Show/Hide This

  Topic: Amani ya Tanzania: Laana au baraka?

  Report Post
  Page 1 of 8 123 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 151
  1. #1
   Abel's Avatar
   Member Array
   Join Date : 2nd July 2007
   Posts : 16
   Rep Power : 703
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Amani ya Tanzania: Laana au baraka?

   Na Chris Alan

   KATIKA pitapita zangu za kusaka habari nilipata fursa ya kukutana na aliyekuwa mbunge wa Shinyanga Mjini, Leonard Derefa. Mbunge huyu aliwakilisha jimbo hilo kwa vipindi viwili tangu mwaka 1995 hadi 2005, kwa miaka 10 mfululizo alikuwa ni mtu wa kuwafurahisha wenzake pale bungeni. Wengi walikuwa wakimtania kwa jina la Buraza.

   Siku moja nikiwa kwenye gari moja naye kutoka viwanja vya Bunge kwenda Area D, alinieleza kitu kimoja ambacho hadi leo ninakizingatia sana katika kauli zangu ninazotoa. Alisema alipata kuwauliza vijana wa Kisukuma kwamba kauli mbiu ya Shinyanga ni tajiri kwa kusema “chini ni dhahabu na almasi, juu ni pamba na ng’ombe” inawasaidia nini kama wao wenyewe wanaishi katika nyumba za tembe?

   Derefa au Buraza alinieleza kwamba alikuwa hafurahishwi na kauli za vijana kushabikia utajiri wasiokuwa nao. Kwa maana hiyo aliwaka kila atakayesifu utajiri wa mkoa wa Shinyanga ni vizuri akiwa walau anamiliki chochote kati ya hivyo, kwamna ana shamba la pamba, au ana ng’ombe au ana mgodi wake wa dhahabu na almasi, kwa kufanya hivyo kauli mbiu ya kuunadi mkoa huo kwa kubarikiwa vitu hivyo inaweza kuwa na maana kwao.

   Ukweli wa kauli ya Buraza, inaelezeka katika maeneo mengi tu ya maisha yetu ya kila siku. Kuna wengi wetu tunaotamani sana kujinasabisha na mafanikio hata kama katika hayo hatuna chochote tulichochangia au kufaidika nayo.

   Wapo wanaopenda kukaa karibu na wakubwa kwa sababu tu ya kutaka waonekane kwamba nao wamo katika kundi hilo hata kama hawana hata harufu ya ukubwa. Ninachosema hapa ni kama vile alivyosema Buraza kwamba ni faida gani mtu kutamba na kitu fulani hata kama hakina maslahi ya karibu wala ya mbali kwake?

   Kauli ya Buraza wiki hii ilinijia kwa hisia kali zaidi hasa baada ya kubahatika kusoma hotuba ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, aliyoitoa kwenye Umoja wa Matifa juu ya Changamoto za Milenia (MCG).

   Brown ni kiongozi ambaye amekuja na moto mkali zaidi kuhusu nchi masikini kusaidiwa, akiwa anafuata nyayo za mtangulizi wake, Tony Blair. Brown katika hotuba hiyo aliwauliza watu wa mataifa makubwa tajiri duniani kwamba miaka saba ndani ya mkakati wa kupunguza umasikini duniani wamefanya nini kuondoa vikwazo vya kibiashara, kupunguza vifo vya watoto, kuangamiza malaria, ukimwi na VVU, kifua kikuu na changamoto nyingine zinazokabili mataifa ya nchi mamsikini; ili mataifa ya nchi zinazoendelea na hasa Afrika ziishi maisha ya staha zaidi na ya utu?

   Brown aliwakumbusha wakuu wa mataifa hayo tajiri kwamba imebakia miaka minane tu kabla ya kufika mwaka 2015 ambao ndiyo lengo limewekwa kuondoshwa kwa umasikini duniani, lakini kwa bahati mbaya mno, mwelekeo wa mambo hauonyeshi dalili njema. Aliyakumbusha mataifa haya kuwa waaminifu katika ahali walizoweka mwaka 2000 ya kutokomeza umasikini duniani!

   Katika hotuba hiyo, ninayothubutu kutaja kama moja ya hotuba za kutalitakia kila la kheri bara la Afrika na nchi za ulimwengu wa tatu kwa ujumla, Brown alieleza jinsi tatizo la huduma za afya zilivyo ngumu katika nchi za Tanzania, Msumbiji na Malawi. Itakumbukwa kwamba Brown mwaka juzi alitembelea nchi za Afrika nchi hizo hapo juu zikiwamo.

   Aliwasilisha takwimu ambazo sina sababu ya kuzihoji kwamba Tanzania ina madaktari 800, wauguzi 3,600; Malawi madaktari 250 na wauguzi 3,800; wakati Msumbiji ina madaktari 500 na wauguzi 4,000. Kiongozi huyu mpya wa Uingereza taifa linalomwaga misaada ya mabilioni ya fedha na nafasi nyingi za masomo kwa Tanzania kila mwaka, alionyesha kwamba kiwango hicho cha wataalamu wa sekta ya afya ni kidogo sana kwa mataifa haya kuweza kutimiza malengo ya milenia. Kwamba tatizo la kitabibu kwa mataifa haya linaweza kuwa si la kugawa dawa tu bali la kutokuwa na wataalam wa kutosha wa sekta ya afya.

   Kwa ulinganifu wa takwimu za Brown, Tanzania inaelekea kuwa mkiani mwa majirani hao wake kwa nchi za SADC, kwani daktari mmoja Tanzania atahudumia watu 47,500 wakati muuguzi mmoja atahudumia watu 10,555 kwa idadi ya watu milioni 38; Malawi daktari mmoja atahudumia watu 48,000 wakati muuguzi mmoja atahudumia watu 3,157 kwa idadi ya watu milioni 12; na kwa Msumbiji daktari mmoja atahudumia watu 40,000 na muuguzi mmoja watu 5,000 kwa idadi ya watu milioni 20.

   Hali hii ndiyo imeamsha mawazo ya kukumbuka maneno ya Buraza kwamba hivi idadi hii kubwa ya watu na nyimbo hizi za amani na utulivu ambazo tumeimba tangu uhuru, vina maana gani hasa kwetu kama hata mataifa ambayo yalipata kuwa kwenye kundi la failed states yaani mataifa ambayo yalifikia kiwango cha kusambaratika kwa kukosa mwelekeo wa utawala ama kwa sababu ya vita au utawala mbovu yanaweza kutushinda sisi leo hii licha ya kuwa kisiwa cha amani?

   Ninajua wapo watu wenye kiu na nguvu za kutetea amani na utulivu, na ninajua watakereketwa kiasi cha kutoa majibu ya makala hii, lakini naomba niwaulize, hivi hii amani na utulivu miaka yote hii imetusaidia nini hasa?

   Ninauliza haya si kwa sababu sijui maana ya utulivu na amani, ila ninauliza kwa sababu hapa kwetu imekuwa na matokeo hasi (yaani negative correlation) katika maendeleo. Huwezi kuwa na taifa lenye amani, utulivu, ardhi yenye rutuba, madini ya kila aina, watu wengi, maji, mito na mvua za kutosha, na kikubwa zaidi ambayo inafanya uchaguzi wa kubadilishana madaraka kwa amani kila baada ya miaka mitano, halafu ikawa hasongi mbele kwa mwendo wa roketi.

   Hapa ndipo ninashawishika kuchukua maneno ya Buraza Derefa kwamba ni faida gani hasa kutambia vitu hivi?

   Tanzania ilipigana vita mara mbili kuikomboa Msumbiji, vita vya uhuru vilivyomalizika mwaka 1975 kwa Samora Michel kuwa Rais, lakini ikapigana tena vita kuisadia Frelimo dhidi ya Renamo chama kilichoasi chini ya uongozi wa Alfonso Dlakama, gharama yake ni kubwa. Lakini leo tunaelezwa kwamba Msumbuji iliyofikia hatua ya failed state hadi tulipoikomboa mara ya pili sasa imetuacha kama takwimu hizi hapo juu zinavyoonyesha.

   Malawi hata kusimulia inasikitisha, ni nchi iliyoendeshwa kwa mkono wa chuma na Dk Hastings Kamuzu Banda hadi mwaka 1994 Elson Bakili Muluzi aliposhinda uchaguzi wa kwanza na huru wa vyama vingi. Malawi ni nchi masikini kwa maana nyingi. Haina maliasili za maana, haina watu wengi, haina viwanda na pengine chini ya Banda amani ya kweli haikuwako, leo hii eti tunalinganishwa na kufananishwa nayo.

   Ni kutokana na hisia na muonekano huu ninajiuliza swali la Buraza, nini hasa kimetusibu sisi kama taifa? Hatuwezi kusonga mbele kwa kasi inayofanana na sifa ya amani na utulivu wetu kwa nini?

   Wapo watu wanaotaka kujenga hoja kwamba Tanzania inasonga mbele kwenye mstari wa maendeleo kwa kasi inayostahili, hawa kwa hakika ni watu waliopotoka. Kila uchao hali za watu wetu zinazidi kuwa duni, uchumi wetu unazidi kuwa duni, gharama za maisha zinazidi kupaa; hivi ni vitu vya dhahiri. Ni kwa jinsi hii ninafikia hatua ya kujiuliza nap engine kuomba majibu kwa wasomaji wangu na wachangiaji wengine, amani yatu ni baraka au laana?

  2. #2
   Charlo's Avatar
   Member Array
   Join Date : 18th September 2007
   Posts : 15
   Rep Power : 692
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default

   Asilimia mia kwa mia nakubaliana nawe bwana Abel,mimi nu mkenya ninayeishi na kufanya kazi tanzania kwa mda sas wa miaka minane.

   Elimu ndio kitu tu kitakacho okoa taifa hili. Watu wengi huwa hapa hawajui kutofautisha ukweli na uongo. Wakubwa hapa inaonekana wanahaki ya kuchezea raslimali za inchi pasipo hata kuulizwa na mtu yeyote.

   Sio kitu kigeni kuona gari la serikali linafanya kazi binafsi nyakati za weekend na pia usiku watu wanazitembelea kwenda katika sehemu za starehe. Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanafanyika lakini hakuna mtu ambaye amayeweza kuyafichua kwa sababu ya kuogopa, woga ni mwingi sana hasa kwa watanzania, na mtu mwenye woga huwa ni mtu aliye kosa elimu, kwasababu hujui haki zako na hata kama unazijua hujui namna ya kuzitetea.

   Bado nasisitiza kwamba watanzania wakae karibu sana na wakenya kwa ajili ya kusoma jinsi wanavyofanya biashara zao angalau waige ili waendelee mbele.

  3. #3
   Dua's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th November 2006
   Posts : 3,481
   Rep Power : 6476632
   Likes Received
   24
   Likes Given
   1

   Default

   Quote By charlo View Post
   Bado nasisitiza kwamba watanzania wakae karibu sana na wakenya kwa ajili ya kusoma jinsi wanavyofanya biashara zao angalau waige ili waendelee mbele.
   Sasa Charlo wewe ambaye umesoma umeshindwaje kutetea haki zako hapo Kenya? Natumaini ndio sababu kubwa ambayo hata imekufanya kwa miaka takriban 8 uishi Tanzania. Biashara ambayo unasifia ikiiangalia wanaofanya sio wakenya hasa bali mafirauni kutoka nje.

   Tanzania haina sababu ya kuiga dhuluma inayoendekezwa na Kenya kwa hao mafirauni.
   Dua la kuku halimpati mwewe

  4. Mushobozi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th August 2007
   Location : Buzwagi
   Posts : 599
   Rep Power : 812
   Likes Received
   67
   Likes Given
   6

   Default

   Kuhusu hoja ya madaktari na wasomi kuwa wachache linaumiza sana, ila serikali pia imeshtuka na sasa hivi imejaribu kuongeza vyuo vya madaktari, na pia vilivyokuwepo imevipanua zaidi. Kwa hiyo hali itakuwa angalau kuliko ilivyo sasa.

   Mfano chuo kikuu cha Muhimbili kimefanywa kuwa chuo kamili, na kuongeza udahili, wakati vyuo kama KCMC, Kairuki, Bugando, aghakhan n.k pia vitaongeza idadi ya madaktari kuwa wengi zaidi ya hao 800 waliosemwa. Pia inawezekana vijana wa mwaka huu tu wa kwanza kwa ajiri ya udaktari wakawa wanakaribia idadi hiyo oliyotolewa. Tusidhani tuliposema jumuia ya East Africa isubiri kwanza tulikuwa tunapoteza muda, ila inahitaji uvumilivu na ubunifu wa hali ya juu wa viongozi wetu.

   Maendeleo hayaji mara moja, ni step moja hadi nyingine. Hivi kutoka wanafunzi wa chuo kikuu chini ya 8,000 mwaka 1990 hadi zaidi ya 50,000 mwaka huu kadiri ya loan board sio hatua?

   Sitetei rushwa na ubadhirifu wa mali za uma ila ninajaribu kuwaonyesha hao wakenya kwamba kuna maendeleo yanafanyika kwenye nchi yetu. Makosa yalishafanyika nyuma, hata walioyafanya walishayakili, ni sasa kuangalia kipi kifanyike na kwa wakati gani. Sio kwa nini yalifanyika.

   Daktari anasoma miaka 5 hapa tanzania. Sasa hivi imepita miaka 8 ya millenia, tutoe miaka 3 ya kujipanga, ninadhani mwelekeo huu sio mbaya sana kwa nchi yetu kama kamba itaendelea kukazwa. La msingi tujue tu kuwa kuna wakati tutakuwa vinara katika afrika mashariki na kati kiuchumi, maana vijana wetu wanaosoma ndio watakaoshikilia uchumi wa nchi yetu tofauti na kenya ambayo uchumi uko mikononi mwa wageni.
   Maxence Melo likes this.

  5. Masaka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st October 2007
   Posts : 449
   Rep Power : 776
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Najua wengi hapa hawajaona mazuri yaliyofanywa na ccm kutokana na kashfa mbalimbali ambazo zimeibuliwa na wapinzani wa ccm. Jamani ccm imefanya mengi mazuri nchini. Ukilinganisha nchi zingine kama congo na majirani zetu, ccm imetunza amani ya nchi yetu.

   Kwa hili nawapongeza ccm kwa kazi nzuri sana. Hayo mengine ya ufisadi, tumpe muda JK atayashughulikia kabla ya mwaka 2010.

   Hongera ccm, kidumu chama cha mapinduzi.

  6. ZeMarcopolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th May 2008
   Posts : 12,683
   Rep Power : 141699730
   Likes Received
   5200
   Likes Given
   4322

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Ukweli ni kwamba hata nchi zilizoendelea kuliko zote duniani wananchi wake wana malalamiko yao juu ya usimamiwaji na uendeshwaji wa uchumi na mambo mengine, hivyo kuwepo kwa watanzania wasioridhika na utendaji wa CCM ni jambo la kutarajiwa.
   Maxence Melo likes this.
   "To greed, all nature is insufficient"

  7. Mgaya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st October 2007
   Posts : 523
   Rep Power : 791
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By Masaka View Post
   Najua wengi hapa hawajaona mazuri yaliyofanywa na ccm kutokana na kashfa mbalimbali ambazo zimeibuliwa na wapinzani wa ccm. Jamani ccm imefanya mengi mazuri nchini. Ukilinganisha nchi zingine kama congo na majirani zetu, ccm imetunza amani ya nchi yetu.

   Kwa hili nawapongeza ccm kwa kazi nzuri sana. Hayo mengine ya ufisadi, tumpe muda JK atayashughulikia kabla ya mwaka 2010.

   Hongera ccm, kidumu chama cha mapinduzi.
   Hivi mtu ambaye hana chakula wala maji ya hakika ana amani gani?

  8. KadaMpinzani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st January 2007
   Location : Chadema Restaurant
   Posts : 4,980
   Rep Power : 1716
   Likes Received
   28
   Likes Given
   0

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By zemarcopolo View Post
   Ukweli ni kwamba hata nchi zilizoendelea kuliko zote duniani wananchi wake wana malalamiko yao juu ya usimamiwaji na uendeshwaji wa uchumi na mambo mengine, hivyo kuwepo kwa watanzania wasioridhika na utendaji wa CCM ni jambo la kutarajiwa.
   Unajua mkuu hapo umenena ! Lakini wengi humu sidhani kama kweli they get it, yaani hiyo ndio nature of politics, watu wakianza propaganda zao humu kwa kutegemea kwamba watu watakaa kimya au mambo ya sawa mzee tumekusikia, basi safari hii wamenoa. Wengine politiking is just an interest na ndio maana tunaweza tukakaa humu na kudharauliwa kama wengine walivyosema (walizaliwa na dharau unfortunately) tunaweza kuhimili vikumbo vya aina yoyote ile bila ya kutetereka. Lakini mwingine ukimpa jab kidogo tu basi frustrations to the limit. anyway back to the point ni kwamba, CCM up to this point has done what many thought could not be done, and those who say ccm hasnt done anything is because they overexpected things from CCM!

   Tunashukuru tunaishi kwa amani! Wengine wako nchini kwao lakini hawana amani, au sijui watu wanataka kusikia mambo ya Janja Weed Bongo !

  9. KadaMpinzani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st January 2007
   Location : Chadema Restaurant
   Posts : 4,980
   Rep Power : 1716
   Likes Received
   28
   Likes Given
   0

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By Mgaya View Post
   Hivi mtu ambaye hana chakula wala maji ya hakika ana amani gani?
   nani unayemjua wewe hana maji ?? au nani umesikia hana maji ya kunywa wala chakula ?

  10. Mgaya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st October 2007
   Posts : 523
   Rep Power : 791
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By zemarcopolo View Post
   Ukweli ni kwamba hata nchi zilizoendelea kuliko zote duniani wananchi wake wana malalamiko yao juu ya usimamiwaji na uendeshwaji wa uchumi na mambo mengine, hivyo kuwepo kwa watanzania wasioridhika na utendaji wa CCM ni jambo la kutarajiwa.
   hivi nchi zilizoendelea nazo zina mambo ya buzwagi, na vijisenti?

  11. ZeMarcopolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th May 2008
   Posts : 12,683
   Rep Power : 141699730
   Likes Received
   5200
   Likes Given
   4322

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By Mgaya View Post
   hivi nchi zilizoendelea nazo zina mambo ya buzwagi, na vijisenti?
   Kwa sana tu, wewe uko nchi gani?
   Au unataka mfano toka nchi gani nikuletee?
   "To greed, all nature is insufficient"

  12. KadaMpinzani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st January 2007
   Location : Chadema Restaurant
   Posts : 4,980
   Rep Power : 1716
   Likes Received
   28
   Likes Given
   0

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By Mgaya View Post
   hivi nchi zilizoendelea nazo zina mambo ya buzwagi, na vijisenti?
   nchi gani isiyokuwa na scandal ??

  13. Masaka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st October 2007
   Posts : 449
   Rep Power : 776
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By KadaMpinzani View Post
   Unajua mkuu hapo umenena ! Lakini wengi humu sidhani kama kweli they get it, yaani hiyo ndio nature of politics, watu wakianza propaganda zao humu kwa kutegemea kwamba watu watakaa kimya au mambo ya sawa mzee tumekusikia, basi safari hii wamenoa. Wengine politiking is just an interest na ndio maana tunaweza tukakaa humu na kudharauliwa kama wengine walivyosema (walizaliwa na dharau unfortunately) tunaweza kuhimili vikumbo vya aina yoyote ile bila ya kutetereka. Lakini mwingine ukimpa jab kidogo tu basi frustrations to the limit. anyway back to the point ni kwamba, CCM up to this point has done what many thought could not be done, and those who say ccm hasnt done anything is because they overexpected things from CCM!

   Tunashukuru tunaishi kwa amani! Wengine wako nchini kwao lakini hawana amani, au sijui watu wanataka kusikia mambo ya Janja Weed Bongo !
   Nimefurahi kuona wana ccm mnajitokeza hadharani na kutetea chama. Asante sana Kada, zema, kubwajinga, kuhani mkuu, mapambano, na wengine wote.

   Kidumu chama cha mapinduzi
   Mheshimiwa Kikwete fukuza mafisadi toka kwenye chama na uachane na wana mtandao.

  14. Masaka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st October 2007
   Posts : 449
   Rep Power : 776
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By Mgaya View Post
   hivi nchi zilizoendelea nazo zina mambo ya buzwagi, na vijisenti?
   Hayo mambo yote uliyosema ni ya kawaida. Wizi umeshafanyika lakini sasa tumpe Kikwete hadi 2010 ashughulikie nchi.
   Mheshimiwa Kikwete fukuza mafisadi toka kwenye chama na uachane na wana mtandao.

  15. KadaMpinzani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st January 2007
   Location : Chadema Restaurant
   Posts : 4,980
   Rep Power : 1716
   Likes Received
   28
   Likes Given
   0

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By Masaka View Post
   Hayo mambo yote uliyosema ni ya kawaida. Wizi umeshafanyika lakini sasa tumpe Kikwete hadi 2010 ashughulikie nchi.
   wow ! i was tooo tired of the rhetoric----na propaganda zao !!

  16. Masaka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st October 2007
   Posts : 449
   Rep Power : 776
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By KadaMpinzani View Post
   wow ! i was tooo tired of the rhetoric----na propaganda zao !!
   wapinzani walizidi hapa kwa propaganda zao. Hizi kashfa zote na habari za kutunga wanazoleta hapa zimekutana na kigingi cha kadampinzani and the gang. Tujipange vizuri tu tutawazidi hata hapa JF.
   Mheshimiwa Kikwete fukuza mafisadi toka kwenye chama na uachane na wana mtandao.

  17. BAK's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th February 2007
   Location : Mfaranyaki
   Posts : 40,020
   Rep Power : 429505153
   Likes Received
   21523
   Likes Given
   23298

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By Masaka View Post
   Najua wengi hapa hawajaona mazuri yaliyofanywa na ccm kutokana na kashfa mbalimbali ambazo zimeibuliwa na wapinzani wa ccm. Jamani ccm imefanya mengi mazuri nchini. Ukilinganisha nchi zingine kama congo na majirani zetu, ccm imetunza amani ya nchi yetu.

   Kwa hili nawapongeza ccm kwa kazi nzuri sana. Hayo mengine ya ufisadi, tumpe muda JK atayashughulikia kabla ya mwaka 2010.

   Hongera ccm, kidumu chama cha mapinduzi.
   Duh! Sasa huu ni ufisadi wa kifikra!!! Muafaka unagomba na maneno yanayoashiria kuvunjika amani yanatolewa kati ya pande zote mbili zinazohusika katika mazungumzo ya muafaka. Juzi tu manjangu vinaa waliingia katika nyumba mbali mbali na kuwadaka wazee na kuwaficha ambako hata ndugu zao walikuwa hawajui wamefichwa wapi. Hadi kulipokuwa na rumours kwamba wapemba 10,000 wamejiandaa kuvamia kituo cha polisi ndipo hao jamaa wakaachiwa.

   Tanganyika nako kila kona ni mazungumzo ya mafisadi jinsi wanavyoiangamiza nchi. Ufisadi ambo umekishirikisha pia chama cha mafisadi katika kuchota mabilioni ya shilingi na huku Watanzania walio wengi wakiishi katika maisha ya dhiki. Mkuu wa polisi na Mwanasheria Mkuu wa sirikali walidai kwamba kukamatwa kwa mafisadi kunaweza kusababisha nchi ikalipuka. Kwa maneno mengine mafisadi waachwe tu waiangamize Tanzania maana kuwatia hatiani mafisadi nchi inaweza kabisa kuwaka moto!!!!

   Nchi ambayo haina sheria, wezi wa mabilioni ambayo wameyaweka ndani na nje ya nchi na kununua majumba ya kifahari, magari ya kifahari ndani na nje ya nchi lakini hakuna wakuwagusa!!!! Wananchi wananung'unika kuhusu mafisadi, lakini hakuna anayewajali wala kuwasikiliza. Wanakuja na kuondoka kama vile kila kitu kiko shwari. Leo wako Japan, kesho wako US, kesho kutwa wako UK ili mradi hawajali kelele na manung'ununiko ya wananchi.

   Halafu wewe bila haya wala aibu eti unawapongeza mafisadi na chama chao cha kifisai kwa kulinda amani ya nchi!!!! Ama kweli ukistaajabu ya hayawani utaona ya taahira.

   Wazungu walisema,"If you have nothing important to say it is better to keep quiet." wala hawakukosea!!! Duh!!!! Naam bila wasi wasi wowote huu ni ufisadi wa kifikra.
   Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

  18. Masaka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st October 2007
   Posts : 449
   Rep Power : 776
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   mimi natetea amani na utulivu. hayo mengine yote yatakuja tu kabla ya 2010
   Mheshimiwa Kikwete fukuza mafisadi toka kwenye chama na uachane na wana mtandao.

  19. Masaka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st October 2007
   Posts : 449
   Rep Power : 776
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By Mgaya View Post
   Masaka anadhani kuwa hali ya watu kutopigana tu ndio amani. sijui atasema nini kuhusu mauaji ya pemba ya mwaka 2001
   mauaji haya yako kila sehemu wa wakorofi lazima wadhibitiwe.
   Mheshimiwa Kikwete fukuza mafisadi toka kwenye chama na uachane na wana mtandao.

  20. Mgaya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st October 2007
   Posts : 523
   Rep Power : 791
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Hongera ccm kwa kazi nzuri ya kulinda amani ya nchi

   Quote By Masaka View Post
   mauaji haya yako kila sehemu wa wakorofi lazima wadhibitiwe.
   waliouwawa sio wakorofi. Ina maana unatetea mauaji?

  Page 1 of 8 123 ... LastLast

  LinkBacks (?)

  1. 16th June 2011, 22:22

  Similar Topics

  1. TANZANIA: Baraka na laana
   By whizkid in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 0
   Last Post: 22nd November 2011, 11:46
  2. Dhahabu yagunduliwa Kusini: Laana au Baraka kwa 'Wamachinga'?
   By Udadisi in forum Jukwaa La Biashara na Uchumi
   Replies: 18
   Last Post: 27th June 2011, 23:27
  3. Tanzania ni laana au viongozi?
   By Mkombozi in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 27
   Last Post: 8th December 2010, 00:06
  4. Dunia ya utandawazi laana au faida kwa tanzania
   By ChingaMzalendo in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 1
   Last Post: 21st July 2010, 06:18

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...