Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Waislamu wazindua Jukwaa la KATIBA

    Report Post
    Page 2 of 9 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 164
    1. #1
      dudus's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 2,339
      Rep Power : 1018
      Likes Received
      1323
      Likes Given
      531

      Default Waislamu wazindua Jukwaa la KATIBA

      • Kukutana Diamond Ijumaa
      • Mikoa Yote Nchini Kushiriki
      • Abas Syskes, Masheikh Kuunguruma

      Gazeti la LULU la leo Jumanne - 03 Januari 2012 linaripoti:

      Kongamano la Kitaifa la Uzinduzi wa Jukwaa la Katiba la Waislamu nchini linatarajiwa kufanyika Ijumaa ya wiki hii katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

      Habari za kuaminikia ..... zinafahamisha kuwa, kongamano hilo la siku moja linaloelezwa kuwa la kihistoria litafunguliwa na Abbas Syskes ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ...

      Pia wanasheria, masheikh mbalimbali wa jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake, pamoja na ujumbe kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani watashiriki.

      Akithibistihs habari hizo, ...., Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema hatua zote za maandalizi ya shughuli hiyo zimekamilika. ...

      Akizungumzia maudhui ya kongamano hilo, Sheikh Ponda alisema kuwa ni pamoja na kuzindua rasmi chombo kitakachojishughulisha na utoaji elimu ya katiba kwa jamii ya Waislamu nchini.

      "Chombo hicho ambacho tumekubaliana kitaitwa Jukwaa la Katiba la Waislamu, kitakuwa na jukumu la kuhakikisha Waislamu kote nchini wanakuwa na kauli moja juu ya masuala yanayohusu dini na maisha yao amabayo wangependa yawemo kwenye katiba mpya", alisema.

      Akifafanua namna Jukwaa hilo litakavyofanya kazi hiyo, Sheikh Ponda alisema kuwa, kabla ya kutazama yanayohitajika kuwemo kwenye katiba mpya, watatangulia kutoa elimu juu ya katiba ya sasa ...

      "Baada ya hapo ndipo Jukwaa litaketi na kutafakari kwa kina mahitajio ya waislamu tunayodhani ni muhimu yakaainishwa ndani ya katiba ya nchi", alizungumza Sheikh Ponda.

      ...

      Wakuu kwa muhtasari ni hayo - full stori, tafadhali pata nakala yako ya LULU.
      alyasau likes this.

    2. #21
      dudus's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 2,339
      Rep Power : 1018
      Likes Received
      1323
      Likes Given
      531

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      Quote By dudus View Post
      "Chombo hicho ambacho tumekubaliana kitaitwa Jukwaa la Katiba la Waislamu, kitakuwa na jukumu la kuhakikisha Waislamu kote nchini wanakuwa na kauli moja juu ya masuala yanayohusu dini na maisha yao ambayo wangependa yawemo kwenye katiba mpya", alisema.
      Hapo kwenye red inanipa tabu:-

      Chombo hicho kitaitwa JUKWAA LA KATIBA LA WAISLAMU

      Kitahakikisha Waislamu wanakuwa na kauli moja juu ya masuala yanyohusu DINI ambayo wangependa YAWEPO KWENYE KATIBA

      Kitahakikisha Waislamu wanakuwa na kauli moja juu ya masuala yanyohusu MAISHA YAO ambayo wangependa YAWEPO KWENYE KATIBA

      KATIBA inayozungumziwa hapa sio ya BAKWATA au Taasisi nyinge ya Kiislamu bali KATIBA YA NCHI. Ni lazima kuwa makini baadhi yetu wanapoanza kutaka DINI ZAO ziwepo kwenye KATIBA.

      Kwenye suala la MAISHA kila mtu anahitaji maisha bora kwanini mjadala usijikite kwenye MAISHA YA WANANCHI WOTE badala ya MAISHA YA WAISLAMU TU? Nashindwa kuwaelewa hawa jamaa.
      3D., mwakaboko, bshayo and 1 others like this.

    3. #22
      sweke34's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th September 2010
      Posts : 2,493
      Rep Power : 1259
      Likes Received
      734
      Likes Given
      1240

      Default

      Quote By chama View Post
      Acha kashfa za kidini, kama huna jema la kusema kaa pembeni, waislamu hatuhitaji hiyo special treatment kinachotakiwa ni chombo chenye kutoa miongozo sahihi kwa waumini, Bakwata ilianzishwa kwa nia njema tu lakini ukweli imeshindwa kutekeleza majukumu yake kama chombo, huu ni mwanzo mzuri tu, naamini waislamu wakieleshwa haki zao msingi mabadiliko makubwa ya kisiasa yatatokea Tanzania, kumbuka baadhi ya wanasiasa wetu wameanza kupandikiza chuki za kidini kwa maslahi yao binafsi.

      Chama
      Gongo la Mboto DSM.
      Waislamu kupata chombo chenye kutoa miongozo sahihi kwa Tanzania hii hatutakuja kukiona mpaka tutakapo tangulia mbele ya haki ....labda Allah awashushie chombo hicho ndipo wote kwa pamoja mtaweza kufuata miongozo yake...sorry , hili jukwaa la katiba ni chombo kingine kinachoongeza chaos zaidi kwenye utitiri wa vyombo vingi vinavyowakilisha makundi makundi tu ya waislam badala ya waislam wote kitaifa.

    4. #23
      dudus's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 2,339
      Rep Power : 1018
      Likes Received
      1323
      Likes Given
      531

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      Quote By sweke34 View Post

      Mkuu bandiko lako likiangaliwa kwa jicho makini ni kama lina ka-ukweli fulani vile. Tatizo kuu ninaloliona kwa hawa ndugu zetu ni UBAGUZI dhidi ya wasio waislamu; yaani too much u-sisi. Laiti kwenye mijadala yao hasa inayohusu maslahi ya kitaifa ingelenga utaifa (wananchi wote) zaidi badala ya wao tu. Fikiria kitu kama MAISHA eti watajadili MAISHA (bora) YA WAISLAMU na siyo ya WATANZANIA WOTE yaweje kwenye KATIBA MPYA.

      Inasikitisha kwamba kwao katika masuala ya kawaida na ya msingi ya kila mwananchi kuna mwislamu na asiye mwislamu; inasikitisha sana. Dhambi ya UBAGUZI ni mbaya mno.
      Saint Ivuga, 3D. and bshayo like this.

    5. #24
      sweke34's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th September 2010
      Posts : 2,493
      Rep Power : 1259
      Likes Received
      734
      Likes Given
      1240

      Default

      Quote By Malaria Sugu View Post
      hapa lazima MOU iondoke ndani ya katiba
      Wishful thinking. Imagine serikali irudishe vyuo,hospitali, visima nk kwa kanisa ili kanisa liviendeshe lenyewe....na nyinyi mrudishe yale majengo ya tanesco ya kile chuo chenu cha Kiislam Morogoro...unafikiri ni nani atakaye umia zaidi? Unafikiri serikali itaweza kuziba kwa haraka hilo pengo la huduma za jamii zitakazo rudishwa chini ya kanisa? Hizo ndoto zako za MOU kundoka ni kama vile kukata mbuyu mkubwa kwa kutumia kiwembe kidogo...mwisho wa siku utajichanja tu mwenyewe.

    6. #25
      The Stig's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 495
      Rep Power : 514
      Likes Received
      213
      Likes Given
      56

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      Waislam wako wengi kuliko wakristu TZ, lakini wanavyolalama, utasea ni minority

      Hivi kama hiyo MOU ikifutwa, ndiyo itaondoa matatizo yote ya Waislamu nchini?
      3D. likes this.

    7. #26
      Kanyigo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd October 2011
      Posts : 621
      Rep Power : 514
      Likes Received
      41
      Likes Given
      12

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      ngoja tuwasubiri.

    8. #27
      tedo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th August 2011
      Location : uchochoroni
      Posts : 5,761
      Rep Power : 4696
      Likes Received
      1303
      Likes Given
      913

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      Ngoja tuone.Ila nawashauri waislam mtumie busara na hekima ya hali ya juu sana katika hili mnalotaka kufanya. Naomba msikurupuke kabisa jaribu kutumia wataalam wenu hasa wanasheria katika hili. Angalieni mwisho wa siku msije mkaumbuka.
      3D. likes this.

    9. #28
      Pelekaroho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th September 2010
      Location : Bugula
      Posts : 443
      Rep Power : 533
      Likes Received
      63
      Likes Given
      22

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      Angalizo!
      NCHI HII HAINA DINI
      Ni Afadhali Vita Inayotafuta Haki na Usawa Kuliko Amani Inayopumbaza na Kudhalilisha Utu wa Mwanadamu-G. Lema

    10. #29
      Bobuk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 2,181
      Rep Power : 949
      Likes Received
      889
      Likes Given
      1

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      Hawa waislamu walishangilia sana wakati JK anasaini hiyo sheria ya marekebisho ya katiba,
      wakifikiri wanaikomoa CDM. Matokeo ya kushangilia DHAMBI sasa itaanza kuwatafuna wao.

      Sheria aliyoisani JK hairuhusu, NGOs, vyama vya kiraia, vyama vya Siasa, vyama vya kidini,
      etc kuandaa makongamano ya katiba mpya. Ukifanya hivyo ni kosa la jinai na adhabu yake
      imeaanishwa kwenye sheria hiyo, fani 5 mil(?), kifungo mwaka mmoja(?) jela au vyote viwili kwa pamoja.

      Hayo ndiyo matokeo ya kushangilia DHAMBI. Ninajua serikali inaweza kuwafumbia macho
      hao waislamu kwasababu inafahamu from the word GO ajenda zao ni Mahakama ya kadhi,
      Tanzania kujiunga na OIC na Serikali inawapendelea wakiristu, Ubalozi wa Vatican Tanzania etc.
      Madai kama hayo kulingana na sheria aliyosaini JK anaweza kuyaweka kapuni bila hata kuyasoma
      na asiulizwe ni mtu because he is ALPHA & OMEGA.

    11. #30
      RICH OIL SHEIKH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd January 2012
      Location : NEWALA/QATAR/DAR ES SALAAM
      Posts : 808
      Rep Power : 538
      Likes Received
      123
      Likes Given
      42

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      Quote By dudus View Post
      • Kukutana Diamond Ijumaa
      • Mikoa Yote Nchini Kushiriki
      • Abas Syskes, Masheikh Kuunguruma

      Gazeti la LULU la leo Jumanne - 03 Januari 2012 linaripoti:

      Kongamano la Kitaifa la Uzinduzi wa Jukwaa la Katiba la Waislamu nchini linatarajiwa kufanyika Ijumaa ya wiki hii katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

      Habari za kuaminikia ..... zinafahamisha kuwa, kongamano hilo la siku moja linaloelezwa kuwa la kihistoria litafunguliwa na Abbas Syskes ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ...

      Pia wanasheria, masheikh mbalimbali wa jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake, pamoja na ujumbe kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani watashiriki.

      Akithibistihs habari hizo, ...., Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema hatua zote za maandalizi ya shughuli hiyo zimekamilika. ...

      Akizungumzia maudhui ya kongamano hilo, Sheikh Ponda alisema kuwa ni pamoja na kuzindua rasmi chombo kitakachojishughulisha na utoaji elimu ya katiba kwa jamii ya Waislamu nchini.

      "Chombo hicho ambacho tumekubaliana kitaitwa Jukwaa la Katiba la Waislamu, kitakuwa na jukumu la kuhakikisha Waislamu kote nchini wanakuwa na kauli moja juu ya masuala yanayohusu dini na maisha yao amabayo wangependa yawemo kwenye katiba mpya", alisema.

      Akifafanua namna Jukwaa hilo litakavyofanya kazi hiyo, Sheikh Ponda alisema kuwa, kabla ya kutazama yanayohitajika kuwemo kwenye katiba mpya, watatangulia kutoa elimu juu ya katiba ya sasa ...

      "Baada ya hapo ndipo Jukwaa litaketi na kutafakari kwa kina mahitajio ya waislamu tunayodhani ni muhimu yakaainishwa ndani ya katiba ya nchi", alizungumza Sheikh Ponda.

      ...

      Wakuu kwa muhtasari ni hayo - full stori, tafadhali pata nakala yako ya LULU.

      Bravo MUSLIMS

    12. #31
      Safety last's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th March 2011
      Posts : 2,733
      Rep Power : 963
      Likes Received
      541
      Likes Given
      6

      Default

      Quote By The Stig View Post
      Waislam wako wengi kuliko wakristu TZ, lakini wanavyolalama, utasea ni minority

      Hivi kama hiyo MOU ikifutwa, ndiyo itaondoa matatizo yote ya Waislamu nchini?
      hawako wengi mkuu jumla yao ni milion 13 na usheh kati ya watu 42 milioni

    13. #32
      sweke34's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th September 2010
      Posts : 2,493
      Rep Power : 1259
      Likes Received
      734
      Likes Given
      1240

      Default

      Quote By Bobuk View Post
      Hawa waislamu walishangilia sana wakati JK anasaini hiyo sheria ya marekebisho ya katiba,
      wakifikiri wanaikomoa CDM. Matokeo ya kushangilia DHAMBI sasa itaanza kuwatafuna wao.

      Sheria aliyoisani JK hairuhusu, NGOs, vyama vya kiraia, vyama vya Siasa, vyama vya kidini,
      etc kuandaa makongamano ya katiba mpya. Ukifanya hivyo ni kosa la jinai na adhabu yake
      imeaanishwa kwenye sheria hiyo, fani 5 mil(?), kifungo mwaka mmoja(?) jela au vyote viwili kwa pamoja.

      Hayo ndiyo matokeo ya kushangilia DHAMBI. Ninajua serikali inaweza kuwafumbia macho
      hao waislamu kwasababu inafahamu from the word GO ajenda zao ni Mahakama ya kadhi,
      Tanzania kujiunga na OIC na Serikali inawapendelea wakiristu, Ubalozi wa Vatican Tanzania etc.
      Madai kama hayo kulingana na sheria aliyosaini JK anaweza kuyaweka kapuni bila hata kuyasoma
      na asiulizwe ni mtu because he is ALPHA & OMEGA.
      Nadhani hata JK alishawahi kuwahimiza viongozi wa dini pamoja na waumini wao kutoa mchango wao kwenye katiba mpya ila wasiingize mambo ya dini maana yataleta mafarakano...sasa wenzetu sijui wanatumia viungo gani vya mwili kufikiria!?

    14. #33
      dudus's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 2,339
      Rep Power : 1018
      Likes Received
      1323
      Likes Given
      531

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      Quote By MAFILILI View Post
      Sheikh Ponda asituletee matatizo, kauli zake mara kwa mara ni kama BOKO HARAM
      Naam! Unajua maana ya Boko Haram? Kwa asiyejua maana yake ni neno la Kihausa (Hausa ni kabila fulani linalopatikana zaidi huko Kaskazini mwa Nigeria) lenye maana hii:

      Boko - Elimu ya Magharibi
      Haram - Haramu

      Hivyo Boko Haram = Elimu ya Magharibi Haramu.
      3D. likes this.

    15. #34
      kifuniboy's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 25th November 2010
      Posts : 183
      Rep Power : 470
      Likes Received
      12
      Likes Given
      170

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      Quote By Bobuk View Post
      Hawa waislamu walishangilia sana wakati JK anasaini hiyo sheria ya marekebisho ya katiba,
      wakifikiri wanaikomoa CDM. Matokeo ya kushangilia DHAMBI sasa itaanza kuwatafuna wao.

      Sheria aliyoisani JK hairuhusu, NGOs, vyama vya kiraia, vyama vya Siasa, vyama vya kidini,
      etc kuandaa makongamano ya katiba mpya. Ukifanya hivyo ni kosa la jinai na adhabu yake
      imeaanishwa kwenye sheria hiyo, fani 5 mil(?), kifungo mwaka mmoja(?) jela au vyote viwili kwa pamoja.

      Hayo ndiyo matokeo ya kushangilia DHAMBI. Ninajua serikali inaweza kuwafumbia macho
      hao waislamu kwasababu inafahamu from the word GO ajenda zao ni Mahakama ya kadhi,
      Tanzania kujiunga na OIC na Serikali inawapendelea wakiristu, Ubalozi wa Vatican Tanzania etc.
      Madai kama hayo kulingana na sheria aliyosaini JK anaweza kuyaweka kapuni bila hata kuyasoma
      na asiulizwe ni mtu because he is ALPHA & OMEGA.
      Kaka tafadhali usiseme mambo usiyoyajua waisilamu wangapi unajua tulishangilia hiyo kitu au

      ni kikundi gani kwa mfano unachokijua kilishangilia....ndugu acha udini utatumaliza.

    16. #35
      kifuniboy's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 25th November 2010
      Posts : 183
      Rep Power : 470
      Likes Received
      12
      Likes Given
      170

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      SHIZUKAN...tafadhali acha udini.

    17. #36
      NgomaNgumu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 20th November 2010
      Posts : 192
      Rep Power : 477
      Likes Received
      21
      Likes Given
      0

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      Quote By shizukan View Post
      Wataalam mbali mbali, very good. Naunga mkono 100%. Nachotia shaka ni msimamo wa Waislamu, je wanapenda maoni ya watu wengine, hususan wataalam? Hotuba ya Mh.Dokta pale Masjid Gadaffi, kwenye baraza la idi iligusia jambo moja la mahakama ya kadhi na hapo nilisikia Mh.Dokta akiongelea ushiriki wa Prof....(simkumbuki jina) ambaye ni mtaalamu wa sheria na sharia. Hilo waislamu hawakulipenda na ndio hasa msingi wa kufanywa kongamano hili ambalo dhahiri litaendeshwa kwa hisia na si hali halisi.

      Mimi nachoona hapa ni kama wanataka kuwa wa kwanza kuhukumiwa na sheria ambayo waliishangilia juzi juzi tu hapa iliposainiwa na Mh.Dokta. Unaposhangilia mvua milimani kumbuka maji huelekea bondeni, sasa tuliodhani itawabana CDM kufanya harakati sasa ndio tuone ugumu wa kuchekelea dhambi.

      Na mwisho nikukosoe kidogo (hapo kwenye red). Nature ya Uislamu ni kinyume kabisa na maoni yako. Utanibishia kisiasa au kwa kuchelea usionekane mbaya lkn ukweli hubakia kuwa ukweli. Soma Quran 9:5
      Ofcourse waislam wanakubali ushauri wa watu wengine kwani kawaida ya ushauri hua unakubalika au kukatalika. Usijaribu kubadilisha malengo ya kongamano kwa dhana yako binafsi kwani malengo ya kongamano yametajwa kwa ufasaha kabisa.

      Umejaribu kukosoa kua nature ya uislam sio amani na badala yake ukaleta Quran 9:5 Nimejaribu kuulizia kwa wataalam maana ya hizo verse nikafahamishw kua zilishushwa ktk mazingira maalum. Kwahiy kama unaona mazingira hayo yapo Tz basi ni wewe kuamua.

      Au unataka democrasia ya Cameron na capitalism ya europe. Wacha waislam wapange mambo yao kwani hilo halina maslahi kwa Tanzania tu bali kwa dunia.

    18. #37
      mikatabafeki's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2010
      Posts : 4,873
      Rep Power : 1408
      Likes Received
      778
      Likes Given
      1463

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      ​tutataka kuona they come up with positive thinking.
      when love goes wrong,nothing goes right.

    19. #38
      Songíto's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th October 2011
      Posts : 299
      Rep Power : 853
      Likes Received
      108
      Likes Given
      46

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      nawapongeza waislamu kwa hatua hii thabiti walioichukua, maana ni jukumu lao pia katika kuisaidia serikali kwenye suala zima la kupata katiba mpya.
      ila tu natoa angalizo, mkutano huu uwe kweli wa kujadili katiba na kutafuta suluhisho hasa kwa matatizo ya nchi na yale ambayo yanawasumbua waislamu kwa ujumla ambayo wangependa serikali iyashughulikie ikiwa tu hayaingilii uhuru wa dini nyingine, naomba mkutano huu usiwe wa kuwanyooshea vidole watu wengine wa imani tofauti, mana unaweka kukuta mada ni katiba lakini yatajkayozungumzwa ni ya ukristu, pengo au kakobe kupendelewa na serikali. ikiwa hivo hilo lengo lenu litakuwa halijatimia
      ila kama kweli itakuwa ni juu ya katiba ni vizuri.. pia kama ninyi mnafanya hivi, kesho au keshokutwa mkisikia wakristu wanafanya sawa nanyi basi yasitoke yale maneno au malalamiko ya kusema wanaiongoza serikali au wanaiamrisha serikali, wanaipangia serikali, kumbukeni nao wanayo haki kama ninyi.
      My take: kama waislamu wataendelea na utamaduni huu wa kuandaa utamaduni chanya wa kuyatazama mambo ya msingi kwa taifa kama wanavyokusudia basi kwa hakika watapiga hatua kubwa, mi nadhani ile dhana ya kuwanyooshea vidole wengine saizi ingewekwa pembeni nanyi ndugu zetu, sasa ni wakati wa kujitazama nyinyi kama nyinyi na serikali yetu.
      3D. likes this.

    20. #39
      RICH OIL SHEIKH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd January 2012
      Location : NEWALA/QATAR/DAR ES SALAAM
      Posts : 808
      Rep Power : 538
      Likes Received
      123
      Likes Given
      42

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      Quote By Elungata View Post
      Wale wakristo waliopanga kugomea katibai(nasemea wale wanaongozwa na padri slaa)hivi wamefikia wapi wajama?
      Wamekwama wao ni watu wa blah blah tu.
      Once more into the fray
      Into the last good fight I’ll ever know
      Live or die on this day
      Live or die on this day

    21. #40
      Chintu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2011
      Posts : 763
      Rep Power : 576
      Likes Received
      298
      Likes Given
      348

      Default Re: Waislamu Kuzindua Jukwaa la KATIBA

      Quote By Malaria Sugu View Post
      hapa lazima MOU iondoke ndani ya katiba
      Kumbe ipo kwenye katiba? mi nadhani kama kweli ipo isiondoke ila na waislamu nao waingie MOU kama wanavyo vya kuingia MOU

    Page 2 of 9 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...