Wanafunzi wa Zaidi 1000 Vyuo Vikuu Wajiunga Na CCM - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Jukwaa la Siasa


Jukwaa la Siasa Tanzania & World Politics General Discussion Forum. You need to be registered in order to post your comment(s)


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 6th November 2007, 11:46 AM   #1
Wanafunzi wa Zaidi 1000 Vyuo Vikuu Wajiunga Na CCM
MegaPyne MegaPyne is offline 6th November 2007, 11:46 AM

NI KUTOKA DODOMA NA MORO
JK AWAKABIDHI KADI AWAAHIDI AJIRA


Wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyoko katika mikoa ya Morogoro na Dodoma wameipongeza Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa uamuzi wake wa kuwapatia mikopo wanafunzi wa vyuo va elimu juu .

Wameeleza kuwa utaratibu huo wa Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kkikwete umewawezesha hata watoto wanaotoka katika familia za daraja la ‘tatu’ nao kupata elimu ya juu.

Pongezi hizo zimetolewa na wanafunzi hao, muda mfupi kabla ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Jakaya Kikwete kuwakabidhi kadi za uanachama wa CCM, baada ya wanafunzi hao zaidi ya 1000 kuamua kujiunga na chama hicho. Hafla hiyo ilifanyika jana jioni Jumatatu katika Makao Makuu ya CCM, Dodoma .


Wanafunzi hao ambao kwa kila chuo waliwakilishwa na wenzao wapatao 20 ni kutoka vyo vikuu vya Dodoma, Mtakatifu John, vyuo vya Mipango na Madini,(544), na SUA, Mzumbe na chuo kikuu cha Kiislamu vyote vya Morogoro (566))


“Mhe Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, kwanza tunapenda tukupongeze kwa ushindi mnono ulioupata katika uchaguzi uliomalizika leo (Jumatatu), ushindi huu unaonyesha ni kwa namna gani wajumbe wa mkutano mkuu walivyo na imani nawe” akasema mwakilishi wa wanafunzi kutoka vyuo vya mkoa wa Dodoma.

Akaongeza “ lakini pia tunapenda kutoa shukrani zetu kwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa na mipango mizuri ya kuwapatia wanafunzi wa vyuo vikuu mikopo, asante kwa mikopo hii ambayo imewawezesha watoto kutoka familia za daraja la tatu kupata elimu”

Hata hivyo wamesema wanafunzi hao kuwa pamoja na utaratibu huo mzuri, wanamwomba Rais kuangalia uwezekano wa kuongeza kiwango cha mikopo, kuharakisha upatikanaji wake na pia kuwasaidia wale ambao hawajapata hadi sasa.

“Mhe. Rais kuchelewa kwa mikopo hii kunatufanya wengine tuuze vocha za simu ili tujikimu, lakini pia kuna wenzetu ambao hadi sasa hawajafanikiwa kupata mikopo tunaomba hili uliangalie” akasema mwakilishi wa wanafunzi kutoka Dodoma, kauli iliyoshangiliwa na wanafunzi hao

Wanafunzi hao walimweleza Rais kwamba wamehamasika na kuamua kujiunga na CCM, na kuahidi kuwa watakilinda na wanamuunga mkono Rais katika juhudi zake za kuwatumikia Watanzania ili waweze kuwa na maisha bora.

Aidha wanafunzi hao kwa ujumla wao wamempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa ushindi mnono alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa CCM, na kwamba ushindi wake huo ni kielelezo cha namna gani anavyokubalika mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu na kubwa zaidi ni kwamba wana imani naye.

Wamemwomba Rais apange ratiba ya kuvitembelea vyuo vikuu na kuzungumza na wanafunzi ili nao wapate wasaa mzuri wa kumpongeza. Wamemhakikishia kwamba wataendelea kuwahimiza wanafunzi wa elimu ya juu kujiunga na CCM, na kwamba zile fikra kwamba kuna upinzani dhidi ya CCM katika vyuo vikuu si sahihi.

Akizungumza na wanafunzi hao baada ya kuwakabidhi kadi zao, Rais alisema amefurahishwa sana na idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka Dodoma na Morogoro ambao wameamua kwa hiari yao kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Akawaeleza kuwa Chama kina mkakati maalum kwa kuwavutia wasomi wengi kujiunga na CCM na kwamba hiyo ni njia bora na sahihi ya kuwaandaa viongozi katika ngazi mbalimbali za serikalini na katika Chama.

“Nimefurahi sana kwa kweli, kwa sababu chama lazima kipate wasomi, na nchi haiwezi kuendelea bila ya wasomi, na duniani hakuna nchi ambayo imeendelea kwa kuwa na watu mbumbumbu. Na ndio maana tulipoingia serikalini tulitoa umuhimu wa pekee katika elimu” akasema Kikwete.

Amewahakikishia wanafunzi hao kwamba, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imejiwekea mkakati maalum wa kuwaajiri wanafunzi waliohitimu chuo kikuu kuanzia ngazi ya tarafa.

Akawaeleza kuwa wasisite kwenda kufanya kazi katika tarafa kwani huko ndio kunakowafungulia uzoefu na fursa ya kupanda katika safu za uongozi ziwe za ukatibu tawala, ukuu wa wilaya, ukuu wa mikoa na nafasi nyingine nyingi.

“Tunamkakati maalum wa kuwaajiri wanafunzi, na mwaka huu tunaanza na wanafunzi wapatao 500 kutoka SUA, na ninapenda niwahakikishie kwamba vijana wasomo ambao tumewaajiri katika nafasi ya ukuu wa wilaya 12 kati yao wanafanya vizuri sana, hii inaonyesha umuhimu wa kuwaajiri wasomi” akasisitiza Rais.

Akizungumzia kuhusu suala la mikopo ya wanafunzi, Rais amewaahidi wanafunzi hao, kwamba kabla ya kuondoka mkoani Dodoma atahakikisha anakutana na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo na kuangalia matatizo yaliyojitokeza ili kuyapatia ufumbuzi.

“Nataka niwahakikishie kwamba kabla sijaondoka hapa Dodoma nitakutana na Waziri na Mwenyekiti wa Bodi na kuangalia wapi pana tatizo na kulitafutia ufumbuzi, maana suala hili la mikopo limeingiliwa na watu wengi wakiwamo wanasiasa, lakini hatima yake anayeathirika ni mwanafunzi” akasema Rais na kushangiliwa na wanfunzi hao.

Amewaeleza kuwa Serikali inaandaa utaratibu wa kuboresha njia za mawasiliano kati ya Bodi ya Mikopo na wanafunzi wa vyuo vikuu.

Rais Kikwete pia alitumia fursa hiyo kuwaeleza wanafunzi hao juhudi na mikakati mbalimbali inayofanywa na Serikali katika uboreshaji na upanuzi wa elimu nchini kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu na kwamba imejipanga vema kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Kuhusu ombi la kutembelea vyuo vikuu, Rais ameahidi kupanga utaratibu na kwa kuanzia atakitembelea chuo kikuu cha Dodoma kabla hajaondoka.

Awali Katibu Mkuu wa CCM Yusufu Makamba aliwataka wanachama hao wapya kila mmoja wao kushawishi wanachama wapya watano kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Source: Subirini Magazeti ya Kesho.

 
MegaPyne's Avatar
MegaPyne
Senior Member
Points: 687,791, Level: 100 Points: 687,791, Level: 100 Points: 687,791, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
Join Date: Thu May 2006
Posts: 546
Thanks: 0
Thanked 8 Times in 5 Posts
Views: 2164
Reply With Quote
  #2  
Old 6th November 2007, 11:55 AM
Mtanzania Mtanzania is offline
Mtanzania has no status.
JF Premium Member
Points: 645,736, Level: 100 Points: 645,736, Level: 100 Points: 645,736, Level: 100
Activity: 5% Activity: 5% Activity: 5%
 
Join Date: Thu May 2006
Location: UK
Posts: 4,923
Thanks: 62
Thanked 234 Times in 105 Posts
Rep Power: 33
Mtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enough
Default

Mkuu,

Hawa vijana inaweza kuwa njaa zaidi ya mapenzi yao.

Inatakiwa vyama vya siasa visiwatumie wanafunzi kwenye mapambano yao. Wanafunzi wanajua CCM wameshika mpini na wao makali, kweli hapo kuna cha mapenzi tena?

Nafikiri ni makosa kwa JK na yeye kuingia kwenye politics za namna hiyo.
Reply With Quote
  #3  
Old 6th November 2007, 12:03 PM
Gembe's Avatar
Gembe Gembe is offline
Gembe ni mshauri
JF Senior Expert Member
Points: 1,172,087, Level: 100 Points: 1,172,087, Level: 100 Points: 1,172,087, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Tue Sep 2007
Location: kamnyonge
Posts: 2,386
Thanks: 40
Thanked 55 Times in 30 Posts
Rep Power: 67
Gembe is a jewel in the roughGembe is a jewel in the roughGembe is a jewel in the roughGembe is a jewel in the roughGembe is a jewel in the roughGembe is a jewel in the roughGembe is a jewel in the roughGembe is a jewel in the roughGembe is a jewel in the roughGembe is a jewel in the roughGembe is a jewel in the rough
Default

je wanawakilisha mawazo ya wanafunzi au wamechukuliwa kama propaganda?
hawa ni makada wa chama tu,nijuavyo mie..Mzumbe na sua ni tawi kubwa la watu wa sisiemu..
Reply With Quote
  #4  
Old 6th November 2007, 12:05 PM
Ben Ben is online now
Ben The Little Boy among Men
JF Senior Expert Member
Points: 648,728, Level: 100 Points: 648,728, Level: 100 Points: 648,728, Level: 100
Activity: 56% Activity: 56% Activity: 56%
 
Join Date: Thu Jan 2007
Posts: 2,201
Thanks: 254
Thanked 271 Times in 173 Posts
Rep Power: 68
Ben is a jewel in the roughBen is a jewel in the roughBen is a jewel in the roughBen is a jewel in the roughBen is a jewel in the roughBen is a jewel in the roughBen is a jewel in the roughBen is a jewel in the roughBen is a jewel in the roughBen is a jewel in the roughBen is a jewel in the rough
Default

Hao nao njaa.Ila CCM wanafanya uharamia kuwawekea wanafunzi maisha magumu kwanza halafu baadae waone njia pekee ya kujiokoa ni kujiunga na CCM kupata mlo.Damn and shame! Hao wasomi nao uchwara yaani hawajaona nchi inavyooza kwa uongozi huu mbovu wa Vasco Da'Gama na hicho chama kokoro?

Ndio maana hata huyo mwakilishi wa wananchi amesisitiza kuhusu maswala yaq mkopo.CCM haina nchi inatakiwa iongoze kwa kufuata kanuni na sheria.Sasa Kuikwete asije akatumia suala Mikopo kwa ajili ya Maslahi ya CCm na kuwahujumu wanafunzi.Hata bila kujiunga na CCM ni wajibu wao kutoa mikopo kwa wanafunzi wote aidha wako upinzani ama laa.

Hii inatia kinyaa,Hao wanafunzi nao wanashindwa kufikiria yaani wasomi ambao tulitegemea wataichallenge govt kuhusu Ufisadi,utawala usio na madili ya kazi,rushwa nk ndio wamekua vinara wa kujikomba.

Najua ni haki ya kila mtu kuingia katika chama chochote cha siasa but sio kama hawa walivyofanya.WAMELISALITI TAIFA LETU.Damn!
Reply With Quote
  #5  
Old 6th November 2007, 12:06 PM
Ufunuo wa Yohana Ufunuo wa Yohana is offline
Ufunuo wa Yohana Mambo ambayo hayanabudi kutokea siku za mwisho
JF Senior Expert Member
Points: 111,618, Level: 100 Points: 111,618, Level: 100 Points: 111,618, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Tue Oct 2007
Posts: 316
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 23
Ufunuo wa Yohana will become famous soon enoughUfunuo wa Yohana will become famous soon enoughUfunuo wa Yohana will become famous soon enoughUfunuo wa Yohana will become famous soon enoughUfunuo wa Yohana will become famous soon enoughUfunuo wa Yohana will become famous soon enoughUfunuo wa Yohana will become famous soon enoughUfunuo wa Yohana will become famous soon enough
Default

Wasomi kwa sasa hawana msaada wowote katika kudai haki za wanyonge msiwategemee!!
Angalieni mitaala yao huko vyuoni ni siasa ya kulinda mafisadi nina uhakika wanayoyasema si kweli bali ni kujikomba tu

ndoto zao ni siku moja wawe nao mafisadi kama hao wanowapomgeza

nchi hii iko mbioni kukombolewa na wanyonge wenyewe wala si hao wanaojiita wasomi


Mungu akise ndiyo hakuna kiumbe chini ya mbingu kitasema hapana

Mungu ibariki Tanzania.
Reply With Quote
  #6  
Old 6th November 2007, 12:11 PM
Dua's Avatar
Dua Dua is offline
Dua busy at the moment.
JF Senior Expert Member
Points: 644,099, Level: 100 Points: 644,099, Level: 100 Points: 644,099, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Tue Nov 2006
Posts: 3,534
Thanks: 0
Thanked 3 Times in 2 Posts
Rep Power: 32
Dua will become famous soon enoughDua will become famous soon enoughDua will become famous soon enoughDua will become famous soon enoughDua will become famous soon enoughDua will become famous soon enoughDua will become famous soon enoughDua will become famous soon enough
Default

Kama ni kweli alishindwaje kuwasaidia wanafunzi waliokuwa Ukraine tayari na walianza kusoma baada ya mwaka moja akawatelekeza. AIBU HIYO JK, WEWE ULISOMESHWA KWA PESA YA WALIPA KODI.
__________________
Dua la kuku halimpati mwewe
Reply With Quote
  #7  
Old 6th November 2007, 12:21 PM
Rwabugiri Rwabugiri is offline
Rwabugiri has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 166,840, Level: 100 Points: 166,840, Level: 100 Points: 166,840, Level: 100
Activity: 2% Activity: 2% Activity: 2%
 
Join Date: Tue Jul 2007
Posts: 2,305
Thanks: 10
Thanked 8 Times in 8 Posts
Rep Power: 27
Rwabugiri will become famous soon enoughRwabugiri will become famous soon enoughRwabugiri will become famous soon enoughRwabugiri will become famous soon enoughRwabugiri will become famous soon enoughRwabugiri will become famous soon enoughRwabugiri will become famous soon enoughRwabugiri will become famous soon enough
Default

yale yale maigizo wanafunzi 20 kuwakilisha wenzao 1000!!!

-kwani pesa za mikopo ni za CCM ama ni kodi zetu? ama ndo yale yale ya Amani na utulivu kuwa ni sera ya CCM

Tumechoka mbadala lazima miaka zaidi ya 40 umasikini tuuuu kisa UFISADI unao endekezwa na CCM, hata muigize kwamba wamejiunga wasomi laki saba na nusu .. kita eleweka tu!
Reply With Quote
  #8  
Old 6th November 2007, 12:34 PM
Masanilo's Avatar
Masanilo Masanilo is offline
Masanilo is alcoholic
JF Premium Member
Points: 826,872, Level: 100 Points: 826,872, Level: 100 Points: 826,872, Level: 100
Activity: 46% Activity: 46% Activity: 46%
 
Join Date: Tue Oct 2007
Location: Swat valley
Posts: 7,059
Thanks: 1,055
Thanked 1,106 Times in 724 Posts
Rep Power: 77
Masanilo is a jewel in the roughMasanilo is a jewel in the roughMasanilo is a jewel in the roughMasanilo is a jewel in the roughMasanilo is a jewel in the roughMasanilo is a jewel in the roughMasanilo is a jewel in the roughMasanilo is a jewel in the roughMasanilo is a jewel in the roughMasanilo is a jewel in the roughMasanilo is a jewel in the rough
Default

Thats too cheap!!! Yale yale alofanya Mathayo kwa wanafunzi wa SUA 1998..Wanafunzi hao wanatumika bila wao kujua. Tatizo ninaloliona hapo ni mtu kushindwa kujua haki zake za msingi..hata kama huna chama ni wajibu wa serikali kusomesha na kutoa mikopo kwa wanafunzi wanafikia viwango. Sasa jamani JK ameamua kujizolea sifa za ubwete kwa hao wanafunzi 20 wakiwakilisha wenzao 1000 !!! Kali kweli kweli...

Jamani mwenye CV ya Makamba naomba anirushie huyo mzee sijui anaujuzi gani zaidi ya kuwa mfundisha siasa jeshini na kubebwa bebwa mpaka sasa... mzee anaweka usanii hata kwenye mambo ya msingi...I love you Makamba teh teh teh
__________________
To be able to do everything by knowing nothing is dangerous

E-mail:
masanilo@jamiiforums.com
Reply With Quote
  #9  
Old 6th November 2007, 12:41 PM
Chakaza's Avatar
Chakaza Chakaza is online now
Chakaza mchukia mafisadi
JF Premium Member
Points: 108,860, Level: 100 Points: 108,860, Level: 100 Points: 108,860, Level: 100
Activity: 12% Activity: 12% Activity: 12%
 
Join Date: Sat Mar 2007
Posts: 906
Thanks: 54
Thanked 124 Times in 89 Posts
Rep Power: 25
Chakaza will become famous soon enoughChakaza will become famous soon enoughChakaza will become famous soon enoughChakaza will become famous soon enoughChakaza will become famous soon enoughChakaza will become famous soon enoughChakaza will become famous soon enoughChakaza will become famous soon enough
Default

Hekaya zilezile za Abunuwasi
Reply With Quote
  #10  
Old 6th November 2007, 02:04 PM
Hume Hume is offline
Hume has no status.
Senior Member
Points: 117,822, Level: 100 Points: 117,822, Level: 100 Points: 117,822, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Tue Sep 2007
Posts: 206
Thanks: 1
Thanked 10 Times in 9 Posts
Rep Power: 23
Hume will become famous soon enoughHume will become famous soon enoughHume will become famous soon enoughHume will become famous soon enoughHume will become famous soon enoughHume will become famous soon enoughHume will become famous soon enoughHume will become famous soon enough
Default

Wangekuwa wamehamia upinzani hapo ingekuwa news au?

Anyway, wanafunzi wa vyuo vikuu huwa sielewi kabisa mambo yao.
Walivaa kijani na njano Diamond baada ya kufatwa na magari kutoka vyuoni, wakachukua kadi za ccm kibao, wiki iliyofuata walewale wakaandamana kwenda jangwani na kashfa kibao dhidi ya serikali kwa kushindwa kutekeleza habari yao ya mikopo.

Leo tena wanasifia na hapohapo anapouliza mtu asiyeridhishwa na mwenendo wa mikopo anashangiliwa, hiyo inatoa picha gani?

Na wao wameamua kuleta ushkaji na serikali ya kishkaji?
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
1000, ccm, vikuu, vyuo, wajiunga, wanafunzi, zaidi


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Kashfa ya Richmond: The FACTS FairPlayer Celebrities Forum 1354 12th March 2010 01:37 PM
Tambwe Hiza anaishabikia CCM iliyopoteza mwelekeo MwanaCCM Habari na Hoja mchanganyiko 1 4th December 2009 10:39 AM
Majibu ya Mwanakijiji kwa Bodi ya Mikopo Halisi Jukwaa la Elimu (Education Forum) 36 22nd July 2007 08:24 AM
Prof Msola Kawasilisha Bajeti Halisi Jukwaa la Siasa 5 22nd July 2007 02:09 AM
CCM na mbinu chafu za kushinda uchaguzi MwanaCCM Habari na Hoja mchanganyiko 0 7th March 2007 10:11 PM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 05:09 PM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com