Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mchango wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

    Report Post
    Page 3 of 9 FirstFirst 12345 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 167
    1. #1
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,722
      Rep Power : 1594
      Likes Received
      912
      Likes Given
      29

      Default Mchango wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

      Mwka 1964 siku thelathini baada ya uhuru wa bandia wa Zanzibar, wanamapinduzi kumi na nne wakiongozwa na mpigania uhuru John Okello aliwaongoza kwenye mapinduzi ya Zanzibar yaliyokuwa na umwagaji mkubwa wa damu.

      Baada ya mapinduzi kufanikiwa John Okello [kiongozi wa mapinduzi] alichukua jukumu la kutangaza mapinduzi kwenye radio Zanzibar, ikumbukwe pia wakati mapambano yakiendelea ..aliyekuja kuwa rais wa Zanzibar mzee Karume na Babu walikuwa mafichoni na hawakushika wala bisibisi kwenye mapinduzi na hata ukiangalia ile picha ya wanamapinduzi ya kwanza John Okello amevalia kipolisi na amekaa kama kiongozi rasmi.

      Baada ya hali kutulia Okello anamtangaza Karume rais na Abdulrahman Babu kuwa Waziri mkuu. Na ndie aliyeenda kumpokea Karume kutoka alikokuwa amejificha kwa siku kadhaa.

      Baada ya siku chache mzee Karume akamfukuza Zanzibar kama mbwa John Okello [Field Marshal] na bila kujali mchango wake anatokomea kusikojulikana na historiaa ya mapinduzi ikafutwa na nafasi ya Okello ikaja kuwa mkwezi, mpiga tofali ambaye alibahatika kupiga picha [akiwa amekaa kitini katikati tu kwa sababu ya kuwa na kipaji cha kuongea - (kumbuka kuwa hata kiswahili chake kilikuwa 0kibovu)]

      Naomba kuchokoza mada kuhusu nafasi ya John Okello kwenye mapinduzi, kwa nini historia ilifunikwa?

      Je aliishia wapi,..wapenda historia ya kweli wameshatamani hata kujua lilipo kaburi lake..kumbukeni wenzetu Kenya baada ya kugundua hila wanahaha kutafuta kaburi la Field Marshal Dedan Kimathi...mbona wapenda hitoria Zanzibar na Tanganyika kwa jumla hamumtendei haki JOHN OKELLO [FIELDMASHAL]?

    2. Miaka 50

    3. #41
      Safari_ni_Safari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2007
      Location : Kibaruani
      Posts : 11,883
      Rep Power : 24131
      Likes Received
      4612
      Likes Given
      2624

      Default Re: Mchango Wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

      In the middle


      Soki Ozali Mwasi Yaka, Soki Ozali Mobali Koya Te


    4. #42
      Gsana's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th August 2010
      Location : Dar es salaam
      Posts : 2,227
      Rep Power : 888
      Likes Received
      214
      Likes Given
      30

      Default Re: Mchango Wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

      Nilipata kuijua historia ya Zanzibar mwaka 2006,nilisikitika sana. Kuna matukio makubwa yanayoweza kukutoa chozi ukifuatilia upande wa pili wa Tanzania! Pia sihafiki historia ya kweli ya Tanzania kufundisha shuleni,vingnevo baada ya darasa watoto wanaweza kuingia mtaani kwa mapinduzi ya pili. Ukiangalia watu aliowafukuza mwl.Nyerere baada ya uhuru kwamba walikuwa wanaandaa mapinduzi pale mkwajuni kindoni,ukisoma jinsi dr.Ahammed Salimu anavohusishwa na zanzibar,worse uyu John Okello,ni majonzi matupu! Mwaka 2006 walitoa habari ya Maisha magumu ya Field Marshall John Okello alivokuwa anaishi Kenya surbubs,hamna mtz hata mmoja alijitokeza kujua mambo yake. Mwaka 2007 nilienda pale Vijana Hostel karibu na mango garden,ndo tulipokuwa tunalaza gari wakati ule,nilikuta ukuta wa hostel umejazwa picha za John Okello akila shida uko Kenya,yani niliona ajabu kubwa! Jaman uyu mtu hajafa,nahisi bado yu hai kenya,unless mtu alete taarifa ya Kifo chake,ikiwezekana wapenda historia tumtafute! Ni hayo wanaJf!

    5. #43
      alsaidy's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd February 2009
      Posts : 239
      Rep Power : 568
      Likes Received
      17
      Likes Given
      61

      Default Re: Mchango Wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

      Quote By Jasusi
      alsaidy,
      Samahani sana lakini Ghassany kachakachua historia. Huwezi kuandika historia based on heresay.
      Mkuu Jasusi,

      Sijui umepata muda wa kukipitia kitabu chote au labda una mashaka na maandishi yake?

      Mimi binafsi nina amini kabisa ni ukweli kilichoandikwa beside reference zake baadhi ya watu wanasema ni hadithi za kusimuliwa.

      If that is the case naomba mwenye Historia ya kweli ambayo inapingana na ya Harith Ghassany atuwekee hapa watu wapate kuchambua na mtu mwenyewe apate kuamua which History to follow based on source.
      "Whoever submits his whole self to Allah, and is doer of good, has grasped indeed the firmest hand-hold and to Allah shall all things return" (Luqman 31:22)

    6. #44
      bitimkongwe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st October 2009
      Posts : 1,653
      Rep Power : 817
      Likes Received
      202
      Likes Given
      83

      Default Re: Mchango Wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

      Jasusi, at this stage nani atakuwa na historia ya kweli? Kitabu cha Ghassany sijakisoma chote lakini wengi wa aliowafanyia interview walikuwa wameshuhudia hayo mapinduzi na baadhi walishiriki.Nadhani katika wanamapinduzi original basi ni Ramadhani Haji tu ndiye aliye hai na hivi sasa ni mzee sana na akili zimeshakimbia.

      Okello alikuwa kibarua mchonga mawe tu na ushahidi upo mpaka leo nenda pale soko la Chake Chake yale mawe ya kuchongwa yaliyowekwa ni kazi ya Okello. Yeye hakuwa Mzanzibari by any standard (hata hiyo ya kikoloni) na alikuja kama kibarua. Kuna Mzee mmoja sasa hivi marehemu aliwahi kunieleza vipi Okello alipata ile tetesi ya matayarisho ya Mapinduzi. Inasemekana alisikia watu wanasema siri zao na yeye akasema yuko tayari kujiunga ili kumpinga Mwarabu. Alilazimisha kujiunga na kwa kuogopa siri isije kutoka basi ikabidi wamuingize kwenye mpango huo. Bahati yake ni kwamba yeye aliwahi kuwa askari huko anakotoka ijapokuwa hajawahi kukubali hata siku moja (soma kitabu chake).

      Alizidisha vitisho kila mtu alitaka kumchapa viboko elfu tisa, mia tisa na tisini na tisa (soma kitabu chake) mpaka ikawa hamkani Zanzibar hakukaliki ni viboko tu. Sasa kama mtu mwenyewe siyo raia si afukuzwe tu.

      Ukisoma kitabu cha Clayton utaona kwamba mpango wa kumuondoa ulipangwa na Karume na Nyerere kwa pamoja, kwani aliambiwa anaitwa Tanganyika na alipoondoka tu basi huku nyuma aliambiwa asikanyage Zanzibar kwa vile si raia. Alipofika Dar akaambiwa yeye si raia na hatakiwi hapo, akaishia Kenya ambako aliwekwa Shimo la Udongo wakati mipango ya kumrejesha kwao Uganda inaendelea.

      Baadae walimrejesha kwao Uganda na kwa vile alikuwa na reputation ya kufanya Mapinduzi (theory mpya kwa wakati ule) basi alipokewa kwa suspicion kubwa sana hata huko kwao Uganda. Maisha hayakuwa mazuri kwake na baadae inasemekana alifariki.

    7. #45
      Visenti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th July 2008
      Posts : 605
      Rep Power : 677
      Likes Received
      117
      Likes Given
      276

      Default Re: Mchango Wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

      Quote By bitimkongwe
      Baadae walimrejesha kwao Uganda na kwa vile alikuwa na reputation ya kufanya Mapinduzi (theory mpya kwa wakati ule) basi alipokewa kwa suspicion kubwa sana hata huko kwao Uganda. Maisha hayakuwa mazuri kwake na baadae inasemekana alifariki.
      .........Okello then stayed in Kenya, in Congo-Kinshasa and in Uganda. He was incarcerated multiple times and was last seen with the Ugandan president Idi Amin in 1971 and vanished afterwards. In the book “Revolution on Zanzibar”, written by Don Petterson, it is more or less assumed that Idi Amin saw him as a threat (after Amin promoted himself, Okello reportedly joked that "now Uganda has two field marshals") and had arranged his assassination. This remains speculative, however.
      "Speed in a wrong direction is irrelevant" - M.Ghandi

    8. FemaTV & Radio

    9. #46
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,646
      Rep Power : 4015
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Mchango Wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

      Quote By Phillemon Mikael
      maprofessa mahiri wetu mko wapi kwa historia ya kweli,upo wapi haroub othman,proffesa mazrui, baregu na wengine tele wasomi..wanazuoni.

      Historia ya mataifa yetu hapa afrika mashariki imepindishwa ,andileni upya.....
      kwa nini tunawafundisha watoto ...uwongo..
      Hilo nalo neno! Kwanini historia ya Tanzania inapindishwa karibu kila eneo?
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    10. #47
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1742
      Likes Received
      1518
      Likes Given
      2835

      Default Re: Mchango Wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

      Quote By bitimkongwe
      Jasusi, at this stage nani atakuwa na historia ya kweli? Kitabu cha Ghassany sijakisoma chote lakini wengi wa aliowafanyia interview walikuwa wameshuhudia hayo mapinduzi na baadhi walishiriki.Nadhani katika wanamapinduzi original basi ni Ramadhani Haji tu ndiye aliye hai na hivi sasa ni mzee sana na akili zimeshakimbia.

      Okello alikuwa kibarua mchonga mawe tu na ushahidi upo mpaka leo nenda pale soko la Chake Chake yale mawe ya kuchongwa yaliyowekwa ni kazi ya Okello. Yeye hakuwa Mzanzibari by any standard (hata hiyo ya kikoloni) na alikuja kama kibarua. Kuna Mzee mmoja sasa hivi marehemu aliwahi kunieleza vipi Okello alipata ile tetesi ya matayarisho ya Mapinduzi. Inasemekana alisikia watu wanasema siri zao na yeye akasema yuko tayari kujiunga ili kumpinga Mwarabu. Alilazimisha kujiunga na kwa kuogopa siri isije kutoka basi ikabidi wamuingize kwenye mpango huo. Bahati yake ni kwamba yeye aliwahi kuwa askari huko anakotoka ijapokuwa hajawahi kukubali hata siku moja (soma kitabu chake).

      Alizidisha vitisho kila mtu alitaka kumchapa viboko elfu tisa, mia tisa na tisini na tisa (soma kitabu chake) mpaka ikawa hamkani Zanzibar hakukaliki ni viboko tu. Sasa kama mtu mwenyewe siyo raia si afukuzwe tu.

      Ukisoma kitabu cha Clayton utaona kwamba mpango wa kumuondoa ulipangwa na Karume na Nyerere kwa pamoja, kwani aliambiwa anaitwa Tanganyika na alipoondoka tu basi huku nyuma aliambiwa asikanyage Zanzibar kwa vile si raia. Alipofika Dar akaambiwa yeye si raia na hatakiwi hapo, akaishia Kenya ambako aliwekwa Shimo la Udongo wakati mipango ya kumrejesha kwao Uganda inaendelea.

      Baadae walimrejesha kwao Uganda na kwa vile alikuwa na reputation ya kufanya Mapinduzi (theory mpya kwa wakati ule) basi alipokewa kwa suspicion kubwa sana hata huko kwao Uganda. Maisha hayakuwa mazuri kwake na baadae inasemekana alifariki.
      Asante ila umeandika kishabiki zaidi na sijui lengo ni nini hapa!

      Umemdharau Okello, na kusema vitu vingi ambavyo unajicontradict mwenyewe! tafuta na andika historia sahihi, na ushabiki usiwepo hapa, unacholinda ni nini?

      Okello ndiye aliyeongoza mapinduzi, kwa taarifa yako video za kipindi hicho zipo!

      Okello unayemdharau ndiye aliyemkabidhi Karume na Babu nchi! tena kupitia redioni, I mean kama angekuwa na tamaa ya madaraka alikuwa ameisha kiteka kisiwa!!

      Jina la Okello litabaki kuwa ni symbo na ni watu ambao baada ya kutumika na Nyerere na Karume walikuwa dumped!!

      Ukweli unabaki kuwa
      Shamte ndiye baba wa taifa la Zanzibar
      Ukweli unabaki Nyerere amefuta historia za heroes wengi wa Tanzania kumzidi yeye

      Karume+Nyerere =unapata wahuni fulani tu waliotutawala na leo tuna suffer matendo yao!

      Quote By Visenti
      .........Okello then stayed in Kenya, in Congo-Kinshasa and in Uganda. He was incarcerated multiple times and was last seen with the Ugandan president Idi Amin in 1971 and vanished afterwards. In the book “Revolution on Zanzibar”, written by Don Petterson, it is more or less assumed that Idi Amin saw him as a threat (after Amin promoted himself, Okello reportedly joked that "now Uganda has two field marshals") and had arranged his assassination. This remains speculative, however.
      unajifagilia na hiyo avatar!! umesema speculations sina comment na kama ni kweli ilikuwa hofu yako tu (avatar) kwani Okello alikuwa siyo mroho wa madaraka!
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    11. #48
      Pendulum's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 6th November 2010
      Posts : 7
      Rep Power : 434
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Mchango Wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

      Bwana Phillemon, tafadhali tafiti kwanza kuliko kuegemea historia ya mapinduzi ambayo imejaa utata mtupu. Mimi sikubaliani na mtazamo wako kumfananisha Okello na Che Guevara ni upofu! Tafuta ukweli. Nchi hii ina mashujaa wa kweli ambao wamezimwa makusudi na hawajulikani kwa kizazi cha sasa.

    12. #49
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7367
      Likes Received
      6151
      Likes Given
      22273

      Default Re: Mchango Wa John Okello [che Guevara wa East Africa] umefutwaje?

      Quote By mtu chake
      Wakati huo huo tusisahau kuwa wengine ambao tunalazimishwa kuwasahau ni
      Abdulwahid na Ally Sykes, Hamza Mwapachu, Tewa Said Tewa,Ali Migeyo , Suedi Kagasheki,Dossa Azizi,Abdulkarim Karimjee,Chifu Abdieli Shangali wa Machame, Kleist Sykes,Ally Sykes na Abdulwahid Sykes

      kwa uchache sasa huyo Okello alikwa ni just one in a million na at least eyey leo anazungumzwa,




      umenikumbusha mbali sana haya majina...kn wanaosema waislam ndiyo walianza harakati za kudai uhuru? nisaidieni maana kuna jamaa yangu mmoja ana udini sana hasa katika suala la historia ya uhuru..
      Kuna wengine wawili waliosahauliwa, hawa ni Robert Makange na jamaa mwingine akiitwa Baghdelah walifungwa jela na mkoloni katika harakati za uhuru.

    13. #50
      Bramo's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 21st October 2009
      Location : Mtimbwani
      Posts : 1,680
      Rep Power : 0
      Likes Received
      445
      Likes Given
      300

      Default John Okello --> Shujaa aliyesahauliwa Mapinduzi ya Zanzibar

      Field Marshal John Gideon Okello (1937, Wilayani Lango Uganda – 1971?) Alikuwa ni mwana mapinduzi wa Afrika ya Mashariki na Kiongozi wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyo mng'oa Sultan Jamshid Bin Abdulah.

      Maisha yake

      Alianza kuishi maisha ya uyatima akiwa na miaka 11. Alipofikisha umri wa miaka 15 aliondoka nyumbani kwao na kwenda kutafuta ajira katika maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki.
      Kuanzia mwaka 1944 alikuwa amefanya kazi nyingi ikiwa ni pamoja na ukarani, mtunza bustani na mfanyakazi katika idara na shughuli mbalimbali. Hata hivyo, alijifunza kufanya biashara ya kuuza matofali na baadaye alimudu kufanya kazi ya uashi, lakini alikamatwa mjini Nairobi, kutokana na sababu ambazo hazikuelezwa; hata hivyo yeye mwenyewe aliwahi kuelezwa kuwa alikamatwa kutokana na makosa yaliyohusiana na hali ya jinsia. Alifungwa miaka miwili gerezani. Kifungoni ndiko kulikomfanya awe na fikra za kimapindizi.
      Mara nyingi umekuwapo uvumi kuwa huenda Okello alikuwa amepata mafunzo yake nchini Cuba, lakini jambo hili halikuwahi kuthibitishwa na Okello mwenyewe.

      Mapinduzi

      Mwaka 1959 aliingia kisiwani Pemba katika harakati zake za kutafuta ajira kwenye mashamba ya karafuu, lakini badala yake alijiunga na jeshi la polisi.
      Hata hivyo, baadaye alijiunga na Chama cha Afro-Shirazi kilichokuwa kinapinga jamii ya watu wachache kuhodhi uchumi wa Zanzibar na Pemba.
      Inaelezwa kuwa Okello alikuwa muumini mzuri wa dini. Aliamini kuwa alipewa amri hizo na Mungu akiwa kwenye ndoto kuuondoa utawala wa mabavu wa Waarabu na kuanzisha serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Pemba.
      Usiku mmoja kabla ya mapinduzi hayo, Okello aliwaamuru watu wake kuua vijana wote wa Kiarabu waliokuwa na umri kati ya miaka 18 na 25, lakini wasiwadhuru kina mama wajawazito na wazee na pia wasifanye ubakaji.
      Januari 12, 1964 akiwa anaungwa mkono na asilimia kubwa ya watu waliokuwa wanakandamizwa – wengi wao wakiwa Waafrika – Okello na kikosi chake waliweza kuingia katika mji wa Stone Town, Zanzibar, kulikokuwa maskani ya Sultan.
      Inaelezwa kuwa takriban watu 10,000 waliuawa, licha ya kwamba kikosi cha Okello kilikuwa na silaha duni. Okello na kikosi chake walilishangaza Jeshi la Polisi Zanzibar na kuchukua ofisi zao.
      Kwenye hotuba yake iliyotangazwa kwa njia ya redio, Okello alitangaza kuwa yeye ni ‘Field Marshal wa Zanzibar na Pemba’ na alimwamuru Sultan aue familia yake na kisha ajiue mwenyewe, la sivyo Okello ataifanya kazi hiyo mwenyewe.
      Hata hivyo, Sultani mwenyewe alikuwa tayari ameshajipatia maficho ya usalama nchini Uingereza, na waziri mkuu pamoja na mawaziri wengine pia waliwahi kutoroka.
      Kuwekwa pembezoni
      Kutokana na kufanikiwa kwa mapinduzi hayo, Okello alitangaza Baraza la Mapinduzi na Sheikh Abeid Amani Karume kuwa Rais. Kiongozi wa Chama cha Umma, Abdulrahman Mohamed Babu, akawa waziri mkuu. Baadaye alikuja kuwa Makamu wa Rais.
      Sheikh Karume na Babu hawakuwa wamejulishwa kuhusu mapinduzi hayo ya kijeshi kwani wote walikuwa Tanganyika, lakini walirudi Zanzibar walikokaribishwa na Okello.
      Lakini pamoja na shughuli yote aliyoifanya si Karume wala Babu waliomhitaji tena. Okello aliondoka kuelekea Tanganyika na kuanzia wakati huo alizuiwa kurudi Zanzibar na alipigwa marufuku pia asionekane Tanganyika na Kenya.

      Kutengwa

      Kuna wengi walifanya mambo yanayofanana na Okello. Miongoni mwao ni Ernesto Guevara de la Serna maarufu kama Che Guevara, aliyeshiriki kikamilifu kwenye mapinduzi ya Cuba licha ya kwamba alikuwa ni mzaliwa wa Argentina.
      Leo hii Che Guevara ni jina linalosifika na kuheshimika nchini Cuba kutokana na mchango wake. Haiyumkiniki jina la Okello nalo lingekuwa ni jina la kuheshimika kwenye na kukumbukwa kwenye Mapinduzi ya Zanzibar lakini ndivyo imekuwa sivyo.

      My Concern:
      Kwanini Tunapoadhimisha Mapinduzi ya Zanzibar John Okello haenziwi??
      Last edited by Bramo; 11th January 2011 at 23:34.

    14. #51
      Gsana's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th August 2010
      Location : Dar es salaam
      Posts : 2,227
      Rep Power : 888
      Likes Received
      214
      Likes Given
      30

      Default Confirmed: John okello ndo mwanamapinduzi Zanzibar,Karume aliwekwa!

      WanaJf salaam! Nakumbuka siku chache palikuwepo na mjadala mzito kuhusu nani aliyeleta mapinduzi Zanzibar na leo kiu yangu ya kujua mambo imetimia. Leo sa1 asubuhi TBC1 wameonesha vizuri kuwa mwanamapinduzi alikuwa mtu mwenye utata wa uraia John Okello akisaidiwa na Engen aliyekuwa mkenya. Kuna mzanzibar aliyekuwa na umri wa miaka 14 Salim S.Salim ameleta waraka pale Tbc akieleza nani alileta uhuru wa zbar,kasema John Okello. Pia Fatma,mama Karume ameeleza kuwa wakati wamelala na Mzee karume alikuwa akisikia risasi nje na wao hawakuwa na taarifa yoyote ya mapinduzi na wala Karume hakujua mapinduzi yatakuwa lini,lakini mpango wa kupindua ulikuwepo pia naye Karume alikuwa anajua kuwa siku moja yatakuwepo.
      Mama Karume kaeleza mengi sana yanayoonesha kuwa Karume hakuhusika,ila baada ya mapinduzi kuna watu walifika kwa karume wakiwa na gari ya kijani na nyingine ya manjano walikuwa wamefunga shoka juu ndo walipofika kwa karume na kupitia mlango wa nyuma waligonga mlango na mama karume alipofungua mlango aliona sura ambazo hakuzikariri wala hakuziona tena,walifika wakasema wanamtaka mzee na kisha waliondoka nae baada ya kukamilisha mapinduzi! Nadhani mama amemaliza utata uliokuwepo hapa Jamvini. WanaJF sasa kwa nini hii historia ya kweli isifundishwe mashuleni na watu wanadanganywa??kwa faida ya nani?? Mwisho: WanaJF kuna kitu kimenstua kwenye mapinduzi,kumbe ASP walikuwa na ishara kama ya Chadema,yani vidole viwili kama ishara ya chadema ya sasa. Hapa akili inasumbuka,ina maana chadema imechagua ishara ya mapinduzi kama ya Zbar au? Ningetaka muelewa anieleshe,ni ombi langu tu! Nawatakia siku njema!

    15. #52
      msomi_wa_zamani's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th November 2010
      Location : Tabora,Tanzania
      Posts : 17
      Rep Power : 433
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Confirmed: John okello ndo mwanamapinduzi Zanzibar,Karume aliwekwa!

      SLOGANI YA "MAPINDUZI DAIMA INAAMANISHA NINI" ?
      UKIFUATILIA KILICHOTOKEA KATIKA MAPINDUZI YA ZANZIBAR,DAMU ILIVYOMWANGWA,HALAFU UNAMSIKIA RAIS WA ZANZIBAR ANASEMA MAPINDUZI DAIMA,SIPATI PICHA.
      WAKATI UMEFIKA SHEREHE ZA KIPUUZI KAMA HIZI ZIFUTWE JAMANI HEE.!!
      ZINAAIBISHA TAIFA.

      MWANA JF ANGALIA HIZI VIDEO MBILI ZILIZOPO KWENYE YOUTUBE

      MAPINDUZI YA ZANZIBAR VIDEO NO :1

      MAPINDUZI YA ZANZIBAR VIDEO NO :2

      SOMA NA MAKALA HII

    16. #53
      Uwezo Tunao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2010
      Posts : 6,867
      Rep Power : 2288
      Likes Received
      1131
      Likes Given
      1478

      Default Re: Confirmed: John okello ndo mwanamapinduzi Zanzibar,Karume aliwekwa!

      Nakuunga sana mkono na thread yako ya mchana niliisoma kiundani sana tu. kweli wana jf great thinkers sio siri na hapo jamvi letu limeleta hali ya leo hii taifa kuelezwa ukweli uliokwepwa kwa miaka mingi mno.

    17. #54
      Chimunguru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2009
      Posts : 7,792
      Rep Power : 2148
      Likes Received
      1221
      Likes Given
      543

      Default Re: Confirmed: John okello ndo mwanamapinduzi Zanzibar,Karume aliwekwa!

      Mmimi nimesoma kile kitabu Cha JOHN OKELLO, hawa akina Karume hawana cha kujivunia pale inasikitisha sana tena sana jamaa walichomfanyia

    18. #55
      msomi_wa_zamani's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th November 2010
      Location : Tabora,Tanzania
      Posts : 17
      Rep Power : 433
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Confirmed: John okello ndo mwanamapinduzi Zanzibar,Karume aliwekwa!

      Quote By Chimunguru
      Mmimi nimesoma kile kitabu Cha JOHN OKELLO, hawa akina Karume hawana cha kujivunia pale inasikitisha sana tena sana jamaa walichomfanyia
      Mkuu hicho kitabu naweza kukipata wapi.

    19. #56
      Edward Teller's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2010
      Location : Area 51
      Posts : 3,431
      Rep Power : 1120
      Likes Received
      570
      Likes Given
      612

      Default Re: Confirmed: John okello ndo mwanamapinduzi Zanzibar,Karume aliwekwa!

      HII NCHI KILA KILICHO CHA UKWELI INAJARIBU KUKIPINDISHA NA KUDANGANYA UMMA,SIJUI LINI SERIKAL ITAACHA KUWADANGANYA WANANCHI WAKE-CHEK LINK HII PIA-
      John_Okello
      “Talk slowly but think quickly”

    20. #57
      Uwezo Tunao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2010
      Posts : 6,867
      Rep Power : 2288
      Likes Received
      1131
      Likes Given
      1478

      Default Re: Confirmed: John okello ndo mwanamapinduzi Zanzibar,Karume aliwekwa!

      Hicho kitabu kinapatikana wapiii???

    21. #58
      Gwaje's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 213
      Rep Power : 475
      Likes Received
      34
      Likes Given
      389

      Default Re: Confirmed: John okello ndo mwanamapinduzi Zanzibar,Karume aliwekwa!

      John Okello anapaswa kuendelea kuitwa field marshal na mwanamapinduzi wa zanzibar waganda wanapaswa kudai fidia ya kuchangia umapinduzi ya zanzibar

    22. #59
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,646
      Rep Power : 4015
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Confirmed: John okello ndo mwanamapinduzi Zanzibar,Karume aliwekwa!

      Toka lini ukweli ukafunikwa chini ya kapeti ikawezekana? Tunaambiwa miaka mingi iliyopita, kuna msomi mmoja wa kigiriki aliwaambia watu dunia ni duara, kanisa likamlaani. Ila baadae ikaonekana kuwa walimuonea maana kweli dunia ni duara.
      Na kuna mifano mingi ambayo inaonyesha jinsi ilivyo ngumu kuuchezea ukweli. Well, historia ya Tanganyika na Zanzibar imepindishwa kwa makusudi kabisa ili kunufaisha watu fulani.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    23. #60
      mams's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th July 2009
      Posts : 604
      Rep Power : 621
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default Re: Confirmed: John okello ndo mwanamapinduzi Zanzibar,Karume aliwekwa!

      Ni siri iliyowazi, John Okelo did everything na kumkabidhi AAK ila jamaa alionekana atakuwa maarufu kisha wakam marginalize Bara na Baadaye akaenda Kenya na kuishia home of origin Uganda. Nako Uganda, inasemekana Idd Amina alimuona ni threat zaidi na inasemekana alipotea ktk mazingira ya ajabu na kuhofia kuuwawa na Idd Amin DADA. Kwani yeye alikuwa ni Field Marshal wa kweli wakati Idd Amin alikuwa ni wa kujipachika. Bado histaria ya Mapinduzi Zanzibar haiwezi kamilika bila yeye na ninadhani kama wote wangekuwa hai basi wangeheshimiana sana. Lakini kitendo chake cha kumkabidhi AAK nadhani ni cha kawaida kwani asingeweza kuwa yeye kwa kuwa alikuwa ni raia wa Uganda na alichofanya ni kumkabidhi mzawa anayekubalika.

    Page 3 of 9 FirstFirst 12345 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Replies: 3
      Last Post: 29th November 2011, 18:10
    2. Replies: 3
      Last Post: 31st January 2011, 14:32
    3. Replies: 0
      Last Post: 3rd January 2011, 02:45

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...