Here it is! 4000th Posting "Huu ni Wakati Wetu" - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Jukwaa la Siasa

Jukwaa la Siasa Tanzania & World Politics General Discussion Forum. You need to be registered in order to post your comment(s)

Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 31st August 2007, 06:46 PM   #1
Here it is! 4000th Posting "Huu ni Wakati Wetu"
Mzee Mwanakijiji Mzee Mwanakijiji is online now 31st August 2007, 06:46 PM

Na. M. M. Mwanakijiji

Kizazi kipya cha viongozi wa Tanzania kimeanza kuingia pole pole madarakani. Hiki ni kizazi cha vijana waliozaliwa mara baada ya Muungano na miaka ishirini baadaye (1965 - 1985). Vijana hawa pole pole wameanza kupanda katika ngazi mbalimbali za uongozi wa Taifa letu kuanzia katika nyanja za elimu, sekta binafsi, ajira ya serikali na katika utumishi wa kuchaguliwa. Katika sehemu hizi zote utawakuta mamia ya kundi la vijana wa kizazi hiki wakichapa kazi na kuchukua nafasi yao kwa taadhima kubwa. Sasa hivi tunao wabunge, wakurugenzi, wahasibu, madaktari, wahandisi, walimu, n.k ambao ni wa kizazi kihi kipya. Kizazi cha wale ambao walizaliwa ndani ya Tanzania huru na iliyoungana, na ambao Ukoloni kwao umebakia kuwa ni historia. Hiki ni kizazi kinachowakilisha mawazo na fikra tofauti kabisa na mawazo na fikira ya kizazi kilichotangulia, kilichozaliwa na kukulia wakati wa Ukoloni na mara baada ya Uhuru na Mapinduzi. Hiki cha sasa ni kizazi cha matumaini.

Hata hivyo kizazi hiki bado kimefungwa milele na kizazi kilichokuwa kabla yake, kizazi cha wale waliokulia enzi za MaDC wazungu, Utawala wa Gavana, na ambao bado kasumba ya Ukoloni bado ilikuwa inawafunga. Kama mnyororo uliovunjwa, kizazi kipya pole pole kinaanza kutupilia mbali mawazo ya kikoloni na fikra za kiukandamizaji na huku kikisaidiwa na mabadiliko ya sayansi, teknolojia, na uchumi kinaanza kudai nafasi yake katika hatima ya taifa hili. Kizazi hiki cha watanzania, kimeanza kwa namna ya pekee kuchukua nafasi yake kwa nguvu katika medani za kisiasa na kijamii za Tanzania. Kizazi hiki hakisubiri kufunguliwa milango, au kukaribishwa. Kinaingia kwa nguvu za hoja.

Kizazi hiki hakiogopi tena. Wakati kizazi kilichotangulia kilikuwa bado kinaendeleza kasumba ya kutukuza na kuogopa viongozi kwa vile wao ni “MaDC” au “wakuu” ambapo wakubwa wao walikuwa bado na mitazamo ya kiutawala ya kikoloni, kizazi hiki kipya hakiko tayari kukubali uongozi wa kishkaji au kiubabaishaji. Kizazi hiki kikiwa kimeshatanda kwenye chama tawala na vile vya upinzani, na pia kikiwa kimeutandaza wigo wake hadi nje ya vyama vya kisiasa, kwa mahesabu makubwa kinaanza pole pole kuweka alama yake katika utawala wa sheria, uhuru wa maoni, na utumiaji wa madaraka ya umma.

Huu ni wakati wakati wetu. Kizazi hiki ambacho licha ya kuwa bado ni kichanga lakini kikiwa kimevuviwa na uongozi wa wazee waliotangulia waliokuwa na mawazo ya kizalendo na kimapinduzi, pole pole kimeanza kutoa changamoto kwa viongozi, watawala, na watendaji ambao bado wamezoea mambo “yale yale” ya huko nyuma.

Ndugu zangu kwa wale tuliozaliwa ndani ya kizazi hiki kipya, huu ndio wakati wetu. Huu ndio wakati wa kusimama na kuhesabiwa, ni wakati wa kuchukua nafasi yetu katika historia ya nchi yetu, na ni wakati ambao bila ya shaka njama toka mbinguni zimetutupia na kutuweka saa na siku kama ya leo! Huu ni wakati wetu!

Ni wakati wetu kuona na kuota zaidi. Wengi ambao tumekulia katika Tanzania iliyokabiliwa na njaa mwazoni mwa miaka ya 70, kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Vita vya kuikomboa Kagera, Ukame wa miaka 80 na mabadiliko makubwa ya kisiasa ya miaka ya 90 ni kizazi ambacho kimepata bahati kubwa. Kizazi hiki ambacho kimepata nafasi zaidi ya kuuona ulimwengu kuliko wazazi wao, kizazi ambacho kimeweza kuingia katika ajira ya kimataifa pasipo hofu wala woga, ni kizazi chenye bahati ambacho mang’amuzi yake hayalingani hata chembe na mang’amuzi ya viongozi ambao walipata nafasi kama hizo miaka ya tisini au sabini! Huu ni wakati wetu!

Hivyo, hiki ni kizazi kinachotamani zaidi, kinachoota zaidi, na kinachowaza zaidi. Kinaota mambo mazuri kwa taifa lake, kinatamani mafanikio tele kwa wana na mabinti wa taifa hilo, na kinachowaza zaidi jinsi gani kizazi hiki kipya kitaweza kuibadilisha Tanzania kuwa lile taifa ambalo wengi wetu tunalitamani na kulistahili. Huu ni wakati wa kizazi hicho!

Huu ni wakati wa kizazi hicho kutenda zaidi kuliko kusema zaidi. Kizazi hiki sasa hivi pole pole na kwa ujasiri mkubwa kinaanza kujihusisha na miradi, utafiti, mipango, na ujasiriamali wa kila aina ili kuweza kujijenga kiuchumi na kuweza kujenga Taifa la kisasa ambapo mawazo ya “kuzamia ng’ambo” yatatoweka na kila mtu ataona fahari kuishi Tanzania. Kizazi hiki kimeanza taratibu kurudi Tanzania na wengine pole pole wameanza kujiandaa kuweka maskani yao Tanzania baada ya kujifunza zaidi kutoka ughaibuni. Kama vile Wachina walivyofanya, na Wahindi walivyofanya, sasa hivi kizazi hiki cha Watanzania nacho kimeanza kutambua kuwa nchi za magharibi hazituhitaji sisi bali nchi zetu zinatuhitaji sisi zaidi. Kizazi hiki pole pole kimeanza kutekeleza wito wa kulitumikia taifa lao! Huu ni wakati wetu!

Huu ni wakati wa kizazi hiki kufanya maamuzi ya makusudi na ya lazima ya kushiriki katika kujenga taifa lenye viongozi walio wawazi, wenye kuwajibika na wenye kutimizia wajibu wao kwa mujibu wa sheria pasipo kuendeleza na kuvumilia uzembe na ufisadi. Kizazi hiki katika kufanya maamuzi kimeanza kuthubutu zaidi. Mgongano tunaouona sasa hivi kati ya baadhi ya viongozi na baadhi ya wawakilishi wa kizazi hiki unatokana na mambo haya. Kwamba, wakati waliolala na kusinzia madarakani wameanza kuamshwa, kizazi kipya siyo tu kinawaamsha ili watimize wajibu wao, bali kinawatishia kabisa kuwa wasipoamka wataondolewa madarakani kwa nguvu ya kura. Kizazi hiki hakiogopi tena viongozi bali kinawaheshimu. Hata hivyo kizazi hiki hakitoi heshima ya bure tu kwa vile mtu ni kiongozi au amewahi kuwa kiongozi kinatoa heshima kwa kiongozi anayestahili heshima hiyo.

Ni kwa sababu hiyo, basi utaona kuwa kizazi hiki hakiombi msamaha hata chembe kwa kuwaumbua viongozi goi goi, wazembe, mafisadi, na wababaishaji. Huu ni wito wa kizazi hiki kwani kile kilichotangulia kimeshindwa kabisa kupambana na maadui wa mafanikio. Huu ni wito wa kizazi chetu kwani huu ni wakati wetu!!

Kizazi hiki kiko tayari kusikiliza ushauri kutoka mtu yeyote, kiko tayari kukoselewa, kiko tayari kuonywa na kupewa maongozi, lakini kama vile simba mtoto afunzwaye, kizazi hiki kiko tayari kuanza kuwinda! Hisia za kiwindaji ziko ndani ya damu ya wana na mabinti wa kizazi hiki!

Wito wangu leo kwa watawala wetu na wale ambao wanaogopa ujio wa kizazi hiki, “ondoeni hofu”! Kizazi hiki siyo maadui wenu, na kizazi hiki siyo wabaya wenu! Kizazi hiki ni kizazi cha watanzania wenzenu wana na mabinti zenu, hiki ni kizazi cha watoto wenu na wadogo zenu! Msiwabane na kuwanyima nafasi kwa vile bado vijana au hawana uzoefu. Wakati umefika wa kuanza kuwaamini na kuwapa nafasi na majukumu zaidi. Msigope wanapowapa changamoto au wanapokuwa na udadisi zaidi! Hiki kizazi ndivyo kilivyo!

Kizazi hiki kimefikia wakati wake, kizazi hiki hakirudi nyuma wala hakitasalimu amri! Wana na mabinti wa kizazi hiki kupitia sehemu zao mbalimbali na majumuiko yao mbalimbali wataendelea kuzungumza kwa uhuru zaidi, uwazi zaidi, na kwa kuthubutu zaidi ili kuweza kuleta mabadiliko yanayohitajika katika safu ya uongozi wa nchi yetu, ili hatimaye tuweze kujenga Taifa la kisasa mno, taifa lenye mafanikio na lenye nafasi ya mafanikio kwa kila raia. Kizazi hiki it is here to stay!!! DEAR CONTRYMEN AND WOMEN, DO NOT BE AFRAID, OPEN THE GATES, OR MOVE OVER! HERE WE COME.

IT IS OUR TIME!

M. M. Mwanakijiji
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"

Mzee Mwanakijiji's Avatar
Mzee Mwanakijiji
JF Premium Member
Points: 12,987,839, Level: 100 Points: 12,987,839, Level: 100 Points: 12,987,839, Level: 100
Activity: 94% Activity: 94% Activity: 94%
Join Date: Fri Mar 2006
Location: Kijijini
Posts: 18,477
Thanks: 8,503
Thanked 4,688 Times in 1,320 Posts
Views: 620
Reply With Quote
  #2  
Old 31st August 2007, 06:49 PM
Geeque Geeque is offline
Geeque is watching you!
JF Senior Expert Member
Points: 171,157, Level: 100 Points: 171,157, Level: 100 Points: 171,157, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Fri Aug 2007
Posts: 797
Thanks: 17
Thanked 55 Times in 24 Posts
Rep Power: 24
Geeque will become famous soon enoughGeeque will become famous soon enoughGeeque will become famous soon enoughGeeque will become famous soon enoughGeeque will become famous soon enoughGeeque will become famous soon enoughGeeque will become famous soon enoughGeeque will become famous soon enough
Send a message via MSN to Geeque Send a message via Yahoo to Geeque Send a message via Skype™ to Geeque
Default

Hongera sana Mazeee kwa kazi nzuri.
__________________
Check out EastAfricanTube at eastafricantube.com
&
Bongo Radio at bongoradio.com
Reply With Quote
  #3  
Old 31st August 2007, 07:24 PM
Bi. Senti 50's Avatar
Bi. Senti 50 Bi. Senti 50 is offline
Bi. Senti 50 has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 152,096, Level: 100 Points: 152,096, Level: 100 Points: 152,096, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Tue Apr 2007
Posts: 375
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 23
Bi. Senti 50 will become famous soon enoughBi. Senti 50 will become famous soon enoughBi. Senti 50 will become famous soon enoughBi. Senti 50 will become famous soon enoughBi. Senti 50 will become famous soon enoughBi. Senti 50 will become famous soon enoughBi. Senti 50 will become famous soon enoughBi. Senti 50 will become famous soon enough
Default

mmh... i might change my mind. I'm touched.

thank you.
Reply With Quote
  #4  
Old 31st August 2007, 07:31 PM
Shy Shy is offline
Shy is yours
Banned
Points: 2,380,404, Level: 100 Points: 2,380,404, Level: 100 Points: 2,380,404, Level: 100
Activity: 9% Activity: 9% Activity: 9%
 
Join Date: Thu Nov 2006
Posts: 4,258
Thanks: 0
Thanked 170 Times in 112 Posts
Rep Power: 0
Shy will become famous soon enoughShy will become famous soon enoughShy will become famous soon enoughShy will become famous soon enoughShy will become famous soon enoughShy will become famous soon enoughShy will become famous soon enoughShy will become famous soon enough
Send a message via Yahoo to Shy
Default

Be honest with yourself, and with everyone else as well. There are some things you like and other things you dislike, and that's just fine.
Be fully accepting of yourself, and of others as well. You are who you are, with your dreams and passions, preferences and interests, and each person is delightfully unique.

What you run from or hide from or seek to deny, grows bigger and more influential as a result. By getting things out in the open, by seeing them for what they truly are, you become free of their control.

You are where you are and life is the way it is. The more completely you accept it, the more power you have to do something about it.

This moment carries enormous opportunity. No positive purpose is served by fighting against it.

Instead, accept what is, the way you are, the way you feel, and the things that life has brought to you. Then you can make the very most of it all.

Mdudu for Pwani Forums
http://*****************/viewforum.php...8fafb3eec39fef

Last edited by Shy; 31st August 2007 at 07:42 PM..
Reply With Quote
  #5  
Old 31st August 2007, 07:35 PM
Kalamu Kalamu is offline
Kalamu has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 127,114, Level: 100 Points: 127,114, Level: 100 Points: 127,114, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Sun Nov 2006
Posts: 1,164
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 26
Kalamu will become famous soon enoughKalamu will become famous soon enoughKalamu will become famous soon enoughKalamu will become famous soon enoughKalamu will become famous soon enoughKalamu will become famous soon enoughKalamu will become famous soon enoughKalamu will become famous soon enough
Default Plagiarism

Quote:
View Post
Be honest with yourself, and with everyone else as well. There are some things you like and other things you dislike, and that's just fine.
Be fully accepting of yourself, and of others as well. You are who you are, with your dreams and passions, preferences and interests, and each person is delightfully unique.

What you run from or hide from or seek to deny, grows bigger and more influential as a result. By getting things out in the open, by seeing them for what they truly are, you become free of their control.

You are where you are and life is the way it is. The more completely you accept it, the more power you have to do something about it.

This moment carries enormous opportunity. No positive purpose is served by fighting against it.

Instead, accept what is, the way you are, the way you feel, and the things that life has brought to you. Then you can make the very most of it all.
I can swear, I've seen this somewhere; word for word.
It is honorable to acknowledge the source.
__________________
'Mwalimu' Kasema: It can be Done. Play your Part.
Reply With Quote
  #6  
Old 31st August 2007, 07:47 PM
Mzee Mwanakijiji's Avatar
Mzee Mwanakijiji Mzee Mwanakijiji is online now
Mzee Mwanakijiji anawashangaa wanaoitetea sheria mbovu
JF Premium Member
Points: 12,987,839, Level: 100 Points: 12,987,839, Level: 100 Points: 12,987,839, Level: 100
Activity: 94% Activity: 94% Activity: 94%
 
Join Date: Fri Mar 2006
Location: Kijijini
Posts: 18,477
Thanks: 8,503
Thanked 4,688 Times in 1,320 Posts
Rep Power: 44
Mzee Mwanakijiji is on a distinguished roadMzee Mwanakijiji is on a distinguished road
Send a message via MSN to Mzee Mwanakijiji Send a message via Skype™ to Mzee Mwanakijiji
Default

a quote from inspirational speaker Ralph Marston
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
Reply With Quote
  #7  
Old 1st September 2007, 04:29 AM
Mkandara Mkandara is offline
Mkandara Aviator
JF Premium Member
Points: 580,633, Level: 100 Points: 580,633, Level: 100 Points: 580,633, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Thu Mar 2006
Location: T dot
Posts: 7,289
Thanks: 463
Thanked 747 Times in 325 Posts
Rep Power: 80
Mkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the rough
Default

Duh,
Mzee wangu yaani ndio unataka kung'atuke?... ama kweli tumezeeka. Tahadhali tu mkumbuke hadithi ya kule mlikotoka, Msiiweke kapuni mtakwisha..kwa kuwakumbusha tu kumbukeni Mtawala mweusi ni hatari kuliko yule mweupe kwa sababu huyu ni ndugu yako, jirani yako na mzazi wako...msemo wa Komandoo kumkoma nyani giledi.. mtazame usoni!

A re-reading of Nyerere's major essays and hindsight reflection on the first 25 years of Tanzanian independence, suggest that his central domestic preoccupations were fourfold:-
1). The development of the Tanzanian economy, which he saw as a sine qua non for the accomplishment of most if not all other objectives;
2) securing and retaining national control of the direction of Tanzania's economic development;
3) creating political institutions that would be widely participatory and sustain the extraordinary sense of common purpose which in these early years united Tanzanians under his leadership and that of the Tanzanian African National Union (TANU); and
4) building a just society in Tanzania that would be genuinely equitable for all its citizens.

Ushauri wa mzee aliyezaliwa kabla ya Uhuru! - Hata ubepari unayakubali mawazo haya!
__________________
Exploration of reality
Reply With Quote
  #8  
Old 1st September 2007, 05:06 AM
Mzee Mwanakijiji's Avatar
Mzee Mwanakijiji Mzee Mwanakijiji is online now
Mzee Mwanakijiji anawashangaa wanaoitetea sheria mbovu
JF Premium Member
Points: 12,987,839, Level: 100 Points: 12,987,839, Level: 100 Points: 12,987,839, Level: 100
Activity: 94% Activity: 94% Activity: 94%
 
Join Date: Fri Mar 2006
Location: Kijijini
Posts: 18,477
Thanks: 8,503
Thanked 4,688 Times in 1,320 Posts
Rep Power: 44
Mzee Mwanakijiji is on a distinguished roadMzee Mwanakijiji is on a distinguished road
Send a message via MSN to Mzee Mwanakijiji Send a message via Skype™ to Mzee Mwanakijiji
Default

Mkandara, safi kabisa.. kwani pasipo kuwa na dira ni vigumu kufika mtu anakotaka.
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
Reply With Quote
  #9  
Old 1st September 2007, 01:06 PM
Mpaka Kieleweke Mpaka Kieleweke is offline
Mpaka Kieleweke IS NOW AVAILABLE
JF Senior Expert Member
Points: 1,111,508, Level: 100 Points: 1,111,508, Level: 100 Points: 1,111,508, Level: 100
Activity: 6% Activity: 6% Activity: 6%
 
Join Date: Tue Feb 2007
Posts: 1,892
Thanks: 14
Thanked 94 Times in 55 Posts
Rep Power: 27
Mpaka Kieleweke will become famous soon enoughMpaka Kieleweke will become famous soon enoughMpaka Kieleweke will become famous soon enoughMpaka Kieleweke will become famous soon enoughMpaka Kieleweke will become famous soon enoughMpaka Kieleweke will become famous soon enoughMpaka Kieleweke will become famous soon enoughMpaka Kieleweke will become famous soon enough
Default

Hongera ,nawaambia vijana kuwa kila kizazi kina wajibu ,je umetimiza wajibu wako kwako binafsi,familia yako,kijiji chako, mkoa wako taifa lako, bara lako na ulimwengu kwa ujumla.

Tafakari na pia hujachelewa waweza kuanza kutimiza wajibu wako bado ni mapema sana.

Hongera mjj kwani walau umesema na umewaamsha wengi.
Reply With Quote
  #10  
Old 1st September 2007, 09:24 PM
John Mnyika's Avatar
John Mnyika John Mnyika is offline
John Mnyika has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 454,674, Level: 100 Points: 454,674, Level: 100 Points: 454,674, Level: 100
Activity: 2% Activity: 2% Activity: 2%
 
Join Date: Fri Jun 2006
Location: Tanzania
Posts: 788
Thanks: 4
Thanked 182 Times in 61 Posts
Rep Power: 25
John Mnyika will become famous soon enoughJohn Mnyika will become famous soon enoughJohn Mnyika will become famous soon enoughJohn Mnyika will become famous soon enoughJohn Mnyika will become famous soon enoughJohn Mnyika will become famous soon enoughJohn Mnyika will become famous soon enoughJohn Mnyika will become famous soon enough
Default Kizazi Kipya, Maisha Mapya!

Quote:
View Post
Na. M. M. Mwanakijiji

Kizazi kipya cha viongozi wa Tanzania kimeanza kuingia pole pole madarakani. Hiki ni kizazi cha vijana waliozaliwa mara baada ya Muungano na miaka ishirini baadaye (1965 - 1985). Vijana hawa pole pole wameanza kupanda katika ngazi mbalimbali za uongozi wa Taifa letu kuanzia katika nyanja za elimu, sekta binafsi, ajira ya serikali na katika utumishi wa kuchaguliwa. Katika sehemu hizi zote utawakuta mamia ya kundi la vijana wa kizazi hiki wakichapa kazi na kuchukua nafasi yao kwa taadhima kubwa. Sasa hivi tunao wabunge, wakurugenzi, wahasibu, madaktari, wahandisi, walimu, n.k ambao ni wa kizazi kihi kipya. Kizazi cha wale ambao walizaliwa ndani ya Tanzania huru na iliyoungana, na ambao Ukoloni kwao umebakia kuwa ni historia. Hiki ni kizazi kinachowakilisha mawazo na fikra tofauti kabisa na mawazo na fikira ya kizazi kilichotangulia, kilichozaliwa na kukulia wakati wa Ukoloni na mara baada ya Uhuru na Mapinduzi. Hiki cha sasa ni kizazi cha matumaini.

Hata hivyo kizazi hiki bado kimefungwa milele na kizazi kilichokuwa kabla yake, kizazi cha wale waliokulia enzi za MaDC wazungu, Utawala wa Gavana, na ambao bado kasumba ya Ukoloni bado ilikuwa inawafunga. Kama mnyororo uliovunjwa, kizazi kipya pole pole kinaanza kutupilia mbali mawazo ya kikoloni na fikra za kiukandamizaji na huku kikisaidiwa na mabadiliko ya sayansi, teknolojia, na uchumi kinaanza kudai nafasi yake katika hatima ya taifa hili. Kizazi hiki cha watanzania, kimeanza kwa namna ya pekee kuchukua nafasi yake kwa nguvu katika medani za kisiasa na kijamii za Tanzania. Kizazi hiki hakisubiri kufunguliwa milango, au kukaribishwa. Kinaingia kwa nguvu za hoja.

Kizazi hiki hakiogopi tena. Wakati kizazi kilichotangulia kilikuwa bado kinaendeleza kasumba ya kutukuza na kuogopa viongozi kwa vile wao ni “MaDC” au “wakuu” ambapo wakubwa wao walikuwa bado na mitazamo ya kiutawala ya kikoloni, kizazi hiki kipya hakiko tayari kukubali uongozi wa kishkaji au kiubabaishaji. Kizazi hiki kikiwa kimeshatanda kwenye chama tawala na vile vya upinzani, na pia kikiwa kimeutandaza wigo wake hadi nje ya vyama vya kisiasa, kwa mahesabu makubwa kinaanza pole pole kuweka alama yake katika utawala wa sheria, uhuru wa maoni, na utumiaji wa madaraka ya umma.

Huu ni wakati wakati wetu. Kizazi hiki ambacho licha ya kuwa bado ni kichanga lakini kikiwa kimevuviwa na uongozi wa wazee waliotangulia waliokuwa na mawazo ya kizalendo na kimapinduzi, pole pole kimeanza kutoa changamoto kwa viongozi, watawala, na watendaji ambao bado wamezoea mambo “yale yale” ya huko nyuma.

Ndugu zangu kwa wale tuliozaliwa ndani ya kizazi hiki kipya, huu ndio wakati wetu. Huu ndio wakati wa kusimama na kuhesabiwa, ni wakati wa kuchukua nafasi yetu katika historia ya nchi yetu, na ni wakati ambao bila ya shaka njama toka mbinguni zimetutupia na kutuweka saa na siku kama ya leo! Huu ni wakati wetu!

Ni wakati wetu kuona na kuota zaidi. Wengi ambao tumekulia katika Tanzania iliyokabiliwa na njaa mwazoni mwa miaka ya 70, kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Vita vya kuikomboa Kagera, Ukame wa miaka 80 na mabadiliko makubwa ya kisiasa ya miaka ya 90 ni kizazi ambacho kimepata bahati kubwa. Kizazi hiki ambacho kimepata nafasi zaidi ya kuuona ulimwengu kuliko wazazi wao, kizazi ambacho kimeweza kuingia katika ajira ya kimataifa pasipo hofu wala woga, ni kizazi chenye bahati ambacho mang’amuzi yake hayalingani hata chembe na mang’amuzi ya viongozi ambao walipata nafasi kama hizo miaka ya tisini au sabini! Huu ni wakati wetu!

Hivyo, hiki ni kizazi kinachotamani zaidi, kinachoota zaidi, na kinachowaza zaidi. Kinaota mambo mazuri kwa taifa lake, kinatamani mafanikio tele kwa wana na mabinti wa taifa hilo, na kinachowaza zaidi jinsi gani kizazi hiki kipya kitaweza kuibadilisha Tanzania kuwa lile taifa ambalo wengi wetu tunalitamani na kulistahili. Huu ni wakati wa kizazi hicho!

Huu ni wakati wa kizazi hicho kutenda zaidi kuliko kusema zaidi. Kizazi hiki sasa hivi pole pole na kwa ujasiri mkubwa kinaanza kujihusisha na miradi, utafiti, mipango, na ujasiriamali wa kila aina ili kuweza kujijenga kiuchumi na kuweza kujenga Taifa la kisasa ambapo mawazo ya “kuzamia ng’ambo” yatatoweka na kila mtu ataona fahari kuishi Tanzania. Kizazi hiki kimeanza taratibu kurudi Tanzania na wengine pole pole wameanza kujiandaa kuweka maskani yao Tanzania baada ya kujifunza zaidi kutoka ughaibuni. Kama vile Wachina walivyofanya, na Wahindi walivyofanya, sasa hivi kizazi hiki cha Watanzania nacho kimeanza kutambua kuwa nchi za magharibi hazituhitaji sisi bali nchi zetu zinatuhitaji sisi zaidi. Kizazi hiki pole pole kimeanza kutekeleza wito wa kulitumikia taifa lao! Huu ni wakati wetu!

Huu ni wakati wa kizazi hiki kufanya maamuzi ya makusudi na ya lazima ya kushiriki katika kujenga taifa lenye viongozi walio wawazi, wenye kuwajibika na wenye kutimizia wajibu wao kwa mujibu wa sheria pasipo kuendeleza na kuvumilia uzembe na ufisadi. Kizazi hiki katika kufanya maamuzi kimeanza kuthubutu zaidi. Mgongano tunaouona sasa hivi kati ya baadhi ya viongozi na baadhi ya wawakilishi wa kizazi hiki unatokana na mambo haya. Kwamba, wakati waliolala na kusinzia madarakani wameanza kuamshwa, kizazi kipya siyo tu kinawaamsha ili watimize wajibu wao, bali kinawatishia kabisa kuwa wasipoamka wataondolewa madarakani kwa nguvu ya kura. Kizazi hiki hakiogopi tena viongozi bali kinawaheshimu. Hata hivyo kizazi hiki hakitoi heshima ya bure tu kwa vile mtu ni kiongozi au amewahi kuwa kiongozi kinatoa heshima kwa kiongozi anayestahili heshima hiyo.

Ni kwa sababu hiyo, basi utaona kuwa kizazi hiki hakiombi msamaha hata chembe kwa kuwaumbua viongozi goi goi, wazembe, mafisadi, na wababaishaji. Huu ni wito wa kizazi hiki kwani kile kilichotangulia kimeshindwa kabisa kupambana na maadui wa mafanikio. Huu ni wito wa kizazi chetu kwani huu ni wakati wetu!!

Kizazi hiki kiko tayari kusikiliza ushauri kutoka mtu yeyote, kiko tayari kukoselewa, kiko tayari kuonywa na kupewa maongozi, lakini kama vile simba mtoto afunzwaye, kizazi hiki kiko tayari kuanza kuwinda! Hisia za kiwindaji ziko ndani ya damu ya wana na mabinti wa kizazi hiki!

Wito wangu leo kwa watawala wetu na wale ambao wanaogopa ujio wa kizazi hiki, “ondoeni hofu”! Kizazi hiki siyo maadui wenu, na kizazi hiki siyo wabaya wenu! Kizazi hiki ni kizazi cha watanzania wenzenu wana na mabinti zenu, hiki ni kizazi cha watoto wenu na wadogo zenu! Msiwabane na kuwanyima nafasi kwa vile bado vijana au hawana uzoefu. Wakati umefika wa kuanza kuwaamini na kuwapa nafasi na majukumu zaidi. Msigope wanapowapa changamoto au wanapokuwa na udadisi zaidi! Hiki kizazi ndivyo kilivyo!

Kizazi hiki kimefikia wakati wake, kizazi hiki hakirudi nyuma wala hakitasalimu amri! Wana na mabinti wa kizazi hiki kupitia sehemu zao mbalimbali na majumuiko yao mbalimbali wataendelea kuzungumza kwa uhuru zaidi, uwazi zaidi, na kwa kuthubutu zaidi ili kuweza kuleta mabadiliko yanayohitajika katika safu ya uongozi wa nchi yetu, ili hatimaye tuweze kujenga Taifa la kisasa mno, taifa lenye mafanikio na lenye nafasi ya mafanikio kwa kila raia. Kizazi hiki it is here to stay!!! DEAR CONTRYMEN AND WOMEN, DO NOT BE AFRAID, OPEN THE GATES, OR MOVE OVER! HERE WE COME.

IT IS OUR TIME!

M. M. Mwanakijiji

Kaka Mwanakijiji

Nilitoa udhuru kwamba nitakuwa msomaji zaidi ya kuchangia hapa JF. Na mara baada ya udhuru huo miezi kadhaa imepita sijaandika ujumbe wowote humu. Nilitaka kuandika kukupongeza kwa kukaribia kufikisha posts 4000 lakini nilidhamiria kuendelea kuwa kimya. Hata hivyo ujumbe wako huu umenigusa na kunigutua, sitaitendea haki dhamira yangu kama nisoweka wazi hisia zangu za pongezi kwako.

Umenikumbusha maneno ya Frantz Fanon; umenikumbusha maneno ya Mwalimu Nyerere katika wosia wake wa mwisho kwa Vijana pale Kirumba. Mwalimu katika hotuba yake hiyo miaka michache kabla ya kufa kwake aliweka bayana utume wa kizazi kipya..nakumbuka mrindimo wa sauti yake..akitamka kila kizazi kina utume wake..akieleza walivyoweza na waliposhindwa kutimiza utume wao...alijaribu kubashiri utume wa kizazi kipya...lakini zaidi nakumbuka maneno yake mawili ambayo aliyarudia rudia kuhimiza nini kizazi kipya kianze ili kutimiza utume wako...alisema...THINK...and UNITE....na akamalizia kwa kusema ujumbe huo aliutoa kwa vijana wa Tanzania na Vijana wa Afrika....maandiko yako ni sehemu ya kufiri kwako...ngazi ya pili sasa ni kuungana...

Umenikumbusha pia mwito wa mwanamuziki Profesa Jay katika wimbo NI WAKATI....naye anamalizia kwa kusema SHIRIKI KAMA UNAJALI....DEMOKRASIA SIO WAKATI WA UCHAGUZI TU....

Umenikumbusha harakati za vijana wa TYVA(www.vijanavision.org) na hasa ile AJENDA YA VIJANA 2005 na zile hotuba mbalimbali katika uzinduzi wake(nakumbuka SHY aliweka hapa baadhi ya nukuu!, naomba kama una hotuba kamili ya Edward Kinabo uiweke).

Umenikumbusha wimbo wa Bob Marley akitoa changamoto kwa kizazi kipya...sijui nani ana lyrics za ule mwimbo wa Bob Marley kwa VIJANA....its time to be counted(as you always says)....IT'S TIME TO GET UP AND STAND UP.....kama Nesta alivyowahi kughani....unaweza kuwaghilibu watu wachache kwa muda mchache lakini huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote....

Umenikumbusha kampeni zangu za uchaguzi pale Ubungo....huu ndio ulikuwa ujumbe wangu mahususi KIZAZI KIPYA, MAISHA MAPYA....

Natamani Eric Ongara naye aje kuchangia katika suala hili...yeye ni muumini zaidi wa utume wa kizazi kipya.......

Ombi langu kwako....ujumbe wako uuweke kwenye PDF na kuuwekea nakshi kama ulivyofanya kwa yale majibu kuhusu Ndege ya Lowasa...halafu unitumie kwenye mnyika@yahoo.com, nauhitaji kupindukia kuna vijana ningependa kuwapatia nakala kama ulivyo.

Naomba unipatie ujumbe huo ndani ya wiki hii

Lets all dare to think and think to dare....

There is nothing for us without us.....

Vijana wa vyama 18 vya Kenya walitutembelea hapa ofisini juzi...tulizungumza mambo kadhaa kuhusu utume wa kizazi kipya...wakaanza kulalama kwamba kule kwao 'young people are manipulated by their party leaders in tribal lines'....I blasted them...why should they wait to be manipulated? Why shouldn't you manipulate them instead? If you reject to be manipulated who will they manipulate? Are they able to go to the streets themselves if young people decide otherwise?

Pamoja tutashinda....

Tuwe wakala wa mabadiliko tunayotaka kuyaona...

JJ
__________________
Kizazi Kipya, Maisha Mapya
New Generation, New Life

Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli
Real Change, Real Freedom

John Mnyika

Last edited by Ole; 1st September 2007 at 09:51 PM..
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
4000th, huu ni wakati wetu, posting

Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On

Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Ni wakati wa kuacha woga! Invisible Habari na Hoja mchanganyiko 6 4th June 2009 10:01 PM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!

All times are GMT +3. The time now is 12:19 PM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com