Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni; aanza kwa kasi!

    Report Post
    Page 2 of 8 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 158
    1. #1
      Ustaadh's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th October 2009
      Posts : 408
      Rep Power : 576
      Likes Received
      7
      Likes Given
      1

      Default Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni; aanza kwa kasi!

      WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amewataka wananchi waliopora viwanja na maeneo ya wazi nchini na kujenga, wajisalimishe kwa mazungumzo, kwa sababu huenda wakaokoa hata matofali kabla hatua zaidi hazijachukuliwa.

      Profesa Tibaijuka alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati ya wizara hiyo na kueleza kuwa masuala ya ardhi yasipofanyiwa kazi, sekta nyingine zitazorota.


      “Umefika wakati sasa, tunataka kubadilisha mwonekano wa miji ... na kwa wanaosema wanatumia jeuri ya pesa, tutawashughulikia, lakini baada ya kufanya utafiti wa kutosha, kwa sababu hatuwezi kukurupuka, hivyo waliopora viwanja tunawataka wajisalimishe,” alisema Profesa Tibaijuka ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia Makazi (UN-Habitat).


      Alisema, migogoro ya ardhi hawataimaliza bila wananchi kuwasaidia na kwa sasa, watarudisha askari wa ardhi ili kuhakikisha wanapunguza migogoro ikiwamo ya wanaojenga holela na katika maeneo ya wazi.


      Tibaijuka alisema, kati ya hekta 900,000 ni asilimia mbili tu ya maeneo ndiyo yaliyopimwa, hivyo wizara yake itahakikisha inapimwa, ili miji iwe katika hali inayotakiwa kwa sababu kwa sasa hairidhishi.


      Aidha, Profesa Tibaijuka alisema si maendeleo yote yanahitaji fedha, hivyo kwa muda huu waliopewa na Rais, kuna mambo ambayo watayafanyia kazi kwa haraka ikiwamo kuandika majina ya mitaa yote.


      “Watu wengi hawatambui mitaa wanayoishi inaitwaje, kwa sababu wala haina majina na unakuta anashindwa kabisa kuelekeza, lakini tukiiandika tutawasaidia, hivyo tutafanya jambo hili kwa haraka maana haihitaji fedha,” alifafanua mbunge huyo wa Muleba Kusini.


      Katika hatua nyingine, alisema kuna upungufu wa nyumba milioni tatu nchini, hivyo wanapaswa kujenga miji kwa kuboresha nyumba zilizopo na kuzijenga ambazo hazina viwango na kuziuza kwa wananchi.


      “Wananchi wanatakiwa kutambua wanahitaji nyumba au ardhi, lakini watambue kama ni viwanja lazima waende nje ya mji, ila kama ni nyumba zipo ila zinahitaji maboresho na tutafanikiwa, kwa kuwa na benki za nyumba na mikopo ya nje, kwa sababu sekta binafsi pekee hazitaweza bila kuwa na fedha ... tuwaachie wahandisi wetu wajenge nyumba sisi tununue,” alisema.


      Alisema, watafanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na Ofisi ya Mazingira ili kuhakikisha miji inakuwa safi na salama; na kuboresha bonde la Mto Msimbazi, Dar es Salaam, ambalo limefanya hali ya hospitali ya Taifa Muhimbili kuwa mbaya.


      Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Patrick Rutabanzibwa, alikiri baadhi ya wafanyakazi wake kushiriki kugawa maeneo ya wazi na kueleza kuwa tayari ameanza kuwachukulia hatua za kisheria, ikiwamo kufanya mabadiliko ya vitengo kwa nia ya kuboresha utendaji kazi.


      “Uvamizi wa maeneo ni mtandao wa watu wa wizarani na manispaa nami nimejitolea kuwashughulikia na tayari kuna waliokuwa wamepora viwanja na nimewataka wavirudishe na wengine walipora na kuwauzia wafanyabiashara wakubwa,” alisema Rutabanzibwa.


      Pia alisema wamesimamisha ujenzi wa eneo la wazi katika hoteli ya Palm Beach na kuahidi kufanya kazi bila kuhofia kashfa, kwani zipo tuhuma amevumishiwa na amezipeleka kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).


      Kwa upande wao, mawaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mary Nagu (Uwekezaji na Uwezeshaji) na William Lukuvi (Sera, Uratibu na Bunge), waliripoti rasmi katika Ofisi ya Waziri Mkuu na kuzungumza na wakuu wa idara, vitengo na taasisi chini ya Ofisi hiyo.


      Mawaziri hao waliwataka watendaji kufanya kazi kwa ubunifu, ushirikiano, upendo, uwazi na bidii zaidi, ili kukidhi matarajio ya wananchi.


      Nagu alisisitiza umuhimu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji bila ngojangoja ambayo ni chanzo cha kuwakatisha tamaa wawekezaji.


      Alisema hakuna uchumi duniani uliofanya vizuri bila uwekezaji, iwe wa kutoka nje au ndani ya nchi husika. Alibainisha kuwa Watanzania ndio wanatakiwa kushika hatamu ya uchumi wao.


      Lukuvi alisisitiza watendaji kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa kasi zaidi ili kuongeza ufanisi na hatimaye kufikia malengo ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taifa kwa jumla.


      Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu aliwaambia watendaji wakuu wa wizara hiyo kuwa anawapa uhuru wa kufanya uamuzi wenye tija na ufanisi na atakayeshindwa atajiondoa mwenyewe.


      Alizungumza na wakurugenzi wakuu wa idara za uchukuzi na wa taasisi mbalimbali akijitambulisha kwao rasmi na kuanza kazi.


      Nundu aliwataka kufahamu dhima waliyonayo katika kuendeleza sekta ya uchukuzi ili katika kipindi cha miaka mitano ijayo, fursa zilizomo zitumike vyema pamoja na kuboresha huduma za usafiri.


      Aliwataka kupeana ushauri ili wasonge mbele, kuwa wadilifu na waaminifu huku wakitoa huduma kwa dhati na kwa wakati muafaka.


      “Hakikisheni mnawajibika kulingana na wakati, katika suala la uchukuzi hatupo peke yetu ulimwenguni, zingatieni matakwa ya wateja,” alisema Nundu na kuongeza:


      “Fanyeni kazi kila mmoja kwa madaraka aliyonayo, toeni uamuzi wenye tija bila upendeleo na hata ubinafsi na hiyo iwe ahadi yenu kwetu,” alisema.


      Alisema, anatarajia kuimarisha kampuni ya reli, kwa lengo la kuipa uwezo wa kutoa huduma bora kwa kusafirisha abiria na mizigo ya ndani na nchi jirani, na kuendelezwa kama mhimili wa mpango wa maendeleo wa eneo la ukanda wa kati.


    2. #21
      Byendangwero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Posts : 833
      Rep Power : 605
      Likes Received
      28
      Likes Given
      0

      Default Re: Profesor Tibaijuka atamweza Mahanga?

      Kinacholeta utata katika nchi hii ni kuwa na viongozi wanaoshikiria nyadhifa zinazowapa madaraka kadha wa kadha lakini wanashindwa kutumia madaraka hayo kwa kuingiliwa visivyo halali na wakubwa zao. Ninalolitegemea kwa Prof. nikwamba, hali hiyo ikitokea kwake, ni vema akaachie ngazi kuliko kujiruhusu kuwa ngazi ya kupandia.

    3. #22
      furahi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2010
      Posts : 450
      Rep Power : 532
      Likes Received
      34
      Likes Given
      163

      Default Re: Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni

      The sama old Song!

    4. #23
      QUALITY's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th September 2010
      Posts : 845
      Rep Power : 612
      Likes Received
      109
      Likes Given
      344

      Default Re: Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni

      Profesor Tibaijuka atamweza Mahanga?

      Katika serikali ya Tanzania kumekuwa na mtindo wa kulindana kati ya viongozi, ndiyo maana hata wakati ajenda za mafisadi na ubadhilifu mwingine wa mali za umma ulipofumuka, viongozi waliopaswa kuchukua hatua walifyata mkia.

      Sasa jana (kupitia ITV news ya saa mbili usiku) Professor Tibaijuka ambaye aliteuliwa kuwa waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi alisema “wale wote waliovamia maeneo ya wazi, wajisalimishe”. Mahanga ambaye ni naibu waziri katika serikali ya kikwete ni mmoja wa wananchi wanaoongoza katika kuvamia maeneo mengi ya wazi. Sasa kwa wakazi wa Tabata, wanafahamu pale Bima, kushoto ipo Nyantare Social Hall na Nyantare Bar. Zikiwa zimekamata eneo lililokuwa la wazi na lina ukubwa unaokadiriwa kuwa kama meta kati ya 400 na 600! Hilo lilikuwa eneo la wazi, kwa sasa ni kitega uchumi cha mheshimiwa!

      Pale Segerea, anajenga ghorofa katika eneo la wazi. Sasa Tibaijika ataweza kumkabili kiongozi mwenziwe na kumbomolea vitega uchumi vyake?

      Yetu macho, tunasubili kuona nani atamvika paka kengere!!

    5. #24
      Mzalendo80's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th October 2010
      Location : Magogoni, Tanganyika
      Posts : 2,280
      Rep Power : 964
      Likes Received
      821
      Likes Given
      1589

      Default Re: Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni

      Punda haendi bila ya kusukumwa pumbafu zao, wameona mwaka huu wameshindwa uchaguzi na wamechakachua sasa ndio wanajifanya kuwa wanafanyakazi ilituwaamini tena. Subirini 2015 mtakiona cha moto chenu hatuwataki ccm ondekeni kwenye nchi yetu mmeshanshindwa kazi wapisheni wanaume Mmeshafanya ufisadi sana na kuiba sasa ndio mnajifanya mnataka kufanyakzi toka 1964 mlikuwa wapi kujenga nchi.

    6. #25
      Amanikwenu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 1st December 2009
      Posts : 187
      Rep Power : 531
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni

      Naomba tumpe Muda tuone.


    7. #26
      Hatudanganyiki's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th August 2010
      Posts : 10
      Rep Power : 453
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Prof. Tibaijuka anapotaka wengine warudishe ardhi: Yeye vipi?

      Waziri mpya wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof Anna Tibaijuka jana aliibuka na kuwataka watu wote waliopora ardhi ya serikali na viwanja vya wazi na na kujenga katika maeno ya fukwe wajisalimishe haraka wizarani kwake kabla ya hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

      Kwa kuwa ni vizuri viongozi kama yeye wakaongoza kwa kuonyesha mifano ni vyema Prof Anna Tibaijuka akarejesha ardhi ya serikali zaidi ya ekari 100 aliyochukua katika ranchi ya utafiti wa magonjwa ya mifugo iliyoko wilaya ya Kinondoni.

      Prof Anna Tibaijuka alitumia ardhi hiyo kwa ajili ya kujenga shule ya sekondari ya wasichana iitwayo Barbro Johansen. Na mara tu alipochaguliwa kuwa Waziri wa Mifugo Mhe John Magufuli aliwahi kutoa wito na kuwataka wote waliomilikishwa ardhi za ranchi za taifa kurejesha ardhi husika kwa maslahi ya sekta ya mifugo.

      Kana kwamba hiyo haitoshi, Prof Anna Tibaijuka akaingilia na kuchukua line ya maji iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya vijiji vilivyoko jirani na shule yake. Mpaka sasa wakazi wa vijiji hivyo ambao idadi yao inakua kwa kasi sana hawana huduma ya maji ya safi ya bomba.

      Najua Prof Anna Tibaijuka anaweza kujitetea kuwa ardhi ilitolewa kwa ajili ya maslahi ya taifa. Lakini kama kweli ardhi hiyo ingekuwa ni kwa maskahi ya taifa na sio binafsi, ada zinazolipwa katika shule yake zingekuwa nafuu kuwawezesha watoto kutoka familia maskini waweze kumudu kuingia shuleni hapo. Raisi Jakaya Kiwete amewahi mara kadhaa kuzitaka shule binafsi kupunguza ada wananzotoza ili kuwawezesha watoto kutoka familia maskini kumudu kusoma katika shule hizo.

      Aidha kama mradi huo ungelikuwa ni kwa ajili ya maslahi ya taifa na sio binafsi, wakazi wa vijiji jirani na shule hiyo wangepatiwa huduma ya maji safi ya bomba kutoka shuleni hapo hasa ikizingatiwa kuwa shule hiyo ilichukua line ya maji ya vijiji na hivyo kuwakosesha wanakijiji huduma hiyo.

      Naomba kuwasilisha!!!!!!!!!!

    8. #27
      Kinyambiss's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2007
      Posts : 1,407
      Rep Power : 905
      Likes Received
      33
      Likes Given
      18

      Default Re: Prof Tibajuka: Rudisha ardhi ya Serikali ekari 100 uliyochuka na kujenga shule

      wapunguze ada nini? Private schools are expensive everywhere, serikali itoe elimi ya sekondari bure angalau umpaka f4. Kuliko ranch mbovu bora shule atakama ni private, anachangia sekta ya elimu. Na haujatoa maelezo kama hiyo ardhi ilichukuliwa kinyume na sheria au kwa kufwata taratibu za ubinafsishaji. Watu mnakuja tuu na hoja bila kuziweka ipaswavyo...

    9. #28
      Jatropha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th April 2009
      Posts : 1,061
      Rep Power : 745
      Likes Received
      48
      Likes Given
      6

      Default Re: Prof Tibajuka: Rudisha ardhi ya Serikali ekari 100 uliyochuka na kujenga shule

      Quote By Kinyambiss View Post
      wapunguze ada nini? Private schools are expensive everywhere, serikali itoe elimi ya sekondari bure angalau umpaka f4. Kuliko ranch mbovu bora shule atakama ni private, anachangia sekta ya elimu. Na haujatoa maelezo kama hiyo ardhi ilichukuliwa kinyume na sheria au kwa kufwata taratibu za ubinafsishaji. Watu mnakuja tuu na hoja bila kuziweka ipaswavyo...
      hakuna taratibu zozote zilizofuatwa wala kubinafsishwa. Ni afadhali waliojenga kwenye open space kwa kuwa ni halamsauri na wizara yake ndio iliwapatia offer na Tile deeds na building permits.

    10. #29
      Babuyao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th June 2009
      Posts : 1,720
      Rep Power : 855
      Likes Received
      177
      Likes Given
      148

      Default Re: Prof Tibajuka: Rudisha ardhi ya Serikali ekari 100 uliyochuka na kujenga shule

      Shule inakuwa kwa maslahi ya taifa pale tu wanafunzi wanapolipa ada ndogo? Wakilipa sana basi hakuna tena maslahi ya taifa? Uelewa wako wa maslahi ya taifa uko chini sana!
      Pili, hii thread yako ni kama ya kutaka kumkomoa au kumnyamazisha waziri Tibaijuka. Unataka asikemee uozo kwa vile naye - kwa mawazo yako - aliwahi kukosea. Kwa maneno mengine unataka akae kimya. Nadhani si sahihi mtazamo wako.
      God writes straight with crooked lines.

    11. #30
      Buchanan's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 19th May 2009
      Location : Somewhere!
      Posts : 9,398
      Rep Power : 9005
      Likes Received
      852
      Likes Given
      340

      Default

      Quote By Hatudanganyiki View Post
      Waziri mpya wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof Anna Tibaijuka jana aliibuka na kuwataka watu wote waliopora ardhi ya serikali na viwanja vya wazi na na kujenga katika maeno ya fukwe wajisalimishe haraka wizarani kwake kabla ya hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

      Kwa kuwa ni vizuri viongozi kama yeye wakaongoza kwa kuonyesha mifano ni vyema Prof Anna Tibaijuka akarejesha ardhi ya serikali zaidi ya ekari 100 aliyochukua katika ranchi ya utafiti wa magonjwa ya mifugo iliyoko wilaya ya Kinondoni.

      Prof Anna Tibaijuka alitumia ardhi hiyo kwa ajili ya kujenga shule ya sekondari ya wasichana iitwayo Barbro Johansen. Na mara tu alipochaguliwa kuwa Waziri wa Mifugo Mhe John Magufuli aliwahi kutoa wito na kuwataka wote waliomilikishwa ardhi za ranchi za taifa kurejesha ardhi husika kwa maslahi ya sekta ya mifugo.

      Kana kwamba hiyo haitoshi, Prof Anna Tibaijuka akaingilia na kuchukua line ya maji iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya vijiji vilivyoko jirani na shule yake. Mpaka sasa wakazi wa vijiji hivyo ambao idadi yao inakua kwa kasi sana hawana huduma ya maji ya safi ya bomba.

      Najua Prof Anna Tibaijuka anaweza kujitetea kuwa ardhi ilitolewa kwa ajili ya maslahi ya taifa. Lakini kama kweli ardhi hiyo ingekuwa ni kwa maskahi ya taifa na sio binafsi, ada zinazolipwa katika shule yake zingekuwa nafuu kuwawezesha watoto kutoka familia maskini waweze kumudu kuingia shuleni hapo. Raisi Jakaya Kiwete amewahi mara kadhaa kuzitaka shule binafsi kupunguza ada wananzotoza ili kuwawezesha watoto kutoka familia maskini kumudu kusoma katika shule hizo.

      Aidha kama mradi huo ungelikuwa ni kwa ajili ya maslahi ya taifa na sio binafsi, wakazi wa vijiji jirani na shule hiyo wangepatiwa huduma ya maji safi ya bomba kutoka shuleni hapo hasa ikizingatiwa kuwa shule hiyo ilichukua line ya maji ya vijiji na hivyo kuwakosesha wanakijiji huduma hiyo.

      Naomba kuwasilisha!!!!!!!!!!
      Nchi hii huwa mnaniacha hoi, tuhuma za mtu huwa zinaonekana wakati anapotaka kufanya jambo jema au kugombea nafasi ya uongozi! All in all mpaka hapo tutakapoondokana na ubinafsi ndipo Tanzania itakapoondokana na maovu, si kwa sasa watu wenye nia njema huzushiwa tuhuma ambazo hazipo: ie kupora mke, uraia, nk!

    12. #31
      Henge's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 5,440
      Rep Power : 1678
      Likes Received
      920
      Likes Given
      1673

      Default Re: Prof Tibajuka: Rudisha ardhi ya Serikali ekari 100 uliyochuka na kujenga shule

      Quote By buchanan View Post
      nchi hii huwa mnaniacha hoi, tuhuma za mtu huwa zinaonekana wakati anapotaka kufanya jambo jema au kugombea nafasi ya uongozi! All in all mpaka hapo tutakapoondokana na ubinafsi ndipo tanzania itakapoondokana na maovu, si kwa sasa watu wenye nia njema huzushiwa tuhuma ambazo hazipo: Ie kupora mke, uraia, nk!
      hawa mafisadi wanataka aache kufanya kazi yake vizuri! Mwacheni afanye kazi yake hayo mengine ulikuwa wapi kusema!? Huu ndo uzushi sasa. Kwahiyo ashindwe kufanya kazi kisa alijenga shule miaka ya nyuma!
      TUKIWAKAMATA MAFISADI NCHI ITAYUMBA by PINDA

    13. #32
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,510
      Rep Power : 41651
      Likes Received
      6280
      Likes Given
      1088

      Default Re: Prof Tibajuka: Rudisha ardhi ya Serikali ekari 100 uliyochuka na kujenga shule

      Mimi nilishasema huyu mama longolongo nyingi, na kitu muhimu zaidi ya huyu mama ni power structure ya serikali ya Kikwete.

      Sitegemei mabadiliko yoyote ya msingi mpaka power structure ibadilike.
      Allow others to say their say, but always say your piece, it's only right.


    14. #33
      Henge's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 5,440
      Rep Power : 1678
      Likes Received
      920
      Likes Given
      1673

      Default Re: Prof Tibajuka: Rudisha ardhi ya Serikali ekari 100 uliyochuka na kujenga shule

      Quote By kiranga View Post
      mimi nilishasema huyu mama longolongo nyingi, na kitu muhimu zaidi ya huyu mama ni power structure ya serikali ya kikwete.

      Sitegemei mabadiliko yoyote ya msingi mpaka power structure ibadilike.
      unayosema kilanga ni kweli but tunaposubili power structure ibadilike kwa katiba kubadilishwa huyu mama afanye kazi yake! Asiiingiliwe na mafisadi!
      TUKIWAKAMATA MAFISADI NCHI ITAYUMBA by PINDA

    15. #34
      Hatudanganyiki's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th August 2010
      Posts : 10
      Rep Power : 453
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Prof Tibajuka: Rudisha ardhi ya Serikali ekari 100 uliyochuka na kujenga shule

      Quote By babuyao View Post
      shule inakuwa kwa maslahi ya taifa pale tu wanafunzi wanapolipa ada ndogo? Wakilipa sana basi hakuna tena maslahi ya taifa? Uelewa wako wa maslahi ya taifa uko chini sana!
      Pili, hii thread yako ni kama ya kutaka kumkomoa au kumnyamazisha waziri tibaijuka. Unataka asikemee uozo kwa vile naye - kwa mawazo yako - aliwahi kukosea. Kwa maneno mengine unataka akae kimya. Nadhani si sahihi mtazamo wako.
      kutokana na ukubwa wa kiwango cha ada wazazi wanachotakiwa kulipwa katika shule hiyo, hoja kuwa ardhi hiyo inatumika kwa maslahi ya taifa haina mashiko kabisa. Badala yake inachingia kukua kwa matabaka kati ya walionacho na wasio nacho.

      Chimbuko la yeye kupata ardhi hiyo ni maombi ya vijiji jirani kuiomba serikali ardhi kutoka ranchi hiyo ili kujenga shule ya msingi na sekondari za serikali. Wakati huo mkuu wa wilaya ya kinondni akiwa ni rita mlaki badala ya kushugulikia maombi ya wananchi wa vijiji jirani akatumia maombi ya wananchi kumpatia ardhi hiyo. Zaidi ya miaka 10 watoto kutoka maombi ya wananchi kutolewa, watoto wa wao wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata shule ya msingi na sekondari-na wakati mwimngine kupata ajali za magari. Hapa maslahi ya taifa yako wapi.arudishe kwanza ardhi ya serikali ndipo awe na moral authority ya kusema hayo anayosema.

      Hoja kuwa nataka kumnyamazisha haina msingi. Ninachosema ni kuwa prof anna tibaijuka hana morala authority ya kufanya ahayo anayodai kutaka kuyafanya kwa kuwa naye ni sehemu ya ufisadi huo.

      Taarifa zilizopo ni kuwa shule hiyo ilitakiwa kuwalenga wasichana kutoka familia zenye vipato vya chini.

    16. #35
      Hatudanganyiki's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th August 2010
      Posts : 10
      Rep Power : 453
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Prof Tibajuka: Rudisha ardhi ya Serikali ekari 100 uliyochuka na kujenga shule

      Quote By henge View Post
      hawa mafisadi wanataka aache kufanya kazi yake vizuri! Mwacheni afanye kazi yake hayo mengine ulikuwa wapi kusema!? Huu ndo uzushi sasa. Kwahiyo ashindwe kufanya kazi kisa alijenga shule miaka ya nyuma!
      viwanja vya wazi, fukwe nk zote ni mali ya serikali na ranchi ya taifa pia n i mali ya serikali. Kama ni kurudisha kila mtu arudishe alicho nacho. Si wengine kuonewa na wengine kubaki na mali na ardhi za serikali.

    17. #36
      Mtu wa Mungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2010
      Posts : 426
      Rep Power : 522
      Likes Received
      14
      Likes Given
      1

      Default Re: Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni

      Ndiyo maana nchi hii itaendelea kubaki underdeveloped kwa miaka mingi ijayo!!!!! Huyu mama (prof) alikuwa mwalimu wa UDSM,kufuatiwa na Ukurugenzi UN (Habitat)-hajawaelewa wabongo!!!!!!!!Muulizeni je aliweza kubadilisha gheto za Harare alipokuwa UN?

      Mwambieni kwa gia hiyo hafiki mbali kwa wabongo!!!!!!!!! Hivi anawaelewa wenye viwanja halisi hivi ?? anavyojaribu kutuhadaa ili tuamini kwamba Manzese is going to turn into O'Bay??????!!! Hizi ni siasa nyepesi za akina ------!!! We ngoja afumue tu-atakapoanza kufikia kwa wenyewe akina EL, AC, RA, JK, Salama, Lidhwani, Miraji, Ben&Anna Co Ltd, Yusufu, nk nk nk,atanyamaza fyata!!!!!, na ndiyo atakuwa ameishia hapo mpaka 2015!!!!!!!!!! Labda mkongwe aliyevuma enzi hizo mhe. Lyatonga atamwonea huruma amnong'oneze yaliyompata na kesi ya dhahabu wakati akiwa Naibu WM enzi zake, alipokuwa akienda kwa top gia akiondoa viti maofisini asubuhi!

      WanaJF matatizo yetu ya msingi origin yake ni laana kutokana na viongozi waliotangulia (miaka ya 1967) wakifuatia wote wliotangulia na kuendelezwa na ------ kuendelea kukabidhi nchi kwa mashetani badala ya Mungu; maendeleo huletwa na Mungu, siyo mashetani-shetani kazi yake ni kuharibu; kuchukua rasilimali zote za nchi kama madini (dhahabu, uranium, bati tanzanait, na mengine utaongezea), samaki wa bahari yetu kuu, wanyama wa mbuga zetu, magogo ya miti ya misitu yetu-kuwatajirisha wairan akina RA na akina Ahmadinejad : Pale alipo ------, akina sheikh yahya na lile jopo la washirikina wa Bagamoyo wapatao 100 ndiyo walinzi wake!!!!-ndiyo maana ana ulinzi wa majini (mashetani) ya sheikh yahaya.!!!

      Nchi hii imelaaniwa
      !!!-tutasubiri bila kuona maendeleo tangu utoto wetu wa wa miaka ya 1967 mpaka siku Mungu atakapotambuliwa na kupewa heshima na utukufu wake!!!!!!!! Kabla ya hapo tutaendelea kuishi kwa kutegemea bakuli za ------ kila kukicha!!!!!!!!


    18. #37
      Mtu wa Mungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2010
      Posts : 426
      Rep Power : 522
      Likes Received
      14
      Likes Given
      1

      Default Re: Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni

      Tena kama itaweza kumfikia kwamba pale Art Gallery Mbezi Beach jirani na kanisa la Assembies of God jnmba mmoja tajiri amejenga katikait ya barabara; tena jirani na flats za NSSF njemba mwingine amejenga katikati na kuziba kabisa barabara yote!!!!!! Akituondolea hawa manjemba!!!!!!!!!!!! watu wa Mbezi Beach pamoja na wanaJF tutamtumia pongezi!!!!!!!!!!!!!!!!!

    19. #38
      Mtu wa Mungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2010
      Posts : 426
      Rep Power : 522
      Likes Received
      14
      Likes Given
      1

      Default Re: Profesor Tibaijuka atamweza Mahanga?

      Mtihani huo Anna!!!!!!!!! Watanzania wamekusoma!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! !!!!!!!

    20. #39
      Mtu wa Mungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2010
      Posts : 426
      Rep Power : 522
      Likes Received
      14
      Likes Given
      1

      Default Re: Tibaijuka awavaa mafisadi wa ardhi

      Tunamtakia kila la kheri!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! !!!

    21. #40
      Che Guevara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd May 2009
      Posts : 669
      Rep Power : 1051
      Likes Received
      70
      Likes Given
      21

      Default Re: Profesor Tibaijuka atamweza Mahanga?

      Ngoja tusubiri tuone kama Prof Tibaijuka 'will walk the walk'.
      Nakumbuka Magufuli aliwahi 'kumlipua' naibu waziri wake Rita Mlaki (akiwa ardhi).
      Prof afanye kweli vinginevyo ataanza kuumbuka mapemaaaaaa.......
      "You must be the change you want to see in the world" - Mahatma Gandhi (1869-1948)

    Page 2 of 8 FirstFirst 1234 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Prof Tibaijuka- Kauli yako
      By CHUAKACHARA in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 2
      Last Post: 16th August 2011, 10:27
    2. Prof. Tibaijuka ahamishia kibao kwenye 'beacons'
      By Rutashubanyuma in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 12
      Last Post: 19th January 2011, 02:58
    3. Was BAWATA Prof. Tibaijuka's brain-child?
      By Kashaijabutege in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 1
      Last Post: 3rd January 2011, 16:44
    4. Speed ya Prof. Tibaijuka yaanza kupata vikinza
      By Rutashubanyuma in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 37
      Last Post: 18th December 2010, 14:17
    5. Hongera Prof Tibaijuka kwa 2009 Göteborg Award
      By Ngareni3 in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 20
      Last Post: 19th July 2009, 10:10

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...