JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini!

  Report Post
  Page 41 of 45 FirstFirst ... 313940414243 ... LastLast
  Results 801 to 820 of 898
  1. Ibambasi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th July 2007
   Location : Ipandikilo
   Posts : 1,390
   Rep Power : 993
   Likes Received
   378
   Likes Given
   2765

   Default Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini!

   Kwa kuwa Katiba ya Tanzania ya 1977 inaniruhusu kutoa maoni yangu alimradi sifunji sheria, na kwa kuwa slogan/motto/kaulimbiu ya JF ni "where we dare to talk openly" basi napenda kusema haya yafuatayo.

   Nimekuwa nafuatilia kwa kina mjadala wa Mahakama ya Kadhi na mambo ya udini kwa ujumla katika nchi yetu. Wengi wanadai kuwa Tanzania ni secular state, haina dini. Pia kuwa haipaswi kuchanganya dini na siasa katika utawala wa nchi kwani madhara yake yanafahamika. Sawa, haya ni maoni na hoja za watu mbalimbali. Lakini mimi nataka kujua swala moja, wanasema Tanzania haina dini, je ni kwa nini katika orodha ya sikukuu zinazotambuliwa rasmi kiserikali kuna Idd, Krismas, Pasaka, etc? Hizi ninvyojua ni sherehe za zile dini zinazoitwa za "kweli",i.e Uislamu na Ukristo.

   Na pia katika sherehe hizi viongozi wa kitaifa hualikwa na kuhutubia as if wako katika shughuli za kitaifa.Sasa inakuwa Serikali ya Tanzania haiizitambui sherehe kama Diwali za wahindu au zile zetu sisi tunaoitwa "wapagani"? Ni lini na ni wapi Serikali yetu hii imewahi kuingilia kati udhalilishaji wa dini yetu "wapagani" ambao kila siku tunatukanwa kuwa tunaabudu mashetani na hao wakrosto na waislamu? Kuna mhubiri mmoja wa Kiislamu aliwahi kushtakiwa Mahakama Kuu aliposema Yesu si Mungu, na likawa zogo la kitaifa lakini sijawahi kusikia serikali hii hii imeingilia kati kuhusu udhalilishaji wa wazi wa imani zetu za jadi na hao watu wa dini za "kweli"

   Pili viongozi wa kitaifa wanapowaita viongozi wa "dini" sijawahi kuona Mwanamalundi au Nyunguyamawe wakiwa pale Ikulu na ngozi na manyoya yao na singa zao mikononi zaidi ya kina Askofu fulani na Shehe fulani. Hii inaashiria nini kwa wale wanaodai kuwa Tanzania haina udini? Ina maana kina Mngungwa mwa Mnyenyelwa sio viongozi wa "dini"?

   Tatu katika "documents" zote za Kiserikali zinazohitaji sahihi au uthibitisho toka kwa viongozi wa dini sijawahi kuona cheo cha "mfumu" zaidi ya "padre", "imamu/sheikh", "mchungaji", na maneno kama hayo (rejea fomu za kuomba mikopo bodi ya elimu ya juu). Sasa kwa mtu kama mimi ninyeambiwa naabudu "mashetani" wapi serikali inanitambua katika hizo documents zake?

   Nne katika mijadala yote na makongamano ya kitaifa yanayohusisha viongozi wa dini nai lini kina sie tuliwahi kufuatwa na kuitwa?Je kina Pengo watakubali kukaa meza moja na sisi tunaoabudu "mizimu" ili tujadiliane masuala ya Taifa letu?Inavyoonekana ukiongelea dini hapa Tanzania unamaanisha Uislamu na Ukristo.Hata huu mjadala wa Mahakam ya kadhi wahusika wakuu wa malumbano ni hao hao.Sisi tukiamka kuchangia tuaambiwa "wapagani" na waabudu "mizimu" na "uchawi" hivyo hatuna "locus standi" ya kuongea!!

   Ukweli ni kuwa Tanzania ni nchi ya dini "kuu" mbili,Uislamu na Ukristo,ndo maana hata katika kufanya maamuzi mengi ya kitaifa wataitwa mashehe na mapadre/wachungaji kuwakilisha upande wa kidini.Waislamu na wakristo wamefaidi rasilmali nyingit tu za nchi hii at the expense ya watu wa dini nyingine(mf. majengo ya TANESCO Morogoro kutumika kwa ajili ya chuo kikuu cha kiislamu).Najua baadhi yenu humu mtaudhika na ukweli huu,kuwa nina "pepo" na kuwa "nishindwe na nilegee"!!!

   Yapo mengi tu ya kuweza kuthibitisha kuwa nchi hii ni ya kidini na hizo dini zinafahamika.

   Hivyo for any critical observer (ambaye ataweka upenzi wa kidini pembeni,Koba you get me?) ataniunga mkono kuhusu issue hii unless aamue kufumba macho na kuita nyekundu kuwa nyeupe iliyopitiliza rangi!!!

   NB:Kinachonisikitisha zaidi hizi dini "kuu" 2 ni za nje,sio zetu waafrika na zimetumika katika maouvu yote ambayo historia ya dunia hii imeshuhudia:utumwa,ukoloni,ube pari,ukandamizaji,mauaji (kama ya wale wahindi wekundu kule Amerika ya kusini yaliyofanywa na wamisionari wa kikatoliki wa kireno), vita vya kidini (crusades),n.k...

   Tulimkosea nini Mungu sisi watu weusi?
   Mkandara, Pasco, Jackbauer and 6 others like this.

  2. Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 26,980
   Rep Power : 17073751
   Likes Received
   13805
   Likes Given
   2623

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By Josephine View Post
   Nimekuwa nikifuatilia mijadala mingi na wengi wameami ni kweli swala la udini limegeuka kuwa sera.
   Swala la dini, haliwezi kuwa sera ya siasa katika nchi ambayo kikatiba haina dini.Mwalimu Nyerere, pamoja na mapungufu yake mengi, alijitahidi kulieleza hili kwa urefu katika hotuba zake nyingi.

   Kwa hiyo swala la dini linakuwa sera ya siasa katika nchi yetu tunaposema kwamba nchi yetu haina dini, na udini ni kitu cha kupigwa vita. Kwa sababu serikali yetu haina dini, sera ya Tanzania

   Kuhusiana na dini haipo zaidi ya kusema "serikali haina dini. Kwa hiyo kama unaongelea wanaopinga udini ukasema wanafanya udini kuwa sera, utakuwa umeacha kuangalia kwamba kupinga udini ni sera ya uongozi nchini mwetu tangu uhuru.
   Nikiimaanisha sera nikitu ambacho kinatekelezeka na mwishoni tumeona swala nyeti la Taifa letu Tume ya Taifa ikilaumiwa kusheheni watu wa dhehebu moja.
   Hatujawahi kuwa na "quotas" za uongozi kwa mujibu wa dini au ukabila. Unaweza kuwa na tume iliyojaa waislam au wakristo walio secular. Muungano wetu umekaa katika nature ya kwamba kitu chochote kitakachotakiwa kuwa na sura ya muungano, kwa maana ya kushabihi watu wa bara na visiwani kwa nusu-nusu, kinawezekana kubeba waislam wengi kwa maana idadi ya waislam na wakristo kwa bara karibu inafanana, na ile ya Zanzibar ni karibu 100% waislam.

   Mie ningependa kuona malalamiko yanayojikita katika vitendo vya watu, na sio dini zao.

   Mimi kwa upande wangu nimekuwa nikifuatilia uteuzi wa viongozi katika nyanja mbalimbali na kugundua mambo flani.Ambayo leo naomba nisiyaweke hadharani.

   Haya ni mawazo yangu na utafiti wangu na nimeleta hapa kupata mawazo yenu, naomba nisihukumiwe kwakuwa inawezekana nikawa nimekosea.

   Leo tunasehemu au pande mbili za viongozi:

   1. Viongozi wanaomtumikia Mungu katika haki na kweli - (wale wanaomuamini Mungu na wala njia zao hazimuhusishi shetani)
   2. Viongozi wanaomtumikia Shetani na ufalme wake - (wale ambao njia zao zote zinategemea ufalme wa giza)
   Ukielewa kuwa dini si sera ya kisiasa, huwezi kuhusisha imani ya mungu na uongozi.Hii ni simplification kubwa kwa sababu suala la uongozi lina mengine mengi ambayo hayahusishi imani ya dini moja kwa moja, mambo kama elimu, uadilifu (mtu anaweza kuwa muadilifu bila ya imani ya dini, na anaweza kuwa na imani ya dini asiwe muadilifu) utawala wa sheria (sehemu ambayo kuna sheria lakini haitumiki viongozi wanaweza kukosa sababu ya kuwa waadilifu) etc

   Kuhusisha moja kwa moja imani ya mungu na uongozi bora, vitu ambavyo havina uhusiano wa moja kwa moja ni makosa. Kwa sababu unavyomuelewa mungu wewe ni tofauti na anavyomuelewa mwingine. Mungu huyo huyo unayesema anawafanya viongozi waongoze kwa haki anaweza kuwapa viongozi wengine kisingizio cha kufanya mabaya yao.

   Si jambo geni kwetu hapa jamvini kusikia vitu hivi juu ya viongozi wetu,kwakua twazijua nyendo zao.

   Cha msingi hapa ningependa tujadili, je swala la udini lipo?
   Udini upo, rejea hotuba za Nyerere alivyokemea udini.
   Au ni swala la umoja katika ufalme wa giza kwani mwisho wa utekelezaji unakuwa wa yule wanae mwamini na kumuabudu.
   Ukishaongelea habari za "ufalme wa giza" umeshaingiza dini.
   Tumesikia habari za freemason, uganga hadi kwenye kumbi za bunge nk. lakini pia tuchukue nafasi hii kuwajadili na kuzitazama mienendo ya maofisa wote katika ngazi za juu maeneno mbalimbali misimamo na mienendo yao ikoje.
   Tuwachunguze mienendo yao katika context gani? Mie sina haja ya kujua kiongozi wangu anaabudu vipi, au hata kama haabudu. Hii ndiyo maana ya secularism ambayo nchi yetu inafuata. Nyerere - kwa mujibu wake mwenyewe- alishindwa kujua idadi ya mawaziri wake Wakatoliki alipotaka kujibu swali la anao wangapi, kwa sababu serikali ilikuwa hairekodi dini zao.

   Kama una kiongozi kaua, huyo ni muuaji, lete habari za muuaji tuzijadili. Hayo mengine Freemason sijui anakwenda kwa babu Bagamoyo si ya msingi. Wengine hatuoni tofauti kati ya anayekwenda Mlingotini Bagamoyo na anayekwenda Azania Front kanisani, zote ni nyumba za imani tu.
   Nasema hili kwa kuwa kama unamuamini Mungu ndani ya moyo wako utajawa utukufu wa Mungu na si hila za shetani, vinginevyo utakuwa mawindo.
   Wengine hatuamini kwamba kuna Mungu wala shetani. Mungu na shetani ni wewe mwenyewe mwanadamu kutegemea na matendo yako. Sasa ukiongea sana habari za Mungu na shetani katika siasa tunaweza kukuona huna sera unaishia kwenye propaganda za dini. Unaleta udini.Unawabagua secular humanists na watu wasioamini katika dini/Mungu.

   Na kama ndani ya moyo wako umejaa hila za ibilisi, mawazo yako yatatawaliwa na mienendo ya kuzimu.
   Ibilisi ni nani? Kuzimu ni wapi? Hapa hoja yako ni nini? Uongozi wa siasa au mwenendo wa watu kidini? Nikikwambia hao Freemasons unaowasema wanamuamini shetani wanamuamini "mungu" zaidi ya baadhi ya wakristo na waislam unaweza kubisha?
   tunapofikiria kupambana ili tushinde na kuwa na Taifa huru,
   Nikukumbushe kwamba taifa huru ni lile lenye kutoa uhuru wa ibada, uhuru wa kuabudu au kutoabudu, uhuru wa kuwa na dini au kutokuwa na dini, uhuru wa kuamini mungu au kutoamini mungu. Ukiwabagua secular people wasioamini mungu una violate principle za taifa huru.
   yatupasa kuangalia nyanja zote za Kiroho na Kimwili.
   Kiroho unaenda kuangalia kanisani/ msikitini. Nchi yetu ni secular na haitoi nafasi ya kujadili mambo ya kiroho katika siasa, unless unaongelea kwamba nchi yetu haina dini na unakemea udini. Yesu / nabii Issa mwenyewe alisema mpeni mungu ya mungu, na Kaisari ya Kaisari. Kwa nini unataka kuchanganya?
   Vinginevyo mafanikio yetu hayatafikia pale tunapotaka kwa kipo kitu kitashindikana.
   Pia hatuwezi kufanikiwa kwa kuchanganya dini na siasa.
   Pia yatupasa kumjua adui yetu ili kujipanga vema. Adui yetu ni Roho ya udini, mtu binafsi anayeeneza udini, au ni Ufalme wa giza unaotaka kuimarisha misingi yake duniani?
   Ukishaongelea habari za "mungu", "roho ya giza" ukawasema vibaya Freemasons bila hata kutujuza sababu, tayari unakuwa ushaleta udini.

   Inabidi ueleze mambo kwa lugha iliyo clear na secular ili kutatua tatizo la kimwili. Kama unataka kutoa suluhisho la tatizo la kiroho, hilo ni suala jengine.
   Invisible, Paul S.S and OLESAIDIMU like this.
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..

  3. Kongosho's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st March 2011
   Location : Location loading...
   Posts : 36,102
   Rep Power : 138795812
   Likes Received
   23217
   Likes Given
   23195

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Dini na Siasa? Tukivichanganya tu hapa basi.

   tanzania kila mtu ana uhuru wa kuabudu anachotaka ili mradi asivunje sheria za nchi
   Ndio maana kuna watu hata viapo wanatumia katiba kuonesha wanaapa kufuata taratibu halali za nchi.

   Hii ya kuabudu iachwe kwa watu na sio taifa.

   Labda sijaelewa ulichotaka kusema, itawekwaje kwenye katiba hii?
   Kwamba kiongozi lazima awe anamwamini Mungu? au awe wa dini gani? au mgawanyo wa dini bara na visiwani?

   Kweli sijakupata.
   Last edited by Kongosho; 16th April 2012 at 17:42.
   Dont study me, you won't graduate!!!

  4. jmushi1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2007
   Posts : 15,990
   Rep Power : 32245451
   Likes Received
   5342
   Likes Given
   6370

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By Kiranga
   Swala la dini, haliwezi kuwa sera ya siasa katika nchi ambayo kikatiba haina dini.Mwalimu Nyerere, pamoja na mapungufu yake mengi, alijitahidi kulieleza hili kwa urefu katika hotuba zake nyingi.

   Kwa hiyo swala la dini linakuwa sera ya siasa katika nchi yetu tunaposema kwamba nchi yetu haina dini, na udini ni kitu cha kupigwa vita. Kwa sababu serikali yetu haina dini, sera ya Tanzania kuhusiana na dini haipo zaidi ya kusema "serikali haina dini. Kwa hiyo kama unaongelea wanaopinga udini ukasema wanafanya udini kuwa sera, utakuwa umeacha kuangalia kwamba kupinga udini ni sera ya uongozi nchini mwetu tangu uhuru.
   Mkuu, swala la dini pengine linaweza lisiwe sera kama unavyosema.

   Hata hivyo matokeo mengi ya hizo "sera" yanaweza kuwa yana implications za kidini.

   So unaweza kuona it can be a hidden agenda within the so called "policies"

   Pia nilishawahi kusema the same thing, kwamba udini upo na ulikuwepo.

   Jitihada za mwalimu hazikuwa kuuzia, bali kuukemea na kuutokomeza.
   "One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato

  5. Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 26,980
   Rep Power : 17073751
   Likes Received
   13805
   Likes Given
   2623

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By jmushi1 View Post

   Kimsingi unasema, hata kama dini si sera, unaweza kuwa na sera inayotumika kidini.

   Hapo tatizo lako si udini, ni sera mbovu zinazoweza kutumika kidini. Ni kweli kwamba udini huu unatokana na hizi sera kama vile ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini ulivyoweza kuendelezwa kwa kutumia apartheid, lakini kama unataka mabadiliko ya msingi, kama unataka kuondoa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini, huanzi kuwaambia watu wapendane kabla hujabadili mfumo na kuondoa institutional apartheid. Ndiyo maana mie naona kama kuna sera mbaya zinazochochea udini zitajwe, tuzimulike hapa.

   Sera hizo ni zipi hasa?

   Maana kama nilivyosema hapo juu, mnaweza kuona sehemu kuna udini, kumbe nature ya muungano imekaa kufanya kuwe na muonekano wa udini.
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..

  6. jmushi1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2007
   Posts : 15,990
   Rep Power : 32245451
   Likes Received
   5342
   Likes Given
   6370

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By Kiranga View Post
   Sera hizo ni zipi hasa?

   Maana kama nilivyosema hapo juu, mnaweza kuona sehemu kuna udini, kumbe nature ya muungano imekaa kufanya kuwe na muonekano wa udini.
   Mkuu kuna sera zisizo rasmi, na zile ambazo ni rasmi.

   Kuhusu hilo la muungano kuwa na "muonekano wa udini" unaotokana na "nature" yake, je huo muungano haukuwa created na watu?Na unaposema "nature yake" utawaelewesha wananchi kivipi kwamba hiyo nature haijatokana na creation ya muungano huo?

   Tumeona wananchi wamekuwa na tabia ya kupenda usawa, na hivyo kuwepo na malalamiko ya udini ie "mfumo kristo" nk.

   Kwahiyo unaweza kuona kuwa ili vyama vya siasa vipate wafuasi, lazima vinakuwa na sera ambazo mimi naziita siyo rasmi, ie kuhakikisha kile wanachokiita "uwiano" nk
   "One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato

  7. Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 26,980
   Rep Power : 17073751
   Likes Received
   13805
   Likes Given
   2623

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By jmushi1 View Post
   Mkuu kuna sera zisizo rasmi, na zile ambazo ni rasmi.
   Hizo sera zisizo rasmi ni u-Makaveli huo. Ukishasema sera maana yake ni rasmi.

   Kuhusu hilo la muungano kuwa na "muonekano wa udini" unaotokana na "nature" yake, je huo muungano haukuwa created na watu?
   Muungano umeundwa na watu.

   Na unaposema "nature yake" utawaelewesha wananchi kivipi kwamba hiyo nature haijatokana na creation ya muungano huo?
   Nature hii ni sehemu ya historia ya Zanzibar iliyokuwapo miaka takriban elfu kabla ya muungano, kwamba Zanzibar kwa kuwa kisiwa kilichotembelewa na waarabu mapema kabisa, kikaota mizizi ya uislam mapema kabisa, basi upande huo wa muungano kuwa na uislamu takriban 100% is a historical fact. Huwezi kusema muungano ndio uliofanya Zanzibar iwe na waislam karibu 100%

   Tumeona wananchi wamekuwa na tabia ya kupenda usawa, na hivyo kuwepo na malalamiko ya udini ie "mfumo kristo" nk.
   Watu wanaweza kulalamikia "mfumo kristo" kwa sababu tu wasomi wa kwanza wa elimu ya magharibi walikuwa watu waliosomea seminari ambao ilikuwa likely kuwa wakristo zaidi.

   Wengine wanaweza kulalamika kwamba tume ya katiba mpya imejaa waislam simply because tume ina waislam na wakristo kutoka bara, halafu wawakilishi wote wa Zanzibar ni waislam kwa ku reflect population ya Zanzibar.

   Kwa hiyo waislam wataona wanaonewa (hawapati nafasi za elimu ya juu) na wakristo wataona wanaonewa (hawajapewa nafasi za kutosha katika tume ya katiba) kumbe hamna lolote.

   The grass is always greener on the other side.

   Kwahiyo unaweza kuona kuwa ili vyama vya siasa vipate wafuasi, lazima vinakuwa na sera ambazo mimi naziita siyo rasmi, ie kuhakikisha kile wanachokiita "uwiano" nk
   Hizo sera zisizo rasmi ndizo zitaviua vyama hivi. Ukishaanza kuendesha chombo rasmi kwa sera zisizo rasmi huwezi kupata mpaka wa kuacha kutumia sera zisizo rasmi. Utakiuka "rule of law" mpaka kufanya akaunti ya chama kuwa akaunti yako binafsi, kwa kisingizio cha "sera isiyo rasmi".

   Ukishasema "sera" maana yake ni rasmi. Sera isiyo rasmi is an oxymoron. Katika matumizi ya kawaida, sera isiyo rasmi ina connotation ya kitu kibaya kinachofanywa lakini hakiwezi kuwa declared wazi.

   Kwa mfano mtu anaweza kusema "CHADEMA ina sera isiyo rasmi ya undugunaizesheni". Kwa sababu kama sera ni nzuri na si ya kuionea aibu, kwa nini usiifanye rasmi?
   mpayukaji likes this.
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..

  8. jmushi1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2007
   Posts : 15,990
   Rep Power : 32245451
   Likes Received
   5342
   Likes Given
   6370

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By Kiranga View Post
   Hizo sera zisizo rasmi ni u-Makaveli huo. Ukishasema sera maana yake ni rasmi.   Muungano umeundwa na watu.   Nature hii ni sehemu ya historia ya Zanzibar iliyokuwapo miaka takriban elfu kabla ya muungano, kwamba Zanzibar kwa kuwa kisiwa kilichotembelewa na waarabu mapema kabisa, kikaota mizizi ya uislam mapema kabisa, basi upande huo wa muungano kuwa na uislamu takriban 100% is a historical fact. Huwezi kusema muungano ndio uliofanya Zanzibar iwe na waislam karibu 100%   Watu wanaweza kulalamikia "mfumo kristo" kwa sababu tu wasomi wa kwanza wa elimu ya magharibi walikuwa watu waliosomea seminari ambao ilikuwa likely kuwa wakristo zaidi.

   Wengine wanaweza kulalamika kwamba tume ya katiba mpya imejaa waislam simply because tume ina waislam na wakristo kutoka bara, halafu wawakilishi wote wa Zanzibar ni waislam kwa ku reflect population ya Zanzibar.

   Kwa hiyo waislam wataona wanaonewa (hawapati nafasi za elimu ya juu) na wakristo wataona wanaonewa (hawajapewa nafasi za kutosha katika tume ya katiba) kumbe hamna lolote.

   The grass is always greener on the other side.   Hizo sera zisizo rasmi ndizo zitaviua vyama hivi. Ukishaanza kuendesha chombo rasmi kwa sera zisizo rasmi huwezi kupata mpaka wa kuacha kutumia sera zisizo rasmi. Utakiuka "rule of law" mpaka kufanya akaunti ya chama kuwa akaunti yako binafsi, kwa kisingizio cha "sera isiyo rasmi".

   Ukishasema "sera" maana yake ni rasmi. Sera isiyo rasmi is an oxymoron. Katika matumizi ya kawaida, sera isiyo rasmi ina connotation ya kitu kibaya kinachofanywa lakini hakiwezi kuwa declared wazi.

   Kwa mfano mtu anaweza kusema "CHADEMA ina sera isiyo rasmi ya undugunaizesheni". Kwa sababu kama sera ni nzuri na si ya kuionea aibu, kwa nini usiifanye rasmi?
   Kama watu wameunda muungano, na huo muungano una nature ya udini matatizo siyo ya watu?Tulia tafakari.

   Unajicontradict na maneno yako mwenyewe.
   "One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato

  9. TIMING's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th April 2008
   Location : Roaming...
   Posts : 21,702
   Rep Power : 922984
   Likes Received
   6972
   Likes Given
   8076

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   HUWEZI KUTENGANISHA DINI NA SIASA

   Siasa inaenda kwenye utawala, utii na uaminifu, na dini inahubiri busara, utii na uaminifu!!

   Dini zilienea na zinaenea kisiasa na siasa zinaenezwa kwa kutumia misingi iliyozipa nguvu dini

   it is complicated!! what we dont want ni chuki za dini kutumika kisiasa au chuki za kisiasa kutumika kidini (kitu ambacho kwa sasa kinashika kasi ya ajabu)
   ....Time is the wisest counselor !!!

  10. Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 26,980
   Rep Power : 17073751
   Likes Received
   13805
   Likes Given
   2623

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By jmushi1 View Post
   Kama watu wameunda muungano, na huo muungano una nature ya udini matatizo siyo ya watu?Tulia tafakari.

   Unajicontradict na maneno yako mwenyewe.
   For the umpteenth time.

   Watu wameunda muungano, muungano inherently una potentialities za kutoa muonekano wa udini kwa sababu Zanzibar ni karibu 100% waislam.

   Hii habari ya Zanzibar kuwa 100% waislam ilikuwepo mamia ya miaka kabla ya muungano, kwa hiyo huwezi kulaumu muungano kwamba unafanya mambo yanayojipa unusunusu kati ya bara na visiwani yakitokea kuwa na waislam wengi kwa sababu Zanzibar is disproportionately Muslim. Kwa hiyo hata kama bara tuko 50% Christian na 50% Muslim, na Zanzibar iko 1005 Muslim, hiyo nusu ya Zanzibar tu itafanya muonekano wa tume uwe 50% Muslim, ukija kuweka na hiyo 50% of the remaining 50% utakuta nchi iko 50/50 kati ya Waislam na Wakristo, lakini tume imekuwa 75/ 25 favoring Muslims.

   Hapa huna tatizo la udini. Tatizo lako ni nature ya muungano iko dilapidated kiasi cha watu wachache wa Zanzibar wanakuwa disproportionately represented kwa sababu za kihistoria.

   Kama wewe ni mdini unaweza kuona udini hapo.

   Lakini kama una macho ya kutazama zaidi ya udini utaweza kuona mambo mengine mengi tu ambayo hayana udini. Unaweza kuja na wabara/ wapwani. Unaweza kuja na kusema kwamba muungano hauna equal representation etc.

   Hiyo contradiction uliyoiona haipo kwa sababu umeibase kwenye assumption ambayo mie sijaisema. Muungano hauna nature ya udini, muungano una nature ya kutokuwa na equal representation.Hiyo appearance ya udini si tatizo hasa, hilo ni tip of the iceberg tu. Na always kinachozamisha meli si tip of the iceberg , ni lile lililo chini ya maji. huu muonekano wa udini ni dalili ya ugonjwa, ugonjwa wenyewe ni muungano hauko representative.

   Kwa hiyo kuna matatizo ya watu in so far as wameunda muungano ambao unavipa visiwa vyenye watu na rasilimali zisizozidi za wilaya ya Kahama nguvu ya nusu ya watu milioni arobaini.
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..

  11. Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 26,980
   Rep Power : 17073751
   Likes Received
   13805
   Likes Given
   2623

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By TIMING View Post
   HUWEZI KUTENGANISHA DINI NA SIASA

   Siasa inaenda kwenye utawala, utii na uaminifu, na dini inahubiri busara, utii na uaminifu!!

   Dini zilienea na zinaenea kisiasa na siasa zinaenezwa kwa kutumia misingi iliyozipa nguvu dini

   it is complicated!! what we dont want ni chuki za dini kutumika kisiasa au chuki za kisiasa kutumika kidini (kitu ambacho kwa sasa kinashika kasi ya ajabu)
   Wapi unatoa hii habari ya siasa ni utii na uadilifu? Ushawahi kuona tirades za Tea Party? Zina utii na uadilifu zile? Siasa zinazotaka uwajibikaji kwa kila mtu nazo zinataka utii?
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..

  12. Gaijin's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st August 2007
   Posts : 11,898
   Rep Power : 24987
   Likes Received
   5095
   Likes Given
   2566

   Default

   Quote By Josephine View Post

   Cha msingi hapa ningependa tujadili, je swala la udini lipo? Au ni swala la umoja katika ufalme wa giza kwani mwisho wa utekelezaji unakuwa wa yule wanae mwamini na kumubudu

   .............

   Pia yatupasa kumjua adui yetu ili kujipanga vema. Adui yetu ni Roho ya udini, mtu binafsi anayeeneza udini, au ni Ufalme wa giza unaotaka kuimarisha misingi yake duniani?
   Yaani unachotaka tujadili ni uwepo wa ufalme wa giza kwenye mienendo y viongozi wetu wa kisiasa?!

   Ufalme wa giza ndio dubwashka gani hasa?

   Kinsingi ni kuwa katiba ya nchi haitambui kitu kinachoitwa ufalme wa giza. Pia katiba hiyo hiyo haibagui watu katika makundi ya kiimani na ufuasi, iwe wa giza au wa nuru

   Hayo mahitimisho aina ya "Ufalme wa giza unaotaka kuimarisha misingi yake duniani?" yakajadiliwe misikitini.
   TIMING likes this.

  13. Mkandara's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd March 2006
   Location : T dot
   Posts : 15,848
   Rep Power : 124739373
   Likes Received
   7421
   Likes Given
   7106

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Unapotaka kuutazama Udini nadhani ni muhimu sana tuutazame hata Ukabila na jinsi gani tumeweza kuudhibiti hadi sasa. Japokuwa katiba yetu inasema wazi kwamba nchi yetu haina dini isipokuwa watu wake, maneno haya hayana tofauti na kusema pia kwamba nchi yetu haina Kabila isipokuwa kila watu wake ndio wenye makabila..Sasa iweje leo tunazungumzia sdana Udini iwapo Ukabila tumeweza kuudhibiti kwa kiasi kikubwa..

   Ukabila bado kabisa haujapewa nafasi kubwa ktk kutuvuruga wananchi lakini Udini umeweza kupenyeza ktk siasa na maisha ya Watanzania hivyo kipimo cha UTU wetu kimeanza kuwa na vigezo tofauti kinyume kabisa na vile vya UTU. Na ndo maana hata katiba hiii huwasikii wasukuma wakisema mbona hakuhna msukuma ktk tume wakati kabia letu ndilo kubwa kuliko yote nchini, huwasikii Wanyamwezi na wengineo wakitumia makabila yao kudai uuwioano ktk ujenzi wa Katiba. Lakini tumona madai ya Udini na Uzanzibar. Bara kwa sababu kuna tatizo ktk maswala haya mawili.. DINI na UTAIFA wa Zanzibar maana watu wanaichukulia Bara kama ni serikali wakati sio..hakuna nchi inayoitwa tanzania Bara hivyo sisi tunataka uuwiano upi ikiwa hakuna nchi inayoitwa bara!.

   Japokuwa Azimio Jipya anasema kwamba yeye anaamini UTU lakini tatizo ni kwamba huo UTU haujengwi na mtu mmoja na ndio maana katiba ilisisitiza umuhimu wa sharti ya maneno yale ili kujenga UTU wetu kwa malengo ya kujenga Utaifa. Na siku zote ktk maisha ukiona mahala pana mzozo mkubwa baina ya watu ktk makundi yao ujue kuna TATIZO hapo la kiimani, roho zao zinawasuta na kujiona tofauti na mtu ama kundi jingine hivyo UTU unapotea maana UTU hauna matabaka ama haki na usawa kwa uuwiano bali haki na usawa wa sheria za mapokeo.

   Udini nchini upo, tena umepamba moto sana wala sii kwa viongozi bali kwa wananchi zaidi, na sasa umefikia mahala ambapo hata viongozi wetu wenyewe wanaogopa kuzungumzia maana kwanza atatazamwa dini yake na kile hatua ya uongozi wake utapimwa kwa dini yake ktk maamuzi yoyote yale. Toka nimejiunga JF nimekuwa nikipima sana mtazamo wa watu wengi na hasa mada zinazohusu imani hizi mbili za Kiislaam na Kikristu, pia nilipokuwa Tanzania nimejaribu sana kuwasoma watu wanavyotazama hizi imani zao za dini nikagundua kwamba ipo haja kubwa sana ya kupambana na adui huyu mkubwa ambaye anaingia kwa kasi ya ajabu.

   Na nimejaribu sana kuzisoma sababu zake, chanzo chake na kwa nini imefikia hali hii, nikagundua kwamba muafaka wa MoU ndio chachu iloshindikana kumezwa na Waislaam. Na nilijaribu zaidi kuelewa undani wa muafaka huu unawakwaza wapi zaidi na kwa nini unawakwaza hadi imefikia wao kuanza kuwashambulia wakristu na hata kusema kwamba nchi yetu imejengwa kwa mfumo Kristu. Na haya ndio niliyokusanya.

   1.Ushiriki wa serikali KISIRI ktk muafaka bila kuwahusisha wadau wengine.
   2. Kurudishiwa Makanisa shule na Hospital pasipo wadau wengine kurudishiwa zao isipokuwa wajenge mipya kama wanataka.
   3. Ruzuku na nafuu ya kodi inayopewa makanisa ambazo zimekuja gundulika ni billioni 90 kwa mwaka..
   4. Pamoja na nafuu hizo gharama za elimu na Afya ni kubwa wakati kazi ya kanisa ni kutoa huduma Bure kama lilivyoasisiwa.
   5. Shule za wengine (waislaam ) zinachukua failures wakati zile za kanisa zinachukua wanafunzi waliofanya vizuri japokuwa ni Private pia Hospital zao zinapewa madaktari wa serikali wakati zile za binafsi au waislaam wanajitegemea kuajiri na kulipa mishahara.

   Kuwepo kwa madai haya kumeonekana ni chuki ya Waislaam kwa Wakristu na toka hapo ilipotokea dini hizi mbili zimeendesha siasa mbaya za upinzani kiasi kwamba imefika hadi ktk siasa na utawala wa nchi yetu. Hapa hakuna tena UTU bali ni vita na siku zote malengo ya vita hayatazami nani mwenye haki bali atakuwa mshindi hivyo silaha zinazotumika ni kutafuta ushindi sio haki na UTU tena..Hii ni hatari sana kwa Taifa letu.

   Hayo wakuu zangu, ndio madai niliyoakusanya nilipokuwa Dar na niliyasoma na kufikiria kwamba kama hii ndivyo ilivyo na ndicho kinawakwaza basi ni bora tuuvunje muafaka huu na itafutwe mbinu nyingine ya kuendesha hizi shule na Hospital zetu. Kwa hiyo hapa tuna kazi kubwa sana ndugu zangu kuweza kupata suluhu ya jambo hili maana ndilo litakalo kuja ibomoa Tanzania japokuwa tumeweza sana kujilinda na Ukabila ambao kidogo sana umepenyeza ktk ajira na maswala madogo madogo ya kijamii ambayo siwezi sena ni Ukabila..

   Na tatizo kubwa la Udini wetu ni Umaskini, umaskini siku zote huzua inda, chuki, kikorosho na hata kuchaguana maana kiola mmoja wetu anahofia yeye kushuka kesho hivyo ili kuweka ulinzi ktk nafasi yake iwe kisiasa ama kikazi huchagua watu anaweza kuwaamini. Kama tungekuwa matajiri au Taifa tajiri wala swala hili lisingefika mbali lakini maadam ni maskini litakuja kula UTU wooote ulikwisha jengwa.

   Wakuu zangu nawaomba sana Great Thinker mnifahamu ya kwamba mimi huweka Ubishi sio lazima ndivyo nachoamini bali hutazama upande wa pili na kujenga changamoto ambazo mtu ama watu wengine wanavyo ama watakavyo itazama hoja nzima. Pia zipo mada ambazo nimechangia kwa mawazo yangu binafsi kama mimi pale napozungumza mtazamo wangu. Hivyo ndivyo nilivyojifunza kujadili (debate) na kinachohesabika ni nguvu ya hoja ktk tafakari sanifu kifikra ambazo hujenga njia na mbinu nyingi tofauti ktk kutatia matatizo yetu. Najua wengi huwa hawanielewi ama kwa kutojua kujenga hoja ama kwa makusudi ya kutaka ubishani japokuwa ni mapenzi yangu kubishana Kimjadala.
   Exploration of reality

  14. TIMING's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th April 2008
   Location : Roaming...
   Posts : 21,702
   Rep Power : 922984
   Likes Received
   6972
   Likes Given
   8076

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By Kiranga View Post
   Wapi unatoa hii habari ya siasa ni utii na uadilifu? Ushawahi kuona tirades za Tea Party? Zina utii na uadilifu zile? Siasa zinazotaka uwajibikaji kwa kila mtu nazo zinataka utii?
   Mkuu kama nimesoma michango na mleta mada vizuri, then its about kuaminishana kuliko facts, na nilichoweka ni context ileile ya kuaminishana, na ndicho kinachoendelea hata kwenye majukwaa

   tunaaminishwa tofauti kulingana na wakati fulani kunufaisha a few
   ....Time is the wisest counselor !!!

  15. jmushi1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2007
   Posts : 15,990
   Rep Power : 32245451
   Likes Received
   5342
   Likes Given
   6370

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By Kiranga
   For the umpteenth time.

   Watu wameunda muungano, muungano inherently una potentialities za kutoa muonekano wa udini kwa sababu Zanzibar ni karibu 100% waislam.
   Kwahiyo nothing should be done?

   Hii habari ya Zanzibar kuwa 100% waislam ilikuwepo mamia ya miaka kabla ya muungano, kwa hiyo huwezi kulaumu muungano kwamba unafanya mambo yanayojipa unusunusu kati ya bara na visiwani yakitokea kuwa na waislam wengi kwa sababu Zanzibar is disproportionately Muslim. Kwa hiyo hata kama bara tuko 50% Christian na 50% Muslim, na Zanzibar iko 1005 Muslim, hiyo nusu ya Zanzibar tu itafanya muonekano wa tume uwe 50% Muslim, ukija kuweka na hiyo 50% of the remaining 50% utakuta nchi iko 50/50 kati ya Waislam na Wakristo, lakini tume imekuwa 75/ 25 favoring Muslims.
   Hiyo ni demokrasia ya namba?Unajuwa demokrasia ya "electorate"?Numbers sometimes means nothing by themselves.Ndo maana unaona Bush alishinda uchaguzi licha ya kupata kura chache zaidi ya Gore.
   Before, nilishasema kama tunataka katiba ya muungano, ni lazima hilo liwe reflected.

   Kama wewe ni mdini unaweza kuona udini hapo.
   O!

   Lakini kama una macho ya kutazama zaidi ya udini utaweza kuona mambo mengine mengi tu ambayo hayana udini. Unaweza kuja na wabara/ wapwani. Unaweza kuja na kusema kwamba muungano hauna equal representation etc.
   Wewe ndo una macho ya kutazama "zaidi ya udini" ambayo yanakuonyesha kuwa wengine ni wadini?Kuna utofauti gani kati ya unavyoona wewe na vile ninavyoona mimi kuhusiana na udini na wadini?Wewe kuona mtu(mimi) ninaweza kuwa mdini kuna tofauti gani na mimi nilivyoona kuwa "watu ni wadini"?

   Hiyo contradiction uliyoiona haipo kwa sababu umeibase kwenye assumption ambayo mie sijaisema. .
   Hakuna contradiction, ni simple, kama muungano umekuwa created na watu, halafu una nature ya udini, basi inawezekana kabisa watu hao wakawa wadini.
   Invisible likes this.
   "One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato

  16. Azimio Jipya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th November 2007
   Location : Universal Space Station
   Posts : 3,359
   Rep Power : 5535
   Likes Received
   1051
   Likes Given
   1740

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By Mkandara View Post
   ... Japokuwa Azimio Jipya anasema kwamba yeye anaamini UTU lakini tatizo ni kwamba huo UTU haujengwi na mtu mmoja na ndio maana katiba ilisisitiza umuhimu wa sharti ya maneno yale ili kujenga UTU wetu kwa malengo ya kujenga Utaifa. Na siku zote ktk maisha ukiona mahala pana mzozo mkubwa baina ya watu ktk makundi yao ujue kuna TATIZO hapo la kiimani, roho zao zinawasuta na kujiona tofauti na mtu ama kundi jingine hivyo UTU unapotea maana UTU hauna matabaka ama haki na usawa kwa uuwiano bali haki na usawa wa sheria za mapokeo....

   Mkandara,

   Ni hakika siko peke yangu! Mbegu ya UTU ndio kwanza inachipua kwa jamii ya Kitanzania. Tafiti zote muhimu zinadhibitisha kuwa kuiotesha mbegu hii ndani ya jamii husika huhitaji si chini ya Mika 40 hadi 50 kabla ya kuanza kuonyesha matunda au machipukizi na yenyewe ikawa tayari kujaribiwa!

   Naomba unielewe kwani sitatumia dhana husika kuelezea hili ila nitatumia vielelezo ambavyo tayari viko na kuonekana lakini visivyoeleweka hadi vitakapotolewa maelezo na ufafanuzi.

   Founding principal ya Taifa la Tanzania is a driving and uniting force which can be called UTU if you wish! Kwa jamii kama hii hakuna namna nyingine ingeweza kufikia kuungana kamamilivyo kutoka ilivyokuwa kabla ya Uhuru. Driving and uniting Force The UTU ... kwa uanagalifu mkubwa ndio imetumika kuunganisha Makabila, matabaka mbalimbali, watu wa dini tofauti na tofauti nyingine mbalimbali ... na kuifanya Tanzania kuwa very unique Africa na Duniani.

   Kinachotokea sasa ni kuwa The Force ya UTU is just being tested! Ili wale waliokuwa wameibeba waitetee na kuipigania kwa vitendo sio kwa imani tena! Na ndicho kinachotokea ...chunguza utaona ...peoples power etc!!

   Lakini dhana nzima iko so deep in the Unconsciousness ya Kila Mtanzania aliyekuwa Kijana 40 t0 50 years ago ... na kikuweli unknowingly hawako radhi kuiona ikopotea kwani its the human nature itself!!

   Kwa sababu it was kind of the Idea ilikuwa imposed kwa imani bila kueelimishana na kuufikia muafaka wa kitaifa juu ya NGUVU YA UTU kuwa ndio inayolibeba Taifa ... Sasa itakuwa imekomaa na wananchi watakuwa tayari kuijadili of course with some little pain to pay and make it happen!!

   Kwa kuwa waliotangulia was good enough ... walitumia imani zaidi kuliko ...UNDERSTANDING TO IMPOSE IT DEEP IN ALL TANZANIAN MIND ...Utaona kuwa uhuru wa mwaka 1961 basically ulikuwa unamaanisha kuwa ni Uhuru wa UTU yaani ile katiba ya TANU NA KATIBA YA NCHI VILIJENGEKA TOKA KWENYE DHANA YA UTU WA TAIFA KAMA MSINGI WA TAIFA.

   Kufanya tukio ligande kwenye fahamu na fikra za jamii ... Mwenge ambao unachukua analogy ya UTU WA TAIFA historically ukAwashwa Juu ya mlima Kilimanjaro. Jambo hili sio rahisi kusaulika akilini mwa Jamii na hii ilikuwa na imapct kubwa sana psychologically. Tena juzi hapa wame activate and refresh... ingawa viongozi wa sasa wamepotoka na kwenda kinyume kabisa cha dhana ya tukio la msingi kuwashwa kwa mwenge ... lakini HIVYO ni VIZURI kwani watu makini eventually subconsciously watahoji ... Maana halisi will be brought to the surface ... reasonably and possibly under a hot discussion hiki tunachofanya hapa ni mwanzo tu au ... Chukulia kama sasa CHADEMA WAITEKE DHANA HII NA NGUVU YA UMMA iwe clearly define kama NGUVU YA UTU WA TAIFA JIPYA LA TANZANIA ... itaamsha all the barred Forces ... AND VIRTUES ZA UTU kama Upendo, amani, haki, heshima etc!! na angalia kwa karibu vuguvugu wanalokwenda nao ... They can accidentally trigger a huge changing force in subconscious of Tanzania and no one will stop the changes ..stay tuned!!

   Chukulia Dhana ya UTU kama msingi wa Taifa ielimishwe infact ni kuwa reactivated and rejuvenated ...(Iwe collied wisely na dhana ya peoples power ...)

   Yaani utu kwenye Kazi

   Utu kwenye siasa

   Utu kwenye uchumi

   Utu kwenye ulinzi

   Utu kwenye elimu

   Utu kwenye usatwi wa jamii

   Utu na maendeleo ..

   Kama alama ya mwenge wa uhuru inisimamia Dhana Ya UTU!! Then JWTZ watumie alama hiyo kwani wanalinda na kutetea UTU wa Watanzani kwenye mipika ya nchi ...

   Kama Mwenge wa uhuru unasimamia Dhana ya Utu Basi Polisi/Magereza waulinde utu wa jamii na watumie alama hiyo kama nembo yao.

   Kama mwenge wa uhuru unasimamia dhana ya Utu basi Nembo ya serekali iwe na alama hiyo kama alama ya Utu wa Taifa na ikibidi kila mkoa iwewepo kwa namna moja au nyingine...

   Kama mwenge wa uhuru unasimamia dhana ya Utu kwenye elimu basi alama hiyo iwe nembo ya shule kwenye Vyuo na shule mbalimbali

   Kama mwenge wa uhuru unasimamia dhana ya Utu na tunataka Uchumi unaosimamiwa na utu basi tuwe na azimio la utu lenye kuashiriwa na nembo hiyo kama lile la Arusha 1967.

   Nk ... Nk ...

   SWALI ... Hivi kwani sivyo ilivyo? ... TAFAKARI Bila kujali wewe ni chama gani, jinsia gani, kabila gani, dini gani, kanda gani, umri gani ... kwani huo ndiou Utanzania uio Utu wetu wa Taifa unaowakilishwa na alama ya Mwenge wa uhuru na sasa Mwenege unabidi ukimbizwe sio physically lakini Kielimu na kwa fikra kamili za Nguvu Ya UTU wa Taifa!!!!
   Mkandara and Axe like this.
   Never Get Angry; Never Make Threat; Reason With People;
   "Napenda the logic of the words because in some ways it says about individual-not to use emotions-when scrutinizing something, whether it involves you or not" ...-by AshaDiii @ Jamiiforums 26th July 2011.

  17. Azimio Jipya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th November 2007
   Location : Universal Space Station
   Posts : 3,359
   Rep Power : 5535
   Likes Received
   1051
   Likes Given
   1740

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By Mkandara View Post
   ..Na nimejaribu sana kuzisoma sababu zake, chanzo chake na kwa nini imefikia hali hii, nikagundua kwamba muafaka wa MoU ndio chachu iloshindikana kumezwa na Waislaam. Na nilijaribu zaidi kuelewa undani wa muafaka huu unawakwaza wapi zaidi na kwa nini unawakwaza hadi imefikia wao kuanza kuwashambulia wakristu na hata kusema kwamba nchi yetu imejengwa kwa mfumo Kristu. Na haya ndio niliyokusanya.

   1.Ushiriki wa serikali KISIRI ktk muafaka bila kuwahusisha wadau wengine.
   2. Kurudishiwa Makanisa shule na Hospital pasipo wadau wengine kurudishiwa zao isipokuwa wajenge mipya kama wanataka.
   3. Ruzuku na nafuu ya kodi inayopewa makanisa ambazo zimekuja gundulika ni billioni 90 kwa mwaka..
   4. Pamoja na nafuu hizo gharama za elimu na Afya ni kubwa wakati kazi ya kanisa ni kutoa huduma Bure kama lilivyoasisiwa.
   5. Shule za wengine (waislaam ) zinachukua failures wakati zile za kanisa zinachukua wanafunzi waliofanya vizuri japokuwa ni Private pia Hospital zao zinapewa madaktari wa serikali wakati zile za binafsi au waislaam wanajitegemea kuajiri na kulipa mishahara.

   Kuwepo kwa madai haya kumeonekana ni chuki ya Waislaam kwa Wakristu na toka hapo ilipotokea dini hizi mbili zimeendesha siasa mbaya za upinzani kiasi kwamba imefika hadi ktk siasa na utawala wa nchi yetu. Hapa hakuna tena UTU bali ni vita na siku zote malengo ya vita hayatazami nani mwenye haki bali atakuwa mshindi hivyo silaha zinazotumika ni kutafuta ushindi sio haki na UTU tena..Hii ni hatari sana kwa Taifa letu.

   Hayo wakuu zangu, ndio madai niliyoakusanya nilipokuwa Dar na niliyasoma na kufikiria kwamba kama hii ndivyo ilivyo na ndicho kinawakwaza basi ni bora tuuvunje muafaka huu na itafutwe mbinu nyingine ya kuendesha hizi shule na Hospital zetu. Kwa hiyo hapa tuna kazi kubwa sana ndugu zangu kuweza kupata suluhu ya jambo hili maana ndilo litakalo kuja ibomoa Tanzania japokuwa tumeweza sana kujilinda na Ukabila ambao kidogo sana umepenyeza ktk ajira na maswala madogo madogo ya kijamii ambayo siwezi sena ni Ukabila..

   Na tatizo kubwa la Udini wetu ni Umaskini, umaskini siku zote huzua inda, chuki, kikorosho na hata kuchaguana maana kiola mmoja wetu anahofia yeye kushuka kesho hivyo ili kuweka ulinzi ktk nafasi yake iwe kisiasa ama kikazi huchagua watu anaweza kuwaamini. Kama tungekuwa matajiri au Taifa tajiri wala swala hili lisingefika mbali lakini maadam ni maskini litakuja kula UTU wooote ulikwisha jengwa..
   Mkandara

   Haya uliyogelea hapa nafakiri ni ya muhumu. Ninaamni kuwa kwakeli ni changamoto katika kufufua na kulinda Utu wa Taifa usioegeemea dini, itikadi, ukanda, jinsia nk.

   Nafikiri hayana budi kutokea ili kutufikirisha na kutufanya kuchangia katika ujenzi wa Utanzania na Utaifa wetu!

   Hiki ni kipindi cha kutumia fikra, tafakari na makubaliano yanayohitaji upembuzi yakinifu ili kufikia maswala ya msingi kitaifa tofauti na hapo zamani yalikuwa yanafanywa na viogozi wawili au watatu kwa niba ya jamii au Taifa!!
   Mkandara likes this.
   Never Get Angry; Never Make Threat; Reason With People;
   "Napenda the logic of the words because in some ways it says about individual-not to use emotions-when scrutinizing something, whether it involves you or not" ...-by AshaDiii @ Jamiiforums 26th July 2011.

  18. Paul S.S's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th August 2009
   Location : Bongo
   Posts : 5,270
   Rep Power : 9849
   Likes Received
   1805
   Likes Given
   1448

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Mimi naamini Dini na siasa havipaswi kuchanganywa hata kidogo. hivi ni vitu viwili tofauti kabisa

   DINI ni imani, na imani is not a fact........
   Imani ya dini A inaweza ikawa ni nguvu za kiza za imani ya dini B

   Tuhukumianane kisiasa kwa matendo yetu kwa mujibu wa katiba na taratibu za nchi yetu tulizo jiwekea na si kwa kudhani fulani ananguvu za giza

   UDINI unaozungumzwa leo ni ile hisia kuwa watu wa imani fulani wanaona mtu wa imani nyingine anapendelea dini yake kwa kutumia mamlaka aliyonayo kitaifa
   Hii hupelekea sasa malumbano hatimaye mtifuano kwa kila mmoja kuona dini yake inaonewa
   Mkandara likes this.
   Tunataka mabadiliko bora, na si bora mabadiliko

  19. Mkandara's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd March 2006
   Location : T dot
   Posts : 15,848
   Rep Power : 124739373
   Likes Received
   7421
   Likes Given
   7106

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Azimio Jipya,
   Nakubaliana na wewe sana kulingana na vitabu, hekima na taaluma inayotumika kuutafisri UTU wa binadamu..Unajua kuna usemi ya kwamba katika viumbe woote duniani hakuna hasidi kama binadamu pamoja na kwamba ndiye aliyejaaliwa Akili ya kuweza kutafakari, kupembua, kuchambua kabla ya kufanya maamuzi kati ya jambo BAYA na ZURI.. Kwa karne nyingi sana binadamu tumekuwa tukiweka mifumo ya kibinadamu kupambana na Unyama wetu - Barbarian kwa kutumia maneno kama civilization kujitenga na unyama ama nafsi ya pili ambayo huitwa Sheitan..Na katika vita hiyo wenzetu walitumia dini kuweza kuzipoza nyoyo za waliopotea ( watu wabaya) ili warudishe upendo na kuyaona mabaya ya matendo yao na ndio waliyowakoa wakapata Uhuerru wao, na walikuja na vitabu hadi Afrika wakifundisha Upendo.

   Tatizo langu kubwa na Watanzania ni ukweli kwamba juhudi za mageuzi yetu bila WATU wake kukubali kubadilika, kukubali kutumia vitabu vya upendo baina yetu kama funzo la kwanza ktk kupitia mitihani ya Umri kama ulivyozungumza hapo juu na kutafuta njia rtrahisi kufikia haya ya mbele ambayo wenzetu wameisha yapata hapo ndipo natishika zaidi. Ikumbukwe tu kwamba wakati Ulaya wanapingania mageuzi ya kijamii hawakuwa na mfano mzuri mbele yao, isipokuwa kueneza Upendo.. walipigana vita ya hali na mali kuondakana na udhalimu ili kujenga jamii inayopendana wakisema - Love and Peace.

   Na ktk jitihada hizo za vita, coup, maandamano walishika Biblia au Kuran mikononi kwa sababu ndio elimu iliyoweza kuujenga UTU wao kama binadamu ktk kujenga Upendo. Na through Upendo na umoja wao waliweza kushinda vita kubwa sana ambazo umma huu hatujapata kuuona. Vita ya panga,mishale mikuki na marungu wakikutana macho kwa macho askari zaidi ya millioni kila upande ktk uwanja wazi tena kwa kuahidiana tukutane kesho Jangwani sasa nane mchana tuzichape. Hawa watu waliongozwa na moyo mkubwa wa uzalendo ktk kupigania UTU wao na identity yao kutokana na imani za kiroho..

   Wao leo wako hatua nyingine ya mageuzi, wanataka mageuzi ya KIUCHUMI na utakuta kwamba vita kubwa ya nchi zao ni sii tena kujitambua, sio tena kwa matabaka baina yao ama kujenga UTU bali wanatazama fursa na uwezo wa kubadilisha MAZINGIRA yao - Urbanism. Na ktk jitihadia hizi wamejikuta walijikuta wakigundua mambo mengi ya mengi ya technoligia, sayansi na uwajibikaji ambayo wamejikuta wakivumbua vitu vya ajabu zaidi ya vile vya kwanza. sasa hivi sio tu wanataka kujitosheleza wao bali wanatazama mahityaji ya dunia nzima ktk utajirisho.

   Sisi nchi za Kiafrika ambao bado kabisa tumeshindwa kuondoa tofauti zetu, tena tunalaani hata ujio wa Biblia na Kuran kwa sababu vilitumika kutupumbaza zaidi na hivyo tunatazama zaidi mbele ktk mabadiliko ya Kiuchumi ilihali sisi wenyewe nafsi zetu zimejaa inda, chuki na kikorosho kwa sababu hatukuwahi kujitambua sisi ni nani. Tunataka mabadiliko tuendelee kuwa na usafiri wa kileo, Miji mizuri kama Dubai, Utawala wenye uongozi bora kati ili hali ndani ya nafsi zetu hatuna uzalendo, imani wala maadili yanayotujenga kama Taifa moja - Hatuna zaidi ya Katiba na sheria zilizotungwa kwa kutazama who we are today.

   Bado tuna Identity conflict na hatutaki kujitambua sisi ni nani na kitu gani kina tuunganisha wote, nini nafasi yetu kidunia isipokuwa kwa kuiga waliotutangulia maana sio Udini tu unaotuburuza, hata lugha yetu wenyewe Kiswahili sasa hivi kinapigwa vita. Wengine wanaanza hata ku question waasisi wa Uhuru wetu, wana mquestion Nyerere na Azimio la Arusha, mbio za Mwenge, mashujaa wetu na mengine mengi kwa sababu tumesha anza kupoteza Identity hata ile iliyotupatia Uhuru wetu. Hatuna guidance isipokuwa katiba ambayo ni chimbuko la mkono wa mtu usiojenga imani za watu kiroho..

   Binafsi yangu nakukubali sana mkuu wangu na pengine haupo pekee lakini nadhani vita unayopigana ama kuitangaza sidhani kama inazama vichwani mwa wananchi ambao wanataka mabadiliko ya Kiuchumi bila kujali kwanza kuzibadili nafsi zao na kujenga Upendo kwa sababu ya umaskini wa hali na mali halafu hakuna adui isipokuwa maskini wengine wanaotaka kujitajirisha. Hili ni sinia la Biriani limemwagwa janvini sijui ni utaratibu gani utaweza zuia mikono ya walafi waliokuja na ndizi tayari mifukoni..

   Binafsi, siamini kabisa kwamba Tanzania hii ya leo inaweza kubadilika kiuchumi iikiwa watu wake bado hawajabadilika na tatizo kubwa hatutaki kusikia Ukweli toka upande wa pili unaotazama kwanza mabadiliko ya WATU isipokuwa wanataka mabadiliko ya MAZINGIRA mbele ya maisha yao. Na ukweli ni kwamba MAZINGIRA hayajibadilishi yenyewe isipokuwa ni Watu wanaoweza kuyabadilisha sasa ikiwa wao hawataki kubadilika isipokuwa kuyabadili mazingira kwanza yawe kama Ulaya. sasa kama Dini zetu haziwezi kutubalisha na kuwa waungwana wenye maadili ya kumwogopa Mungu kutuongoza ktk mabadiliko yetu ya kinafsi sijui kitu gani kitaweza... Mkuu wangu tuna kazi kubwa sana mbele.

   Tuupige vita Udini kwa nguvu zote maana dini zimekuja tuongoke ktk kuujenga UTU, chuki na fitna tuziweke kando na tumwogope Mola maana binadamu kwa hulka habadiliki isipokuwa kwa hofu ya asoyajua. Hata kama utasema mambo yanayoudhi na kuchukiza watu lakini kuna ukweli mdogo tu wa kutuweka pamoja badala ya kusambaratika, kutukanya ktk Unafiki dhulma na Ufisadi na kuuenzi UTU wa Mtanzania japokuwa hupatikana kwa gharama kubwa sana, basi tuwe sote ktk mtihani na changamoto hii.. Tukubali kupoteza madogo ya kidunia tukajenga hofu ya laana na chuki ya unyama wa binadamu ili kuzikosha nafsi zetu ziwe civilized.
   Last edited by Mkandara; 18th April 2012 at 14:40.
   Azimio Jipya and Josephine like this.
   Exploration of reality

  20. TIMING's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th April 2008
   Location : Roaming...
   Posts : 21,702
   Rep Power : 922984
   Likes Received
   6972
   Likes Given
   8076

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By paulss View Post
   Mimi naamini Dini na siasa havipaswi kuchanganywa hata kidogo. hivi ni vitu viwili tofauti kabisa

   DINI ni imani, na imani is not a fact........
   Imani ya dini A inaweza ikawa ni nguvu za kiza za imani ya dini B

   Tuhukumianane kisiasa kwa matendo yetu kwa mujibu wa katiba na taratibu za nchi yetu tulizo jiwekea na si kwa kudhani fulani ananguvu za giza

   UDINI unaozungumzwa leo ni ile hisia kuwa watu wa imani fulani wanaona mtu wa imani nyingine anapendelea dini yake kwa kutumia mamlaka aliyonayo kitaifa
   Hii hupelekea sasa malumbano hatimaye mtifuano kwa kila mmoja kuona dini yake inaonewa
   Great thinker

   HIvyo vitu vimeshachanganyika... cha maana ni kumanage mchanganyiko kama walivyofanya akina Suleimani, na wengine

   We cant turn a blind eye on the mix btn politics and imani.... the bestw e can do is ku-face issues head-on na kuweka wazi kwamba udini upo, ni mbaya na unatakiwa kutenganishwa na siasa to an extent possible to be tolerated
   Last edited by TIMING; 18th April 2012 at 14:40.
   Mkandara and Paul S.S like this.
   ....Time is the wisest counselor !!!

  21. Paul S.S's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th August 2009
   Location : Bongo
   Posts : 5,270
   Rep Power : 9849
   Likes Received
   1805
   Likes Given
   1448

   Default Re: Tunaposema udini ni kweli kuna udini au kuna kitu cha ziada?

   Quote By TIMING View Post
   Great thinker

   HIvyo vitu vimeshachanganyika... cha maana ni kumanage mchanganyiko kama walivyofanya akina Suleimani, na wengine

   We cant turn a blind eye on the mix btn politics and imani.... the bestw e can do is to turn a blind eye; au ku-face issues head-on na kuweka wazi kwamba udini upo, ni mbaya na unatakiwa kutenganishwa na siasa to an extent possible to be tolerated
   Mkuu labda unifumbue macho katika hili unaposema hivyo vitu vimechanganyika
   Mkandara and TIMING like this.
   Tunataka mabadiliko bora, na si bora mabadiliko

  Page 41 of 45 FirstFirst ... 313940414243 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Replies: 0
   Last Post: 25th May 2011, 18:29
  2. Jamani tupende KULA chakula ASILIA
   By Lucchese DeCavalcante in forum Jamii Photos
   Replies: 13
   Last Post: 4th November 2010, 13:16

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...