JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Waziri wa Fedha, Dr Mgimwa awasilisha Bajeti ya serikali 2013 - 2014

  Report Post
  Page 18 of 20 FirstFirst ... 81617181920 LastLast
  Results 341 to 360 of 397
  1. Luiz David's Avatar
   Member Array
   Join Date : 13th June 2013
   Posts : 56
   Rep Power : 440
   Likes Received
   20
   Likes Given
   0

   Default Waziri wa Fedha, Dr Mgimwa awasilisha Bajeti ya serikali 2013 - 2014

   Wana jamii, leo ndiyo siku ambayo hatma ya maisha ya mtanzania kiuchumi kwa mwaka wa fedha 2013/2014 inaenda kuainishwa na waziri wetu wa fedha dr W.Mgimwa pale atakapo wasilisha bajeti ya serikali.

   ===================

   Isome:

   Bajeti-2013/14 - Tanzania

   Kifupi:

   - Katika kipindi cha Julai hadi Aprili 2013, Serikali ilikopa shilingi bilioni 1,364.7 kutoka soko la ndani la mitaji kwa ajili ya kulipia dhamana za Serikali zilizoiva pamoja na shilingi bilioni 809.1 kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

   - Mwaka 2012/13 Serikali ilikadiria kupata mikopo yenye masharti ya kibiashara shilingi bilioni 1,254.1, sawa na Dola za Kimarekani milioni 800 kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika bajeti ya mwaka 2012/13 iliyopitishwa na Bunge lako tukufu. Hadi kufikia Mei 2013, Serikali ilipokea shilingi bilioni 947, sawa na dola milioni 600 kutoka benki ya Stanbic, na shilingi bilioni 59.2, sawa na dola milioni 37 kutoka benk ya Credit Suisse.

   - Serikali ilikadiria kutumia shilingi bilioni 15,191.9 katika mwaka 2012/13. Mgawanyo wa matumizi ya Serikali katika kipindi hiki ulikuwa kama ifuatavyo: shilingi bilioni 10,597.1 zilitengwa kwa matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 4,594.8 zilikadiriwa kutumika kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

   - Hadi kufikia Aprili 2013, matumizi ya kawaida bila kujumuisha malipo ya hatifungani zilizoiva (rollover) yalifikia shilingi bilioni 7,582.6, sawa na asilimia 82 ya makadirio ya mwaka. Kati ya kiasi hicho, malipo ya mishahara ya watumishi wa Serikali, katika wizara, Idara zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Taasisi za Umma yalikuwa shilingi bilioni 3,209.2 sawa na asilimia 85 ya makadirio ya mwaka ya shilingi bilioni 3,781.1.


   - Hadi mwishoni mwa Machi 2013, Deni la Taifa (likijumuisha deni la umma na sekta binafsi) lilikuwa shilingi bilioni 23,673.53 ikilinganishwa na deni la shilingi bilioni 20,276.6 Machi 2012 likiwa ni ongezeko la asilimia 17. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 18,282.02 ni deni la nje na shilingi bilioni 5,397.50 ni deni la ndani. Deni la nje, linajumuisha deni la umma la shilingi bilioni 15,203.34 na deni la sekta binafsi ni shilingi bilioni 3,078.69. Kiasi hicho cha deni la nje kinajumuisha deni halisi shilingi bilioni 16,087.43 na malimbikizo ya riba ya shilingi bilioni 2,194.59. Deni la ndani linajumuisha hati fungani za muda mrefu kiasi cha shilingi bilioni 4,261.03 na dhamana za Serikali za muda mfupi kiasi cha shilingi bilioni 1,136.48.

   Waziri anapendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332 kama ifuatavyo: -

   (i) Kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira kutoka asilimia 14 hadi asilimia 13. Hatua hii inalenga katika kutoa nafuu ya kodi kwa mfanyakazi;

   (ii) Kuanzisha kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni (commission) ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu za mkononi. Kodi hiyo itakusanywa na kampuni za simu kutoka kwa wakala wanaotoa huduma za kusafirisha fedha kupitia simu za mkononi;

   (iii) Kutoza kodi ya zuio kwa kiwango cha asilimia 5 kwenye malipo yatokanayo na huduma mbali mbali kama vile huduma za ushauri wa kitaalamu na nyinginezo (Consultancy services and other services). Kodi hii itatozwa bila kujali kama kuna Namba ya Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN) au la. Lengo la hatua hii ni kudhibiti na kulinda mapato ya Serikali;

   (iv) Kutoza kodi ya zuio kwenye bidhaa zinazonunuliwa na Serikali na Taasisi zake kwa kiwango cha asilimia 2 bila kujali kama kuna Namba ya Utambulisho wa Mlipa kodi (TIN) au la. Lengo la hatua hii ni kudhibiti na kulinda mapato ya Serikali;

   (v) Kufuta msamaha wa kodi ya zuio kwenye ukodishaji wa ndege kwa walipa kodi wasio wakazi (non-resident). Hatua hii inalenga katika kupunguza misamaha ya kodi na kuhuisha mapato ya Serikali;

   Hatua hizi za Kodi ya Mapato kwa pamoja zitaongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 131,686.

   Waziri anapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:-

   (i) Kuongeza kiwango cha Ushuru wa Bidhaa kwenye magari yasiyo ya uzalishaji (Non-Utility Motor Vehicles) ya umri wa zaidi ya miaka 10 kutoka asilimia 20 hadi asilimia 25. Hatua hii inalenga katika kupunguza uagizaji wa magari chakavu, kulinda mazingira na kupunguza ajali;

   (ii) Kuanzisha kiwango kipya cha Ushuru wa Bidhaa cha asilimia 5 kwenye magari ya uzalishaji (Utility Motor Vehicles) yenye umri wa zaidi ya miaka 10 yanayotambuliwa katika HS Code 87.01, 87.02 na 87.04. Hatua hii haitahusisha magari chini ya HS Code 8701.10.00; na HS Code 8701.90.00 ambayo kimsingi ni matrekta yaliyounganishwa; na magari yasiyounganishwa chini ya HS Code 8702.10.11; 8702.10.21, 8702.10.91; 9702.90.11, 8702.90.21; 8702.90.91; HS Code 87.04; 8704.10.10; 8704.21.10; 8704.22.10; 8704.23.10; 8704.31.10, na 8704.32.10, 8704.90.10. Lengo la kuanzisha kiwango kipya cha ushuru ni kupunguza uagizaji wa magari chakavu, kulinda mazingira na kupunguza ajali. Aidha, matrekta na magari yasiyounganishwa hayatatozwa ushuru huu kwa nia ya kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya uunganishaji wa magari na hivyo kuongeza ajira na mapato ya serikali;

   (iii) Kurekebisha viwango vya Ushuru wa bidhaa kwenye mafuta ya Petroli kama ifuatavyo: -

   a] Mafuta ya Dizeli kutoka kiwango cha sasa cha shilingi 215 kwa lita hadi shilingi 217 kwa lita ikiwa ni ongezeko la shilingi 2 tu;
   b] mafuta ya Petroli kutoka kiwango cha sasa cha shilingi 339 kwa lita hadi shilingi 400 kwa lita; na,
   c] mafuta ya Taa kiwango hakitabadilika kwa kiwango cha sasa;


  2. MduduWashawasha's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th March 2008
   Location : Dar es salaam
   Posts : 659
   Rep Power : 835
   Likes Received
   76
   Likes Given
   9

   Default Re: Waziri wa Fedha, Dr Mgimwa awasilisha Bajeti ya serikali 2013/14

   Nadhani hapa tuna masomo mengi..kuba ni kwamba Urais si kitu cha kukimbilia kwa ajili ya kushow off.Mi sioni maisha bora katika bajeti hii wala zilizopita na sina hakika na zijazo.Nilitegea issues kama serikali kufuta misamaha ya kodi isiyo na msingi,kuweka mitambo kwenye kila kampuni ya simu kurekodi namba za simu zinazopigwa,muda wa maongezi,na ujumbe mfupi na kuweka kukusanya kodi inavyostahili.
   kila siku bia,soda , sigara .itokee muujiza watu wote waamua kuacha kunywa pombe na kufanya mazoezi sijui itakuwaje.Hapa walevi wa sigara na pombe ndo ma heroes wa nchi hii.wanachangia kipato kikubwa sana .HALALISHENI NA BANGI /UNGA BASI

  3. masumbwe's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 17th October 2012
   Posts : 115
   Rep Power : 486
   Likes Received
   17
   Likes Given
   3

   Default Re: Waziri wa fedha awasilisha bajeti ya serikali.

   Quote By Mwanza Live View Post
   Anaendelea kuwasilisha anasema bajeti hii itatoa kipaumbele katika secta za elimu,maji nishati nk,huku ikilenga pia kupunguza misamaha ya kodi.
   Hawa jamaa waongo kweli eti kipaumbele ni elimu wakti bajeti ya wizara ya elimu kwenye idara ya ukaguzi wamewapa bil 1 badala ya bil 11 walizoomba, hapo mtu anasema eti kipaumbale elimu

  4. zumbemkuu's Avatar
   JF Bronze Member Array
   Join Date : 11th September 2010
   Location : street dweller
   Posts : 8,633
   Rep Power : 355221031
   Likes Received
   4045
   Likes Given
   13802

   Default Re: Waziri wa Fedha, Dr Mgimwa awasilisha Bajeti ya serikali 2013/14

   Quote By Prisoner 46664 View Post
   Mkuu,

   hati fungati ni nini?!
   hahahahahahaha!
   dah! mkuu kweli una haki yakutafuta budget ya kiinglish, hata mimi sijui mkuu.
   ''Overcome the devils with a thing called love'' bob marley

  5. Getstart's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th October 2012
   Posts : 4,578
   Rep Power : 32372583
   Likes Received
   1166
   Likes Given
   1853

   Default Re: kampeni za kitoto ndani ya bajeti

   Quote By SONGOKA View Post
   Ovyo kabisa, ndugu mgimwa na CCM wamechekesha. Wanajaribu kuwahadaa vijana waendesha bodaboda kuwa wamewaondolea kodi ya mapato (road license), ili kuwateka na kuwavutia kundini hasa wakati huu wa kuelekea 2015. lakini mlango wa nyuma petrol imeongezwa kwa sh 61 kwa lita moja. Ongezeko hili kwa mwaka ni mara mbili na nusu ya gharama za road license. Mh waziri alisoma kwa mbwembwe sana omission hiyo tena mara mbili lakini akapita kama farasi alipofika kwenye petrol. KIMSINGI HAWATADANGANYIKA na TUTAWAELEZA JANJA YENU YA KITOTO
   Tatizo wabunge waligurahia sana kuongeza bajeti kwenye maeneo yenye maslahi kwao. Ikiwemo, maji na umeme vijijini, mfuko wa vijanawanawake n.k. Matokeo yake ndiyo haya. Serkali kuongeza kodi ya petrol kwa kiasi kikubwa hicho kitakuwa na madhara kwenye bei ya chakula na gharama zingine. Natumaini wataliona ili na wiki ijayo walikatae ili serkali itafute chanzo kingine cha mapato. Kwa nini wasizitoze sahihi kampuni hizi za simu,?

  6. only83's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th October 2010
   Location : Dodoma-Mjengoni
   Posts : 4,964
   Rep Power : 10514
   Likes Received
   1980
   Likes Given
   1983

   Default Re: kampeni za kitoto ndani ya bajeti

   Hivi huyu Dr Mgimwa Phd yake ni ya chuo gani? Maana nimekuwa na shaka na uwezo wake, hawana tofauti na Mkulo kwa uwezo wa kufanya mambo.
   "Wasio na elimu takribani 77% ndio wanaongoza kumpenda JK na CCM (Afrobarometa, 2013)"
  7. BONGOLALA's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th September 2009
   Posts : 11,650
   Rep Power : 85903717
   Likes Received
   3751
   Likes Given
   440

   Default Re: kampeni za kitoto ndani ya bajeti

   matunda ya rais wa china kuja tanzania yameanza kulipa sasa,huku Kova akisisitiza kuzipigia marufuku Boxer za India,Mgimwa anahimiza vijana wanunue pikipiki za mchina,biashara ya mchina kushamiri zaidi tanzania

  8. Prince Tumbo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th April 2013
   Posts : 913
   Rep Power : 620
   Likes Received
   231
   Likes Given
   115

   Default Re: kampeni za kitoto ndani ya bajeti

   Visima vya mafuta vingi ni vyao,kwani hujuwi?...ng'ombe kakondeana lakini anakamuliwa tu...haya majamaa yana roho kama ya NCHEMBA MWIGULU..harafu yote yanafanana roho utadhani ni baba mmoja, ukiliona hili ni sawa na lingine...huko ccm labda kuna viapo vya kuwa na roho za namna hii...wizi wa fedha na wanyama wetu polini,kubambika kesi,kumwagia watu tindikali,kung'oa kucha,kuiba kura...ukoo wa panya huu,baba,mama na watoto wote sharubu na wote wezi...

  9. only83's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th October 2010
   Location : Dodoma-Mjengoni
   Posts : 4,964
   Rep Power : 10514
   Likes Received
   1980
   Likes Given
   1983

   Default Re: kampeni za kitoto ndani ya bajeti

   Quote By Getstart View Post
   Tatizo wabunge waligurahia sana kuongeza bajeti kwenye maeneo yenye maslahi kwao. Ikiwemo, maji na umeme vijijini, mfuko wa vijanawanawake n.k. Matokeo yake ndiyo haya. Serkali kuongeza kodi ya petrol kwa kiasi kikubwa hicho kitakuwa na madhara kwenye bei ya chakula na gharama zingine. Natumaini wataliona ili na wiki ijayo walikatae ili serkali itafute chanzo kingine cha mapato. Kwa nini wasizitoze sahihi kampuni hizi za simu,?
   Mkuu, ile hotuba haina maana, kuna vyanzo kibao vya mapato sijui inakuaje...Kuna madini, utalii, gesi, simu, nk. Kukimbilia kupandisha petroli na dizeli, road licence, nk ni kutaka kutuangamiza watanzania wa kipato cha chini na kati. Hawa ni wahuaji, ningetamani kama tungekuwa na wanaharakati wenye akili kama wale wa Kenya tungeandamana mpaka malango ya Bunge kuonyesha kutufurahishwa kwetu na hii bajeti ya mauti.
   "Wasio na elimu takribani 77% ndio wanaongoza kumpenda JK na CCM (Afrobarometa, 2013)"  10. SONGOKA's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th March 2012
   Location : umasaini
   Posts : 1,076
   Rep Power : 800
   Likes Received
   561
   Likes Given
   280

   Default Re: kampeni za kitoto ndani ya bajeti

   Quote By only83 View Post
   Hivi huyu Dr Mgimwa Phd yake ni ya chuo gani? Maana nimekuwa na shaka na uwezo wake, hawana tofauti na Mkulo kwa uwezo wa kufanya mambo.
   huyu jamaa hata mi nashaka sana na PHD yake, anapunguza kodi ya mshahara kwa asilimia moja..mshahara wenyewe ndo huo wamegoma kuongeza, kumwokoa mwananchi wangepunguza hii kodi kwa asilimia hamsini ili mfanyakazi aweze kumudu gharama nyingine zinazopanda. ovyo sana huyu jamaa

  11. Mjanga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th February 2011
   Location : "MWILINI MWANGU"
   Posts : 1,146
   Rep Power : 779
   Likes Received
   231
   Likes Given
   29

   Default Re: kampeni za kitoto ndani ya bajeti

   Hivi ni vijana wangapi wanamiliki Bodaboda na bajaji hapa Tz ambao watanufaika na ondoleo la tozo ya Road License??
   Huku ni kuwahadaa vijana hili wawatumie 2015. Na mazuzu ya Magamba yanafikiri kila waTz wote ni mazuzu- madhara ya kutumia m+a+k+a+l+i+o kufikiri badala ya Kichwa!
   "A broken heart won't heal if you keep on giving it to the same person that broke it"


  12. Mwamba Usemao Kweli's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th October 2012
   Posts : 703
   Rep Power : 604
   Likes Received
   134
   Likes Given
   16

   Default Re: BUNGE LA TANZANIA na MAKOFI KWA WAHISANI

   Upofu mbaya unawatesa

  13. Lukolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd December 2009
   Location : Iringa
   Posts : 5,121
   Rep Power : 86242795
   Likes Received
   3037
   Likes Given
   2058

   Default Re: Waziri wa Fedha, Dr Mgimwa awasilisha Bajeti ya serikali 2013/14

   Mbona sioni kuondolewa kwa misamaha ya kodi kwenye madini, viwanda na uwekezaji mwingine ambako watu wanasamehewa misahamaha kwa kiasi kikubwa sana? Sasa wanabaki kuwabana wasafirisha hela kwa njia ya simu, mbinu ambayo inatumiwa zaidi na maskini badala ya kuelekeza nguvu kwenye migodi?
   Nitashangaa sana kama wabunge watapitisha hili wazo la kodi za MPesa, Tigo Pesa na nyinginezo. Ni kodi za kihuni kabisa. Labda watoze asilimia moja na si asilimia kumi. Ni kuwaumiza maskini, wasio na uwezo wa kutumia mabenki ambao hiyo ndiyo njia yao rahisi ya kuhifadhi hela na kununua bidhaa.
   Kama mtu alikuwa waziri au hata mkuu wa mkoa katika serikali ya Kikwete, hafai kuwa Rais wa Tanzania. Kimsingi mtu huyo ni sehemu ya uongozi mbovu na wa hovyo ulioliingiza taifa letu katika umaskini mkubwa na mdororo wa uchumi tulionao sasa. Kama mtu huyu alijua namna ya kuiokoa nchi na hakufanya hivyo, ina maana alitusaliti watanzania na hafai kuwa Rais wa nchi. Kama hakujua ni nini cha kumshauri Kikwete ili Mambo yaende sawa, ina maana hana analolijua. Je anataka awe Rais ili afanye nini ilihali hakuna alijualo?

  14. ericmzee's Avatar
   Member Array
   Join Date : 20th April 2013
   Posts : 96
   Rep Power : 455
   Likes Received
   15
   Likes Given
   23

   Default Re: kampeni za kitoto ndani ya bajeti

   Sijui ni mliberali yule mtu!!!!??? Alikuwa anacheka cheka tu kama anatekenywa vile, anakosea kosea kusoma as if hakuipitia???? (Aibu)
   Faith is about trusting God even when you don't understand his plan.

  15. Kamanda Kazi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th December 2012
   Location : Mwanza, Tanzania
   Posts : 2,619
   Rep Power : 977
   Likes Received
   676
   Likes Given
   363

   Default Re: Bajeti ya serikali yaJamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

   Quote By Getstart View Post
   Mimi ninawashangaa mnpokuwa na mchecheto wa bajeti ambayo imekwishajadiiwa bungeni kuitia mawasilisho ya Wizara zote. Kipya ni kipi zaidi ya ongezeko la kodi
   kumbe uko kama mimi!!! mimi huwa nawashangaa watu wanaacha shughuli zao eti wanawahi kusikiliza hotuba ya bajeti. sijui, labda wao huwa wanawahi foleni ya kugawiwa pesa!!

  16. Mpatanishi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st July 2011
   Location : Kinondoni, Dar es salaam
   Posts : 1,672
   Rep Power : 3084668
   Likes Received
   312
   Likes Given
   73

   Default

   Quote By GIB View Post
   habari wana jf. mimi ni mwalimu wa secondary nimeajiriwa miaka kadhaa iliyo pita. mshahara wangu kwa sasa ni shilingi 354,000/= kwa mwezi. napanda daladala kwenda na kutoka kazini. na vuta kasigara, mara moja moja napata ka bia. na simu kwaajili ya kuwasiliana na baba na mama yangu pamoja na ndugu zangu walio mbali sanaaa na mimi. na majukumu mengi kama watanzania wengine wenye extended family. na michango ya harusi na vitu kama hivyo. naomba msaada wenu. je hii bajeti itanisaidie kujikomoa na hili lindi na umasikini? maana nimesikia wabunge wakipiga vigelegele ni vya furahaa au vyo kulia.?
   asante
   mkuu ww mbona hueleweki, umeajiriwa miaka kadhaa iliyopita????!!!! Bado unapokea mshahara wa 354,000 mbona waliojiriwa mwaka huu tu wameanza na 378,000!!

   Ww vipi mwalimu?? Au ulikopa mkopo bank??? Mana kama kweli uliajiriwa miaka kadhaa iliyopita ulitakiwa uwe unalipwa zaidi ya hapo

  17. kinauche's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th October 2012
   Posts : 6,044
   Rep Power : 1815
   Likes Received
   1343
   Likes Given
   38

   Default Re: kampeni za kitoto ndani ya bajeti

   Quote By SONGOKA View Post
   Ovyo kabisa, ndugu mgimwa na CCM wamechekesha. Wanajaribu kuwahadaa vijana waendesha bodaboda kuwa wamewaondolea kodi ya mapato (road license), ili kuwateka na kuwavutia kundini hasa wakati huu wa kuelekea 2015. lakini mlango wa nyuma petrol imeongezwa kwa sh 61 kwa lita moja. Ongezeko hili kwa mwaka ni mara mbili na nusu ya gharama za road license. Mh waziri alisoma kwa mbwembwe sana omission hiyo tena mara mbili lakini akapita kama farasi alipofika kwenye petrol. KIMSINGI HAWATADANGANYIKA na TUTAWAELEZA JANJA YENU YA KITOTO
   Nimemshangaa sana huyu waziri kufanya kampeni wakati wa kusoma hotuba. Nilikuwa namwona kama mstaarau fulani hivi lakini leo ameni-put off kweli. Anatafuta chea popularity kwa vijana wa bodaboda na bajaji.


   Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

  18. Bartazar's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th October 2011
   Posts : 696
   Rep Power : 656
   Likes Received
   113
   Likes Given
   79

   Default Re: Bajeti ya serikali yaJamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

   Trilioni 18 sijui zinatoka wapi! Kumi na tano tu hazikufikiwa, itakuwe 18?!!

  19. masatujr1985's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th October 2011
   Location : Anumbeye
   Posts : 1,355
   Rep Power : 784
   Likes Received
   283
   Likes Given
   68

   Default Re: BUNGE LA TANZANIA na MAKOFI KWA WAHISANI

   wadau wa maendeleo ama maadui wa maendeleo? Mitaala inawatambua hivyo

  20. zamlock's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th December 2010
   Posts : 3,769
   Rep Power : 1310
   Likes Received
   579
   Likes Given
   1

   Default Re: kampeni za kitoto ndani ya bajeti

   mimi nilisha sema kuwa ccm wote awafai kabisa kama mgimwa ndo akuna kitu kabisa

  21. meningitis's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th November 2010
   Location : sewahaji
   Posts : 7,151
   Rep Power : 0
   Likes Received
   3240
   Likes Given
   277

   Default Bajeti ya kipuuzi afya ni kwa hisani ya wafadhili tu!

   nimejaribu kuisikiliza kwa makini bajeti iliyowasilishwa na mgimwa kwa mbwembwe nyingi nimeona haina mashiko kabisa hasa katika swala la afya ambalo lilileta matafaruku mkubwa mwaka jana.hakuna kipengele kinachogusa moja kwa moja masuala ya afya.kwa nini iwe hivyo?sababu ni moja tu,kwamba kwa kuwa afya inapata hisani ya watu wa marekani na kadhalika.huu ni upuuzi wa hali ya juu.napinga kwa nguvu zote utegemezi wa wahisani katika suala nyeti la afya.
   ni upuuzi kuwekeza bilioni sita kwa TBC huku afya ikiwa ni tegemezi.ni upuuzi kuwekeza bilioni 2 kwa mikopo ya kinamama ambayo haitawafikia huku huduma ya afya kwa kinamama na watoto ikitegemea wahisani.ni upuuzi kuwekeza mabilioni kwa vijana ambao hawana afya(wanywa viroba)!nasema ni bajeti ya kipuuzi kuwahi kutokeaa!!
   kama waziri mwinyi kashindwa kuongea na kuomba fedha zaidi kwa ajili ya wizara ya afya basi mimi nawasilisha malalamiko yangu kupitia JF.

   ni kwanini tunashindwa kuwaamuru wachimbaji wa madini na rasilimali ya mafuta wachangie japo aslimia 2% tu katika afya?kwa nini tuwakamue watu wanaotumia Mpesa,Tigo pesa,airtel money,wanunuzi wa magari,wavuta sigara kuchangia elimu huku tukiwaacha barick na Tanzanite one wakituachia mashimo?
   AnOtHeR PrOtEsTEr HaS CrOsSed ThE liNe!!!!


  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...