JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

  Report Post
  Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast
  Results 21 to 40 of 119
  1. #1
   R.B's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th May 2012
   Posts : 4,428
   Rep Power : 0
   Likes Received
   1245
   Likes Given
   746

   Default JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limevitaka vyombo vya habari kuacha kuandika taarifa za mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), badala yake taarifa rasmi zitakuwa zikitolewa na jeshi hilo kila baada ya wiki mbili.

   Katazo hilo limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Meja Erick Komba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya mgogoro huo.

   Alisema hali hiyo inatokana na jeshi hilo kubaini kuwa baadhi ya vyombo vya habari nchini vinaandika habari za uchochezi zinazotaka kuziingiza vitani nchi ya Tanzania na Rwanda.

   Meja Komba alisema hategemei kama kutakuwa na chombo chochote cha habari kitakachotoa habari kuhusu maendeleo ya mgogoro huo bila kupata taarifa rasmi kutoka jeshi hilo.

   Alionya kuwa chombo chochote kitakachokwenda kinyume kitakuwa kina tatizo.
   Meja Komba alisema wananchi wanapaswa kuelezwa kuwa kikosi cha Tanzania kilichoko DRC ni sehemu ya Brigedia ya SADC, iliyotoa mchango wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa (Monusco).

   Alitaja majukumu ya kikosi hicho kuwa ni kuzuia waasi wa M23 na wengine kujitanua, kuvunja nguvu zao na kuyapokonya silaha makundi yote ya waasi.
   “Kwa kuzingatia kuwa kikosi chetu kiko chini ya majeshi ya Monusco, inamaanisha kuwa operesheni hiyo ni ya Umoja wa Mataifa,” alisema.

   Aliongeza kuwa Tanzania haikupeleka kikosi chake DRC kwa ajili ya kupigana na M23, pia ieleweke kuwa haina tatizo na Rwanda kuhusiana na operesheni hiyo ambapo Rwanda ilitoa ridhaa kikosi cha Tanzania kwenda DRC.

   Meja Komba alisema Rwanda ni miongoni mwa wanachama wa nchi za Maziwa Makuu, ambayo imesaidia kwa kuruhusu kikosi cha Tanzania kupitisha vifaa na zana katika nchi yake kupeleka DRC.

   “Tanzania inashiriki katika operesheni hiyo ya ulinzi wa amani nchini DRC kutokana na mgogoro kati ya serikali na waasi hususan kikundi cha M23,” alisema.
   Mgogoro huo ulianza Aprili mwaka jana, ambapo kikundi cha M23 kilijitoa katika jeshi la serikali na kuanzisha mapigano yaliyosababisha hali ya usalama nchini DRC kuwa mbaya.

   Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe Benard, amesema kuwa marais Jakaya Kikwete na Paul Kagame wa Rwanda wamemaliza tofauti zilizokuwa zimejitokeza kati yao hivi karibuni.
   Marais hao walikutana na kufanya kikao cha faragha jijini Kampala nchini Uganda juzi baada ya mkutano wa viongozi wa nchi za Maziwa Makuu na baadaye kutoa taarifa kwa waandishi wa habari.

   Kuzorota kwa mahusiano kati ya viongozi hao kulikuja kufuatia kauli ya Rais Kikwete ya kumtaka Rais Kagame kukaa meza moja na vikundi vya waasi wa nchi yake vilivyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ushauri ulioonekana kumkera Rais Kagame.

   Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Membe alisema marais hao walitumia mazungumzo yao yaliyochukua muda wa saa moja kujadiliana na kueleweshana mambo mbalimbali yaliyosababisha kutoelewana.
   “Baada ya mkutano huo ambao uliwapa fursa za kuchambua, kujadili na kurejesha mahusiano ya kihistoria kati ya nchi hizi mbili, marais wetu walitoka na nyuso za furaha,” alisema.

   Moja ya maazimio ya kikao chao ni kuwa na vikao vingine kati ya Rwanda na Tanzania katika siku zijazo.

   “Kwa kweli kikao kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame kimeondoa majungu yote, kimekata fitina, uongo na maneno ya kuchombeza yaliyokuwa yakitawanywa na watu mbalimbali hapa nchini na hata kule Kigali,” alisema.

   Mbali ya kikao hicho pia Rais Kikwete alifanya kikao kingine cha faragha na Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambapo walipata muda wa kujadiliana kwa kina kuhusu mambo mbalimbali kuhusu nchi zao na mambo ya migogoro katika nchi za Maziwa Makuu.

   Akizungumzia yale yaliyokubaliwa katika mkutano wa viongozi wa nchi za Maziwa Makuu, Membe alisema kuwa mkutano huo kwanza ulimruhusu Rais Museveni aendelee kusuluhisha vita ya serikali ya DRC na waasi.

   Alisema kuwa viongozi hao walilaani mashambulizi ya M23 yaliyojeruhi na kumuua Meja Mshindo wa Tanzania aliyekuwa miongoni mwa askari walioko nchini Congo katika kusimamia amani chini ya Umoja wa Mataifa.


  2. chief_mtemi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd June 2013
   Posts : 529
   Rep Power : 533
   Likes Received
   113
   Likes Given
   0

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Mimi siachi hata na nitakuwa na post humu na mods wakiwa wanafuta nitakuwa na wapm tu.huwezi kumpangia mtu jinsi ya kupata habari anayoitaka kwann iwe kwa tz wakati bbc aljazeera VOA n.k wanaendelea kuto taarifa jamani wana jf huu si u k.sasa huyu kaja na amri za kijeshi ambazo hazitekelezeki uraiani

  3. figganigga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th October 2010
   Location : dar es salaam
   Posts : 12,507
   Rep Power : 166336936
   Likes Received
   5643
   Likes Given
   15533

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Itakua dunia nzima au tanzania tu? Mimi nikizicopy kutoka bbc au telegraph itakuwaje?. wanatuonea. Tanzania tuna haki ya kupata habari. Mia
   We live in stronger world where the poor walk miles to get food, and the rich walk miles to digest food

  4. uvugizi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th October 2012
   Location : Tabora-Bujumbura-Kigoma
   Posts : 852
   Rep Power : 634
   Likes Received
   279
   Likes Given
   284

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   labda kikwete na kagame wameambiana kuwa tunachonganishwa . lakini wao wana wajibu wa kupima taarifa mimi naona bado hawajapatana kidhati na ndiyo maana wamekurupuka , itakuwa kila mmoja anasema mimi nimesikia toka TZ/RW unanilaumu kulikoni mzee mwenzangu, sasa hapo soon utasikia na rwanda wanakataza taarifa za jeshi kuripotiwa wakihisi eti ni kahatua kamaridhiano. kumbe mtusi ansubiria kumi na nane zake zitimie

  5. Echolima's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th October 2007
   Posts : 2,345
   Rep Power : 85904426
   Likes Received
   745
   Likes Given
   1137

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Mimi binafsi toka awali nilikuwa napinga sana watu kushabikia VITA na Rwanda wengine hata walikuwa hawaitambui MONUSCO Badala yake kila M23 wanapopigwa na Majeshi ya Monusco vyombo vyetu vya habari Vilitoa HONGERA kwa JWTZ ni sawa maana nao ni sehemu ya Monusco.Lakini kitendo cha kusema askari wetu wa JWTZ waende mpaka KIGALI hii haikubaliki kabisa.Na kuhusu hili katazo JWTZ wamechelewa sana kulitoa hasa ukichukulia na Teckinologia ya leo hili katazo halina maana kabisa.

  6. Kimbunga's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 4th October 2007
   Location : Jimboni kusaka ridhaa
   Posts : 10,998
   Rep Power : 7214
   Likes Received
   5186
   Likes Given
   1702

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Quote By UmkhontoweSizwe View Post
   Amri za kikomunisti kumbe bado zipo?!
   Dawa siyo kuzuia kuandika, dawa ni kuwachukulia hatua za kimaadili na kisheria wale wanaoandika habari za uzushi au za kutunga.
   Wanajeshi wetu wako vitani, lakini mnataka habari tuwe tunapata baada ya wiki mbili! Jeshi lisifanye upuuzi kama wa wanasiasa. Kunatakiwa kuwe na briefing kila siku.
   Duh JF sijui nacho ni chombo cha habari! Kama ndivyo ina maana nayo imepigwa marufuku?


  7. Deo Corleone's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th June 2011
   Posts : 11,913
   Rep Power : 96234
   Likes Received
   4581
   Likes Given
   1221

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   ujinga!

  8. Vianelly Vian's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th July 2011
   Posts : 324
   Rep Power : 591
   Likes Received
   76
   Likes Given
   20

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Quote By Bramo View Post
   JF itakuwa excluded katika hilo katazo.
   Watatusamehe kwa hilo
   Nilikuwa sijajua kumbe wewe ndiye mmiliki Wa jf du hongera mkuu na tunashukuru kwa tamko lako

  9. Crashwise's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd October 2007
   Location : Safarini
   Posts : 21,080
   Rep Power : 372936426
   Likes Received
   7647
   Likes Given
   4407

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   nikisema jwtz limejaa wabalaji akina R.B na wapuuzi wenzako mnanishambulia kwa matusi haya sasa andika tena habari za wabakaji kwenye kigazeti uone watakavyo kubaka kama walivyo wafanyia wana mtwara..

  10. manucho's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st April 2012
   Posts : 3,411
   Rep Power : 1248
   Likes Received
   92
   Likes Given
   1

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Amri za Geshi bana au nao siasa ndiyo zimeshaingia geshini?? Wasije wakatofautiana kesho ukamsikia Membe anatoa taarifa ya Geshi.
   Haya geshi tumemisikieni vizuri, vp kuhusu CNN,BBC,DW,UBC,CITIZEN etc nao mmeahawaambia wasitoe habari yoyote au tukiona hizo habari kwenye TV tufunge macho na kwenye radio tuzibe masikio tukisikia hizo habari???
   Geshi hizi zama nyingine ktk khabari.

  11. Crashwise's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd October 2007
   Location : Safarini
   Posts : 21,080
   Rep Power : 372936426
   Likes Received
   7647
   Likes Given
   4407

   Default

   Quote By Echolima View Post
   Mimi binafsi toka awali nilikuwa napinga sana watu kushabikia VITA na Rwanda wengine hata walikuwa hawaitambui MONUSCO Badala yake kila M23 wanapopigwa na Majeshi ya Monusco vyombo vyetu vya habari Vilitoa HONGERA kwa JWTZ ni sawa maana nao ni sehemu ya Monusco.Lakini kitendo cha kusema askari wetu wa JWTZ waende mpaka KIGALI hii haikubaliki kabisa.Na kuhusu hili katazo JWTZ wamechelewa sana kulitoa hasa ukichukulia na Teckinologia ya leo hili katazo halina maana kabisa.
   sasa umeandika nini maana naona umejikanyaga tu..

  12. Precise Pangolin's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 4th January 2012
   Posts : 10,549
   Rep Power : 408525
   Likes Received
   2564
   Likes Given
   955

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Quote By Crashwise View Post
   nikisema jwtz limejaa wabalaji akina R.B na wapuuzi wenzako mnanishambulia kwa matusi haya sasa andika tena habari za wabakaji kwenye kigazeti uone watakavyo kubaka kama walivyo wafanyia wana mtwara..
   Mkuu Crashwise hawa akina R.B ndio wabakaji wakubwa huko Mtwara

  13. Stoudemire's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th March 2012
   Posts : 849
   Rep Power : 662
   Likes Received
   189
   Likes Given
   1596

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Nadhani heading imekosewa kwakuwa jeshi halina mamlaka hayo.

   Itakuwa jeshi limevitaka/kuviomba vyombo vya habari kuacha kuandika taarifa za kichochezi.

  14. C programming's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th November 2011
   Location : kenya
   Posts : 1,141
   Rep Power : 700
   Likes Received
   325
   Likes Given
   18

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Quote By gfsonwin View Post
   hivi hili ndilo suluhisho kweli?? Ama kweli tz bado sana

   nina support sana ila daa kwa hili sidhani inaweza ikawa ni suluhisho kwa karne hii maana kwa uzoefu wangu kukaa na jamii siku hizi taarifa wanachi wengi kupitia hivi wanachi lazima watapeana taarifa tuu kwa njia hizi hata kama mtu hana t.v
   1.facebook
   2.yotube
   3.blogs tofauti
   4.aljazeera/sky news/bbc
   5.twitter
   6.whats up
   7.redio mbaoo
   8.vijiwe vya wazee kahawa
   9.vijiwe vya bangi na sigara
   10.vilabu vya pombe haramu
   11.kwenye madaladala
   12.vijiwe vya wazee wacheza bao na karata
   13.vijiwe vya pool table

   ushauli wangu....ni kutoa elimu wa wananchi ..ya kujielewa....ni vigumu sana kuzuia watu kupeana taarifa japo zipo za ukweli na nyingine si za kweli na zingine uchochezi

  15. Mwl.RCT's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd July 2013
   Location : http://bit.ly/MWLRCT
   Posts : 3,648
   Rep Power : 104008027
   Likes Received
   1195
   Likes Given
   340

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Quote By UmkhontoweSizwe View Post
   Amri za kikomunisti kumbe bado zipo?!
   Dawa siyo kuzuia kuandika, dawa ni kuwachukulia hatua za kimaadili na kisheria wale wanaoandika habari za uzushi au za kutunga.
   Wanajeshi wetu wako vitani, lakini mnataka habari tuwe tunapata baada ya wiki mbili! Jeshi lisifanye upuuzi kama wa wanasiasa. Kunatakiwa kuwe na briefing kila siku.
   • Yap ni kweli hiki ndicho alipaswa kusisitiza, na si vinginevyo.
   Kwa hitaji la QSAT, SpyCam Code & IPTV Account
   Piga Simu: 0717 545 762 Au Fungua bit.ly/MWLRCT

  16. Gabhiteka Manji's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 6th April 2012
   Posts : 142
   Rep Power : 519
   Likes Received
   43
   Likes Given
   82

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Katiaka zama hizi za uwazi unaotokana na maendeleo ya teknolojia,bado kuna watu wanaamini kuzuia habari kutasaidia.Ni kosa kubwa kwa kitengo cha PR na maboss wa JWTZ kwa ujumla kuzuia taarifa, wanapaswa kuhamasisha mawasiliano ili kuondoa mikanganyiko isiyokuwa ya ulazima.

  17. #36
   Swat's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th October 2012
   Posts : 4,238
   Rep Power : 11851872
   Likes Received
   1835
   Likes Given
   77

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Kwa dunia ya sasa yenye teknologia kubwa ni ngumu kuzuia watu wasipeane taarifa. Kinachotakiwa,chanzo chochote cha taarifa kihakikishe kinatoa au kinasambaza taarifa reliable na credible. Si kuzuia. Hivi JW itawezaje kuzuia taarifa zinazosomwa na kuonwa kila siku na watanzania toka DW,ALJAZEERA,CNN,BBC,ABC NEWS,CCTV,CBN,FOX NEWS,REUTERS,VOA,RFI,NYASATIME S,CITIZEN,UBC nk. Wote hawa na wengineo wameshakatazwa wasionyeshe au kuandika lolote?. Nadhani uwezo huo hawana. Magazeti TV na radio za Tanzania yasipoonyesha au kuandika habari zinazohusu Tanzania au maendeleo huko DRC watanzania watapata habari toka nje ambazo nyingine zinaweza kuwa ni za uongo. Nadhani watu wa information wa Jw wafanye kazi kisasa zaidi.

  18. #37
   Tina's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th July 2007
   Posts : 550
   Rep Power : 22648
   Likes Received
   493
   Likes Given
   24

   Default

   Quote By UmkhontoweSizwe View Post
   Amri za kikomunisti kumbe bado zipo?!
   Dawa siyo kuzuia kuandika, dawa ni kuwachukulia hatua za kimaadili na kisheria wale wanaoandika habari za uzushi au za kutunga.
   Wanajeshi wetu wako vitani, lakini mnataka habari tuwe tunapata baada ya wiki mbili! Jeshi lisifanye upuuzi kama wa wanasiasa. Kunatakiwa kuwe na briefing kila siku.
   Uko sahihi mkuu, kama sasa tunaambiwa M23 wanajikusanya upya kujibu mapigo na jeshi litasubiri wiki mbili zijazp ndio watuambie, je, waandishi waliopo Goma nao wameambiwa?

  19. #38
   Quick's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 4th November 2010
   Posts : 153
   Rep Power : 655
   Likes Received
   21
   Likes Given
   1

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   ah basi mi na-follow @fardc13, Monusco, M23 drc napata news kila sekunde through twitter..

  20. #39
   joely's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th November 2010
   Posts : 928
   Rep Power : 750
   Likes Received
   382
   Likes Given
   71

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Ulinzi wa taifa ni jukumu la kila raia mwema

  21. Matola's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th October 2010
   Posts : 27,471
   Rep Power : 411037124
   Likes Received
   16662
   Likes Given
   12575

   Default Re: JWTZ: Marufuku kuandika mgogoro wa DRC

   Nadhani hili tangazo mimi halinihusu kwahiyo sina la kuchangia, nina information nyingi zaidi ya rais na siku hizi hata ninaposafiri kwa barabara sihitaji tena kusoma vibao vya kilometers maana Galaxy yangu inatosha kuiuliza kwenye Google map.

   Hili ni tangazo kutoka kwa mtu mjinga ambaye hana tofauti na maafisa vilaza wa uhamiaji ambao ukipeleka maombi ya passport wanataka upeleke barua ya mwaliko wakati hawajui unaweza ukafunguwa email account kwa jina la kizungu halafu ukajitumia mwenyewe kwenye account nyingine.


  Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...