Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Waziri Mkuu ametoa wapi mamlaka haya?

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 34
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,613
      Rep Power : 46736
      Likes Received
      16709
      Likes Given
      8544

      Default Waziri Mkuu ametoa wapi mamlaka haya?

      Ilikuwa ni huko Tarime. Wananchi wakawa wamejiandaa kumpokea Waziri Mkuu "kwa mabango" ya kuhoji mambo mbalimbali. Polisi wakaona kwa sababu zao kuwa hilo halipaswi kutokea, wakawatia mbaroni raia wale. Mbunge wao akalalamika mbele ya Waziri Mkuu. Waziri Mkuu "akawakumbusha" Polisi kuwa kila mtu ana haki ya maoni n.k "akawaamuru" waachilie raia wale. Polisi wakatii. Watu wakashangilia na kuona Waziri Mkuu ni mtetezi wa Katiba na haki za raia. Wakamshukuru. Kati hayo yote, hakuna aliyemuuliza Waziri Mkuu*, ametoa wapi mamlaka hayo ya kuamuru polisi kumwachilia mtuhumiwa au mshtakiwa? Tukiamini kuwa Waziri Mkuu ana uwezo huo je itakuwa kosa kuamuru pia kuwa Waziri Mkuu ana uwezo wa kuamuru mtu ashikiliwe na Polisi au chombo kingine cha usalama (kama TAKUKURU?)

      Utawala wa kiimla, huanza pale ambapo kiongozi anafikiri ana uwezo wa kuamuru jambo likafanyika hata kama hana uwezo huo kisheria. Binafsi, sipendi, tena sitaki, na ninakataa kabisa Waziri Mkuu kujivika madaraka asiyo nayo. Je, siku nyingine akimuamuru Polisi amtwange mtu risasi, polisi atatakiwa kutii amri hiyo? Je, akiamua kuamuru "mbaya wake" atiwe mbaroni kwa kisingizio chochote kwa tu yeye ni Waziri Mkuu, mtu huyo atiwe mbaroni.

      Mhe. Waziri Mkuu, hauna mamlaka hayo, hauna uwezo huo kisheria. Niko tayari kusahihishwa kama Waziri Mkuu anayo mamlaka hayo!! Vinginevyo, akome kuamuru mambo yasiyo ndani ya uwezo wake. Katiba yetu inasema hivi kuhusu madaraka ya Waziri Mkuu:

      52.-(1) Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti,
      usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za
      Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
      (2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali
      Bungeni.
      (3) Katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu
      atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au
      mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.

      53.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu
      atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
      (2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya
      Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya
      Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu,
      watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli
      za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

      NB* - Angalia sijatumia jina la Waziri Mkuu aliye madarakani. Nazungumzia mtu yeyote mwenye kushikilia nafasi hiyo. Katika hoja hii hata hivyo ninamzungumzia Mhe. Edward Lowassa (CCM - Monduli)
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    2. #2
      kichwamaji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2006
      Posts : 399
      Rep Power : 721
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Mzee Mwanakijiji

      Alikuwa anatekeleza kifungu 52 (1); kudhibiti, kusimamia, na kutekeleza kazi na shughuli za kila siku za Serikali ya Jamhuri ya Muungano - ikiwamo ulinzi na usalama. Au nimetafsiri vibaya?

    3. #3
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,613
      Rep Power : 46736
      Likes Received
      16709
      Likes Given
      8544

      Default

      kichwamaji, inawezekana uko sahihi. Lakini je anaweza kutumia kigezo hicho kuamuru mtu atiwe kizuizini?
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    4. #4
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,814
      Rep Power : 1616
      Likes Received
      987
      Likes Given
      29

      Default

      hata mkuu wa wilaya anaouwezo wa kuamuru mwananchi ashikiliwe au aachiwe kama hana jinai..na kama anajinai mwananchi yoyote anayo haki ya dhamana....waziri mkuu ametekeleza vema madaraka yake kwa kuwaamrisha polisi wawaachie wananchi waliokuwa wakitekeleza uhuru wao wa kujieleza [freedom of expression]....tena nampoingeza kwa hilo..

    5. #5
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,700
      Rep Power : 21825
      Likes Received
      750
      Likes Given
      3275

      Default

      Haya ni matumizi mabaya ya madaraka taking advantage ya political scenario.

      Swali la msingi ni kujiuliza ni ktk sheria ipi iliyowafanya polisi kuchukua hatua hizo. EL kuchukua/kutoa maamuzi kwa pupa hakumuonyeshi yeye kuwa efficient and effective.

      Kufungu 52(1), ndio kinampa uwezo huo, however kuna kanuni na taratibu zake ktk kutekeleza..............na ndio maana unakuta kuna Idara ya Polisi, UWT, Mahakama, na Magereza

      Je mmeweza kufikir madhara yake kwa Jeshi letu la Polisi.........i.e the image kwa wale wananchi??........ofcourse mwaweza kusema image ya polisi siku zote ni mbaya............lakini ni lazima tu-observe taratibu na kanuni zinazo-complement sheria zetu

      nimaoni tu

    6. #6
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,613
      Rep Power : 46736
      Likes Received
      16709
      Likes Given
      8544

      Default

      Phillemon.. umesema "hata mkuu wa wilaya". KUna sheria inayompa Mkuu wa Wilaya uwezo huo. Hata hivyo bado sijaona mahali popote ambapo kuna sheria inayompa Waziri Mkuu mamlaka hayo. Kuna sheria inayompa Waziri wa Habari uwezo wa kudhibiti vyombo vya habari (ya magazeti ya 1976), kuna ile inayompa Rais uwezo wa aina fulani Preventive Detention Act ya 1962 (na mabadiliko yake ya 1985) na pia ile ya Usalama wa TAifa ya 1970. Nimeziambatanisha sheria hizo tatu for your reference. Sisemi kuwa hawezi kuamuru mambo hayo, ninachohoji ni kuwa sheria gani inampa uwezo huo? Kwenye nchi ya kidemokrasia yenye utawala wa Katiba, kiongozi hupata madaraka yake na uwezo wake kutoka kwenye sheria (pasipo kuvunja Katiba) na hawezi "kujitwalia" uwezo huo kwa bona fide Kama mtu hajapewa mamlaka, hawezi kutumia kama vile anayo.

      Again, niko tayari kusahihishwa.
      Attached Files
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    7. #7
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,814
      Rep Power : 1616
      Likes Received
      987
      Likes Given
      29

      Default

      majukumu ya mkuu wa wilaya ni pamoja na to maintain peace and tranqility in the designated area of jurisdication among other things...

    8. #8
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,613
      Rep Power : 46736
      Likes Received
      16709
      Likes Given
      8544

      Default

      Phil, kwa mkuu wa wilaya nakubaliana na wewe. Nauliza kuhusu Waziri Mkuu.
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    9. #9
      Bwana Mdogo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th July 2007
      Posts : 104
      Rep Power : 630
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Ilikuwa ni huko Tarime. Wananchi wakawa wamejiandaa kumpokea Waziri Mkuu "kwa mabango" ya kuhoji mambo mbalimbali. Polisi wakaona kwa sababu zao kuwa hilo halipaswi kutokea, wakawatia mbaroni raia wale. Mbunge wao akalalamika mbele ya Waziri Mkuu. Waziri Mkuu "akawakumbusha" Polisi kuwa kila mtu ana haki ya maoni n.k "akawaamuru" waachilie raia wale. Polisi wakatii. Watu wakashangilia na kuona Waziri Mkuu ni mtetezi wa Katiba na haki za raia. Wakamshukuru. Kati hayo yote, hakuna aliyemuuliza Waziri Mkuu*, ametoa wapi mamlaka hayo ya kuamuru polisi kumwachilia mtuhumiwa au mshtakiwa? Tukiamini kuwa Waziri Mkuu ana uwezo huo je itakuwa kosa kuamuru pia kuwa Waziri Mkuu ana uwezo wa kuamuru mtu ashikiliwe na Polisi au chombo kingine cha usalama (kama TAKUKURU?)

      Utawala wa kiimla, huanza pale ambapo kiongozi anafikiri ana uwezo wa kuamuru jambo likafanyika hata kama hana uwezo huo kisheria. Binafsi, sipendi, tena sitaki, na ninakataa kabisa Waziri Mkuu kujivika madaraka asiyo nayo. Je, siku nyingine akimuamuru Polisi amtwange mtu risasi, polisi atatakiwa kutii amri hiyo? Je, akiamua kuamuru "mbaya wake" atiwe mbaroni kwa kisingizio chochote kwa tu yeye ni Waziri Mkuu, mtu huyo atiwe mbaroni.

      Mhe. Waziri Mkuu, hauna mamlaka hayo, hauna uwezo huo kisheria. Niko tayari kusahihishwa kama Waziri Mkuu anayo mamlaka hayo!! Vinginevyo, akome kuamuru mambo yasiyo ndani ya uwezo wake. Katiba yetu inasema hivi kuhusu madaraka ya Waziri Mkuu:

      52.-(1) Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti,
      usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za
      Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
      (2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali
      Bungeni.
      (3) Katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu
      atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au
      mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.

      53.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu
      atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
      (2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya
      Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya
      Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu,
      watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli
      za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

      NB* - Angalia sijatumia jina la Waziri Mkuu aliye madarakani. Nazungumzia mtu yeyote mwenye kushikilia nafasi hiyo. Katika hoja hii hata hivyo ninamzungumzia Mhe. Edward Lowassa (CCM - Monduli)
      Mwkjj hapa kuna mambo kama matatu naweza kuyasema, la kwanza vijana wale walikuwa wanatekeleza haki yao ya msingi ''freedom of speech'' kitendo cha police kuwakamata ni kukiuka haki zao.Kwa maana hiyo basi ile ilikuwa ni illegal arrest wanaweza hata kushtaki, kwa hiyo si kweli kwamba polisi walikuwa wanatekeleza majukumu yao bali walikuwa wanavunja sheria za nchi, na ndio maana waziri mkuu alisema, kama kweli walikamatwa kwa sababu hiyo waachiwe,kwa polisi kuwaachia inamaana iyo tu ndio ilikuwa sababu ya kuwakamata. Illegal arrest inaweza kuwa protested na mtu yeyote,ila kwa kuwa waziri mkuu kasema kuna kauzito kake zaidi.

      Pili mikataba ya haki za binadam ambayo Tz imeridhia na kuiweka kwenye katiba inasema wazi kwamba haki zilizoahinishwa humo ni ''minimum standards'' nchi inaweza hata kuongeza zaidi ya hapo, lakini mikataba hiyo imekataza kabisa kabisa kukiuka haki za msingi zilizomo humo. sasa Waziri mkuu katka kuamrisha kwamba mtu furani atiwe kizuizini itakuwa ndo yaleyale ya polisi na kama polisi watatekeleza itakuwa ni kutii amri haramu, siku hizi mzee by Rome statute both command is responsible for his wrong(commander responsibility) na mtekelezaji is also responsible,hakuna kusema niliamrishwa.

      Tatu katiba mzee haisomwi kama wakina Mazinge wanavyotafsiri biblia, eti ''funua matayo tano mstali wa pili'' iyo haipo, katiba inasomwa in total and must be interpreted in the context. sasa sasa kuna vifungu mle vinasema mtu yeyote ana haki ya kuilinda katiba na anapoona katiba inavunjwa ana haki ya kuchukua hatua, unaweza kwenda mahkmani au ukatumia njia nyingine muafaka, waziri mkuu is not exceptional, ana obligation as kiongozi kulinda katiba,and as a citize. kama nilivyosema hapo juu polisi walikuwa wanavunja katiba, waziri mkuu katekeleza wajibu wake. Kama ambavyo hata wangwe au mwananchi mwingine yeyete angekemea kitendo hicho,ila kwa bongo yetu mpaka aseme mkubwa ndio watu wasikie otherwise utaozea jera.

    10. #10
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,613
      Rep Power : 46736
      Likes Received
      16709
      Likes Given
      8544

      Default

      bwana mdogo, naona una miss point yangu. Sizungumzii hata kidogo suala la wale watu kukamatwa (kama ilitokana na sababu halali au la) na wala sizungumzii haki ya raia kuona Katiba inalindwa. Ninazungumzia specific act, ya Waziri Mkuu kuamuru afisa wa jeshi la Polisi kufanya au kutofanya jambo fulani ambalo ofisa huyo alikuwa analifanya akiamini kuwa anatekeleza majukumu yake halali. Chombo chenye uwezo wa kuamua kuwa mtu fulani kashikwa kihalali au la ni mahakama. Waziri Mkuu kwa kufikiri "anatetea Katiba" hawezi kujiamulia kutoa agizo fulani.

      Tukifuata mtiririko wa mawazo yako ina maana Waziri Mkuu anaweza kuona mtu ameonewa na badala ya kuacha sheria ifuate mkono (ili kuthibitisha hatia au la ya mtu yule) basi ataingilia kati na kusema "naona Katiba imevunja, naamuru mumwachie". Sizungumzii Waziri au raia yoyote kutoa maoni kuwa jambo fulani si haki au ni ukiukwaji wa sheria. Nazungumzia specifically uwezo wa Waziri Mkuu kutoa amri inayoingilia utendaji kazi wa vyombo vya usalama. Uwezo huo ameutoa wapi?
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    11. #11
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,814
      Rep Power : 1616
      Likes Received
      987
      Likes Given
      29

      Default

      mjj nakupata ..lakini wakuu woote wa wilaya wanaripoti kwa WAZIRI MKUU na waziri mizengo pinda [waziri wa ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa] ndiye anayempa briefing waziri mkuu za utendaji wa wilaya na halmashauri zake kila siku..]..inaonekana kuwa kiutendaji waziri mkuu wa sasa ana power kuliko sumaye....maana hii ofisi ya tawala za mikoa ina nguvu sana na mara zote rais kama hamuamini waziri mkuu wake huwa anabaki nayo ofisini kwake...mfano wakati wa mkapa pale magogoni sumaye alikuwa na jukumu la kusimamia utendaki wa siku hadi siku wa serikali[mawaziri]..maafa na bunge ,jukumu muhimu la provitional admn alilichukua rais mkapa mwenyewe akimkasimu brig gen hassan ngwilizi ..jukumu lakumuarifu moja kwa moja masuala ya kila siku ya tawala za mikoa na serikali za mitaa akiwa na cheo cha WAZIRI WA NCHI [OFISI YA RAIS ] TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA...

      MIAKA YA NYUMA KIDOGO RAIS MWINYI HII ofisi alikuwa ameiacha huru ikijitegemea kulikuwa na WAZIRI WA SERIKALI ZA MITAA NA TAWALA ZA MIKOA ..MH KINGUNGE NGOMBALE MWIRU.hapo inamaana halazimiki kutoa taarifa za utendaji wa siku hadi siku on daily basis anakuwa na some autonomy ya kuamua baadhi ya mambo [kwa kufuata mamlaka aliyokasimiwa na katiba]na kumuarifu waziri mkuu na rais badaye ..lakini ukimpata waziri mbovu anaweza kusababisha matatizo makubwa mikoani....mawaziri pekee waliopata kuaminiwa kusimamia ofisi hiyo moja kwa moja ni rashid kawawa,anna abdalah na ngombale mwiru...

    12. #12
      YournameisMINE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2007
      Location : Peramiho
      Posts : 3,794
      Rep Power : 1158
      Likes Received
      16
      Likes Given
      0

      Default

      Jamaa wasanii sana, EL kaona mwanya wa ku-score vi-point na hakupoteza nafasi hiyo. Je kafanya hivyo kinyume cha sheria? Jibu ni hapana.
      To these ppl its just a game and at times they seem to play it better. Waliokamatwa walitumika kama political ponies............its extremly sad and cheap!!

    13. #13
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,814
      Rep Power : 1616
      Likes Received
      987
      Likes Given
      29

      Default

      ..vile vile mnatakiwa mkitaka kuelewa mamlaka ya waziri mkuu msome katiba vizuri...pia kujua chain of command ya police lazima msome police force act..kwa mfano mkuu wa mkoa anao uwezo wa ku m command RPC,MKUU WA WILAYA anauwezo wa ku m command OCD...SASA naamini kwa kuwa hawa wote wako chini ya waziri mkuu kiutendaji ina maana waziri mkuu anao uwezo wa kutoa amri HALALI na ikatekelezwa ZINGATIA NI AMRI HALALI TU!!! na polisi trained hatekelezi amri ambayo si halali ndio maana mara nyingi polisi anaweza kuambiwa na mkuu wa wilaya akamate mtu kisiasa atatekeleza kulinda heshima ya mkubwa hadhrani lakini badaye lazima ATAMWACHIA HURU BILA MASHARTI[mfano kuna wana harakati walikamatwa wakati wa mkutano wa IMF pale movenpick walikamatwa kwa kuonesha mabango kwa amri ya mkubwa mmoja ..lakini aliachiwa mara tu baada ya kufikishwa central tena bila masharti]...sasa kwa hili la kuonesha mabango ..lowassa alitoa amri halali!!!

    14. #14
      Bwana Mdogo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th July 2007
      Posts : 104
      Rep Power : 630
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      bwana mdogo, naona una miss point yangu. Sizungumzii hata kidogo suala la wale watu kukamatwa (kama ilitokana na sababu halali au la) na wala sizungumzii haki ya raia kuona Katiba inalindwa. Ninazungumzia specific act, ya Waziri Mkuu kuamuru afisa wa jeshi la Polisi kufanya au kutofanya jambo fulani ambalo ofisa huyo alikuwa analifanya akiamini kuwa anatekeleza majukumu yake halali. Chombo chenye uwezo wa kuamua kuwa mtu fulani kashikwa kihalali au la ni mahakama. Waziri Mkuu kwa kufikiri "anatetea Katiba" hawezi kujiamulia kutoa agizo fulani.

      Tukifuata mtiririko wa mawazo yako ina maana Waziri Mkuu anaweza kuona mtu ameonewa na badala ya kuacha sheria ifuate mkono (ili kuthibitisha hatia au la ya mtu yule) basi ataingilia kati na kusema "naona Katiba imevunja, naamuru mumwachie". Sizungumzii Waziri au raia yoyote kutoa maoni kuwa jambo fulani si haki au ni ukiukwaji wa sheria. Nazungumzia specifically uwezo wa Waziri Mkuu kutoa amri inayoingilia utendaji kazi wa vyombo vya usalama. Uwezo huo ameutoa wapi?
      Mwkjj nimekupata,ila sijui kama source za info hiyo ni moja na yangu au tofauti, mimi gazeti nililosoma limenukuu maneno ya waziri mkuu hivi ''KAMA KWELI WAMEKAMATWA KWA KUTEKELEZA HAKI YAO BASI NAAMURU WAACHIWE'' nilivyoelewa mimi sentensi ya waziri mkuu ina qualification mwanzo,, ''kama kweli'' kwa maana alitoa amri waachiwe kama tu wamekamatwa kwa kutekeleza haki yao,lakini kama kuna mambo mengine hapo katikati labda walifanya fujo au vipi basi amri ya waziri mkuu haiendi to that extent. iyo qualification mzee Mwkjj ni muhimu sana kujua uwigo wa amri ya waziri mkuu, it was very specific to very specific issue ambayo imelindwa na katiba. unless source yangu imenimiss lead so far i see nothing wrong kwenye amri yake

    15. #15
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,814
      Rep Power : 1616
      Likes Received
      987
      Likes Given
      29

      Default

      ukweli ni kuwa kwa chain waziri mkuu au waziri yeyote tofauti na waziri wa mambo ya ndani hawezi kutoa amri tena hadharani kwa mtu kama MKUU WA MAJESHI,MKUU WA USALAMA,MKUU WA MAGEREZA,MKUU WA POLISI[IGP] NA MAAFISA WENGINE WAANDAMIZI ...HAWA WANAPOKEA AMRI MOJA KWA MOJA KUTOKA KWA AMIRI JESHI MKUU..NA HATA KAMA WAZIRI MKUU,WA ULINZI AU WA USALAMA ANAYO MAAGIZO INAMLAZIMU KUMSHAURI RAIS KWANZA...mtu akiwa waziri wa usalama ,au ulinzi anakuwa pale kama kamisaa wa kusimamia sera tu lakini hana uwezo wa kumuamrisha...sana sana anaweza kuwaamrisha maafisa waandamizi tena kwa orders ambazo ziko clear ..mfano kama alivyofanya lowassa ile order iko very clear ...wale walikuwa wanatekeleza haki yao ya kikatiba ...ingekuwa hana uwezo nayo sanasana angei contain tu at the way deemed fit na kuwaachia polisi wafuate command chain kutekeleza ...

    16. #16
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,613
      Rep Power : 46736
      Likes Received
      16709
      Likes Given
      8544

      Default

      phillemon, Polisi hawako chini ya Waziri Mkuu. Sheria inayounda jeshi la polisi na mabadiliko yake haiweki jeshi la Polisi chini ya Waziri Mkuu kama vile JWTZ haiko chini ya waziri mkuu. Ni kweli kuna amri halali ambazo Waziri Mkuu anaweza kutoa kutokana na wadhifa wake as long as haziingilii sheria ya vyombo husika, au vinginevyo. Wakati Rais Mkapa alipowaamuru maafisa wanne (nikikumbuka sawasawa) wa jeshi la POlisi waachishwe kazi kwa manufaa ya umma, maafisa wale walipokata rufaa, Mahakama ilikubaliana nao kuwa Rais hana mamlaka ya kisheria ya kuwafukuza kazi maafisa wa ngazi zile.

      So, ninachosema kuwa Kiongozi yeyote anaweza kuamuru lolote lile akijisikia, au akifikiri kuwa ana mamlaka ya kufanya hivyo. Hata hivyo haina maana kuwa ana mamlaka hayo. Na as a matter of fact, hata pale inapokubalika mamlaka hayo yapo kisheria yanaweza kupingwa kwenye mahakama halali ili kuthibitisha kuwa mamlaka hayo hayavunji Katiba.

      MaDC na wakuu wa mikoa wanaweza kutoa amri kadhaa, hata hivyo amri hizo ni lazima zikubalike kisheria. Waziri Mkuu hata hivyo, hawezi kwenda kuamuru JWTZ kufanya jambo fulani kwa vile ati yeye ni Waziri Mkuu. Anaweza kutoa ushauri (kama raia mwingine na labda sababu ya wadhifa wake ushauri wake unakuwa na kaujiko kaina fulani) hata hivyo ushauri huo hauwezi kuchukuliwa kama amri.

      Kwenye suala la Tarime, Waziri mkuu angeweza kusema "Nimesikia kuwa kuna vijana ambao walikuwa wanatoa maoni yao kwa mabango n.k na maafisa wa polisi wameamuru kukamatwa, maoni yangu nikuwa kama hiyo ndiyo sababu pekee ya kukamatwa kwao, nataka Polisi waangalie kama vijana hao wamevunja sheria au la, kama hawajavunja sheria basi waachiwe. Na kama polisi wanaamini wamevunja sheria basi wawafikishe mahakamani ili haki ipate kutendeka".
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    17. #17

      Mwkjj i'm not trying to be hard but to get to the point. constructing a sentensi is very important.neno moja linaweza change meaning nzima ya the whole sentensi, ndio maana wanasiasa wajanja sana katika maneno yao. mara nyingi zinakuwa ni political statement than legal. I insist kama mimi ningekuwa polisi na wale vijana katika kutekeleza haki yao wakafanya na mambo mengine illegal, kwa statement ya waziri mkuu nisingewaachia, maana kuwaachia ni kukili kwamba ulichofanya ni uvunjifu wa sheria.Na kwa sababu wametekeleza amri hiyo ni ground nzuri sana ya kuwapeleka polisi mahkamani kwa kukiuka sheria maana wanakili hivyo. lakini kama argument ni whether waziri mkuu ana blanket power ya kuwaamuru polisi hana mamlaka hayo kimsingi, lakini ana mamlaka ya kumuamrisha mfano mkuu wa mkoa kufanya jambo furani, na mkuu wa mkoa technically ni rais wa mkoa, anaweza kumuamrisha RPC wake kufanya jambo furani, provided ( is not derogation of fundamental right) sasa kama ni hivyo technically again waziri mkuu anauwezo huo kama atapitia kwa RC

    18. #18
      Msanii's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2007
      Posts : 6,216
      Rep Power : 1932
      Likes Received
      218
      Likes Given
      277

      Default

      tukubali kuwa PM ametumia a verry possible perfoming art in political game....
      " If you hear a voice within you say "you cannot paint", then by all means paint, and that voice will be silenced"
      [email protected]

    19. #19
      Phillemon Mikael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2006
      Location : mwanza,/uk/santa clara
      Posts : 4,814
      Rep Power : 1616
      Likes Received
      987
      Likes Given
      29

      Default

      ndio mwanakijiji unawaongelea kina kamishna MANN aliyekuwa DCI ,unajua alivyofanya jk ndio hivyo hivyo alifanya mkapa ila jk alijifunza,..mkapaalipoingia aliwafukuza kazi makamishna wanne wa jeshi la polisi ...wakashtaki na kushinda wakawa awarded milioni 100 kila mmoja na walilipwa pamoja na mafao na stahili zote za makamishna wastaafu ..ndio maana jk alipotaka kusafisha polisi alishauriwa legal implication zake ndio akaamua kamishna mwansasu aende likizo hadi afikie retirement,kamishna tibasana akapelekwa bench wizara ya katiba,na kamishna adadi akawekwa benchi kwa muda pale foregn na badaye ubalozi zimbabwe...makamishna wanafukuzwa na amiri jeshi mkuu lakini kuna tarattibu zake za kufuata ikiwemo kuunda tume...kama vile ambavyo mkuu wa majeshi hawezi kumfukuza kazi commissioned officer[luteni to above ameshauruiana na amiri jeshi mkuu ambaye definately huapprove uamuzi wa mkuu wa majeshi...kuubariki.

      migongano ya kimamlaka ipo mingi mnakumbuka mwaka 1987 rais mwiny alimfukuza kazi jaji wamahakama kuu pale arusha ..badaye akawa challanged na yule jaji akarudishiwa ujaji -jaji mwakibete[sikui yuko wapi siku hizi yule mzee]..alituhuimiwa kwa rushwa enzi hizo ndio amezindua FAGIO LA CHUMA...MAJAJI WALI RULE KUWA jaji hawezi kufukuzwa kazi na rais [na ndio pekee ambaye rais hana mamlaka nae]..jaji anatawaliwa na commission yao ambayo kama analo kosa hitishwa tume ya majaji wa jumuia ya madola kumchunguza na kama akidhibitika hiyo tume ndio humuarifu rais husika amvue ujaji...na hiyo tume ndio iliyomuona jaji mwakibete hana hatia ..kazini alirudi na fidia akalipwa..sasa sioni kwa nini majaji wawe waoga!!!!..hata kibaki juzi amekwama kuwafukuza majaji wake..amebakia kufanya ukaidi tu wa kutowapangia kazi na hata yule aliyeko east africa court arusha bado anadunda tu!

    20. #20
      YournameisMINE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2007
      Location : Peramiho
      Posts : 3,794
      Rep Power : 1158
      Likes Received
      16
      Likes Given
      0

      Default Swadakta

      Msanii,
      Mie nakubaliana na wewe kwa asilimia zote, ulichosema ndio "bottom line". Wanasheria wetu Mzee Mkjj na Bwana Mdogo nawapongeza sana kwani inaonekani wazi mnajua nini mnachokiongea.......argument zenu ni za kupendeza na ni typical za fani hiyo. lakini kama alivyosema ndugu yetu Msanii hapo juu ilikuwa ni political action for political reasons regardless of the legal meritd......kwani sidhani kama alikuwa na muda wa kuangalia uhalali wa matendo yake. Kwa bahati nzuri inaonekana kwamba hajavunja sheria..........lakini ni kichekesho pale waziri mkuu anapochukua maamuzi kwa kubahatisha, its pathetic and stinks like hell. Godbless Tanzania na watu wake.

    Page 1 of 2 12 LastLast

    Similar Topics

    1. Mashaka: Kazi na Mamlaka ya Waziri Mkuu ya Kikatiba
      By Kasheshe in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 12
      Last Post: 14th June 2012, 08:39
    2. Replies: 13
      Last Post: 27th December 2010, 22:42
    3. Replies: 6
      Last Post: 2nd December 2010, 15:37
    4. Replies: 16
      Last Post: 21st October 2010, 13:20

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...