Ukistaajabu ya Mussa... - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Jukwaa la Siasa


Jukwaa la Siasa Tanzania & World Politics General Discussion Forum. You need to be registered in order to post your comment(s)


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 15th December 2007, 08:09 PM   #1
Ukistaajabu ya Mussa...
Bubu Ataka Kusema Bubu Ataka Kusema is offline 15th December 2007, 08:09 PM

Tangu lini mahakama ikapangiwa muda maalumu wa kumaliza kesi na siri kali!?

Hapa si kuna ushahidi tosha kwamba siri kali inaingilia kazi za mahakama? Kwa jinsi Slaa anavyoendesha siri kali huko bungeni, siri kali itakubali hii kesi isisikilizwe tena? jibu tunalijua.
Je, gharama za kuanza upya kesi hii nani atazibeba? maana jury wanaweza kuwa wamesahau ushahidi uliotolewa na hivyo itabidi kuanza upya.

Kesi ya Slaa yaahirishwa

na Mustafa Leu
Tanzania Daima

KESI namba 20 ya mwaka 2005 iliyofunguliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Karatu, kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo, imeahirishwa kwa muda usiojulikana kutokana na muda uliokuwa umewekwa kusikiliza kesi hiyo kwisha kabla ya kesi kufikia ukingoni.
Akiahirisha kesi hiyo ambayo imekuwa ikiendelea katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa muda wa wiki nzima mfululizo kwa vipindi ya asubuhi na mchana, Jaji Robert Makaramba alisema kuwa, kesi hiyo kuendelea kusikilizwa au kutokuendelea kutategemea na uamuzi wa serikali ambayo itapanga utaratibu mwingine.

Kesi hiyo ilifunguliwa na wanachama watatu wa CCM wakipinga matokeo yaliyokipa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ushindi wa Jimbo la Karatu ambapo, Dk. Willbroad Slaa alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa mshindi kwa kumshinda mgombea ubunge wa CCM, Patrick Tsere ambaye baadaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Mawakili wa pande zote za walalamikaji, utetezi na serikali kwa pamoja walikubaliana na uamzi huo wa kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi taratibu nyingine zitakapopangwa.

Kesi hiyo ilichelewa kuanza kusikilizwa kutokana na walalamikaji kuchelewesha kuwasilisha vielelezo mahakamani katika muda uliokuwa umepangwa.

Hadi jana, alikuwa ni shahidi mmoja tu wa kwanza, Joseph Haim ndiye aliyekuwa akiendelea kutoa ushahidi wake wa kupinga matokeo kati ya mashahidi 25 wanaotarajiwa kutoa ushahidi wao.

Wakili wa utetezi, Tundu Lissu aliiambia mahakama hiyo kuwa, muda uliokuwa umepangiwa kesi hiyo umekwisha kutokana na upande wa walalamikaji kuchelewa kukamilisha vielelezo vyao.

Katika kesi hiyo, mshitakiwa wa kwanza ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wa pili ni Mbunge wa Karatu, Dk. Slaa, hivyo kesi hiyo iwapo itapangwa, lazima izingatie ratiba ya vikao vya Bunge.

Katika hatua nyingine, shahidi wa kwanza wa CCM, Haim alishukuru hatua ya mahakama hiyo ya kuahirisha kesi hiyo ili aweze kuishi huru kwani amekuwa chini ya kiapo tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa na hivyo kukosa amani na uhuru.

Hali hiyo imetokana na kutokukamilika mapema ushahidi wake ambao alikuwa akiutoa mahakamani na hatimaye kuonekana kuchoswa na maswali aliyokuwa akiulizwa mara kwa mara na mawakili kutokana na kukaa kizimbani kila siku asubuhi na mchana.
__________________
~*~Life is Good~*~

 
Bubu Ataka Kusema's Avatar
Bubu Ataka Kusema
JF Premium Member
Points: 12,700,657, Level: 100 Points: 12,700,657, Level: 100 Points: 12,700,657, Level: 100
Activity: 56% Activity: 56% Activity: 56%
Join Date: Sun Feb 2007
Location: Mfaranyaki
Posts: 12,678
Thanks: 1,034
Thanked 1,199 Times in 697 Posts
Views: 251
Reply With Quote
  #2  
Old 15th December 2007, 08:18 PM
Dua's Avatar
Dua Dua is offline
Dua busy at the moment.
JF Senior Expert Member
Points: 644,099, Level: 100 Points: 644,099, Level: 100 Points: 644,099, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Tue Nov 2006
Posts: 3,534
Thanks: 0
Thanked 3 Times in 2 Posts
Rep Power: 32
Dua will become famous soon enoughDua will become famous soon enoughDua will become famous soon enoughDua will become famous soon enoughDua will become famous soon enoughDua will become famous soon enoughDua will become famous soon enoughDua will become famous soon enough
Default Re: Ukistaajabu ya Mussa...

Quote:
Katika hatua nyingine, shahidi wa kwanza wa CCM, Haim alishukuru hatua ya mahakama hiyo ya kuahirisha kesi hiyo ili aweze kuishi huru kwani amekuwa chini ya kiapo tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa na hivyo kukosa amani na uhuru.
Utakuwaje huru wakati unapingana na nafsi yako? Haya ni mazingaombwe kwani wameona CCM na serikali yake wameumbuliwa vya kutosha na kutafuta sababu ya kutokea.
__________________
Dua la kuku halimpati mwewe
Reply With Quote
  #3  
Old 15th December 2007, 08:33 PM
Bubu Ataka Kusema's Avatar
Bubu Ataka Kusema Bubu Ataka Kusema is offline
Bubu Ataka Kusema says life is GOOD!
JF Premium Member
Points: 12,700,657, Level: 100 Points: 12,700,657, Level: 100 Points: 12,700,657, Level: 100
Activity: 56% Activity: 56% Activity: 56%
 
Join Date: Sun Feb 2007
Location: Mfaranyaki
Posts: 12,678
Thanks: 1,034
Thanked 1,199 Times in 697 Posts
Rep Power: 2049
Bubu Ataka Kusema is one of most respected JF members!Bubu Ataka Kusema is one of most respected JF members!Bubu Ataka Kusema is one of most respected JF members!Bubu Ataka Kusema is one of most respected JF members!Bubu Ataka Kusema is one of most respected JF members!Bubu Ataka Kusema is one of most respected JF members!Bubu Ataka Kusema is one of most respected JF members!Bubu Ataka Kusema is one of most respected JF members!Bubu Ataka Kusema is one of most respected JF members!Bubu Ataka Kusema is one of most respected JF members!Bubu Ataka Kusema is one of most respected JF members!
Default Re: Ukistaajabu ya Mussa...

Upande wa walalamikaji ukishindwa kuleta vielelezo vya ushahidi basi kesi ifutwe maana hawana ushahidi wa kutosha. Sasa wanarudi kazini kwa msemo wao wenyewe 'kwenda kujipanga upya' ili itakapoanza kusikilizwa tena warudi na ushahidi wa kupikwa!
__________________
~*~Life is Good~*~
Reply With Quote
  #4  
Old 15th December 2007, 08:45 PM
Jasusi Jasusi is online now
Jasusi is a truth seeker
JF Premium Member
Points: 279,130, Level: 100 Points: 279,130, Level: 100 Points: 279,130, Level: 100
Activity: 18% Activity: 18% Activity: 18%
 
Join Date: Fri May 2006
Posts: 4,185
Thanks: 1,137
Thanked 617 Times in 312 Posts
Rep Power: 32
Jasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enough
Default Re: Ukistaajabu ya Mussa...

Mi nadhani kesi ilishaisha. Yaani mpaka mlalamikaji anakiri kuwa sasa atapata uhuru wa kupumua. Makubwa kweli kweli.
Reply With Quote
  #5  
Old 15th December 2007, 09:04 PM
Mugo"The Great" Mugo"The Great" is offline
Mugo"The Great" has no status.
JF Premium Member
Points: 85,690, Level: 100 Points: 85,690, Level: 100 Points: 85,690, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Sun Oct 2007
Posts: 223
Thanks: 0
Thanked 7 Times in 5 Posts
Rep Power: 23
Mugo"The Great" will become famous soon enoughMugo"The Great" will become famous soon enoughMugo"The Great" will become famous soon enoughMugo"The Great" will become famous soon enoughMugo"The Great" will become famous soon enoughMugo"The Great" will become famous soon enoughMugo"The Great" will become famous soon enoughMugo"The Great" will become famous soon enough
Default Re: Ukistaajabu ya Mussa...

Ama kweli demokrasia yetu iko taabani na ndiyo maana mtindo wa kuweka "VIRAKA" kwenye katiba haufai. Tunataka katiba mpya yenye kutoa "HAKI SAWA" kwa watanzania wote. Inakuwaje "SIRIKALI" kupanga muda wa kesi? Wataalamu wa Sheria tunaomba ufafanuzi hapa.
__________________
Man can believe the impossible, but man can never believe the improbable -Oscar Wilde
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
mussa, ukistaajabu


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007 MwanaCCM Jukwaa la Siasa 313 29th October 2007 10:50 AM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 07:45 AM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com