JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

  Report Post
  Page 5 of 23 FirstFirst ... 34567 15 ... LastLast
  Results 81 to 100 of 448
  1. CHADEMA's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th April 2013
   Location : CHADEMA HQ
   Posts : 426
   Rep Power : 104415630
   Likes Received
   1751
   Likes Given
   83

   Default CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

   Ndugu waandishi wa habari,

   Tumewaiteni hapa mchana huu kwa dharura, kutokana na kujitokeza kwa jambo moja muhimu sana katika mustakabali wa chama chetu na taifa kwa ujumla. Jambo lenyewe ni hili:

   Kwa muda wa siku mbili, kuanzia kesho– tarehe 9 Julai 2013 hadi 10 Julai – kutakuwa na “KONGAMANO LA AMANI” lililoitishwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania – Tanzania Center For Democracy (TCD).

   Kongamano hilo litajadili na kutafakari Amani ya Taifa, litafanyika kwenye hoteli ya White Sands ya jijini Dar es Salaam. Litafuguliwa na Mwenyekiti wa TCD, Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Mheshimiwa James Mbatia na litafungwa na Rais Jakaya Kikwete.

   Baadhi ya washiriki, ni pamoja na mawaziri, viongozi wakuu wa vyama vyenye wabunge ambavyo ni wanachama wa TCD – Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), United Democracy Party (UDP), Tanzania Lebour Party (TLP), NCCR- Mageuzi na CHADEMA.

   Aidha, chama cha UPDP nacho kitashiriki mkutano huo kwa niaba ya vyama vingine ambavyo havina wabunge.

   Ndugu waandishi wa habari,
   CHADEMA kikiwa mmoja wa wadau wakubwa wa TCD, kimepokea mwaliko wa mkutano huo. Hata hivyo, tunapenda kutumia nafasi hii, kupitia kwenu, kuutangazia umma na Watanzania wote wanaotutakia mema na kulitakia mema taifa hili, kwamba hatutashiriki mkutano huo kwa sababu zifuatazo:

   Kwanza, Mwenyekiti wa TCD, Mheshimiwa Mbatia kwa makusudi amekiuka maazimio ya kikao ya kuteuwa Mwezeshaji wa mkutano huo na badala yake akafungamana na CCM kuteuwa watu wanaowataka wao.

   Pili, CHADEMA haitashiriki mkutano huo kwa kuwa Amani haijadiliwi. Amani inatengenezwa na kuwapo kwa mazingira ya haki na usawa; na kwamba aliyebobea katika uvunjaji wa haki hizo, ni serikali yenyewe.

   Katika mazingira haya, CHADEMA inaona hakuna umuhimu wa kushiriki kwenye mkutano ambao washiriki ni wale wale wanaotuhumiwa kuvunja haki za binadamu.

   Tatu, Amani siyo ya vyama vya siasa pekee yake. Amani inahusisha wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wa kidini, taasisi za kiraia na mashirika yasiokuwa ya kiserikali. Taarifa zilizopo, ni kwamba mkutano huu haukushirikisha viongozi wa kidini, na hivyo, tunadhani kuwa siyo jambo zuri kama kweli tunataka kutafuta amani ya taifa.

   Nne, CHADEMA haitashiriki mkutano huo kwa kuwa aliyepanga, aliyefadhili na aliyeitisha mkutano huo kwa mgongo wa TCD, ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mizengo Kayanza Peter Pinda, ambaye ndani ya nafsi yake, haonekani kuwa na dhamira ya dhati ya kuwapo amani katika taifa letu.

   Ndugu waandishi wa habari;
   Ninyi ni mashahidi wa jinsi Waziri Mkuu Pinda alivyo mstari wa mbele katika kuhubiri kauli za chuki, uhasama, uchochezi, ubabe na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini. Siyo mara moja wala mbili, Waziri Mkuu Pinda amesikika, tena ndani ya Bunge, akihamasiha vyombo vya usalama kuvunja sheria kwa kupiga, kuteka na kung’oa meno watu wanaotumia haki zao za kikatiba kushinikiza serikali kuchukua hatua dhidi ya maovu.

   Tano, CHADEMA haitashiriki katika mkutano huo kwa kuwa Serikali ya CCM inayofadhili mkutano huu, imejaa unafiki kwa kuhubiri amani mchana, wakati usiku inachochea uhasama wa kidini, kisiasa na inawagawa Watanzania kwa misingi ya imani za kidini na vyama.

   CHADEMA inao ushahidi usio na chembe ya mashaka, kwamba mifarakano mingi inayotokea kwenye jamii, mapigano katika koo mbalimbali, ugomvi wa kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji, machafuko kwenye mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani, sababisho lake kuu ni CCM kuvitumia vyombo vya dola, ili kukibeba chama hicho.

   Tunataka umma utuelewe, kwamba tuna dhamira ya dhati ya kuona Tanzania inakuwa kisiwa cha amani, lakini hatutakubali kushiriki katika vikao ambavyo wanaoviongoza hawana dhamira hiyo. Ili amani iweze kupatikana, ni sharti kuwepo mijadala inayoingia kwenye viini vinavyosababisha amani ikosekane na hatua hiyo ianze kuchukuliwa na ionekane inachukuliwa na serikali.

   CHADEMA iko tayari, kufanya kazi ya kutafuta amani na wale wanaopenda demokrasia. CHADEMA haifanyakazi na wanafiki wa amani.

   Imetolewa na:
   Benson Singo Kigaila,
   Mkurugenzi wa Oganaizesheni ma Mafunzo,
   Dar es Salaam
   Last edited by CHADEMA; 8th July 2013 at 19:01.

  2. Mwita Maranya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st July 2008
   Location : Ikorongo Game Reserve
   Posts : 10,518
   Rep Power : 2478338
   Likes Received
   7785
   Likes Given
   6980

   Default re: CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

   Quote By Simiyu yetu View Post
   Mwita wewe unajira gani unatumika kama tambala la deki tangu umepelekwa kata ya mianzini kwenda kuitetea chadema ukagongwa na chama kimekufa mianzini ndo basi tena ulidhani bongo ni moshi.

   Aibu yako au aibu yenu mtaendelea kusamaratishwa,bado arusha j.pili mtagongwa tena mnajiita chaga development manfesto(chadema) mtaipata tu.
   Unajua wewe Simiyu ninakuhurumia kwakuwa hata hujitambui, unapelekwa pelekwa tu kama boya.
   Asubuhi nimekusoma ukilalamika kwa dada yako mmoja kuwa kwa hizi siku chache ukizokuwa umepigwa ban hapa JF maisha yako yalikuwa magumu sana kwakuwa hukuwa unapata posho yako ya 7,000 ambayoi huwezi kuipata bila kuitumikia.

   Sasa kweli unaweza kuthubutu kuninyoshea kidole katika mazingira kama hayo ambayo unafahamu kabisa bila hii ajira ya dharura ya lumumba project utarudia kazi yako ya awali ya kuokota chupa za plastic mjini na kwenda kuuza katika viwanda vya wahindi ilki ujipatie japo hela ya kununua mihogo hapo barabarani.
   Honesty is a very expensive GIFT. Do not expect it from cheap people.

  3. Mzee's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd February 2011
   Location : DUNIANI
   Posts : 9,926
   Rep Power : 165034
   Likes Received
   1811
   Likes Given
   3338

   Default re: CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

   Mvunjaji wa Amani hawezi kushiriki kongamamo la Amani.
   Ingekuwa ni jambo la kusikitisha kama Chadema wangeshiriki.

   Chadema lengo lao ni kuvuruga Amani na mshikamamo wa Taifa.
   DR. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

  4. Simiyu Yetu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th April 2013
   Posts : 16,405
   Rep Power : 0
   Likes Received
   2893
   Likes Given
   837

   Default re: CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

   Eti hatutashiriki,nimecheka sana kwani kelele za chura humzuia ng'ombe kunywa maji tokeni haraka sana.

  5. Makala Jr's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th August 2011
   Location : Africa
   Posts : 3,396
   Rep Power : 14549
   Likes Received
   1077
   Likes Given
   1

   Default

   Simiyu yetu; Amani iliyokuwepo enzi za uzima wa mwasisi wa taifa Mwl.Nyerere ilitokana na kuheshimu utu na thamani ya ubinadamu suala linalopiganiwa na CHADEMA kwa sasa. Leo hii CCM mnajivunia ukatili kwa kuwafananisha Watanzania mathalani wana Mtwara na kuwafananisha na wanyama huku mkijitapa kuwakata mapembe, huko ni kukosa busara,ushawishi na ushirikiano katika uongozi.Kama mnataka amani mbona hamjawakata "Mapembe" mafisadi wa EPA,RICHMOND,MEREMETA,RADAR na majangili walioko ndani ya chama chenu?

  6. Matagwamenji's Avatar
   Member Array
   Join Date : 15th May 2013
   Posts : 19
   Rep Power : 436
   Likes Received
   1
   Likes Given
   2

   Default re: CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

   Jamani watz tunakwenda wapi? si vema kujadgji watu. tujadili masuala. hoja zote hapo ni za kweli, amani unaumbwa na siyo kujadiliwa watu watowe mada wengine wachangie. TUREJEE KWNY MISINGI YA TAIFA<HAKI NA USAWA> MUNGU IBARIKI TANZANIA.

  7. Mungi's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 23rd September 2010
   Location : JF
   Posts : 16,733
   Rep Power : 201413717
   Likes Received
   9023
   Likes Given
   5180

   Default re: CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

   Quote By Simiyu yetu View Post
   Vipi sura ya slaa imekaa kama nini hata kwenye aina ya viumbe vya mungu sidhani kama ipo,pinda anakunyima raha ee,pole pinda kaletwa na mungu utafanya nini wewe kidampa tu.
   Pinda ni product ya SHETANI ndiyo maana anafanya mambo ya kipumbavu kila wakati. Kung'oa watu kucha na meno yeye, kuua watu yeye, kupiga watu yeye!!!!!!!!

   Weka Pinda mbali na binadamu!!
   God will not permit any troubles to come upon us, unless He has a specific plan by which great blessing can come out of the difficulty..

  8. utaifakwanza's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st February 2013
   Posts : 12,076
   Rep Power : 28563
   Likes Received
   921
   Likes Given
   938

   Default CHDEMA; amani HAIJADILIWI

   CHADEMA imesema inaamini kuwa amani haijadiliwi bali huja yenyewe. nanukuu "Pili,Chadema haitashiriki mkutano huo kwa kuwa Amani haijadiliwi"
   ........

   maneno hayo yapo ktk moja ya matamko ya chama hicho kususia vikao vya kujadili viashiria vya kuvunjika kwa amani ya nchi ambapo wadau mbalimbali wameandaa kongamano la kujadili na hatimaye kuja na majibu ya namna ya kushirikiana kama taifa katika kuilinda, kuidumisha na kuienzi amani ya nchi ambayo tumeirithi kutoka kwa babu zetu hususan waasisi wa taifa hili tanzania.

   Kauli hii inanifanya niamini kuwa kuna tatizo katika think tank ya chadema ambayo imedhihirisha ku fail na hivyo kuashiria anguko la chama hicho.

   MY TAKE; mwalimu nyerere aliwahi kusema kuwa anayekula nyama za watu huwa haachi.
   Last edited by utaifakwanza; 8th July 2013 at 19:47.

  9. matawi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th March 2010
   Posts : 2,027
   Rep Power : 1001
   Likes Received
   227
   Likes Given
   91

   Default

   Quote By Philip Dominick View Post
   Ahsante chadema
   Naunga mkono hoja, wacha wafu wazikane. Amani ya kweli siyo hii bali Mungu akipenda tutakombolewa muda si mrefu

  10. Matagwamenji's Avatar
   Member Array
   Join Date : 15th May 2013
   Posts : 19
   Rep Power : 436
   Likes Received
   1
   Likes Given
   2

   Default re: CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

   Jamani watz tunakwenda wapi? si vema kujadgji watu. tujadili masuala. hoja zote hapo ni za kweli, amani Inaumbwa na siyo kujadiliwa watu watowe mada wengine wachangie. TUREJEE KWNY MISINGI YA TAIFA<HAKI NA USAWA> MUNGU IBARIKI TANZANIA.

  11. OSOKONI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th October 2011
   Location : yamaguchi
   Posts : 4,836
   Rep Power : 1482
   Likes Received
   1263
   Likes Given
   957

   Default Re: Chadema:: Taarifa kwa vyombo vya habari

   Napenda na kuthamini msimamo usiotetereka wa chama changu!
   Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!

  12. Mwita Maranya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st July 2008
   Location : Ikorongo Game Reserve
   Posts : 10,518
   Rep Power : 2478338
   Likes Received
   7785
   Likes Given
   6980

   Default re: CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

   Quote By Kiranga View Post
   Ana miliki ya Ikulu tangu 2005. Ndiyo maana Mbowe na Slaa hawawezi kufanya dhifa ya kitaifa pale kumkaribisha Obama.At best wataalikwa tu.

   Kwa tunaojali etymology, miliki inatoka katika mzizi wa neno Malik, mtawala, ndo hapo unapata na malkia, mke wa mtawala.

   Kwa msingi huu Kikwete kama rais huwezi kusema hana miliki ya Ikulu, as a matter of fact kikatiba Tanzania rais ana dhamana ya kumiliki ardhi ya Tanzania nzima, achilia mbali Ikulu tu.
   Arifu kuwa na dhamana na kuwa na milki ni vitu viwili tofauti. Kikwete amekabidhiwa dhamana kwa kipindi kifupi tu lakini mmiliki bado ni yule yule.
   Honesty is a very expensive GIFT. Do not expect it from cheap people.

  13. Jackbauer's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th October 2010
   Location : EAST LONDON
   Posts : 5,873
   Rep Power : 31968
   Likes Received
   1838
   Likes Given
   350

   Default Re: Chadema:: Taarifa kwa vyombo vya habari

   TCD itajadili mambo ya mahakamani?

   Utesaji wa Ulimboka

   kufungiwa kwa mwanahalisi

   mauaji ya mwangosi

   mauaji ya father mushi

   mauaji ya mchungaji

   mabomu ya Olasiti na Soweto

   Mauaji ya raia yaliyofanywa na Polisi...n.k

   Baada ya kujadili nini kitafuatia?

   Ni kongamano la utafunaji na perdiems tu.

  14. OSOKONI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th October 2011
   Location : yamaguchi
   Posts : 4,836
   Rep Power : 1482
   Likes Received
   1263
   Likes Given
   957

   Default Re: Chadema:: Taarifa kwa vyombo vya habari

   Quote By Kimetah View Post
   pamoko kamanda
   acha lugha za kihuni hapa jukwaani!
   Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!

  15. chikutentema's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th December 2012
   Posts : 5,058
   Rep Power : 375599
   Likes Received
   1470
   Likes Given
   6736

   Default re: CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

   Quote By Kurugenzi ya Habari View Post
   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

   Ndugu waandishi wa habari,
   Tumewaiteni hapa mchana huu kwa dharura, kutokana na kujitokeza kwa jambo moja muhimu sana katika mustakabali wa chama chetu na taifa kwa ujumla. Jambo lenyewe ni hili:
   Kwa muda wa siku mbili, kuanzia kesho– tarehe 9 Julai 2013 hadi 10 Julai – kutakuwa na “KONGAMANO LA AMANI” lililoitishwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania – Tanzania Center For Democracy (TCD).
   Kongamano hilo litajadili na kutafakari Amani ya Taifa, litafanyika kwenye hoteli ya White Sands ya jijini Dar es Salaam. Litafuguliwa na Mwenyekiti wa TCD, Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Mheshimiwa James Mbatia na litafungwa na Rais Jakaya Kikwete.
   Baadhi ya washiriki, ni pamoja na mawaziri, viongozi wakuu wa vyama vyenye wabunge ambavyo ni wanachama wa TCD – Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), United Democracy Party (UDP), Tanzania Lebour Party (TLP), NCCR- Mageuzi na CHADEMA.
   Aidha, chama cha UPDP nacho kitashiriki mkutano huo kwa niaba ya vyama vingine ambavyo havina wabunge.
   Ndugu waandishi wa habari,
   CHADEMA kikiwa mmoja wa wadau wakubwa wa TCD, kimepokea mwaliko wa mkutano huo. Hata hivyo, tunapenda kutumia nafasi hii, kupitia kwenu, kuutangazia umma na Watanzania wote wanaotutakia mema na kulitakia mema taifa hili, kwamba hatutashiriki mkutano huo kwa sababu zifuatazo:

   Kwanza, Mwenyekiti wa TCD, Mheshimiwa Mbatia kwa makusudi amekiuka maazimio ya kikao ya kuteuwa Mwezeshaji wa mkutano huo na badala yake akafungamana na CCM kuteuwa watu wanaowataka wao.
   Pili, Chadema haitashiriki mkutano huo kwa kuwa Amani haijadiliwi. Amani inatengenezwa na kuwapo kwa mazingira ya haki na usawa; na kwamba aliyebobea katika uvunjaji wa haki hizo, ni serikali yenyewe.
   Katika mazingira haya, CHADEMA inaona hakuna umuhimu wa kushiriki kwenye mkutano ambao washiriki ni wale wale wanaotuhumiwa kuvunja haki za binadamu.
   Tatu, Amani siyo ya vyama vya siasa pekee yake. Amani inahusisha wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wa kidini, taasisi za kiraia na mashirika yasiokuwa ya kiserikali. Taarifa zilizopo, ni kwamba mkutano huu haukushirikisha viongozi wa kidini, na hivyo, tunadhani kuwa siyo jambo zuri kama kweli tunataka kutafuta amani ya taifa.

   Nne, Chadema haitashiriki mkutano huo kwa kuwa aliyepanga, aliyefadhili na aliyeitisha mkutano huo kwa mgongo wa TCD, ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mizengo Kayanza Peter Pinda, ambaye ndani ya nafsi yake, haonekani kuwa na dhamira ya dhati ya kuwapo amani katika taifa letu.
   Ndugu waandishi wa habari;
   Ninyi ni mashahidi wa jinsi Waziri Mkuu Pinda alivyo mstari wa mbele katika kuhubiri kauli za chuki, uhasama, uchochezi, ubabe na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini. Siyo mara moja wala mbili, Waziri Mkuu Pinda amesikika, tena ndani ya Bunge, akihamasiha vyombo vya usalama kuvunja sheria kwa kupiga, kuteka na kung’oa meno watu wanaotumia haki zao za kikatiba kushinikiza serikali kuchukua hatua dhidi ya maovu.

   Tano, CHADEMA haitashiriki katika mkutano huo kwa kuwa Serikali ya CCM inayofadhili mkutano huu, imejaa unafiki kwa kuhubiri amani mchana, wakati usiku inachochea uhasama wa kidini, kisiasa na inawagawa Watanzania kwa misingi ya imani za kidini na vyama.
   CHADEMA inao ushahidi usio na chembe ya mashaka, kwamba mifarakano mingi inayotokea kwenye jamii, mapigano katika koo mbalimbali, ugomvi wa kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji, machafuko kwenye mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani, sababisho lake kuu ni CCM kuvitumia vyombo vya dola, ili kukibeba chama hicho.

   Tunataka umma utuelewe, kwamba tuna dhamira ya dhati ya kuona Tanzania inakuwa kisiwa cha amani, lakini hatutakubali kushiriki katika vikao ambavyo wanaoviongoza hawana dhamira hiyo. Ili amani iweze kupatikana, ni sharti kuwepo mijadala inayoingia kwenye viini vinavyosababisha amani ikosekane na hatua hiyo ianze kuchukuliwa na ionekane inachukuliwa na serikali.

   CHADEMA iko tayari, kufanya kazi ya kutafuta amani na wale wanaopenda demokrasia. Chadema haifanyakazi na wanafiki wa amani.

   Imetolewa na:
   Benson Singo Kigaila,
   Mkurugenzi wa Oganaizesheni ma Mafunzo,
   Dar es Salaam
   Hakuna msimamo uliowahi kutolewa na viongozi wangu mimi nikauona haufai na nikaupinga..............naunga mkono tena mngesema tunashiriki mimi ningeshangaaa sana........

  16. Kiranga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th January 2009
   Posts : 27,953
   Rep Power : 77628742
   Likes Received
   14703
   Likes Given
   2693

   Default Re: CHDEMA; amani HAIJADILIWI

   Hawa watu mara nyingine mtu unafikiri unashindwa hata pa kuanzia.

   Amani haijadiliwi?

   Na majadiliano yote ya amani duniani, kuanzia Northern Island mpaka South Africa mpaka Mashariki ya kati kinachojadiliwa ni nini?

   Hivi Mnyika kaenda likizo au vipi?

   Huu upuuzi unapitapitaje? Kuna hata a proofreading process?

   Hii ni official commique ya CHADEMA jamani au ni wafuasi tu wameitoa?
   “Sanity is not truth. Sanity is conformity to what is socially expected. Truth is sometimes in conformity, sometimes not.”: Pirsig, Zen and the Art..

  17. OSOKONI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th October 2011
   Location : yamaguchi
   Posts : 4,836
   Rep Power : 1482
   Likes Received
   1263
   Likes Given
   957

   Default Re: Chadema:: Taarifa kwa vyombo vya habari

   Quote By Jackbauer View Post
   TCD itajadili mambo ya mahakamani?

   Utesaji wa Ulimboka

   kufungiwa kwa mwanahalisi

   mauaji ya mwangosi

   mauaji ya father mushi

   mauaji ya mchungaji

   mabomu ya Olasiti na Soweto

   Mauaji ya raia yaliyofanywa na Polisi...n.k

   Baada ya kujadili nini kitafuatia?

   Ni kongamano la utafunaji na perdiems tu.
   hivi jinai na ugaidi ni wa kujadili au kukamata watuhumiwa na kuwafikisha kwa pilato?
   Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!

  18. Daudi Mchambuzi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th November 2010
   Location : Arusha
   Posts : 13,510
   Rep Power : 429499693
   Likes Received
   7217
   Likes Given
   40049

   Default re: CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

   Quote By obamabongoleo View Post
   nyie ni washari watanzania tumeshawajua, hamuwezi kushiriki kujenga amani ya nchi
   Amani ya nchi haijengwi kwa kujadili.
   Kinara wa kupiga na kuua raiya anaanda dhifa ya kunywa damu mnazomwaga kwa mabomu na risasi za moto.

   Amani bila haki ni upuuzi.

   Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   "UJINGA NI NUSU YA KIFO"

  19. Makala Jr's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th August 2011
   Location : Africa
   Posts : 3,396
   Rep Power : 14549
   Likes Received
   1077
   Likes Given
   1

   Default Re: CHDEMA; amani HAIJADILIWI

   Mods ondoeni uzi huu kwasababu hauna tija,kuna mwingine ila mleta maada ameanzisha ili kuharibu mjadala wa thread yenye tamko!

  20. chikutentema's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th December 2012
   Posts : 5,058
   Rep Power : 375599
   Likes Received
   1470
   Likes Given
   6736

   Default re: CHADEMA: Hatutashiriki Kongamano la Amani la TCD, limefadhiliwa na CCM!

   Quote By obamabongoleo View Post
   TCD ni jumuiko la vyama vya siasa vyenye wabunge unaposema haikushirikisha taasisi za dini unamaanisha nini??? acheni uzuzu chadema
   Bila uwepo wa dini mbalimbali na mafundisho ya upendo hakuna kitu kinaitwa amani acha upaka shume wewe

  21. TOWNSEND's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th May 2011
   Location : kwa ngulelo
   Posts : 2,442
   Rep Power : 1027
   Likes Received
   401
   Likes Given
   35

   Default Re: Chadema:: Taarifa kwa vyombo vya habari

   misingi ya amani ni utawala wa sheria

  Page 5 of 23 FirstFirst ... 3456715 ... LastLast

  Tags for this Topic

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...