04/11/2010
Kamanda wa kanda maalumu ya kipolisi ya mkoa wa Dar Es Salaam, Suleiman Kova amesema jeshi la polisi limepokea habari za siri kuwa kuna makundi ya watu wanaohamasisha wananchi kwa malipo ili wafanye maandamamo ya shari kufuatia matokeo ya uchaguzi yanayoendelea kutangazwa.
Kufuatia hali hiyo, Kova amewataka wananchi kujiepusha na mikusanyiko hiyo, vinginevyo jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote watakao shiriki vitendo hivyo.
source : TBC

Reply With Quote




Follow Us Here