Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Bei ya umeme Z'bar yafikishwa kwa Lowassa

    Report Post
    Results 1 to 10 of 10
    1. BAK
      #1
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,597
      Rep Power : 44964
      Likes Received
      8345
      Likes Given
      8333

      Default Bei ya umeme Z'bar yafikishwa kwa Lowassa

      Bei ya umeme Z'bar yafikishwa kwa Lowassa

      na Mwandishi Wetu
      Tanzania Daima

      SAKATA la kupanda kwa bei ya umeme Zanzibar limezidi kupata sura mpya baada ya viongozi kuamua kulifikisha suala hilo kwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Waziri Kiongozi wa SMZ, Shamsi Vuai Nahodha.
      Katika maamuzi yaliyofanywa hivi karibuni, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Mafuta (EWURA), iliruhusu Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 21.7 kwa Tanzania Bara na asilimia 168 kwa Zanzibar, kwa maelezo kuwa kwa muda mrefu bei ya umeme Zanzibar ilikuwa ya chini mno.

      Suala hilo limefikishwa katika ngazi hizo za juu baada ya kukosekana kwa muafaka kutokana na majadiliano yaliyokuwa yakiendelea tangu kutangazwa kwa bei hizo mpya.

      Hayo yalielezwa na Ofisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Salum Hassan, alipozungumza na Tanzania Daima kuhusiana na kikao kilichowahusisha viongozi kutoka Zanzibar na Tanzania Bara, kujadili suala la ongezeko la bei ya umeme.

      "Baada ya kikao, uamuzi uliofikiwa ni kwamba suala hilo ajenda yake itapelekwa kwa viongozi wa juu, Waziri Mkuu Lowassa na Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha kutafutiwa ufumbuzi," alisema.

      Hassan alisema katika kikao hicho, menejimenti ya Tanesco ilibainisha kuwa katika mapendekezo yake, ilitaka bei ya Zanzibar ipandishwe kwa asilimia 39 tu, lakini jambo la kushangaza, EWURA imepandisha kwa asilimia 168.

      Alieleza kwamba katika kikao hicho, menejimenti ya EWURA ilijitetea kuwa haikufahamu mapendekezo ya Tanesco na ndiyo maana ikapandisha kwa kiwango hicho.

      Alisema kwa kuwa viwango hivyo vya bei vinapangwa na Bodi ya EWURA kupitia chombo maalumu cha udhibiti wa huduma za nishati na maji, menejimenti ya EWURA haina uwezo wa kutengua maamuzi yake.

      "Wenzetu wa EWURA wamesema hawana uwezo wa kutengua maamuzi yaliyofikiwa na bodi ndiyo maana tumeamua suala hili tulipeleke ngazi za juu za uongozi litafutiwe ufumbuzi," alisema Salum.

      Alieleza hadi sasa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), linaendelea kutumia bei ya zamani hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.

      Salum alisema iwapo bei mpya zilizopendekezwa na EWURA zitatumika, wananchi wa Zanzibar wataathirika kwa kiasi kikubwa kwa vile kima hicho hakilingani na kipato cha wananchi.

      Alisema hivi sasa Zanzibar inatumia megawatt 40 za umeme na kutumia kati ya sh milioni 800 hadi 900 kwa mwezi kwa ajili ya kununua umeme huo.

      Ofisa huyo alisema kulingana na viwango vipya vilivyotangazwa na EWURA Zanzibar, hivi sasa italazimika kutumia sh bilioni 2.1 kwa mwezi kununua umeme, kiwango ambacho ni kikubwa mno.

      "Tutaendelea kutumia viwango vya zamani hadi hapo vikao vya ngazi ya juu vya viongozi watakapolipatia ufumbuzi tatizo hilo," alisema.

      Aliwataka wateja wao kuondoa wasiwasi kwa vile serikali inaendelea kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo, ili kuepusha athari iwapo viwango vipya vitaanza kutumika.

      Wiki iliyopita ujumbe kutoka Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) na baadhi ya maofisa wa Wizara ya Maji, Nishati na Ardhi Zanzibar, ukiongozwa na Meneja wa ZECO, Juma Ishaq, walikwenda Dar es Salaam katika mchakato wa kulizungumzia suala hilo.
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    2. Miaka 50

    3. #2
      Kibunango's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2006
      Location : Tampere
      Posts : 6,804
      Rep Power : 44130
      Likes Received
      368
      Likes Given
      1428

      Thumbs up Re: Bei ya umeme Z'bar yafikishwa kwa Lowassa

      Quote By Bubu ataka kusema

      Aliwataka wateja wao kuondoa wasiwasi kwa vile serikali inaendelea kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo, ili kuepusha athari iwapo viwango vipya vitaanza kutumika.

      Bora... manake hawa EWURA wanafikili Zenj tunachimba mafuta....
      Last edited by Kibunango; 8th January 2008 at 13:59. Reason: word error
      Save Water Drink Beer. "Alcohol doesn't solve any problem,
      But, if you think again, neither does milk."
      Vituko Vya Zenj

    4. #3
      Rev. Kishoka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th March 2006
      Location : USA
      Posts : 4,352
      Rep Power : 2558
      Likes Received
      243
      Likes Given
      185

      Default Re: Bei ya umeme Z'bar yafikishwa kwa Lowassa

      Nafikiri ni wakati muafaka kwa Zanzibar kuwa na kampuni yao ya umeme ambayo inazalisha umeme na si kusambaza umeme tuu.

      Sijui ni kwa nini Serikali inatudanganya wananchi kuwa wataruhusu kampuni nyingine kuzalisha umeme, wakati EWURA na Tanesco ndio wanapandisha bei kinoma namna hiyo.

      Serikali inabidi ilipe deni inalodaiwa (including SMZ) na si kusukuma deni hili kwa wananchi kwa kuongeza viwango.
      Amani Iwe Nanyi,

      Camerlengo

      Plu Camerlenghi- Revolutionary Right Reverend Kishoka

      "Any existence deprived of freedom is a kind of death." Gen. Michel Aoun

      'Who comes to give greeting to the Inkosi-kaas? Who would taste her kiss, whereof the fruit is death? I, the Woodpecker, I, the Slaughterer, I the Swiftfooted! I, Umslopogaas!"

    5. #4
      Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2007
      Location : Mbagala, Jeshini
      Posts : 3,739
      Rep Power : 1174
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default Re: Bei ya umeme Z'bar yafikishwa kwa Lowassa

      Siasa kila mahali sasa viwango vya umeme na Lowasa wapi na wapi?
      Mkulima kala Mbegu......

    6. #5
      Kibunango's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2006
      Location : Tampere
      Posts : 6,804
      Rep Power : 44130
      Likes Received
      368
      Likes Given
      1428

      Arrow Re: Bei ya umeme Z'bar yafikishwa kwa Lowassa

      Quote By Masatu
      Siasa kila mahali sasa viwango vya umeme na Lowasa wapi na wapi?
      Siasa imeingia hapa.... Cheki nukuu hii
      Hassan alisema katika kikao hicho, menejimenti ya Tanesco ilibainisha kuwa katika mapendekezo yake, ilitaka bei ya Zanzibar ipandishwe kwa asilimia 39 tu, lakini jambo la kushangaza, EWURA imepandisha kwa asilimia 168.
      Zaidi kwa kuwa bodi ya EWURA haiwezi kupangua maamuzi yake, basi Lowassa akitoa maamuzi, hapana shaka wataridhika.

      Rev. Kishoka:
      Hapana shaka kuanzia kuanzishwa kwa TUKUZA huko visiwani, ZECO wamekuwa wakinunua umeme bila ya kukopa. Ili kuweza kupata malimmbikizo toka Idara mbalimbaili za SMZ, ZECO wamefunga TUKUZA hizo katika idara hivyo kuweza kulipwa malimbikizo ya madeni ingawa katika kiwango kidogo.

      Wazo la Zenj kujitegea kwa umeme kwa kuwa na kampuni yake ni zuri, katika awamu ya tano ya SMZ wazo hilo lilikuwepo ila pingamizi lilikuwa katika hiyo selikali ya muungano.

      Zaidi EWURA wanapaswa kujua Zenj ni mteja no1 wa Tanesco. Hivyo wawe makini na hesabu zao ambazo zimehusu zaidi ubinafsi.
      Save Water Drink Beer. "Alcohol doesn't solve any problem,
      But, if you think again, neither does milk."
      Vituko Vya Zenj

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      Shakazulu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd February 2007
      Posts : 909
      Rep Power : 807
      Likes Received
      197
      Likes Given
      529

      Default Re: Bei ya umeme Z'bar yafikishwa kwa Lowassa

      Quote By Masatu
      Siasa kila mahali sasa viwango vya umeme na Lowasa wapi na wapi?
      Inatia wasiwasi kama huoni uhusiano kati ya bei ya umeme na siasa. Hebu angalia wenzako wanavyoona uhusiano uliopo.

      UK

      Darling plans meeting on fuel price


      Chancellor Alistair Darling has called for a meeting with energy regulators Ofgem to review the reasons for recent dramatic rises in fuel prices.

      In a sign of concern about the impact on the economy of double-digit hikes in bills, Mr Darling indicated he was conscious of the link between energy prices and macro-economic stability.

      Energy suppliers Npower last week sparked anger among customers when they announced hikes of 17.2% for gas and 12.7% for electricity, increasing typical bills by £95 for gas and £64 for electricity and taking the average dual power bill over £1,000 a year.

      The announcement, coming against the backdrop of oil trading at more than 100 US dollars a barrel, raised concerns that other power companies may follow suit, with a knock-on effect on the British economy.

      In a letter to Ofgem chairman Sir John Mogg and chief executive Alistair Buchanan, obtained by The Times, Mr Darling asked for a meeting soon to discuss the implications of the price rises.

      And he appeared to suggest he wants to explore claims from some experts that the energy companies do not need to pass on commodity price increases to consumers at once.

      Mr Darling wrote: "I would be interested in receiving your assessment of gas and electricity supply and market conditions both in the UK and Europe and likely future trends..."

      He added: "Increases in... energy prices has reminded us of the relationship between energy prices, macro-economic stability and government's objectives around tackling fuel poverty."

      Karl Brookes, spokesman for consumer watchdog Energywatch, said: "Energywatch is not convinced the market is working in the best interests of consumers and we are pleased this review is taking place."

      "If you believe we are in a fully-fledged competitive market you would expect suppliers to respond in a more innovative way than instantly responding to wholesale prices by hitting the consumer in the pocket."

    9. #7
      MzalendoHalisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2007
      Posts : 3,942
      Rep Power : 1397
      Likes Received
      72
      Likes Given
      120

      Default Re: Bei ya umeme Z'bar yafikishwa kwa Lowassa

      Wazenji walipie tu umeme kama watu wa bara- actually pamoja na kupanda kwa bei Visiwani bado viwango vya malipo ni kidogo tofauti na bara!

      Hii kukimbilia kwa Lowasa au Nahodha ya nini? Kama kuna kusaidiwa basi iwe kwa watumiaji wote wa visiwani na bara. Au SMZ walipie tu hiyo tofauti ili Watz wa Visiwani waendelee kulipia kidogo!
      Uadilifu Kiwe Kigezo Muhimu Zaidi Kuwa Kiongozi Tanzania Kwa Sasa!

    10. #8
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,826
      Rep Power : 2968
      Likes Received
      2433
      Likes Given
      3510

      Default Re: Bei ya umeme Z'bar yafikishwa kwa Lowassa

      ..kuna thread ilikuwa inasema Zenj wanalipa kidogo kuliko Bara. hebu tuipitie hiyo.

      ..je, inawezekana pamoja na ongezeko la 168% bado wateja wa Zenj wanapata umeme kwa bei nafuu kuliko Wabara?

    11. #9
      Mtu wa Pwani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2006
      Posts : 4,250
      Rep Power : 1491
      Likes Received
      159
      Likes Given
      147

      Default Re: Bei ya umeme Z'bar yafikishwa kwa Lowassa

      mie nnaona vizuri watupandishie zaidi.

      ili tuamke tujue nguo ya kuazima hasitiri ------.

      sasa wakienda huko kwenye mazungumzo watajua vya kuzungumza baada ya kuoneana haya.

      wapasuliane kijulikane linaenda au ndio mwisho wa safari.

      mtu kubashiwa na dume mwenziwe aibu
      Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown

    12. #10
      Fundi Mchundo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2007
      Posts : 4,351
      Rep Power : 2678
      Likes Received
      194
      Likes Given
      136

      Default Re: Bei ya umeme Z'bar yafikishwa kwa Lowassa

      Ninavyoelewa mimi hii ni bei ya Tanesco kwa Zeco na haihusiani kabisa na bei ambayo ZECO ataamua kumuuzia mteja wake. Zeco ina uhuru kabisa wa kuendelea kumuuzia mteja wake bei aliyoizoea na kutafuta sehemu nyingine tofauti kati ya bei hiyo na ile ambayo EWURA amependekeza. Vilevile ZECO ana uhuru wa kumuuzia mteja wake umeme kwa bei ZAIDI ya ile EWURA aliyopendekeza. Uamuzi ni wao.

    Similar Topics

    1. Nguzo ya umeme ni mali ya Tanesco au Mteja anayeunganishiwa umeme?
      By PrN-kazi in forum Business & Economic Forum
      Replies: 16
      Last Post: 26th June 2012, 17:42
    2. Replies: 3
      Last Post: 28th July 2011, 18:31
    3. Replies: 23
      Last Post: 29th June 2011, 09:47
    4. Edward Lowassa Nimewakosea nini Watanzania? (Huyu SI LOWASSA)
      By Fake Lowassa in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 63
      Last Post: 5th June 2011, 12:52
    5. Replies: 4
      Last Post: 16th February 2011, 16:29

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...