili la muungano kwanza
      There is a higher court than courts of justice and that is court of conscience.

      It supersedes all other courts.
      Mohandas Gandhi

    4. FJM
      #3
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,174
      Rep Power : 2568
      Likes Received
      5323
      Likes Given
      4587

      Default Re: Jaji Warioba: Kazi ya kukusanya maoni yaiva

      Hii nchi tumeshakuwa na viongozi wa ajabu kweli kweli.Celina Kombani kuongoza wizara ya sheria na katiba? Walikuwa wanafikiria nini?

    5. #4
      Luambano steve's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 30th July 2012
      Posts : 8
      Rep Power : 344
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Jaji Warioba: Kazi ya kukusanya maoni yaiva

      wiz mtpu

    6. #5
      mizambwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2008
      Posts : 1,438
      Rep Power : 975
      Likes Received
      367
      Likes Given
      1808

      Default Re: Jaji Warioba: Kazi ya kukusanya maoni yaiva

      Wezi tu hawa.

      Mbona kazi hii sasa hivi inafanywa na viongozi wa Matawi ya CCM kwa kukusanya maoni ya Wanachama wa CCM na kuwalazimisha kujaza jinsi chama kinavyotaka iwe.



      MIZAMBWA
      NABII MTARAJIWA!!!
      SASA NIMEAMINI KUWA TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA!!!!, TUANDAE KABURI LA KUIZIKA MWAKA 2015

    7. Miaka 50

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...