JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

  Report Post
  Results 1 to 10 of 10
  1. #1
   BAK's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th February 2007
   Location : Mfaranyaki
   Posts : 43,970
   Rep Power : 429505982
   Likes Received
   26189
   Likes Given
   28962

   Exclamation Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

   Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

   Mwandishi Wetu
   Raia Mwema
   Novemba 25, 2009
   Kikwete yaanza kumshinda

   Sasa hata Dk. Shein azoza   SIKU chache tu baada ya kutuma ujumbe kwamba akipita mwakani hatabeba mawaziri wazee, Rais Jakaya Kikwete ameanza kutekeleza azma hiyo kwa kuwatangazia mawaziri wake kwamba amechoshwa nao kwa kuwa hawamsaidii, imefahamika.

   Habari ambazo Raia Mwema imepata zinasema kwamba Rais Kikwete na hata wasaidizi wake, Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wamekuwa wakali isivyo kawaida yao katika vikao vyao vya kazi.
   Kwa mujibu wa habari hizo, katika kipindi kiasi cha wiki mbili zilizopita, Rais Kikwete amekutana na mawaziri wake mara mbili na katika vikao hivyo amesema waziwazi kwamba mawaziri wake hawamsaidii kama alivyotarajia wakati akiwateua.


   "Hakikua kikao cha baraza, lakini alizungumza kwa ukali akiwaambia kwamba alipowateua alikuwa na matumaini makubwa nao kwamba atakuwa amepunguza kwa kiasi kikubwa uzito wa kazi.
   "Akawaambia amekuwa akilazimika kufanya mambo mengi ambayo yangeweza kufanywa na mawaziri wake aliowaamini na akawapa dhamana," anaeleza ofisa mmoja wa serikali aliyezungumza na Raia Mwema wiki kwa masharti ya kutotajwa gazetini.

   Mtoa habari huyo amesema wiki iliyopita Rais Kikwete alikuwa mkali kwa wasaidizi wake kuliko ilivyopata kutokea tangu aingie madarakani mwishoni mwa mwaka 2005.

   Imefahamika kwamba kabla ya kikao cha wiki iliyopita, kilichofanyika nje ya Dar es Salaam, Rais Kikwete aliwaita mawaziri wake ghafla katika hatua ambayo ilizua hofu miongoni mwao wakiamini kwamba huenda alitaka kuvunja Baraza lake.

   Habari zaidi zinasema katika kikao cha awali waziri mmoja mwanamke alikwepa kuhudhuria baada ya kupata fununu kwamba Rais Kikwete alikuwa amekerwa na baadhi ya kauli zake za hivi karibuni.

   Habari zinaeleza kwamba, hata Dk. Shein ambaye anafahamika ya kuwa mara nyingi hana hulka ya ukali amebadilika, na sasa naye ameanza kuwa mkali waziwazi katika vikao vya utendaji.
   "Kuna kikao kimoja ambacho baada ya Rais kumbana waziri mmoja kutokana na kuwasilisha waraka uliokuwa umejaa mapungufu, Makamu naye alizungumza kwa ukali akimtaka waziri huyo kuacha kufanya mambo bila kufuata taratibu," anasema mtoa habari huyo.   Dk. Shein

   Anaongeza: " Katika kikao hicho Rais alimkatiza waziri huyo mara kwa mara akitaka ufafanuzi na wakati mwingine kumlazimisha waziri huyo kubadili baadhi ya mambo ambayo aliona yana makosa mengi katika waraka wake.”


   Ukali wa ghafla wa Rais Kikwete, Dk. Shein na Pinda unatajwa kuwa umechochewa na utendaji usioridhisha wa mawaziri wengi unaosababisha viongozi hao wa juu kabisa kulazimika kufanya kazi ya ziada.
   Katikati ya habari hizo ni hali kwamba mawaziri wengi wanashindwa kuitetea na kuisimamia Serikali ndani na nje ya Bunge, mbele ya umma na katika shutuma nyingi zinazotajwa kwenye vyombo vya habari. Anasema mtoa habari huyo: "Rais alieleza wazi kwamba anakerwa na taarifa za mara kwa mara katika vyombo vya habari zikionyesha udhaifu mkubwa wa Serikali yake huku wasaidizi wake wakiwamo mawaziri wakishindwa kutoa hoja zenye nguvu au mkakati mahususi wa kukabiliana na taarifa hizo.”

   Japo tathmini inaonyesha kwamba si rahisi katika muda mfupi uliobaki kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu kuwa na mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, Raia Mwema imearifiwa ya kuwa tayari mchakato umeanza ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa wa kuchunguza mienendo ya watu wakiwemo wajumbe wa sasa wa Baraza la Mawaziri na wajumbe watarajiwa ikibidi kufanyika kwa mabadiliko.

   Habari zaidi zinaeleza kwamba yamekuwapo mapendekezo kwa Rais Kikwete ya kutaka abadili baadhi ya mawaziri waliopo kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wakitajwa kuwa wako msitari wa mbele katika inayotajwa kuwa ni vita ya ufisadi katika hatua ya kukisafisha Chama cha Mapinduzi (CCM) katika tuhuma za ufisadi na migawanyiko ya dhahiri ili kuvutia kura katika uchaguzi wa mwakani.
   Mbali ya kuingiza sura mpya na kupunguza baadhi ya mawaziri, kuna taarifa kuwa yapo mapendekezo kwa Rais ya uwezekano wa kupandisha ngazi naibu mawaziri walioonyesha uwezo mkubwa.

   Haya yakiendelea zimekuwapo taarifa za wizara mbalimbali ambako wafanyakazi wanawalalalimikia mawaziri wao kwa utendaji kazi usioridhisha.

   Kati ya waliotajwa na wafanyakazi hao ni pamoja na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati; Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya na Naibu wake, Dk. Makongoro Mahanga; Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsha Mwangunga na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Sophia Simba.

   Lakini akizungumza na Raia Mwema wiki iliyopita Chiligati alisema “hawezi kufanya mtihani na kujisahihishia mwenyewe.”
   “Hayo maoni ya watu siwezi kuyaingilia, mimi siwezi kufanya mtihani na kujisahihisha mwenyewe lakini naamini watendaji ofisi wanajua naingia ofisini saa ngapi na natoka saa ngapi,” alisema Chiligati na alipoulizwa kuhusu shughuli za chama kuingilia majukumu ya serikali, alisisitiza kutotaka kujisahihishia mtihani.
   Katikati ya mwezi huu akizungumza na vijana wa kutoka nchi mbalimbali za Afrika mjini Dar es Salaam, Rais Kikwete alituma salamu za mwanzo kwa wateule wake kwa kuwaambia vijana hao ya kuwa endapo atajaliwa kuongoza tena Tanzania mwakani, atafanya jitihada kubwa kuondokana na sura za wazee ambao atawabadilisha na vijana.

   Akizungumza katika mkutano wa vijana hao wa kulea viongozi wa Afrika, Rais Kikwete alisema atafanya mabadiliko makubwa kwenye Serikali yake akshinda uchaguzi ujao.
   Alisema Kikwete: “Wale viongozi wa rika langu, lazima waanze kuwaachia nafasi vijana. Tunahitaji wakuu wa wilaya vijana zaidi, wakuu wa mikoa vijana zaidi na hata mawaziri vijana zaidi. Ndivyo ilivyotokea kwetu sisi wakati tukiwa vijana.”
   Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action


  2. taffu69's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th February 2007
   Posts : 2,098
   Rep Power : 5034
   Likes Received
   526
   Likes Given
   432

   Default Re: Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

   Kila aina ya usanii utaonekana kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2010, vilio vyote kutoka kwa wananchi? Walikuwa wapi muda wote matatizo ya maji, njaa, umeme, huduma mbovu za afya na elimu, mikataba ya kuiteketeza nchi na mengineyo lukuki wasiyaone tangu walipoingia madarakani?.

  3. Ulimbo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th August 2009
   Posts : 642
   Rep Power : 757
   Likes Received
   65
   Likes Given
   10

   Default Re: Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

   Ssi tunachotaka ni huduma nzuri ambazo ni haki ya raia kikatiba. Kama watagombana au mawaziri watabadilishwa, si la msingi kama ambavyo kila kiongozi angetekeleza wajibu wake bila upendeleo au kwa ajili ya kutimiza matakwa yake ya kujinufahisha binafsi. Acha wajikosoe, wakiwajibika vizuri, hiyo ndo neema kwetu wananchi.

  4. Gelange Vidunda's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th August 2008
   Posts : 309
   Rep Power : 741
   Likes Received
   20
   Likes Given
   37

   Default Re: Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

   Until I see the Prezidaa actually do something I will remain with my set notion that he can't do jack schiit, nada, nothing!

   And the same old shit goes on, over and over, same old tired song.......ain't this a b*@^h!
   "Ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora"
   Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa.

  5. Mpita Njia's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd March 2008
   Posts : 7,031
   Rep Power : 3452
   Likes Received
   1102
   Likes Given
   911

   Default Re: Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

   Hana lolote, he us out to save his skin. Ni njia nyingine ya JK kutaka kujisafisha mbele ya wananchi ili aonekane safi isipokuwa wenye matatizo ni watendaji wake. Asilolijua ni kuwa watu wenye akili watamuona mwenye hatia kwa sababu kwanza yeye ndiye aliyewateua hao watu ambao wameshindwa kufanya kazi kwa matarajio yake. Pili, ana mamlaka ya kuwatimua au kuwabadilisha kwa jinsi anavyopenda yeye, kuwafikea tu itasaidia nini na imeshaonyesha kuwa hili ni sikio la kufa?
   I assume full responsibility for my actions, except the ones that are someone else's fault.


  6. #6
   kilema's Avatar
   Member Array
   Join Date : 23rd February 2009
   Location : MRINI
   Posts : 59
   Rep Power : 664
   Likes Received
   0
   Likes Given
   0

   Default Re: Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

   TATIZO LETU WATANZANIA NI KUTOKUWA NA MALENGO REALISTIC NA NDIO MAANA HATUWEZI KUWABANA VIONGOZI WETU. TUNAISHIA KUPEW ALILIMIA KADHAA BARABARA KADHAA? NINA MASHAKA KAMA MAWAZIRI WENYEWE WAKO NA MALENGO YA NAFASI WANAZOTUMIKIA

   TUKITAKA KWENDA MBELE BASI TUCHAGUE VIONGOZI WALIO NA MALENGO YA KUELEWEKA ILI TUWEZE KUPIMA MAFANIO YAKE. MFANO KATIKA KIPINDI CHANGU NITAJENGA SHULE FULANI MTAA FULANI YENYE MADARASA KADHAA KWA KUWANGO FULANI. BARABARA ZA MITAA FULANI ZENYE UREFU WA MITA KADHAA ZITATIWA LAMI.NITAONDOA FOLENI HAPA JIJINI KWA MIKAKATI HII. N.K.
   SIYO MTU ANAKUJA MIMI NTAJENGA MASHULE NITAJENGA HOSP. NITALETA MAJI SAFINA SALAMA. WANAOOMBA UONGOZI WAKITOA AHADI WAJE NA MIPANGO KAZI YA NAMNA YA KUTIMIZA HIZO AHADI ZAO. 2010 hATUDANGANYIKI
   OMBENI MTAPEWA: TAFUTENI MTAPATA:BISHENI HODI MTAFUNGULIWA

  7. #7
   Mchili's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th August 2009
   Posts : 732
   Rep Power : 778
   Likes Received
   38
   Likes Given
   50

   Default Re: Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

   Usanii mtupu, alitegemea nini alipokua anawateua bila kuangalia uwezo wao!!! Hata mawaziri washajua udhaifu wake, sawa na mbwa hana meno anakubwekea una haja ya kukimbi?

  8. Field Marshall ES's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th April 2006
   Posts : 13,876
   Rep Power : 196824
   Likes Received
   722
   Likes Given
   225

   Default Re: Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

   Quote By Mpita Njia View Post

   1. Hana lolote, he us out to save his skin. Ni njia nyingine ya JK kutaka kujisafisha mbele ya wananchi ili aonekane safi isipokuwa wenye matatizo ni watendaji wake.

   2. Asilolijua ni kuwa watu wenye akili watamuona mwenye hatia kwa sababu kwanza yeye ndiye aliyewateua hao watu ambao wameshindwa kufanya kazi kwa matarajio yake.

   3. Pili, ana mamlaka ya kuwatimua au kuwabadilisha kwa jinsi anavyopenda yeye, kuwafikea tu itasaidia nini na imeshaonyesha kuwa hili ni sikio la kufa
   ?
   - Strong analysis, safi sana!

   Respect.


   FMEs!

  9. MwanaFalsafa1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th February 2008
   Posts : 5,598
   Rep Power : 10040
   Likes Received
   738
   Likes Given
   504

   Default Re: Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

   “Hayo maoni ya watu siwezi kuyaingilia, mimi siwezi kufanya mtihani na kujisahihisha mwenyewe lakini naamini watendaji ofisi wanajua naingia ofisini saa ngapi na natoka saa ngapi,” alisema Chiligati

   Sijui kama wenzangu mmenotice hapo lakini hivi huyu Chiligati anajua kwamba kuingia kazini muda unaotakiwa na kutoka muda unao takiwa haku maanishi ni mchapa kazi? Mtu anaweza akaingia kazini saa mbili asubuhi atoka saa kumi asubuhi lakini utendaji wake usiwe wa kuridhisha. Kusema ukweli kauli ya hapo juu ya Chiligati imenifanya nimuone huyu jamaa ni hana common sense.

  10. MwanaFalsafa1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th February 2008
   Posts : 5,598
   Rep Power : 10040
   Likes Received
   738
   Likes Given
   504

   Default Re: Mtikisiko wazuka Baraza la Mawaziri

   Alisema Kikwete: “Wale viongozi wa rika langu, lazima waanze kuwaachia nafasi vijana. Tunahitaji wakuu wa wilaya vijana zaidi, wakuu wa mikoa vijana zaidi na hata mawaziri vijana zaidi. Ndivyo ilivyotokea kwetu sisi wakati tukiwa vijana.”

   Issue siyo kujaza tu vijana. La muhimu ni kuwaka watu ambao wanaweza kufanya kazi ipasavyo. After all JK, EL na wengi wa hao mawaziri hawaku anza leo wala jana uongozi na wote ni a product ya ujana huo huo. What's the point of raising the youth of today to be the failures of tomorrow?


  Similar Topics

  1. Baraza la Mawaziri
   By Mokoyo in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
   Replies: 24
   Last Post: 23rd December 2010, 22:44
  2. baraza la mawaziri
   By Gaza in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 20
   Last Post: 17th November 2010, 14:56
  3. Replies: 0
   Last Post: 14th November 2010, 16:25
  4. baraza la mawaziri
   By Dr.Mbura in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 6
   Last Post: 5th November 2010, 09:35
  5. Baraza La Mawaziri!
   By Ab-Titchaz in forum International Forum
   Replies: 49
   Last Post: 29th April 2008, 14:54

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...