Tanzania hakuna udini serikalini, hizo ni conspiracy theories tu za watu wa makundi fulani wanapoona matokeo wasiyoyapenda, hasa hasa ni za watu wachache nje ya serikali wenye udini. Mkapa alishutumiwa kuwapendelea wakristo kwenye utawala wake, mimi sikuona upendeleo wowote alioufanya, mwenye ushahidi aweke hapa. Sasa hivi kuna watu wanamtuhumu Kikwete kuwa anawapendelea waislamu katika utawala wake, sijaona upendeleo wowote alioufanya hadi sasa, mwenye ushahidi pia anakaribishwa. Namaanisha ushahidi, si maneno ya umbea ya kudai eti nasikia hivi nasikia vile!
Huo ukabila nimeuona kiasi fulani kwa makabila machache, na sasa hivi unajengeka kwa kasi mijini, hasa vyuoni na kwenye mashirika ya umma. Siku moja nilikaribishwa kwenye shughuli ya chama cha watu wa kabila fulani pale chuoni mlimani Dar, walikuwa wamealika pia vigogo wa kabila hilo kutoka universities na mashirika mbalimbali. Katika kutaja mafanikio yao, vigogo hao walikuwa wanakitaarifu chama hicho cha wanafunzi idadi ya "homeboys" waliokwisha kuwasaidia kuingia kwenye maofisi yao, na kuwahimiza kuhusu nafasi nyingine zilizoko wazichangamkie. Sasa hii ndio nepotism, maana asiyekuwepo kwenye shughuli hii atapata taarifa ya nafasi hizi zikiwa zimeshajazwa na watu wenye "sifa", maana kinachoangaliwa hapo ni cheti ambacho wote waliowahishiwa taarifa wan sifa hiyo.
Ila kwa wachagga nina maoni tofauti kuhusu jinsi wanavyoweza kumudu ukabila. Miaka 10 niliyoishi kwa wachagga, nilijifunza kuwa wachagga kama kabila hawana uwezo wala organization ya kusimama pamoja kupambana na hayo makabila mengine kama suala ni ukabila. Wao ni opportunists, wana-pair na yeyote atakayewawezesha kupata hela (awe mhindi, mwarabu,yeyote yule), na wanamtema yeyote asiyewasaidia kwenye hela hata kama ni mchagga mwenzao. Wenyewe kwa wenyewe hawana solidarity yoyote, hata wakianzisha vyama vyao vya kusaidiana kikabila huwa haimei. Kwanza kabila lenyewe la "wachagga" halipo, kuna vikabila vidogovidogo ambavyo kwa pamoja wanajiita wachaga, lakini kimsingi ni tofauti sana. Wapo wauru, wamachame, wakibosho, warombo, wavunjo, wakilema, nk, na wote hawa kila mmoja anamdharau mwenzie vibaya sana na hawawezi kufanya kitu cha solidarity kamwe. Wanaweza tu kufanya partnership ya biashara, ambayo pia wangeweza kufanya na mtu yeyote, lakini undugu hakuna! Katika shule moja niliyofundisha kulikuwa na Headmaster akiitwa Mushi (wenyewe tulimwita Mzee Mushi), basi alikuwa na tuhuma kibao, na aliyekuwa kinara wa kusukuma mbele hizi tuhuma alikuwa mchaga (sasa huyu simtaji). Siku moja nikawa interested nikamwuliza mbona unamwandama sana ndugu yako? Akanijibu "wewe, ndugu yangu gani, acha kabisa! Huyu ni mmachame ati, mmachame si mtu!". Duh, niliishiwa nguvu, nilitegemea anijibu kuwa labda hawezi kuficha uovu kwa kisingizio cha undugu, kumbe yeye anapambana na "mmachame"! Kwa hiyo hawa wanaojiita wachaga, ubaguzi wao ni katika level ambayo ni below uchaga, ambayo kitaifa madhara yake kisiasa siyaoni. Ni ma-opportunists tu kama wahindi, wanafuata pale penye maslahi ya kiuchumi kwanza (ndio maana mzee Mkapa alipochangisha yale mamilioni ya "kukomboa" majimbo ya Kilimanjaro, aliyarejesha yote CCM isipokuwa lile moja alilokuwa anamlazimishia shemeji yake, CCM wenyewe wakaamua kumpiga chini na kumpa Ndesamburo. Na bado hapo kuna "money factor" ya Ndesamburo ambaye pia ni "mzima" idara hiyo).
Kama kuna mchaga wa kuyapinga niliyosema ajitokeze, nasisitiza siwashambulii wajameni, ni wajomba wa baba yangu nawaheshimu, lakini hayo ndiyo ninayoyajua kwa undani kuwahusu. Wao ni pesa mbele, dini na kabila baadae.
Nahitimisha kusema kuwa udini Tanzania kuna kikundi cha watu wachache wanaopenda kuonesha dunia kuwa upo wakati kimsingi haupo, na kimegawanyika vikundi vidogo viwili. Akiwa rais mkristo, kile kimoja kinaamka na kudai waislamu wanaonewa, kingine kinalala. Akichaguliwa rais mwislamu, kile kingine kinaibuka kichinichini na kudai anapendelea waislamu. Labda siku tukipata asiye na dini kabisa tutaona watasemaje. Na tena kigezo chao cha kulalamika upendeleo ni kuangalia majina ya wateuliwa, ambayo wameyaweka katika makundi ya majina ya kikristo na kiislamu. Mimi siamini kuwa majina kama hayo yapo. Hivi majina John au Mary ni ya dini gani? Maana Yesu Kristo alipozaliwa alikuta tayari kuna watu wanaitwa hivyo, kwa hiyo ukristo uliyakuta hayo majina yapo. Ni ya kikristo hayo? Kwa msingi upi? Na Mihayo ni jina la dini gani? Si la kikristo kwa nini? Maana wamishenari walipokuja kutuhubiria walikuta tayari tunaitwa majina haya, kama Yesu alivyowakuta wao na majina yao. Sasa sie huku tuna matatizo, tukiona jina Gunda Mihayo, tunasema la kisukuma, lakini Mary John ati ni la kikristo, mbona ni la kizungu tu? Maftaha ni jina la kiislamu? Si la kiarabu? Na Ufunguo je, haliwezi kuwa jina la kiislamu? Au hili litaitwa la "kiswahili"? Nahisi pia tukianza kuwapa wanetu majina ya asili kama wanavyofanya wazaire labda tuhuma za udini zitapungua, lakini wataibuka wa kupekua majina ya kina "Mwakabima", "Masawe", "Rutachungululwa", na tuhuma za ukabila zitaibuliwa. Kumbe tunahitaji kwanza sura ya kitaifa kabla ya hizi dini, kabila nk, ambayo hakika itahitaji vizazi na vizazi kuijenga.
Na hao tunaowatuhumu ati wameteuliwa kwa "udini" unakuta wala hawashiki hizo dini! Maana JK angekuwa anateua mawaziri au mabosi wengine kiislamu, ningetegemea atafute ushauri wa mashehe, ili ateue waislamu "safi", kwa msingi wa dini, lakini hatujaona ushahidi wa namna hiyo.
Naishia hapa kwa leo.
Follow Us Here