JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

  Report Post
  Page 16 of 21 FirstFirst ... 61415161718 ... LastLast
  Results 301 to 320 of 404
  1. n00b's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th April 2008
   Posts : 928
   Rep Power : 28530
   Likes Received
   2089
   Likes Given
   229

   Default Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   Wakuu,

   Tetesi zilizonifikia ambazo SI NZURI (kwa tunaopenda kuona wenzetu hata tukiwa na tofauti nao) zinaashiria kama kuna kitu kisicho cha kawaida kimemkuta bwana huyu hii leo.

   Vyanzo vyangu vya kuaminika vinanihabarisha kuwa bwana huyu yamemkuta ya kumkuta. Kuna mwenye kuwa na 'ukweli' au 'tetesi' zaidi?

   ==============
   UPDATES:
   ==============

   Taarifa za awali zinadai kamwagiwa Tindikali maeneo ya Msasani City Mall muda wa saa 2.

   Ni jirani na Ubalozi wa Marekani na jirani kabisa na Police Oysterbay.

   Jamaa aliyefanya kitendo hicho alitoka mbio, mlinzi akamkimbiza lakini bahati mbaya akateleza na kuanguka na jamaa akawahi pikipiki na kutoweka eneo la tukio.

   Said amelazwa Trauma (AMI) Hosp - Masaki.

   Kapata madhara macho yote mawili ila moja ndilo limeumia zaidi sehemu ya juu.

   Mwenyewe anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua na madaktari wanamhudumia.

   Polisi wanahaha kutafuta wahusika kwa nguvu kubwa na huenda akakamatwa mhusika mapema sana.


   ==============

   Some useful topics on JF:


   ===============
   Mmiliki wa Home Shopping Centre amwagiwa tindikali usoni|Dar es Salaam.


   Mtu asiyejulikana juzi usiku alimvamia mmiliki wa maduka ya Home Shopping Centre, Said Mohammed Saad (pichani) na kumwagia maji usoni yanayodhaniwa kuwa ni tindikali.

   Tukio hilo lililotokea juzi saa 1 usiku karibu na kituo cha Polisi cha Oysterbay, lilithibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Ally Mlege kwa kusema kuwa bado polisi wanaendelea na uchunguzi wao ili kuwabaini waliohusika.

   “Ni kweli tukio hili limetokea ila polisi wanaendelea na uchunguzi. Tukikamilisha uchunguzi tunatarajia kutoa taarifa kamili za tukio zima,” alisema na kuongeza;

   “Hatuna haja ya kuficha ukweli wa tukio hili, uchunguzi wetu ukikamilika na watuhumiwa wakikamatwa kila mtu atajua.”

   Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa mtu huyo, alimkuta Saad akiwa anazungumza na mmoja wa wafanyakazi wake katika duka lake jipya lililopo karibu na Kituo cha Polisi cha Oysterbay.

   “Wakati akizungumza na mfanyakazi wake, huyo mtu alikuwa kama anapita na alichomoa kitu fulani na kummwagia Saad usoni na kisha kukimbia,” zilieleza taarifa hizo na kuongeza;

   “Baada ya tukio hilo alipelekwa katika Hospitali ya AMI, sasa hatujui kama bado yupo hapo au ameondoka, ila sisi tulizungumza naye na alitueleza mwonekano wa mtu aliyemwagia tindikali.”

   Taarifa hizo zilifafanua kwamba polisi wanazitumia taarifa hizo walizopewa na Saad, ili kuweza kumkamata mhusika.

   Taarifa hizo zilifafanua kuwa polisi wanapanga tena siku ya kumhoji kwa mara ya pili Saad, kwamba watataka kufahamu kama mfanyabiashara huyo alikuwa akipewa vitisho au ujumbe wowote, kabla ya kukutwa na tukio hilo.

   Hata hivyo, habari nyingine zilizolifikia Mwananchi Jumapili zilieleza kuwa mtu huyo baada ya kummwagia Saad tindikali, alipanda pikipiki na kutokomea eneo hilo.


   “Walikuwa wawili, mmoja alikwenda kufanya unyama na mwingine alibakia katika pikipiki, baada tu ya kumwagia tindikali mtu yule alikimbia mpaka pale alipokuwa imesimama pikipiki, alipanda na kuondoka kwa kasi,” zilieleza habari hizo.

   Taarifa zilizopatikana jana asubuhi zilieleza kuwa ndugu na marafiki wa mfanyabiashara huyo, walikuwa katika mipango ya kumpeleka nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

   Chanzo: Mwananchi
   ==============
   Katika picha, ni eneo lilipotokea tukio la kumwagiwa Tindikali

   Last edited by n00b; 20th July 2013 at 00:36.
   I seriously mean it when I say, 'Get a life'


  2. Sir Leem's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th March 2008
   Posts : 535
   Rep Power : 809
   Likes Received
   69
   Likes Given
   6

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   Yupo Johannesburg anapata matibabu amesafirishwa asubuhi sana ,inasemekana amepata athari ya jicho mmoja na mkono umeunguzwa sana na tindikali ,inasemekana huenda ikawa vita vya kibiashara!!

  3. kapotolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th September 2010
   Location : Tanzania
   Posts : 3,691
   Rep Power : 85924969
   Likes Received
   2100
   Likes Given
   655

   Default

   Quote By FaizaFoxy View Post
   -Kazaliwa wapi? = Tunduru au Songea, kwani walikuwa wakiishi huko kabla ya kuhamia Dar.
   -Kasomea wapi? = Amesoma Tunduru, Songea na Dar, sidhani kama alimaliza sekondari.
   -Anatoka familia gani? = Familia yake ni ya Mzee wa kimahara aliyehamia Tanzania enzi za "maguo-guo", mama yake ni mtu wa Tanga na ana undugu na Omar Mapuri, balozi wa uchina na ambae aliwahi kuwa waziri wa Mbo ya ndani.
   -Je ni Myemen au Msaudia? = Ni Mtanzania na kwa mujibu wa habari za JF ana Uraia pia wa nchi hizo.
   -Passport ya Tanzania kaipataje? = Kazaliwa Tanzania na mama'ke ni Mtanzania
   -Alipewa uraia lini? = hajapewa kazaliwa kama Mtanzania.
   -Je ni kweli kontena zake hazikaguliwi? = Kuna ukweli katika hilo.
   -Je ni kweli ndiye balozi mdogo wa Tanzania China? = Hilo sijawahi kusikia.
   -Pesa kapata wapi? = aliziona fursa zilizopo Tanzania akazichangamkia.
   -Ana influence gani kwenye biashara tanzania = Ana inflence kubwa sana na anakuwa haraka haraka kiniashara mpaka anatisha.
   -Je ni kweli kuhusu tuhuma za walimuua dada yao kule baharini? = Uongo.
   -Analindwa na nani? = Angekuwa analindwa kiasi hicho angemwagiwa tindikali?
   -Analipa kodi (tax ref number yake ya TRA ) = Waulize TRA
   -ana assets zipi? = Ana majumba mengi Tanzania, Yemen na Dubai na biashara kubwa kubwa hususan kiwanda cha mshuka na foronya na maduka ya home shopping centre na mengineyo kama ya vifaa vya ujenzi na juzi juzi nasikia kafunguwa shopping center mpya huko Oysterbay (alipomwagiwa tindikali).
   -Kwa nini anapigwa sana vita? = Amejijengea chuki kwa ufedhuli na kibri chake na kutoelewana na watu.
   -Amesaidi vipi jamii ya Tanzania? = Kuingiza bidhaa kwa njia za mkato.
   -Je yumo kwenye siasa za Tanzania? = Hayumo
   -Maadui zake ni akina nani? = Kila mtu.
   -Ndugu zake ni akina nani? = wapo wengi tu.
   -Kwa nini yeye? = Mkorofi
   wewe ni faizafoxy original au fake? nimeku-miss sana, asante kwa majibu yako.

  4. omujubi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th December 2011
   Location : Bumbire Island
   Posts : 4,078
   Rep Power : 31858
   Likes Received
   1932
   Likes Given
   4378

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   Quote By REMSA View Post
   FaizaFoxy umejibu vema,kama ni mtihani basi tuseme una A+
   nimefurahishwa na kurejea kwa FaizaFoxy , labda atatujuzi kilichokuwa kimemsibu, kaeleza vizuri sana yaani unbiased.
   Tusiruhusu wasiotaka mabadiliko kuamua juu ya mustakabali wa mabadiliko - Onyesha ushirikiano!

  5. tosaby's Avatar
   Member Array
   Join Date : 20th April 2013
   Posts : 62
   Rep Power : 448
   Likes Received
   10
   Likes Given
   12

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   Quote By Ritz View Post
   Hiyo sheria ya wapi au fikra zako una uhakika gani na unachokisema hakuna anayejua tuwe na subira tutasikia mengi.

   Umetaja mtu kupigwa risasi kwa sababu tu unamchukia kama una ushahidi wowote kuhusu huyu jamaa basi visaidie vyombo vya dola.

   Kwa hiyo wewe mtu akiwa mkorofi apigwe risasi ndiyo dawa.
   Ritz kwa nn unasisitiza kila mara watu wapeleke ushahidi kwenye vyombo vya dola kuhusu huyu jamaa na raia wengi wamekwambia shutuma zake zipo hadi kwa amiri jeshi mkuu lkn hamna kilichofanyika ukadai wivu wa kike sasa acha hukumu nyingine zitolewe bila kufuata sheria wm si amesema wapigwe tu.Ila nakuomba ukuipata nafasi hebu upost thread kuhusu huyu jamaa ukirefer hile ya raia mwema ya 2010 na ile nyingine ya june-2012 ya kamanda mmoja ili uje side b kwn nahisi unafahumu mengi sana ili wengi tuelimike

  6. bwanaharusi's Avatar
   Member Array
   Join Date : 5th June 2011
   Posts : 37
   Rep Power : 541
   Likes Received
   18
   Likes Given
   23

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   mhhhhh Polisi Obay hawana haja ya kuhangaika

   wajisajili JF kisha kila kitu watapata humu


  7. Naibili's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th January 2011
   Location : MCHAGONI
   Posts : 1,661
   Rep Power : 39983
   Likes Received
   404
   Likes Given
   53

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   so he deserve! mwisho wa ubaya ni aibu, sheria ilipindiashwa na kuwanyima haki wengine, sasa ni zamu yake. wanasema malipo ni hapa hapa
   UJINGA NI KILEMA by NAIBILI

  8. bwanaharusi's Avatar
   Member Array
   Join Date : 5th June 2011
   Posts : 37
   Rep Power : 541
   Likes Received
   18
   Likes Given
   23

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   Quote By Radhia Sweety View Post
   Huyu jamaa balaa. Afadhali angekufa tu
   kwani wakati anaiba dola iko wapi?

  9. Nyakageni's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st February 2011
   Posts : 12,309
   Rep Power : 71520190
   Likes Received
   2287
   Likes Given
   1068

   Default

   Quote By omujubi View Post
   There are currently 4298 users browsing this thread. (128 members and 4170 guests)
   ....mengi huenda yakaibuka hapa!
   hadi Manji hapa yupo! Na mtoto wa mfalme Riz1.

  10. change123's Avatar
   Member Array
   Join Date : 8th October 2010
   Posts : 65
   Rep Power : 581
   Likes Received
   23
   Likes Given
   8

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   Quote By Nyakageni View Post
   Aisee! Ile 'mall' ya jirani na ubalozi wa Marekani imefunguliwa? Au ni yake?
   Yap, MALL ni ya kwao, inaelekea kala cha mtu au wivu tu wa binadamu wakaamua kumkomoa. Get well soon.

  11. kitali's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th April 2012
   Posts : 726
   Rep Power : 635
   Likes Received
   220
   Likes Given
   2

   Default

   Quote By Wanitakiani View Post
   Ni kweli, amemwagiwa tindikali usiku huu na watu wasiojulikana. Ni Said Mohammed Mahmoud, mdogo wake Gharib.
   sahihisho Said ndio mmiliki wa hiyo kampun akina Gharib, Abdallah, Swallah, na huyo mwingine ni ndugu zake wadogo yeye ndio mkubwa, kwa kifup wanamiliki Home shopping, Amana benk, kampun ya ujenz, Msasan Mall, kampun ya kuagiza na kupokea mizigo bandarin hizo ni chache kati ya msururu wa makampun walionayo, kwakifupi jamaa shule hajaenda ila hicho kichwa chake ni kama vichwa vya maprof 20 pale mliman, pamoja na kwamba kuna jins wameiweka ccm mfukon huyu jamaa anajituma balaa niliwah kufanya nae kaz flan yuko vizur sana kichwan, na kwa kias kikubwa anauendesha uchumi wa kariakoo.

  12. Nyakageni's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st February 2011
   Posts : 12,309
   Rep Power : 71520190
   Likes Received
   2287
   Likes Given
   1068

   Default

   Quote By bwanaharusi View Post
   mhhhhh Polisi Obay hawana haja ya kuhangaika

   wajisajili JF kisha kila kitu watapata humu
   Charles Kenyela, ni member humu, walimwita mChadema na kushushwa cheo

  13. Tumsifu Samwel's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th July 2007
   Posts : 1,407
   Rep Power : 1120
   Likes Received
   137
   Likes Given
   109

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   Quote By Ritz View Post
   Kwa hiyo wewe mtu akiwa mkorofi apigwe risasi ndiyo dawa.
   Mkuu mbona unajitia upofu? umesahau kauli ya "liwalo na liwe" Kwamba "wa pigwe tu" kupigwa kupo kwa aina nyingi mkuu.

   Inasikitisha sana huko tuendako ni kubaya sana....

  14. Nyakageni's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st February 2011
   Posts : 12,309
   Rep Power : 71520190
   Likes Received
   2287
   Likes Given
   1068

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   Na inasemekana ni moja ya watoa mabilioni kufadhili CCM na kwa sasa yuko na alhaji Abdallah Richmonduli Lowassa. Nina hofu na; Membe? Sitta?

  15. Jorojik's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st December 2012
   Posts : 902
   Rep Power : 633
   Likes Received
   314
   Likes Given
   322

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   Quote By Sigma View Post
   Si tu mwalimu.
   Hata mwanafunzi anaweza kuwa na access ya conc. HCL, H2SO4.
   two decades ago as a student I used to "steal" a tinge of Conc.HCL and Iron II sulphide (FeS) bars nakuja nazo bwenini usiku namix nje ya bweni upepo unakotokea, harufu inayotokea hapo mtahama bweni.... (they used to describe it as a rotten egg)
   Mkuu ulikuwa unajifunza ugaidi bila kujua. Tehe tehe tehe, just a joke.

  16. Mponjori's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st February 2011
   Location : ukarawa
   Posts : 2,213
   Rep Power : 1057
   Likes Received
   530
   Likes Given
   21

   Default

   Quote By Mo-TOWN View Post
   Kweli polisi ni dhana tu kwa TZ. Ikumbukwe mpaka leo hii watuhumiwa wa milipuko huko AR bado kukamatwa
   polisi ni watuhumiwa namba 1 mlipuko wa Arusha watajikamataje? 2015 ifike haraka tuyaondoe haya majizi Ccm.

  17. petrinamwana's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th December 2011
   Posts : 422
   Rep Power : 550
   Likes Received
   49
   Likes Given
   13

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   SIKU HIZ ukiona mtu anakukaribia kashika dumu kimb ia jiami mapema hata kama amebeba maji utamsogelea ukishajua kwenye dumu kuna maji si tindikali

  18. Jorojik's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st December 2012
   Posts : 902
   Rep Power : 633
   Likes Received
   314
   Likes Given
   322

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   Quote By kitali View Post
   sahihisho Said ndio mmiliki wa hiyo kampun akina Gharib, Abdallah, Swallah, na huyo mwingine ni ndugu zake wadogo yeye ndio mkubwa, kwa kifup wanamiliki Home shopping, Amana benk, kampun ya ujenz, Msasan Mall, kampun ya kuagiza na kupokea mizigo bandarin hizo ni chache kati ya msururu wa makampun walionayo, kwakifupi jamaa shule hajaenda ila hicho kichwa chake ni kama vichwa vya maprof 20 pale mliman, pamoja na kwamba kuna jins wameiweka ccm mfukon huyu jamaa anajituma balaa niliwah kufanya nae kaz flan yuko vizur sana kichwan, na kwa kias kikubwa anauendesha uchumi wa kariakoo.
   Kati ya watu wenye vichwa vibovu, maprofesa wapo. Fast learners hawasomagi hadi sijui degree tatu (PhD), wakijitahidi bachelor, then wanaingia mtaani kutatua matatizo ya jamii. Waangalie akina Bilgate.

  19. mitutwe pazi's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 16th February 2013
   Posts : 153
   Rep Power : 475
   Likes Received
   26
   Likes Given
   18

   Default

   Quote By timbilimu View Post
   Ni kweli amemwagiwa tindikali,nimethibitishiwa na wafanyakazi wa hapo.
   Jamani hata mimi rafiki yangu ni mfanyakazi wa home shoping center nimempigia simu anithibitishie taarifa hizi na amethibitisha kwamba ni kweli. kwa sasa jamaa(mgonjwa) anafanyiwa utaratibu wa kusafirishwa kupelekwa Afrika kusini kwa matibabu.

  20. Manyi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th December 2011
   Posts : 3,250
   Rep Power : 1158
   Likes Received
   591
   Likes Given
   387

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   Quote By Sir Leem View Post
   Yupo Johannesburg anapata matibabu amesafirishwa asubuhi sana ,inasemekana amepata athari ya jicho mmoja na mkono umeunguzwa sana na tindikali ,inasemekana huenda ikawa vita vya kibiashara!!
   Hii habari nimeipata asubuhi pia mkuu, ni kweli yupio Jberg na jicho moja limeharibika vibaya sana!

  21. change123's Avatar
   Member Array
   Join Date : 8th October 2010
   Posts : 65
   Rep Power : 581
   Likes Received
   23
   Likes Given
   8

   Default Re: Said Mohamed Saad - Mmiliki wa Home shopping Centre, amwagiwa tindikali!

   Quote By GHANI View Post
   Nadhani hiki ni kile kikundi cha chadema red bregade kimeanza kazi, serikali inahitaji kukifuta hiki chama cha waasi mara moja, dr slaa na mbowe wafungwe kifungo cha maisha na adhabu nzito.huu ndio uwe msemo wetu wana J.F ''CHADEMA HAIKUBALIKI, TUIPIGE VITA''.
   wewe kama huna comment weka mikono kwenye ma------ yako, sio kundika pumba, usione sifa kuitaja CHADEMa kwenye issue kama hii wakati unaju sio siasa. Kimtazamo tu inaelekea una uwezo mdogo sana wa kufikiri.


  Page 16 of 21 FirstFirst ... 61415161718 ... LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...