Re: Anne Kilango achukua fomu ya kuwania spika wa bunge
Changieni....lakini mkae mkijua kwamba CCM wanaye mtu 'wao' tayari. Duru za siasa ndani ya chama cha mapinduzi zinaainisha kuwa Mh. JK ametoa mwongozo na jina la nani awe spika. Walio karibu na JK wanasema 'mzee' hakufurahia spika Sitta alivyosimamia mijadala mbalimbali katika bunge lililopita ikiwemo issue ya Richmond iliyopelekea kupoteza uwaziri mkuu kwa swahiba wake wa karibu sana Mh. Lowassa ambaye kwa kauli yake Jk anasema 'hawakukutana barabarani'. Hivyo JK hayuko tayari kuruhusu kiti cha uspika kikaliwe na mtu ambaye si "ndiyo mzee" kwa matakwa yake na ya kamati kuu ya CCM.
Ukipewa kazi ya kurina asali, mikono yako ikatapakaa asali, je utaisugua mikono kwenye vumbi ili kujisafisha au utailamba?
Follow Us Here