Haha, atakuwa mkuu wa usalama wa taifa? Kwani Lwakatare ni usalama wa taifa? Kwa hiyo atapanda cheo hadi kwenda kuwa mkuu wa usalama wa taifa? Kama huyu ni usalama wa taifa basi ni mfanyakazi wa Ikulu, maana usalama wa taifa wanafanya kazi ya Ikulu.
Na kwa kuzingatia kwamba amekubali hadi kurekodiwa video wakati anaongea hayo, basi ni dhahiri kwamba hii video na yenyewe imetengenezwa kwa makusudi kama sehemu ya propaganda ya kuimaliza CHADEMA. Huyu Lwakatare alikuwa CUF, hatujui ni kwanini aliondoka huko, labda ni baada ya kufanikisha mikakati ya kukiua. Na sasa ameletwa kuja kutengeneza skendo ndani ya CHADEMA ili mupate nafasi ya kukipaka matope!
So far kwa kuwa umesema huyu ni usalama wa taifa, basi nina uhakika kesho tu atakuwa keshatimuliwa CHADEMA arudi huko Ikulu kwenu. Sina uhakika kama haya anayoongea Lwakatare yanakiwakilisha CHADEMA. Nina uhakika mikakati mikubwa kama hiyo lazima ingeshirikisha viongozi wakubwa na si huyu jamaa peke yake.
Na kwa sasa
Independent Voter umenifumbua macho kwamba huyu ni usalama wa taifa, na hivyo anahusiana na Ikulu. So mipango yote hii ni dhahiri imeratibiwa na Ikulu kama sehemu ya kuimaliza CHADEMA. Na ni wazi kwamba mmemtoa Kibanda kama mbuzi wa kafara.
Topic closed! Hakuna cha kuendelea kujadili so far, kama Lwakatare ni usalama wa Taifa.
Follow Us Here