JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

  Report Post
  Page 2 of 25 FirstFirst 1234 12 ... LastLast
  Results 21 to 40 of 499
  1. Salary Slip's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd April 2012
   Posts : 9,882
   Rep Power : 348571074
   Likes Received
   6031
   Likes Given
   3859

   Default Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...
   Hatimaye Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewaandikia barua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo, ambao wiki iliyopita walivuliwa nafasi za uongozi, zinazoeleza mashtaka ya makosa 11 wanayotuhumiwa kuyatenda dhidi ya chama hicho.

   Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alisema barua hizo, ambazo Zitto na Dk. Mkumbo, walitarajiwa kukabidhiwa jana, zinawataka wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua zaidi, ikiwamo kufukuzwa uanachama.

   Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, siku mbili baada ya Zitto na Dk. Mkumbo, kuitisha mkutano na waandishi wa habari, Jumapili wiki iliyopita na kusema hadi siku hiyo walikuwa hawajapata barua hizo zaidi ya kusikia suala hilo kwenye vyombo vya habari.

   Mnyika alisema mashtaka ya makosa, ambayo Zitto na Dk. Mkumbo wanatuhumiwa kuyatenda, yanahusiana moja kwa moja na ukiukwaji wa katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama hicho.
   Alisema uamuzi wa kuwavua nafasi za uongozi ulifikiwa na Kamati Kuu (CC) ya Chadema katika vikao vyake vilivyofanyika wiki iliyopita.
   Mnyika alisema baada ya maamuzi hayo ya CC, juzi sekretarieti yake ilikutana kwa mujibu wa kazi zake za kikatiba.

   Alisema ikiwa sehemu ya utekelezaji wa maamuzi ya CC, sekretarieti ilikamilisha mapitio ya yaliyojiri pamoja na maamuzi ya CC juu ya suala hilo pamoja na kukamilisha barua hizo kwa wahusika.

   “Na naomba kuwajulisha tu kwamba, leo (jana) wahusika wote (Zitto na Dk. Kitila) watapatiwa barua zao kwa maana kwamba barua zao ziko tayari zinazoeleza maamuzi ya Kamati Kuu,” alisema Mnyika.

   Alisema maamuzi ya CC hayakuhusu tu kuwavua uongozi, bali yalihusu vilevile kutakiwa kuandikiwa kujieleza ni kwa nini wasichukuliwe hatua za ziada, ikiwamo kufukuzwa uanachama kutokana na makosa waliyoyafanya na waliyokifanyia chama.

   “Na kwa kweli ni makosa waliyoyafanya na ambayo wamekifanyia chama yalielezwa na maamuzi ya Kamati Kuu yaliyotangazwa,” alisema Mnyika.

   MAKOSA YANAHUSIANA NA WARAKA
   Alisema makosa hayo yalihusiana na waraka ulioandikwa, ambao kimsingi ulikiuka katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama.

   “Sasa kwenye mashtaka yao na barua zao ambazo leo watakabidhiwa kumeeleza mashtaka na makosa 11, ambayo watajwa wameyafanya ya kukiuka kanuni, katiba na itifaki ya chama,” alisema Mnyika.

   Alisema mashtaka waliyoandikiwa, yamejikita katika maamuzi ya CC, ambayo yalihusu waraka wa siri.

   “Na siyo masuala, ambayo wahusika baada ya Kamati Kuu kupitisha maamuzi yale wameyasema kwenye vyombo vya habari masuala ambayo siyo yaliyoifanya Kamati Kuu ifikie maamuzi iliyoyafikia,” alisema Mnyika.

   Aliongeza: “Kwa hiyo tayari wahusika wameandikiwa barua na nisisitize kwamba, maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu ya chama yamefanywa kwa mujibu wa katiba, kanuni, maadili na itifaki ya chama.”

   Maamuzi hayo ya CC yalimvua Zitto, ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini wadhifa za Naibu Katibu Mkuu na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida.

   Kwa maana hiyo, Zitto ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) Mjumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, amebaki kuwa mwanachama wa kawaida.

   Aidha, uongozi wa wabunge wa Chadema uliagizwa na CC kumwandikia barua Zitto ya kumwondoa katika nafasi ya Naibu Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Fedha haraka iwezekanavyo kwa tuhuma za kukisaliti chama.

   Pia aliyekuwa Mjumbe wa CC, Dk. Kitila, na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, ambao nao wamevuliwa nyadhifa zote za uongozi na kubaki kuwa wanachama wa kawaida.

   Akijibu yaliyozungumzwa na Zitto na Dk. Kitila baada ya maamuzi ya CC dhidi yao, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, alisema ni maneno ya kupoteza lengo kwa kuwa walivuliwa nafasi za uongozi kwa sababu ya waraka ule na siyo kwa sababu ya kile alichokiita uongo wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

   ‘Uongo’ wa PAC unaodaiwa na Lissu, ni kauli iliyowahi kutolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto akisema hakuna chama chochote cha siasa, ikiwamo Chadema, ambacho hesabu zake zimekaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

   Lissu alisema hata Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatambua kuwa Chadema ni kati ya vyama, ambavyo hesabu zake zimekaguliwa.

   Alisema Chadema ina nyaraka zinazothibitisha hilo tangu mwaka 2010, 2011 na 2012, ambazo Zitto alipokuwa Naibu Katibu Mkuu alipaswa kuzijua.

   Lakini alisema Zitto alishindwa kuzijua nyaraka hizo kwa sababu alipokuwa kiongozi wa chama hakuwa na mazoea ya kufika ofisini, badala yake amekuwa akiishia kukitungia uongo chama.

   “(Zitto) Anatumia jukwaa la PAC kutukanyaga kwa hoja za uongo,” alisema Lissu.

   Mbali na hilo, Lissu alisema pia kuwa Zitto na Dk. Mkumbo hawakuvuliwa nafasi za uongozi katika chama kwa sababu ya yeye (Zitto) kukataa kupokea posho au kuuza majimbo ya uchaguzi, ambayo Chadema ilisimamisha wagombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

   Kuhusu hoja kwamba CC haina mamlaka ya kumvua mwanachama nafasi ya uongozi bali Baraza Kuu la chama, alisema haina msingi kwa kuwa katiba ya Chadema imeipa mamlaka CC kama itaona kuna dharura ya kufanya hivyo.

   Alitoa mfano akisema mwaka 2004 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Amani Kabourou alivuliwa nafasi hiyo na CC. Pia mwaka 2007, CC ilimvua Umakamu Mwenyekiti Taifa, marehemu Chacha Wangwe.

   Alisema vipindi vyote hivyo, Zitto alikuwapo na alishuhudia hayo.

   “Sasa kama CC ilikuwa sahihi vipindi vyote hivyo basi na sasa ni sahihi,” alisema Lissu.

   Alisema mashtaka ya makosa 11, ambayo Zitto na Dk. Kitila wanatuhumiwa kuyatenda hawawezi kuyaweka hadharani, bali watawakabidhi wahusika na kwamba, kama wao wataamua kufanya hivyo hilo litakuwa juu yao.

   Hata hivyo, alisema wanaweza kuyaweka hadharani baada ya CC kupokea utetezi kutoka kwa watuhumiwa.

   Alisema mwaka 2012, Chadema ilitengeneza mwongozo unaomtaka mwanachama kutangaza kusudio la namna ya kugombea uongozi katika chama na kwamba, walifanya hivyo ili kuzima chokochoko zilizokuwa zimekithiri kuelekea kwenye uchaguzi katika siku za nyuma.

   Kwa mujibu wa Lissu, mwongozo huo unataka mwanachama atangaze wazi kusudio lake hilo kwa kupeleka barua kwa Katibu Mkuu na siyo kwa kujificha na kuchafua wengine.

   “Kama wangekuwa wanataka mtu wao (awe mwenyekiti wa Chadema) wangetangaza. Maamuzi ya Kamati Kuu ni uthibitisho kwamba hakuna tunayemuogopa,” alisema Lissu.

   Alisema ni kweli suala la PAC lilijadiliwa katika vikao vya CC, lakini halikuwa hoja ya kuwashtaki wahusika.

   FEDHA ZA SABODO

   Kuhusu Sh. milioni 100 zilizowahi kutolewa na mfanyabiashara Mustafa Sabodo kwa Chadema mwaka 2009, Lissu alisema zipo kwenye ripoti ya CAG na ile iliyopelekwa na chama kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na kwamba, hajawahi kumsikia Zitto akihoji fedha hizo na zile za ruzuku ya chama kwenye vikao vya chama.

   CHANZO: NIPASHE

   =============
   Quote By Taswira View Post
   MASHITAKA 11 dhidi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, yamebainisha kuwa kosa kubwa la kiongozi huyo kijana, ni nia yake ya kutaka kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe.

   Chanzo chetu cha habari kilichoona mashitaka hayo kabla ya kutumwa kwa washitakiwa, kimebainisha kuwa makosa saba kati ya makosa 11, yanahusu kugombea uenyekiti Taifa, au kumkashifu Mwenyekiti wa Taifa.

   “Ukiona hayo mashitaka yenyewe ndugu yangu, yanajirudia rudia na kuzunguka katika kosa moja la nia ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa… angalia kosa la kwanza, kosa la tatu, tano, sita nane na tisa, ni kama vile kuwania uenyekiti ndio kosa kubwa.

   “Hata hivyo kwa jinsi mgawanyiko ulivyo ndani ya chama sasa, nakuhakikishia hawa jamaa (Zitto, Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba), watarudishwa katika nyadhifa zao na hakuna atakayeadhibiwa,” alisema mtoa taarifa wetu.

   Alinukuu kauli ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu aliyehoji kama makosa wanayotuhumiwa akina Zitto ni makubwa kiasi cha kuyeyusha mema aliyoyafanya katika chama. “Si umesikia akina Baregu wakizungumza? Kwa mashitaka yale nakuhakikishia kitakachofanyika ni kufunika kombe mwanaharamu apite,” alisema mtoa habari wetu.

   Kosa la kwanza
   kwa Zitto, Dk Mkumbo na Mwigamba, wanadaiwa kuvunja Kanuni ya Chama inayokataza kukashifu chama, kiongozi au mwanachama yeyote. Katika maelezo ya kosa hilo, akina Zitto wanadaiwa kumkashifu Mwenyekiti wa Taifa, Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema.

   Moja ya madai katika mashitaka hayo, ni kilichoandikwa katika Mkakati wa Mabadiliko 2013, kuwa Mbowe amekuwa akinunua vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei anayoijua mwenyewe na ambayo haihojiwi popote. Wanadaiwa pia wamemkashifu Dk Slaa kwa kudai ni mdhaifu kwa kumruhusu Mbowe kuingilia shughuli za kiutendaji.

   Zitto na wenzake wanadaiwa katika kosa la pili, kutokuwa wawazi na wa kweli wakati wote na kushirikiana na vikundi vya majungu na udanganyifu kinyume na Kanuni za Uendeshaji kipengele cha 10.1 (VIII.

   Katika kosa la tatu, wanadaiwa kutoa tuhuma juu ya viongozi wenzao bila kupitia vikao halali na utaratibu wa ngazi zilizowekwa, kinyume na kanuni ya 10.1 (X).

   Katika kosa la nne, akina Zitto wanadaiwa kujihusisha na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini au ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya chama, miongoni mwa jamii, kisiasa au kijamii. Katika kosa hilo wanadaiwa kwenda kinyume na kipengele cha 10.1 (IV), cha Kanuni za Uendeshaji wa Chama.

   Akina Zitto katika kosa la tano, wanadaiwa kujihusisha na vitendo vya kuchonganisha na kuzua migogoro kwa viongozi wa chama au wanachama, kinyume na kifungu cha 10.1 (IX), cha Kanuni za Uendeshaji wa Chama.

   Katika kosa la sita ambalo mtoa habari wetu alisema ndio kubwa, Zitto na wenzake wanadaiwa kutekeleza mpango wa kusudio la kugombea uenyekiti wa Chama Taifa, bila kutangaza kusudio la kutangaza nafasi hiyo.

   Hatua hiyo inadaiwa kuwa ni kinyume na kifungu 2.C cha Muongozo wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi ya Uongozi wa Chama, Mabaraza na Serikali wa 2012.

   Zitto na wenzake katika kosa la saba, wanadaiwa kutengeneza mitandao ya kuwania uongozi ndani ya chama kwa nia ya kujihakikishia ushindi kinyume na kanuni ya 2 (D), ya Muongozo wa Kuwania Uongozi.

   Katika kosa la nane, Zitto na wenzake wanadaiwa kuwachafua viongozi na wanachama wengine wenye kusudio/nia ya kutaka kugombea nafasi ya uenyekiti kinyume na kifungu 2 (E) cha Muongozo wa Kuwania Uongozi.

   Katika kosa hilo, kumewekwa maelezo ya ziada kuwa kosa hilo linaunganishwa na kosa la kwanza ambalo washitakiwa wanadiwa kuwakashifu Mbowe, Dk Slaa na Lema.

   Kosa la tisa, akina Zitto wanadaiwa kujihusisha na upinzani dhidi ya chama na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama wakati wa uchaguzi wa chama, kinyume na kifungu cha 10.3 (IV), cha Kanuni za Uendeshaji.

   Kosa la kumi linamhusu Zitto peke yake, ambapo anaidaiwa kukashifu chama na kiongozi wa chama nje ya Bunge kinyume na kifungu 2 C (B), kikisomwa pamoja na kifungu 3 B cha Kanuni za Mwenendo wa Maadili ya Wabunge.

   Katika hilo Zitto kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa chama yaani Dk Mkumbo na Mwigamba na mtu mwingine ambaye hajajulikana, wanadaiwa kusambaza waraka uitwao Mkakati wa Mabadiliko 2013.

   Mkakati huo, unadaiwa kukashifu chama na/ au viongozi wake wakuu kama ilivyoelezwa katika kosa la kwanza, tatu, nne na nane.

   Mwisho katika kosa la 11, Zitto na wenzake wanadaiwa kuchochea mgawanyiko ndani ya chama kinyume na kanuni ya 3 F ya Kanuni za Mwenendo wa Maadili ya Bunge.


   CHANZO: HabariLeo


  2. Ochutz's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st May 2011
   Posts : 465
   Rep Power : 629
   Likes Received
   102
   Likes Given
   18

   Default

   Quote By Young Tanzanian View Post
   hahahaahaha...kwa speech ya lisu tayari zitto anahujumiwa...eti hatutaki kuweka tuhuma wazi ila si alizozisema zitto na dk.mkumbo...eti ukiwa na nia ya kugombea unaandka barua kwa katibu mkuu hivi kweli kuna kitu kama hicho dunia ipi..et ohh zito ajawahi kuhoji pesa za sabodo na ruzuku kwenye vikao vya chama..sasa atahoji ili nani atekeleze? Mbowe au mkwe wake au vibaraka wa mbowe? Na watueleze ni kwa nini zitto alijitoa kuwa signatory kama si ufisadi wa mbowe na kufanya chama mali yake ikiwemo kukiuzia chama magari chakavu..kukikopesha chama ruzuku kama pesa yake..etc chadema ni saccos ya mbowe na mtei full stop vbaraka wengne wa mbowe njaa zinawasumbua mwsho umefka go zito go zito toa uozo chadema si mama yako wala baba yako..mvuto wa zitto kisiasa na uwezo wake wa kujenga hoja ndio umeifksha chadema pale ilipo toka enzi za buzwagi saga adi leo...chadema masalia wanaoshinda ufipa ni waganga njaa ndio maana mbowe anawawin kirahisi...mbowe si mwanasiasa ni bussines man na silaha anatafta pensheni kwa hili mnyka na umeonyesha udhaifu sana kwa sababu silaha tunajua alishakuwa mtumwa wa mbowe na mtei wewe nawe umeingia uko mnyka kuwa saccos member?
   Your brain matches your name perfectly...

  3. #22
   Suip's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st September 2010
   Posts : 415
   Rep Power : 654
   Likes Received
   65
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By Salary Slip View Post
   Hivi mzazi wako au mtu yoyote utamdharau kwasababu tu ya elimu yake ndogo??!!

   Raisi Mwinyi alikuwa na elimu gani alipokuwa Raisi wa nchi hii?

   Acheni unafiki na kuendekeza siasa kwenye kila jambo!
   Wakati ule sio leo kila wakati na mambo yake mwaka 1985-1995 ni historia nyingine,ilikuwa mfumo wa chama kimoja leo mfumo wa vyama vingi.

  4. expirience man's Avatar
   Member Array
   Join Date : 16th November 2013
   Posts : 61
   Rep Power : 418
   Likes Received
   14
   Likes Given
   11

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Kama hujui taratibu za ukaguzi wa hesabu tafadhari waombe watu wakusaidie

  5. Mjuni Lwambo's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 25th April 2012
   Location : Lyamidati-Shinyanga.
   Posts : 4,748
   Rep Power : 91272205
   Likes Received
   1533
   Likes Given
   1528

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Quote By Chasha View Post
   Kwanza wanawachelewesha sana, Tusha Choka nao,
   Ndoto za CCM za kuweka mwenyekiti kibaraka ndio zinayeyuka hivi hivi wakiona.
   FAITH backed by ACTION towards fulfilling a definite major purpose is a form of wisdom, and THOUGHT concentration on a definite purpose is POWER!

  6. tunalazimika's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th November 2010
   Posts : 1,093
   Rep Power : 783
   Likes Received
   249
   Likes Given
   119

   Default

   Quote By muheza2007 View Post
   Watu wanapigana na ukweli, hivi mwenye elimu ndogo tumuiteje?
   profeseriiiiiii au DJ


  7. Makete Kwetu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th January 2012
   Posts : 526
   Rep Power : 608
   Likes Received
   158
   Likes Given
   51

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Quote By Young Tanzanian View Post
   Na watueleze ni kwa nini zitto alijitoa kuwa signatory
   We mtu usijitoe ufahamu kwa maksudi...kama hujusikiliza vuzuri press ya jana Zitto hakuwahi kuwa signatory...subili ndumila kuwili wako aje atoa ufafanuzi ndo uanze kutoa povu....

  8. asakuta same's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd March 2011
   Posts : 15,063
   Rep Power : 429499989
   Likes Received
   4907
   Likes Given
   4521

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Zitto hahisi aibu kutetewa na CCM?

  9. sempa101's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th June 2013
   Posts : 365
   Rep Power : 503
   Likes Received
   59
   Likes Given
   0

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Tatizo la cdm wote waliobaki wanawaogopa mtei,mbowe slaa mtumwa tu wa mtei na mbowe

  10. Dr Emma John's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th May 2013
   Posts : 720
   Rep Power : 578
   Likes Received
   162
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By Adharusi View Post
   Nimegundua watu wanachuki binafsi na Zito,hawataki ukweliii:vijana Wachadema si walisema Shibuda aliwaambia kipindi kile kesi ya Ugaidi,Waseme wametumwa na Mbowe na Slaa,ukitaka kujua ni unafiki wa kina Kileo na wenzao ndo huu,kwa akili ya kawaida kama yale maneno yana ukweli nani anakigawa CHAMA?????????
   Tuache UNAFIKI
   Samahani lakini,nirudi katika waraka nimeusoma huu waraka mara nyingi,sioni tatizo,zaidi ya kuwa na mambo mazuri kwa Chadema yenye afya kama yatafanyiwa kazi,bila hata Zito kuwa kiongozi,mimi kutoka Moyoni nataka Slaa na Mbowe waondoke katika Uongozi,pia Zito asiwe kiongozi wote wabaki kuwa washauri na wajumbe
   Nakubali Zitto Kabwe ana Udhaifu wake lakini Mbowe na Slaa sio Malaika!
   Swali kwa Wadau maana huu waraka tumejadili kihisi kumuhusu Zitto wakati yeye ajauandaa,Je ikitokea ukakamatwa waraka unamuhusisha Mbowe kutaka kusiwe na Ukomo katika nafasi ya Uenyekiti je mbowe achukuliwe Hatua gani????
   Toka asubuhi mpaka sasa unacopy na kupaste maneno hayahaya kama kasuku pimbi wewe! Kama huna cha kuandika si uwe msomaji tu?

  11. amakyasya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th June 2013
   Posts : 3,462
   Rep Power : 3076408
   Likes Received
   846
   Likes Given
   173

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Quote By Adharusi View Post
   Nimegundua watu wanachuki binafsi na Zito,hawataki ukweliii:vijana Wachadema si walisema Shibuda aliwaambia kipindi kile kesi ya Ugaidi,Waseme wametumwa na Mbowe na Slaa,ukitaka kujua ni unafiki wa kina Kileo na wenzao ndo huu,kwa akili ya kawaida kama yale maneno yana ukweli nani anakigawa CHAMA?????????
   Tuache UNAFIKI
   Samahani lakini,nirudi katika waraka nimeusoma huu waraka mara nyingi,sioni tatizo,zaidi ya kuwa na mambo mazuri kwa Chadema yenye afya kama yatafanyiwa kazi,bila hata Zito kuwa kiongozi,mimi kutoka Moyoni nataka Slaa na Mbowe waondoke katika Uongozi,pia Zito asiwe kiongozi wote wabaki kuwa washauri na wajumbe
   Nakubali Zitto Kabwe ana Udhaifu wake lakini Mbowe na Slaa sio Malaika!
   Swali kwa Wadau maana huu waraka tumejadili kihisi kumuhusu Zitto wakati yeye ajauandaa,Je ikitokea ukakamatwa waraka unamuhusisha Mbowe kutaka kusiwe na Ukomo katika nafasi ya Uenyekiti je mbowe achukuliwe Hatua gani????
   Kama umeusoma waraka huo na huoni tatizo lolote,kwa nini ulifanywa kuwa wa siri? Tatizo wewe ni shabiki wa Zitto hata kama amekosea unashabakia tu.Hauna tofauti na shabiki wa mpira ambaye timu yake ikifungwa bado anaishabikia tu.

  12. #31
   Rubi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th October 2009
   Posts : 1,603
   Rep Power : 941
   Likes Received
   246
   Likes Given
   197

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Quote By Salary Slip View Post
   Nimegundua ni vigumu kwa Zitto na Kitilla kusalimika baada ya kusoma kauli hii iliyotolewa na Lissu kwa waandishi jana.

   Habarileo limemnukuu Lissu kama ifuatavyo:

   "Waraka huu umetoa matusi mazito dhidi ya Mwenyekiti wetu,ikiwamo kuitwa kuwa ana elimu ya chini na ana akili ndogo na nzito,halafu mtu huyo huyo alietoa matusi hayo dhidi ya kiongozi wake wa chama anadai eti anakiheshimu chama,kwa hili tumewashitukia,"alisema.

   Ndugu mwana JF kama kweli hii ndio kauli kwenye waraka huo kuna kusalimika hapa?

   Ni vigumu kwa Zitto na Kitila kusalimika kuliko ilivyo vigumu kwa Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
   Maskini wanatia huruma. Wao wakiwaambia wengine wanaakili ndogo ni sawa. Ila wakiambiwa wao ukweli wanawayawaya eti matusi. Kweli haya ni maajabu ya LEMA. BASI NGOJA MIMI NISEME MBOWE ANA AKILI KUBWA SIO NDOGO.
   Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee.

  13. Ngongo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th September 2008
   Location : Mlima Meru
   Posts : 9,589
   Rep Power : 244522924
   Likes Received
   6584
   Likes Given
   7152

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Mtaanzisha thread nyingi mwisho wa siku Zitto atatakiwa kujibu tuhuma zake ndani ya siku 14 tangu akabidhiwe barua yake.

  14. amakyasya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th June 2013
   Posts : 3,462
   Rep Power : 3076408
   Likes Received
   846
   Likes Given
   173

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Quote By Simiyu Yetu View Post
   Ndiyo tatizo la watanzania mtu anaelimu ndogo anataka kuitwa anaelimu kubwa mambo gani haya.
   Bora elimu ndogo lakini uwe na hekima,kuliko elimu kubwa bila hekima vinginevyo maraisi wetu wangekuwa maprofesa na mawaziri wenye mamasters.

  15. Zogwale's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th July 2008
   Posts : 10,955
   Rep Power : 201427449
   Likes Received
   3113
   Likes Given
   1323

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Hivi katika makosa hayo 11 hakuna la hukumu ya kunyongwa hadi kufa???? Hawatakiwi waendelee kueneza virusi!!! Kirusi katika chama ni hatari sana hiki!!!
   "Kama unaingia Ikulu kwa njia ya rushwa, je ni biashara gani iko huko ya kuwezesha kulipa fadhila ya rushwa hiyo???"

  16. kibaravumba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st December 2012
   Posts : 2,103
   Rep Power : 35268
   Likes Received
   660
   Likes Given
   44

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Quote By muheza2007 View Post
   Watu wanapigana na ukweli, hivi mwenye elimu ndogo tumuiteje?
   Hivi mwanao akikuambia mk¤nd.u wako utacheka cheka tu kwa vile unao?Au niweke picha ndo uelewe?maana unajitoa ufahamu makusudi tu.

   Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

  17. gongolamboto's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd February 2011
   Posts : 332
   Rep Power : 615
   Likes Received
   66
   Likes Given
   70

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Quote By fikirikwanza View Post
   Kama mahesabu ya CDM hayajakaguliwa sio suala la CDM, ni suala la CAG na msajili wa vyama; sasa CDM iingekuwa inawafuata waje kufanyakazi yao??? je ndo kazi zinafanyika hivyo??? hilo suala kamwe haliwezi kuwa la CDM ni watu wajinga tu kama wasaliti wanaweza kufikiria hilo ni la chama wakati ni la wenye majukumu hayo.
   Wewe kweli ----- sana. Unafanya kazi wapi? Taasisi za serikali au taasisi zote zinazopata pesa toka serikalini zina jukumu la kuhakikisha kwamba hesabu zao zinakaguliwa na CAG. Umeelewa wewe -----. Mnaongea vitu msivyovijua mbwa nyie, mnanikera sana. CDM,CCM ,TLPna wajinga wengine kama unavyowaita walitakiwa kuhakikisha hesabu zao zinakaguliwa na CAG. Hiyo ni pesa yetu walipa kodi, inaliwa na wapiga kelele na waanzisha maandmano tu. Kuna adhabu stahili zinazopaswa kuchukuliwa kwa taasisi yoyote ambayo haijakaguliwa na CAG ikiwa ni pamoja na adhabu ya kifungo kwa wahusika.
   A Conference is a gathering of important people who individually can't do
   anything but together can decide that nothing can be done

  18. Tarime2015's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 26th November 2013
   Posts : 8
   Rep Power : 406
   Likes Received
   22
   Likes Given
   2

   Default

   Quote By COARTEM View Post
   RED: Huo ndiyo utakuwa muafaka wa msingi ili kuunganisha wanachama wote.
   GREEN:100% nakubaliana na wewe.
   BLUE: Watasema umetengenezwa na CCM,TISS wakishirikiana na ZZK.
   Cha ajabu sisi wana chadema hatutaki kusikia wala kukemea maovu ya Mbowe.

  19. Salary Slip's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd April 2012
   Posts : 9,882
   Rep Power : 348571074
   Likes Received
   6031
   Likes Given
   3859

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Quote By kibaravumba View Post
   Hivi mwanao akikuambia mk¤nd.u wako utacheka cheka tu kwa vile unao?Au niweke picha ndo uelewe?maana unajitoa ufahamu makusudi tu.

   Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
   Huu ni mfano sahihi kabisa kwa watu kama hawa.

   Akileta ubishi mtumie picha kwa PM

  20. Jeremiah's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th February 2009
   Location : Geita
   Posts : 633
   Rep Power : 780
   Likes Received
   113
   Likes Given
   128

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Quote By Young Tanzanian View Post
   hahahaahaha...kwa speech ya lisu tayari zitto anahujumiwa...eti hatutaki kuweka tuhuma wazi ila si alizozisema zitto na dk.mkumbo...eti ukiwa na nia ya kugombea unaandka barua kwa katibu mkuu hivi kweli kuna kitu kama hicho dunia ipi..et ohh zito ajawahi kuhoji pesa za sabodo na ruzuku kwenye vikao vya chama..sasa atahoji ili nani atekeleze? Mbowe au mkwe wake au vibaraka wa mbowe? Na watueleze ni kwa nini zitto alijitoa kuwa signatory kama si ufisadi wa mbowe na kufanya chama mali yake ikiwemo kukiuzia chama magari chakavu..kukikopesha chama ruzuku kama pesa yake..etc chadema ni saccos ya mbowe na mtei full stop vbaraka wengne wa mbowe njaa zinawasumbua mwsho umefka go zito go zito toa uozo chadema si mama yako wala baba yako..mvuto wa zitto kisiasa na uwezo wake wa kujenga hoja ndio umeifksha chadema pale ilipo toka enzi za buzwagi saga adi leo...chadema masalia wanaoshinda ufipa ni waganga njaa ndio maana mbowe anawawin kirahisi...mbowe si mwanasiasa ni bussines man na silaha anatafta pensheni kwa hili mnyka na umeonyesha udhaifu sana kwa sababu silaha tunajua alishakuwa mtumwa wa mbowe na mtei wewe nawe umeingia uko mnyka kuwa saccos member?
   Umeambiwa tuhuma ziko kwenye barua walizoandikiwa. Na huenda zikawekwa wazi baada ya watuhumiwa kutoa utetezi wao. Sasa huelewi nini au ulisha amua kufa na ccm. Mtu afukuzwe CDM wanaosikikitika na kulia ccm. I can not imagine.

  21. Edward Sambai's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th November 2013
   Posts : 1,534
   Rep Power : 421989
   Likes Received
   825
   Likes Given
   111

   Default re: Haya ndiyo Makosa 11 anayotuhumiwa Zitto Kabwe na chama chake cha CHADEMA...

   Jambo la muimu hapa kwa wale wote wanaopinga maamuzi ya CC ni kwamba, Je! Msaliti anapokamatwa ni adhabu ipi inayomstaili?


  Page 2 of 25 FirstFirst 123412 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Replies: 62
   Last Post: 24th November 2013, 02:09
  2. Muendelezo wa Zitto Kabwe Kuasi chama?
   By 1800 in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 113
   Last Post: 30th August 2012, 10:03
  3. Haya ndiyo makosa ya Masha kisheria
   By Mzee Mwanakijiji in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 12
   Last Post: 27th February 2009, 12:59

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...