JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Kakobe aitunishia misuli TANESCO

  Report Post
  Page 1 of 6 123 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 109
  1. Ng'wanza Madaso's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st October 2008
   Location : Sanga Nh'walugesha
   Posts : 2,223
   Rep Power : 1124
   Likes Received
   228
   Likes Given
   871

   Default

   Askofu Kakobe azuia Tanesco kupitisha nyaya eneo la Kanisa   Askofu mkuu wa Kanisa la Full Gospel Fellowship, Zacharia Kakobe kwa kushirikiana na waumini wake amewazuia wafanyakazi wa Shirika la umeme (Tanesco) kupitisha nyaya za umeme eneo la kanisa lakeNa Leon Bahati

   ASKOFU mkuu wa Kanisa la Full Gospel Fellowship, Zacharia Kakobe ameligomea Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupitisha mbele ya kanisa lake njia ya umeme ya msongo mkubwa wa kilovolti 132.

   Akofu huyo pamoja na mamia ya waumini wake, jana walikusanyika mbele ya kanisa hilo lililo kando ya Barabara ya Sam Nujoma karibu na Mwenge, jijini Dar es Salaam wakiwa tayari kupambana baada ya kupata taarifa kwamba mafundi wa Tanesco wangewasili kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kupitisha njia hiyo ya umeme.

   "Mimi nimejiandaa kuongoza waumini wangu katika kukabiliana na yeyote. Mimi nipo tayari kufa na nitahakikisha hawapitishi njia hiyo labda wawe wameniua," alilalamika.

   Alilalamika kuwa iwapo umeme wa msongo huo utapitishwa eneo hilo utaathiri mitambo inayosaidia kunasa, kupaza na kurekodi sauti kwenye ibada zinazofanyika kanisani hapo pamoja na mpango wake wa kuanzisha kituo cha televisheni cha kanisa.

   Isitoshe, alisema kwamba tayari Tanesco wamemuarifu kuwa itabidi wayang'oe mabango mawili ambayo yaligharimu Sh120 milioni ili kupisha mradi huo.

   "Kama Watanzania haijatokea vita ya dini, basi ndiyo hii. Ni kubwa kuliko ile ya Wabarbeig," alisema Askofu Kakobe na kuitaka serikali iingilie kati suala hilo ili kuepusha dhahama inayoweza kutokea.

   "Mimi na waumini wangu tumekubaliana tutakesha hapa usiku na mchana. Maana nasikia huwa wanaweza kuja usiku kubomoa mabango haya," alisema Askofu huyo mwenye maelfu ya waumini jijini Dar es Salaam.

   Mwananchi lilipowasili jana eneo hilo ilikuta mamia ya waumini hao pamoja na Askofu Kakobe wakionekana kutokuwa na silaha yoyote lakini wakisisitiza kuwa wako tayari kwa vita dhidi ya mtu yeyote atakayefika eneo hilo kwa lengo la kung'oa mabango yao.

   "Walifikiri kwa kuwa sisi ni walokole tutakaa kimya, lakini sisi tunasema katika hili hakuna cha kusema tutamwachia Mungu. Mungu yuko 'busy' (anakabiliwa na majukumu mengi) ana kazi nyingi, hili ni jukumu letu," alisema Askofu Kakobe.

   Alilalamika kwamba utawala wa Rais Kikwete unalikandamiza kanisa lake huku akidai kuwa kama ingekuwa madhehebu mengine ya dini, kitendo kama hicho kisingetokea.

   "Wanachokifanya hakina adabu! Kwa (askofu mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp) Pengo isingekuwa rahisi. Wanamuonea Kakobe kwa kuwa ni mnyonge," alilalamika Kakobe akisema yuko tayari kufa ili mradi ahakikishe njia hiyo ya umeme haiwekwi karibu na kanisa lake.

   Alibainisha kuwa awali njia hiyo ilikuwa ipite upande wa pili wa barabara mkabala na kanisa hilo, lakini wakazi wengi wa eneo hilo walipinga kitendo hicho hata pale walipoahidiwa kufidiwa.

   "Hawa waliokataa, hata pale walipoahidiwa kufidiwa, wengi ni wasomi wa chuo kikuu. Eneo hilo ndilo lenye nafasi kubwa. Lakini wakaona upande huu hauna wasomi wanaweza kukubali kirahisirahisi tu.

   Mimi katika hili nasema hapana," alisema Kakobe.

   Kakobe alisisitiza kuwa yeye na waumini wake wameamua kuwa watakuwa wakikesha eneo hilo kuhakikisha watapambana na yeyote atakayefika kung'oa mabango yao.

   Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alisema asingeweza kuwasiliana moja kwa moja na mwandishi wa Mwananchi lakini akaahidi kutuma taarifa ambayo hata hivyo haikujibu maswali ya msingi ambayo yanalalamikiwa na Askofu Kakobe.

   Ingawa taarifa hiyo haikugusia sababu za Tanesco kutotumia upande wa barabara ambao una nafasi kubwa na badala yake kubanana na makazi ya watu upande ambao kanisa hilo lipo, alisema Tanesco imefanya uchunguzi wa kitaalamu na kubaini kwamba njia hiyo ya umeme haiwezi kumuathiri binadamu wala mazingira yake.

   Alieleza kuwa njia hiyo inapita kwenye eneo la hifadhi ya barabara na tayari wamepata kibali cha Wakala wa Barabara (Tanroads) kujenga njia hiyo ya umeme inayolenga kukidhi mahitaji ya umeme jijini ambayo yameongezeka kutokana na wingi wa shughuli za kibinadamu jijini.

   Alisema mradi huo unaofadhiliwa na serikali ya Japani na unahusisha ujenzi wa njia kuu ya umeme wa msongo 132kV kutoka Ubungo mpaka Makumbusho na kituo cha kupozea umeme Makumbusho.

   "Shirika lingependa kuwataarifu wakazi wa maeneo hayo na wananchi kwa ujumla kuelewa kuwa hakuna madhara yoyote watakayopata wananchi wanaoishi na kupita maeneo yaliyo karibu na njia hiyo ya umeme," alisema Badra na kuongeza:

   "
   Shirika la umeme lilifanya utafiti wa kina na wa kitaalamu pamoja na wa kimazingira kabla ya kuanza ujenzi wa mradi huo na Baraza la Taifa za Mazingira (NEMC) lilijiridhisha na kuridhia kuwa ujenzi huo hautakuwa na matatizo au madhara yoyote kwa wakazi au wapita njia wa maeneo yaliyo karibu na njia hiyo ya umeme."

   Katika kufafanua namna njia hiyo itakavyojengwa ili wananchi wasidhurike, alisema nguzo zinazobeba umeme huo zinajengwa kwa urefu unaofuata viwango vya ujenzi wa msongo wa 132kV mijini ambavyo ni mita 23, akisema ndivyo vinavyokubalika kimataifa, na kuhakikisha usalama wa wakazi na wananchi katika maeneo hayo.

   Vile vile alisema mikono inayoshika vikombe vya waya za umeme katika nguzo hizo vitaelekezwa upande wa barabarani kwa umbali wa mita tatu kutoka kwenye nguzo.

   "Shirika lingependa wananchi waelewe kuwa ujenzi wa njia hiyo ya umeme wa namna hiyo katika maeneo ya mijini ni teknolojia inayoendelea kutumika sehemu nyingine duniani mfano, Japani," alisema.

   Source: Mwananchi

   My take:1... Naomba wataalamu wanifafanulie hapo penye maandishi mekundu pls,
   2...Wana JF naomba msaada wenu wa mawazo hapo penye Bluu na Light blue kuhusu huyu bwana mtu wa Mungu kuongelea vita badala ya kuongelea amani.
   THE DOG IS OK, BEWARE OF OWNER.


  2. #2
   Msanii's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th July 2007
   Posts : 6,502
   Rep Power : 2117
   Likes Received
   498
   Likes Given
   926

   Default Re: Askofu Kakobe azuia Tanesco kupitisha nyaya eneo la Kanisa

   Persopnally namfahamu Kakobe.
   Ila kwa hili amebadilika sana. Niliamini kwamba angepiga GOTI na kumwomba Mungu (ambaye yupo busy kusikiliza maombi yetu na kuangalia dhambi zetu) ili hawa mabest wa dowans wasiweke nguzo zao hapo yaani wabatilishe njia. Ila hiyo ya kusema kwamba tutapambana na serikali naona amejitwalia mamlaka ya kifikra ya waumini wake kwamba wajae ari na hamasa ya vurugu endapo wazee wa kata umeme wakifika hapo.

   Pia eleweni kwamba Kakobe ana hasira za kubomolewa parking ya magari kupisha ujenzi wa barabara, nakumbuka kabla kanisa halijameguka alikuwa na wataalam wa kila aina ambao ndio waliofanikisha na kusimamia kitaalam kanisa lake kujengwa within 21 days, I mean siku 21 kamili kanisa na upauaji ulifanyika pamoja na ofisi zake zilizopo chini ya kanisa (underground). sasa wataalam hawa (niliongea nao) walishawasiliana na wizara husika na kuwatengenezea plan mbadala kuepuka kumega eneo la maegesho ya magari ya kanisa. Sasa alipowatimua baada ya kujichanganya na siasa (wao walimpinga kwa hilo) akasahau kufuatilia na alikosa watu wenye ushawishi kwani hatua za awali zilishaanza kuchukuliwa kumega eneo la pili (kimchoro) kupisha upanuzi wa sam nujoma road. Sasa baada ya kuliwa eneo lake, jamaa wanakuja wanamwekea Superkilowatts mbele ya uso wake. naamini hasira zake zina msingi ulioanza mbali sana.

   Pili hawa tanesco wapuuzi kweli kweli, huwezi kupitisha msongo mkubwa wa umeme mahala ambapo kuna mkusanyiko na public activities, labda mfikirie kuwahamisha. wanaposema umeme huo hauna madhara mbona wanazuia watu kujenga jirani au chini ya nguzo au lines zenye msongo mkubwa wa umeme??

   Kakobe na Tanesco wooote mnataka kutuvunjia amani.
   Serikali iache ubabe na Kakobe punguza jazba. kuwa kama Daniel ambae alisugua goti mpaka nebukadreza alisema kuwa Mungu wa danieli ndiye Mungu mkuu.
   Katiba mpya ituletee Taasisi imara na si viongozi imara- Msanii
   [email protected]

  3. MziziMkavu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd February 2009
   Location : European Union
   Posts : 36,477
   Rep Power : 429504380
   Likes Received
   22043
   Likes Given
   68192

   Default

   Kakobe na Waumini Wake Wakesha Kulinda Tanesco Wasipitishe Umeme   January 05, 2010


   Askofu Mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible fellowship lililopo Mwenge jijini Dar es salaam na wauminini wake wameweka kambi nje ya kanisa hilo ili kuishinikiza Tanesco wasipitishe umeme mkubwa karibu na kanisa lao.

   Kakobe na waumini wa kanisa lake wameweka kambi kwa muda usiojulikana wakiwa wamevalia sare ya tisheti zenye maneno ya kuibeza Tanesco na Serikali yenye ujumbe unaosomeka kwa mbele "Tanesco mwogopeni Mungu" na nyuma "Baada ya richmond mmegeukia kanisa!!".

   Askofu mkuu wa kanisa hilo Zacharia Kakobe amesema kuwa endapo umeme huo utapitishwa pale jamii itarajie mpambano baina yao na Tanesco.

   Kakobe aliwataka Tanesco kwenda kujifunza kwake masuala ya umeme kwani amesoma kuliko wao na watarajie kupata upinzani mkubwa kutoka kwa waumini hao wenye uelewa mkubwa wa athari ya ememe huo.

   Alisema kinachofanya waumini hao kukesha hapo kwa muda wote ni kutokana na kutojua ni muda gani nyaya hizo zitapitishwa eneo hilo, hivyo wameona bora waendelee kuwepo kwa muda wote ili kuhakikisha hazipitishwi.

   "Huu ni ufisadi unaofanyika hapa,na tutakuwa hapa mpaka kieleweke hata kama ni mwaka mzima kwani huu umeme chuo kikuu waliukataa kutokana na madhara yake hivyo sisi hatuutaki pia na tutapambana" alisema Askofu Kakobe.

   Aidha alisema kuwa ujumbe katika tisheti hizo utakuwa unabadilika kulingana na matukio yatakayokuwepo kwani hawatojali gharama kwani uhuru ni gharama kubwa kuliko fedha zinazotumika kutengeneza tisheti hizo.

   Aidha Askofu Kakobe aliilaumu Serikali kwa kusema kuwa imekuwa na upendeleo kwa misikiti katika operesheni zake tofauti na inavyofanyika katika makanisa ya kiroho.

   "Serikali inapendelea misikiti zaidi kuliko kanisa,mfano Tabata dampo katika uvunjaji wa nyumba msikiti haukuguswa na zinatumika gharama kubwa na ushirikishwaji unakuwepo" alisema Kakobe.

   Pia Kokobe aliendelea kusema kuwa hayo yanayofanyika hapo Serikali haiwezi wala kuthubutu kuyafanya katika makanisa mengine hasa kwa Kardinal Pengo.

   "Huu ni ujinga mtupu,na kama angekuwa Kardinal Pengo asingethubutu kuuruhusu kufanyika kwake kamwe" alisema.

   Alibainisha kuwa ni juzi tu Serikali imemuita yeye kuwa ni kichuguu tu hivyo anataka kuwadhihirishia kuwa hawawezi kumkanyaga vile wapendavyo na wasitarajie hilo kutokea kamwe.

   Baadhi ya waumini waliokuwepo kanisani hapo wamesema kuwa wanaungana na Askofu wao ili kuhakikisha nyaya hizo hazipitishwi eneo hilo na watakuwepo kwa muda wote.

   "Tupo tayari hata kuzolewa na tinga tinga lakini hawapitishi nyaya hizo hapa na tutakuwepo kwa masaa 24 na tutahakikisha hilo linatekelezeka" walisema waumini.

   Muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jackson Mgesa alisema kuwa wapo kambini hapo kwa hali ya tahadhari na kuishinikiza Tanesco kutopitisha nyaya hizo kwani hazihitajiki kupitishwa eneo hilo kama walivyofanya chuo kikuu cha Dar es salaam.

  4. #4
   SMU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th February 2008
   Location : Mavurunza
   Posts : 6,219
   Rep Power : 209637540
   Likes Received
   2295
   Likes Given
   3379

   Default Re: Kakobe na Waumini Wake Wakesha Kulinda Tanesco Wasipitishe Umeme

   Siitizami hii kama habari ya kidini. Ingependeza kama habari hii ingekaa kwenye jukwaa la 'Habari Mchanganyiko' au kwengineko lakini sio hapa kweye jukwaa la Dini.
   "Rather than love, than money, than fame, give me truth" ----Thoreau

  5. Bujibuji's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th February 2009
   Location : NYUMBANI PANONO
   Posts : 23,631
   Rep Power : 51528095
   Likes Received
   12921
   Likes Given
   10024

   Default Kakobe aitunishia misuli TANESCO   Pale kwenye kanisa la full gospel kuna vijana kama sabini na nne wamevaa ma tshirt yameandikwa tanesco muogopeni mungu kwa mbele na nyuma yameandikwa Richmond imewashinda mnakimbilia makanisa.

   Wamesema watakaa hapo hadi waje kutolewa kwa bunduki.

   Sababu ya kufanya hivyo ni kugomea kung'olewa kwa mabango ya kanisa lao ili kupisha usimikaji wa nguzo za TANESCO zinazotoka Ubungo kwenda sub station ya Makumbusho.
   KAZI NDIO MSINGI WA MAENDELEO. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUENDELEA KWA MSINGI WA FEDHA. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUJITAWALA KAMA INATEGEMEA MSAADA KUTOKA NCHI ZA NJE- J. K. NYERERE


  6. PakaJimmy's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th April 2009
   Posts : 16,256
   Rep Power : 16106769
   Likes Received
   8178
   Likes Given
   3665

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   Tafsiri yake ni mbaya sana!

   Maneno hayo kwenye tshirts yanasikitisha, maana yamekaa kiswahili zaidi, hasa kama kweli yanasema "..Richmond imewashinda...!..

   Anyway ni ukweli, lakini hatua ya kuprint tshirts maalum za ishu hiyo ni ya mwelekeo hasi sana.

   SASA hao vijana wana nia gani...wana mpango wowote wa kupingana na dola katika zoezi hilo, au wamejiandaa kwa maombi?
   "The only thing that walks back from the tomb with the mourners and refuses to be buried is the character of a man.
   What a man is, survives him... it can never be buried"
   (GENEKAI-Jamiiforums, 4th November 2010 07:32PM).
   [email protected]

  7. Mdau's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th March 2008
   Posts : 1,488
   Rep Power : 1001
   Likes Received
   182
   Likes Given
   112

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   ningekuwa kamanda Kova,ningemkamata Kakobe kwa uchochezi na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani......

  8. Nasolwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th June 2008
   Posts : 1,713
   Rep Power : 1119
   Likes Received
   243
   Likes Given
   59

   Unhappy Re: KAKOBE VS Tanesco

   Quote By Mdau View Post
   ningekuwa kamanda Kova,ningemkamata Kakobe kwa uchochezi na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani......
   Mimi nilitegemea Bwana Askofu Kakobe angekuwa msitari wa mbele kumaliza matatizo kama haya kwa njia za amani zenye kuonyesha UWEPO WA MUNGU badala yake yeye anatumia njia za kibabe, vitisho vya mapambano bila silaha ambayo mwisho wa siku ni uvunjifu wa amani na kumwagika damu isiyo na hatia kwa ajili ya ubinafsi wa kutaka kuzuia swala muhimu lenye maslahi ya taifa. Ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko mwenye dhambi kufika mbinguni.

  9. Mike 1234's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd February 2009
   Location : Mikocheni
   Posts : 1,639
   Rep Power : 980
   Likes Received
   148
   Likes Given
   117

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   Mi nilishasema mtu huwezi kuibuka tu ktk karne hii na kujiita askofu bila kupitia chuo chochote cha kiuchungaji,lazima huyo mtu anamatatizo na hili la kakobe ni mfano halisi tshirts za richmondi wapi na wapi na wanacho kidai huu ni upuuzi na uchochezi,eti kasema ingekuwa ni msikiti usingeguswa au kanisa la pengo hivi kweli huyu jamaa ana akili sawa sawa kweli? na huu si uchochezi? mi ningekuwa kova saa nyingi nilishatuma vijana wa kazi kufanya mambo yao

  10. Lole Gwakisa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th November 2008
   Posts : 3,536
   Rep Power : 1380
   Likes Received
   764
   Likes Given
   460

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   Mwisho wa utapeli wa Kakobe unakaribia.
   Kama anataka siasa aingie tu mzima mzima kama Mtikila.Hao vijana 70 woote wanaingia selo moja tu!!
   Tanesco ni shirika la serikali na si la mtu na kujidai kupambana na Tanesco ni kuvua shati ili upambane na serikali.
   Kanisa la Kakobe liko barabarani, halina parking wala sidhani kama lina kibali cha kukalisha waumini wengi katika confined space.
   Hili suala la Kakobe Vs Tanesco litamuumbua.

  11. Saint Ivuga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st August 2008
   Posts : 25,340
   Rep Power : 88801448
   Likes Received
   7583
   Likes Given
   13009

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   sad story
   JF the best place to be. and the POWER of God be with us all the time.

  12. MwanajamiiOne's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 24th July 2008
   Location : On My Seat
   Posts : 10,468
   Rep Power : 201426665
   Likes Received
   6402
   Likes Given
   5755

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   Yaani imani ni kitu kibaya sana hebu fikiria hao wote wameacha kwenda makazini kizitafutia familia zao mlo wanalinda mabango ambayo yangeweza wekwa vizuri upya baada ya nyaya kupita au wanalipwa na Kakobe??

   Hivyo tu ni mabango je angeambiwa abomoe sehemu ya jengo hilo la kanisa si wangelala barabarani! samaki wekundu kabisa!!! Mxsixiis
   Serebuka unaweza pendwa tena, serebuka unaweza penda tena - Mwasiti, 2014

  13. TANMO's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th April 2008
   Location : Tanzagiza
   Posts : 8,727
   Rep Power : 15037362
   Likes Received
   3975
   Likes Given
   5014

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   Kakobe anastahili kuwekwa kwenye lile kundi la Mapapa la mzee Mengi kwa sababu anafanya watu waache shughuli zao kulinda kanisa kwa ajili ya maslahi yake mwenyewe huku akitumia jina la Mungu.
   Do Something......

  14. SMU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th February 2008
   Location : Mavurunza
   Posts : 6,219
   Rep Power : 209637540
   Likes Received
   2295
   Likes Given
   3379

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   "Rather than love, than money, than fame, give me truth" ----Thoreau

  15. Albedo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th February 2008
   Posts : 5,582
   Rep Power : 54733566
   Likes Received
   1391
   Likes Given
   623

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   Why is Kakobe Protesting? Kabla ya kutoa allegations tungejadili sababu zinazomfanya mtumishi huyu wa Bwana apinge Tanesco kupitisha Power Transmission facility karibu na Kanisa lake
   "SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM" Chris Lukosi kada wa CCM


  16. bm21's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th May 2008
   Location : Britain
   Posts : 781
   Rep Power : 850
   Likes Received
   14
   Likes Given
   24

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   Quote By PakaJimmy View Post
   Tafsiri yake ni mbaya sana!

   Maneno hayo kwenye tshirts yanasikitisha,maana yamekaa kiswahili zaidi, hasa kama kweli yanasema "..Richmond imewashinda...!..

   Anyway ni ukweli, lakini hatua ya kuprint tshirts maalum za ishu hiyo ni ya mwelekeo hasi sana.

   SASA hao vijana wana nia gani...wana mpango wowote wa kupingana na dola katika zoezi hilo, au wamejiandaa kwa maombi?

   Nafikiri tunahitaji maelezo zaidi kabla ya kumshutumu Kakobe. Je hayo mabongo yapo ndani ya road reserve, or power supply reserve?, Kama hayapo kwenye reserve kuna makubaliano yoyote ya kulipana fidia yaliyofikiwa na maamuzi yake yalikuwaje? Nafikiri tukipata majibu haya tutajua nani mkorofi. Kimsingi hata kama lile ni eneo halali la Kakobe, TANESCO wakilitaka lazima walipate lakini wanastahili kufuata taratibu.

  17. MwanajamiiOne's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 24th July 2008
   Location : On My Seat
   Posts : 10,468
   Rep Power : 201426665
   Likes Received
   6402
   Likes Given
   5755

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   Hivi na hizi Tshirt zimechapishiwa wapi? Aliyefanya kazi hii haweziwekwa matatani? au sheria zinasemaje hapa?
   Serebuka unaweza pendwa tena, serebuka unaweza penda tena - Mwasiti, 2014

  18. SMU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th February 2008
   Location : Mavurunza
   Posts : 6,219
   Rep Power : 209637540
   Likes Received
   2295
   Likes Given
   3379

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   Quote By bm21 View Post
   Nafikiri tunahitaji maelezo zaidi kabla ya kumshutumu Kakobe. Je hayo mabongo yapo ndani ya road reserve, or power supply reserve?, Kama hayapo kwenye reserve kuna makubaliano yoyote ya kulipana fidia yaliyofikiwa na maamuzi yake yalikuwaje? Nafikiri tukipata majibu haya tutajua nani mkorofi. Kimsingi hata kama lile ni eneo halali la Kakobe, TANESCO wakilitaka lazima walipate lakini wanastahili kufuata taratibu.
   Kuna habari hii imenukuliwa kutoka Nifahamishe.com inatoa mwanga juu ya malalamiko yake.

   Askofu Mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible fellowship lililopo Mwenge jijini Dar es salaam na wauminini wake wameweka kambi nje ya kanisa hilo ili kuishinikiza Tanesco wasipitishe umeme mkubwa karibu na kanisa lao. Kakobe na waumini wa kanisa lake wameweka kambi kwa muda usiojulikana wakiwa wamevalia sare ya tisheti zenye maneno ya kuibeza Tanesco na Serikali yenye ujumbe unaosomeka kwa mbele "Tanesco mwogopeni Mungu" na nyuma "Baada ya richmond mmegeukia kanisa!!".

   Askofu mkuu wa kanisa hilo
   Zacharia Kakobe amesema kuwa endapo umeme huo utapitishwa pale jamii itarajie mpambano baina yao na Tanesco.

   Kakobe aliwataka Tanesco kwenda kujifunza kwake masuala ya umeme kwani
   amesoma kuliko wao na watarajie kupata upinzani mkubwa kutoka kwa waumini hao wenye uelewa mkubwa wa athari ya ememe huo.

   Alisema kinachofanya waumini hao kukesha hapo kwa muda wote ni kutokana na kutojua ni muda gani nyaya hizo zitapitishwa eneo hilo, hivyo wameona bora waendelee kuwepo kwa muda wote ili kuhakikisha hazipitishwi.

   "Huu ni ufisadi unaofanyika hapa,na tutakuwa hapa mpaka kieleweke hata kama ni mwaka mzima kwani
   huu umeme chuo kikuu waliukataa kutokana na madhara yake hivyo sisi hatuutaki pia na tutapambana" alisema Askofu Kakobe.

   Aidha alisema kuwa
   ujumbe katika tisheti hizo utakuwa unabadilika kulingana na matukio yatakayokuwepo kwani hawatojali gharama kwani uhuru ni gharama kubwa kuliko fedha zinazotumika kutengeneza tisheti hizo.

   Aidha Askofu Kakobe aliilaumu
   Serikali kwa kusema kuwa imekuwa na upendeleo kwa misikiti katika operesheni zake tofauti na inavyofanyika katika makanisa ya kiroho.

   "Serikali inapendelea misikiti zaidi kuliko kanisa,mfano
   Tabata dampo katika uvunjaji wa nyumba msikiti haukuguswa na zinatumika gharama kubwa na ushirikishwaji unakuwepo" alisema Kakobe.

   Pia Kokobe aliendelea kusema kuwa
   hayo yanayofanyika hapo Serikali haiwezi wala kuthubutu kuyafanya katika makanisa mengine hasa kwa Kardinal Pengo.

   "Huu ni ujinga mtupu,na kama angekuwa Kardinal Pengo asingethubutu kuuruhusu kufanyika kwake kamwe" alisema.

   Alibainisha kuwa
   ni juzi tu Serikali imemuita yeye kuwa ni kichuguu tu hivyo anataka kuwadhihirishia kuwa hawawezi kumkanyaga vile wapendavyo na wasitarajie hilo kutokea kamwe.

   Baadhi ya waumini waliokuwepo kanisani hapo wamesema kuwa wanaungana na Askofu wao ili kuhakikisha nyaya hizo hazipitishwi eneo hilo na watakuwepo kwa muda wote.

   "Tupo tayari hata kuzolewa na tinga tinga lakini hawapitishi nyaya hizo hapa na tutakuwepo kwa masaa 24 na tutahakikisha hilo linatekelezeka" walisema waumini.

   Muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jackson Mgesa alisema kuwa
   wapo kambini hapo kwa hali ya tahadhari na kuishinikiza Tanesco kutopitisha nyaya hizo kwani hazihitajiki kupitishwa eneo hilo kama walivyofanya chuo kikuu cha Dar es salaam.
   "Rather than love, than money, than fame, give me truth" ----Thoreau

  19. kisikichampingo's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 28th October 2009
   Posts : 129
   Rep Power : 643
   Likes Received
   4
   Likes Given
   0

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   Printer ni mfanyabiashara. Hata ukimpelekea 'art work' iliyoandikwa 'Yesu si Mungu' ata print. Mbona magazeti yetu, hasa NIPASHE yana print matangazo ya waganga wa jadi wanaodai wanazo dawa za mapenzi, za kurefusha uume, n.k? wala hawashtakiwi?
   Kuhusu Kakobe, nina wasiwasi kwamba anapokwenda sipo!!

  20. Nyamayao's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd January 2009
   Location : Njoro
   Posts : 6,985
   Rep Power : 178022
   Likes Received
   2262
   Likes Given
   1913

   Default Re: KAKOBE VS Tanesco

   Quote By SMU View Post

   huyu mzee hiyo pesa ya ku print hizo tshirt c angeenda kusaidia hos/yatima? halafu wanashinda hapo cku nzima? familia zinaishije...bwana weee kazi ipo.
   Leo hii Yesu angekuwepo, si ajabu angeenda saluni kupunguza sharubu, angeenda kwa Maumba kushona Tuxedo na angekua na IPAD....TIMING


  Page 1 of 6 123 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Misuli ya mkunduni haemorroids
   By Bayo in forum JF Doctor
   Replies: 67
   Last Post: 27th July 2014, 20:32
  2. UMEME, Tanesco, Ngeleja OMBENI MSAMAHA Kwa KAKOBE
   By werawera in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 60
   Last Post: 28th December 2011, 20:08
  3. Wabunge, waziri watunishiana misuli
   By issenye in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 31
   Last Post: 27th May 2011, 23:12
  4. Tanesco, Kakobe na tatizo la umeme.
   By Stevemike in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 7
   Last Post: 18th March 2011, 17:10
  5. Chadema waitunishia Polisi misuli
   By Negotiator in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 1
   Last Post: 29th November 2010, 12:43

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...