Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mchango wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

    Report Post
    Page 1 of 9 123 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 167
    1. #1
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,722
      Rep Power : 1594
      Likes Received
      912
      Likes Given
      29

      Default Mchango wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

      Mwka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa Zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru John Okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.

      Baada ya mapinduzi kufanikiwa John Okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio Zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa Zanzibar mzee Karume na Babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza John Okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.

      Baada ya hali kutulia Okello anamtangaza Karume rais na Abdulrahman Babu kuwa Waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea Karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.

      Baada ya siku chache mzee Karume akamfukuza Zanzibar kama mbwa John Okello [Field Marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya Okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]

      Naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya John Okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?

      Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu Kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la Field Marshal Dedan Kimathi...mbona wapenda hitoria Zanzibar na Tanganyika kwa jumla hamumtendei haki JOHN OKELLO [FIELDMASHAL]?

    2. Miaka 50

    3. #2
      Kichuguu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th October 2006
      Location : Popote Porini
      Posts : 6,833
      Rep Power : 3270
      Likes Received
      1300
      Likes Given
      914

      Default

      Philemon umesema ukweli,

      Historia ya Tanzania imekuwa na tabia ya kufuta michango ya wale ambao hawakupendwa na wakubwa: John Okello akiwa mmoja wao.

      Ingawa sijasoma maandiko yaliyopo kuhusu historia ya Tanzania kwa muda mrefu ukweli wa kuwa majina kama ya Okello, Kambona, na Kanali Mahafudhi yamefutika kabisa katika historia ya Tanzania. Bibi Titi Mohammed alipata bahati baada ya kurudi CCM na hivyo kurudisha jina lake katika historia lakini nalo lilikuwa limeshapotea.

      Tutafute utaratibu wa kutunza historia kamilifu ya nchi bila kujali uhusiano wa wahusika na "ukoo wa mfalme" ulikuwaje.
      Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

    4. #3
      Join Date : 5th September 2006
      Posts : 10,054
      Rep Power : 3352
      Likes Received
      238
      Likes Given
      0

      Default

      Wakati huo huo tusisahau kuwa wengine ambao tunalazimishwa kuwasahau ni
      Abdulwahid na Ally Sykes, Hamza Mwapachu, Tewa Said Tewa,Ali Migeyo , Suedi Kagasheki,Dossa Azizi,Abdulkarim Karimjee,Chifu Abdieli Shangali wa Machame, Kleist Sykes,Ally Sykes na Abdulwahid Sykes

      kwa uchache sasa huyo Okello alikwa ni just one in a million na at least eyey leo anazungumzwa

    5. #4
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,722
      Rep Power : 1594
      Likes Received
      912
      Likes Given
      29

      Default

      maprofessa mahiri wetu mko wapi kwa historia ya kweli,upo wapi haroub othman,proffesa mazrui, baregu na wengine tele wasomi..wanazuoni.

      Historia ya mataifa yetu hapa afrika mashariki imepindishwa ,andileni upya.....
      kwa nini tunawafundisha watoto ...uwongo..

    6. #5
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,612
      Rep Power : 2890
      Likes Received
      3831
      Likes Given
      12203

      Default

      Phillemon,
      Tafuta kile kitabu aliandika Okello juu ya mapinduziya Zanzibar. Utaanza kujiuliza Karume alikuwa na role gani pale. Pia ya kusikitisha zaidi, alipofukuzwa Zanzibar hakuruhusiwa hata kuchukua mizigo yake--achilia mbali malipo/compesation yake.

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      Besty's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2006
      Posts : 300
      Rep Power : 711
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By phillemon mikael
      Mwka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa zanzibar ...john okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio zanzibar,...baada ya siku chache mzee karume anamfukuza zanzibar kama mbwa ...
      YAITWAYO "MAPINDUZI"

      John Okello alitoka kwao Uganda, Injin aliyetoka kwao Kenya na Mfaranyaki aliyetoka Tanganyika, na kuivamia nchi huru usiku wa manane wa kuamkia tarehe12 Januari 1964. Wananchi, mafisadi kwa sababu ya maslahi ya nafsi zao hawakuhisi uchungu kuipoteza nchi yao, wala kuzipoteza roho za wazee wao, za ndugu zao na za marafiki zao. Kwa mujibu wa kitabu cha huyo aliyejipa ujamadari wa hayo 'mavamizi' ya Januari 12, 1964, John Okello, amesema kuwa watu waliyokufa katika 'mavamizi' hayo ni 13,000. Hii ni idadi ndogo kabisa aliyopenda kuitaja.

      Ukatili, ushenzi na unyama uliofanywa katika visiwa hivi vilivyokuwa na ustaarabu wa kupigiwa mfano, hauwezi hata kuhadithika. Wengi waliokuwa wanaijua Zanzibar, waliona taabu kuyaamini waliyokuwa wameyasikia yametokea Zanzibar kutokana na hayo yenye kuitwa 'mapinduzi'. Ilifika hadi, siku hiyo ya 'mavamizi' washenzi na makatili hao kuwanajisi maiti wa kike. Kitendo hicho hakijawai kufanyika katika nchi nyingi ulimwenguni zenye ubinaadamu na ustaarabu wake. Lenye kuzidi kushangaza na kusikitisha ni kumsikia mwananchi mwenye kujulikana kuwa yeye ndiye mwongozi wa hao wenye kujiita "progressives" akasema kuwa, watu waliyouliwa katika hayo yenye kuitwa 'mapinduzi' ni 491! Duh!

      Mwenyewe Okello alieongoza hayo mauwaji amesema kuwa wamekufa wananchi 13,000. Hata wangekuwa watano tu, bali ni binaadamu, ni wananchi, jee, ndio wawe wamestahiki kuuliwa kwa kuvamiwa nchi yao na wageni ambao wewe na wenzio kama wewe mmechanganyika na hao wageni katika kuifisidi nchi na wananchi wake? La kustaajabisha zaidi - ni pale ilipojulikana kuwa haya yote yalipangwa kabla - kwa siku 30 tu yaaani Desemba 10 mpaka Januari 11 ilitosha kujuwa uovu wa Serikali hata ikastahiki kupinduliwa? Hata ingelikuwa ni ovu hivyo, bali njia za kuiondowa za kikatiba zilikuwepo ambazo zingaliweza kutumika, khasa na hao Wapinzani. Haikuhitaji hata kidogo kutumia nguvu. Lakini hakika khasa ni kuwa mambo yalikwisha pangwa zamani, hayo yalikuwa ni matekelezo tu!!

    9. #7
      Game Theory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th September 2006
      Posts : 10,054
      Rep Power : 3352
      Likes Received
      238
      Likes Given
      0

      Default

      source or link?

    10. #8
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,612
      Rep Power : 2890
      Likes Received
      3831
      Likes Given
      12203

      Default

      DrWHO,
      Good question. Atupe source yake siyo kuandika tu yale anayoyafikiria moyoni mwake. Kama asemavyo rafiki yangu FD lazima uangalie kila upande wa shillingi, lakini toa source.

    11. #9
      Game Theory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th September 2006
      Posts : 10,054
      Rep Power : 3352
      Likes Received
      238
      Likes Given
      0

      Default

      maana kuna watu kibao walikuwa mashujaa wa Tanzania waliachwa ka kusudi wakati wanaandika historia sasa hizi kelele za Okello naona haziishi

      Iweje watu kama akina Suedi Kagasheki na Dosa Aziz wasipewe kipaumbele wakati Okello mnataka kumfanya Mungu Mtu?

      charity begins at home na tunao our sons and daughters ambao walipigania na kumwaga damu zao pale lakini husikii kitu
      Last edited by Game Theory; 19th November 2006 at 18:28.

    12. #10
      Besty's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2006
      Posts : 300
      Rep Power : 711
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default

      Kwa nini tusiwaenzi kina Chief Mkwawa, Mangi Sina, Mangi Mandara, Wakina Chief Songea Mbano na Chief Chabruma wa kule Ruvuma, au Saidi Milambo wa tabora, wakina Isike, Kinjekitile, au Chief Masanja, Chief Mataka wa kule kwa wayao? Who's Okello?

    13. #11
      Game Theory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th September 2006
      Posts : 10,054
      Rep Power : 3352
      Likes Received
      238
      Likes Given
      0

      Default

      Okello was a foreigner lakini kazi yake ilipokwisha akaambiwa kuwa muda wake ushaisha aanze

      sasa kuna jopo linaanza ku re write history

      huko nyuma walifanya hayo na leo hii wanarudia hayo hayo

    14. #12
      FairPlayer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th February 2006
      Location : UK
      Posts : 4,383
      Rep Power : 1550
      Likes Received
      456
      Likes Given
      205

      Default

      Besty,

      Tulia kwanza, are you allright?!?, tunazungumzia utaifa, Znz ni taifa sio kabila, dalili za kupenda ukabila ni dalili za ubinafsi na ufinyu wa kufikiri.

      FD
      Bigjahman likes this.
      A positive thinker!

    15. #13
      Besty's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2006
      Posts : 300
      Rep Power : 711
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Thumbs down

      Quote By fikiraduni
      Besty,

      Tulia kwanza, are you allright?!?, tunazungumzia utaifa, Znz ni taifa sio kabila, dalili za kupenda ukabila ni dalili za ubinafsi na ufinyu wa kufikiri.

      FD
      Kuna sehemu ambayo nimezungumzia ukabila? au umeshindwa kuelewa nilicho andika? Fikiri kabla ya kujibu tafadhali, kina Chief Mkwawa, Mangi Sina, Mangi Mandara, Wakina Chief Songea Mbano na Chief Chabruma wa kule Ruvuma, au Saidi Milambo wa tabora, wakina Isike, Kinjekitile, au Chief Masanja, Chief Mataka wa kule kwa wayao hawa ni alama ya taifa letu la Tanzania na ndio hawa tunapaswa kuwaenzi, watu hawa walionyesha uzalendo wa hali ya juu kulitetea Taifa letu la Tanganyika...

    16. #14
      Rubabi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th November 2006
      Posts : 188
      Rep Power : 675
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Mzee Philemon ahsante kwa kutoa topic hiii.Kwa ukweli mchango wa Okello katika mapinduzi ya waafrika umesahaulika sana.Inatakiwa ijengwe sanamu kubwa ya Okello kwa kuwa naamini kuwa huyu ni shujaa na jasiri mkubwa kuliko wote afrika ya mashariki,sidhani kama kuna mwanamapinduzi yoyote anayemkaribia huyu.

      Bahati mbaya mafanikio yake yametekwa na karume na wengine....lakini naamini Tanzania na Zanzibar tutamkumbuka mtu huyu miaka ijayo..wakati wanahistoria wetu watakapoacha mtindo wao wa kuchanganya historia na siasa.

      Ndio watu wengi walikufa,lakini revolution sio tea party,watu wanakufa lakini mafanikio ya kuondoa tabaka la makupe ambao waliwatweka wazanzibari mika zaidi ya 500 ya utumwa sio mchezo.

      Cha kushangaza, 'wanahistoria' wetu wa so called udsm no one among them has ever written anything on Okello,wenywewe huangalia 'mashujaa' wa nje tu.

      Ni aibu kubwa kwa watanzania!!!

      Ahsante Phil kwa insight yako!!

    17. #15
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,722
      Rep Power : 1594
      Likes Received
      912
      Likes Given
      29

      Default

      respect bro,,saluti pia kwa waazilishi wa TAA na TANU,kina sykes waliosahauliwa japhet kirelo[meru] na wengine...saluti

    18. #16
      dondola's Avatar
      Member Array
      Join Date : 14th November 2006
      Posts : 50
      Rep Power : 650
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Besty
      kina Chief Mkwawa, Mangi Sina, Mangi Mandara, Wakina Chief Songea Mbano na Chief Chabruma wa kule Ruvuma, au Saidi Milambo wa tabora, wakina Isike, Kinjekitile, au Chief Masanja, Chief Mataka wa kule kwa wayao hawa ni alama ya taifa letu la Tanzania
      Kweli machifu wetu hawa walionyesha uzalendo halisi , bila influence yeyote ya nje, licha ya kuwa jamii zao ziliishi kwenye 'ujima' (afrika ya leo, wapinzani/wanaharakati wengi, hubebwa na wageni). Chifu tuliyefundishwa kumtukana, Mangungo wa Msovero, aliyeuza ardhi kwa wageni, leo hii warithi wake tunawasifia kwa kuinua uchumi :D
      Thin line between creativity and madness

    19. #17
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,722
      Rep Power : 1594
      Likes Received
      912
      Likes Given
      29

      Default

      home.globalfrontiers.com/zanzibar/zanzibar_revolution.htm

      please members ,go through these catches above ,i am afraid to say that mapinduzi yanayosheherekewa lewa its just a nightmare ,i dont see anywere unless in zanzaibar gorvernment side of story the role of abeid karume and fellows in revulution ,walijificha hadi kina okello walipomaliza kazi ndio wakaibuka,revolutionarry gorvernment should come out watuambie kwa nini hawataki kumsikia okello na pia inaonekana wwaliopigana kikweli hawajaenziwa....

    20. #18
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,722
      Rep Power : 1594
      Likes Received
      912
      Likes Given
      29

      Default

      home.globalfrontiers.com/zanzibar/zanzibar_revolution.htm[/URL

      angalia na hapo juupia ,kwenye mtandao hapa chini kuhusu abeid amani karume ,hakuna mahali panaposema yeye ndie aliongoza haya mapinduzi wanayosheherekea leo...

      www.tanemb.se/karumeprofile.htm

      nashauri haya mambo ya kuendeleza mapinduzi hadi leo ambayo haykuwa na uongozi wa KARUME muache unganeni mjenge nchi...

    21. #19
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,722
      Rep Power : 1594
      Likes Received
      912
      Likes Given
      29

      Default

      http://home.globalfrontiers.com/zanz...revolution.htm

      endelea kuangalia hapa chini ,HISTORIA YA MAISHA YA OKELLO,namna alivyopindua na kisha kutimuliwa na karume na baadaye akaishia kwenye mikono ya iddi AMIN.....hiii KALI ZAIDI

      en.wikipedia.org/wiki/john_okello

      sasa nani anayo historia inayotambulika duniani inayosema tofauti na hii .aweke hapa....

    22. #20
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,722
      Rep Power : 1594
      Likes Received
      912
      Likes Given
      29

    Page 1 of 9 123 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Replies: 3
      Last Post: 29th November 2011, 18:10
    2. Replies: 3
      Last Post: 31st January 2011, 14:32
    3. Replies: 0
      Last Post: 3rd January 2011, 02:45

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...