Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 26
    1. #1
      John Mnyika's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th June 2006
      Location : Tanzania
      Posts : 926
      Rep Power : 13538
      Likes Received
      1095
      Likes Given
      11

      Default CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Issued exclusively through JF; press corps, feel free to use it in your stories tommorrow:

      TAARIFA KWA UMMA

      Taarifa inatolewa kwa umma na kwa vyombo vya habari kwamba Kamati Kuu ya CHADEMA inaendelea na kikao chake cha kawaida kilichoanza saa 5 asubuhi Dar es salaam katika Hoteli ya Keys Mbezi leo tarehe 2 Disemba na kikao hicho kitamalizika kesho tarehe 3 Disemba 2009.

      Ajenda za kikao hicho ni: Yatokanayo na muktasari wa Kikao kilichopita; Hali ya Siasa Tanzania; Tathmini ya Uchaguzi wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji; Kupanga shughuli za kutekeleza Mpango Mkakati wa chama kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010; Kuthibitisha Makatibu wa Wilaya/Mikoa na sekretariati zao; Taarifa za Rufaa mbalimbali za uchaguzi wa ndani ya chama; Taarifa ya Zanzibar; Taarifa kuhusu Mfumo wa uanachama kwa njia ya kieletroniki (E-Membership); Taarifa ya Fedha; Uteuzi wa Bodi ya Wadhamini; Tarehe za mikutano ya Baraza Kuu na Mkutano Mkuu.

      Aidha tunasikitika kupokea kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini na mmoja wa waasisi wa CHADEMA Kanali (Mstaafu) Geofrey Marealle kilichotokea jana usiku. CHADEMA inatuma salamu za pole kwa familia ya marehemu na wanaCHADEMA wote duniani kutokana na msiba huo. Salamu za rambi rambi zitatolewa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe mara baada ya kutaarifiwa utaratibu mzima wa mazishi toka kwa familia ya marehemu.

      Imetolewa tarehe 2 Disemba 2009 saa 11 jioni na Katibu Mkuu; Dr Wilbroad Slaa.
      Ni wakati wa Mabadiliko ya Kweli; tuwajibike!
      Napatikana pia kupitia Facebook, Twitter na mnyika.blogspot.com

    2. Study Abroad

    3. #2
      NgomaNzito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2008
      Posts : 513
      Rep Power : 682
      Likes Received
      10
      Likes Given
      0

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Sawa Bw. Mnyika

      Mbona hakuna agenda ya kina kafulila na mwenziwe Juju na hii habari ya wanachama wanaotaka kujitoa kwa wingi
      No Wicked Heart Shall Prosper

    4. #3
      Mwita Maranya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2008
      Location : Ikorongo Game Reserve
      Posts : 7,909
      Rep Power : 11993
      Likes Received
      5244
      Likes Given
      5097

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Mkuu mbona agenda ya Kafulila & Juju sijaiona? au mtawajadili/mliwajadili kwenye mengineyo? au sisimizi hawajadiliwi? na hili la zitto kuwapa nccr mageuzi magari kwa ajili ya kampeni ya kafulila mmeliangaliaje?
      ni hayo tu mkuu.
      Honesty is a very expensive GIFT. Do not expect it from cheap people.

    5. #4
      Jabulani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th March 2009
      Location : Kituo cha Polisi Jamii
      Posts : 2,968
      Rep Power : 1368
      Likes Received
      819
      Likes Given
      254

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Quote By John Mnyika
      ...Taarifa kuhusu Mfumo wa uanachama kwa njia ya kieletroniki (E-Membership); Taarifa ya Fedha; Uteuzi wa Bodi ya Wadhamini; ...
      Tutaomba uendelee kutupasha hata baada ya kikao
      Kamanda wa Polisi Jamii - Kanda Maalumu

    6. #5
      Kibunango's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2006
      Location : Tampere
      Posts : 6,802
      Rep Power : 44129
      Likes Received
      368
      Likes Given
      1424

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Quote By NgomaNzito
      Sawa Bw. Mnyika

      Mbona hakuna agenda ya kina kafulila na mwenziwe Juju na hii habari ya wanachama wanaotaka kujitoa kwa wingi
      Hao wamejitoa wenyewe Chadema, na hawajakata rufaa ya kuvuliwa vyeo vyao sasa agenda ni ya nini ilihali Katibu Mkuu alishalimaliza kila kitu!

      Sana sana Katibu huyo atatoa taarifa tu juu ya hao sisimizi pale itakapobidi.
      Save Water Drink Beer. "Alcohol doesn't solve any problem,
      But, if you think again, neither does milk."
      Vituko Vya Zenj

    7. Miaka 50

    8. #6
      Josh Michael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2009
      Location : Kibandani
      Posts : 2,503
      Rep Power : 1006
      Likes Received
      50
      Likes Given
      348

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      CHADEMA kazi nzuri sana,
      Those who are too smart to engage in politics are punished by being governed by those who are dumber. ~Plato:D

    9. #7
      Pdidy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 12,283
      Rep Power : 3442
      Likes Received
      1322
      Likes Given
      855

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Quote By John Mnyika
      Issued exclusively through JF; press corps, feel free to use it in your stories tommorrow:

      TAARIFA KWA UMMA

      Taarifa inatolewa kwa umma na kwa vyombo vya habari kwamba Kamati Kuu ya CHADEMA inaendelea na kikao chake cha kawaida kilichoanza saa 5 asubuhi Dar es salaam katika Hoteli ya Keys Mbezi leo tarehe 2 Disemba na kikao hicho kitamalizika kesho tarehe 3 Disemba 2009.

      Ajenda za kikao hicho ni: Yatokanayo na muktasari wa Kikao kilichopita; Hali ya Siasa Tanzania; Tathmini ya Uchaguzi wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji; Kupanga shughuli za kutekeleza Mpango Mkakati wa chama kuelekea uchaguzi wa mwaka 2010; Kuthibitisha Makatibu wa Wilaya/Mikoa na sekretariati zao; Taarifa za Rufaa mbalimbali za uchaguzi wa ndani ya chama; Taarifa ya Zanzibar; Taarifa kuhusu Mfumo wa uanachama kwa njia ya kieletroniki (E-Membership); Taarifa ya Fedha; Uteuzi wa Bodi ya Wadhamini; Tarehe za mikutano ya Baraza Kuu na Mkutano Mkuu.

      Aidha tunasikitika kupokea kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini na mmoja wa waasisi wa CHADEMA Kanali (Mstaafu) Geofrey Marealle kilichotokea jana usiku. CHADEMA inatuma salamu za pole kwa familia ya marehemu na wanaCHADEMA wote duniani kutokana na msiba huo. Salamu za rambi rambi zitatolewa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe mara baada ya kutaarifiwa utaratibu mzima wa mazishi toka kwa familia ya marehemu.

      Imetolewa tarehe 2 Disemba 2009 saa 11 jioni na Katibu Mkuu; Dr Wilbroad Slaa.
      wanafiki watupu hawa..,wanadiscuss nini...watu wanazulumiwa kura zao wanashindwa kutoa hata mchango wa wakili ati jichangisheni muende mahakamani...dems chama....ndio maana kafulila maneno yake yasipoaminiwa hivi sasa yataaminiwa na wajukuu wa chadema ipo siku

    10. #8
      Charuka's Avatar
      Member Array
      Join Date : 20th October 2009
      Posts : 56
      Rep Power : 498
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Ni kikao cha kawaida, au cha dharula?

    11. #9
      Yetu Macho's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 15th June 2008
      Location : Tanzania
      Posts : 200
      Rep Power : 597
      Likes Received
      10
      Likes Given
      2

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      RIP- Marialle

      Chadema songeni mbele, msiyape muda mambo ya kina Kafulila na Juju maana wameondoka kama walivyoingia. Ni haki yao, ila ni muhimu sana mkazungumzia sana maadili ya uongozi (Kwenye mengineyo) maana tusipo wekana sawa hatutaweza linda imani kubwa watanzania waliyoanza kutuonyesha.

      Mnyika:- Tafadhali kwenye mengineyo hoji hatma ya chama hasa viongozi wa chama wanapojitokeza wazi wazi kuunga mkono mahasimu wa chama tena wale wanaotukana chama na viongozi wenzao. Nini mipaka ya uongozi na ushabiki wakiswahiba.

      Yetu macho

    12. #10
      Kaa la Moto's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th April 2008
      Location : Bristol
      Posts : 6,819
      Rep Power : 1942
      Likes Received
      428
      Likes Given
      4188

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Naitakia kamati kuu kikao chema na chenye mafanikio katika kujenga na kuimalisha Chama chetu.
      Nawaaminia viongozi wetu kuwa mtafanya yaliyo kweli. Achana na propaganda za kijani, songeni mbele tuijenge nchi yetu kwa faida ya watoto na wajukuu wetu.
      wakati Cuf wanataka kuchukua nchi mwaka 2000 CCM walikuja na single ya kusema Cuf ni waislamu na kwa sasa wanadai sisi Chadema ni chama cha wakristo sasa CCM nacho ni cha watu gani? Watu wakajibu mashetaaaaaniiiiii.!---Wana Kigoma.

      ....Pamoja na kansa ya uongozi wa CCM watu wataendelea kukichagua,au watu wanaweza wakachoka na kusema potelea mbali wakachagua chama KINGINE....Julius. Kambarage. NYERERE"

    13. #11
      Kakalende's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2006
      Posts : 2,910
      Rep Power : 1228
      Likes Received
      381
      Likes Given
      371

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Vipi kikao cha kawaida inakuwa 'BREAKING NEWS!' kunani Chadema?

    14. #12
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,002
      Rep Power : 2557
      Likes Received
      781
      Likes Given
      28

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Quote By NgomaNzito
      Sawa Bw. Mnyika

      Mbona hakuna agenda ya kina kafulila na mwenziwe Juju na hii habari ya wanachama wanaotaka kujitoa kwa wingi

      Mimi ndiyo maana nasema members hapa ama JF tumepoteza mwelekeo . Yaani Kafulila kujiondoa kwenye Chama inatakiwa kuwa agenda ?Jamani waacheni watu wafanye kazi .Hiyo ni issue itakuja kwenye yatokanayo . Sasa kama kuna mtu anaka kujiondoa Chadema naye iwe agenda kwamba wawazuie ama iweje ?

      Kwenye fedha ndiko tunataka kusikai watasema nini maana Mbowe katuhumiwa kula pesa nk .Kwenye fedha tunataka kuona Changes na signatories wanakuwa watu ambao ni watendaji na Mbowe aachie sahihi . Chadema wawe na Accountant ambaye hataliliwa kwamba ni mchaga .

    15. #13

      Quote By Kakalende
      Vipi kikao cha kawaida inakuwa 'BREAKING NEWS!' kunani Chadema?

      Kakalenda aliye leta habari hii kama breaking news ni Chadema ama wao wametoa taarifa za Kikao ? Haya hayafanywi na CCM ama ndiyo mwelekeo wenyewe tumepoteza ana kwa huwa tunaweza kubonyeza hapa na ku hoji ?

    16. #14
      Kigogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2007
      Location : Calabash
      Posts : 8,137
      Rep Power : 2082
      Likes Received
      1219
      Likes Given
      313

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Quote By NgomaNzito
      Sawa Bw. Mnyika

      Mbona hakuna agenda ya kina kafulila na mwenziwe Juju na hii habari ya wanachama wanaotaka kujitoa kwa wingi
      acha wajitoe kwa wingi maana wataingia wengine kwa wingi so hiyo sio hoja ya kujadili wala kuifanya ajenda
      ______________________________ _
      Niko tayari kufa huku nimesimama kuliko kuishi huku nimepiga magoti....

    17. #15
      Kigogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2007
      Location : Calabash
      Posts : 8,137
      Rep Power : 2082
      Likes Received
      1219
      Likes Given
      313

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Quote By Lunyungu
      Mimi ndiyo maana nasema members hapa ama JF tumepoteza mwelekeo . Yaani Kafulila kujiondoa kwenye Chama inatakiwa kuwa agenda ?Jamani waacheni watu wafanye kazi .Hiyo ni issue itakuja kwenye yatokanayo . Sasa kama kuna mtu anaka kujiondoa Chadema naye iwe agenda kwamba wawazuie ama iweje ?

      Kwenye fedha ndiko tunataka kusikai watasema nini maana Mbowe katuhumiwa kula pesa nk .Kwenye fedha tunataka kuona Changes na signatories wanakuwa watu ambao ni watendaji na Mbowe aachie sahihi . Chadema wawe na Accountant ambaye hataliliwa kwamba ni mchaga .

      asante sna kiongozi kwa maneno hayo..hayo ndo ya msingi kuzungumza katika kikao hicho ili akina Ngoma Nzito na mwenzie Kanda2 watafute mengine ya kuongea
      ______________________________ _
      Niko tayari kufa huku nimesimama kuliko kuishi huku nimepiga magoti....

    18. #16
      Albedo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th February 2008
      Posts : 4,974
      Rep Power : 1571
      Likes Received
      1075
      Likes Given
      554

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Quote By Lunyungu
      Mimi ndiyo maana nasema members hapa ama JF tumepoteza mwelekeo . Yaani Kafulila kujiondoa kwenye Chama inatakiwa kuwa agenda ?Jamani waacheni watu wafanye kazi .Hiyo ni issue itakuja kwenye yatokanayo . Sasa kama kuna mtu anaka kujiondoa Chadema naye iwe agenda kwamba wawazuie ama iweje ?

      Kwenye fedha ndiko tunataka kusikai watasema nini maana Mbowe katuhumiwa kula pesa nk .Kwenye fedha tunataka kuona Changes na signatories wanakuwa watu ambao ni watendaji na Mbowe aachie sahihi . Chadema wawe na Accountant ambaye hataliliwa kwamba ni mchaga .
      Kwa hiyo Mangi wanyang'anywe fursa ya kuwa wahasibu au
      "SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM" Chris Lukosi kada wa CCM

    19. #17
      Lunyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2006
      Location : Malampaka
      Posts : 8,002
      Rep Power : 2557
      Likes Received
      781
      Likes Given
      28

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Quote By Pdidy
      wanafiki watupu hawa..,wanadiscuss nini...watu wanazulumiwa kura zao wanashindwa kutoa hata mchango wa wakili ati jichangisheni muende mahakamani...dems chama....ndio maana kafulila maneno yake yasipoaminiwa hivi sasa yataaminiwa na wajukuu wa chadema ipo siku

      Unasema uko serious ama unapunguza uchovu ? Unadhani kwenda mahakamani kudai kuibiwa kura ndiyo jibu la shida ya uchaguzi TZ ? Kesi ngapi TZ hadi sasa nilienda Mahakamani na CCM wakashinda ? Hii si issue hapa ya kwenda Mahakamani mie nataka Chadema na wapinzi wote na sisi tuwaunge mkono na si kuwafunga kengele mnakimbilia JF kuandika kuda Tume ya Uchaguzi ya wote ambayo JK haiteuwi hii ndiyo jibu na mwisho wa CCM . Lakini JF kama wakazi wa Dar .NI wajanja sana na husema sana wanaujua ukweli lakini serikali za mitaa wameipa CCM tena sasa akili hii ? Mnataka hao wapinzani mnaowapigia kelele waje kupiga kura hadi mitaani kwenu ?

      Issue si Mangi kutolewa kwenye Pesa ni kwamba Mbowe kama kweli anatuhgumiwa kutuia vibaya pesa basi aondolewe ama aache kwa utashi wake ajiondoe awaachie wengine ndiyo maana ya mgawanyo wa kazi na madaraka .Wafanya siasa waendelee na watu wa pesa ambao ni Professionals wakiwa ni wanachama waaminifu waachwe wafanye kazi . Haiwezekani Komu awe accountant na kesho anasimama jukwaani huko mikoani pesa anatembea nazo ama inakuwaje ? Chadema liangalieni hili .

    20. #18
      Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2007
      Location : Mbagala, Jeshini
      Posts : 3,739
      Rep Power : 1173
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Quote By Lunyungu
      Mimi ndiyo maana nasema members hapa ama JF tumepoteza mwelekeo . Yaani Kafulila kujiondoa kwenye Chama inatakiwa kuwa agenda ?Jamani waacheni watu wafanye kazi .Hiyo ni issue itakuja kwenye yatokanayo . Sasa kama kuna mtu anaka kujiondoa Chadema naye iwe agenda kwamba wawazuie ama iweje ?

      Kwenye fedha ndiko tunataka kusikai watasema nini maana Mbowe katuhumiwa kula pesa nk .Kwenye fedha tunataka kuona Changes na signatories wanakuwa watu ambao ni watendaji na Mbowe aachie sahihi . Chadema wawe na Accountant ambaye hataliliwa kwamba ni mchaga .
      Lunyungu,

      Maneno yako ni sawia kabisa, na uzuri wako wewe unasimama kwenye ukweli hufuati upepo wa bendera.
      Mkulima kala Mbegu......

    21. #19
      ELNIN0's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th November 2009
      Posts : 2,526
      Rep Power : 987
      Likes Received
      248
      Likes Given
      50

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Quote By NgomaNzito
      Sawa Bw. Mnyika

      Mbona hakuna agenda ya kina kafulila na mwenziwe Juju na hii habari ya wanachama wanaotaka kujitoa kwa wingi
      Mkuu, Kamati kuu ya chama haiwezi jadili individuals hiyo issue alishalizwa zamani na katibu mkuu wake basi.

      By the way hao watu ni kina nani as far as Chadema is concerned? nafikiri hata kuendelea kuwaongelea hapa kwenye JF ni makosa its like we dont have crucial issues to put fowared for discussions....tuna mambo ya maana kujadili si kafulia na wenzake.

      Mnyika asante sana kutuhabarisha na tunawatakia kheri katika mkutano wenu kamanda.

      Aluta...

    22. #20
      Mchili's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th August 2009
      Posts : 623
      Rep Power : 624
      Likes Received
      13
      Likes Given
      6

      Default Re: CHADEMA yaitisha kikao cha Kamati Kuu

      Quote By NgomaNzito
      Sawa Bw. Mnyika

      Mbona hakuna agenda ya kina kafulila na mwenziwe Juju na hii habari ya wanachama wanaotaka kujitoa kwa wingi
      Too low

    23. FemaTV & Radio
    Page 1 of 2 12 LastLast

    Similar Topics

    1. Kikao cha kamati ya ushauri (RCC) RUVUMA kinaendelea
      By Paxman in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 1
      Last Post: 25th November 2011, 12:08
    2. Yaliyojiri kwenye kikao cha kamati kuu ya CDM 30.04.2011
      By GeniusBrain in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 236
      Last Post: 6th May 2011, 15:01
    3. kikao kamati kuu ya CCM
      By kisururu in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 6
      Last Post: 1st May 2011, 23:43
    4. Replies: 50
      Last Post: 20th March 2011, 17:11
    5. Tutegemee nini baada ya kikao cha kamati kuu ya ccm leo?
      By Don Alaba in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 34
      Last Post: 21st January 2011, 08:27

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...