Wadau mmesikia haya ya Zanzibar... CUF imepigwa chenga ama ? - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Jukwaa la Siasa


Jukwaa la Siasa Tanzania & World Politics General Discussion Forum. You need to be registered in order to post your comment(s)


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 24th November 2009, 09:41 PM   #1
Wadau mmesikia haya ya Zanzibar... CUF imepigwa chenga ama ?
Lunyungu Lunyungu is offline 24th November 2009, 09:41 PM

Date::11/24/2009Shamhuna,Khatib watia doa shangwe ya Karume, Maalim SeifNa Salma Said, Zanzibar
Â
WAKATI Zanzibar ikiendelea kushangilia maafikiano ya kihistoria baina ya Rais Amani Abeid Karume na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, juu ya uwezekano wa kuwepo kwa Serikali ya Mseto, mawaziri wawili wamejitokeza hadharani kutia doa shangwe hizo.

Wameeleza bayana kuwa Serikali ya Mseto si muhimu visiwani hapa.

Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Ali Juma Shamhuna na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Muungano), Mohammed Seif Khatib, wametofautiana na msimamo wa Karume ambaye alisema kuwa uamuzi wa kuwa na Serikali ya Mseto ni wa Wazanzibari wenyewe.

Tamko hilo la Karume alilitoa siku chache baada ya kukutana kwa faragha na Maalim Seif, ambaye baadaye aliitisha mkutano wa hadhara na kueleza kuwa CUF imeamua kumtambua rais huyo kwa kuwa kufanya hivyo kutarahisisha mazungumzo ya kutafuta muafaka.

Lakini Shamhuna, ambaye pia ni Waziri wa Habari wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ), alisema Zanzibar haihitaji Serikali ya Mseto wala Serikali ya Umoja wa Kitaifa, bali kinachotakiwa ni kujenga utamaduni wa kukubali matokeo ya uchaguzi ya kushinda na kushindwa.

Alisema hayo katika kipindi cha “Harakati za Kisiasa” kinachorushwa hewani kila siku ya Jumanne na kituo cha redio cha Zenji FM, ambacho kinamilikiwa na Waziri Seif.

Tamko hilo la Shamhuna lilirudiwa kwa siku tatu mfululizo; Jumapili, Jumatatu na jana asubuhi, kuonyesha kuwa hakuna haja ya ajenda hiyo ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwenye mazungumzo ya muafaka baina ya vyama hivyo viwili vikuu visiwani Zanzibar.
Â
“Zanzibar haihitaji Serikali ya Mseto wala Serikali ya Umoja wa Kitaifa wala serikali ya nini hapana, la msingi ni tujenge utamaduni wa kukubali kushindwa na kushinda... tukijenga utamaduni huo tutafanya kazi kwa pamoja na rais atakayeingia madarakani atachagua watu wenye uwezo wa kufanya kazi,” alisema Shamhuna.
Â
Shamhuna alisema watu wengi wanafikiri kwamba suluhisho la mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar ni kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na serikali hiyo ndio itakayoweza kuondoa matatizo yaliyopo, lakini hilo sio sahihi kwa kuwa hata ikiundwa serikali ya umoja matatizo bado yataendelea kuwepo.

“Masuala yaliyopo yanatokana na baadhi yetu kuweka mbele umimi na si utaifa kwa hivyo kuundwa au kutokuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa hakutusaidia,” alisema.

“Kadiri umimi utakavyokuwepo miongoni mwetu wana siasa, tatizo bado litaendelea. Solution (suluhisho) ni kuondoa umimi. Hakuhitajiki hotuba wala hakuhitajiki mikutano, kunataka management,” alisema Shamhuna kwa kujiamini.

Shamhuna alikwenda mbali zaidi na kusema watu wanasahau kwamba Zanzibar ni nchi ya kimapinduzi na wanadhani kwamba ni nchi ya watu kupiga kura na kutangazwa tu huku wengine wakifikiri kuwa Zanzibar ni nchi yenye watu walegevu legevu.
Â
Lakini hakufafanua anamaanisha nini, ingawa suala la mapinduzi limekuwa likizua mgogoro baina ya wafuasi wa vyama hivyo viwili, baadhi wakipinga mapinduzi hayo na wengine wakiunga mkono.

Akizungumzia urais, Shamhuna alisema Zanzibar haihitaji rais kijana wala mzee, lakini inahitaji rais meneja ambaye ataweza kuwakusanya watu wote pamoja na kukabiliana na changamoto zilizopo sasa katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Â
“Karume anamaliza muda wake; nikiulizwa tunataka rais wa aina gani nitajibu tunataka rais meneja (kiongozi) sijui nimefahamika,” alisema waziri huyo machachari.
“Kwa hapa tulipofikia, tunataka tuwe na kiongozi meneja na sio lazima awe kijana kama wengi mnavyodhani. Zanzibar hatutaki rais kijana wala mzee, tunataka meneja ili aweze kuondoa challenges (changamoto) zote...sasa nani ana quality (ubora) ya umeneja,” alihoji.
Â
Alisema rais wa aina hiyo atachagua watu wenye kuweza kufanya kazi hata bila ya kujali ametoka wapi.
Â
“Sio huyu anatoka wapi na huyu anatoka wapi watu ni inclusive government (serikali inayojumuisha) na sio idadi ya watu kutoka chama cha siasa... tufanye hivyo kwa matakwa yetu na sio kulazimishwa, hapo tutajenga umoja na tutafanya kazi.”
Â
Shamhuna alisema mbio za urais kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2010 tayari zimeshaunda makundi zaidi ya matatu na kwamba tayari wapo watu wameshaanza kupigia debe viongozi wao. Alisema watu hao wameanza kutoa lugha za vitisho kuwa mgombea wa kundi lao asipopitishwa na CCM, hawatakipigia kura chama hicho.
Â
“Tunawasikia wanasema hivyo wengine wanasema sasa ni zamu yetu; wengine wanasema sisi vijana tuchagueni ili tufanye mabadiliko ya nchi; wengine wameamua kunyamaza kimya; tegemeo lao hatulijui. Sasa tuna makundi matatu mpaka manne hivi yanayotafuta urais wa Zanzibar,” alisema Shamhuna. Â
Â
Akizungumzia suala linalopendekezwa na baadhi ya watu kuwa safari hii rais atoke Pemba ili kupunguza joto la kisiasa, Shamhuna aliwaita watu wenye mapendekezo hayo kuwa wamefilisika kisiasa.
Â
“Zanzibar hatuchagui rais kwa zamu na suala la kusema sasa zamu yetu Wapemba; zamu yetu  Waunguja limekwisha. Hiyo ni hoja batili na anayezungumza lugha hiyo sijui nimuite kwa lugha gani,” alisema Shamhuna.
Â
“Rais Amani anaondoka na Rais Kikwete anaendelea kipindi cha pili na hapa mitazamo tofauti kwa kuwa anayeondoka anataka arithiwe na ni nani huyo wa kurithi?

“Muungano unataka apatikane mtu kutoka Zanzibar ambaye ataweza kufanya naye kazi hivyo ndio mitizamo miwili ya msingi hii, mitizamo ya kuwa anatoka Pemba au Unguja ni mitizamo ya umimi na huko ni kufilisika kisiasa kwa jinsi navyoangalia suala hilo haraka haraka.”
 Â
Naye Waziri Seif, ambaye anatajwa kama mmoja wa watu wanaoweza kujitokeza kuwania urais wa Zanzibar, aliwaambia wananchi wa kisiwani Pemba wiki hii kwamba umoja wa Wazanzibari hauhitaji kushirikishwa chama kingine chochote kwa kuwa CCM pekee inaweza kuweka umoja na mshikamano kwa kuwa hiyo ndio sera ya chama hicho.

Aliwaambia wananchi wa kisiwa hicho kwamba MwanaCCM wa Pemba anakuwa ni CCM wa kweli kweli kwa kuwa wanakabiliana na mambo mbalimbali yanayofanywa na wapinzani, lakini wameweza kumudu na kuvumilia bila ya kutoka katika chama hicho.

“Nikwambieni ndugu zangu kuwa katika suala la umoja hakuna haja ya kushirikiana na chama kingine kwani CCM wenyewe tunaweza sana kuwaunganisha Wazanzibari wote. Na huku Pemba, CCM anakuwa wa kweli kweli maana vitimbi na vituko anavyofanyiwa na wafuasi wa CUF ni vingi, lakini bado anaweza kubakia kuwa CCM, hilo si jambo dogo,” alisema Khatib katika kipindi kilichorushwa na Zenj FM wakati wa ziara yake kisiwani Pemba.

Hii ni mara ya pili kwa Waziri Shamhuna kupingana na viongozi wakuu wa nchi katika kipindi cha miaka mitatu. Oktoba 5, 2006 Shamhuna alipingana na Rais Kikwete kuhusu suala la mwafaka wa Zanzibar.

Wakati Rais Jakaya Kikwete akisema utatuzi wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar umefikia mahali pazuri, Shamhuna, aliibuka na kusema kamwe serikali ya umoja wa kitaifa au ya mseto haitaundwa visiwani.

Shamhuna alitoa msimamo alipokuwa akiwahutubia viongozi wa ngazi mbalimbali na wazee wa CCM wa Kikombweni Wilaya ya Kaskazini A, Unguja na hotuba hiyo kutangazwa na vyombo vya habari vya SMZ.
 "Hakuna Serikali ya Mseto itakayoundwa nchini kama inavyodaiwa na viongozi wa chama cha upinzani," alisema Shamhuna.
Facebook

Lunyungu
JF Senior Expert Member
Points: 1,638,424, Level: 100 Points: 1,638,424, Level: 100 Points: 1,638,424, Level: 100
Activity: 2% Activity: 2% Activity: 2%
Join Date: Tue Dec 2006
Location: Malampaka
Posts: 4,705
Thanks: 1
Thanked 203 Times in 111 Posts
Views: 585
Reply With Quote
  #2  
Old 24th November 2009, 10:25 PM
Masatu Masatu is offline
Masatu Is Magumashi
JF Senior Expert Member
Points: 733,039, Level: 100 Points: 733,039, Level: 100 Points: 733,039, Level: 100
Activity: 4% Activity: 4% Activity: 4%
 
Join Date: Mon Jan 2007
Location: Mbagala, Jeshini
Posts: 3,741
Thanks: 0
Thanked 88 Times in 66 Posts
Rep Power: 0
Masatu is infamous around these parts
Default Re: Wadau mmesikia haya ya Zanzibar ? CUF imepigwa chenga ama ?

Wewe yanakuhusu nini? yako ya Chadema yanawashinda.....
__________________
Mkulima kala Mbegu......
Reply With Quote
The Following User Says Thank You to Masatu For This Useful Post:
Ngida1 (25th November 2009)
  #3  
Old 24th November 2009, 10:57 PM
Buchanan's Avatar
Buchanan Buchanan is online now
Buchanan has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 327,673, Level: 100 Points: 327,673, Level: 100 Points: 327,673, Level: 100
Activity: 64% Activity: 64% Activity: 64%
 
Join Date: Tue May 2009
Posts: 3,103
Thanks: 529
Thanked 1,133 Times in 684 Posts
Rep Power: 27
Buchanan will become famous soon enoughBuchanan will become famous soon enoughBuchanan will become famous soon enoughBuchanan will become famous soon enoughBuchanan will become famous soon enoughBuchanan will become famous soon enoughBuchanan will become famous soon enoughBuchanan will become famous soon enough
Default Re: Wadau mmesikia haya ya Zanzibar ? CUF imepigwa chenga ama ?

Uzuri wa Shamhuna huwa ni mkweli na haumi maneno! Karume anapodai kuwa suala la serikali ya mseto anawaachia Wazanzibari wenyewe ni kuuma maneno bila kuelezea ukweli wa mambo! Seif na Libumba mmeliwa mchana kweupeee!
__________________
"Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu...Mdhalimu kwa kiburi chake asema Hatapatiliza. Jumla ya mawazo yake, ni Hakuna Mungu!" (Zab. 14:1, 10:4).
Reply With Quote
The Following User Says Thank You to Buchanan For This Useful Post:
Ngida1 (25th November 2009)
  #4  
Old 24th November 2009, 11:03 PM
Tumain's Avatar
Tumain Tumain is offline
Tumain has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 232,557, Level: 100 Points: 232,557, Level: 100 Points: 232,557, Level: 100
Activity: 83% Activity: 83% Activity: 83%
 
Join Date: Sun Jun 2009
Posts: 2,792
Thanks: 897
Thanked 837 Times in 553 Posts
Rep Power: 26
Tumain will become famous soon enoughTumain will become famous soon enoughTumain will become famous soon enoughTumain will become famous soon enoughTumain will become famous soon enoughTumain will become famous soon enoughTumain will become famous soon enoughTumain will become famous soon enough
Default Re: Wadau mmesikia haya ya Zanzibar ? CUF imepigwa chenga ama ?

Quote:
View Post
Wewe yanakuhusu nini? yako ya Chadema yanawashinda.....
Kaka CUF ni chama cha kisiasa..kwa Tanzania nzima kinategemewa kuchukua nchi na kuongoza wananchi wote ..wanachama na wasio wanachama..hivyo kina mhusu kila mtu Mtanzania..so usituambia haimhusu

Mimi nilijua hili deal ni maumivu kwa CUF na ikifika 2010 kazi yenu ndio imekwisha..mgawanyiko kati ya wanachama na viongozi ..take my words.
__________________
"60 Years of Palestine Invasion Must End Now You Can Make a Difference Boycot Israel Product Now"
Reply With Quote
  #5  
Old 24th November 2009, 11:17 PM
Lunyungu Lunyungu is offline
Lunyungu Kisu Kikali Mno
JF Senior Expert Member
Points: 1,638,424, Level: 100 Points: 1,638,424, Level: 100 Points: 1,638,424, Level: 100
Activity: 2% Activity: 2% Activity: 2%
 
Join Date: Tue Dec 2006
Location: Malampaka
Posts: 4,705
Thanks: 1
Thanked 203 Times in 111 Posts
Rep Power: 33
Lunyungu will become famous soon enoughLunyungu will become famous soon enoughLunyungu will become famous soon enoughLunyungu will become famous soon enoughLunyungu will become famous soon enoughLunyungu will become famous soon enoughLunyungu will become famous soon enoughLunyungu will become famous soon enough
Default Re: Wadau mmesikia haya ya Zanzibar ? CUF imepigwa chenga ama ?

Seif atawekwa na labda kufukuzwa chama maana amepata amani na kula kwa mgongo wa marehemu walio mwaga damu. Waha tuone na majibu ya CUF yatakuwaje. Hivi Zanzibar kuna viongozi wakuu wangapi ?
Reply With Quote
The Following User Says Thank You to Lunyungu For This Useful Post:
Ngida1 (25th November 2009)
  #6  
Old 24th November 2009, 11:44 PM
Sonara Sonara is online now
Sonara has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 182,714, Level: 100 Points: 182,714, Level: 100 Points: 182,714, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Thu Oct 2008
Posts: 379
Thanks: 4
Thanked 24 Times in 12 Posts
Rep Power: 22
Sonara will become famous soon enoughSonara will become famous soon enoughSonara will become famous soon enoughSonara will become famous soon enoughSonara will become famous soon enoughSonara will become famous soon enoughSonara will become famous soon enoughSonara will become famous soon enough
Default Re: Wadau mmesikia haya ya Zanzibar ? CUF imepigwa chenga ama ?

Quote:
View Post
Seif atawekwa na labda kufukuzwa chama maana amepata amani na kula kwa mgongo wa marehemu walio mwaga damu. Waha tuone na majibu ya CUF yatakuwaje. Hivi Zanzibar kuna viongozi wakuu wangapi ?

Wapo wachache lakini nguvu zao ni kubwa kiasi kulitikisa Bunge la Tanzania na Rais wake, mfano mmoja ni ule wa BUTIAMA walipofoka kidogo tu Bunge zima lilitulia kama vile wapo kwa kinyozi.
Reply With Quote
  #7  
Old 25th November 2009, 01:07 AM
De Novo's Avatar
De Novo De Novo is offline
De Novo loves NWA!
JF Premium Member
Points: 234,135, Level: 100 Points: 234,135, Level: 100 Points: 234,135, Level: 100
Activity: 56% Activity: 56% Activity: 56%
 
Join Date: Sat Apr 2008
Location: Dar - Tz
Posts: 3,675
Thanks: 984
Thanked 978 Times in 606 Posts
Rep Power: 29
De Novo will become famous soon enoughDe Novo will become famous soon enoughDe Novo will become famous soon enoughDe Novo will become famous soon enoughDe Novo will become famous soon enoughDe Novo will become famous soon enoughDe Novo will become famous soon enoughDe Novo will become famous soon enough
Default Re: Wadau mmesikia haya ya Zanzibar ? CUF imepigwa chenga ama ?

sidhani kama mkutano wa seif na karume ulikuwa na lengo la kuunda serikali ya mseto, ule mkutano ulikuwa na mamlaka makugwa zaidi, and that was interest of zanzibaris

Tuache kauchochezi
__________________
I am on the move...
Reply With Quote
The Following User Says Thank You to De Novo For This Useful Post:
Liz Senior (25th November 2009)
  #8  
Old 25th November 2009, 06:29 AM
Ngida1's Avatar
Ngida1 Ngida1 is offline
Ngida1 has no status.
JF Premium Member
Points: 76,127, Level: 100 Points: 76,127, Level: 100 Points: 76,127, Level: 100
Activity: 4% Activity: 4% Activity: 4%
 
Join Date: Tue Aug 2009
Posts: 162
Thanks: 122
Thanked 39 Times in 35 Posts
Rep Power: 21
Ngida1 will become famous soon enoughNgida1 will become famous soon enoughNgida1 will become famous soon enoughNgida1 will become famous soon enoughNgida1 will become famous soon enoughNgida1 will become famous soon enoughNgida1 will become famous soon enoughNgida1 will become famous soon enough
Default Re: Wadau mmesikia haya ya Zanzibar ? CUF imepigwa chenga ama ?

Quote:
View Post
Wewe yanakuhusu nini? yako ya Chadema yanawashinda.....
Nd. Masatu,
Tafadhali zihurumie mbavu zetu!!!
Hayo aliyoyasema Shamhuna ndio msimamo wa SMZ na yale ya Karume ilikuwa babaisha ***** tu! Kwa kweli inatia uchungu, Maalim Seif baada ya miaka zaidi ya 10 ndio sasa anajua maslahi ya Wa-zanzibari? Sasa zogo lote lile lilikuwa la nini? Kwa mimi Seif ndio awe wa mwanzo kupandishwa mahakamani kwa kuwarejesha nyuma Wa-zanzibari kwa ugomvi ambao kumbe sio wa kweli.
Reply With Quote
  #9  
Old 25th November 2009, 08:19 AM
Liz Senior's Avatar
Liz Senior Liz Senior is offline
Liz Senior has no status.
JF Premium Member
Points: 85,292, Level: 100 Points: 85,292, Level: 100 Points: 85,292, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Thu Apr 2007
Posts: 162
Thanks: 18
Thanked 37 Times in 24 Posts
Rep Power: 23
Liz Senior will become famous soon enoughLiz Senior will become famous soon enoughLiz Senior will become famous soon enoughLiz Senior will become famous soon enoughLiz Senior will become famous soon enoughLiz Senior will become famous soon enoughLiz Senior will become famous soon enoughLiz Senior will become famous soon enough
Default Re: Wadau mmesikia haya ya Zanzibar ? CUF imepigwa chenga ama ?

Quote:
View Post
sidhani kama mkutano wa seif na karume ulikuwa na lengo la kuunda serikali ya mseto, ule mkutano ulikuwa na mamlaka makugwa zaidi, and that was interest of zanzibaris

Tuache kauchochezi
Utashangaa wengi wanye maoni hasi kuhusu Znz ni watu wa bara! Wengi wao wanayajua yanayotokea Znz kwa kusoma magazetini...(waandishi wetu mnawajua vizuri)...hawana taarifa sahihi kuhusu hali za wazanzibari na ugumu wa maisha yao. Shamhuna! Kati ya wote! Hivi yeye na dada yetu "Asha Ngedere" wana tofauti?
Reply With Quote
  #10  
Old 25th November 2009, 08:28 AM
FirstLady1's Avatar
FirstLady1 FirstLady1 is online now
FirstLady1 has no status.
JF Premium Member
Points: 303,030, Level: 100 Points: 303,030, Level: 100 Points: 303,030, Level: 100
Activity: 100% Activity: 100% Activity: 100%
 
Join Date: Wed Jul 2009
Posts: 3,443
Thanks: 561
Thanked 746 Times in 534 Posts
Rep Power: 27
FirstLady1 will become famous soon enoughFirstLady1 will become famous soon enoughFirstLady1 will become famous soon enoughFirstLady1 will become famous soon enoughFirstLady1 will become famous soon enoughFirstLady1 will become famous soon enoughFirstLady1 will become famous soon enoughFirstLady1 will become famous soon enough
Default Re: Wadau mmesikia haya ya Zanzibar ? CUF imepigwa chenga ama ?

habari za siasa jamani zinaumiza kichwa huwezi fanya jambo likaonekana zuri
na huwezi kumfurahisha kila mtu
__________________
2010 niko kikazi zaidi
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
ama, chenga, cuf, haya, imepigwa, mmesikia, wadau, zanzibar


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Muungano na kero zake: Tuuvunje? Sam Jukwaa la Siasa 3853 28th January 2010 12:42 PM
Tukumbuke Zamani: Historia Ya Taifa Letu Katika Picha Field Marshall ES Jamii Photos 1261 6th January 2010 04:40 PM
Hotuba ya Seif Shariff! JokaKuu Jukwaa la Siasa 131 11th December 2009 05:12 PM
Muafaka CCM na CUF, pande mbili za shilingi! MwanaCCM Jukwaa la Siasa 148 13th July 2009 10:13 AM
Islam and the catholic crusade movement in zanzibar Shy Habari na Hoja mchanganyiko 6 19th September 2008 06:28 PM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 02:09 PM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com