Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mishahara au Masihara

    Report Post
    Results 1 to 2 of 2
    1. #1
      Mtanganyika's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th July 2007
      Location : US
      Posts : 1,357
      Rep Power : 1281
      Likes Received
      106
      Likes Given
      20

      Default Mishahara au Masihara

      Wakati Bunge la Jamuhuri muungano likiendelea kupiga mbiu kuhusu bajeti, wafanyakazi wa serikali wameendamana kupinga kima cha chini cha shiling 84,000

      Kwa mtu mwenye maono madogo ambaye afahamu Tanzania anaweza sema 84,000 ina tosha, lakini kwa mtu mwenye upeo wa kufikiri hujiuliza kwanza, ni kiasi gani thamani ya pango nchini Tanzania, jee mlipuko wa bei (inflation) ukoje, jee kiasi hiki ni kwa watu gani, wanafunzi au wana familia? na maswali mengine mengi.

      Kinacho sikitisha ni kuona wabunge wanazidishiwa mishahara kwa kazi isiyo ya maana wanayo fanya. Nini bunge la Tanzania linafanya? kuuza Madini kwa bei nafuu, kumruhusu Mkapa kununua ndege au Lowasa kusaini mkataba na Kampuni hewa ya Richmond? Hakuna mtu anayeweza kulitetea bunge hilo lililo na tabia ya mwenda wazimu, kuropoka pasipo sababu.

      Kuwalipa watu wenye familia shilling 84000 ni kuwatukana matusi, 84,000 ni theluthi ya matumizi Lowasa na mawaziri wake.
      Swala linalo sikitisha ni kwamba mueshimiwa Kikwete, amabaye mara zote hupiga mbiu kwamba anatetea walala hoi safari hii ameamua kuwalalia walala hoi. Kinacho nishangaza ni kwamba hawa mna walipa 84000 wakati nyinyi mkijiongezea millioni za fedha ndio walio wachagua kuwaweka madarakani.

      Nini hadhari za kiwangoi kidogo hiki, moja corruption will hike in high percentage every single day, sidhani kama kuna kiongozi atakeye thubutu kufungua mdomo wake na kusema chochote kuhusu rushwa wakati mfanyakazi analipwa 84000.
      Madhara ya pili, less utilizing of labor skills, huwezi kumplipa mtu shilling 84000 kisha ukategemea awe productive 100%, huo utakuwa ni wendawazimu na kama sio uchizi, the effect of this is reduction of human production which cause effects on public.

      Muda umefika wa bunge mbiu kuwa bunge vitendo, nakuacha mabishano kama watoto wa kike wa miaka 10 wanapobishana kwamba nani ni mchumba wa nani.

    2. Miaka 50

    3. #2
      Joo Wane's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th March 2007
      Posts : 116
      Rep Power : 646
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default

      Wakati mwingine unashindwa kuelewa hivi tuna serikali makini kweli? Hivi kwa shilingi 84,000 mtu utaishije toka tarehe 1 mpaka 31 ya kila mwezi. Maana hata ukipangia bajeti hiyo 84,000 kwa namna yoyote ile haiwezekani. Na wabunge huko dodoma wanatetea maslahi yao tu eti posho ya siku tshs 120,000 na mshahara kwa mwezi 1,500,000 kwa kazi gani wanayofanya? Haki ipo wapi?. Namuomba Mungu atushushie uwezo wa kutambua na kufahamu kuwa sisi ndio tuliowaweka hao viongozi madarakani na uwezo wa kuwaondoa tunao sisi wenyewe, na atupe nguvu ya kuwaondoa haraka sana kwa "amani"

    4. Study Abroad

    Similar Topics

    1. Niliwamisi, acheni masihara...........!
      By Asprin in forum JF Chit-Chat
      Replies: 131
      Last Post: 2nd September 2011, 15:13
    2. Tanzania ni nchi ya masihara
      By Ngambo Ngali in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 3
      Last Post: 7th July 2011, 11:10
    3. Ni ongezeko la mishahara au masihara?
      By masasi in forum Tanzania 2010-2015
      Replies: 4
      Last Post: 5th August 2010, 17:53
    4. Masihara Yaivuruga Harusi
      By MziziMkavu in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 2
      Last Post: 15th April 2010, 11:14
    5. Kikwete Acheni Masihara......
      By Indume Yene in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 12
      Last Post: 20th March 2008, 18:24

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...