Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mobile Search - Tufikirie Mbele zaidi

    Report Post
    Results 1 to 2 of 2
    1. Shy
      #1
      Shy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2006
      Posts : 4,922
      Rep Power : 0
      Likes Received
      75
      Likes Given
      0

      Default Mobile Search - Tufikirie Mbele zaidi

      Mauzo ya simu za mikononi kwa baadhi ya sehemu duniani yanatazamiwa kufikia bil 1 mpaka mwaka 2009 na simu za mikono zinazotumia mtandao ni nyingi zaidi ya mara 4 ukilinganisha na computer zilizounganishwa katika mtandao .

      Kampuni ya Dotmobi (www.dotmobi.net) inasema theluthi mbili ya watu wote duniani wameunganishwa na simu za viganja duniani leo hii na zaidi ya nusu ya watu wote ulimwenguni wanatazamiwa kuanza kutumia simu zilizounganishwa na internet hapo mwaka 2008 .

      Uchunguzi uliofanywa na IPSOS unasema kwamba 29% ya watumiaji wote wa simu za mikononi uingereza walitafuta habari na taarifa kwa kutumia simu hizo kwa mwaka 2005 , sijui idadi ya Tanzania au afrika kwa ujumla makampuni ya simu yanaweza kutueleza zaidi .

      Taarifa hizi zinavutia na kutia moyo na itaanzisha njia zuri zaidi za watu kuweza kutangaza bidhaa na biashara zao zingine kwa njia ya simu za viganja ingawa hatujawahi kusikia habari sana kuhusu matangazo ya simu hizi mara kwa mara na ni kampuni chache sana zinajitokeza katika kutangaza bidhaa zao kwa njia ya simu

      Mfano Tanzania tulikuwa na sherehe za sabasaba makampuni ya simu yangewekeana mkataba maalumu wa kutangaza bidhaa za watu wengine ambao wako ndani ya mabanda ya sabasaba , au mfano niko katika gari naenda mjini nikifika mbuyuni natakiwa kupata tangazo katika simu mbele yako ni office za dstv mambo kama haya

      Mpaka sasa makampuni mengi ya matangazo na watangazaji wenyewe hawatilii mkazo sana kutangaza kwa njia ya simu za mikono katika ripoti moja iliyotolewa na Forrester Research inayoitwa "Interactive Marketing Channels to Watch in 2007." Inasema ni asilimia 13 tu ya watangazaji hutumia ujumbe mfupi sms na asilimia 11 tu hutuma matangazo yao katika tovuti zinazotumia WAP .
      Kwa Tanzania nimeona kuna mfano livingroom , kismati sms na kampuni zingine zilizojitokeza kutangaza bidhaa zao kwa njia hii ya simu za mikono , hata televisheni ya ITV ina mchezo wake wa kipima joto sina uhakika kama hutumia zile namba kutangaza bidhaa za watu wengine au biashara zao ila kwa Celtel mfano siku fulani niliwahi kupata tangazo lao kwa simu yangu walitangaza bidhaa Fulani za cocacola .

      Inavyoonekana watangazaji wengi na makampuni mengi ya simu za mikono hawana uhakika kuhusu biashara hii , pia watu wengi wanaotumia simu za mikono hawajapata elimu ya kutosha na sababu za kutangaza katika search engine za simu za mikono kama CELTEL inawateja mil 2 kwa taarifa nilizonazo sioni sababu ya kwanini washindwe .

      MIPAKA NA UJUAJI WA MOBILE SEARCH

      Ingawa kuna itadi kubwa ya watumiaji wa simu za mikono ambao hutembelea mitandao kadhaa ya tovuti kuna mipaka na mambo kadhaa ambayo kwa kiasi Fulani yanaweza kuzuia ukuaji wa mobile search pia .

      · GHARAMA NA UENDESHAJI – usafirishaji wa taarifa toka sehemu moja kwenda kwingine inaweza kuwa ni shuguli pevu ukifananisha na mtandao wa computer , mfano niko mbuyuni napata tangazo la DSTV kesho nikienda Mbezi Beach natakiwa nipate tangazo nikokaribu na WHITESANDS hapa wataalamu wanasemaje ? ITAENDELEA

      · UKUBWA WA KIOO - ( screen size )Simu nyingi zina vioo vidogo kwahiyo inampa mtumiaji wakati mgumu anapotembelea tovuti zingine kwa njia ya simu yake

      · URAISI WA KUTUMIA – ( Ease of use ) kwa sababu ya udogo wa kioo ( screen ) mtumiaji anapata wakati mgumu kutafuta na kuclick vitu katika kurasa.

      · CONTENT NDOGO – Watoa huduma wengi wa simu hawawapi wateja wao content zima au zote za tovuti ay huduma wanazotafuta katika mtandao

      USHINDANI NA KUPANUKA KWA WIFI

      Sababu ingine ambayo inaweza kuzuia ukuaji wa mobile search ni kuongezeka au kukua kwa huduma za kasi za WIFI katika sehemu nyingi , viwanja vya ndege , mahoteli , vyuo , maduka makubwa na kadhalika na wakati mwingi ni bure , hii inawafanya watu watumie laptops , PDA na zana zingine zaidi ya simu za mikono .

      CLICK http://pwani.blogspot.com/2007/08/ma...le-search.html KWA HABARI ZAIDI

    2. RukaaJuu Final

    3. #2
      PanguPakavu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th July 2007
      Posts : 224
      Rep Power : 655
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default enterprenuers wako wapi???

      Quote By shy
      mfano niko mbuyuni napata tangazo la DSTV kesho nikienda Mbezi Beach natakiwa nipate tangazo nikokaribu na WHITESANDS hapa wataalamu wanasemaje ? ITAENDELEA
      kwa kupitia technolojia kama Global Positioning System (GPS)and Artificial Inteligence,technologia hiyo ya matangazo kutokana na position uliyopo yapo nchi za wenzetu huku.
      yani they are soo customized in such a way that,even different options an recommendations are available...,ushauri kwa makampuni TZ ni kutokuwa waoga.watanzania ni watu wanaojua ku-catch up.

      Quote By shy
      Inavyoonekana watangazaji wengi na makampuni mengi ya simu za mikono hawana uhakika kuhusu biashara hii , pia
      watu wengi wanaotumia simu za mikono hawajapata elimu ya kutosha na sababu za kutangaza katika search engine za simu za mikono kama CELTEL inawateja mil 2 kwa taarifa nilizonazo sioni sababu ya kwanini washindwe
      kwa kweli ni jambo la kushangaza sana,mie naamini hiyo area ni very potential.it can be done.
      halafu kwa vijana tanzania,vipiiiiii???tuamke!!! siku hizi technolojia au matumizi mapya ya technlojia huvumbuliwa na vijana(hasahasa),au kwa kifupi watu binafsi.sio makampuni.
      ni kiasi tu cha kukaa chini na kubuni njia nzuri ya kuwezesha.kama celtel sijui voda hawaoni umuhimu,watakuja uona pale unapokuwa na patent rights(sijui zipo huko kwetu).na njia pekee ni wao kununua huduma zako.
      naongelea interprenuers hapa!!vijana,sio kulalamika tu hakuna ajira wakati ajira umeshika mkononi(simu)

      mfano:-kwani inashindikana vipi watu kupata headlines za magazetini kwenye simu za mkononi TZ?kupata taarifa za hali ya hewa?kupata bei za mazao sokoni??yote hayo direct kiganjani??

      ku-generalize,nashauri enterprenuers wa-exploit hilo eneo kwani ni muhimu sana kwenye technolojia ya mawasiliano.zile enzi za simu kuwa kifaa cha msg na kupokea call zimepitwa na wakati.

    4. Miaka 50

    Similar Topics

    1. Replies: 9
      Last Post: 18th August 2011, 18:52
    2. USA, Japan, German, and China ipi iko mbele zaidi kisayansi na kiteknolojia?
      By Sumbalawinyo in forum Tech, Gadgets & Science Forum
      Replies: 51
      Last Post: 16th June 2011, 07:11
    3. Tufikirie juu ya miundombinu Ya chuo kikuu cha Dodoma
      By fikirini in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 7
      Last Post: 28th May 2011, 08:31
    4. Kwa wale wanaotumia Mobile kwa ku chat angalieni namna ya Ku Setup Mobile
      By MziziMkavu in forum Tech, Gadgets & Science Forum
      Replies: 1
      Last Post: 8th February 2011, 07:41

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...