JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

  Report Post
  Page 2 of 2 FirstFirst 12
  Results 21 to 36 of 36
  1. R.B's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th May 2012
   Posts : 4,426
   Rep Power : 0
   Likes Received
   1244
   Likes Given
   746

   Default MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood, ameng'ara mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, baada ya kufanikisha mradi wa uchimbaji wa visima vya maji 23 kwa ajili ya maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

   Kinana alizindua mradi huo wa maji ya visima mjini hapa juzi, wakati akiangalia utekelezaji wa Ilani ya CCM na kupokea kero za wananchi ambapo alitumia nafasi hiyo kuzindua visima hivyo ambavyo vimegharimu zaidi ya Sh milioni 363.

   Akizungumzia zaidi miradi ya visima hivyo, Kinana, alisema mbunge huyo ameonyesha dhamira ya kweli ya kazi ya uongozi ambayo ameamua kuifanya kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wake.

   Alisema umuhimu wa viongozi kuwatumikia wananchi ambao wameamua kuwachagua kwa ajili ya kuwatumikia na uchimbaji wa visima hivyo ni wazi kuwa kazi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM inafanyika vizuri na hilo ni jambo jema.

   Alisema lengo la CCM ni kuona tatizo la maji linapata ufumbuzi na kilichofanywa na Abood ni moja ya mambo muhimu wakati Serikali nayo ikiendelea kuwatumikia wananchi wake, hasa kwa kuzingatia kuwa CCM ndiyo iliyoshika dola na Ilani yake ndiyo inatekelezwa.

   “Abood ameonyesha wazi kuwa anajali wananchi wake, anatambua wajibu wake na hii ndiyo sifa ya uongozi. Naamini kwa kazi hii atakuwa mbunge wenu kwa kipindi kirefu ndani ya jimbo hilo. Kila ninakopita naona anashangiliwa na wananchi wake na wanampenda,” alisema Kinana.

  2. RedArmy's Avatar
   Member Array
   Join Date : 8th January 2013
   Posts : 44
   Rep Power : 459
   Likes Received
   8
   Likes Given
   1

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   inavyoelekea wewe sio mkazi wa jimbo la morogoro mjini.kama kweli jitokeze kwenye mojawapo ya mikutano yake ya hadhara mbele ya wananchi wa jimbo hili halafu useme hayo uliyoandika na utapata majibu ambayo sidhani kama utayasahau maishani kutoka kwa wananchi wa jimbo hili.sie wananchi wa morogoro mjini hatutaki wabunge wa kuganga njaa.uelewe ya kuwa sio kila jambo lipelekwe bungeni kama ambavyo unavyofikiria.kazi ya mbunge ni kutatua na kuyashughulikia matatizo ya wananchi ama kwa kuyatatua mwenyewe kama mbunge au kuiomba serikali kusaidia kutatua.nadhani wewe bado umelala wakati wananchi wa morogoro wameshaamka,huu mwaka wa 3 sasa.ww ndio kwanza bado upo kitandani umefumbua macho.inaelekea ndugu yangu njaa inakusumbua.pole sana.

  3. Kilaza's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th February 2013
   Posts : 3,329
   Rep Power : 3507
   Likes Received
   1338
   Likes Given
   0

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   Afande sele mbunge moro town 2015

  4. Gronkjaer's Avatar
   Member Array
   Join Date : 20th April 2013
   Posts : 86
   Rep Power : 453
   Likes Received
   11
   Likes Given
   68

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   Morogoro tunakero nyingi sana mfano nanenane tunapata maji msimu wa masika ikifika kiangazi hakuna maji ...hivyo visima kwetu si hoja ..

  5. RedArmy's Avatar
   Member Array
   Join Date : 8th January 2013
   Posts : 44
   Rep Power : 459
   Likes Received
   8
   Likes Given
   1

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   duuuuuuuuuuuuuuuuuuuu.sasa hututakii mema wana moro.anashindwa kulea familia yake ataweza kutumikia wananchi.nadhani mihadarati,bangi,madawa ya kulevya,kuvua nguo hadharani yatahalalishwa siku hiyo.ewe bwana kwa uwezo wako,tuepushe na maoni haya ya shangwa francis.

  6. Bigirita's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th February 2007
   Location : 3.0758° S, 37.3533° E
   Posts : 13,156
   Rep Power : 171804295
   Likes Received
   4129
   Likes Given
   5895

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   Quote By Mr. Zero View Post
   Upuuzi wa mwaka ........ yaani baada ya miaka 50 ya uhuru bado tunategemea maji ya vision mijini. Sasa huko vijijini itabidi wasubiri miaka mingine 50 kama CCM itaendelea kuongoza.
   Ni mambo ya kusikitisha kuona of all places, morogoro mjini panachimbwa visima. Sehemu yenye vyanzo vikuu vya maji ya mito mikubwa kabisa inayomwaga maji baharini.

   Ni akili ndogo ya kuwahadaa wanananchi masikini wasiojua wamepewa pipi.

   Haina tofauti na kujifanya kutoa msaada wa basi na lory kuwazika watu. Kwanini usitoe msaada wa dawa na vitanda kwenye health facilities?.
   * LOVE COMES NATURALLY; HATE IS TAUGHT.....by nngu007 wa JF

  7. macho_mdiliko's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2008
   Posts : 4,443
   Rep Power : 1563
   Likes Received
   1756
   Likes Given
   1656

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   Quote By watundawangu View Post
   Tena visima vichache hivi, alitakiwa kujenga mara kumi ya hivi Huyu alishatuibia sana kwa nauli ya mabasi yake!! Asitufanye wajinga!
   Mkuu na wewe unaingie kwenye mtego wa kushangilia visima? Hii nchi ina uwezo wa kuwapatia watu wote maji ya bomba tena masafi. Ni wizi na uvivu wao tu ndio unawaumbua! Na yeye mwenyewe anatumia maji ya visima au anawachimbia ''ngombe'' wanywe na yeye astarehe na mkewe kwa fedha wanayokwapua?

  8. Bigirita's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th February 2007
   Location : 3.0758° S, 37.3533° E
   Posts : 13,156
   Rep Power : 171804295
   Likes Received
   4129
   Likes Given
   5895

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   Quote By commited View Post
   mention maeneo vilipo chimbwa, isije kuwa kama huyu
   Attachment 91185
   soma kwa makini hiyo vocha
   Au kama hiiii......
   Click image for larger version. 

Name:	uploadfromtaptalk1366913196269.jpg 
Views:	24 
Size:	28.8 KB 
ID:	91504
   * LOVE COMES NATURALLY; HATE IS TAUGHT.....by nngu007 wa JF

  9. Gronkjaer's Avatar
   Member Array
   Join Date : 20th April 2013
   Posts : 86
   Rep Power : 453
   Likes Received
   11
   Likes Given
   68

   Default

   Quote By Bigirita View Post
   Ni mambo ya kusikitisha kuona of all places, morogoro mjini panachimbwa visima. Sehemu yenye vyanzo vikuu vya maji ya mito mikubwa kabisa inayomwaga maji baharini.

   Ni akili ndogo ya kuwahadaa wanananchi masikini wasiojua wamepewa pipi.

   Haina tofauti na kujifanya kutoa msaada wa basi na lory kuwazika watu. Kwanini usitoe msaada wa dawa na vitanda kwenye health facilities?.
   naungana na wewe kwa asilimia zote........

  10. Mr. Zero's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th June 2007
   Posts : 6,620
   Rep Power : 85901699
   Likes Received
   1355
   Likes Given
   218

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   Quote By Bigirita View Post
   Ni mambo ya kusikitisha kuona of all places, morogoro mjini panachimbwa visima. Sehemu yenye vyanzo vikuu vya maji ya mito mikubwa kabisa inayomwaga maji baharini.

   Ni akili ndogo ya kuwahadaa wanananchi masikini wasiojua wamepewa pipi.

   Haina tofauti na kujifanya kutoa msaada wa basi na lory kuwazika watu. Kwanini usitoe msaada wa dawa na vitanda kwenye health facilities?.
   We wacha tu!!

   Yaani Watanzania kama hatukulogwa basi tumelaaniwa................... . siyo bure!!!
   "Mimi na Rais Kikwete hatukukutana barabarani" by Lowasa

  11. macho_mdiliko's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2008
   Posts : 4,443
   Rep Power : 1563
   Likes Received
   1756
   Likes Given
   1656

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   Quote By RedArmy View Post
   inavyoelekea wewe sio mkazi wa jimbo la morogoro mjini.kama kweli jitokeze kwenye mojawapo ya mikutano yake ya hadhara mbele ya wananchi wa jimbo hili halafu useme hayo uliyoandika na utapata majibu ambayo sidhani kama utayasahau maishani kutoka kwa wananchi wa jimbo hili.sie wananchi wa morogoro mjini hatutaki wabunge wa kuganga njaa.uelewe ya kuwa sio kila jambo lipelekwe bungeni kama ambavyo unavyofikiria.kazi ya mbunge ni kutatua na kuyashughulikia matatizo ya wananchi ama kwa kuyatatua mwenyewe kama mbunge au kuiomba serikali kusaidia kutatua.nadhani wewe bado umelala wakati wananchi wa morogoro wameshaamka,huu mwaka wa 3 sasa.ww ndio kwanza bado upo kitandani umefumbua macho.inaelekea ndugu yangu njaa inakusumbua.pole sana.
   Hizi ni ''kazi'' za mbunge kwa mujibu wa watu wenye ufinyu wa mawazo! Ukishaoona mbunge anatoa fedha mfukoni eti za kuchimba visima basi ujue ni kielelezo cha tatizo kubwa sana la uongozi kuanzia kwa mbunge mwenyewe mpaka kwa rais

  12. Emanuel2020's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 26th April 2013
   Posts : 3
   Rep Power : 0
   Likes Received
   0
   Likes Given
   3

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   Yaani hapa kweli hamna kitu wala hakuna watu waelewa!!!
   1. Inaelekea Bigirita na Gronkjaer nyie wote ni wageni Morogoro.
   2. Hamuelewi mnachosema!
   3. Mbunge gani wa Chadema amewahi kufanya hivi?
   4. Kwa ushahidi wa FastaFasta nunueni au kodisheni au azimeni gazeti la Mwananchi la jana Tarehe 25/04/2013 na musome kurasa za ndani ili mufahamu na muelewe na mujue kama ni nini amefanya na anafanya Mh. Abood kwenye kitengo cha AFYA.
   5. Nendeni hospitali za Mafiga, Chamwino, Kingolwira na MUkaulize nani ameleta vifaa hapo?
   6. Na sasa Hospitali ya Wilaya inajengwa Mkundi, Gharama yake ni MILLIONI 650. bado mtasema...... kweli hamna shukrani
   7. Jamani huyu mbunge wetu siyo wa kuganga njaa!! wala hatunishi misuli bungeni!!!

  13. ndangija's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 15th March 2013
   Posts : 159
   Rep Power : 472
   Likes Received
   42
   Likes Given
   14

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   Quote By macho_mdiliko View Post
   Hizi ni ''kazi'' za mbunge kwa mujibu wa watu wenye ufinyu wa mawazo! Ukishaoona mbunge anatoa fedha mfukoni eti za kuchimba visima basi ujue ni kielelezo cha tatizo kubwa sana la uongozi kuanzia kwa mbunge mwenyewe mpaka kwa rais
   Safi sana macho umeonyesha una ukomavu na weledi mkubwa sana .kiukweli ni kwa sababu ya umasikini wetu tunadhani kazi ya mbunge ni kuchimba visima au kugawa dawa mahospitalini.Sera zikitekelezwa vyema hilo ni jukumu la serikali.

   Hapa bongo tumedanganywa na tumenogewa kuwa jukumu la mbunge ni kufanya hayo.

   Hakuna mbunge atakayeweza kuendesha jimbo kwa fedha zake za mfukoni. na ndio maana tunasema ktk viwango vya mbunge bora abood hayumo.

   Chukulia asilimia 75 ya wakazi wa morogoro ni masikini,tunahitaji mbunge atakayetetea masikini hawa ili sera mbovu zinazowakosesha maendeleo ziondoke ili wapate maendeleo.

   Muda umefika na wanainchi wameshaelevuka, zama za kuchukua shilingi kumi za watu halafu ukarudishi shilingi moja na kuwadanganya umewasaidia zimepitwa na wakati....

  14. Averos's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th August 2010
   Location : Home
   Posts : 542
   Rep Power : 685
   Likes Received
   95
   Likes Given
   106

   Default

   Quote By nkongu ndasu View Post
   kina abood wanatumia vipesa vyao kuwakandamiza wana morogoro, hayo ndo mafisadi papa, waarabu ni janga kwa taifa letu!
   Umekurukupa dogo! hujui usemacho,

  15. Emanuel2020's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 26th April 2013
   Posts : 3
   Rep Power : 0
   Likes Received
   0
   Likes Given
   3

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   Friday, April 26, 2013

   TASWIRA YA UZINDUZI WA MASHINE YA UTRA-SOUND HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO .

   SETI YA MASHINE YA ULTRASOUND YENYE THAMANI YA SH 25 MILIONI
   Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa idara ya X-RAY Daktari Alban Ndekeye kulia na Daktari Paul Henry wa kitengo cha idara ya X-RAY wakati wa uzindua wa mashine ya ultrasound mpya yenye thamani ya sh25 milioni kwa ajili ya hospita ya rufaa ya mkoa Morogoro.

  16. mwaxxxx's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st July 2012
   Location : morogoro
   Posts : 838
   Rep Power : 645
   Likes Received
   221
   Likes Given
   1

   Default

   Quote By Emanuel2020 View Post
   Yaani hapa kweli hamna kitu wala hakuna watu waelewa!!!
   1. Inaelekea Bigirita na Gronkjaer nyie wote ni wageni Morogoro.
   2. Hamuelewi mnachosema!
   3. Mbunge gani wa Chadema amewahi kufanya hivi?
   4. Kwa ushahidi wa FastaFasta nunueni au kodisheni au azimeni gazeti la Mwananchi la jana Tarehe 25/04/2013 na musome kurasa za ndani ili mufahamu na muelewe na mujue kama ni nini amefanya na anafanya Mh. Abood kwenye kitengo cha AFYA.
   5. Nendeni hospitali za Mafiga, Chamwino, Kingolwira na MUkaulize nani ameleta vifaa hapo?
   6. Na sasa Hospitali ya Wilaya inajengwa Mkundi, Gharama yake ni MILLIONI 650. bado mtasema...... kweli hamna shukrani
   7. Jamani huyu mbunge wetu siyo wa kuganga njaa!! wala hatunishi misuli bungeni!!!
   Acha kupotosha umma,,,, sio huyu abood aliyeunga mkono nguzo za umeme zing'olewe kihonda-kayenzi zipelekwe tungi kwa sababu za kisiasa???
   ..sio huyu abood aliyeanzisha e-mail ya ofisi kwa ajili ya kero za wananchi but hajibu hizo kero?
   ..sio huyu abood anayeogopa kuulizwa maswali jukwaani?

  17. Emanuel2020's Avatar
   Junior Member Array
   Join Date : 26th April 2013
   Posts : 3
   Rep Power : 0
   Likes Received
   0
   Likes Given
   3

   Default Re: MBUNGE wa Morogoro Mjini (CCM), Abdulaziz Abood achimba visima 23 vya maji

   Mwaxxxx, katika watu mbumbumbu wewe ndiyo wakwanza.
   Usiwadanganye watu kwa sababu ya posho unayopata from Chadema.
   ... Kihonda nguzo za umeme zinasambazwa.
   ... Tungi, Tubuyu, Mjimwema nguzo za umeme zinasambazwa kama kweli wewe unaijua Morogoro utaenda kuangalia.
   ...Mh. Abood hatumii e-mail kusikiliza shida za watu!! Mh. Abood anawafuata watu kusikiliza shida zao na ana ofisi ambayo inapokea na kusikiliza shida na kero za wananchi.
   ... Mh. Abood haogopi kuulizwa maswali na anaulizwa maswali na anayajibu iwe kwenye mikutano au akiwatembelea mitaani au katika makazi yao.
   ...Pole sana rafiki yangu unapoteza muda mwingi kwa kufikiria jimboi la Morogoro mjini wakuwatoa CCM na Abood HAYUPO!!
   ...Abood kazi anazofanya ni za kutekeleza Ilani ya CCM 2010/2015.

  Page 2 of 2 FirstFirst 12

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...