Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: CCM na usultani mweusi!

    Report Post
    Results 1 to 8 of 8
    1. #1
      nginjanginja's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 27th September 2007
      Posts : 6
      Rep Power : 597
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default CCM na usultani mweusi!

      Watanzania tunajigamba kuwa tumefanikiwa kuutokomeza usultani kwa msingi kwamba tumewarejeshea wananchi/wadau mchakato mzima wa kujipatia viongozi wao ima ikiwa ni kwa kuwachagua au kuwateua. Hata hivyo, tunahitaji ukweli wa dai hili kutokana na tabia nzima iliyomo na iliyozoeleka ndani ya CCM katika upatikanaji wa viongozi ambayo ni yenye kukinzana na na dhana yote ya hapo juu.

      Dalili kwamba ndani ya CCM kuna usultani mweusi ni kutokana na tabia ya viongozi walioko madarakani ama waliowahi kuweko madarakani kuamua kwa makusudi kuwaachia jamaa zao (watoto wao) nafasi hizo kwa misingi ya kurithishana, jambo ambalo ni sifa kuu ya usultani.

      Mifano hai ya kuthibitisha hoja hiyo ni kama ifuatayo:

      Marehemu Abeid Amani Karume aliekuwa rais wa mwanzo wa Zanzibar amerithiwa na mwanawe Amani Abeid Karume ambae ni raisi wa sasa wa Zanzibar. Marehemu Yussuf Himid aliekuwa waziri na member wa baraza la mapinduzi amerithiwa na mwanawe Mansoor Yussuf Himid ambae ni Waziri wa nishati, ardhi na ujenzi. Mwengine ni marehemu Thabitin Kombo ambae nae pia alikuwa waziri katika serikali ya awamu ya kwanza na pia member wa baraza la mapinduzi amerithiwa na mwanawe Mahmood Thabiti kombo ambae ni naibu waziri wa habari na michezo, na kubwa lililopo sasa ni hata mzee Mwinyi nae anaonekana kwenda mbio katika kumuandaa kijana wake Dr Hussein Mwinyi ili nae aje arithi nafasi aliyokuwa nayo baba yake ya kuwa raisi wa zanzibar. Je! CCM tunataka kuwaambia watanzania kuwa hakuna watu wengine Tanzania wenye sifa ama kama walizonazo warithi hao au hata zilizo bora zaidi ya hizo na kuweza kushika nyadhifa kama hizo kwa misingi ya uwezo na uzalendo?

    2. Miaka 50

    3. #2
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,670
      Rep Power : 21816
      Likes Received
      736
      Likes Given
      3195

      Default

      Karibu sana jamvini nginja

      unajua tena mambo/mazoea ya kupigiwa saluti

    4. #3
      Alnadaby's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th September 2006
      Posts : 557
      Rep Power : 759
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default

      Ni kuendeleza mapinduzi matukufu ya kumuondoa Sultani mweupe wa asili ya Kiarabu kwwa kutumia dozi ile ile ya 1964.lazima warithishane kwa sababu kiapo cha mapinduzi daima bado kipo na wajumbe wa baraza la mapinduzi wapo na wataendelea kudumu milele.Inshallah Dr.Mwinyi atakuwa Rais wa Zanzibar na kama hamtaki shauri yenu.Sisi tunawatakia kila la kheri wazaliwa na wana wa hao wakulu wa kale.
      SUCCESS USUALLY COMES TO THOSE WHO ARE TOO BUSY TO BE LOOKING FOR IT.

    5. #4
      tuongee's Avatar
      Member Array
      Join Date : 16th August 2007
      Posts : 19
      Rep Power : 605
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      I am just trying to think that mchezo wa siasa unatend ku-run in families like michezo mingineyo, think of the Ngasas, Amiris, Matumlas, Mogellas, Alis (Mohd),..... maybe the list is inexhaustible! Is "like father like son" applicable in politics? What answer do you expect of a daugther/son of a prominent politician unapomwuliza "what do you want to be when you grow up? I think think am making myself clear of the hoja am trying kujenga.

      let's talk

    6. #5
      Rwabugiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Posts : 2,738
      Rep Power : 1158
      Likes Received
      67
      Likes Given
      31

      Default

      Quote By tuongee
      I am just trying to think that mchezo wa siasa unatend ku-run in families like michezo mingineyo, think of the Ngasas, Amiris, Matumlas, Mogellas, Alis (Mohd),..... maybe the list is inexhaustible! Is "like father like son" applicable in politics? What answer do you expect of a daugther/son of a prominent politician unapomwuliza "what do you want to be when you grow up? I think think am making myself clear of the hoja am trying kujenga.

      let's talk
      Nadhani kwa Tanzania na CCm is more than that!

      Kuna hii hali ya chama ambacho kimetawala zaidi ya miaka 40 baada ya waasisi wake kutangualia mbele haki, kugeuka na kuwa chama cha wenye pesa ama kujuana ama cha koo kama tunavo shuhudia kwa sasa!

      Haingii akilini, kwamba kabla Jk hajawa rais tulikuwa hatusikii habari za vikwetes kwenye nyanja za juu za Siasa!, Lakini sasa kuanzia mama, baba,mtoto, babamkubwa wote ndani!, mara hauja kaa sawa eti mama January?? hivi hao wanaibuka tu baada ya waume/ wazazi wao kuwa wakulu? mbona siku zote hawakuwepo? ama ndo huko kupokezana kwenyewe?

      Na je kwa hali hiyo haimaanishi na kusababisha kwamba mwenzangu na mie hata kama unao uwezo wa kuongoza kwa vile siyo wa koo/familia hizo/ama huna pesa ya kuhonga ndo basi?

      Ndo maana nakubaliana na mtoa hoja kwamba tunako elekea tuta anza mambo ya koo za falme kama vile wao ndo wamezaliwa kutawala!

      Ni bora tukaiga hata kwa majirani zetu kenya walivo amua kumpiga chini mtoto wa Moi na hivo kuukwepa mtego huo, bila kustuka ndiko tunako elekea!


    7. #6
      Msanii's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2007
      Posts : 6,207
      Rep Power : 1927
      Likes Received
      210
      Likes Given
      249

      Default

      dawa yao ni uwamwaga tu ktk sanduku la kura ili warithishane shame vizuri
      " If you hear a voice within you say "you cannot paint", then by all means paint, and that voice will be silenced"
      [email protected]

    8. #7
      Mtu wa Pwani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2006
      Posts : 4,250
      Rep Power : 1491
      Likes Received
      159
      Likes Given
      152

      Default

      nnaategemea kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.

      msisitizo usiwe mbona wanarithishana msisitizo uwe jee wanarithi kiutaratibu tuliojiwekea?

      kama ni kugombea jee haki na uhuru ilipatikana tokea uteuzi hadi kupiga kura?

      ikiwa utaratibu umefatwa na hakuna malalamiko ya uonevu na kupendeleana mie sioni tatizo.

      na haki na utaratibu ukipindwa hata awe anatoka familia ya utumwa na awe mweusi kama lami au mweupe kama jua bado siungi mkono.
      Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown

    9. #8
      Ng'ondya's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 26th July 2007
      Posts : 1
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      bado hiyo unayodai haijawa hoja ya kuujustify usultani mweusi eti kwasababu uliuondoa usultani mweupe. issue hapa sio ni aina gani ya usultani unafaa na upi haufai. na kama tunakubaliana in principles kuwa usultani mweusi una wiana na ule mweupe kama ulivyoeleza juu ya dhana nzima ya kupeana madaraka kwa misingi ya kurithishana,mbona dhana nzima ya mapinduzi itakuwa ni yenye kujicontradict, kwasababu tumeondoa nini na halafu tunafanya nini. miongoni mwa ahadi kuu za mapinduzi ni kutaka kuwarejeshea wananchi na waafrika in particular at tha particular time ile haki ya kuweza kuchagua viongozi kwa ridhaa yao na kuachana na ule mfumo wa kurithishana. rudi kwenye kumbukumbu za ahadi za mapinduzi na sio tu za tanzania/zanzibar, almost nchi zote zilizojikomboa kutoka katika mikono ya wakoloni had common goal la kuwarudishia wananchi/wazawa haki hiyo ya kuchaguwa na kuchaguliwa na kuachana na mfumo potofu wa kurithishana.

    Similar Topics

    1. Replies: 48
      Last Post: 29th October 2010, 18:42
    2. Sultani Jamsheed hakukana kiti cha Usultani wa Zanzibar
      By Mzee Mwanakijiji in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 172
      Last Post: 8th February 2010, 15:15
    3. Usultani mpya ktk siasa za Tanzania
      By inawezekana in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 9
      Last Post: 12th August 2009, 18:13
    4. Replies: 12
      Last Post: 31st July 2009, 14:52

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...