JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

  Report Post
  Page 14 of 18 FirstFirst ... 41213141516 ... LastLast
  Results 261 to 280 of 341
  1. utaifakwanza's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st February 2013
   Posts : 12,076
   Rep Power : 28563
   Likes Received
   921
   Likes Given
   938

   Default Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   Anazungumzia mambo mbalimbali, ameanza na suala la vurugu na mahusiano mabaya kidini yaliyoibuka hapa nchini. Suala la kuchinja, kuuawa kwa viongozi wa dini na esp kuuawa kwa padri mushi kule zanzibar

  2. jmushi1's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2007
   Posts : 16,110
   Rep Power : 32245502
   Likes Received
   5418
   Likes Given
   6437

   Default Re: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   Quote By Kitoabu
   We unachinja bhanaaa! We una kata kichwa tu.
   Quote By Remote View Post
   kwani kuchinja ni nini?
   Ni ibada mkuu...
   "One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato

  3. Zacharia Kifyasi's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 23rd December 2012
   Posts : 135
   Rep Power : 480
   Likes Received
   23
   Likes Given
   0

   Default Re: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   Futuhi comed

  4. ferre.g's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd March 2013
   Location : MWANZA
   Posts : 2,199
   Rep Power : 1021
   Likes Received
   305
   Likes Given
   159

   Default Re: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   Yaleyale..hana jipya lolote...mjinga tu huyo..yeye ndo kaasisi leo anataharuki?...ebo?mshenzi mkubwa huyo.

  5. OKW BOBAN SUNZU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2011
   Posts : 13,746
   Rep Power : 103785778
   Likes Received
   4680
   Likes Given
   1080

   Default Re: Mh. Rais anena: Mbona kuna mabucha ya nguruwe watu hawapigani?

   Quote By Malyenge View Post
   Nguruwe huwa hachinjwi na wala waislamu hawali nguruwe.... Mgogoro wa uchinjaji unakuja pale mnyama aliyeruhusiwa kuliwa kwa sharti la kuchinjwa inakuwa pale ambapo yule asiyeruhusiwa kuchinja anachinja, maana yake analisha watu vibudu. Nguruwe anajulikana ni najsi na hivyo haruhusuwi kuliwa sasa kwa nini mgombane kwa kitu kisichoruhusiwa kuliwa? Kwani ukila wewe najsi (mfano ukila ng'ombe aliyekufa kibudu) bila kuwashirikisha na wengine kuna tatizo gani? Mbaya zaidi ninyi waktristo mnataka kutulisha na sisi waislamu vitu haramu hapo ndo hatukubali.....Vibudu vyenu mnataka kuvifanya public na ligitimate kwa kila mtu....Hapo lazima mapigano makali yatatokea.

   Suluhisho ni ninyi mkavila ninyi wengewe individually manyumbani kwenu na si kuanzisha mabucha. Mbaya zaidi mnakashfu uislamu na elimu nzima ya kuchinja mnataka kuonesha kwamba kuchinja siyo issue kama mlivyofanya katika mambo ya KUTAHIRIWA eti mnasema kutahiriwa nyama ya govi si kitu. Sasa kama hujatahiriwa unapata wapi mamlaka ya kuchinja?......
   Unachoandika ni pale upeo wako wa kufikiri upoishia.......isimaanishe kwamba upo sahihi
   • Ukizungumzia kuchinja kwa imani na mimi nitakuuliza ni wapi maandiko yangu ynaposema nichinjiwe na shehe. Ni wazi dini yako ilikuja baada ya kristo, niambie kabla nani alichinja
   • Nani alikuambia kuwa nguruwe ni najisi kwa imani yangu

   Nyongeza, nijibu maswali haya kunisadia maarifa kuhusu uislam

   • Nani alimpa utume Mtume Mohamad.....nipe aya au hadithi
   • Nipe nguzo kuu za uislam, mf mkiristu kuna usiue, usiibe n.k
   • Ni nini mwanamke/mwanaume anapofiwa anatakiwa kumfanyia mwenza wake aliyefariki kama ishara ya kumuaga
   Mbele Mungu nyuma Mungu katikati CHADEMA by Gwankaja Gwakilingo waJF

  6. adolay's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th December 2011
   Posts : 5,562
   Rep Power : 175909284
   Likes Received
   1937
   Likes Given
   1786

   Default Re: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   Quote By ozunuh View Post
   1 /4/2013 happy wajinga day!!!
   wewe ndiyo huelewi!!

   Tunakwambia tulioshuhudia akitoa hutoba asubuhi TBC1 kama huamini shauri yako au nenda TBC1 ukathibitishe.

  7. emilwayne's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th November 2011
   Posts : 266
   Rep Power : 563
   Likes Received
   18
   Likes Given
   10

   Default HOTUBA YA KIKWETE - jana

  8. Kitoabu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th July 2011
   Posts : 5,484
   Rep Power : 11184
   Likes Received
   958
   Likes Given
   518

   Default

   Quote By Remote View Post
   kwani kuchinja ni nini?
   Kumbe hata kuchinja hujui sasa nawewe unagombea kuchinja kweli we unania njema na taifa hili?

  9. OKW BOBAN SUNZU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th August 2011
   Posts : 13,746
   Rep Power : 103785778
   Likes Received
   4680
   Likes Given
   1080

   Default Re: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   Quote By ferre.g View Post
   Yaleyale..hana jipya lolote...mjinga tu huyo..yeye ndo kaasisi leo anataharuki?...ebo?mshenzi mkubwa huyo.
   Punguza jazba mkuu, huyu ni rais wetu au sio?
   Mbele Mungu nyuma Mungu katikati CHADEMA by Gwankaja Gwakilingo waJF

  10. PACHOTO's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th December 2011
   Posts : 607
   Rep Power : 590
   Likes Received
   153
   Likes Given
   119

   Default Re: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   Quote By Kitoabu View Post
   Ila makanisani ume tamallak
   sana tu mkuu maana yapo hata makanisa ya mashoga kama co shoga huruhusiwi kuingia
   http://www.gaychristian101.com/Gay-A...ng-Church.html

  11. kukukakara's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st July 2012
   Posts : 389
   Rep Power : 551
   Likes Received
   75
   Likes Given
   11

   Default Re: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   Wana JF
   Kwa heshima na taadhima hebu ktk mada hii tuonyeshe kuwa kuna uwepo ma GT humu. Namaanisha kuwa hebu jamvi hili litumike kutoa majawabu ya baadhi ya mambo magumu ambayo yaumiza vichwa nchi.

   Hili la uchinjaji lingeamuliwa hivi:
   Ndugu wananchi;
   Swala la nani achinje kati ya muislam na mkristo ni jambo geni sana nchini mwetu na wala haliwahi kutarajiwa. Tuna hakika halipo humu hivijivi bali kwa kusudi maalum ya kuharibu umoja na amani ya nchi hii au ubishi huu ni ongezeko la uhasama wa kidini unadhihiri kila kunapokucha.
   Nikumbushe tu kidogo kuwa imani za dini zinaambatana na kanuni zake kwa mfano; wakati wakristo wanaruhusu ndoa ya mke moja, waislamu wao wanaoa hadi wanne.
   Muislamu haingii na viatu msktini lakini mkristo havui akiingia kanisani, Marehemu wa kikristo aweza zikwa baada ya wiki ila sio kwa muislam. Vivyo hivyo Wakati mkristo anakula nyama iliyochinjwa sio kibudu, mwislamu anajali sio tu kuchinjwa ila ichinjwe na muislamu, tena si muislamu tu bali aliyeruhusiwa wanasema kupewa kisu.
   Wakristo walikula nyama bila kuhoji nani kachinja miaka yote na waliishi na waislamu kwa amani ndani ya kanuni nyingi sana tofauti za kiimani na kama nilivyoainisha baadhi hapo juu.
   Kwa hiyo ndugu wananchi kwa ajili ya amani na mshikamano wa taifa hili; turudi katika utaratibu wetu tuliozoea na wananchi tunawaomba radhi sana kama aidha kwa maksudi au kwa kujisahau au kupitiwa serikali ilishindwa kuchukua hatua mahsusi kwa jambo hili na mengine yanayofanana na hili na kupelekea ubishi huu kuwepo na unapelekea amani ya taifa kutoweka

   Ni matarajio yetu kuanzia leo nchi yetu inazika migogoro yote ya kidini na tunakuwa wamoja ili iwe kumgundua adui atokae nje ya mipaka yetu kama yupo na yeyote atakaekiuka agizo hili na mengine yenye kukataza uchochezi wa kidini, basi atakuwa adui wetu wa ndani na tushighulike nae ipasavyo.

   Asalamwalekum
   Bwana Asifiwe
   Wengine hamjambo
   Mungu Ibariki Tanzania

  12. Nyanko's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th July 2012
   Posts : 260
   Rep Power : 527
   Likes Received
   65
   Likes Given
   83

   Default Re: HOTUBA YA KIKWETE - jana

   Sioni kama kuna jipya, nilitarajia kama raisi kutolea maagizo na kuchukua action kwa baadhi ya masuala ambayo sasa yanaashiria hatari kwa usalama wa nchi.
   MIKATABA 16 - hakuna kitu as if mambo ni shwari.
   KUPOROMOKA GHOROFA - propaganda tupu labda tumpongeze kwa kutembelea wahanga.
   UDINI - hapo ndiyo failure kabisa, maana aliyoendelea kuyasema ni yale yale ya siku zote ambayo huongeza gap zaidi kati ya Dini hizi mbili.
   Ninachohofia sasa ni yale matamko ya wale wasaidizi wake yatakayofuata baada ya hotuba hii ndiyo yatakayochafua kabisa hali ya hewa (mfano Mzee Wasira n.k)

  13. kimalando's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 7th January 2011
   Posts : 103
   Rep Power : 0
   Likes Received
   10
   Likes Given
   31

   Default Re: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   Quote By sajo View Post
   Anajaribu kubalance ionekane wakirsto nao wana vurugu kwani wanawachukiza waislamu kwa kukojolea vitabu vyao vya dini(hoja ya kipuuzi).
   Kama kawaida yake kujaribu kubalance katika teuzi zake hata kama wanaoteuliwa sio wazuri. Hii sio vizuri ni kujidanganya wakati ukweli unajulikana!!

  14. adolay's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th December 2011
   Posts : 5,562
   Rep Power : 175909284
   Likes Received
   1937
   Likes Given
   1786

   Default Re: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 MACHI, 2013

   MONDAY, APRIL 01, 2013 MROKI   Rais Jakaya Mrisho Kikwete
   Ndugu Wananchi;
   Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na kunipa fursa ya kuzungumza nanyi kwa kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa kila mwisho wa mwezi. Leo ninayo mambo matatu ninayopenda kuzungumza nanyi.
   Ziara ya Rais wa China Nchini Tanzania
   Ndugu wananchi;
   Jambo la kwanza ni ziara ya Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China aliyoifanya nchini kwetu kati ya tarehe 24 na 25 Machi, 2013. Lengo la ziara yake ilikuwa kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya China na Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wakazi wa Dar es Salaam kwa kumpokea vizuri mgeni wetu na ujumbe wake. Wameondoka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu na watu wake.

   Kwa niaba yenu, nimepokea salamu za shukrani kutoka kwa Rais Xi Jinping akielezea kufurahishwa na mapokezi mazuri tuliyowapatia. Naomba tuendelee kuonesha moyo wa upendo na ukarimu kwa wageni wetu wengine mashuhuri watakaotutembelea siku za usoni.
   Ndugu wananchi;
   Nami pia, nimemshukuru sana Mheshimiwa Xi Jinping kwa kukubali mwaliko wangu na kufanya ziara ya kihistoria na yenye mafanikio makubwa kwa nchi yetu. Ameifanyia nchi yetu jambo la heshima kubwa na kumbukumbu isiyosahaulika. Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kuitembelea, tena siku kumi tu baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi yake. Na, kubwa zaidi ni kutumia fursa ya ziara yake hapa nchini kutangazia dunia Sera ya China kwa Afrika katika kipindi cha uongozi wake.
   Tumefarijika sana kusikia kuwa uhusiano na Afrika bado unapewa kipaumbele cha juu na viongozi wapya wa China. Pia, kuwa China itaendelea kukuza biashara na uwekezaji na kuongeza misaada ya maendeleo kwa Afrika ikiwemo kutoa nafasi 18,000 za mafunzo kwa vijana wa Kiafrika. Kama mtakumbuka nchi zetu mbili zilitiliana saini mikataka 16 ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali. Misaada ya maendekeo kwa maeneo yetu ya kipaumbele nayo imejumuishwa.

   Ndugu Wananchi;
   Rais Xi Jinping alielezea na kusisitiza dhamira yake na ya Serikali na Chama cha Kikomunisti cha China ya kudumisha na kukuza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na China. Kama mjuavyo uhusiano huo ulianzishwa mwaka 1964 na waasisi wa nchi zetu, yaani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania na Mwenyekiti Mao Zedong aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa China na Waziri Mkuu wake Chou En Lai.
   Rais wa China aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika medani ya kimataifa na kuchangia katika jitihada zetu za kujiletea maendeleo kwa kuongeza misaada ya maendeleo. Katika miaka 49 ya uhusiano na ushirikiano na China nchi yetu imepata misaada mingi ya maendeleo ikiwemo Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere ambao ulizinduliwa na Rais Xi Jinping wakati wa ziara yake.
   Ndugu wananchi;
   Kuna miradi kadhaa mikubwa inayoendelea kutekelezwa nchini, Bara na Zanzibar, kwa msaada wa Serikali ya China. Wakati wa ziara yake, Rais Xi Jinping iliahidi kuendelea kutusaidia miradi mingine ya maendeleo kama tulivyoomba wakati wa mazungumzo yetu licha ya ile ambayo ilitiwa saini siku ile.

   Ajali ya Kuporomoka Jengo la Ghorofa
   Jijini Dar es Salaam
   Ndugu Wananchi;
   Jambo la pili ninalotaka kuzungumzia ni ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa 16 lililokuwa linajengwa katika jiji la Dar es Salaam. Ajali hiyo iliyotokea juzi tarehe 29 Machi, 2013 imeleta msiba na simanzi kubwa nchini. Mpaka sasa maiti za ndugu zetu 30 zimepatikana. Watu17 waliweza kuokolewa, wanne kati yao bado wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Wengine walitibiwa na kuruhusiwa. Kazi ya kufukua eneo la ajali inaendelea na sasa inakaribia kufikia ukingoni.
   Ndugu Wananchi;
   Mimi na viongozi wenzangu tulipata nafasi ya kwenda kuangalia eneo la ajali. Hali niliyoiona pale imenihuzunisha sana. Lazima nikiri, hata hivyo, kwamba nimeridhishwa sana na juhudi kubwa za uokoaji zilizokuwa zinafanywa na wanajeshi wetu wakishirikiana na taasisi, mashirika binafsi na wananchi. Napenda kutumia nafasi kutoa shukrani maalum kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Saidi Meck Sadick kwa uongozi wake madhubuti. Pia nampongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ndugu Raymond Mushi, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Ndugu Suleiman Kova pamoja na Maafisa na askari wa JWTZ, na wale wote walioshiriki na wanaoendelea kushiriki katika juhudi za uokoaji.
   Nawapongeza pia madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hospitali nyinginezo kwa jitihada zao za kuokoa maisha ya waliojeruhiwa. Nawapa pole wale wote waliofiwa na wapendwa, ndugu na jamaa zao katika ajali hii. Nawaomba wawe na moyo wa subira huku sote tukiungana nao kuwaombea marehemu wetu wapate mapumziko mema peponi. Kwa waliojeruhiwa, tunawaombea wapone upesi.
   Ndugu Wananchi;
   Maneno mengi yanasemwa kuhusu chanzo cha ajali ile. Alimradi kila mtu ana dhana yake. Niliagiza vyombo na mamlaka husika wachukue hatua zipasazo kuchunguza sababu za ghorofa hilo kuanguka na watakaothibitika kusababisha maafa hayo wachukuliwe hatua zipasazo. Wa kushtakiwa Mahakamani washitakiwe na wa kufutiwa leseni za kufanya shughuli za ujenzi au taaluma zao wafutiwe bila ajizi. Jambo la msingi la kusisitiza ni kuwa mamlaka zinazohusika na usimamizi wa ujenzi lazima zitimize ipasavyo wajibu wake. Naamini kama mamlaka hizo zingetimiza ipasavyo wajibu wake ajali hii ingeepukika. Halmashauri za miji na wilaya zina wajibu maalum kwenye ujenzi katika maeneo yao. Watimize wajibu wao. Yaliyotokea Dar es Salaam yawe fundisho kwa wote.

   Ndugu Wananchi;
   Ni matumaini yangu kuwa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi na Bodi ya Usajili wa Wahandisi itakamilisha mapema uchunguzi wake ili ukweli ujulikane. Bodi ya Usajili wa Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi na Baraza la Taifa la Ujenzi nao washirikishwe kwa ukamilifu ili ukweli upatikane na hatua stahiki zichukuliwe. Pia naomba washauri namna bora ya kukomesha ajali za aina hiyo siku za usoni.

   Uhusiano wa Wakristo na Waislamu
   Ndugu Wananchi;
   Jambo la tatu ninalopenda kuzungumza nanyi leo ni uhusiano wa Waislamu na Wakristo nchini. Jambo hili nimeshalizungumzia mara kadhaa siku za nyuma, lakini nalazimika kulisemea tena kutokana na hali ilivyo sasa. Tumefikia mahali ambapo kama viongozi na waumini wa dini hizi kubwa mbili hawatakubali kubadili muelekeo wa sasa, tunakoelekea ni kubaya. Nchi yetu nzuri tutaivuruga na sifa yake ya miaka mingi ya Waislamu na Wakristo kuishi pamoja kidugu, kwa upendo, ushirikiano na kuvumiliana itatoweka. Tanzania itaacha kuwa kisiwa cha amani na kuingia katika orodha ya nchi zenye migogoro na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe.

   Ndugu Wananchi;
   Nyaraka na kauli kali kali zinazotolewa na viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu zinanishawishi kuamini haya niyasemayo. Nyaraka na kauli hizo zina mambo mawili makuu. Kwanza, kwamba kila upande unatuhumu, kushutumu na kulaumu upande mwingine kwa kufanya vitendo viovu dhidi ya dini yake. Kauli na mihadhara ya kudhalilisha dini za wengine, kunajisi vitabu vitakatifu, kuchoma moto nyumba za ibada, mzozo kuhusu nani achinje na kuuawa kwa viongozi wa dini ni baadhi ya mambo yanayotolewa mifano.
   Na, pili kwamba kila upande unailamu Serikali kwa kupendelea upande mwingine. Wakristo wanalaumu kwamba mihadhara ya kudhalilisha Ukristo inaendeshwa na Serikali haichukui hatua. Aidha, Wakristo wanateswa na viongozi wao kuuawa na Waislamu, lakini Serikali haichukui hatua. Kwa ajili hiyo wanadai kuwa Serikali imeshindwa kulinda uhai wa raia wake. Wanasema pia kwamba Serikali inapendelea upande wa Waislamu.

   Ndugu Wananchi;
   Waislamu nao wanadai kuwa kitabu chao kitakatifu, yaani Quran Tukufu, kinadhalilishwa kwa kuchanwa, kuchomwa moto na kukojolewa na Wakristo na Serikali haichukui hatua yo yote ya maana. Waislamu wananyanyaswa katika nchi yao, wanakamatwa ovyo, hawapewi fursa sawa na kwamba Serikali inawapendelea Wakristo. Wanasema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa Kikristo. Mimi binafsi wananishutumu kuwa napendelea kushiriki zaidi kwenye shughuli za Wakristo kuliko za Waislamu kama vile harambee za kujenga Makanisa na shule za Makanisa. Naambiwa kuwa mwepesi kushiriki maziko ya Maaskofu kuliko Masheikh wanapofariki. Ipo Misikiti mitatu hapa Dar es Salaam wamenisomea itikafu nife. Katika itikafu hiyo wamewajumuisha Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ndugu Suleiman Kova.
   Ndugu Wananchi;

   Napenda kuwahakikishia Watanzania wenzangu kuwa mimi na Serikali ninayoiongoza, hatupendelei upande wo wote. Hatufurahishwi na kitendo cha mtu kudhalilisha dini ya mwenzake ndiyo maana wapo wahadhiri wa dini ya Kiislamu na wahubiri wa dini ya Kikristo wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa nyakati mbalimbali. Vyombo vya usalama vinatambua wajibu wake huo na kama haifanyiki ni ulegevu wa mtu tu katika kutimiza wajibu wao na siyo kwamba ni sera na maelekezo yangu au ya Serikali. Mtakumbuka kuwa mara kadhaa nimewakumbusha Wakuu wa Mikoa na Wilaya na wakuu wa vyombo vya usalama kuacha ajizi katika kutimiza wajibu wao kwenye suala hili.

   Ndugu Wananchi;
   Mimi binafsi sibagui, hushiriki shughuli za Waislamu na Wakristo kila ninapoalikwa labda nikose nafasi kwa sababu nyinginezo. Nimeshafanya shughuli nyingi za Waislamu kama vile Maulid ya Mtume Muhamad S.A.W., safari za Hija, ujenzi wa misikiti na madrasa na mengineyo mengi. Nimeshashiriki mazishi ya Masheikh kama nifanyavyo kwa Maaskofu na watu mbalimbali Waislamu na Wakristo. Pale ambapo sikushiriki mazishi ya Sheikh au Askofu itakuwa ni kwa sababu ya kubanwa na shughuli nyingine ambazo lazima nifanye mimi, au taarifa ilikuwa ya muda mfupi. Kwa upande wa Waislamu desturi yetu ya kuzika mara mtu anapofariki huwa kikwazo kwangu kushiriki hasa ikiwa ni nje ya Dar es Salaam kwa sababu ya taratibu za kumsafirisha Rais kutoka mahali pamoja kwenda pengine siyo nyepesi. Wakristo hawana utaratibu huo, huwa wanaweza kusubiri hivyo huniwia rahisi kushiriki.

   Ndugu Wananchi;
   Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali yetu haijashindwa kulinda usalama wa raia wake au viongozi wa dini na nyumba za ibada. Kama ingekuwa hivyo, tungeshuhudia mauaji ya raia, viongozi wa dini na matukio ya kuchomwa nyumba za ibada yakiwa mengi hapa nchini. Lakini hivyo sivyo. Nawasihi sana ndugu zangu Wakristo na Waislamu kuwa tusiyachakulie matukio ya kuuawa kwa Mchungaji Mathayo Kachila kule Buseresere, Geita, na Padri Evaristus Mushi kule Zanzibar, au kumwagiwa tindikali Sheikh Fadhili Soroga, Naibu Mufti wa Zanizbar, kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda na kuchomwa moto kwa Makanisa Zanzibar na Mbagala, Dar es Salaam kuwa ni kielelezo na ushahidi wa Serikali kushindwa kutimiza wajibu wake.
   Kila tukio lina mazingira yake, hakuna ushahidi wa vyombo vya Serikali kuzembea. Hakuna ushahidi wa matukio hayo kuunganika. Mpaka sasa hatujapata ushahidi wa kuwepo kikundi cha Waislamu wanaopanga kuua viongozi wa Kikristo na kuchoma moto Makanisa hapa nchini.

   Ndugu Wananchi;
   Kifo cha Mchungaji Mathayo Kachila wa Buseresere ni matokeo ya vurugu zilizosababishwa na mzozo kati ya Wakristo na Waislamu kuhusu kama nyama iliyochinjwa na Wakristo Kanisani nayo iuzwe kwenye bucha iliyopo pale kijijini ambayo kwa mazoea huuzwa nyama iliyochinjwa na Waislamu. Katika ugomvi na vurumai hizo ndipo watu kadhaa wa pande zote walijeruhiwa na Mchungaji kupoteza maisha. Si tukio unaloweza kulihusisha na mengineyo nchini. Ni la pale pale Buseresere na limeanzishwa na kuhusisha Wakristo na Waislamu wa Buseresere kwa sababu zao.
   Hivi kama kusingekuwepo na mzozo wa nyama ile kuuzwa katika bucha ile kuumizana kule na mauaji yale yangetokea? Kabla ya mzozo ule Wakristo na Waislamu wa Buseresere hawakuwa na ugomvi baina yao. Walikuwa wanaishi kidugu na kushirikiana katika shughuli zao za kujitafutia riziki huku kila mmoja akimuabudu Mungu kwa misingi ya dini yake. Hivyo kutumia tukio hilo kutoa wito kwa Wakristo wote kuwa kuuawa kwa Mchungaji Kachila ni sawa na kuuawa kwa Wakristo wote nchini kulikofanywa na Waislamu ni kulikuza tatizo isivyostahili. Busara ituongoze kutafuta njia ya kuwapatanisha Wakristo na Waislamu wa Buseresere wazungumze, waelewane na waendelee kuishi pamoja kama ilivyokuwa awali. Hata mzozo wa kuchinja wanaweza kuumaliza. Mbona bucha za kitimoto zipo na watu hawajapigana. Kutumia mzozo wa Buseresere kueneza chuki kati ya Wakristo na Waislamu nchi nzima si sawa. Hatuwatendei haki Watanzania.

   Ndugu Wananchi;
   Kuuawa kwa Padri Evaristus Mushi wa Zanzibar ni tukio linalojitegemea halina uhusiano kabisa na lile la Buseresere, Geita. Hapakuwa na mzozo kuhusu nani achinje. Bado uchunguzi wake unaendelea na tumehusisha vyombo vya upelelezi vya nje vishirikiane na vyetu kufanya uchunguzi. Tumefanya hivyo kwa sababu ya ugumu uliopatikana katika uchunguzi wa matukio ya kabla yake. Yaani ile la kupigwa risasi na kujeruhiwa kwa Padri Ambrose Mkenda na kumwagiwa tindikali kwa Naibu Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhili Soroga. Bado hakuna mafanikio ya kutia moyo. Na bado tunajiuliza kama matukio hayo matatu yanahusiana. Je, Makanisa kuchomwa moto kule Zanzibar nako kuna uhusiano wowote na matukio yale matatu? Uchunguzi unaoendelea unaweza kufumbua fumbo hilo.
   Kuna watu wanadhani yanahusiana na kwa sababu nzuri. Lakini inabaki kuwa ni dhana ya kibinadamu mpaka ukweli halisi utakapobainika. Bado kazi ya uchunguzi inaendelea kufanywa na vyombo vya usalama vya nchi yetu wakishirikiana na wenzao wa nje. Katika mazingira hayo, ni mapema mno kumnyooshea kidole mtu ye yote na kuilaumu Serikali ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Serikali siyo mshirika katika mauaji hayo, na haina sababu ya kufanya hivyo. Ndiyo maana tunahangaika usiku na mchana kupata jawabu.

   Ndugu Wananchi;
   Hali kadhalika tukio la Makanisa ya Mbagala, Dar Es Salaam kuvamiwa, kubomolewa, mali kuibiwa na kuchomwa moto tarehe 12 Oktoba, 2012 nalo lina mazingira yake maalum. Chanzo chake ni mzozo uliotokana na tukio la kusikitisha la kijana mmoja Mkristo kukojolea Kitabu Kitakatifu cha Waislamu, yaani Quran Tukufu. Pamoja na maelezo kuwa walikuwa na ubishi wa kitoto na kijana mwenzake, lakini kitendo hicho kiliwakasirisha Waislamu. Kijana huyo alifikishwa kituo cha Polisi. Baadhi ya Waislamu wenye msimamo mkali walifika kituoni hapo wakidai wapewe huyo kijana wamuadhibu wao. Jeshi la Polisi lilikataa. Kukatokea mzozo kati ya waumini hao na Polisi na baada ya kushindwa walichokitaka baadhi yao walipotoka pale, wakaenda kufanya uhalifu wa kuvunja, kuiba na kuchoma moto Makanisa.

   Ndugu Wananchi;
   Baada ya tukio la Mbagala hapajakuwepo na tukio la kuchomwa Kanisa mahali popote kwa upande wa Bara. Aidha, hapajawahi kuwepo tishio lililothibitika la watu kutaka kuchoma Kanisa popote. Lakini maneno ya vitisho vya kuchoma Makanisa yako mengi hasa kupitia mitandao ya simu za mkononi. Kila ujumbe wa namna hiyo ulipofikishwa kwenye vyombo vya usalama uchunguzi umefanywa na hata hatua za tahadhari kuchukuliwa lakini hakuna hata taarifa moja iliyothibitika kuwa na chembe ya ukweli. Hata dalili hazijakuwepo.
   Tulichojifunza ni kuwa ujumbe na vitisho vya aina mbalimbali hupelekwa kote, kwa Wakristo na Waislamu. Upo unaowalenga Wakristo ukiwaambia wenzao Waislamu wanapanga kuwadhuru. Na upo wanaopelekewa Waislamu wakiambiwa Wakristo wanao mipango mibaya dhidi yao. Watanzania wenzangu nawaomba mtanabahi na mjue kuwa wapo watu wanacheza mchezo mchafu wa kuwagonganisha na kutaka kuwagombanisha Wakristo na Waislamu kwa sababu wanazozijua wao na kwa faida yao. Wanapandikiza chuki kwa lengo la kutaka Wakristo na Waislamu wagombane. Wanapandikiza chuki baina ya Serikali na waumini wa dini zetu kuu mbili ili ionekane Serikali imewatelekeza raia wake. Ni mchezo mbaya, tusikubali kucheza ngoma tusiyoijua. Hivi ndugu zangu mmekaa chini na kujiuliza kumetokea nini kipya hata leo kuwa na mhemko kama huu kati ya Wakristo na Waislamu na kutishia kuleta vita baina nchini kote?

   Ndugu Wananchi;
   Serikali haijapuuzia kila palipotokea matukio ya uhalifu. Watu 76wanaotuhumiwa kuharibu na kuchoma moto Makanisa kule Mbagala na kufanya fujo kituo cha Polisi wamekamatwa na kesi zao zinaendelea Mahakamani. Kwa upande wa tukio la Buseresere lililosababisha kifo cha Mchungaji Mathayo Kachila, watu 17, wakiwemo waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu walikamatwa na kesi zao zinaendelea. Wapo walioshitakiwa kwa mauaji na wapo walioshitakiwa kwa kufanya vurugu. Jeshi la Polisi bado linawatafuta watu wengine waliohusika na uhalifu huo ili na wao wakamatwe. Kwa upande wa Zanzibar, watu 10wanaotuhumiwa kuchoma Makanisa wamekamatwa na kesi zao zinaendelea. Bado hajakamatwa mtu kwa tukio la mwisho la kuchoma Kanisa baada ya kuuawa Padri Evaristus Mushi. Uchunguzi unaendelea.

   Ndugu Wananchi;
   Kwa upande wa kujeruhiwa kwa Padre Mkenda, bado uchunguzi haujakamilika pamoja na kuwapo taarifa kadhaa zinazoendelea kufanyiwa kazi. Kuhusu uchunguzi wa mauaji ya Padre Mushi, baada ya jitihada kubwa kufanyika ikiwa ni pamoja na kushirikisha nchi zilizobobea katika uchunguzi wa makosa ya aina hii, hatua ya kutia moyo imefikiwa. Mtu mmoja amekamatwa na wengine wanaendelea kutafutwa.

   Ndugu Wananchi;
   Kwa upande wa kanda na vituo vya redio nako pia Serikali imechukua hatua. Watu kadhaa wamekamatwa na kufikishwa Mahakamani katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kurekodi na kusambaza kanda zinazochochea chuki na vurugu za kidini. Wapo Waislamu na Wakristo. Wapo watu wengine ambao wanaendelea kutafutwa. Zipo taarifa kuwa baadhi yao wamekimbilia nchi za nje. Jeshi la Polisi limeomba msaada wa Polisi wa Kimataifa, yaani Interpol, kusaidia kuwatafuta na kuwarejesha nchini. Vituo viwili vya radio yaani Kwa Neema FM cha Sengereme na Radio Imani cha Morogoro vimefungiwa kwa muda wa miezi sita. Baada ya muda huo kupita, Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano itaamua ipasavyo.

   Ndugu Wananchi;
   Nimeyaeleza haya kwa kirefu kuwahakikishia kuwa Serikali inajali usalama wa raia wake wa mali zao na amani na utulivu wa nchi yetu. Kamwe hatujashindwa kulinda raia wa nchi wa yetu na yapo mambo mengi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika kuhakikisha kuwa Watanzania wa dini zote, makabila yote, rangi zote na mahali po pote walipo wako salama. Tunataka kuona watu wanaendelea kuishi kwa amani, upendo, ushirikiano na mshikamano kama tulivyokuwa tunaishi siku zote. Tunapenda kuona Watanzania wanaepuka mambo yanayowabagua na kusisitiza yale yanayowaunganisha. Tujiepushe kuyapa kipaumbele yale yanayotugawa.

   Ndugu Wananchi;
   Athari za mzozo kuhusu kuchinja kule Geita iwe fundisho kwetu sote. Tuazimie sote kuwa yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Hebu tufikirie maisha yetu Watanzania yatakuwaje kwenye shughuli za kijamii kama vile sherehe, harusi, ngoma na misiba iwapo tutaanza kuwa na chakula tofauti kwa Waislamu na Wakristo. Fikiria itakuwaje kwenye hospitali, shule na vyuo pawe na majiko mawili au labda hata mabwalo mawili ya chakula kwa Waislamu na Wakristo. Jeshini nako kuwe na majiko na mabwalo ya Waislamu na Wakristo. Hali iwe hivyo hivyo kwenye migahawa na maeneo mengine yenye huduma ya chakula.
   Ndugu zangu, tunataka kuipeleka wapi nchi yetu? Tunataka kujenga nchi ya namna gani? Mimi naamini tukifanya hivyo huo utakuwa ndiyo mwanzo wa kubaguana kwa kila kitu na kila jambo na kuligawa taifa kwa namna ambayo hatutakuwa wamoja tena. Huko tunakoelekea siko, ni kubaya. Tubadilike, na wakati ni huu. Viongozi wa dini waongoze njia wawaepushe waumini wao na taifa letu na janga hili.

   Ndugu Wananchi;
   Bado narudia kusisitiza umuhimu wa viongozi wa dini zetu kubwa mbili kukutana na kuizungumzia hali hii na kuipatia ufumbuzi. Ni wao kuliko mtu mwingine ye yote wenye majawabu ya matatizo haya. Ni masuala yanayohusu imani za dini na yanafanywa na viongozi wa dini na wafuasi wao kwa jina la dini zao. Serikali ina wajibu wa kulinda amani. Kazi yetu itakuwa rahisi kama waumini hawatafanya vitendo vitakavyosababisha uvunjifu wa amani. Wa kuongoza waumini lipi jema na lipi baya ni viongozi wa dini.

   Ndugu Wananchi;
   Nimeshakutana na viongozi kadhaa wa madhehebu na taasisi za dini za Kikristo na Kiislamu kuzungumza nao kuhusu jambo hilo. Nimepata faraja kuona kuwa wote wanasikitishwa na mambo yanayotokea hivi sasa na wameona busara ya viongozi wa dini kuzungumza ili kuondoa tofauti zilizojitokeza. Wanakiri kuwa hali ilivyo sasa siyo ya kawaida kwa Tanzania na Watanzania. Kuna upepo mbaya wa shetani unapita ambao viongozi wa dini wana wajibu wa kuhakikisha kuwa hali ya hewa inasafishwa na kurejesha nchi yetu na watu wake katika maisha tuliyoyazoea. Maisha ambayo waumini wa dini tofauti wanaishi pamoja kwa udugu, upendo, ushirikiano na mshikamano kwa misingi ya ubinadamu wao na Utanzania wao.
   Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, ameshaeleza dhamira ya Serikali ya kuitisha mkutano wa viongozi wa dini mapema mwezi ujao. Ni matumaini yangu kuwa wote watashiriki wenyewe bila ya kutuma wawakilishi. Lazima tupate jawabu kwa maslahi ya taifa letu na watu wake.

   Ndugu Wananchi;
   Kabla ya kumaliza hotuba yangu napenda kutumia nafasi hii kuwaomba na kuwasihi waandishi wa habari wasaidie kuliepusha taifa letu kuingia katika vita vya kidini. Waache kushabikia taarifa zinazochochea na kujenga uhasama baina ya waumini wa dini zetu. Nawaomba wapime athari za taarifa zao kabla ya kuziandika au kuzitangaza. Wawe makini na maneno wanayotumia. Katika hali tuliyonayo sasa lazima sote tuazimie kuondoa tofauti za kidini na kujenga umoja miongoni mwa Watanzania wa dini zote. Wasipofanya hivyo, wataliingiza taifa katika mgogoro mkubwa ambao hauna msingi kama ilivyotokea katika nchi jirani. Nawaomba wamiliki wa vyombo vya habari kutambua kuwa wanao wajibu wa kuhakikisha vyombo vyao havitumiki kuleta mifarakano kwa kuchochea uhasama baina ya Wakristo na Waislamu.

   Hitimisho
   Ndugu Wananchi;
   Naomba kumaliza kuwa kusisitiza kuwa wananchi wote kudumisha umoja na mshikamano wetu. Tuishi kwa upendo, umoja, mshikamano na ushirikiano bila kujali tofauti ya dini zetu, kabila, rangi au mahali atokako mtu. Hizo ndizo tunu za taifa letu la Tanzania ambazo hatuna budi kuzienzi, kuzilinda na kuzidumisha. Narudia kuwahakikishia kuwa Serikali haipendelei dini yo yote na wala haina mpango wa kushiriki kuangamiza dini yo yote au waumini wao. Serikali kupitia vyombo vyake vya usalama itaendelea kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia wake na mali zao kama inavyofanya siku zote. Kama kuna mtu anaona kuwa maisha yake au mali zake zipo hatarini, aende kutoa taarifa Polisi. Hatua zipasazo zitachukuliwa.

   Ndugu Wananchi;
   Mwisho nawatakia sikukuu njema ya Pasaka. Tusherehekee kwa amani na utulivu. Tusherehekee pamoja.
   Mungu Ibariki Afrika!
   Mungu Ibariki Tanzania!
   Asanteni kwa Kunisikiliza

  15. adolay's Avatar

   Nasikitika nimeipata hotuba hii lakini sikuiweka vizuri hasa picha ya Rais haipo na maelezo ya kwanza kwanza

   hayajakaa sawa
   . lakini ndiyo hotuba iliyotolewa asubuhi leo TBC1

   Naomba radhi wanajanvi kwa usumbufu huo hapo mwanzoni

  16. PACHOTO's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th December 2011
   Posts : 607
   Rep Power : 590
   Likes Received
   153
   Likes Given
   119

   Default Re: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   Quote By adolay View Post

   safi sana JK, ujmewaambia ukweli kama watachinja basi wale wenyewe na co kuleta kwenye public

  17. BAK's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th February 2007
   Location : Mfaranyaki
   Posts : 43,970
   Rep Power : 429505982
   Likes Received
   26189
   Likes Given
   28962

   Default Re: HOTUBA YA KIKWETE - jana

   Janga la Taifa
   Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

  18. Mu-sir's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th October 2010
   Posts : 3,107
   Rep Power : 10430
   Likes Received
   1053
   Likes Given
   1061

   Default Re: HOTUBA YA KIKWETE - jana

   Hivi kweli tuna Rais Tanzania au tunaongozwa na mazoea
   your I can is more important than you I.Q

  19. Manager's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st April 2011
   Posts : 522
   Rep Power : 645
   Likes Received
   69
   Likes Given
   401

   Default Re: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   Quote By genekai View Post
   Ndo maana inakuwa rahisi kwenu kuvaa mabomu na kujilipua kwa kuwa hamjui hata mnacho kiamini. Hivi Qur an umeisoma kweli na kuielewa kweli? nenda kwenye Qur an toleo la The Islamic foundation 2006 na soma tafsir(footnotes) ya Sura tul Mayyda 5 (Qur 5:5) uone ni kina nani wanaruhusiwa kuchinja. Ndo maana huwa nasema kuwa bila kuinvest kwenye elimu, itakuwa rahisi kwa mtu kumiliki rocket ranger yenye thamani ya 2000 U$d wakati miguuni yuko peku hadi msalani. Au just to wipe your butt with fingers as a sign of purity and considering bacon unclean, or being ready to wear grenades just to commit suicide in order for you to have 72 virgins in heaven but we call that "hell". Katika madhehebu yenu, ni moja tu ambalo its followers can reason out nalo ni Ahmadiyya. Nikikosa BAN leo siipati tena, Mods, i was only quoting!!!!
   Je wanawake wanapata 72 husbands??? Kama sivyo huu ni ubaguzi!
   "Sometimes a majority simply means that all the fools are on the same side!"

  20. isotope's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th April 2012
   Posts : 2,408
   Rep Power : 972
   Likes Received
   794
   Likes Given
   622

   Default Re: HOTUBA YA KIKWETE - jana

   Alikuwa anamjibu Kard. Pengo, eti serikali haijashindwa kuwalinda wananchi wake. Akasahau kuwa taifa liko kwenye msiba wa kuporomoka kwa jengo uliosababishwa na udhaifu serikali yake.

  21. Ndibalema's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th April 2008
   Location : Mbagala
   Posts : 10,890
   Rep Power : 291617815
   Likes Received
   4218
   Likes Given
   3898

   Default Re: Live on TBC1: Hotuba ya Rais mwisho wa mwezi Machi 2013

   Mods. enough is enough.
   Naomba hii topic ifungwe. nimeshabofya 'report abuse'
   "Makalio ya sufuria hayaogopi moto"

  Page 14 of 18 FirstFirst ... 41213141516 ... LastLast

  Tags for this Topic

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...