Re: Zitto awasha moto
well, hii move ya Mh. Zuberi Zitto nadhani ameicheza katika wakati muafaka, wote tunafahamu, ukipuliza moto ili uwake hupulizi mara moja. tena unapuliza kwa interval.
hapa tusiangalie Zitto as Zitto per se, kama an object of the move, bali tuangalie misingi ya accountability itakayowekwa na move nzima.
Huwezi kusema unaendesha mambo kwa kanuni na taratibu halafu unazivunja kanuni hizo unless umezivunja kwa bahati mbaya, lakini hata kama umezivunja kwa bahati mbaya uking'amua kwamba ulikosea huna budi kukiri kuwa ulikosea na wakati huo ukijaribu kuweka mambo sawa ili ikiwezekana usikosee kosa la namna hiyo tena na tena.
Kumcriticize mh. kwa move, ambayo mosi ana haki nayo kutokana na yeye kuwa mhanga wa maamuzi ambayo ana imani hakutendewa haki ni zaidi ya kutomtendea haki. unataka wananchi wa Kighoma waliomchagua mh .Zuberi Zitto waamini kwamba mbunge wao ni muongo kwa hiyo hafai?.
Pili as a politician, wakati wowote wa kugrab opportunity haipaswi kuiachia hivihivi. Nyerere alipata kuishinda hoja ya serikali Tatu kwa kurejea katika kanuni tu za chama, G55 na mahoja yao mazito wakakwama kuvunja hoja ya kanuni za chama. sasa sembuse leo kanuni za bunge ndo zivunjwe?.
Tatu, popote pale katika mihimili yote mitatu ya uongozi, kunahitajika changamoto, na hii ndiyo dhana nzima ya demokrasia, kutoitumia demokrasia vizuri hatuwezi kumlaumu yeyote, leo hii tukiendelea kutoa changamoto za kuiweka mihimili yote hii katika msitari ulionyooka ni matumaini yangu kutakuwa na umakini katika maamuzi yanayohusu maslahi ya umma.
Simba na nguvu zote alizonazo kofi moja halimwangushi nyati. Wapinzani wanatakiwa kuweka presha na kwa calculated timing.
Chadema kama mnapokea misaada kutoka nje bila kufanya tathmini, angalieni mkishika dola msije mkaiuza Tanzania na watu wake kwa vijimisaada vichache- Hao wanaowapa misaada hawana permanent Friends/Enemies, bali wana permanent Interests.
Follow Us Here