Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Makamba: Msinihukumu kwa mabaya, I love you

    Report Post
    Results 1 to 8 of 8
    1. #1
      KadaMpinzani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st January 2007
      Location : Chadema Restaurant
      Posts : 5,011
      Rep Power : 1629
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Post Makamba: Msinihukumu kwa mabaya, I love you

      Makamba: Msinihukumu kwa mabaya, I love you

      2007-11-06 08:33:34
      Na Beatrice Bandawe, Dodoma


      Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, (pichani kulia) juzi alilazimika kuwaomba wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kura kwa kutomhukumu kwa mabaya yake na kuwaambia: `Ilove you`.

      Bw. Makamba ambaye mara baada ya kuwaambia wajumbe hao `I love you` (nawapenda), waliripuka kwa mayowe ya vicheko, alisema kuwa binadamu yuko mara tatu.

      Alifafanua kwamba upande wa kwanza wa binadamu ni vile anavyojifahamu mwenyewe, anavyofahamika na wenzake na anavyofamika na Mungu.

      Alisema kwa jinsi anavyojifahamu yeye, anafaa kuchaguliwa katika uchaguzi huo.

      Bw. Makamba ambaye aligombea kundi la viti 20 la NEC Taifa, hata hivyo, alichaguliwa kwa ushindi mnono.

      `Chonde chonde wajumbe nichagueni I Love you,` alisema kwa kuweka msisitizo.

      Aliwataka wanachama hao kutomhukumu kwa mabaya yake kwani hata Mungu aliwasamehe waliomkosea.

      `Nawaombeni mninusuru na chama chetu,` alisema na kuongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu aliochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, amepambana na kuwagaragaza wapinzani.

      Alisema kama wajumbe watamuangusha, hata wapinzani watafurahi na kusema CCM wameangusha Katibu Mkuu wao.

      Aidha, alisema vyombo vya habari pia vitapata ya kuandika na kuweka kwenye vichwa vya habari kwamba Makamba agaragazwa na wana-CCM wenzake.

      Bw. Makamba ambaye alikuwa akitoa kauli hiyo wakati aliposimama kwenye jukwaa la kuombea kura, mara baada ya kumaliza kujinadi, Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, alimjibu kwa kumwambia: `We love you too,` na kusababisha ukumbi mzima kushangilia.

      SOURCE: Nipashe

    2. Study Abroad

    3. #2
      Kufakunoga's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th September 2007
      Posts : 35
      Rep Power : 602
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      hapo ndio utaamini kwamba CCM ni wasanii si mchezo,huyu ni msanii namba mbili.anashindwa kuwaeleza wapiga kura wake amefanya mambo gani ya maendeleo,anakazania kuwagalagaza wapinzani,je hiyo ndiyo sera ya maisha bora kwa kila mtanzania?

    4. #3
      Gembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2007
      Location : kamnyonge
      Posts : 2,586
      Rep Power : 1515
      Likes Received
      64
      Likes Given
      54

      Default

      Chama cha mapinduzi si mama yangu na wala si dini yangu,siwezi kuabudu usanii..
      Naomba kuungana na Mwanakijiji kuacha kuwaombea viongozi hawa..
      toka makamba ameingia haya yametokea.

      1.Suala la Muafaka limekosa mwelekeo ulio thabiti,rejea ilifikia kipindi ukataka kuvunjika.

      2.amewatusi viongozi wa CCM wa Tanga,na nina uhakika hata baada ya kuwaambia I Love you hawakumchagua sababu sio kipenzi chao..

      Mie naona imetosha,Tafakari

    5. #4
      KadaMpinzani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st January 2007
      Location : Chadema Restaurant
      Posts : 5,011
      Rep Power : 1629
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default

      yoo bad umeishia njiani, sie tutajikongoja hivyo hivyo !

    6. #5
      Jafar's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2006
      Location : Msoga, Chalinze
      Posts : 1,249
      Rep Power : 895
      Likes Received
      13
      Likes Given
      0

      Default

      Usishangae, CCM ni waoga wa mabadiliko/mapinduzi. Nilishanga style ya kuunda ya JK ya kishamba ya kuunda tume ya madini ikiingiza hata mashehe na mapdri. Hivi ikitokea sekta nyingine ya kiuchumi ina matatizo ataunda tume nyingine kuongoza. Ina maana mawaziri 60 alionao hawatoshi au ni "compitency issue"?. Kuunda tume ni upuuzi, kama anaona hawezi kusimamia vizuri apishe watu waendelee.

      Nimekasirishwa.

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      Idimi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2007
      Location : Ikwiriri
      Posts : 4,647
      Rep Power : 13618
      Likes Received
      833
      Likes Given
      318

      Exclamation Makamba's Legacy

      I am not quite sure if Lt, Makamba is really representative of sisiemu's views, vision, mission and legacy. I have been making a close follow-up of what he has been promulgating since he was a regional commissioner in Dar, he seems to be more than a partisan, calling 'wapinzani' mapaka.
      He has constantly been blaspheming opposition and anyone who is against his views. Do we all deserve this blasphemy and insults simply because we do not belong to sisiemu?
      A successful man is one who makes more money than his wife can spend. A successful woman is one who can find such a man!
      [email protected]

    9. #7
      KadaMpinzani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st January 2007
      Location : Chadema Restaurant
      Posts : 5,011
      Rep Power : 1629
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Jafar
      Usishangae, CCM ni waoga wa mabadiliko/mapinduzi. Nilishanga style ya kuunda ya JK ya kishamba ya kuunda tume ya madini ikiingiza hata mashehe na mapdri. Hivi ikitokea sekta nyingine ya kiuchumi ina matatizo ataunda tume nyingine kuongoza. Ina maana mawaziri 60 alionao hawatoshi au ni "compitency issue"?. Kuunda tume ni upuuzi, kama anaona hawezi kusimamia vizuri apishe watu waendelee.

      Nimekasirishwa.
      babu, sio ccm inayoogopa mapinduzi, ukizingatia kikaitwa chama cha mapinduzi, hivi unataka kuniambia wewe ulipokuja hapo ulipo haikuwa vigumu kuadapti mazingira ? je ulikuwa muoga, usiye na uhakika na mafanikio ya nia zako au ulikuwa na uhakika ? ccm KAMWE HAIOGOPI MAPINDUZI HENCE CHAMA CHA MAPINDUZI !

    10. #8
      S. S. Phares's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2006
      Posts : 3,041
      Rep Power : 1246
      Likes Received
      16
      Likes Given
      106

      Default

      Makamba ni msaani stadi sana...

    11. Miaka 50

    Similar Topics

    1. Replies: 28
      Last Post: 18th August 2011, 22:39
    2. Weekend special for friends:...give love.....get love......
      By NewDawnTz in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 7
      Last Post: 19th June 2011, 16:26
    3. Waliomwombea mabaya Makamba walie tu....................
      By Rutashubanyuma in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 16
      Last Post: 4th December 2010, 19:55

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...