TiGo Says
    Show/Hide This

    Topic: Kikwete: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

    Report Post
    Page 1 of 5 123 ... LastLast
    Results 1 to 30 of 121
    1. #1
      Mzito Kabwela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 8th December 2009
      Location : MPUMBULI
      Posts : 2,486
      Rep Power : 0
      Likes Received
      435
      Likes Given
      80

      Default Kikwete: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      NA MWANDISHI WETU
      7th June 2010

      Rais Jakaya Kikwete amesema matukio ya mimba kwa wanafunzi wa kike nchini yanasababishwa na viherehere vya wanafunzi wenyewe.

      Aidha, Rais Kikwete amekiri kwamba matukio ya mauaji ya vikongwe pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), yanalidhalilisha taifa.

      Rais Kikwete alitoa kauli hizo katika kijiji cha Kisesa wilayani Magu jana wakati akihutubia wananchi kwenye ufunguzi wa mashindano ya ngoma kwa kabila la Wasukuma; ngoma ambazo zinajulikana kama 'Bulabo'.

      " Kila anayepata Ukimwi anaufuata mwenyewe na wengine ni viherehere vyao; kwa mfano watoto wa shule," alisema Rais Kikwete wakati akijibu risala ya Mkurugenzi wa Makumbusho ya Bujola, Fadha Frasince Sandhu, ambaye alisema ujumbe wa mashindano hayo mwaka huu ni vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

      Kwa mujibu wa Rais Kikwete, suala la zinaa kwa bianadamu, siyo la lazima hivyo binadamu anaweza kujizuia ama kujikinga kwa kutumia kondomu.

      " Na kwa bahati mbaya shughuli ile (uzinzi) binadamu hana dharura nayo, hivyo unaweza kutumia kondomu kama unaona kwamba huwezi kutii amri ya sita ama huwezi kuwa mwaminifu katika ndoa yako," alisema kauli ambayo ilizua vicheko miongoni mwa watu waliohudhuria ufunguzi huo. Aliwashauri wananchi watakaoshiriki kwenye mashindano hayo wawe na tahadhari dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.

      " ...katika mambo yanayolitia aibu taifa hasa kwa watani wangu Wasukuma, ni pamoja na mauaji ya albino na vikongwe eti tu kwa sababu wana macho mekundu. Ni mambo ya fedheha sana ingawa yanakwenda yanapungua lakini yanalidhalilisha taifa," alisema.

      Aliwataka washiriki wa mashindano hayo walisaidie taifa katika kupiga vita mauaji ya aina hiyo.

      Rais Kikwete alifuatana na wabunge kadhaa akiwemo Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (CCM) pamoja na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM).

      Aidha, Rais Kikwete amepewa jina la Mungubabu, ikiwa na maana busara na uwezo wa kuongoza nchi kama Mungu.

      Mashindano ya 'bulabo' yalianza mwaka 1954 kupitia Kanisa Katoliki Bujola, lengo likiwa ni kuweka burudani mara baada ya mavuno.

      CHANZO:
      NIPASHE

    2. #2
      TIMING's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 18,658
      Rep Power : 4797
      Likes Received
      5195
      Likes Given
      5895

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      alikua anatania tu!!!!
      ..... Just a thought!!

    3. #3
      Oxlade-Chamberlain's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 26th May 2009
      Location : dodoma
      Posts : 6,995
      Rep Power : 4245
      Likes Received
      618
      Likes Given
      640

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      tuache utani wakuu haya maneno kayatoa raisi?
      "Nobody has enough talent to live on talent alone. Even when you have talent, a life without work goes nowhere". A. Wenger

    4. #4
      Invisible's Avatar
      Robot Array
      Join Date : 11th February 2006
      Location : Here...!
      Posts : 8,761
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      2877
      Likes Given
      1892

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By Arsene Wenger View Post
      tuache utani wakuu haya maneno kayatoa raisi?
      Kama hakuyatoa yeye si ungesikia Nipashe linafungiwa? - lakini alikuwa anatania tuuu
      Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!
      24/7 Email SUPPORT: support@jamiiforums.com

    5. #5
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 33,155
      Rep Power : 20735
      Likes Received
      5034
      Likes Given
      360

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Lakini ana hoja hapo....
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    6. #6
      Rufiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2006
      Posts : 1,359
      Rep Power : 881
      Likes Received
      161
      Likes Given
      21

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Mmmmh, haya makubwa jamani. Kweli Rais wa nchi anaona watu wanaopata Ukimwi au mimba ni vihelehele vyao . Kweli hii inasikitisha ....

    7. #7
      Oxlade-Chamberlain's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 26th May 2009
      Location : dodoma
      Posts : 6,995
      Rep Power : 4245
      Likes Received
      618
      Likes Given
      640

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By mzittokabwela View Post
      Aidha, Rais Kikwete amepewa jina la Mungubabu, ikiwa na maana busara na uwezo wa kuongoza nchi kama Mungu.
      kuna watu wanajua kukufuru duniani.
      "Nobody has enough talent to live on talent alone. Even when you have talent, a life without work goes nowhere". A. Wenger

    8. #8
      Rufiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2006
      Posts : 1,359
      Rep Power : 881
      Likes Received
      161
      Likes Given
      21

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Kwa hiyo wote waliopata ukimwi ni via sexual intercourse, vipi wale waliozaliwa nao au waliopata through blood transfusion ? Na jee Rais anasend message gani kwa wale wanaowarubuni watoto wa shule ambao ni below 18? Jee hao watoto wa kike are they matured enough to make aninformed decisions...those are the questions that our president was supposed to ponder before blaming students and AIDS patients

    9. #9
      Mambo Jambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th July 2008
      Posts : 1,041
      Rep Power : 710
      Likes Received
      12
      Likes Given
      0

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By mzittokabwela View Post
      NA MWANDISHI WETU
      7th June 2010

      " Kila anayepata Ukimwi anaufuata mwenyewe na wengine ni viherehere vyao; kwa mfano watoto wa shule,"

      CHANZO:
      NIPASHE
      Inabidi aangalie kauli anazotoa, hii si kauli nzuri hata kidogo, vipo vitu vingi vinavyosabisha watu kupata ukimwi na wakati mwingine siyo kwa kujitakia au kuwa wazembe, huu ni unyanyapaa kwa mtu aliyekuja na kauli ya Tanzania bila ukimwi inawezekana....inasikitisha sana.
      A wise man once told me, luck isn't some mystical energy that dances around the universe randomly bestowing people with safisfaction and joy..you creat your own luck.

    10. #10
      Mdau's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th March 2008
      Posts : 1,035
      Rep Power : 728
      Likes Received
      71
      Likes Given
      53

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      mmekosea,hawezi kusema haya maneno!!

    11. #11
      Oxlade-Chamberlain's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 26th May 2009
      Location : dodoma
      Posts : 6,995
      Rep Power : 4245
      Likes Received
      618
      Likes Given
      640

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By Nyani Ngabu View Post
      Lakini ana hoja hapo....
      ukitazama haraka haraka yap lakini kwa undani yeye kama kiongozi ni kama mzazi pia.

      sasa mkuu nyani ngabu majukumu ya mzazi au kiongozi ni kutoa muongozo sio kusema kumwambia mwanao kiherehere chake.swala la ngono lina ushawishi mkubwa sana na ni rahisi mno binadamu yoyote kuingia mkenge si mkubwa wala mtoto.

      Kuna maneno mengi ya busara na ya kuelimisha ambayo Kikwete angetumia yangeweza kuwa msaada kwa hawa wanafunzi kuliko kuwaambia kiherehere na wazazi pia tunahitajika kuwaongoza watoto wetu vizuri na kuwaelimisha swala zima la ngono na sio kuwalaumu tu.

      anyway ni simlaumu sana kwani kashatoa kauli nyingi za ajabu ajabu nadhani ni kwa vile uwezo wake wa kuongoza ni mdogo sana.
      "Nobody has enough talent to live on talent alone. Even when you have talent, a life without work goes nowhere". A. Wenger

    12. #12
      Mambo Jambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th July 2008
      Posts : 1,041
      Rep Power : 710
      Likes Received
      12
      Likes Given
      0

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By mzittokabwela View Post
      NA MWANDISHI WETU
      7th June 2010

      Aidha, Rais Kikwete amepewa jina la Mungubabu, ikiwa na maana busara na uwezo wa kuongoza nchi kama Mungu.

      CHANZO:
      NIPASHE
      Duuh, baada ya hotuba, hii kitu ikafuata.
      A wise man once told me, luck isn't some mystical energy that dances around the universe randomly bestowing people with safisfaction and joy..you creat your own luck.

    13. #13
      Mambo Jambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th July 2008
      Posts : 1,041
      Rep Power : 710
      Likes Received
      12
      Likes Given
      0

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By Nyani Ngabu View Post
      Lakini ana hoja hapo....
      Ipi?
      A wise man once told me, luck isn't some mystical energy that dances around the universe randomly bestowing people with safisfaction and joy..you creat your own luck.

    14. #14
      TIMING's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 18,658
      Rep Power : 4797
      Likes Received
      5195
      Likes Given
      5895

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By Invisible View Post
      Kama hakuyatoa yeye si ungesikia Nipashe linafungiwa? - lakini alikuwa anatania tuuu
      Very true mkuu... inasikitisha kwamba ameweka wote under one cluster wakati majority ni victims wa abuse, tena from people around them waliotakiwa wawalinde hawa wadogo zetu!!!

      Siamini kabisa hii itapita kama kauli nyingine kwani tuna wanaharakati kwa gender wazuri sana, LAKINI SI UNAJUA TENA RAIS WETU KWA UTANI?? WE SUBIRI AJE TENDWA HAPA ATASEMA RAIS ALIKUA ANATANIA
      ..... Just a thought!!

    15. #15
      MpigaFilimbi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th April 2008
      Location : Uvunguni
      Posts : 925
      Rep Power : 697
      Likes Received
      66
      Likes Given
      29

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Anaitwa Mungubabu tena? Acheni huo utani, hekima na busara hizo wanazijua wasukuma tu? Tuna kazi kwelikweli kuelimisha huu umma wa watanzania wanaopenda kusujudia watu na kuwapamba kwa sifa ambazo hawana..sijui tuna tatizo gani?
      "If you are going through HELL, keep going..."-W.Churchill

    16. #16
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 33,155
      Rep Power : 20735
      Likes Received
      5034
      Likes Given
      360

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By Mambo Jambo View Post
      Ipi?
      Wasichana wanaopata mimba ni viherehere vyao...
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    17. #17
      jmushi1's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 2nd November 2007
      Posts : 11,278
      Rep Power : 3204
      Likes Received
      1904
      Likes Given
      3386

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Waandishi waweke wazi kama ni kweli alisema "Kila anayepata ukimwi" ni kihere here....Unless alikuwa akizungumzia baadhi ya wanaopata ukimwi na si "Kila" anayepata ukimwi,kuna utofauti kwasababu si kweli "Kila" anayeupata ukimwi anaupata kwa njia ya zinaa.
      "LEADERSHIP IS ACTION NOT POSITION OR EDUCATION"-Donald H. Mcannon

    18. #18
      TIMING's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 18,658
      Rep Power : 4797
      Likes Received
      5195
      Likes Given
      5895

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By Rufiji View Post
      Kwa hiyo wote waliopata ukimwi ni via sexual intercourse, vipi wale waliozaliwa nao au waliopata through blood transfusion ? Na jee Rais anasend message gani kwa wale wanaowarubuni watoto wa shule ambao ni below 18? Jee hao watoto wa kike are they matured enough to make aninformed decisions...those are the questions that our president was supposed to ponder before blaming students and AIDS patients
      Mkuu, nadhani mkulu amekosa elimu ya ukimwi, jamii na makuzi hasa kwa ajili ya public speaking!!! kuna kauli ambazo ni za kuturudisha nyuma hasa kwenye fight against HIV/AIDS, TB na malaria... his statement ni confimration kwamba hajaiva kwenye vita dhidi ya stigma!!!

      Pia tukumbuke kwamba kuna watoto wanzaliwa na virusi kutoka kwa mama, na wapo wengi sana under 18 siku hizi kwani hawakua wakibahatika kupimwa kwani huduma za PMTCT [prevention of mother to child transmission] hazikua active na wazungu walikua hawajaleta pesa
      ..... Just a thought!!

    19. #19
      Anyisile Obheli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th December 2009
      Location : Rohoni
      Posts : 3,072
      Rep Power : 1035
      Likes Received
      30
      Likes Given
      70

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By Arsene Wenger View Post
      tuache utani wakuu haya maneno kayatoa raisi?
      aaah mie sishangai kwani tz kuna raisi ama mropokaji tu, with no sence in how he is talking about.

      mazungumzo ya mtu yanamtambulisha ana hekima ya kiasi gani, vipi kwa wanao bakwa na kupata ujauzito?
      ........................HAKUNA TIBA YA KIFO............
      HESHIMU WATU NA PIA JIHESHIMU, KISHA, MPENDE MUNGU

    20. #20
      Mambo Jambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th July 2008
      Posts : 1,041
      Rep Power : 710
      Likes Received
      12
      Likes Given
      0

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By Nyani Ngabu View Post
      Wasichana wanaopata mimba ni viherehere vyao...
      Hawa wanaopata mimba siyo wote wana viherehere, wengine ni ugumu wa maisha, utoto, na njaa kali...kunawengine huwa wanavamiwa kijinsia kwa nguvu na ndugu zao wa karibu baba/uncle etc.

      Naukiangalia kwa macho mawili nani angesaidia kusaidia ugumu wa maisha na njaa kali kama siyo mtuhumu.
      A wise man once told me, luck isn't some mystical energy that dances around the universe randomly bestowing people with safisfaction and joy..you creat your own luck.

    21. #21
      Oxlade-Chamberlain's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 26th May 2009
      Location : dodoma
      Posts : 6,995
      Rep Power : 4245
      Likes Received
      618
      Likes Given
      640

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      na nina huakika kuna mijitu ilimpigia makofi na kucheka aliposema maneno haya.
      "Nobody has enough talent to live on talent alone. Even when you have talent, a life without work goes nowhere". A. Wenger

    22. #22
      Kang's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2008
      Posts : 2,887
      Rep Power : 1085
      Likes Received
      310
      Likes Given
      14

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Hahaha! Hatuna Rais sisi jamani! KIMEO!
      “Society is like a stew. If you don't stir it up every once in a while then a layer of scum floats to the top.”

    23. #23
      Luteni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th January 2010
      Posts : 2,269
      Rep Power : 890
      Likes Received
      224
      Likes Given
      73

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Watu wanaweza kusema huwa tunamuonea rais kwa kukosoa kila anachofanya lakini ni yeye anayefanya watu wamseme, pamoja na kiherehere alitakiwa atambue ni wananchi wake wanaopata matatizo ambayo mengi si ya kujitakia inawezekana yanasababishwa na hali mbaya ya uchumi, alitakiwa aseme maneno ya kutia moyo si ya dhihaka.

      Kuna wakati fulani Nyerere aliulizwa huwa anajifunza nini akutanapo na wananchi sehemu mbalimbali anapotembelea hasa vijijini, alisema "nikipita barabarani na kumwona mwanamke amebeba kuni kichwani jembe begani na mtoto mgongoni huwa inanigusa na kunikumbusha wajibu wangu kwa wananchi walionichagua", hayo ndiyo maneno yanayotakiwa kutamkwa kiongozi na si haya ya rais wetu wa sasa.
      Luteni is a True Revolutionist.

    24. #24
      Mzito Kabwela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 8th December 2009
      Location : MPUMBULI
      Posts : 2,486
      Rep Power : 0
      Likes Received
      435
      Likes Given
      80

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By Invisible View Post
      ..................... lakini alikuwa anatania tuuu
      Ina maana mwandishi wake wa hotuba mheshimiwa Januari Yusuph Rajab Makamba huwa anachomekea viutani kwenye hotuba za bosi wake au Muungwana ana asili ya kutania tania hadi awe anatania hata kwa ishu ya kulia?

    25. #25
      Mambo Jambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th July 2008
      Posts : 1,041
      Rep Power : 710
      Likes Received
      12
      Likes Given
      0

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Mafataki sasa full kujiachia.
      A wise man once told me, luck isn't some mystical energy that dances around the universe randomly bestowing people with safisfaction and joy..you creat your own luck.

    26. #26
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 33,155
      Rep Power : 20735
      Likes Received
      5034
      Likes Given
      360

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Whatever happened to personal responsibility?
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    27. #27
      Epason's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th November 2009
      Location : Endagulda
      Posts : 75
      Rep Power : 448
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Alikuwa na hoja, ila angetafuta namna nzuri ya kuiwakilisha kulingana na status yake, au angemtafuta moja wa watendaji wake kwenye mihadhara husika kufikisha ujumbe wa bwana mkubwa. Pia jamii zetu tuwe majaji wazuri wa kupima uwezo wa kiongozi na si kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa (kuna ka ujima hapa!!).

    28. #28
      Oxlade-Chamberlain's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 26th May 2009
      Location : dodoma
      Posts : 6,995
      Rep Power : 4245
      Likes Received
      618
      Likes Given
      640

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By Nyani Ngabu View Post
      Whatever happened to personal responsibility?
      baada kutoa muongozo ndio unawakumbushia sasa "personal responsibility" yao sio kuwalaumu tu moja kwa moja.
      "Nobody has enough talent to live on talent alone. Even when you have talent, a life without work goes nowhere". A. Wenger

    29. #29
      Mzito Kabwela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 8th December 2009
      Location : MPUMBULI
      Posts : 2,486
      Rep Power : 0
      Likes Received
      435
      Likes Given
      80

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Wakuu huyu bwana ni very intelligent. Anaongea with experience. Haropoki tu. Huwezi jua labda alishakutana nao wenye viherehere akawagonga mimba.....

    30. #30
      bnhai's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2009
      Posts : 652
      Rep Power : 580
      Likes Received
      8
      Likes Given
      3

      Default Re: JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

      Quote By Arsene Wenger View Post
      baada kutoa muongozo ndio unawakumbushia sasa "personal responsibility" yao sio kuwalaumu tu moja kwa moja.
      Ukiunganisha doti utaona anazungumzia uzinzi na ndio maana habari ikatoka hivyo. Lakini pia ukisoma quoatation ya mwandishi na title utaona havifanani.

    Page 1 of 5 123 ... LastLast

    Similar Topics

    1. Replies: 5
      Last Post: 5th November 2010, 13:54
    2. Kesi za mimba za wanafunzi
      By funzadume in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 25
      Last Post: 3rd October 2010, 07:58
    3. Kikwete: Walioambukizwa UKIMWI ni kiherehere chao
      By Marksman in forum Tanzania 2010-2015
      Replies: 47
      Last Post: 1st October 2010, 12:31
    4. Ni kweli kikwete amesema wanaoishi na vvu ni "kiherehere chao"?
      By bwegebwege in forum Tanzania 2010-2015
      Replies: 1
      Last Post: 28th September 2010, 20:56

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...