JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

  Report Post
  Page 4 of 9 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
  Results 61 to 80 of 171
  1. Manyerere Jackton's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th December 2012
   Posts : 2,104
   Rep Power : 11778959
   Likes Received
   3498
   Likes Given
   797

   Default Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   Taarifa kutoka South Africa, kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania

   1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.

   2. Upasuaji huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa taya lake la kushoto.

   3. Kuhusu jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.

   4. Wakati akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama aliyofayiwa.

   5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.

   Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.

   --

   Neville C. Meena,
   Secretary General,
   Tanzania Editors Forum - TEF,
   Dar es Salaam - Tanzania.
   Cell: +255 - 787 - 675555
   +255 - 753 - 555556

   ============
   UP DATE
   ============

   Quote By Manyerere Jackton View Post
   Wapendwa, habari za uhakika zilizofika sasa hivi kutoka hospitalini Afrika Kusini alikolazwa Kibanda ni kwamba ameshatolewa jicho moja ambalo liliharibiwa kabisa na wavamizi. Tayari ameshatoka Theater.Tutaendelea kujuzana.
  2. utaifakwanza's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st February 2013
   Posts : 12,082
   Rep Power : 28564
   Likes Received
   921
   Likes Given
   938

   Default

   Quote By Josephine View Post
   Mzee wa usafi,nakuunga mkono.
   sipendi watu wanafiki.
   Huyu kijana alinikera sana siku ya ulimboka.
   wewe mwenyewe huaminiki

  3. Raimundo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd May 2009
   Posts : 5,411
   Rep Power : 132849542
   Likes Received
   1324
   Likes Given
   1084

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   BTW wale FBI si bado wako nchini? Tuwape hii kazi au?

  4. Mzawa Halisi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th February 2009
   Posts : 484
   Rep Power : 749
   Likes Received
   149
   Likes Given
   356

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   Quote By utaifakwanza View Post
   Pole sana kibanda. Namshukuru rais kikwete kwa kukujulia hali, huo ndio uungwana
   Naamini raisi kwa nafasi yake anatakiwa afanye zaidi ya kumtembelea hospitali.

   Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

  5. marejesho's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th January 2011
   Location : MULA
   Posts : 5,457
   Rep Power : 1027527
   Likes Received
   2670
   Likes Given
   1327

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   Pole sana Kibanda.

  6. Bangoo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th November 2011
   Posts : 5,592
   Rep Power : 6492
   Likes Received
   985
   Likes Given
   0

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   Mpaka 2015 mtaona mengi sana, ni mbinu za kuzima kama walivyozima analogia! Mtaona mengi sana
   serikali inahusika na unyama huo kwa % zote..


  7. Kibanga Ampiga Mkoloni's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th August 2007
   Location : Here! here!
   Posts : 11,918
   Rep Power : 176097909
   Likes Received
   3880
   Likes Given
   2565

   Default

   Quote By Manyerere Jackton View Post
   Wapendwa, habari za uhakika zilizofika sasa hivi kutoka hospitalini Afrika Kusini alikolazwa Kibanda ni kwamba ameshatolewa jicho moja ambalo liliharibiwa kabisa na wavamizi. Tayari ameshatoka Theater.Tutaendelea kujuzana.
   So Sad Hujafa hujaumbika, Mungu ampe uzima arudi kazini na naamini atarudi kwa nguvu zaidi kama alivyokuwa kubenea baada ya kuvamiwa, Na wabaya wake kwa vyovyote wakae mkao wa kula.

  8. The Invincible's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th May 2006
   Location : Online
   Posts : 3,216
   Rep Power : 1443
   Likes Received
   487
   Likes Given
   1

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   Pole sana Kibanda!

   Ila mh! Alijiiingiza katika vita asiyoijua?
   Jiunge na timu ya kuondoa CCM madarakani

  9. Ronal Reagan's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th November 2010
   Posts : 3,507
   Rep Power : 1266
   Likes Received
   954
   Likes Given
   419

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   Very sad. Please get well soonest wishes Mr. Kibanda.

  10. Kokolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th March 2008
   Posts : 377
   Rep Power : 781
   Likes Received
   72
   Likes Given
   4

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   NAMUOGOPA ABDURAHMAN KINANA

   Na Absalom Kibanda

   Kwa mara nyingine tena, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeandika historia mpya baada ya kufanya mabadiliko mazito katika safu yake ya uongozi wa kitaifa.

   Ni mabadiliko mazito si kwa sababu tu yamefanywa na CCM ambayo imekuwa na rekodi ya kubadili sura za watendaji wake kwa namna na kwa njia tofauti, bali kutokana na ukweli kwamba safari hii mabadiliko hayo yamehusisha watu wazito, wenye historia ya kipekee katika medani ya uongozi ndani na nje ya chama hicho.

   Ingawa kwa mtazamo wa haraka haraka, mabadiliko hayo yanaweza yakaonekana kuwa ni ya kuyabeza au kuyapuuza kama ilivyotamkwa na baadhi ya wadadisi wa mambo wakiwamo wachambuzi wa masuala ya siasa na hata wanazuoni, ukweli unabaki pale pale kwamba kile kilichofanywa na CCM kinaweka alama ya kipekee katika mwenendo wa siasa za kitaifa za siku zijazo.

   Wasifu mzito na historia za kutukuka za baadhi ya wateule wanaounda timu ‘mpya’ ya viongozi watendaji wa CCM kwa kiwango kikubwa ndicho kitu kikubwa pekee kinachosababisha mtu yeyote makini ajikute akipata shida kuyabeza yale yaliyofanywa na chama hicho tawala mwishoni mwa wiki kule Dodoma.

   Msuko mpya wa safu ya wakuu wa idara za CCM uliotangazwa na Rais Jakaya Kikwete ukiwajumuisha wanasiasa wasiojua mizaha wawapo kazini kama alivyo Philip Mangula, au makada wa muda mrefu wa chama hicho wa kariba ya Muhammad Seif Khatib na Zakia Meghji una kila sababu ya kutafutiwa dawa mahususi na makamanda wa kambi ya upinzani ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipambana kuing’oa CCM madarakani.

   Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

   Kwa muktadha wa makala ya leo na kwa kuzingatia nafasi kuu ya utendaji aliyopewa, nitazungumzia kwa sehemu tu wasifu wa Kinana, mtu ambaye naamini anapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu na wakati mwingine kudhibitiwa ili kasi yake ya kukijenga chama alichopewa dhamana ya kukinusuru isije ikasababisha kuyumba kama si mauti ya kisiasa kwa baadhi ya vyama vya upinzani.

   Ni wazi kwamba, kuteuliwa kwa Kinana kuwa Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa, akirithi mikoba iliyomshinda, Wilson Mukama, kumetutia ganzi baadhi yetu ambao kwa muda mrefu tumekuwa ‘mashabiki’ au waumini wa kuchagiza kwa njia ya kalamu na wakati mwingine katika mijadala ya wazi kwamba, taifa lilikuwa na haja ya kutafuta mabadiliko ya uongozi kutoka nje ya chama tawala.

   Sitaki kuwa miongoni mwa wapenda mabadiliko ambao kwa njia za kujifariji au za kujipa matumaini hewa wameingia katika mkumbo wa jumla jumla wa kumbeza Kinana kwa namna wanayotaka kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba, mtu huyo anaweza akasukumwa kirahisi kwa namna ile ile ilivyopata kuwa kwa watangulizi wake kadhaa waliopata kushika wadhifa huo.

   Hupaswi kuwa na akili nyingi kutambua kwamba, umahututi wa CCM kisiasa, kulikokifikisha chama hicho tawala kufikia hatua ya kupoteza dira na kuanza kuliona kaburi la kupoteza madaraka ya dola ndiko kulikorejesha hekima za usikivu kichwani mwa Kikwete hata akalazimika kuwarejesha akina Kinana, Mangula, Seif Khatib na Meghji katika kilinge cha siasa za ushindani mkali ndani na nje ya CCM.

   Siyo siri hata kidogo kwamba, hekima hii mpya ya Kikwete ya kumrejesha Kinana ulingoni, ambaye siku chache tu zilizopita alitangaza kustaafu siasa huku akisema alikuwa akikusudia kuwaachia vijana kusukuma gurudumu la uongozi, inahusisha kichwa zaidi ya kimoja kutoka ndani na nje ya CCM.

   Kama ilivyo kwa wengi wengine nilianza kulisikia jina la Kinana likihusishwa na ukatibu mkuu wa CCM miaka miwili au mitatu iliyopita hali ambayo ilipata kusababisha nifikie uamuzi hata wa kumuuliza yeye mwenyewe kuhusu taarifa hizo.

   Jibu ambalo Kinana mwenyewe alipata kunipa kwamba alikuwa akipenda kuona akiendelea kupata fursa ya kukitumikia chama chake kama mshauri na kwa nyakati mahususi kama zile za kampeni na si kwa nafasi ya ukatibu mkuu lilikuwa likinipa sana faraja.

   Kilichokuwa kikinipa faraja si kingine chochote bali fikra zangu (sahihi au potofu) ambazo siku zote zilikuwa zikinifanya niamini kwamba, ukatibu mkuu kwa Kinana ilikuwa ni silaha moja ya maangamizi kwa vyama vya upinzani ambavyo naamini vinapaswa kuendelea kupewa fursa ya kuaminiwa na kukomaa.

   Katika mazingira ambayo CCM imeweza kuepuka zahama ya kumeguka vipande viwili kwa kuzingatia maono aliyokuwa nayo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwangu mimi Kinana wa zama hizo alikuwa na anaendelea kubakia kuwa tishio kubwa kwa ustawi wa upinzani ambao ni rutuba muhimu kwa maendeleo ya demokrasia na misingi ya utawala bora.

   Hili ndilo ambalo naamini wapinzani wanapaswa kulitazama na kulitafakari nyakati hizi wanapoendesha harakati zao za kukabiliana na maguvu ya dola na haya mapya ya hoja ambazo aghalab zitaongozwa na Kinana nyakati hizi taifa linapojiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa miaka mitatu ijayo.

   Haitoshi kwa kina Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Dk. Willibrod Slaa na Zitto Kabwe kumbeza Kinana na timu ya watendaji wake eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.

   Wapinzani na wachambuzi wa mambo wanapaswa kujua na kutambua kwamba, Kinana ni mwanasiasa wa vitendo, msomaji mzuri wa vitabu, ripoti, taarifa, magazeti, msikilizaji na msikivu mzuri wa mambo mepesi na mazito kuliko alivyokuwa ‘utopia’ Mukama anayeamini na kuzitetea nadharia zisizotekelezeka.

   Si hilo tu, wapinzani wanapaswa kutambua kwamba, historia yake ya uaskari alioutumikia miaka 20 hadi mwaka 1972 akifikia cheo halisi cha jeshi cha Kanali ikimhusisha na mafunzo mahususi ya kimkakati ni sehemu ya mambo ambayo yanatawala nidhamu ya kazi ya aina ya kipekee iliyomfanya Kinana akawa jemedari wa mapambano ya CCM tangu mwaka 1995 hadi leo.

   Wachambuzi wa mambo, nikiwamo mimi mwenyewe ambao siku zote tumekuwa tukiiona CCM kuwa chama kinachokufa kwa maana ya kuchungulia kaburi, tunapaswa kuanza kutafakari upya mawazo yetu hayo, nyakati hizi Kinana alipopewa dhamana ya kuwa mtendaji wake mkuu.

   Tutakuwa wendawazimu iwapo tutamlinganisha Kinana na Mukama na kusahau kwamba huyu aliye kilingeni leo ndiye aliyemuongoza Benjamin Mkapa katika mapambano makali ya kisiasa mwaka 1995, zama Augustine Mrema alipokuwa tishio la kwanza la kweli dhidi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu.

   Alikuwa ni Kinana aliyefanya kazi kubwa katika kipindi chote cha kampeni akiratibu na kuongoza kampeni zote za Mkapa zilizomjumuisha pia Mwalimu Nyerere katika mazingira ambayo wengi walikuwa wakiamini CCM ilikuwa katika mwelekeo wa anguko la kihistoria.

   Kinana ambaye kabla ya mwaka 1995 alikuwa tayari amepata kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi alitumia vyema mbinu za medani na zile za kidemokrasia na kiplomasia kumjengea uhalali Mkapa ambaye wakati huo alikuwa mwanasiasa ambaye hakuwa akijulikana sana.

   Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, siku chache tu baada ya kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza mwaka 1995, kwa sababu ama ya ulevi wa madaraka au kwa kutingwa na kazi za kimamlaka, Mkapa alisahau kazi kubwa aliyofanyiwa na Kinana.

   Ni katika kipindi hicho cha kati ya mwaka 1995 na 2000 ndipo nilipokutana kwa mara ya kwanza na mara kadhaa na Kinana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam nikiwa nimeongozana na mhariri wangu, Muhingo Rweyemamu, ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni ambako nilipata fursa ya kumsikiliza na kuufahamu upeo mkubwa wa kuona mambo aliokuwa nao mwanasiasa huyo.

   Tangu wakati huo hadi wakati wa kampeni za mwisho za mwaka 2010, niliendelea kukutana kwa nyakati fupi fupi na Kinana na mara kadhaa nikawa mtu wa kufuatilia na kuzisikiliza kwa makini, habari zake kutoka ama kwa marafiki au maadui zake wa kisiasa.

   Sikushangazwa hata kidogo niliposikia tena kwamba, Mkapa alilazimika kumuangukia tena Kinana na kumuomba aongoze tena kampeni zake mwaka 2000 kabla ya Kikwete naye hajafanya kile alichofanya mtangulizi wake alipomuomba mwanasiasa huyo adhibiti joto la kiti cha urais mwaka 2010.

   Uwezo wake mkubwa wa kisiasa, umakini wake na upeo mkubwa alionao katika kuona na kuchambua masuala ya siasa, uchumi na jamii ndivyo vitu ambavyo kwanza kwa nyakati tofauti vimepata kumfanya Kinana awe Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa miaka 10, Mbunge wa Afrika Mashariki na Spika wa Bunge hilo.

   Si ajabu hata kidogo kwamba, hata kabla ya kufikia huko, ni Kinana huyo huyo ambaye alipata kuwa Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Rais wa Tanzania katika eneo la Maziwa Makuu na kabla ya hapo akiwa Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) zama akiwa Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa Rais Ali Hassan Mwinyi.

   Uzoefu wake katika siasa za kiraia unaanzia mwaka 1972 wakati alipostaafu jeshi akiwa Kanali baada ya kulitumikia kwa miaka 20 ndiyo ambao amekuwa akiutumia kama silaha kubwa ya kukijua chama chake na pengine kumfanya awe mmoja kati ya watu wachache ambao wamepata kuwafanyia kazi marais wote wane wa Tanzania.

   Anarithi mikoba ya Mukama akiwa mmoja wa wanasiasa wachache wa CCM wa rika ile ile la kina Kikwete ambaye alilikimbia na kulikana kundi la mtandao mwaka 2005 ambalo baadhi yetu tunaamini kuwa, ndilo lilisababisha kuzaliwa kwa siasa mpya za kupakana matope, kuzushiana na kuhujumiana ndani na nje ya CCM.

   Lakini pengine kubwa katika yote hayo anaingia madarakani huku akiwa na hazina ya uzoefu mkubwa wa kuongoza mapambano dhidi ya vyama vya upinzani na kushinda katika mazingira ambayo aghalab yamekuwa yakiacha vidonda visivyopona kwa wapinzani tangu mwaka 1995. Huyu si mtu wa kumpuuza au kumbeza hata kidogo.[


   5. Jana Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa mahakamani.

   Neville C. Meena,
   Secretary General,
   Tanzania Editors Forum - TEF,
   Dar es Salaam - Tanzania.
   Cell: +255 - 787 - 675555
   +255 - 753 - 555556

   ============
   UP DATE
   ============

   [/QUOTE]

  11. Kibanga Ampiga Mkoloni's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th August 2007
   Location : Here! here!
   Posts : 11,918
   Rep Power : 176097909
   Likes Received
   3880
   Likes Given
   2565

   Default

   Quote By utaifakwanza View Post
   Pole sana kibanda. Namshukuru rais kikwete kwa kukujulia hali, huo ndio uungwana
   Hivi ni kipo bora , angehakikisha watuhumiwa wanakamatwa au kwenda kumjulia hali?

  12. Kibanga Ampiga Mkoloni's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th August 2007
   Location : Here! here!
   Posts : 11,918
   Rep Power : 176097909
   Likes Received
   3880
   Likes Given
   2565

   Default

   Quote By utaifakwanza View Post
   Rais kikwete tuna imani na wewe, tunakuomba ukomeshe vitendo hivi vya kinyama.
   Hahaaa! Pole sana!

  13. Molemo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2010
   Posts : 13,190
   Rep Power : 146133716
   Likes Received
   8483
   Likes Given
   618

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   Hii habari imenisikitisha sana.Mungu amponye Kibanda.

  14. Lukolo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd December 2009
   Location : Iringa
   Posts : 5,122
   Rep Power : 86242795
   Likes Received
   3038
   Likes Given
   2058

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   JK hatutaki tu wasakwe, tunataka vitendo hivi vya kihuni vikomeshwe nchini? Hivi wewe unasikia fahari gani kuongoza nchi ambayo watu wanatekwa, wanapigwa risasi na hata kuteswa bila ya vyombo vya dola kujua? Wewe usalama wako unaamini upo wapi, kama usalama wa watu unaowaongoza ni ziro? JK, kama utaendeleza porojo zako kama ulivyozoea, the next person kutekwa, kuteswa na kuuawa utakuwa wewe.
   Kama mtu alikuwa waziri au hata mkuu wa mkoa katika serikali ya Kikwete, hafai kuwa Rais wa Tanzania. Kimsingi mtu huyo ni sehemu ya uongozi mbovu na wa hovyo ulioliingiza taifa letu katika umaskini mkubwa na mdororo wa uchumi tulionao sasa. Kama mtu huyu alijua namna ya kuiokoa nchi na hakufanya hivyo, ina maana alitusaliti watanzania na hafai kuwa Rais wa nchi. Kama hakujua ni nini cha kumshauri Kikwete ili Mambo yaende sawa, ina maana hana analolijua. Je anataka awe Rais ili afanye nini ilihali hakuna alijualo?

  15. mtolewa's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 18th January 2011
   Posts : 189
   Rep Power : 592
   Likes Received
   48
   Likes Given
   9

   Default Re: Kibanda atolewa jicho moja!!!

   Quote By Manyerere Jackton View Post
   Jaribu kuweka bayana hii sentesi! Sijaambua kitu! Nini kitatokea?
   sijui bayana nini kitatokea ila Yehova amenionyesha watu wenye maandishi yaliyoandikwa kwa damu Walazendo wa nchi
   wakishangilia na kutoa shukrani kwa Mungu na nilipotazama ilikuwa majira ya joto.
   NOT YET UHURU, KWA HIYO ALLUTA CONTINUA!

  16. Rugaijamu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th July 2010
   Location : Barazani kwangu.
   Posts : 2,409
   Rep Power : 8202801
   Likes Received
   557
   Likes Given
   331

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   Mbona kimya mpaka leo hii, hakuna hata taarifa inayoelezea kukamatwa watu waliohusika na unyama huu kulikoni?
   Alipouwawa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza hata wiki haikupita tayari watuhumiwa walishakamatwa, hili vipi?Au wanashindwa kukamatana wenyewe?

   Mi nadhani sasa wakati umefika kwa Watanzania kuacha woga na kupambana kikweli kikweli na hii serikali dhalimu, haina faida kwetu, imeshindwa kila nyanja, kila sekta, HAITUFAI.
   Ona leo ndugu yetu ameshatiwa ulemavu tayari, hana jicho moja! Lakini sisi tuko kimya, TUNAISHIA KUTOA MATAMKO NA KULAANI.....NJIA HII SIO WAKATI WAKE, WAKATI WAKE UMEPITA!

   Tuamke watanzania, tuchukue hatua stahiki dhidi ya hawa manyang'au!

  17. mahoza's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th March 2012
   Posts : 712
   Rep Power : 637
   Likes Received
   149
   Likes Given
   558

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   get well soon mpiganaji dua zetu ziko nawe.

  18. christine ibrahim's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th February 2012
   Location : earth
   Posts : 10,449
   Rep Power : 314919685
   Likes Received
   3458
   Likes Given
   32772

   Default

   Quote By Crashwise View Post
   Vitendo wakati yeye ni mhusika mkuu...unakumbuka swala la kubenea, Dr Ulimboka, Mwandishi wa channel ten.....
   Si ndo hapo mkuu!yaani haya mambo yanaumiza,basi 2

  19. taffu69's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th February 2007
   Posts : 2,098
   Rep Power : 5035
   Likes Received
   526
   Likes Given
   432

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   Quote By Bangoo View Post
   Mpaka 2015 mtaona mengi sana, ni mbinu za kuzima kama walivyozima analogia! Mtaona mengi sana serikali inahusika na unyama huo kwa % zote..
   Mtandao wa Membe ndani ya CCM umeanza kazi ya kunyamazisha wasiotaka kuwaunga mkono

  20. Arushaone's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st March 2012
   Location : Arusha
   Posts : 13,868
   Rep Power : 429499694
   Likes Received
   10614
   Likes Given
   26373

   Default

   Quote By Crashwise View Post
   hivi hajaenda kwenye mazishi na jua kwasasa ameshanunua suti ya kujiandaa kwenda kesha..kama ni raisi tunae yaani ningekuwa polisi ningemkamata uzururaji..........
   Word! Crashwise.

  21. KALYOVATIPI's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th August 2011
   Posts : 1,421
   Rep Power : 770
   Likes Received
   174
   Likes Given
   2

   Default re: Kibanda afanyiwa upasuaji, atolewa jicho moja!

   Nimejenga picha kama jf kungekuwa hakuna uhuru wa maoni kwa kutumia majina bandia matukio kama ya kibanda yangekuwa ndo habari ya mjini tz yatisha. Kweli atujui kusoma lkn picha twaona. Karibuni mbinga liuli.


  Page 4 of 9 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...