Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Tume mpya ya uchaguzi yaundwa Zanzibar

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 32
    1. #1
      Mtu wa Pwani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2006
      Posts : 4,250
      Rep Power : 1490
      Likes Received
      159
      Likes Given
      147

      Default Tume mpya ya uchaguzi yaundwa Zanzibar

      Karume ateua Tume ya Uchaguzi Zanzibar

      *Ni ya wajumbe mchanganyiko wa itikadi

      Na Ali Suleiman, Zanzibar

      RAIS Amani Abeid Karume, ametangaza Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) mpya na kumteua Bw. Khatib Mwinchande Khatib, kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.

      Kwa mujibu wa taarifa za Ikulu iliyotolewa jana, wajumbe wa Tume hiyo wakiwamo wawili kutoka CUF ambao ni Bw. Ayoub Bakari Hamad na Wakili wa Kujitegemea, Bw. Nassor Khamis Mohamed.

      Wengine ni Bw. Said Bakari Jecha, ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Jaji Omar Othman Makungu, Bw. Abrahman Rashid Mohamed na Bibi Mwanabakari Maalim Ahmed, ambaye ni mjumbe pekee mwanamke katika Tume hiyo.

      Uteuzi huo umekuja baada ya Tume ya awali iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake, Bw. Masauni Yussuf Masauni kumaliza muda wake.

      Katika Tume iliyopita, ni mjumbe mmoja pekee aliyerudi ambaye ni Mwenyekiti, Bw. Mwinchande.

      Tume hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwamo kufanya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

      Pia tume hiyo wakati ikiwasilisha taarifa yake kwa Rais ilisema yapo marekebisho yanayohitaji kufanyiwa kazi kwa lengo la kuboresha uchaguzi mkuu kuwa huru na wa haki zaidi.

      naam jee tume hii itakuwa ni jibu la wazanzibari? jee tume hii itaweza kutuvusha tusirejeee tulipotoka au kufikia walipofika ndugu zetu wakenya?
      Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown

    2. Miaka 50

    3. #2
      Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2007
      Location : Mbagala, Jeshini
      Posts : 3,739
      Rep Power : 1173
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      Changa la macho hilo... hakuna jipya another Kiviutu in making....
      Mkulima kala Mbegu......

    4. #3
      Idimi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2007
      Location : Ikwiriri
      Posts : 4,649
      Rep Power : 13619
      Likes Received
      835
      Likes Given
      318

      Default Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      Tume huru sio hoja sana kwa siasa za Zenji.
      Swali linakuja kwamba: Je sirikali ya muungano itaendelea kutuma askari kwa wingi na mamluki wengine kwenda visiwani kupiga kura? Iwapo suala hili litajibiwa basi tutakuwa na maoni tofauti kuhusu hiyo tume.
      Vinginevyo naungana na Masatu kwamba hili suala ni kiini mazingaombwe.
      Tutarudi kule kule kwa Kivuitu
      A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man!
      [email protected]

    5. #4
      Kibunango's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2006
      Location : Tampere
      Posts : 6,802
      Rep Power : 44129
      Likes Received
      368
      Likes Given
      1427

      Default Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      kazi ipo kwenye daftali la kudumu...
      Save Water Drink Beer. "Alcohol doesn't solve any problem,
      But, if you think again, neither does milk."
      Vituko Vya Zenj

    6. #5
      Kibunango's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2006
      Location : Tampere
      Posts : 6,802
      Rep Power : 44129
      Likes Received
      368
      Likes Given
      1427

      Arrow Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      Quote By Masatu
      Changa la macho hilo... hakuna jipya another Kiviutu in making....
      Hapa jipya lipo, waliochaguliwa wanachukua nafasi ya tume iliyomaliza muda wake. Aidha wajumbe wote ni watu waadilifu ndio maana wamechaguliwa. Kwa upande mwingine Mh.Karume anamaliza muda wake hivyo sidhani ka atakuwa anamteua mtu ili kuja kupata fadhila zake. Aidha siasa za Zenj ni tofauti sana na siasa za Kenya.

      Malalamiko makubwa katika Tume iliyomaliza muda wake ni usahihi wa Daftali la kudumu la wapiga kura. Maadamu mwenyekiti amerudi tena, hapana shaka ataweza kuondoa kasoro zilizotokea katika daftali hilo muhimu.
      Save Water Drink Beer. "Alcohol doesn't solve any problem,
      But, if you think again, neither does milk."
      Vituko Vya Zenj

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      Idimi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2007
      Location : Ikwiriri
      Posts : 4,649
      Rep Power : 13619
      Likes Received
      835
      Likes Given
      318

      Default Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      Quote By kibunango

      Sawa mtu wa Zenji, na tusubirie muda ufike tuone mapya ya tume hii. Long live Zanzibar, log live Tanzania.
      A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man!
      [email protected]

    9. #7
      Mtanzania's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2006
      Location : UK
      Posts : 5,273
      Rep Power : 5565
      Likes Received
      287
      Likes Given
      77

      Default Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      Quote By kibunango
      Hapa jipya lipo, waliochaguliwa wanachukua nafasi ya tume iliyomaliza muda wake. Aidha wajumbe wote ni watu waadilifu ndio maana wamechaguliwa. Kwa upande mwingine Mh.Karume anamaliza muda wake hivyo sidhani ka atakuwa anamteua mtu ili kuja kupata fadhila zake. Aidha siasa za Zenj ni tofauti sana na siasa za Kenya.

      Malalamiko makubwa katika Tume iliyomaliza muda wake ni usahihi wa Daftali la kudumu la wapiga kura. Maadamu mwenyekiti amerudi tena, hapana shaka ataweza kuondoa kasoro zilizotokea katika daftali hilo muhimu.
      Mawazo kama yako ndio yatafanya nchi yetu iingie kwenye janga kama Kenya.

      Tatizo kwa Zenji ni kuanzia tume ya uchaguzi, daftari la wapiga kura, uhuru wa ku kampeni bila bugudha nk.

      Karume angesubiri kidogo na kushirikisha wadau wengine kuteua tume huru. Hii ya sasa ni mazingaombwe yale yale ya Afrika.
      Kuna sehemu Masanja ameandika, adui wa maendeleo ya Waafrika ni Waafrika wenyewe.

      Miaka na miaka tunashindwa kutatua jambo kama hili ambalo liko wazi.

      Kama mtu hana mawazo mabaya kwanini aogope tume ambayo iko huru kwenye macho ya kila mtu?

    10. #8
      Kibunango's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2006
      Location : Tampere
      Posts : 6,802
      Rep Power : 44129
      Likes Received
      368
      Likes Given
      1427

      Default Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      Jukumu la kuteua Tume lipo chini ya rais,hivyo ni wajibu wake kuteua tume kwa wakati wake. Hilo la kusubiri sijui una maana gani? Tena awashirikishe wadau wengine...! wadau gani hawo? Jaribu kufafanua hapo.

      Zenj inakwenda kwenye mwaka wa 15 tokea chaguzi ya kwanza ya vyama vingi. Katika muda wote huo imekuwa ikijifunza mengi na imeweza kufahamu mengi katika chaguzi hizo. Wanamageuzi wa kweli wanaweza kudhibitisha hilo.

      Uhuru wa Tume, Uhuru wa Kampeni na uhuru wa kupiga kura ni mpana sana sasa kulinganisha na mwaka 1995. Sasa kama unaona kuna mapungufu, ni vema ukayataja ili yaweze kujadiliwa na sio kurukia kwenye kuhukumu tu.

      Tatizo la wengi ni kutojua jinsi ya kujadili hoja, badala yake hukimbilia kwenye kuhukumu tu.
      Save Water Drink Beer. "Alcohol doesn't solve any problem,
      But, if you think again, neither does milk."
      Vituko Vya Zenj

    11. #9
      Mtanzania's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2006
      Location : UK
      Posts : 5,273
      Rep Power : 5565
      Likes Received
      287
      Likes Given
      77

      Default Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      Quote By kibunango
      Jukumu la kuteua Tume lipo chini ya rais,hivyo ni wajibu wake kuteua tume kwa wakati wake. Hilo la kusubiri sijui una maana gani? Tena awashirikishe wadau wengine...! wadau gani hawo? Jaribu kufafanua hapo.

      Zenj inakwenda kwenye mwaka wa 15 tokea chaguzi ya kwanza ya vyama vingi. Katika muda wote huo imekuwa ikijifunza mengi na imeweza kufahamu mengi katika chaguzi hizo. Wanamageuzi wa kweli wanaweza kudhibitisha hilo.

      Uhuru wa Tume, Uhuru wa Kampeni na uhuru wa kupiga kura ni mpana sana sasa kulinganisha na mwaka 1995. Sasa kama unaona kuna mapungufu, ni vema ukayataja ili yaweze kujadiliwa na sio kurukia kwenye kuhukumu tu.

      Tatizo la wengi ni kutojua jinsi ya kujadili hoja, badala yake hukimbilia kwenye kuhukumu tu.
      Naona unaongea ----- tupu, hakuna ambacho Zenji mmejifunza kuhusu matatizo ya uchaguzi.

      Mna bahati kwamba mna wajomba zenu bara, mkiiba kura wanakuja kuwasaidieni ili msichinjane kama Kenya.

      mmeiletea aibu Tanzania kwa kutoa wakimbizi shauri ya ujinga wenu, leo unataka kuongea nini hapa?

      Maisha ya binadamu yana thamani na lazima kila juhudi ichukuliwe ili kuhakikisha hata mnyonge anaishi. Lakini sidhani mmejifunza, mwaka 2010 mtaua wengine kama mlivyofanya 1995, 2000 na 2005.

      Palipo na nia kila kitu kinawezekana. Katiba inatungwa na watu na kama
      Wazanzibri mnataka kutatua matatizo yenu mnaweza kabisa kwa kuitumia katiba hiyo hiyo kukaa pamoja na kuyatatua.

      Lakini kila nikiangalia sioni kabisa kwamba mnataka kujifunza, badala yake ni ujinga ule ule tu. Nchi toka 1964 mpaka leo ni umaskini tu wa kunuka bado mnajiona mna haki ya kuongoza hata kwa nguvu.

      Acheni ujinga wenu na ngojera zenu hapa, wadanganyeni hao Wadanganyika lakini tunaelewa hakuna la maana mnalofanya hapa zaidi ya kutetea matumbo yenu na ndio maana mnaleta ----- huu.

      Inabidi Watanzania kuanza kuchukia kwani sitaki hata Mtanzania mmoja afe kwasababu ya watu ambao ki ukweli hawastahili hata kuongiza kata. Wamepewa nafasi za kuongoza na wamezitumia vibaya.

      Acheni Wazanzibari wajiamulie kwa njia ya haki wanataka kuongozwa na nani.

      Baada ya kuona yaliyotokea Kenya, sasa nimechukia kweli kweli.

    12. #10
      Mwanamalundi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2007
      Posts : 1,633
      Rep Power : 0
      Likes Received
      471
      Likes Given
      171

      Default Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      Quote By Mtu wa Pwani
      RAIS Amani Abeid Karume, ametangaza Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) mpya na kumteua Bw. Khatib Mwinchande Khatib, kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
      Ha ha ha ha ha ha ha ha!!!!! Mwinyichande mwenyekiti ya tume??? msinivunje mbavu mie!!! Huyu bwana na CCM ni kama samaki na bahari, yaani haelewi somo. Nadhani sasa chama cha kafu inabidi kiingize katika ilani yao ya uchaguzi suala la muafaka kama moja ya sera yao. Kwamba wanaingia katika uchaguzi ili kuendeleza vikao vya muafaka baada ya uchaguzi. Hapa ni mwendo mdundo, muafaka mtindo mmoja mpaka kunako 2050!!!!

    13. #11
      Mnhenwa Ndege's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 5th December 2007
      Posts : 247
      Rep Power : 634
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      inatakiwa kazi ianze sasa kwa wapinzani kubaini kuwa hii tume ni huru kweli.

    14. #12
      Idimi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2007
      Location : Ikwiriri
      Posts : 4,649
      Rep Power : 13619
      Likes Received
      835
      Likes Given
      318

      Default Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      Kibunango,
      Wasiwasi wa wengi wetu hapa ni kwamba tunataka tume ambayo itasema "HAPANA" kwa askari kupigishwa kura Zanzibar kwa namna yoyote ile. Tunataka tume ambayo itatuhakikishia kwamba daftari la kudumu la wapiga kura "HALIBAKWI" na kuwabagua baadhi ya watu, ambapo ikifika siku ya kupiga kura majina yao hayaonekani, kisa tu wanatoka chama fulani ama eneo fulani.
      Sasa ukizingatia haya, je tume hii ina 'reputation' hiyo tajwa? Je aliyefanya haya chini ya tume staafu si ni huyu huyu mwenyekiti aliyebakizwa? Hatarudia yale yale?
      Tunahofia isije watu wakakimbia na maboksi ya kura vichakani halafu hawachukuliwi hatua!
      Wasiwasi wa wengi wetu uko hapo!
      A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man!
      [email protected]

    15. #13
      Mwanamalundi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2007
      Posts : 1,633
      Rep Power : 0
      Likes Received
      471
      Likes Given
      171

      Default Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      Quote By IDIMI
      Kibunango,
      Wasiwasi wa wengi wetu hapa ni kwamba tunataka tume ambayo itasema "HAPANA" kwa askari kupigishwa kura Zanzibar kwa namna yoyote ile. Tunataka tume ambayo itatuhakikishia kwamba daftari la kudumu la wapiga kura "HALIBAKWI" na kuwabagua baadhi ya watu, ambapo ikifika siku ya kupiga kura majina yao hayaonekani, kisa tu wanatoka chama fulani ama eneo fulani.
      Sasa ukizingatia haya, je tume hii ina 'reputation' hiyo tajwa? Je aliyefanya haya chini ya tume staafu si ni huyu huyu mwenyekiti aliyebakizwa? Hatarudia yale yale?Tunahofia isije watu wakakimbia na maboksi ya kura vichakani halafu hawachukuliwi hatua!
      Wasiwasi wa wengi wetu uko hapo!
      Idimi you are raising an interesting fact here. This chairperson is part of CCM blood veins. This should send a strong warning to CUF. Watch out CUF, watch out CUF!!!!!

    16. #14
      Mtu wa Pwani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2006
      Posts : 4,250
      Rep Power : 1490
      Likes Received
      159
      Likes Given
      147

      Default Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      nnapenda niweke masahihisho kuwa mwenyekiti aliepita alikuwa ni mzee masauni na huyu wa sasa ni mwinyi chande huyu alikuwa ni kamishna kipindi kile.

      na sijasikia CUF kusema lolote hadi sasa huenda hawana mashaka na uteuzi huo.
      Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown

    17. #15
      Joel Ndaki's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 4th January 2008
      Posts : 2
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Tume mpya ya uchaguzi yaundwa Zanzibar

      Hii ni tume nyingine ya kisanii, subirini mtayaona.Mwenyekiti wa tume mwalimu wa darasani,halafu ni kada wa CCM!Wajumbe wenyewe ni mbili kwa tatu!

    18. #16
      Idimi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2007
      Location : Ikwiriri
      Posts : 4,649
      Rep Power : 13619
      Likes Received
      835
      Likes Given
      318

      Default Re: Tume mpya ya uchaguzi yaundwa Zanzibar

      Quote By Joel Ndaki
      Hii ni tume nyingine ya kisanii, subirini mtayaona.Mwenyekiti wa tume mwalimu wa darasani,halafu ni kada wa CCM!Wajumbe wenyewe ni mbili kwa tatu!
      Na zogo lenyewe ltaanzia hapa haswaa! Kwa sababu iwapo wajumbe wa CUF watashindwa kukubaliana na wenzao wa sisiemu, si wataamua kupiga kura ili yaishe? Na ndio hapa wale watatu watakapowazidi wale wawili wa "si yu efu".
      A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man!
      [email protected]

    19. #17
      Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2007
      Location : Mbagala, Jeshini
      Posts : 3,739
      Rep Power : 1173
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default Re: Tume mpya ya uchaguzi yaundwa Zanzibar

      Kwanini wajumbe ni kutoka CCM na CUF tu? Huko ZnZ hakuna Chadema?
      Mkulima kala Mbegu......

    20. #18
      Mtu wa Pwani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2006
      Posts : 4,250
      Rep Power : 1490
      Likes Received
      159
      Likes Given
      147

      Default Re: Tume mpya ya uchaguzi yaundwa Zanzibar

      Quote By Masatu
      Kwanini wajumbe ni kutoka CCM na CUF tu? Huko ZnZ hakuna Chadema?

      chadema hawana mvuto zenji

      na kwa sera zao na mambo yao wakatafute mdako wacheze
      Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown

    21. #19
      Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2007
      Location : Mbagala, Jeshini
      Posts : 3,739
      Rep Power : 1173
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default Re: Tume mpya ya uchaguzi yaundwa Zanzibar

      Quote By Mtu wa Pwani
      chadema hawana mvuto zenji

      na kwa sera zao na mambo yao wakatafute mdako wacheze
      Makubwa haya....
      Mkulima kala Mbegu......

    22. #20
      Kibunango's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2006
      Location : Tampere
      Posts : 6,802
      Rep Power : 44129
      Likes Received
      368
      Likes Given
      1427

      Arrow Re: TUME mpya ya uchaguzi yaundwa ZANZIBAR

      Quote By Mtanzania
      Naona unaongea ----- tupu, hakuna ambacho Zenji mmejifunza kuhusu matatizo ya uchaguzi.

      Mna bahati kwamba mna wajomba zenu bara, mkiiba kura wanakuja kuwasaidieni ili msichinjane kama Kenya.
      Kaka mbona unalia? Jibu maswala niliyokuuliza na sio kulia lia hapa.

      Kwa taarifa yako Mapendekezo yaliyotolewa na Tume iliyomaliza muda wake ambayo kwa undani ni kutokana na malalamiko n kasoro zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita ni kama yafuatayo....
      • Mapendekezo haya ni chini ya Tume ya Rais ya pamoja ya utekelezaji Muafaka wa CCM na CUF.

      • Aidha timu ya wataalamu walioshiriki katika kutoa ushauri inaundwa na Bw. Ron Gould kutoka Canada na Profesa Chris Peter kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wataalumu wengine toka ndani na nje ya Tanzania

      Nafasi ya naibu mkurugenzi wa uchaguzi na wasaidizi wakurugenzi wa uchaguzi imeondolewa na sasa imependekezwa kuwa na muundo wa divisheni sita.

      Divisheni ya kwanza ni ofisi ndogo ya uchaguzi Pemba itakayosimamia shughuli za kiutawala, fedha na shughuli nyengine zote za uchaguzi, ikiwemo kumshauri Mkurugenzi wa Tume hiyo.

      Divisheni ya pili ni ya uchaguzi ambayo itakuwa ikimshauri Mkurugenzi kuandaa utekelezaji wa taratibu za uandikishaji wapiga kura, uteuzi wa wagombea, kampeni za uchaguzi, upigaji kura, kuhesabu na kutangazwa kwa matokeo.

      Divisheni ya tatu ni ya utawala na uendeshaji itakayosimamia shughuli za mafunzo kwa wafanyakazi, uajiri na haki za wafanyakazi kwa kuzingatia kanuni za utumishi.

      Divisheni ya nne ni ya habari na uhusiano itakayokuwa na majukumu ya kujenga uhusiano kati ya vyombo vya habari na Tume na utoaji wa elimu kwa wananchi.

      Divisheni ya tano ni ya fedha, ukaguzi na bajeti itakayokuwa na majukumu ya kuandaa bajeti ya fedha na malipo yanayofanyika kuhakikisha yanakidhi mahitaji yote ya upatikanaji na utumiaji wa fedha.

      Divisheni ya sita ni ya sheria itakayofanyakazi ya kumshauri Mkurugenzi wa Uchaguzi masuala yote ya sheria za uchaguzi na kuwa Mwakilishi wa Tume ya Uchaguzi mahakamani wakati inapohitajika kutoa au kujibu hoja kuhusu masuala yote ya uchaguzi yanayotokana na Katiba ya Zanzibar, Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zinazotungwa.

      Mapendekezo mengine...

      Kuwepo na ofisi katika kila wilaya ili kuendeleza zoezi la uandikishaji wapiga kura watakaokuwa wamefikisha umri unaotakiwa kisheria.

      Kuangalia watu waliohama katika maeneo na kuingia katika maeneo mengine, ili kuhakikisha wanashiriki katika uchaguzi bila matatizo yoyote.

      Sasa kama bado una dukuduku soma hapo juu vizuri, kama hukufahamu uliza swali na sio kulia lia hapa.
      Last edited by Kibunango; 4th January 2008 at 21:42. Reason: errors
      Save Water Drink Beer. "Alcohol doesn't solve any problem,
      But, if you think again, neither does milk."
      Vituko Vya Zenj

    23. Study Abroad
    Page 1 of 2 12 LastLast

    Similar Topics

    1. Lubuva Mwenyekiti mpya Tume ya Uchaguzi!
      By Halisi in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 150
      Last Post: 18th January 2012, 18:34
    2. Tume yaundwa kuchunguza bodi ya Pius msekwa, shame on you gov
      By BASIASI in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 3
      Last Post: 19th August 2011, 10:17
    3. Replies: 28
      Last Post: 17th December 2010, 13:10
    4. Replies: 2
      Last Post: 9th November 2010, 14:48
    5. Replies: 1
      Last Post: 4th November 2010, 09:05

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...