JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Full Text: Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bajeti 2013/2014 iliyosomwa na Freeman Mbowe

  Report Post
  Page 13 of 17 FirstFirst ... 31112131415 ... LastLast
  Results 241 to 260 of 337
  1. Molemo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2010
   Posts : 13,190
   Rep Power : 146133716
   Likes Received
   8483
   Likes Given
   618

   Default Full Text: Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bajeti 2013/2014 iliyosomwa na Freeman Mbowe

   Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mh. Freeman Mbowe, atatoa hotuba yake leo kwa saa 1 bungeni, muda si mrefu kutokea sasa! Atazungumza vitu muhimu sana vyenye maslahi kwa Watanzania na taifa.

   Afisa Habari a Chadema Tumaini Makene yupo bungeni kutuletea kila litakalojiri.Pia tunatajia Makene atatuwekea hotuba kamili muda sio mrefu.

   Pia wabunge wa Chadema wamekwishaonya dhidi ya mbinu yoyote ya kukatisha hotuba ya Mbowe wakati akiunguruma.Tayari kuna hofu kuu upande wa serikali kufuatia hotuba hiyo inayosubiriwa kwa hamu na kila mpenda demokrasia nchini.

   =========================

   HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI OFISI YA WAZIRI MKUU, MHE.FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB); KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014

   1. UTANGULIZI


   Mheshimiwa Spika,
   Kufuatia marekebisho kadhaa ya kanuni hususan zinazolenga kwa sasa Utaratibu wa Kutunga Sheria kuhusiana na mambo ya fedha, nasi kama Kambi Rasmi ya Upinzani tutafanya marekebisho katika utaratibu tutakaotumia katika kutoa maoni yetu kwa Serikali.

   Kwa muda mrefu, kufuatia utaratibu wa mfumo wa bajeti ulivyokuwa huko nyuma, tulitumia muda mwingi kuishauri serikali namna bora ya kuboresha bajeti na utendaji wake wa kazi. Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana, serikali hii imekuwa siyo sikivu vya kutosha hata kama pale ambapo ushauri unaotolewa uko wazi kwa masilahi na mustakabali mwema wa Taifa letu.

   Aidha, pale ambapo Serikali imechukua maoni yetu, mara nyingi imekuwa haina ustaarabu wa kutambua, kukiri na kushukuru mchango wa Kambi ya Upinzani, bali mbele ya macho ya umma imeendelea kutoa kebehi kujaribu kuuaminisha umma kuwa vyama vya upinzani havina ufumbuzi mbadala kwa matatizo yanayolikabili Taifa.

   Mheshimiwa Spika,
   Tatizo kubwa la Serikali inayoongozwa na CCM ni kukosa weledi wa kutekeleza kikamilifu vipaumbele vyake pamoja na kuviainisha kupitia Mpango wake wa miaka 5, bajeti na programu mbalimbali. Hali hii inaweza kutafsiriwa kama uwezo duni wa kusoma alama za nyakati ikiwemo kubuni na kusimamia inachokiamini. Ni dhahiri vilevile unapolazimika kufanya jambo usiloliamini au lisilo kipaumbele chako, bali cha kulazimishwa na mazingira unatekeleza bila kujua undani wake na hatma yake ni kuharibu zaidi.

   Mheshimiwa Spika,
   Kwa kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ni mtambuka, Mwaka huu tutajielekeza kuzungumzia mambo makuu machache ambayo sisi tunaamini ni vipaumbele muhimu ambavyo Waziri Mkuu na wasaidizi wake wanapashwa kuja na majibu ya kueleweka kwa Watanzania. Aidha, mengine yatawasilishwa kupitia hotuba zetu mbalimbali katika Wizara husika.

   2. TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA MSTAKABALI WA TAIFA


   Mheshimiwa Spika,
   Tarehe 18 Novemba, 2011 Bunge lako tukufu lilipitisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011. Kufuatana malalamiko mengi kuhusu utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria hiyo na kufuatia vikao kati ya Mheshimiwa Rais na Kamati Maalum ya CHADEMA pamoja na wadau wengine, Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho wakati wa Mkutano wa Sita wa Bunge hili uliofanyika mwezi Februari mwaka 2012.

   Marekebisho hayo yalikuwa ni awamu ya kwanza ya awamu tatu za marekebisho ya Sheria hiyo kwa mujibu wa makubaliano yetu na Mheshimiwa Rais. Awamu nyingine mbili za marekebisho zilitarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka jana, yaani 2012. Hata hivyo, hadi nasoma maoni haya leo hii, Sheria ya Marekebisho ya Katiba haijafanyiwa marekebisho mengine yoyote.

   Mheshimiwa Spika,
   Mara baada ya marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kupitishwa mwaka jana, Mheshimiwa Rais alifanya uteuzi wa wajumbe na watendaji wakuu wa Tume na Tume yenyewe ilianza kazi mwezi Mei, 2012. Kwa maana hiyo, hadi kufikia leo Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeshafanya kazi kwa karibu mwaka mmoja.

   Kwa masikitiko makubwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda kulijulisha Bunge lako tukufu kwamba katika kipindi hiki mtiririko wa matukio kadhaa ndani na nje ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba imethibitisha kwamba haina weledi, dhamira au nia ya kusimamia mchakato huru usiofungamana na upande wowote.

   Katika mwaka wa kwanza wa mchakato wa upatikanaji Katiba mpya, Tume ya Mabadiliko ya Katiba imethibitisha hofu tuliyokuwa nayo toka mwanzo kwamba lengo la mchakato wa Katiba Mpya uliowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ni kuhakikisha kwamba mabadiliko pekee yakayokuwepo ni yale yenye kulinda matakwa ya CCM na Serikali yake au yale pekee yatakayokuwa na Baraka za “Status Quo”.

   Mheshimiwa Spika,
   Kwanza, Tume haikuweka utaratibu wowote madhubuti wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala yote yanayohusu Katiba Mpya ili kuwaandaa wananchi kuchangia maoni yao kwa Tume wakiwa na uelewa wa kutosha. Badala yake, wakati wa mikutano ya Tume ya kupokea maoni ya wananchi, wajumbe wa Tume walipewa jukumu la kuwaeleza wananchi juu ya Katiba Mpya kwa muda usiozidi nusu saa!

   Kwa kulinganisha, Tume ya Katiba ya Kenya ilifanya kazi ya kutoa elimu kwa umma kwa nchi nzima kwa muda wa miezi sita kabla ya kuanza kukusanya maoni ya wananchi wa Kenya juu ya Katiba Mpya. Matokeo yake ni kwamba mchakato wa Katiba Mpya wa Kenya umeiletea nchi hiyo Katiba Mpya ya mwaka 2010 ambayo imeanza kudhihirisha ubora wake kwa jinsi ambavyo mambo yatokanayo na Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo wa hivi karibuni yalivyotatuliwa.

   Mheshimiwa Spika,
   Pili, muda uliowekwa na Tume wa kukusanya maoni ya wananchi ulikuwa mdogo sana ukilinganisha na ukubwa wa nchi yetu na wingi wa Watanzania. Katika Majimbo karibu yote ya uchaguzi Tanzania Bara, Tume iliendesha wastani wa mikutano saba kwa kila jimbo kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi.

   Katika mikutano hiyo wananchi walitakiwa kutoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya kwa muda wa dakika tano kila mmoja na mikutano yenyewe ilichukua muda wa masaa matatu ikiwa ni pamoja na muda wa kutambulishana wajumbe wa Tume na mambo mengine yaliyo nje ya kuchukua maoni ya wananchi.

   Mheshimiwa Spika, matokeo yake ni kwamba kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Sinde Warioba kwa waandishi habari tarehe 5 Januari mwaka huu, hadi awamu nne za kukusanya maoni ya wananchi zinakamilika tarehe 19 Desemba, 2012, Tume ilikwisha kufanya mikutano 1,776 kwa nchi nzima. Aidha, kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti Warioba, hadi kufikia kipindi hicho wananchi wapatao 64,737 walikwishatoa maoni yao kwa kuzungumza wakati wananchi 253,486 walitoa maoni kwa njia ya maandishi, na wengine 16,261 walitumia njia ya “posta, tovuti ya Tume, mitandao ya kijamii na ujumbe mfupi wa simu za mkononi....” Kwa hiyo, kwa mujibu wa taarifa hizi za Mwenyekiti wa Tume, kati ya Watanzania takriban milioni 45, ni Watanzania 334,484 ndio waliotoa maoni juu ya Katiba Mpya hadi kufikia tarehe 4 Januari, 2013. Idadi hii ni sawa na asilimia 0.7 ya Watanzania wote! Na hao ndio waliotoa maoni yao kwa muda wa dakika tano kila mmoja, wakiwamo waheshimiwa Wabunge wa Bunge hili tukufu.

   Mheshimiwa Spika, ni wazi, kwa takwimu hizi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa vyovyote vile, Katiba Mpya itakayotokana na maoni haya haiwezi kuwa Katiba Mpya ya Watanzania wote. Utaratibu wa hovyo namna hii utazaa Katiba Mpya ya hovyo!!! Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba utaratibu huu wa hovyo hauwezi kutupatia Katiba Mpya yenye maridhiano ya kitaifa kwa ajili ya kutatua migogoro mingi ya kisiasa, kijamii na kidini ambayo inaikabili nchi yetu kwa sasa.

   Mheshimiwa Spika,
   Tatu, licha ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kutangaza kuwa Tume itakuwa huru katika utekelezaji wa majukumu yake, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona kila dalili za Tume kutokuwa huru au kuutafsiri uhuru vibaya. Kwa mfano, kuna ushahidi kwamba Tume imekuwa na mawasiliano ya karibu na Serikali na Ofisi ya Rais kwa namna ambayo inaashiria Tume kutokuwa huru. Ndio maana katika hotuba yake ya kumaliza mwaka uliopita na kufungua Mwaka Mpya, Rais Jakaya Kikwete alilitangazia taifa ratiba ya kazi za Tume ambayo Tume yenyewe ilikuwa haijawahi kuitoa hadharani.

   Katika hotuba yake hiyo, Rais Kikwete alitangaza sio tu kumalizika kwa awamu za kukusanya maoni ya wananchi, bali pia alitangaza ratiba ya Tume kuanza kuchukua maoni ya vyama vya siasa, taasisi nyingine na ‘makundi maalum’, tarehe ya kutolewa kwa Rasimu ya Kwanza ya Katiba Mpya, Mikutano ya Mabaraza ya Katiba na Bunge Maalum la Katiba na hata tarehe ya kura ya maoni na upitishwaji wa kura ya maoni kuihalalisha Katiba Mpya.

   Mheshimiwa Spika, Rais asingeweza kufahamu ratiba hii yote bila kupatiwa taarifa ama na Tume yenyewe ama na watendaji au watumishi wake au na wajumbe wa Tume. Mbali na taarifa ya kwisha kwa awamu ya tatu ya zoezi la kukusanya maoni ya wananchi, taarifa hizi hazikuwa zimetolewa hadharani na Tume kabla ya hotuba ya Mwaka Mpya ya Rais Kikwete!

   Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imetambua siku zote kwamba msemaji rasmi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni Mwenyekiti wa Tume Joseph Warioba. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haijawahi kusikia wala kuona mahali popote ambapo Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imempa Rais Kikwete jukumu la kuwa msemaji wa Tume. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inahoji kama Rais anaweza kupatiwa taarifa za kina namna hiyo kuhusiana na shughuli za Tume, kuna uhakika gani kwamba yeye au Serikali yake hawatoi kwa Tume maelekezo ya kichinichini juu ya nini cha kufanya, kwa namna gani na kwa wakati gani.

   Mheshimiwa Spika,
   Nne, wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikitoa taarifa za kina juu ya shughuli zake kwa Rais Kikwete na Serikali yake, Tume hiyo hiyo imetangaza wazi wazi kwamba haiwajibiki kwa Bunge kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Sheria. Zaidi ya kumtuma Naibu Katibu wa Tume, viongozi wa Tume kama vile Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume wamekataa kuhudhuria vikao vya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ili kuieleza Kamati juu ya utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Nchi.

   Katika hili, Tume imeungwa mkono na Serikali hiyo hiyo inayoelekea kupata taarifa za kina juu ya utekelezaji wa kazi zake! Hii ni licha ya kupatiwa jumla ya shilingi bilioni 33.944 za walipa kodi wa Tanzania zilizoidhinishwa na Bunge katika mwaka wa fedha 2012/2013 kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake. Kwa hiyo, wakati Tume inaharibu mchakato wa Katiba Mpya kama tulivyoonyesha hapa, Bunge – kwa kupitia kwa Kamati yake – limezuiliwa kuhoji shughuli za Tume kwa hoja kwamba Tume iko huru.

   Mheshimiwa Spika, hii inaweza kuwa mara ya kwanza kwa chombo cha umma kinachotumia mabilioni ya fedha za umma kilichopewa majukumu ya umma na Sheria iliyotungwa na Bunge hili tukufu kukataa kuwa chini ya usimamizi wa kikatiba wa Bunge (parliamentary oversight)!

   Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imesikitishwa sana na kushindwa kwa Kamati husika ya Bunge kudai madaraka yake ya usimamizi yasipuuzwe na Tume na/au Serikali. Udhaifu huu wa Bunge na Kamati unaweza kuligharimu Taifa endapo mchakato wa Katiba Mpya utachakachuliwa na kuliingiza Taifa katika machafuko ya kisiasa, kidini au kijamii.

   Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe kauli mbele ya Bunge hili tukufu juu ya uwajibikaji wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa matumizi ya mabilioni ya fedha za umma iliyoyaidhinishiwa mwaka jana na inayoyaomba mwaka huu wa fedha.

   Mheshimiwa Spika,
   Tano, Tume imetengeneza utaratibu wa mabaraza ya kikatiba ambao kwa ushahidi wa mwanzo tu unaonyesha kwamba hayo ni mabaraza ya CCM na sio mabaraza ya katiba ya Watanzania wote. Hili limefanyika kwa kupitia Mwongozo Kuhusu Muundo, Utaratibu wa Kuwapata Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya (Mamlaka za Serikali za Mitaa) na Uendeshaji Wake, uliotolewa na Tume mwezi Februari mwaka huu. Kwa mujibu wa Muundo huu, wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya watachaguliwa na Kamati za Maendeleo za Kata (maarufu kama ‘WDC’) baada ya kuwa wamechaguliwa moja kwa moja na wananchi katika vijiji na mitaa. Wajumbe wa WDC ni Madiwani wa Kata ambao ni Wenyeviti wake, Watendaji wa Kata ambao ni Makatibu na Wenyeviti wa Vijiji au Mitaa.

   Mheshimiwa Spika, kwa kufuatana na chaguzi za vijiji na mitaa za mwaka 2009, zaidi ya asilimia 90 ya vijiji na mitaa inaongozwa na wenyeviti ambao ni wanaCCM. Aidha, kutokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, zaidi ya asilimia 80 ya Kata zote nchini zinaongozwa na madiwani wa CCM. Hawa ndio waliochagua wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba tangu mwanzoni mwa wiki iliyopita. Matokeo yake, kwa taarifa ilizo nazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutoka sehemu mbali mbali za nchi yetu, kila mahali wagombea ambao hawakuwa wanaCCM walienguliwa katika ngazi ya uchaguzi wa vijiji au mitaa au wameenguliwa na WDC baada ya kushinda katika ngazi hizo.

   Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina ushahidi kwamba viongozi wa kiserikali kama vile Wakuu wa Wilaya na wa Mikoa waliwahamasisha wenyeviti wa vijiji, mitaa na madiwani kuhakikisha kwamba wagombea wote wasiokuwa wa CCM, hasa wa CHADEMA, wanaenguliwa katika chaguzi za vijiji, mitaa au kata. Mfano mzuri ni wa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Jackson Msome aliyeitisha mkutano wa wenyeviti wote wa mitaa ya Musoma Mjini na kuwapa maelekezo ya kuhakikisha kwamba watu wasiokuwa wanachama wa CCM hawapati nafasi katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya au Manispaa hiyo.

   Mheshimiwa Spika, licha ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupatiwa maoni ya wadau kwamba utaratibu huo utaharibu mchakato wa Katiba Mpya, Tume ilikataa kata kata kuubadilisha Muundo wa Mabaraza haya. Ni wazi kwamba Tume inafahamu inachokifanya.

   Ni wazi vile vile kwamba Tume inafahamu matokeo ya hicho inachokifanya, yaani kuundwa kwa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ambayo ni ya wanaCCM. Na wala haihitaji shahada ya uzamivu kufahamu kwamba Mabaraza ya Katiba ya Wilaya yenye kutawaliwa kwa kiasi hicho na wanaCCM yatatoa maoni ya aina gani juu ya Rasimu ya Katiba Mpya yatakayoijadili. Itakuwa ni Katiba Mpya kwa jina tu, mambo mengine ya msingi yatabaki vile vile. Kwa maneno mengine, itakuwa ni Katiba ile ile, ya watu wale wale, wa chama kile kile.

   Mheshimiwa Spika, Uchakachuaji wa mchakato wa Katiba Mpya wa aina hii ndio ulioiingiza Zimbabwe katika machafuko makubwa ya kisiasa toka mwaka 1998 na Kenya mwaka 2007/2008. Kwa utaratibu huu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, inaelekea Serikali ya CCM inaelekea kutotaka kujifunza kutokana na yaliyowakuta jirani zetu wa Kenya na marafiki zetu wa Zimbabwe.

   Mheshimiwa Spika,
   Sita, Serikali imekataa ama imeshindwa kuheshimu makubaliano iliyofikia na wadau mbali mbali ikiwemo CHADEMA, kufanya marekebisho zaidi ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Kwa sababu hiyo, bado haijulikani wajumbe mia moja na sitini na sita watakaotokana na taasisi mbali mbali zilizotajwa na Sheria hiyo watateuliwa kwa utaratibu gani na nani atakayefanya uteuzi huo.

   Vile vile, bado hakuna muafaka juu ya uhalali wa idadi kubwa ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar kushiriki katika mjadala wa Katiba Mpya kwenye masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanzania Bara wakati hakuna mjumbe hata mmoja wa Tanzania Bara anayeweza kushiriki katika mijadala ya kikatiba inayohusu masuala ya Zanzibar yasiyokuwa Mambo ya Muungano.

   Zaidi ya hayo, bado hakuna majibu yanayotosheleza yanayompa Rais mamlaka ya kuliitisha upya Bunge Maalum la Katiba na kulielekeza ‘kuboresha’ masharti ya Katiba Mpya mara baada ya Bunge hilo kuipitisha. Aidha, haijulikani ni uhalali upi wa kisheria na kikatiba utakaoiruhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia na kuendesha kura ya maoni ya kuhalalisha Katiba Mpya kwa sababu Katiba na Sheria za Uchaguzi za sasa hazitambui wala kuweka utaratibu wa kuendesha kura ya maoni.

   Mheshimiwa Spika, kushindwa kwa Serikali kuleta Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ili kufanya marekebisho katika maeneo tajwa ni ushahidi wa wazi kwamba Serikali ya CCM haina nia ya dhati na dhamira safi ya kuhakikisha Tanzania inapata Katiba Mpya inayoistahili.

   Aidha, si nia ya CHADEMA kuendelea kushiriki na kubariki mchakato huu kama ulivyo sasa kwani ishara zote ziko wazi kuwa Katiba inayokusudiwa ni ile tu itakayokidhi matakwa ya Wana- CCM na Washirika wake na hivyo kutokutimiza azma ya kuwa na Katiba itakayoponya majeraha mbalimbali na kurejesha uzalendo, mshikamano na upendo wa dhati miongoni mwa Watanzania na kisha mfumo wa Utawala utakaokidhi mahitaji ya wakati.

   Kwa sababu hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inatangaza rasmi kwamba: CHADEMA itajitoa ushiriki wake katika mchakato wa Katiba Mpya endapo mambo yafuatayo hayatapatiwa ufumbuzi hadi kufikia mwisho wa mwezi huu, yaani tarehe 30 Aprili, 2013:

   • Kufutwa kwa uteuzi/uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata, na badala yake wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wananchi wa Kata husika bila kuchujwa na WDC;
   • Serikali ilete mbele ya Bunge hili tukufu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yatayofanyia maeneo yafuatayo marekebisho:
    • Vifungu vyote vinavyohusu uwakilishi katika Bunge Maalum la Katiba wa taasisi zilizoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba;
    • Vifungu vyote vinavyohusu ushirikishi wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar katika mijadala inayohusu mambo yasiyokuwa ya muungano ya Tanzania Bara;
    • Vifungu vyote vinavyohusu mamlaka ya Rais kuitisha tena Bunge Maalum la Katiba baada ya Bunge hilo kuwa limeshapitisha Rasimu ya Katiba Mpya kwa lengo la kufanya marekebisho katika Rasimu kabla haijapelekwa kwenye kura ya maoni;
    • Vifungu vyote vinavyohusu mamlaka ya kikatiba nay a kisheria yatakayoiwezesha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuendesha na kusimamia kura ya maoni;   3. ANGUKO LA ELIMU TANZANIA: ANGAMIZO LA KIZAZI NA JANGA LA TAIFA.


   Mheshimiwa Spika,
   Nianze kuzungumzia umuhimu wa elimu kwa kumnukuu Rais wa 55 wa Marekani, John F.Kennedy (1917 – 1963);
   “Our progress as a nation can be no swifter than our progress in education. The human mind is our fundamental resource”

   Mheshimiwa Spika,
   Siku za karibuni kumekuwepo mjadala mzito sana kuhusiana na hali ya elimu nchini. Pamekuwepo na malalamiko mengi sana yakiwemo yaliyomtaka Waziri wa Elimu Mhe. Shukuru Kawambwa na Naibu wake Mhe Phillip Mulugo wajiuzulu kama ishara ya uwajibikaji wa kisiasa. Ni dhahiri kuwa elimu yetu kama Taifa imeporomoka kwa kiasi kikubwa cha sasa kuhatarisha mustakabali wetu kama Taifa.

   Mheshimiwa Spika, ni mwaka mmoja tu umepita tangu Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA itoe angalizo kali kwa Serikali juu ya kasi kubwa ya kuporokoka kwa Elimu ya Tanzania na hivyo kuitaka Serikali kuchukua hatua madhubuti ili kuliepusha Taifa na balaa hilo. Hata hivyo, Serikali hii ya CCM imeendelea kupuuza ushauri mzuri inayopewa bure na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na matokeo yake ni kwamba anguko la mwaka huu ni kubwa kuliko maanguko yote yaliyowahi kutokea katika Historia ya Tanzania ambapo asilimia 60.6 (240,903) ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne wamepata daraja sifuri na wengine asilimia 26.02 (103,327) daraja la nne. Jumla ya kufeli huku ni zaidi ya asilimia 86.62 au sawa na

   Mheshimiwa Spika, kufuatia kufeli huku kwa kutisha kwa wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2012, wadau wengi walitaka baadhi ya viongozi wa sekta ya elimu akiwemo waziri kuwajibika. Ni bahati mbaya sana kuwa Waziri Mkuu ni mmoja wapo wa viongozi Wakuu aliyestahili kuchukua hatua za kuwawajibisha wahusika lakini hakufanya hivyo. Badala yake, akakimbilia kuunda tume ya uchunguzi, ilhali yeye mwenyewe Waziri Mkuu, Waziri wake wa elimu na serikali yake yote ikijua fika nini kinasababisha kuporomoka kwa elimu yetu. Yumkini, kama kweli serikali hadi leo haijui sababu ya kuporomoka kwa elimu yetu, basi haina tena sifa wala weledi wa kusimamia siyo tu elimu, bali maisha ya kila siku ya Watanzania.

   Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa kufeli huku hakuwezi kuchukuliwa kama bahati mbaya hasa ikiwekwa maanani kuwa mserereko wa watoto wetu kufeli umeshika kasi chini ya utawala wa Serikali ya awamu ya nne hasa kuanzia mwaka 2007.

   Mheshimiwa Spika, mwaka 2007, ufaulu wa vijana wetu wa kidato cha nne ilikuwa (90.3%), 2008 (83.6%), 2009 (72.5%) na 2010 (50.4%). Kufuatia mserereko huu wa kufeli, serikali iliunda timu iliyoshirikisha wataalam kadhaa kubaini chanzo chake na tiba ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Timu hii iliyokuwa chini ya Uenyekiti wa Bw. Francis M. Liboy wa TAMISEMI ilikamilisha ripoti yake mwaka 2011 na kutoa mapendekezo kadhaa kwa serikali. Waziri wa Elimu Mhe. Shukuru Kawambwa anaijua ripoti hii kwani ndiye aliyeandika dibaji yake. (Angalia kiambatanisho A)

   Mheshimiwa Spika, mbali na ushauri wetu wa mara kwa mara, serikali hii imebeza kwa nguvu zote juhudi mbalimbali zinazofanywa na wadau wengine wenye kuumizwa na kusikitishwa na kuporomoka huku kwa elimu. Watanzania ni mashahidi namna katika Mkutano wa Kumi wa Bunge, hoja binafsi ya Mheshimiwa James Mbatia (Mb) kuhusu udhaifu ulioko katika sekta ya elimu ilivyochukuliwa kimzaha na kutolewa majibu mepesi na Serikali kinyume na kanuni za bunge na hatimaye kuyazima maazimio ya bunge ya kuinusuru elimu ya Tanzania yaliyokuwa yamependekezwa katika hoja hiyo. Ni katika mkutano huohuo wa Bunge ambapo hoja binafsi ya Mheshimiwa Joshua Nassari (Mb) kuhusu Baraza la Mitihani linavyoathiri elimu ya Tanzania iliondolewa katika orodha ya shughuli za mkutano wa kumi wa Bunge bila ridhaa ya mtoa hoja kinyume na kanuni ya 58(5).

   Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali ya CCM chini ya mwavuli wa wingi wa wabunge wake bungeni, cha kuzivuruga hoja hizi na hivyo kusababisha maazimio ya bunge juu ya hoja hizi kutotekelezwa ni udhaifu mkubwa sana kwa chama kinacho tawala cha CCM na Serikali yake na ni ushahidi uliokamilika kwamba Elimu kwao sio kipaumbele cha taifa.

   Mheshimiwa Spika, Serikali ambayo Elimu sio kipaumbele chake, haiwafai Watanzania kwa karne hii. Kuendelea kuukumbatia utawala na aina hii ni kukaribisha maafa yasiyoepukika kwa Taifa. Mbali na kulisababishia Taifa hili aibu kubwa mbele ya majirani zetu na jamii ya kimataifa kwa vijana walio wengi wa Kitanzania kuonekana kuwa na elimu ya mashaka na isiyoweza kuhimili ushindani wa soko la ajira, ubovu wetu wa elimu umedumaza uwezo wetu wa ndani wa kusimamia rasilimali za Taifa, Aidha kambi Rasmi ya Upinzani inawapa angalizo wananchi wote wa Tanzania kwamba haya yote yanatokea kwa kuwa Serikali ya CCM haijaiweka Elimu kuwa kipaumbele cha taifa na kwamba umefika wakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala kwa kuchagua chama chenye nia ya dhati ya kuleta mabadilko kitakachounda Serikali inayojali elimu ya watoto wao na bila shaka chama hicho hakiwezi kuwa CCM tena.

   Mheshimiwa Spika, Taifa kupitia hotuba hii linataka kujua Serikali ina nini cha kusema kuhusiana na utafiti huu iliofanya mwaka 2011, imetekeleza mangapi kati ya mapendekezo 27 yaliyotolewa. Aidha ni kwa nini imeunda tume nyingine kwa kutumia fedha za walipa kodi wa nchi hii ingali ripoti nyingine inayohusu somo hilo hilo ikiwa mkononi.

   3.1. UNYANYAPAA WA FIKRA VYUO VIKUU


   Mheshimiwa Spika, pamoja na nia njema ya katiba ya nchi yetu kuheshimu haki ya uhuru wa mawazo kama ilivyowekwa bayana katika Ibara ya 18(a) na Ibara ya 20(1) kwa kutoa uhuru wa mtu kushirikiana na wengine, kumekuwepo na propaganda mbalimbali hasa kwenye taasisi za elimu ya juu, zenye kuminya nafasi na uhuru wa vyama vya upinzani kuendesha shughuli zake kwa usawa, uwazi na kwa haki katika ngazi ya elimu ya juu kama ambavyo chama tawala kimejiwekea na kujitengenezea mazingira hayo.

   Mheshimiwa Spika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema hivi: "Lakini kutoa uongozi maana yake siyo kuwanyang'anya watu wenyewe mamlaka yao. Watu lazima wafanye uamuzi wao wenyewe kuhusu maisha yao ya baadae kwa kufuata njia za demokrasia. Uongozi hauwezi kuchukua nafasi ya demokrasi; uongozi lazima uwe sehemu ya demokrasi"

   Mheshimiwa Spika, tafakuri ya nukuu hii imekuja wakati ambao ushiriki wa wanafunzi wa elimu ya juu katika siasa unaonekana kulemea upande moja tu wa kukipendelea na kukipa uwezo chama tawala katika shughuli zake kwenye taasisi hizo. CCM wamefikiri na kuamua kuanzisha mkoa maalumu kwa sasa wakitambua kuwa vyuo (hasa vyuo vikuu) haviruhusiwi kuendesha shughuli za siasa vyuoni, kama ilivyo majeshi, makanisa au misikiti na ili kuthibitisha hilo wameelekeza pia shughuli za mkoa maalumu ulioanzishwa zifanyike nje ya chuo. Lakini tujiulize na kutafakari zaidi kuhusu mshindo (impact) wa shughuli za mkoa maalumu wa kisiasa ndani ya himaya za vyuo vikuu na elimu ya juu nchini.

   Mheshimiwa Spika, ni ngumu kuamini kuwa shughuli za siasa vyuoni, ambazo Tanzania Commission of University Act imeweka bayana kuwa ni kosa, zitaweza kudhibitiwa ikiwa vyama vingine vinajiwekea uhalali na mazingira ya kuingiza wanavyuo kwenye siasa, jambo ambalo udhibiti wake ni mgumu kwa mamlaka husika hasa vyuoni kwa kuwa wanavyuo hufanya vikao vya siasa kwa siri, na kwa nyakati ambazo uongozi wa vyuo hauna taarifa.

   Mheshimiwa Spika, kwa uangalifu mkubwa, ningependa kutoa angalizo kuwa, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haitokubali unyanyapaa wa fikra wa aina yoyote utakaoendana na kujenga matabaka kutokana na utofauti wa mitazamo baina ya jamii ya wasomi kwa kuwa, kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu , chimbuko la viongozi mahiri wa nchi hii pamoja na nchi nyingine mbalimbali duniani limechipukia. Kambi Rasmi ya Upinzani, itaendelea na juhudi zake za kuhakikisha kuwa taifa kwa kupitia wanafunzi wa elimu ya juu, wanapata fursa mbalimbali za kuikomboa jamii ya kitanzania ambayo inadumazwa kwa unyanyapaa wa fikra.

   Mheshimiwa Spika, njia pekee ya kufuta unyanyapaa wa fikra kwa vijana waliopo kwenye elimu ya juu ni kwa Serikali kurejesha rasmi na kuruhusu uwepo wa siasa katika elimu ya juu na vyuo vikuu vyote nchini kama shughuli ambazo ni nje ya masomo ili kusaidia kujenga uwanja wa demokrasia katika serikali za vyuo na vile vile itasaidia katika kuweka mazingira ambapo wasomi wetu wanaanza kujifunza mbinu na utendaji wa kisiasa katika mazingira ya elimu ili waweze kujifunza kuishi pamoja, kupingana kwa hoja na kujua jinsi ya kuvumiliana katika mazingira ya tofauti mbalimbali za kiitikadi, imani, na mtazamo kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA ya mwaka 2010. Hapa nikisisitiza maneno ya baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere juu ya kuboresha maisha ya Watanzania:
   "Tukiwasaidia watu wa Tanzania kuendelea, ndiyo tunaiendeleza Tanzania. Maana Tanzania Ni ya Watanzania Na Watanzania Ni wote, Hakuna mtu mwenye haki ya kusema "Mimi ndiyo watu". Wala hakuna Mtanzania mwenye haki ya kusema " Najua linalowafaa watanzania na wengine lazima wafuate".
   INAENDELEA....
   Last edited by Molemo; 11th April 2013 at 12:22.


  2. VUTA-NKUVUTE's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th November 2010
   Location : Where the truth is
   Posts : 4,605
   Rep Power : 94989405
   Likes Received
   5606
   Likes Given
   1295

   Default Dodoma-Mbowe ndiye habari ya leo!

   Ukweli,umahiri katika uwasilishwaji wake,mifano dhahiri na kauli za kiongozi ndizo sifa zinazoelekezwa kwa Ndugu Freeman Aikael Mbowe,Mbunge na Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni. Wananchi wa Dodoma wamekoshwa sana na hotuba ya Mbowe. CCM tunatapatapa kujibu hoja za Mbowe nje ya Bunge na Wabunge wetu wameagizwa kuichanachana hotuba ya Mbowe na kuipa uhai hotuba ya Waziri Mkuu kuanzia kesho. Mwigulu atakuwa mstari wa mbele kimashambulizi kesho. VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam(sasa Dodoma)

  3. Maganga Mkweli's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th July 2009
   Posts : 2,031
   Rep Power : 1159
   Likes Received
   745
   Likes Given
   2101

   Default Re: Dodoma-Mbowe ndiye habari ya leo!

   asante kwa taarifa.. ukweli utasimama daima..
   peopleees power ...
   LIKE NOTHING HAPPENED.... AND LIFE GOES ON...


  4. Man 4 M4C's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd August 2012
   Posts : 705
   Rep Power : 1007
   Likes Received
   99
   Likes Given
   20

   Default Re: Full Text: Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bajeti 2013/2014 iliyosomwa na Freeman Mbowe

   Kama mtu alifumaniwa na mke wa mwanachama mwenzake igunga akalipia uhani 14m kimya kimya hamuoni kuwa hata hapa bado baba yake hajasema kuwa akamatwe apelekwe mahakamani?? Ila ipo siku hata wakizeeka watakuja kunyea debe

  5. Kanundu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd April 2012
   Posts : 891
   Rep Power : 858
   Likes Received
   344
   Likes Given
   297

   Default Re: Dodoma-Mbowe ndiye habari ya leo!

   Quote By VUTA-NKUVUTE View Post
   Ukweli,umahiri katika uwasilishwaji wake,mifano dhahiri na kauli za kiongozi ndizo sifa zinazoelekezwa kwa Ndugu Freeman Aikael Mbowe,Mbunge na Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni. Wananchi wa Dodoma wamekoshwa sana na hotuba ya Mbowe. CCM tunatapatapa kujibu hoja za Mbowe nje ya Bunge na Wabunge wetu wameagizwa kuichanachana hotuba ya Mbowe na kuipa uhai hotuba ya Waziri Mkuu kuanzia kesho. Mwigulu atakuwa mstari wa mbele kimashambulizi kesho. VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam(sasa Dodoma)
   Kwa MAGAMBA, Mwigulu ndiye shujaa. Kwao ukisha weza kuporomosha matusi utapigiwa makofi zaidi ya tunavyo fikiri. Watu wenyewe ni akina Prof. Maji Marefu, Kibajaji n.k. waTanzania kazi tunayo.
   CCM IS LIKE BUYING HAY FOR A DEAD HORSE

  6. Kijitonyama's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 9th April 2013
   Posts : 242
   Rep Power : 7898
   Likes Received
   88
   Likes Given
   0

   Default Re: Mbowe; "Anaewasiliana na Gaidi anahusika na Ugaidi!"

   Quote By Mohamedi Mtoi View Post
   Tatizo wenzetu wa CCM kuna Mantiki hawataki kuiona! Si kwa sababu wana uoni hafifu, ni kwa sababu swala hili la ugaidi wanalitumia kama turufu ya kuinyong'onyeza chadema.

   Hivi umeshajiuliza kuwa Mwigulu angekuwa ni mwana chadema aliyewasiliana na Ludovick kungetokea nini mpaka sasa?!

   Kama Mwigulu amekiri kumfahamu LJ na hata kumtumia fedha masaa machache baadae,kwa nini asiuganishwe?
   Jeshi la police limethibitisha kwa watanzania jinsi linavyohusika na kuandaa hii kesi kwa kuwabambikiza watu. Lazima tuwe makini tunapotaja CCM. Nina imani Mwiguru Nchemba na jeshi lake la police sio CCM. Hawa ni wahuni na vibaraka tu. Wanacheza na vitu ambavyo marahisi watatu wamepita katika taifa letu lakini huwa hawachezei;yaani kutumia usalama wa taifa na jeshi la police kutesa wananchi. Huu ni udhaifu wa uongozi wa hali ya juu.

   Mnajaribu kutudanganya kwamba Evodius alikamatwa Bukoba, akapelekwa Mwanza kuteswa, baadae Dar hili abambikizwe kesi ya kurecord mkanda. Baada ya kushindwa kufanya hivyo, mkambambikiza kesi ya Igunga. Hivi wanadhani wananchi wana ubongo kidogo kama viongozi wa vyombo vya usalama? Kwani mtu akiwa na kesi Igunga, analetwa Dar kufanya nini? huko Igunga hamna Police?

   Huu ulikuwa mpango wa CCM wakisaidiwa na vyombo vya usalama tulivyoviheshimu siku zote lakini heshima inatoweka kila kukicha. Naomba mkumbuke kitu kimoja ambacho wengi wenu hamkutambua. Ni pale ambapo Nape alienda Kilimanjaro na kuanza mkutano wake kwa kuwasimamisha watu ili waombee mambo ya kigaidi wanayofanya Chadema. Sasa sijui walikuwa wanamwomba Mungu gani. Pengine ni shetani wao. Mchezo ulikuwa umepangwa ufanyike hivyo. Yaani baada ya kutekwa huyo Kibanda (ambaye nadhani ilikuwa wrong target), wao walitarajia kuleta video. Baada ya hapo, walitaka kuwakamata viongozi wa Chadema wengi na walitegemea magazeti na habari zote zijae huo uhuni. Kibaya, likawa limeporomoka jengo Dar. Hii ilikwamisha mbinu yao maana vyombo vya habari nchini vilianza kuongelea hilo jengo. Baadae ikatokea kifusi Arusha. Yote haya yalikuwa yanamchelewesha Nape. Nakwambia alishaandaa kila kitu. Baada ya muda kidogo ndo Nape anaonekana anakwenda Kilimanjaro lakini walishapanga haya mambo.

   Sasa watanzania wenzangu ntazidi kuwambia. Hawa mabwana wana mpango wa kuivuruga nchi na kuwafanya nyie watumwa katika nchi yenu. yakitokea machafuko ya aina yoyote, wengi wa hawa watu watakuwa na hela ya kutosha kukimbilia nchi nyingine, na nyie mnaobishana hapa kwenye forum, wengi wetu tutakaa tu. Sasa tufanyeje? waunge mkono baadhi ya watu waliokwisha simama kinyume na utawala ovyo. Chadema si watakatifu lakini wamejaribu. Maisha ya viongozi wao yanawindwa kila kukicha. Wamejitolea maisha yao ili kuwapigania nyie. Wamefanya kitu ambacho wengi wetu tunakiogopa, yaani kuhoji serikali isiyokuwa na sheria hivyo waunge mkono. Msitegemee atajitokeza mtu mtakatifu. Nao wana mapungufu lakini wako far way better ukiwalinganisha na CCM. Baada ya hapo tutafurahia matunda ya nchi yetu kwa kuijenga sisi wenyewe sio kuwaachia mafisadi.

   Tukiendelea kubishana, tutakuwa tunafanya kile mafisadi wanachotaka tukifanye, yaani kusinzia na kuliacha taifa letu likiliwa. Watoto wetu tunawaandalia mazingira gani? watoto wa mafisadi watakuwa vizuri kwa sababu walishatengewa mali za taifa. Watanzania shikana, kemea huu upuuzi!!!

   Walimteka Ulimboka na kumuumiza, madaktari wote sasa hivi wapo chini ya vitanda. Hakuna hata mmoja aliyeendeleza juhudi za Ulimboka. Kwa maana nyingine, Ulimboka alikuwa anapigania watu wajinga sana. Watesi wake wamegundua hiyo njia ni nzuri kuwanyamazisha watu, sasa wanakuja kwenu watanzania. Amkeni pinga upuuzi!!!!!


  7. Rack Fikiri's Avatar
   Member Array
   Join Date : 13th October 2012
   Posts : 23
   Rep Power : 468
   Likes Received
   1
   Likes Given
   0

   Default Re: Full Text: Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bajeti 2013/2014 iliyosomwa na Freeman Mbowe

   Mh. Amejitahidi kuwakumbusha mambo ya mhimu hasa kwenye mpaka mikopo ya elimu ya juu inavyo chakachuliwa

  8. Ghamunga's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 10th September 2012
   Posts : 124
   Rep Power : 493
   Likes Received
   5
   Likes Given
   2

   Default Re: Full Text: Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bajeti 2013/2014 iliyosomwa na Freeman Mbowe

   wabunge wa ccm wakati wa kuchanojagia hoja analalamika na kuanza kutoa hoja zake mwisho anasema anaunga mkono hoja .kama mbunge anaunga yaliyozungumzwa ya nini sasa anapoteza muda awape nafasi wale ambao hawakubaliani na hoja hiyo wewe unayekubaliana ya nini sasa unachangia basi au unajionyesha kwa wapiga kura wako siyo ama vipi.watanzania tunawaona sana hata kama hatukusoma tunajua nini kina endelea


  9. nemasisi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th October 2012
   Posts : 1,762
   Rep Power : 817
   Likes Received
   355
   Likes Given
   84

   Default

   Quote By Mohamedi Mtoi View Post
   Tatizo wenzetu wa CCM kuna Mantiki hawataki kuiona! Si kwa sababu wana uoni hafifu, ni kwa sababu swala hili la ugaidi wanalitumia kama turufu ya kuinyong'onyeza chadema.

   Hivi umeshajiuliza kuwa Mwigulu angekuwa ni mwana chadema aliyewasiliana na Ludovick kungetokea nini mpaka sasa?!

   Kama Mwigulu amekiri kumfahamu LJ na hata kumtumia fedha masaa machache baadae,kwa nini asiuganishwe?
   sipati picha ingekuwaje, siasa za nchi zinapoteza mwelekeo wa jeshi la polisi na ndiyo maana wananchi wengi mtaani wanaamini mambo yote haya ni mpango wa ccm kutafuta nafasi ya kuchafua chadema ili waendelee kubaki madarakani lakini kuna dalili nzuri za mpango huu kushindwa

  10. Molemo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2010
   Posts : 13,190
   Rep Power : 146133716
   Likes Received
   8483
   Likes Given
   618

   Default

   Quote By nemasisi View Post
   sipati picha ingekuwaje, siasa za nchi zinapoteza mwelekeo wa jeshi la polisi na ndiyo maana wananchi wengi mtaani wanaamini mambo yote haya ni mpango wa ccm kutafuta nafasi ya kuchafua chadema ili waendelee kubaki madarakani lakini kuna dalili nzuri za mpango huu kushindwa
   Kwa ujinga wa polisi wameshasababisha tukio lote kuwa la kisiasa na halina nguvu yoyote.

  11. mbukoi's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 17th January 2012
   Posts : 248
   Rep Power : 552
   Likes Received
   70
   Likes Given
   397

   Default Re: Full Text: Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bajeti 2013/2014 iliyosomwa na Freeman Mbowe

   Nchi yenye serikali imara na kambi ya upinzani imara lazima iendelee kwani kila mtu atakuwa mzalendo na michakato ya kitaifa itakuwa fair and unbiased nafikiri hili ndilo lengo haswa la uwepo wa mfumo wa vyama vingi.

  12. Pasco's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 22nd September 2008
   Posts : 17,193
   Rep Power : 400120010
   Likes Received
   16021
   Likes Given
   73180

   Default Re: Full Text: Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bajeti 2013/2014 iliyosomwa na Freeman Mbowe

   Quote By Mwita Maranya View Post
   Pasco kwahiyo unataka nikuelewe kwamba mkifanya tukio la uhalifu mkiwa wawili au watatu halafu mmoja wenu akachomoka akaenda kuripoti polisi juu ya uhalifu mlioufanya yeye anakuwa hana hatia mbele ya sheria?
   Au mimi ndiye sijakuelewa vizuri jinsi hiyo sheria inavyofanya kazi? Ufafanuzi tafadhali...
   Mkuu Mwita Maranya, hivyo ndivyo hali ilivyo!.

   Mkipanga njama za uhalifu kwa pamoja, au mara baada ya jinai kutendeka, ukasaidia kuficha ukweli, wewe pia ni mhalifu uitwae accessories before the fact au after the fact. Endapo mmepanga jinai pamoja, na ukashiriki kwenye jinai hiyo kisha ukawageuka wenzako na kwenda kuripoti polisi, wewe unaweza kupewa msamaha kwa ushirikiano mzuri na kugeuzwa ndio shahidi nambari moja wa jamhuri katika kesi husika depending na the role you played.

   Kama unaikumbuka ile kesi ya uhaini ya mwaka 1982, mwanzo washitakiwa walikuwa 53, wakapungua na kubaki 45, na kesi ilipoanza walibaki washitakiwa 23 tuu, wale wengine ndio waligeuka mashahidi wa jamuhuri!.

   Kama Ludo ametoa ushirikiano wa kutosha kwa kueleza kila kitu, naomba usishangae kama atafutiwa mashitaka na kugeuzwa ndie PW1, na ndio maana kamtaja aliyekuwa akiurekodi ule mkanda!. Mtu mwenye hatari kujuishwa kwenye kesi ya msingi, ni kiongozi wa Chadema, aliyempatia Mwigulu ule mkanda!, ila kitendo cha Mwigulu kuuripoti tuu polisi mara baada ya kuutia mkononi, kunamuweka kwenye safe side!.

   The biggest games people play kwenye kesi za jinai ni kipengele cha "admissibility of evidence" kama alivyosema Mhe. Tundu Lissu, hivyo ni kesi ya nusu saa tuu!, itafanyika "trial within trial" kudetermine mkanda upokelewe kama ushahidi au laa!, wanasheria wa Lwaka, wakifanikiwa kuiaminisha mahakama kuukataa ushahidi huo wa mkanda, then kesi imekwisha!. Au Rwaka, akiithibitishia mahakama, ule mkanda was just acting/pretending, but there was no such plot, then kesi inakwisha!.

   Kama aliyempatia Mwigulu ule mkanda ni kiongozi wa Chadema, aliyeupandisha jf ndio mtu yule yule aliyepandisha scanned paper ya mwandiko wa Rwaka, na the same man aliyeipandisha ile barua ya ZZK, then for sure hiki ni "kirusi!" hatari kuliko, kwa sababu, I can't calculate the motive behind!.

   Pasco.

  13. bushman's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st November 2010
   Posts : 2,219
   Rep Power : 1009
   Likes Received
   570
   Likes Given
   91

   Default Re: Full Text: Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bajeti 2013/2014 iliyosomwa na Freeman Mbowe

   Kidume kaunguruma.

  14. kiwatengu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th April 2012
   Location : Sing'isi Meru
   Posts : 11,610
   Rep Power : 429499242
   Likes Received
   6693
   Likes Given
   4150

   Default

   Quote By thatha View Post
   teh teh teh, huyo lazima atakuwa MSIGWA au MNYIKA, hao ndiyo wanaamini ki
   takachoipeleka CDM ikulu ni maandamano
   Huyu jamaa chilisosi..
   aliwahi kusema atagombea ubunge iringa mjini

  15. yegella's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th November 2010
   Location : Jalalani
   Posts : 2,908
   Rep Power : 256472
   Likes Received
   949
   Likes Given
   735

   Default

   Quote By bagosha bane View Post
   analitikisa kwa kulisukuma au unamaanisha nini hapa kaka.
   kachunge ngommbe na kulala ngozi huku madini yakisombwa na maccm hukuùkiwala$ba masabuli..amka kijana waangalie ndugu zako hata kama wewe unalipwa lumumba..

  16. Sumu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th November 2010
   Location : Abbottabad, Hazara.
   Posts : 4,149
   Rep Power : 1394
   Likes Received
   1370
   Likes Given
   1556

   Default re: Mbowe akiri kuwa CCM bado imetapakaa nchi nzima

   Kwakuwa Mh. Mbowe ameshakiri mapema kwamba CCM imeenea nchi nzima, 2015 sitegemei kumsikia Dr. Slaa akidai ameliona kontena lenye kura.
   Cowards Die Many Times Before Their Deaths, The Valiant Never Taste Of Death But Once - Shakespeare.

  17. Deshmo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th December 2012
   Posts : 3,804
   Rep Power : 1214
   Likes Received
   724
   Likes Given
   778

   Default Re: Full Text: Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bajeti 2013/2014 iliyosomwa na Freeman Mbowe

   Quote By bungeni View Post
   magaidi wa chama chake wamemshinda sembuse bunge la nchi
   http://www.jamiiforums.com/images/st...ilies/blah.gif

  18. Mwana wa Nuru's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd December 2012
   Posts : 348
   Rep Power : 526
   Likes Received
   106
   Likes Given
   55

   Default Re: Full Text: Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bajeti 2013/2014 iliyosomwa na Freeman Mbowe

   Quote By bungeni View Post
   pinda ndio ki dume pekee aliyetoa hotuba ya kulitingisha taifa jana
   Mwenyewe tayari umeshamdunisha kwa kumuita ki-dume na nadhani uko sawa kabisa kwani UNAJUA HAKIKA MBOWE NI DUME na akiongea basi vidume vyote vinaufyata na vijike vyao vinamgwaya na ndio maana haviishi kuiota na kuiotea CDM. Nimeipenda hotuba ya kiongozi wa wananchi na kambi rasmi ya upinzani bungeni.ina maneno murua na yanayoeleza matakwa ya wananchi walio wengi na wasiyoitaka kusikia mafisadi na wapambe wao.Mugu mbariki Freeman , Mungu ibariki CDM, Mungu ibariki Tanzania.

  19. Benaire's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th December 2011
   Posts : 1,940
   Rep Power : 896
   Likes Received
   287
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By Sha Makala View Post
   Mwenyekiti wa chadema mh Freeman Mbowe ameshindwa kuficha ukweli na kukiri kuwa CCM imetapakaa, imeenea kote nchini . Mkt huyo amekiri bungeni alipokuwa anawasilisha maoni yao aliposema mabaraza ya katiba yamejaa CCM. KWAMBA MGOMBEA YEYOTE WA CHADEMA ALIANGUSHWA. TAFSIRI HII NI KWAMBA HATA SERIKALI ZA MITAA CCM ILIVYOENEA ITASHINDA TU. KWA WENYE AKILI CCM ISINGEKUWA IMEENEA WAGOMBEA WA CHADEMA WASINGEANGUKA KOTE MPAKA KUMTIA HOFU MKT HUYO NAKUTISHIA KUJITOA. NAISHANGAA CCM KILA NIENDAKO NAIKUIKUTA.
   Yaani kuna watu sio watanzania eti? Sasa cha kushangaa ni nini hapo...Chama kina miaka zaidi ya hamsini...na tangu kinaanzishwa kipo madarakani...leo unataka kiwe kama UDP (Bariadi tu)

  20. kibaya-kenya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd April 2012
   Posts : 640
   Rep Power : 620
   Likes Received
   158
   Likes Given
   91

   Default Re: Full Text: Hotuba ya Kambi ya Upinzani Bajeti 2013/2014 iliyosomwa na Freeman Mbowe

   Kwani hili la WDC naomba tuweke ushabiki pembeni,ukweli wale wote wliopita ni wateule wa ccm mfano wilaya ya monduli kwa FISADI MKUU yeyote ambaye sio ccm au upande wa LOWASSA hakupitishwa sembuse uwe na dalili za uchadema au uwezo wa kuhoji,
   Ni aibu kwa taifa kabisa,WDC wasiwe na mamlaka ya kuptisha mtu ila ibaki kwa wanakijiji/kata.
   HAPO MONDULI MIE NIMEPIGWA CHINI BAADA YA LOWASSA KUNIKATAA SASA BABU NAHOJI SAANA MAMBO YA HALMASHAURI.
   Ndugu zangu tuungane tudai katiba ya haki.JAJI WARIOBA AMETUANGUSHA SANA
   SHAME UPON CCM

  21. Benaire's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th December 2011
   Posts : 1,940
   Rep Power : 896
   Likes Received
   287
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By Sumu View Post
   Kwakuwa Mh. Mbowe ameshakiri mapema kwamba CCM imeenea nchi nzima, 2015 sitegemei kumsikia Dr. Slaa akidai ameliona kontena lenye kura.
   Hajasema wapiga kura wa CCM wameenea nchi nzima...hapo ndipo uliposhindwa kuelewa..
   Wenyeviti wengi wa mitaa ni ma CCM...ndio alichokuwa akizungumzia.
   Masuala ya wapiga kura kuna demographic changes (vijana wanaofikisha 18 age,wanaokufa,wanaoamua kupiga kura n.k)
   Ndio maana amesema wapige kura wananchi....


  Page 13 of 17 FirstFirst ... 31112131415 ... LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...